Na Shamimu Nyaki - WHUSM
Sekta za Wizara ya Habari ni sekta muhimu zenye mchango mkubwa katika kuchangia uchumi wa nchi na kuleta maendeleo.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dodoma na Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa wakati akiwasilisha Muundo pamoja na Majukumu ya Wizara hiyo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.
Mhe. Bashungwa amesema kwamba Sekta ya Sanaa na Michezo zimechangia katika Ongezeko la pato la Taifa ambapo kwa mwaka 2018, shughuli za burudani zimechangia pato la Taifa kwa asilimia 13.7 na kushika nafasi ya kwanza na mwaka 2019 shughuli hizo zilichangia asilimia 11.2 na kushika nafasi ya tatu.
"Tunashukuru Kamati kwa kutupa mawazo chanya ambayo yatasaidia kuboresha na kuendeleza sekta hizi, naahidi mimi pamoja na timu yangu tutayafanyia kazi mawazo mliyotupa na tayari tumeanza kufanya hivyo katika sekta zote" alisema Mhe. Bashungwa.
Akiendelea kuzungumza Mhe. Bashungwa ameeleza kuwa Wizara tayari imeanza kutengeneza Mpango Mkakati wa Maendeleo ya Michezo pamoja na ujenzi wa Ukumbi wa Michezo na Sanaa (Sports and Arts Arena) ambayo itaanza kujengwa Jijini Dodoma.
Aidha, Mhe. Bashungwa ameeleza kuwa TCRA pamoja na TRA wameanza kushirikiana namna ya kukusanya mapato ya kazi za Sanaa kupitia njia za Kidijiti (Digital Taxation).
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Stasilaus Nyongo Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki ameipongeza Wizara hiyo kwa Mikakati mizuri ya kusaidia Sekta inazozisimia, huku akishauri Wizara hiyo kuongeza ubunifu katika kukusanya mapato ya Serikali kupitia Sanaa na Michezo.
"Nashauri Wizara hii, Wizara ya Elimu pamoja na TAMISEMI kuwa na utaratibu unaotambulika wa kuendesha na kusimamia shughuli za michezo shuleni" Mhe. Nyongo.
Naye Mhe. Jumanne Sagini Mbunge wa Jimbo la Butiama ambaye ni Mjumbe wa Kamati hiyo amepongeza juhudi za Wizara hiyo katika kutekeleza majukumu yake ambapo ameeleza kuwa ipo haja ya kufanya mapitio ya Sera zote zilizochini ya Wizara hiyo ili kama kuna ambazo zinahitaji marekebisho zifanyiwe maboresho ili kuendana na mahitaji ya wakati huu.
Kamati hiyo imepokea taarifa ya Muundo na Majukumu ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambapo kesho Januari 26, 2021 itapokea Taarifa ya Majukumu ya Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo.
Mwishoo....






Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), David Silinde akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), mjini Morogoro, Januari 25, 2021. Wengine kutoka kulia ni Mwenyekiti wa TSC Profesa Willy Komba, Kaimu Katibu wa TSC Moses Chitama na Katibu wa Baraza husika,Lawrence Chankani. 

























Mkurugenzi msaidizi wa tiba asili na tiba mbadala kutoka wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt. Paul Mhame akitoa hotuba ya uzinduzi wa jukwaa hili.
Naibu Mkamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA upande wa utawala na fedha Prof. Amandus Mhairwa akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzindua rasmi jukwaa.
Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko akitia neno kwa wagana hao wa tiba asili na wadau wengine wakati wa uzinduzi wa jukwaa hilo.
Mkuu wa mradi huo wa GRILI Dkt. Faitha Mabiki akieleza kwa kifupia majukumua na malengo ya mradi huo wa GRILI na yale ambayo yamefanyika toka mradi uanzishwe. 
