Sunday, 10 January 2021
Saturday, 9 January 2021
Serikali Yatoa Miezi 3 Kwa Wenye Vifungashio Visivyokidhi Viwango Vya TBS Viondolewe Sokoni
Serikali imetoa miezi mitatu kwa wenye shehena ya vifungashio visivyokidhi viwango vya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) vinaondolewa sokoni.
Agizo hilo limetolewa Januari 8, 2020 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Ofisi hiyo jijini Dodoma kuhusu matumizi ya vifungashio vya plastiki kutumika kama vibebeo vya bidhaa.
Ummy alisema hatua hiyo ya Serikali imechukuliwa baada ya kuwepo kwa vifungashio vinavyotumika kama vibebeo vilivyozagaa madukani, sokoni na maeneo mbalimbali.
Alisema kuwa pamoja na mafanikio yaliyopatikana kutokana na katazo la mifuko ya plastiki siku za hivi karibuni kumejitokeza changamoto ya matumizi ya vifungashio vya plastiki aina ya tubings visivyokuwa na sifa na hivyo kutokukidhi matakwa yaliyowekwa na TBS.
Aidha, Waziri Ummy aliongeza kuwa vifungashio hivi kwa sasa vinazalishwa kwa wingi na kwa ukubwa mbalimbali na vimekuwa vikitumika kama mifuko ya kubebea bidhaa sokoni na kuleta dhana kuwa mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku imerudi kivingine kama “vifungashio”.
Alisema mifuko hii imeanza kuzagaa kwenye mazingira ya mitaa yetu na vijiji vyetu kwa kasi kubwa, na hivyo kurudisha nyuma mafanikio makubwa tuliyoyapata katika kipindi chote cha kupambana na changamoto ya mifuko ya plastiki.
Kwa mantiki hiyo Waziri Ummy aliwataka wasambazaji, wazalishaji wa vifungashio hivi na waagizaji kuacha mara moja kuzalisha, kusambaza, kuuza na kutumia vifungashio hivyo na kusisitiza kuwa baada ya kipindi hicho Serikali haitatoa tangazo lingine lolote kuhusiana na katazo la matumizi ya vifungashio visivyokuwa na ubora.
Waziri huyo alisema Serikali itachukua hatua kali kwa mujibu kisheria na katika kipindi hiki tunaendelea na operesheni maalumu kuwabaini wanaokwamisha mafanikio haya kwa kuzalisha na kusambaza vifungashio hivyo na hatutawavumilia watu hawa.
“Sitaki kuwaathiri wafanyabiashara wadogo wadogo ambao kwangu mimi ndio wananchi ninaotaka kutowaathiri, maana tukisema piga marufuku hizi karoti anaweka wapi hizi nyanya anaweka wapi ubuyu, kwa hiyo lengo la Serikali kuweka miezi mitatu ni kuzingatia hali halisi ya wafanyabiashara ndogondogo ambao ndiyo maana ni watumiaji wa mwisho hivyo tunataka kuwabana twazalishaji ili wanaonunua wanunue vifungashio vyenye ubora,” alisisitiza.
“Napenda kuwakikishia wananchi kuwa Serikali kupitia TBS inayo kanzidata ya wazalishaji wa kutosha wa vifungashio vinavyokidhi viwango na hivyo hapatakuwa na uhaba wa vifungashio vinavyokidhi viwango baada ya kipindi hicho cha miezi mitatu.
Nitumie nafasi hii kuwaasa wazalishaji na wawekezaji wa ndani kuchangamkia fursa hii kwa kuzalisha vifungashio vyenye kukidhi viwango nilivyobainisha,” alisema.
Akizungumzia kuhusu katazo la mifuko ya plastiki Waziri Ummy alisema utekelezaji wa katazo hilo umefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kipindi chote cha mwaka mmoja na nusu tangu Serikali ilipotoa tangazo hilo.
Alitaja mafanikio hayo ni matokeo ya ushirikiano wa wananchi, taasisi, waliokuwa wazalishaji na wasambazaji na makundi mbalimbali yaliyoshiriki katika kuzingatia maelekezo ya Serikali katika kupambana na changamoto ya mifuko ya plastiki.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Joseph Malongo alisema Ofisi hiyo itashirikiana na TBS kuanza kampeni ya kupitia tena mifuko ya ‘non woven’ kwani kuna uwezekano wa kuwepo kwa mifuko isiyo na viwango.
Malongo alisema Serikali ilipoweka katazo la mifuko ya plastiki iliweka pia viwango vya mifuko ya aina hiyo akitaja kuwa ni lazima iwe na uzito wa gramu 70 kwa mita ya mraba moja ili itumike kwa zaidi ya mara moja.
Aliongeza kuwa pia lazima mifuko hiyo iwe na nembo ya TBS ili kuonesha kuwa imekidhi vigezo vinavyotakiwa pamoja na kutambulisha jina la mzalishaji.
Kigezo Kingine ni viwe na lakiri (Seal), ikimaanishwa kuwa kifungashio kinatakiwa kifungashwe na anayefungasha bidhaa yake ili kuuza kabla ya kwenda sokoni.
Waziri Mhagama Apongeza Kilimo Cha Tangawizi Kuchukua Nafasi Ya Mirungi
MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu amewapongeza wakulima wa zao la tangawizi na kukemea kilimo cha Mirungi Wilayani Same Mkoa wa Kilimanjaro.
Ametoa pongezi hizo alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kiwanda cha Kuchakata tangawizi cha Mamba Miamba kilichopo katika Kata ya Myamba Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Januari 7, 2021.
Waziri alifurahishwa na wakulima hao kuwekeza katika kilimo cha tangawizi na kueleza kuwa, ni wakati muafaka kuachana na kilimo cha mirungi kwani Wilaya hiyo imekuwa ikijihusisha na kilimo hicho kwa muda mrefu.
“Wakulima shikamaneni na hakikisheni kilimo cha tangawizi kinakuna na tija na kuachana kabisa na kile cha mirungi, maeneo yenu yana rutuba ya kutosha kwa kilimo yatumieni kuzalisha kwa wingi tangawizi mjikwamue kiuchumi,”alisema waziri Mhagama
Aliongezea kuwa, katika maeneo yaliyokuwa yakimpa shida kwenye mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya aina ya mirungi ni pamoja na wilaya hiyo.
“Faraja ninayoipata leo ni kuona zao la tangawizi sasa linakwenda kuchukua nafasi ya kilimo cha mirungi na niwaombe Kamati ya Ulinzi na Usalama tujitahidi kuhakikisha tunatokomeza ulimaji wa mirungi kwa gharama yoyote”alisisitiza
Mpaka sasa Taifa limefanikiwa kukomesha matumizi na uingizaji wa dawa za kulevya kwa asilimia 90 kwa kuzingatia hatua mbalimbali ambazo zilichukuliwa na Serikali.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Anne Malechela alieleza furaha yake kwa ujio wa Waziri kujionea maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho huku akiahidi kuendelea kushirikiana na uongozi wa mkoa na wananchi kuhakikisha kiwanda kinakuwa na maendeleo endelevu ili kuleta matokeo chanya kwa wakazi wa Same na jamii kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa umma (PSSSF) Bw. Hosea Kashimba alieleza, namna walivyodhamiria kuwekeza katika kiwanda hicho na kuhakikisha kinaendelea kwa miaka mingi na kuleta tija.
“Katika kiwanda hiki tumewekeza kiasi cha Shilingi Bilioni 1.8 kwa kuweka mtaji, na kufanya ukarabati wa majengo, kujenga uzio unaozunguka kiwanda pamoja na mifumo ya umeme kurahisisha shughuli za uendeshaji wake,”alieleza Kashimba
Aliongezea kuwa, hadi desemba 2020 mfuko umetoa shilingi Bilioni 1.3 za Kitanzania zilizotumika kununua mitambo ya kisasa, kufunga mifumo ya umeme kutoka TANESCO, Ukarabati wa jengo na kufunga mashine ambapo hatua hiyo imefikia asilimia 85.
Sambamba na hilo alieleza kuwa, kiwanda kitasindika tangawizi hadi tani 10 kwa siku na kusambaza bidhaa zake katika soko la ndani na nje ya nchi ambapo kitauza unga wa tangawizi katika nchi za Kenya, Uganda , Malawi, Afika Kusini, Uholanzi na nchi za Bara la Asia.
Mkurugenzi alibainisha zaidi ya ajira 40 zinatarajiwa kuzalishwa pindi uzalishaji wa kiwanda utakapoanza ambapo itaongeza tija kwa vijana na kutoa wito kuichangamkia fursa ya uwepo wa kiwanda hicho.
Waziri Lukuvi Aifumua Idara Ya Ardhi Halmashauri Ya Wilaya Chamwino.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amefanya ziara ya kushtukiza leo katika ofisi za ardhi za Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino jijini Dodoma ambapo ameagiza kubadilishwa vituo vya kazi Mkuu wa Idara ya Ardhi Bwana Letare Sinda na Afisa Mipango Miji Bwana David Msemo.
Waziri Lukuvi amefikia uamuzi huo baada kukagua utunzaji wa nyaraka pamoja na maombi ya vibali vya ujenzi yaliyowasilishwa kwenye ofisi ya Mipangomiji kwenye Halmashauri hiyo ambapo, alikerwa na ukiukwaji wa sheria na miongozo ya kutoa vibali vya ujenzi na umilikishaji ardhi ambao umechangia malalamiko ya wananchi kuongezeka.
Lukuvi ameagiza Kamishna wa Ardhi na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi kutoka Makao makuu ya Wizara watume wataalam wengine haraka iwezekanavyo ili wakasimamie uandaaji wa nyaraka za umiliki pamoja na utoaji vibali vya ujenzi katika Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Ameongeza kwamba, Wilaya ya Chamwino ndiyo Wilaya pekee ambayo ilipewa upendeleo na Wizara wa kupatiwa vifaa vya Upimaji, gari la Idara ya ardhi na vifa vya Kompyuta lakini ndiyo Wilaya inayolalamikiwa zaidi katika mkoa wa Dodoma.
‘Jiji la Dodoma linakua kwa haraka sana, Wilaya ya Chamwino ndiyo Wilaya namba moja na Ikulu ipo ndani yake. Ni lazima iwe wilaya ya mfano kwenye utoaji huduma za sekta ya ardhi. Muda wa kufanya kazi kwa mazoea hakuna tena, kila mtaalam afuate miongozo iliyowekwa na Serikali ya kutolea huduma, Alisema Lukuvi’
Lukuvi Alisema, Wilaya ya Chamwino imekuwa na tamaa ya kuuza viwanja kwa gharama kubwa, kiasi cha kuwakatisha tamaa wananchi masikini na wanyonge ambao ndio wazawa wa Chamwino. Hali hii inapelekea wananchi kuyakimbia maeneo yao na kwenda kutafuta maeneo sehemu nyingine na kuanzisha Makazi holela.
Aliongeza kwamba, wananchi wachache wanaoweza kununua viwanja ndani ya Wilaya hiyo, bado wanakutana na changamoto nyingine ya gharama kubwa za vibali vya ujenzi ambapo hata kumbukumbu tuu za jumla ya maombi yaliyopokelewa na yaliyotolewa hakuna.
Mbali na sheria na miongozo kutokufuatwa, Waziri Lukuvi amesema maombi mengi ya vibali vya ujenzi hayajatolewa na hakuna nyaraka yeyote inaoonesha sababu zilizokwamisha maombi hayo.
“Haiwezekani mwananchi alete maombi ya kibali cha ujenzi yeye mwenye na asikifuatilie kama taratibu za utoaji huduma ni rafiki na ziko wazi, Alisema waziri Lukuvi”.
Aidha, Mhe.Waziri amesema kufanya kazi kwa mazoea na kutokuzingatia sheria, taratibu na kanuni katika utoaji wa huduma kunatengeneza mianya ya rushwa na kuzalisha malalamiko ya wananchi.
Katika muongozo wa utoaji vibali vya ujenzi uliotolewa hivi karibuni na Ofisi ya Rais TAMISEMI uliwataka wataalam wote wanaohusika kupitia maombi kuweka utaratibu wa kukutana wote kwa pamoja na kupitia maombi yaliyowasilishwa ili kutoa mwanya kwa kila mtaalam kujiridhisha na kipengele kinachomuhusu. Aidha muongozo huo uliwataka wataalam hao kuhakikisha kibali cha ujenzi kinatolewa ndani ya siku saba tangia maombi yalipowasilishwa.
Naibu Waziri Wa Fedha Na Mipango Azitaka Taasisi Za Elimu Ya Juu Kusimamia Malezi Na Maadili Ya Wanafunzi
Na Farida Ramadhani na Peter Haule, Mwanza
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Mwanaidi Ali Khamis, amevishauri vyuo vya elimu ya juu nchini kuhakikisha vinasimamia malezi na maadili ya wanafunzi wao kutokana na wengi wao kujiunga na masomo wakiwa na umri mdogo.
Mheshimiwa Mwanaidi ametoa rai hiyo wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi la miundombinu ya Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Kituo cha Mafunzo Kanda ya Ziwa – Mwanza kinachojengwa katika kijiji cha Kitumba wilayani Magu mkoani Mwanza kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 2.
Alisema hatua ya Serikali ya kuondoa ada na michango katika elimu ya msingi na sekondari, idadi ya wanafunzi wanaojiunga na masomo ya elimu ya juu imeongezeka baadhi yao wakiwa na umri mdogo huku kukiwa na changamoto ya maendeleo ya kiteknolojia (utandawazi), yanayoathiri tabia na mienendo yao.
Aidha, Mhe. Mwanaidi amekitaka Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, kuhakikisha kuwa kinafanya tafiti mbalimbali zitakazoibua suluhisho na changamoto zinazokwaza maendeleo ya wananchi hususani wa vijijini na kuziandika tafiti hizo kwa lugha rahisi ya Kiswahili ili tafiti hizo ziweze kuwanufaisha wananchi na kuchangia kujikwamua kiuchumi.
Vilevile amekishauri Chuo hicho kuboresha mitaala itakayovutia wanafunzi wengi zaidi wakiwemo wanaotoka nje ya nchi zikiwemo nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Nchi za maendeleo Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC) pamoja na kuanzisha vituo vya umahili ili kuwapa vijana ujuzi utakaosaidia wajiajiri na kujipatia kipato.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Profesa Martha Qorro, alisema kuwa ushauri uliotolewa na Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Mwanaidi Ali Khamis utafanyiwa kazi na chuo hicho wakianza na maadili na malezi ya vijana.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Profesa Hozen Mayaya, akitoa taarifa ya ujenzi wa Kituo hicho cha Mafunzo Kanda ya Ziwa -Mwanza, alisema ujenzi wa miundombinu umefikia asilimia 80 ukihusisha kumbi za mihadhara na madarasa.
“Mradi huu unahusisha ujenzi wa majengo mawili ya taaluma kila moja likiwa na ukumbi mmoja wa mihadhara wenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 440 kila mmoja na darasa moja lenye uwezo wa kuchukua wanafuzi 180 pamoja na ofisi 6 zenye uwezo wa kuchukua wafanyakazi 12.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Magu Bw. Salumu Kali, aliishukuru Wizara ya Fedha na Mipango na uongozi wa Chuo cha Mipango kwa kujenga miundombinu ya chuo katika Wilaya yake hatua itakayochochea maendeleo ya wilaya hiyo.
Alisema kuwa wananchi wa Kijiji cha Kitumba, wilayani Magu, walikipatia Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini ezari 20 bure kwa kutambua umuhimu na mchango wa elimu katika taifa na katika wilaya yao yenye idadi kubwa ya wanafunzi wanaohitimu elimu ya msingi na Sekondari wanaohitaji kujiendeleza kielimu.
Pamoja na pongezi hizo alimwomba Mheshimiwa Mwanaidi Ali Khamis kufikisha ombi lake kwa uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango ili wapatiwe zaidi ya shilingi milioni 750 walizoomba kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa ofisi ya Halmashauri ya Wialaya ya Magu.
Naibu Waziri Mabula Ashtushwa Halmashauri Kuingia Mikataba Na Makampuni Ya Urasimishaji Bila Kuyachunguza
Na Munir Shemweta, WANMM KILIMANJARO
Naibu Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula ameshangazwa na halmashauri za mkoa wa Kilimanjaro kuingia mikataba ya urasimishaji na makampuni zaidi ya nane ambayo yameshindwa kukamilisha kazi suala lililosababisha makampuni hayo kuanza kuchunguzwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU).
Akizungumza na Uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro, Wakurugenzi wa Halmashauri, watendaji wa sekta ya ardhi na Makampuni ya urasimishaji katika kikao chake kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkoa wa Kilimanjaro tarehe 8 Januari 2021 akiwa katika ziara ya siku moja, Dkt Mabula alisema haiwezekani wakurugenzi wote wa halmashauri kuingia mikataba na makampuni zaidi ya nane ya urasimishaji katika mkoa na yashindwe kukamilisha kazi.
” Wakurugenzi wote mko hapa wakati mnaingia mikataba na makampuni ya urasimishaji mliwachunguza kabla ya kuingia mikataba? maana haiwezekani mkoa mzima makampuni yashindwe kukamilisha kazi kwa wakati na naagiza halmashauri zifanye uchunguzi kabla ya kuyapa kazi makampuni” alisema Dkt Mabula.
Alisema, Makampuni ya upimaji hayatakiwi kwenda kinyume na mpango uliowekwa na halmashauri na yanatakiwa kufanya kazi kwa kwenda mtaa kwa mtaa na siyo mtu kwa mtu na kuongeza kuwa halmashauri zinatakiwa kuyachunguza na kuchukua makampuni yenye uwezo na mtaji na siyo kutegemea fedha za wananchi.
Aliiagiza Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipango Miji na Makampuni kuyachunguza makampuni yote ya urasimishaji ambayo hajakamilisha kazi na wakibaini kampuni zisizo kuwa na uwezo basi zifutwe kufanya kazi tena ya upangaji na upimaji nchini.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliongeza kwa kusema kuwa, Wizara ya Ardhi iliona jambo jema kushirikisha sekta binafsi katika zoezi la urasimishaji kwa lengo la kuongeza kasi ya upimaji na kusisitiza kuwa Wizara ya Ardhi inachotaka ni Kampuni inayopewa kazi ni kuwa na angalau asilimia 50 ya mtaji wa kufanya kazi badala ya kutegemea fedha za wananchi.
“Wizara inasema kama huna fedha usitegemee pesa za wananchi kuendesha kazi ya urasimishaji na tusiwafanye wananchi ndiyo mtaji kwa kuwa mwisho itakuwa kero kwa kushindwa kukamilisha kazi” alisema Dkt Mabula.
Mkurugenzi Mtendaji wa moja ya Kampuni za Urasimishaji katika mkoa wa Kilimanjaro ya KILI Surveys LTD Alphonce Mwanshinga alijitetea mbele ya Naibu Waziri Dkt Mabula kwa kueleza kuwa kampuni yake tayari imeshapima viwanja 2,795 na kulipwa shilingi milioni 283,361 huku ikiendelea kudai milioni 247,639,000 kutoka kwa wananchi.
Hata hivyo, alisema changamoto kubwa kwa kampuni yake kushindwa kukamilisha zoezi hilo kwa wakati ni kuwa walipoanza kazi waliendesha zoezi kulingana na uitikio wa wananchi na kuamua kupima kwa wale waliolipa fedha na kuongeza kuwa kampuni yake ya KILI Surveyers LTD inatarajia kukamilisha zoezi la upimaji katika mtaa waliopewa mwisho wa mwezi Januari 2021.
