Thursday, 1 April 2021

DC MBONEKO APONGEZA WANANCHI NYALIGONGO KUANZISHA UJENZI ZAHANATI

...


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyaligongo Kata ya Mwakitolyo wilayani Shinyanga, na kuwapongeza kuanzisha ujenzi wa Zahanati.

Na Marco Maduhu, Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amewapongeza wananchi wa kijiji cha Nyaligongo Kata ya Mwakitolyo wilayani Shinyanga, ambao wanajishughulisha na uchimbaji wa madini ya dhahabu, kwa kujitolea kuanza ujenzi wa Zahanati, ambayo itawaondolea adha ya kufuata matibabu umbali mrefu.

Mboneko ametoa pongezi hizo leo, alipofanya ziara ya kutembelea ujenzi huo wa Zahanati, akiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba, na baadhi ya maofisa wa Polisi, ambapo Serikali ili ahidi kuwa unga mkono ili kukamilisha Zahanati hiyo.

Amesema ni jambo la pongezi kwa wananchi kujitoa wenyewe kuchangia shughuli za maendeleo, ili kutatua baadhi ya changamoto ambazo zinawakabili kuliko kuitegemea Serikali kwa kila kitu, ambapo Zahanati hiyo itakapokamilika, mbali na kuwaondolea adha ya kufuata matibabu umbali mrefu, pia watapunguza vifo vitokavyo na uzazi.

“Nawapongeza sana wananchi wa Nyaligongo kwa ujenzi huu wa Zahanati ambayo itawasaidia kupata huduma za matibabu karibu na kuimarisha afya zenu, ikiwamo kupunguza vifo vya uzaziwa wakati wa kujifungua, na mama akiwa na afya nzuri na nyumbani pana kuwa safi,”amesema Mboneko.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba, amewapongeza wananchi hao kwa kuanzisha ujenzi huo wa Zahanati, na kubainisha kuwa Sera ya afya inasema kuwepo na Zahanati kwa kila kijiji, ambapo miradi hiyo inafaa kuanza kuibuliwa na wananchi wenyewe na kisha Serikali inawaunga mkono kuikamilisha.

Mwenyekiti wa kijiji cha Nyaligongo Masumbuko Lushona, amesema walifanya mkutano wa hadhara na wananchi na kuhamasishana kuchanga pesa ili kuanza ujenzi wa Zahanati kwenye kijiji hicho, kutokana na kuteseka kufuata huduma ya afya umbari mrefu.

Kwa upande wake Mtendaji wa Kata ya Mwakitolyo Samson Lutonja, amesema ujenzi huo wa Zahanati upo kwenye hatua ya Msingi, ambapo unatarajiwa kukamilika mwaka huu kwa gharama ya Sh. Milioni 90.

Nao baadhi ya akina mama Mary Benjamini, wamesema ujenzi wa Zahanati hiyo utakuwa msaada kwao, na kueleze kuwa huduma ya matibabu inapokuwa mbali wanaoteseka hua ni wanawake pamoja na watoto.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyaligongo Kata ya Mwakitolyo wilayani Shinyanga, na kuwapongeza kuanzisha ujenzi wa Zahanati.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba, akizungumza kwenye ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Nyaligongo ambayo imeanzishwa kujengwa na wanachi wenyewe.
Diwani wa Kata ya Mwakitolyo Masalu Nyese, akizungumzia ujenzi huo wa Zahanati namna walivyo hamasishana na Wananchi kuanza kuijenga.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Mwakitolyo Samson Lutonja, akizungumzia ujenzi huo wa Zahanati ya kijiji cha Nyaligongo.
Mary Benjamin mkazi wa kijiji cha Nyaligongo, akielezea umuhimu wa Zahanati hiyo kwenye kijiji hicho.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikagua ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Nyaligongo.
ukaguzi wa ujenzi wa Zahanati hatua ya Msingi ukiendelea.
Muonekano wa Msingi ujenzi wa Zahanati kijiji cha Nyaligongo.

Picha na Marco Maduhu- Shinyanga.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger