Friday, 15 January 2021

MAENEO YENYE MIFUMUKO YA MADINI LAZIMA YARASIMISHWE - PROF. MANYA

Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya akingumza jambo na baadhi ya wadau wa Madini pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu.

 Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya katikati, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka na kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula  wakiwa kwenye kikao kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo

Baadhi ya wadau wa Sekta ya Madini wakifuatilia kikao cha Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya.
Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya akitoa ufafanuzi mara baada ya kikao baina yake na wadau wa madini.
Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya akitoa ufafanuzi mara baada ya kikao baina yake na wadau wa madini.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula akizungumza jambo katika kikao cha Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya, kushoto ni Naibu Waziri wa Madini Prof. Manya

Jengo la Kituo cha Umahiri la Mkoa wa Simiyu

Na Tito Mselem Simiyu,

Imeelezwa kuwa mfumuko wa madini (Rush) ni dharura tu, lazima sehemu zote zenye mifumuko ya madini zirasimishwe ili maeneo hayo yaweze kuchangia maduhuli ya Serikali.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya kwenye kikao baina yake na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo.

Prof. Manya amesema mfumuko wa madini ni kitu cha mpito hakitaachiwa kiendelee kwa muda mrefu na badala yake kirasimishwe ili kisadie kwenye ushirikishwaji wa watanzania kwenye rasilimali ya madini ambayo watanzania wote wanatakiwa kunufaika nayo.

“Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alisema wachimbaji wadogo watafutiwe maeneo ya kuchimba ila lazima wazingatie taratibu na sheria ikiwa ni pamoja na kuwa na leseni ya uchimbaji madini husika”, alisema Prof. Manya.

Prof. Manya aliongeza kuwa, Mkoa wa Simiyu umebarikiwa kuwa na madini mbalimbali ikiwemo madini ya metali kama dhahabu, shaba na nikeli, madini ya ujenzi kama mawe, kokoto, moramu na mchanga, madini ya vito kama amethyst na madini ya viwandani kama chokaa na chumvi.

Aidha, Prof. Manya amesema baadhi ya wachimbaji na wadau wengine wa shughuli za madini hawaelewi vyema Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na Marekebisho yake ya mwaka 2017 kuhusu haki ya leseni ya madini na haki ya ardhi hivyo kupelekea wamiliki wa ardhi kutowaruhusu waliopewa haki ya leseni madini kutofanya makubaliano ya fidia katika maeneo yao na kupelekea shughuli za uchimbaji kutofanyika katika maeneo yaliyotolewa leseni.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula amesema Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini imeshafanya mazungumzo na baadhi ya mabenki ili wapatiwe mikopo wachimbaji wadogo wa madini na kuwatoa hofu ya kwamba wachimbaji wadogo hawakopesheki.

“Tuliziambia taasisi za kibenki kwamba wale ambao wana leseni hai wakopeshwe, hivyo wachimbaji wanapaswa kujiunga ili wapatiwe leseni na waondokane na mfumo walionao wa mifumuko ya madini ambapo wanachimba bila leseni, lazima leseni zitolewe na Rush zikome mara moja”, alisema Prof. Kikula.

Naye, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Mhandisi Yahya Samamba, amewataka wachimbaji wa mkoa wa Simiyu kupendana na kuachana na wivu, majungu, chuki na fitina na badala yake wachimbe kwa kushirikiana ili walete tija kwenye shughuli zao.

Pia Mhandisi Samamba amewapongeza watumishi wa Ofisi ya Madini ya Mkoa wa Simiyu kwa kuvuka lengo la makusanyo ya maduhuli ya Serikali ambapo walipangiwa wakusanye kiasi Tsh milioni 250 na badala yake wamekusanya Tsh bilioni 2.3 ambapo wamevuka lengo kwa zaidi ya asilimia 1700 ndani ya miezi sita.
Share:

The National Examinations Council of Tanzania (NECTA) is expected to release the form four, ftna,sfna and QT result today

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Here we have good news to all Standard Four candidates , Form Two , Certificate of Secondary Education Examination(CSEE) 2020 candidates, that the National Examinations Council of Tanzania (NECTA) is about to release the examination results for Form Two National Assessment, Standard Four National Assessment, Qualifying Test (QT) and Certificate of Secondary Education Examination(CSEE) Examinations […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Accountant at Inchcape Shipping Services

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Accountant     Inchcape shipping services is a global organization providing a services through a connected world in which our customers trade successfully and make better decision in every port. We are expanding our Linear business in Tanzania and are inviting ambitious capable candidates with experience in the shipping and marine industry to apply for the […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Finance Manager at Inchcape Shipping Services

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Finance manager   Inchcape shipping services is a global organization providing a services through a connected world in which our customers trade successfully and make better decision in every port. We are expanding our Linear business in Tanzania and are inviting ambitious capable candidates with experience in the shipping and marine industry to apply for the […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JANUARI 15,2021

















Share:

Thursday, 14 January 2021

Results Based Mgmt Specialist at UNDP

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Results Based Mgmt Specialist  Background The UN Resident Coordinator’s Office (RCO) in Tanzania supports the Resident Coordinator in promoting attainment of the Sustainable Development Goals and the Africa Agenda 2063. It provides strategic guidance and coordination assistance for the design and delivery of the UN’s Cooperation Framework, UN Development Assistance Plan 2015-2022 (UNDAP II). Under […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Officer, GM Product Control at Standard Bank

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Officer, GM Product Control     Job Details Finance: budgeting and forecasting, creating interim and annual financial statements, facilitating internal mergers and acquisitions, as well as dealing with analysts and investors. Job Purpose To provide routine Global Markets & Treasury products reporting on income statement and balance sheet and reconciliation function within the Product Control Division […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Primary School secretary at Braeburn International School

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Primary School secretary     Braeburn International School, Arusha We are looking for a Primary School secretary to join our dedicated team. You must be highly motivated, organised, enjoy working with people, be able to take direction as well as be someone who is able to identify and address issues themselves and be willing and able […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Senior Accountant, Hospitality at Gibbs Farm

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

TITTLE:  SENIOR ACCOUNTANT, HOSPITALITY   LOCATION: ARUSHA- KARATU SUMMARY Gibbs Farm, a high end five-star lodge in the Arusha – Karatu area currently has available a live-in position for a Senior Accountant, reporting to the Lodge Controller. We are currently seeking an experienced, and thorough senior accountant to join our renowned operation. In this role, you will […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Content & Curriculum Development Manager at IRC

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Job Title: Content & Curriculum Development Manager International Rescue Committee Kasulu, Kigoma, Tanzania Requisition ID: req11913 Sector: Education Employment Category: Fixed Term Employment Type: Full-Time Open to Expatriates: No Location: Kasulu, Tanzania Background The International Rescue Committee (IRC) responds to the world’s worst humanitarian crises and helps people to survive and rebuild their lives. Founded in 1933 at the request of […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

WANACHAMA SHINYANGA PRESS CLUB WAPIGWA MSASA KUHUSU MATUKIO YA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO

Mwakilishi kutoka Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Analyse Kaika akitoa elimu ya sheria mbalimbali za ulinzi wa mtoto na wanawake katika mafunzo kwa wanachama wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club- SPC).
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC), Patrick Mabula (aliyesimama) akitoa neno kwa wanachama wa klabu hiyo wakati wa mafunzo ya nafasi ya vyombo vya habari katika kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Mkuu wa idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga, John Tesha (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akifungua mafunzo ya nafasi ya vyombo vya habari katika kumaliza ukatili dhidi ya wanawake na watoto
Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa SPC, Marco Maduhu (kulia) akitoa taarifa ya mradi wa nafasi ya vyombo vya habari katika kumaliza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto wakati wa mafunzo hayo.
 