Baadhi ya Makampuni yaliyopewa kazi ya urasimishaji kwenye mkoa wa Kilimanjaro ni pamoja na Kili Surveys Ltd, Makazi Solution, EM& Contruction Ltd, Land Surveys and Consultancy Services pamoja na Kampuni ya EM Land Consultants.
SHIRIKA LA AGRI THAMANI LIMEWATAKA MADIWANI WA HALMASHAURI MULEBA KUBEBA AGENDA YA LISHE KWENYE MAENEO YAO
![]() |
| MKURUGENZI wa Shirika la Agri Thamani Mhe Neema Lugangira (MB) akiwasilisha mada ya lishe kwenye semina ya Madiwani wa Halmashauri ya Muleba iliyoandaliwa na Shirika hilo |
![]() |
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Emmanuel Sherembi akizungumza jambo wakati wa semina hiyo |
![]() |
| MWENYEKITI wa Halmashauri ya Muleba Emmanuel Sherembi akizungumza jambo wakati wa semina hiyo kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani Neema Lugangira (MB) |
![]() |
| KATIBU wa CCM wilaya ya Muleba akisisitiza jambo kwa Madiwani kuwa lazima ajenda ya lishe itekelezwe na waipe kipaumbele maana ipo kwenye ilani ya CCM ya Uchaguzi ya mwaka 2020/2021 |
MRATIBU wa Lishe kutoka Tamisemi Mwita Waibe na Mganga Mkuu wa wilaya ya Muleba Dkt Modest Mganga wakifurahia namna ambavyo semina ya Lishe imeendeshwa
MKURUGENZI wa Shirika la Agri Thamani Mh Neema Lugangira (MB) akigawa nakala ya mada kwa madiwani iliyokuwa inawasilishwa na Idara ya Afya ya Halmashauri ya Muleba
SHIRIKA la Agri Thamani Foundation limewataka Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera kuendelea kubeba ajenda ya lishe kwenye maeneo yao ili kuweza kudhibiti hali ya udumavu katika wilaya hiyo.
Semina hiyo imewafikia Madiwani wa Kata ,Madiwani wa Viti Maalumu kutoka Kata zote 43 za wilaya ya Muleba.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Agri Thamani Foundation ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Tanzania Bara anayewakilisha Asasi za Kiraia (NGOs) Mhe. Neema Lugangira (Mb.) wakati akizungumza na Madiwani, Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Wakuu wa Idara wa Wilaya ya Muleba wakati wa Semina ya Lishe iliyoandaliwa na Agri Thamani.
Amesema kuwa ili kupunguza udumavu katika wilaya ya Muleba ni kuhakikisha wananchi wanajikita katika mazao lishe pamoja na viongozi hao kushirikiana na watalaam wa lishe na kilimo ili kwenye vikao vya ngazi zao kuweza kutoa elimu iliyosahihi.
Mbunge Neema Lugangira ameongeza kuwa viongozi hao wanatakiwa kushirikiana na watalam wa afya kutoa tathimini ya mara kwa mara kuhusu hali ya lishe kwenye maeneo yao kwani watalam hao hawawezi kuingia sehemu zote kwa wakati mmoja.
"Sisi sote tuna jukumu la kujua hali ya lishe, udumavu n.k. tunapaswa kuangalia katika mtaa wetu, katika kijiji chetu hali ikoje ya lishe na tukikumbana na hali ya lishe duni na viashiria vyake tunatoa taarifa kwa wenzetu upande wa serikali” Alisema Mhe Neema Lugangira (Mb.)
Naye kwa upande wake,Mratibu wa Lishe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI,Mwita Waibe aliwaambia Madiwani kuwa Tamisemi imekuwa ikishirikiana na Agri Thamani kwa karibu huku akilipongeza Shirika hilo kutokana na kwamba ni NGO ambayo inafanya kazi za jamii na kuzifikisha ngazi ya jamii.
Mratibu Mwita aliwasisitizia madiwani wa Halmashauri hiyo waendelee kuyatafsiri mafunzo haya kwa vitendo ili Agri Thamani iweze kupata msingi wa kuandaa Programu zitazoshuka hadi ngazi ya vijiji.
Kwa upande mwingine, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Muleba Agnes Kassela aliwataka Madiwani wa Halimashauri ya Wilaya ya Muleba kwa kutekeleza maagizo hayo kuhusiana na Ajenda nzima ya Lishe kama ilivyo kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi 2020-2025 kwani sasa ni muda wa utekelezaji na wao ndio wasimamizi wakuu wa miradi ya maendeleo.
Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa Halamshauri ya Muleba Bwana Justus Magongo ameiliishukuru Shirika la Agri Thamani kwa niaba ya Wakuu wa Idara na Madiwani kwa kuwapatia elimu hiyo ya lishe ambayo ni muhimu sana.
Alisema watahakikisha wanabeba ajenda ya lishe kwa vitendo kwenye Halmashauri hiyo kupitia vikao vyao na mipango kazi ili kuweza kupunguza kiwango cha udumavu katika Wilaya hiyo.
Mwisho.
WASH Finance Director at Chemonics
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Title: WASH Finance Director Location: Tanzania Company Name: Chemonics International, Inc. Job Description: Chemonics seeks a WASH Finance Director for the anticipated USAID water, sanitation and hygiene (WASH) activity in Tanzania. The Activity’s overall objective is to expand the provision and governance of WASH services and the management of water resources through partnership with the government […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Sanitation & Hygiene Market Systems Director at Chemonics
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Title: Sanitation & Hygiene Market Systems Director Location: Tanzania Company Name: Chemonics International, Inc. Job Description: Chemonics seeks a Sanitation & Hygiene Market Systems Director for the anticipated USAID water, sanitation and hygiene (WASH) activity in Tanzania. The Activity’s overall objective is to expand the provision and governance of WASH services and the management of water […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Water Security & Stewardship Director at Chemonics
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Title: Water Security & Stewardship Director Location: Tanzania Company Name: Chemonics International, Inc. Job Description: Chemonics seeks a Water Security & Stewardship Director for the anticipated USAID water, sanitation and hygiene (WASH) activity in Tanzania. The Activity’s overall objective is to expand the provision and governance of WASH services and the management of water resources through […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Monitoring & Evaluation Officer at SOS Children’s Villages Tanzania
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
SOS Children’s Villages Tanzania is a local non-government organization affiliated to SOS Children’s Villages International, a worldwide child care organization that provides orphaned and destitute children with a permanent home and educational opportunities. Established 60 years ago, SOS Children’s Villages International the umbrella organization, currently has Children’s Villages and other projects in 135 countries around […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Procurement and Logistics Officer at SOS Children’s Villages Tanzania

Executive Assistant to the National Director at SOS Children’s Villages Tanzania
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
SOS Children’s Villages Tanzania is a local non-government organization affiliated to SOS Children’s Villages International, a worldwide child care organization that provides orphaned and destitute children with a permanent home and educational opportunities. Established 60 years ago, SOS Children’s Villages International the umbrella organization, currently has Children’s Villages and other projects in 135 countries around […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
National Office Administrator at SOS Children’s Villages Tanzania

Mama Msaidizi wa SOS Children’s Villages 4 Posts at SOS Children’s Villages Tanzania
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
SOS Children’s Villages Tanzania is a local non-government organization affiliated to SOS Children’s Villages International, a worldwide child care organization that provides orphaned and destitute children with a permanent home and educational opportunities. Established 60 years ago, SOS Children’s Villages International the umbrella organization, currently has Children’s Villages and other projects in 135 countries around […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Program Officer at SOS Children’s Villages Tanzania

Associate Legal Officer (P2) at IRMCT
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Job Opening Posting Title: ASSOCIATE LEGAL OFFICER, P2 Job Code Title: ASSOCIATE LEGAL OFFICER Department/Office: International Residual Mechanism for Criminal Tribunals Duty Station: ARUSHA Posting Period: 07 January 2021 – 05 February 2021 Job Opening Number: 21-Legal Affairs-RMT-145862-R-Arusha (R) Staffing Exercise N/A Org. Setting and Reporting The post is located in the Office of the […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details