Monday, 1 February 2021
Sunday, 31 January 2021
Wakamatwa Kwa Madai Ya Wizi Wa Fedha Kwa Njia Ya Simu
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Ialla jijini Dar es Salaam linawashikilia watu 10 kwa tuhuma za wizi wa mtandaoni na utapeli.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa Ilala, Janeth Magomi imeeleza kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa katika tarehe tofauti ya mwezi Januari mwaka huu katika maeneo tofauti ya Jiji la Dar es Salaam na wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
Aidha, Mgomi ameeleza kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) baada ya wananchi kadhaa kutapeliwa fedha zao. Wananchi hao walitoa taarifa kwa jeshi hilo ndipo ukafanyika msako pamoja na kuweka mtego wa kubaini mtandao wa watuhumiwa hao.
Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoa wa Ilala limewatahadhariasha watumiaji wa huduma za mitandao kuwa makini na watu ambao mara nyingi wanajifanya ni watoa huduma za mitandao husika na kuwalaghai wananchi ili kuwaibia.
Miongoni mwa watuhumiwa waliotiwa mbaroni ni pamoja na Baraka Makwaya, Fatuma Ayoub, Teddy Njauz, Modesta Njauz pamoja na Gift Makwaya.
Serikali yakamilisha ujenzi wa kituo cha kupozea umeme wa SGR
Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limekamilisha ujenzi wa miundombinu ya umeme itakayotumika kuendesha treni ya mwendokasi (SGR) kutoka jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro huku awamu ya pili kutoka mkoani Morogoro kuelekea Matukupola mkoani Dodoma ikitarajiwa kuanza hivi karibuni.
Akizungumza mjini Morogoro mara baada ya kutembelea kituo cha kupozea umeme kilichopo Kingolwira nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amesema kwa sasa ujenzi wa miundombinu hiyo yenye urefu wa kilomita 160 imekamilika kwa asilimia 100.
Kwa upande wake Meneja Mwandamizi wa miradi kutoka TANESCO, Mhandisi Emmanuel Manilabona amesema vituo vyote vya kupoza umeme vilivyopo katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro tayari vimeshakalimika.
IGP Sirro Awataka Polisi Wasaidizi Kufuata Sheria
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka Polisi Wasaidizi waliopo kwenye taasisi mbalimbali nchini kuhakikisha wanaheshimu na kuzingatia sheria sambamba na nidhamu wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kazi za kila siku katika kubaini, kuzuia na kupambana na uhalifu.
IGP Sirro amesema hayo jana jijini Dar es salaam, wakati alipofanya kikao kazi na Polisi Wasaidizi waliopo Kanda Maalum ya Dar es salaam ambapo amesema kuwa, weledi, ufanisi na kujituma kutasaidia kupunguza malalamiko miongoni mwa jamii wanayoihudumia.
Naye Kamishna wa Kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamii Dkt. Mussa Ali Mussa amesema kuwa, uwepo wa Polisi Wasaidizi umesaidia kuwezesha mamlaka na Halmashauri mbalimbali zilizopo nchini kuendelea kuimarika.
Marekani Yasitisha Mpango wa Chanjo kwa Wafungwa
Wizara ya ulinzi ya Marekani imesema itasimamisha mpango wake wa kuwapa chanjo dhidi ya COVID-19 wafungwa wa makosa ya ugaidi wanaozuiwa kwenye kambi ya Guantanamo kufuatia kuongezeka kwa malalamiko katika wakati ambapo nchi hiyo inajikakamua kuwachanja kwanza watumishi wa afya na wazee.
Msemaji wa wizara hiyo John Kirby ameandika hayo kupitia ukurasa wa twitter akisema hakuna mfungwa yoyote kwenye kambi hiyo ambaye tayari amechanjwa.
Kirby amekiri akisema ni kweli rais Joe Biden amesema ana mpango wa kutokomeza virusi vya corona katika siku yake ya kwanza ofisini lakini hakusema atawapa chanjo magaidi kwanza kabla ya Wamarekani.
Kambi ya Guantanamo iliyoko Cuba inawazuia washukiwa wa makosa ya ugaidi ikiwa ni pamoja na Khalid Sheikh Mohammed, mfuasi wa kundi la Al-Qaeda anayedaiwa kupanga shambulizi la Septemba 11.
-DW
Tutatenga Fedha Kwa Ajili Ya Huduma Za Ugani- Prof. Mkenda
Wizara ya Kilimo imesema katika bajeti ya mwaka 2021/22 inatarajia kutenga fedha mahsusi kwa ajili kugharimia huduma za ugani ili kuondoa changamoto zinazotatiza ukuaji wa tija kwenye uzalishaji mazao nchini ikiwemo maslahi ya maafisa kilimo ugani.
Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda ametoa kauli hiyo jana (30.01.2021) jijini Dodoma wakati akifunga kikao kazi baina ya wizara yake na maafisa kilimo toka mikoa 26 na halmashauri zote 185 za Tanzania bara uliojadili hali ya upatikanaji huduma za ugani kwenye kilimo.
“Kilimo kimekuwa na maneno mengi utasikia kilimo ni uti wa mgongo ama kilimo cha kufa na kupona.Sasa tunasema maneno yametosha hebu tuanze hatua moja mbele kwa vitendo tuboreshe utoaji huduma za ugani nchini ili wakulima wahudumiwe kwa vitendo” alisema Prof. Mkenda.
Prof. Mkenda alibainisha kuwa wizara yake imeitisha kikao hicho cha siku mbili ili kujadiliana na wataalam wa kilimo wote pamoja na wadau wa sekta binafsi hali ya kuboresha utoaji huduma za ugani na kuweka mikakati ya kuondoa changamoto za ugani
Alisema kuwa suala la kutokuwepo bajeti mahsusi kwa ajili ya watoa huduma za ugani kwenye ngazi za mikoa, halmashauri na vijiji imekuwa ikiathiri utoaji huduma kwa wakulima kushindwa kulima kwa tija.
Katika kikao hicho Waziri wa Kilimo alirejea kueleza dira ya wizara yake kwa sasa na kutaja mambo manne ya kipaumbele ili kilimo kichangie zaidi ukuaji wa uchumi kwanza ni kuongeza utafiti na uzalishaji mbegu bora za mazao.
Pili, kutoa elimu bora ya kilimo ,tatu kutafuta masoko ya mazao ya wakulima na nne kuhakikisha wakulima na wawekezaji wanapata mitaji yenye riba nafuu toka kwenye taasisi za kifedha nchini.
“Tutawekeza fedha bajeti ijayo na nguvu kukuza utafiti ili tupate mbegu bora zaidi zenye kutoa mavuno bora na tija kwa wakulima” alisisitiza Prof. Mkenda.
Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Charles Mwijage alisema anawapongeza wakulima wa Tanzania pamoja na wataalam wa kilimo kwa kuhakikisha katika kipindi cha miaka mitano ya kwanza ya serikali ya awamu ya tano Tanzania haikupata tatizo la njaa.
“ Kipindi chote kuanzia mwaka 2015 hadi 2020 nchi hii haikupata njaa, tunawashukuru maafisa ugani na wakulima wote wa Tanzania kwa kazi kubwa ya kuhakikisha taifa lina chakula cha kutosha” alisema Mwijage ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.
Mwijage aliiomba serikali kuweka mikakati mizuri na kuongeza bajeti ya kuhudumua watoa huduma za ugani wa serikali waliopo chini ya Ofisi ya Rais Tamisemi na Wizara ya Kilimo ili watatue changamoto za wakulima.
Naye Mwenyekiti wa umoja wa Maafisa Kilimo Halmashauri (DAICOs) Enock Ndunguru aliomba serikali kupitia Wizara ya Kilimo kuwa na mkakati wa kuwahamishia maafisa ugani waliopo halmashauri zote nchini kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa na sasa wawe chini ya Wizara ya Kilimo.
Katika hatua nyingine Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya alisema kwa sasa kuna maafisa ugani kilimo 6700 ambao wanahitaji kuwezeshwa vitendea kazi ili watekeleze majukumu yao ya kusimamia kilimo
Kusaya alisema kwa kuanzia wizara ya kilimo itaendeleza mkakati wa kuwapatia pikipiki maafisa ugani wote 67000 kwa awamu pamoja na kupeleka kifaa maalum cha kupima afya ya udongo (Extension Kit).
Akizungumza kwenye kikao hicho Mbunge wa Musoma Vijijini Prof. Sospeter Muhongo alitoa wito kwa serikali kufanya jitihada za kukifanya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Mwalimu Nyerere (Mwalimu Nyerere University of Agriculture) kilichopo Butiama Mara kianze kudahili wanafunzi mwaka 2021/22 ili kifundishwe maafisa ugani.
“Chuo hiki cha Kilimo cha Mwalimu Nyerere cha Butiama kimekusudiwa kufundisha wataalam wa ugani ,tunaomba kianze mapema mwaka huu 2021 ili tatizo la upatikanaji wataalam wa kilimo hususan vijijini litatuliwe” alisema Prof. Muhongo.
Mwisho
Imeandaliwa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Kilimo
DODOMA
31.01.2021
Naibu Waziri Mabula Awabana Watendaji Sekta Ya Ardhi Kuongeza Kasi Utoaji Hati
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka Watendaji wote wa sekta ya ardhi katika halmashauri kushiriki zoezi la kuandaa hati za ardhi ili kuongeza kasi ya utoaji hati katika maeneo mbalimbali nchini.