Na Damian Masyenene, Shinyanga 
KATIKA mwendelezo wa vita ya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto mkoani Shinyanga, Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) imeanza kutoa mafunzo kwa wanachama wake ili kuwasaidia kutafiti, kuandika, kuandaa vipindi na kuelimisha jamii juu ya vitendo hivyo ili kuvitokomeza. 

Mafunzo hayo ya siku moja yaliyobeba mada ya ‘Nafasi ya vyombo vya habari katika kumaliza ukatili dhidi ya wanawake na watoto’, yamefanyika leo Januari 14, 2020 mjini Shinyanga kwa ufadhili wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT) ikiwa ni hatua za mwanzo za utekelezaji wa mradi wa miezi mitatu wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga. 

Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga, John Tesha amesema kuwa waandishi wa habari mkoani humo wamesaidia kwa kiasi kikubwa kuelimisha, kutoa taarifa na kufichua vitendo hivyo, hivyo akawapongeza kwa juhudi kubwa wanazozifanya na kusisitiza kuwa mkoa huo umepiga hatua katika vita hiyo ikiwemo kuzindua mpango kazi wa miaka mitano. 

Akitoa neno kwa wanachama wake, Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC), Patrick Mabula amebainisha kuwa tangu kuanzishwa kwake klabu hiyo imekuwa msaada mkubwa katika kukemea vitendo vya ukatili mkoani hapo. 

Amesema kuwa Wanawake na watoto wamekuwa kwenye changamoto kubwa za vitendo vya kikatili, hivyo SPC kama jicho kubwa inayo nafasi ya kuifikia jamii na kusaidia kutoa elimu kumaliza tatizo hilo, huku akieleza kuwa SPC kwa ufadhili wa WFT watatekeleza mradi huo kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Januari 21 hadi Aprili 17, mwaka huu. 

“Waandishi mtumie kalamu zenu vyema kuhakikisha mnaongeza ufahamu, kuibua na kukemea kwa namna yoyote vitendo hivi,” amesema. 

Akitoa mafunzo kwa waandishi hao, Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga, Angel Mwaipopo amesema hatua ya utoaji mafunzo kwa wanahabari ni sehemu ya Mpango kazi wa taifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA). 

Angel amebainisha maeneo ya utekelezaji wa mpango huo kuwa ni kuimarisha uchumi wa kaya, kuhakikisha jamii inaendeleza mila chenye pekee, mazingira salama, malezi na kuimarisha familia, utekelezaji na usimamizi wa sheria, utoaji huduma kwa wahanga wa ukatili, mazingira salama shuleni na utaratibu, ufuatiliaji na tathmini. 

Naye Mwakilishi kutoka Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Analyse Kaika akiwafunza wanahabari kuhusu sheria ya ulinzi wa mtoto na wanawake, amewahimiza kujikita katika kuzifahamu sheria na sera zinazowalinda watoto na wanawake ili kuandaa taarifa zenye na zinazosaidia kutokomeza vitendo vya ukatili.
Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga, Angel Mwaipopo akitoa mafunzo ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto mbele ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga
Mwakilishi kutoka Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Analyse Kaika akitoa elimu ya sheria mbalimbali za ulinzi wa mtoto na wanawake katika mafunzo kwa wanahabari mkoa wa Shinyanga
Mwakilishi kutoka Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Analyse Kaika akitoa elimu ya sheria mbalimbali za ulinzi wa mtoto na wanawake katika mafunzo kwa wanahabari mkoa wa Shinyanga
Waandishi wa habari wakifuatilia kwa umakini mafunzo hayo
Viongozi wa SPC nao wakifuatilia kwa umakini mafunzo hayo
Waandishi wakichukua notisi kwenye kwenye mafunzo hayo
Waandishi wakisikiliza kwa umakini na kuchukua notisi kutoka kwenye mafunzo hayo
Wakiendelea kusikiliza kwa umakini
Waandishi wakipata elimu juu ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto
Mkufunzi Angel Mwaipopo akiendelea kutoa elimu kwa waandishi wa habari
Mafunzo yakiendelea kutolewa
Mafunzo yakiendelea
Waandishi wakisikiliza na kufuatilia kwa umakini mafunzo hayo
Elimu ikiendelea kutolewa
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini

Share:

Bashe Aagiza Mhandisi Wa Umwagiliaji Mkoa Wa Tabora Apangiwe Kazi Nyingine


NA TIGANYA VINCENT
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ameiagiza Tume ya Taifa ya Umwagiaji kumpagia kazi nyingine Mhandisi wa Umwagiliaji Mkoa wa Tabora baada ya kushindwa kusimamia skimu ya Umwagiliaji Inala na maeneo mengine mkoani humo.

Hatua hiyo inatokana na udhaifu uliojitokeza katika Skimu Inala , Manispaa ya Tabora ya wakulima kulima ekari 15 badala ya hekta 400 zinazotakiwa kulimwa kwa msimu.

Bashe alitoa kauli hiyo jana mkoani Tabora wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli mbalimbali za miradi ya kilimo ukiwemo wa skimu ya umwagiliaji wa Inala uliopo Manispaa ya Tabora.

Alisema Mhandisi huyo Bahati Balekele ameshindwa kusimamia Skimu hiyo ya kuhakikisha kuwa wanakuwa na uongozi imara ambao utawasimamia wanachama ili walime kwa kiwango kilichokusudia kwa ajili ya kuleta tija ya mradi.

Naibu Waziri huyo alisema inasikitisha kuona kuwa Serikali imewekeza kiasi cha bilioni 2 lakini hadi kufikia jana ni ekari 15 ndio zilizokuwa zimelimwa na kupelekea uwekezaji mkubwa wa fedha za umma kutoonyesha tija.

Bashe aliongeza zipo baadhi ya Skimu mkoani humo ambazo zenye kasoro ndogo ndogo lakini Mhandisi huyo ameshindwa hata kuwahamasisha wakulima waweze kuchangia fedha kwa ajili ya kurekebisha kasoro ili ziendeleze kuzalisha kwa tija.

Kufuatia kasoro katika skimu ya Inala alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala ndani ya wiki mbili kuitisha mkutano wa wakulima wote kwa ajili ya kuchagua uongozi utakaosimamia mradi na kuwapanga wakulima katika mashamba mbalimbali ili waweze kuzalisha kwa tija.

Alisema katika mkutano wakulima wote wapangwe upya katika mashamba ya mradi huo na walime na atakayeshindwa kujitokeza atakuwa amepoteza sifa ya kupata eneo la kulima mpunga katika mradi huo.

Bashe alisema pamoja na mkutano huo ni vema Mkuu huyo wa Wilaya akaangalia uwezekano wa kuandaa taratibu za kuondoa tatizo la watu wawili ambao wamejimilikisha ekari 200 katika eneo la mradi.

Wakati huo huo Bashe amezitaka Halmashauri Mkoani Tabora kuhakikisha wanatenga maeneo makubwa ya kilimo( Block farm) kwa ajili ya uzalishaji mkubwa wa mazao mbalimbali.

Alisema hatua itaziwezesha Halmashauri kuongeza mapato ya ndani ambayo yatawawezesha kujitegemea kwa asilimia mia moja.

“Halmashauri mkiwa ‘serious’ mtaweza kuanzisha block farm za mazao mbalimbali …hatua hiyo itawasaidia kupata fedha nyingi na kuacha tabia ya kufukuza na mamalishe na machinga kutafuta ushuru…mnapokuwa na block farm ni rahisi kwa mtu hata kuwekeza katika kiwanda kwa kuwa mwekezaji atapata malighafi katika eneo moja na kwa wingi” alisisitiza.

Bashe alisema badala ya Halmashauri kukimbilia katika upimaji wa viwanja  hata katika maeneo yanayostahili shughuli za uzalishaji wa mazao ni vema wakatenga mashamba makubwa kwa ajili ya kilimo cha korosho, alizeti, karanga , miembe na mazao mengine ambayo yatawawezesha wakulima kuwa na kipato kikubwa.