Dkt Mabula ametoa agizo hilo mwishoni mwa wiki alipozungumza na wataalamu wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Mara akiwa katika ziara ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi na kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya Serikali kupitia kodi ya pango la ardhi katika mkoa huo.
Alisema, baadhi ya halmashauri nchini zimekuwa na kasi ndogo ya uandaaji hati za ardhi kwa kisingizio cha kuwa na wataalamu wachache wa kuandaa hati wakati halmashauri hizo zina wataalamu mbalimbali wa sekta hiyo na kutolea mfano wataalamu wa Mipango Miji, Warasimu Ramani, Wapimaji na Wathamani aliowaeleza wamekuwa wakisoma chuo kinachotoa taaluma ya sekta ya ardhi.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliongeza kwa kusema kuwa, iwapo watendaji wa sekta ya ardhi watafanya kazi kwa ushirikiano na kupeana malengo ya kuandaa Hati basi kasi ya utoaji hati itaongezeka na hivyo kuifanya wizara kuongeza makusanyo ya maduhuli ya serikali kupitia kodi ya pango la ardhi.
“Ninyi nyote mmesoma katika chuo cha aina moja na mnazifahamu kazi za sekta ya ardhi mnaweza kupeana malengo na kila mmoja akashiriki kuandaa Hati na inapofika hatua ya kukamilisha ndiyo apewe Afisa Ardhi Mteule ili kukamilisha” alisema Dkt Mabula
Kwa mujibu wa Dkt Mabula, kama watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri hawatakuwa wabunifu na kufanya kazi kwa kujiwekea malengo kasi ya utoaji hati itakuwa ndogo na utaifanya wizara kutofikia malengo yake ikiwemo ya makusanyo ya kodi ya pango la ardhi ambayo kwa mwaka 2020/2021 ni bilioni 200.
Naibu Waziri Dkt. Mabula alieleza kupitia kikao hicho kilichohudhuriwa pia na Wakurugenzi wa Halmashauri za mkoa wa Mara kuwa, wakati Serikali ikifikia nusu mwaka wa fedha 2020/2021 makusanyo ya kodi ya ardhi katika halmashauri nyingi yako chini ya asilimia 50 jambo alilolieleza kuwa linatia shaka kama halmashauri hizo zitaweza kutimiza malengo katika muda uliosalia.
Naibu Waziri wa Ardhi Dkt Mabula aliwaambia watendaji hao wa sekta ya ardhi kuwa, katika robo ya mwaka wa fedha 2020/2021 anataka kuona halmashauri zote zinaongeza kasi ya makusanyo kwa kuhakikisha zinawabana wadaiwa sugu ili kulipa malimbikizo ya kodi ya ardhi na na wale wadaiwa watakaokaidi kulipa basi wafikishwe kwenye Mabaraza ya Ardhi ya Nyumba na Wilaya kwa hatua zaidi.
Aliwaeleza wataalam hao wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Mara kuwa, kwa mujibu wa kifungu Na 48(1) (g) cha sheria ya ardhi, Afisa Ardhi anayo mamlaka ya kufuta umiliki wa ardhi kwa mmiliki aliyekaidi kulipa kodi ya pango la ardhi katika kipindi cha miezi sita baada ya kutumiwa ilani ya madai.
Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa Mara Jerome Kiwia alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula kuwa, mkoa huo hadi sasa umeweza kukusanya takriban milioni 890.3 za kodi ya pango la ardhi na kubainisha kuwa, ofisi ya Ardhi katika mkoa huo imejiwekea mikakati ya kuhakikisha kasi ya makusanyo inaongezeka ikiwemo kusambaza ilani za madai kwa wadaiwa sugu na kutumia vyombo vya habari kuhamasisha ulipaji kodi ya pango la ardhi.
Serikali Yaokoa Shilingi Milioni 304 Ujenzi Wa Jengo La Dharura
Wizara ya Afya imeokoa takribani shilingi milioni 389 katika ujenzi wa jengo la Idara ya huduma za wagonjwa wa dharura linalojengwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora- Kitete ambalo limewekwa jiwe la msingi na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Hayo yameelezwa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia Dkt. John Pombe Magufuli alipokua akitoa salamu za wizara hiyo kwa wakazi wa mkoa wa Tabora.
Dkt. Gwajima alisema ujenzi wa jengo hilo litakalo wahudumia wakazi wa Tabora, mikoa ya jirani na hata nje ya nchi kutokana na barabara kuu zinazopita mkoani hapo kwakuwa jengo hilo litakua na uwezo kuwahudumia wagonjwa 50 hadi 60 tofauti na awali ambapo walikua wakihudumia wagonjwa 3 hadi 5.