Alisema hatua hiyo itawasaidia wakulima kuondokana na kilimo cha kimazoea cha kuzalisha mazao kwa ajili ya kuijikimu na kuwa na kilimo cha uzalishaji kibiashara na Halmashauri kupata mapato yake.




Share:

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya Ataka Wakulima Wafundishwe Kilimo Bora Cha Umwagiliaji


Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya ametoa wito kwa maafisa kilimo wa halmashauri za mkoa wa Morogoro kuwafundisha wakulima kanuni bora za kilimo cha umwagiliaji ili waongeze tija na uhakika wa kipato kufuatia serikali kuboresha miundombinu.

Ametoa wito huo leo wilayani Mvomero wakati alipokagua utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa ghala na skimu yaumwagiliaji ya kijiji cha Kagugu inayotekelezwa na Mradi wa kuongeza thamani zao la mpunga (ERPP).

” Wakulima lazima waoneshe kilimo bora kwa kutumia mbegu kidogo na maji kidogo kufuatia mafunzo waliyopatiwa na wataalam wa kilimo cha umwagiliaji ili tija ipatikanae na kuwasaidia kuongeza kipato kupitia zao la mpunga” alisema Kusaya.

Katibu Mkuu huyo ameagua mashamba ya mpunga kijiji cha Kagugu na kuwaelekeza maafisa kilimo wa halmashauri kuwafundisha wakulima kilimo cha kisasa ili mradi wa umwagiliaji uwasaidie kuongeza tija kwa kutumia eneo dogo kisasa.

Kusaya anafanya ziara ya kufuatilia utekelezaji wa mradi wa ERPP unatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi huu Januari ili ukabidhiwe kwa wakulima kupitia halmashauri baada ya Wizara yake kukamilisha miradi yote kumi na moja.

Katibu Mkuu huyo wa Kilimo aliongeza kusema Mradi wa Kuongeza tija na uzalishaji wa zao la Mpunga (ERPP) unaotekelezwa kwa ubia na Benki ya Dunia umefanikiwa kujenga maghala (5),skimu za umwagiliaji (5) na ujenzi wa maabara moja ya kilimo kwa lengo la kusaidia wakulima kuongeza tija katika zao la mpunga hatimaye nchi ijitosheleze kwa chakula na kipato kwa wakulima.

“Lengo la Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli ni kuona miradi hii ya kilimo cha umwagiliaji inamnufaisha mkulima,hivyo tutapenda kuona mara baada ya kuikabidhi kwa wakulima inakuwa endelevu” alisisitriza Kusaya.

Kusaya aliongeza kusema wizara yake inaamini kuwa kilimo cha umwagiliaji ndio mkombozi kwa mkulima kwani atakuwa na uhakika wa kuzalisha mazao yake zaidi ya mara moja katika mwaka kutokana na uwepo wa mabonde yenye maji na miundombinu ya kisasa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Albinius Mugonya alisema wanaishukuru wwizara ya kilimo kwa kufanikisha kukamilisha miradi mitatu ya  ujenzi wa maghala mawili kijiji cha Mbogo Kwamtonga na Kagugu pamoja na skimu ya umwagiliaji ya Kagugu ambazo zitakuza kiapato cha wakulima.

” Sisi wana Mvomero tuna miradi hii mitatu ambapo wakulima 5,673 watanufaika kwenye vijiji vya Mbogo Kwamtonga na Kagugu kwani tayari tija imefikia wakulima wanazalisha tani 5 hadi sita za mpunga kwa hekta” alisema Mugonya .

Mkuu huyo wa wilaya alisema mkakati wa wilaya yake ni kuhamasisha ujenzi wa viwanda vikubwa na vidogo ili kuongeza thamani ya zao la mpunga na kuwafanya wakulima wauze mchele badala ya mpunga ili wapate kiapato kikubwa.