Alitaja gharama za ujenzi wa jengo hilo ni milioni 604.3 ambao zimetolewa kwa ushirikiano na mfuko wa dunia (Global Fund) na ujenzi wake umetumia mfumo wa ‘force Account’ na hivyo limeweza kuokoa fedha hizo na endapo lisingetumia njia hiyo lingegharimu zaidi ya shilingi bilioni moja.
Vile vile Dkt. Gwajima alisema wamepokea maelekezo yote yaliyotolewa na Mhe. Rais na kuahidi yeye na wizara yake kufanyia kazi ikiwemo kuongeza madaktari bingwa, kuwafuatilia wale walioondoka pamoja na jengo la huduma la mama na mtoto kwa ajili ya kujifungua na ICU.
Miradi mingine ya ujenzi wa Idara ya huduma za wagonjwa wa dharura nchini ambayo wizara inashirikiana na Global Fund inatekelezwa na ipo hatua mbalimbali za kukamilishwa katika mikoa ya Ruvuma, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa, Kilimanjaro, Njombe, Mara na Tanga.
Procurement and Logistics Coordinator at Plan International Tanzania
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Procurement and Logistics Coordinator Location: Ifakara, Tanzania Company: Plan International The Organisation Plan International is an independent development and humanitarian organisation that advances children’s rights and equality for girls. We believe in the power and potential of every child. But this is often suppressed by poverty, violence, exclusion and discrimination. And it’s girls who are […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Crane Operator at Gas Entec Co. L.T.D
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
JOB OPPOETUNITY AT GAS ENTEC CO LTD PROJECT TITLE: CONSTRUCTION OF 1200 PASSENGER FERRY SHIP DESIGNATION: Crane Operator (1 POST) PLACE OF WORK: MWANZA JOB SUMMARY: Responsible for Crane Operation and maintenance Inspecting equipment, structures, or materials to identify the cause of errors or other problems or defects. Servicing, repairing, adjusting, and testing machines. DUTIES & […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
1500+ Jobs at JVACEE a Joint venture company of Arab Contractors And El-sewedy Electric (Stigler’s Gorge Project)
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
JVACEE is a Joint venture company of Arab Contractors and El-sewedy Electric, dealing with the scope of Engineering, Procurement & Construction of Julius Nyerere Hydropower Project in Stigler’s Gorge in Tanzania, which is expected to produce 2,115 MW of installed capacity. Job Title: Foreman – Welding 9 Job Description: oversees and manages the welding team or individual […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
7 Job Opportunities at Rural Energy Agency (REA)
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Job Opportunities at Rural Energy Agency (REA) Rural Energy Agency (REA) is an autonomous body under the Ministry of Energy and Minerals of the United Republic of Tanzania. Its main role is to promote and facilitate improved access to modern energy services in rural areas of Mainland Tanzania. REA became operational in October 2007. On […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Procurement And Supplies Officer at Rural Energy Agency (REA)
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
POST: PROCUREMENT AND SUPPLIES OFFICER II – 1 POST POST CATEGORY(S) PROCUREMENT & LOGISTIC MANAGEMENT TRANSPORT AND LOGISTICS EMPLOYER Rural Energy Agency (REA) APPLICATION TIMELINE: 2021-01-28 2021-02-10 DUTIES AND RESPONSIBILITIES Evaluating vendor performance and advices accordingly; Maintaining an up-to-date filing system on pricing and vendors to ensure timely and accurate access to information; Preparing bid documents […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Monitoring And Evaluation Officer at Rural Energy Agency (REA)
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
POST: MONITORING AND EVALUATION OFFICER II – 1 POST POST: CATEGORY(S) BANKING, ECONOMICS AND FINANCIAL SERVICES ENGINEERING AND CONSTRUCTION PROJECT, PLANNING AND POLICY MANAGEMENT STATISTICS AND MATHEMATICS WATER, MINING AND NATURAL RESOURCES EMPLOYER Rural Energy Agency (REA) APPLICATION TIMELINE: 2021-01-28 2021-02-10 DUTIES AND RESPONSIBILITIES Visiting project sites and submit progress reports periodically for projects under implementation and […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Project Engineers at Rural Energy Agency (REA)
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
POST: PROJECT ENGINEER II – 5 POSTS POST: CATEGORY(S) ENGINEERING AND CONSTRUCTION EMPLOYER Rural Energy Agency (REA) APPLICATION TIMELINE: 2021-01-28 2021-02-10 DUTIES AND RESPONSIBILITIES Managing projects contracts; Assisting in project identification, Planning, supervision and appraisal; Providing information and statistics on electricity projects carried out; Analyzing and preparing periodic electricity projects performance reports; Monitoring the progress of the […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details