Naye mratibu wa mradi wa ERPP Mhandisi January Kayumbe alisema kwa sasa miradiyote 11 katika wilaya za Mvomero, Kilosa na Ifakara ipo kwenye hatua za ukamilishaji na kuwa ifikapo mwisho wa mwezi huu itakakuwa tayari kukabidhiwa kwa wakulima.

Mradi wa ERPP ulianza kutekelezwa mwaka mwaka 2015 kwa gharama ya Dola za kimarekani milioni 22.91 toka Benki ya Dunia ukijusisha Tanzania Bara na Zanzibar.

 Jumla ya miradi 11 ikiwemo ujenzi wa skimu 5 za umwagiliaji,ujenzi wa maghala 5 na ujenzi wa maabara moja ya mbegu  inatekelezwa katika mkoa wa Morogoro chini ya ERPP.


Share:

Rais Wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi Na Makamu Wake Wa Kwanza Maalim Seif Shariff Hamad Wamtembelea Rais Dkt. Magufuli Kijijini Chato Leo


 Rais Dkt John Magufuli ameahidi kushirikiana na viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuhakikisha Zanzibar inaendelea kuwa amani na inaendelea kukua kiuchumi.

Dkt Magufuli ametoa kauli hiyo wilayani Chato mkoani Geita akiwa pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapibduzi Dkt Hussein Mwinyi pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Seif Sharif Hamad, waliomtembelea nyumbani kwake na kufanya nae mazungumzo.

Amesema katika siku za mwanzo za uongozi wao, Viongozi hao wamefanya mambo makubwa yanayoashiria mwanga wa maendeleo Visiwani Zanzibar.

Rais Magufuli amewataka Viongozi hao kuendelea kushirikiana katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku na kuendelea kuhubiri amami miongoni  kwa Wakazi wa Zanzibar na Watanzania wote, kwani amani ndio msingi wa maendeleo.


Share:

Infinix Yapasua Anga Kuwafikia Mashabiki Wake Kimataifa


Kampuni pendwa ya simu Infinix Mobility Limited kwa mwaka wa2020 ilifanya matamasha mbalimbali yenye kuhusisha zaidi mashabiki (fans) wake. 

Kati ya matamasha yalionekana kukonga nyoyo za mashabiki ni hii ya kufungia mwaka wa 2020 pamoja Infinix Fanfest na ya HOT 10 Rap Relay Challenge.


Tamasha la Infinx Fanfest lilijumisha wasanii na Fans kutoka nchi mbalimbali kwa pamoja walitengeneza video isiyopungua dakika 45 iliyoruka live @InfinixMobile ambapo kila mmoja aliweza kuonyesha uhodari wake ama wao kupitia kuimba, kucheza na jinsi ambavyo mashabiki walivyopata nafasi ya kushuhudia uwezo wa camera ya NOTE 8 night mode.


Kutoka nchini Tanzania Tamasha hili liliwakilishwa na msanii hemed (PHD),yeye alipata nafasi yakuwafikia mashabiki wa Infinix kupitia wimbo wake pendwa wa Medicine na Kenya iliwakilishwa na msanii maarufu Octopizo yeye alijumuika na Fans wa Infinix nakuimba nao kwa pamoja.
                                                                                                


Kwa ufupi night mode ni teknolijia inayopatikana katika camera ya Infinix NOTE 8 yenye Megapixel 64 na sifa kubwa ya night mode kupiga picha za usiku zenye uangavu na kuvutia lakini pia ukitembelea app ya Infinix Xclub utakutana na picha zilizopigwa kupitia teknolojia ya night model kupitia challenge ya FanFest ambapo mshindi alizawadiwa Infinix NOTE 8.


Kwa mwaka huu wa 2020 kupitia tamasha la FanFest na HOT 10 Rap Relay ambapo mshindi alizawadiwa Infinix HOT 10 nakuingia katika Guiness world record book. 

Hii ni ishara Infinix Mobility inatambua nakuthamini mchango wa mashabiki.


Jiweke karibu na Infinix....tembelea 

https://www.instagram.com/infinixmobiletz/

https://www.infinix.club/

MAWASILINO
0744606222




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger