Wednesday, 18 November 2020
Picha : TAMASHA LA SITA LA JINSIA NGAZI YA WILAYA LAZINDULIWA MBEYA...DC NTINIKA ASISITIZA BAJETI YA MRENGO WA KIJINSIA
Waziri Mkuu Azindua Uchepushaji Maji Mto Rufiji.....Misri yaahidi kufundisha Watanzania 25 kwa miaka mitatu mfululizo
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua kazi ya uchepushaji maji ya mto Rufiji kwenda kwenye handaki ili kupisha ujenzi wa tuta kuu la bwawa la kufua umeme na kusema mradi huo utawezesha nchi kuwa na umeme mwingi na wa kutosha lakini pia utawezesha kufanya biashara ya umeme na nchi za jirani.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatano, Novemba 18, 2020) wakati akizungumza na wananchi na wadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo kwenye eneo la mradi, mkoani Pwani wakati akikagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa uzalishaji umeme kwa kutumia maporomoko ya mto Rufiji.
“Upatikanaji wa umeme wa bei nafuu na uhakika nchini kwetu utachochea ukuaji na mapinduzi katika sekta ya viwanda nchini kwa kushusha gharama za uendeshaji viwandani, kukabiliana na mfumuko wa bei, kuwezesha ushindani wa bidhaa za Tanzania katika masoko ya Afrika Mashariki, Afrika na duniani,” amesema.
Amesema hatua hiyo itaenda sambamba na kuvutia uwekezaji mkubwa, wa kati na mdogo katika sekta mbalimbali nchini kutokana kupungua kwa gharama za umeme katika uzalishaji ikiwa ni pamoja na kuwawezesha Watanzania wote kumudu gharama za umeme mijini hadi vijijini.
Waziri Mkuu amesema mradi huo ambao unafadhiliwa na Serikali kwa asilimia 100 kwa gharama ya sh. trilioni 6.557, unasimamiwa na Mhandisi Mshauri wa Kitanzania kwa asilimia 100. “Serikali imeendelea kuwaamini na kuwatumia wataalamu wa Kitanzania katika kusimamia miradi mikubwa, na kwa kutambua hilo mradi huu unasimamiwa na Mhandisi Mshauri wa Kitanzania kwa asilimia 100,” amesema.
Amesema mradi huo wa kufua umeme kwa kutumia maji wa Julius Nyerere ni mkubwa, wa kimkakati na wa aina yake katika ukanda wa Afrika, ukiwa ni wa kwanza kwa ukubwa kwa Afrika Mashariki na wa nne barani Afrika na akasisitiza kuwe na usimamizi makini na wa viwango ili kuhakikisha unakamilika katika muda uliopangwa.
“Nimeambiwa kwamba, mradi huu unaenda sambamba na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovoti 400 kutoka eneo la mradi hadi Chalinze, yote hii ni kuhakikisha umeme unaotoka hapa unaingizwa kwenye gridi ya Taifa.”
Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na washiriki wa hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said alisema hadi kufikia Oktoba 31, mwaka huu, mradi huo ulikuwa umeshatoa ajira za moja kwa moja 6,364 ambapo kati ya hizo, ajira 5,728 zikiwa ni za Watanzania.
Akielezea hatua iliyofikiwa kwenye usambazaji wa umeme nchini, Katibu Mkuu huyo alisema kwamba hadi sasa vijiji 9,884 kati ya 12,264 viliyopo nchini vimekwishapatiwa umeme. “Tuna mpango wa kukamilisha vijiji vyote vilivyobakia ndani ya miaka miwili ijayo,” alisema.
Wakati huohuo, Waziri wa Nyumba na Huduma za Mijini wa Misri, Dkt. Assem el Gazzar amesema Rais wa nchi hiyo, Abdel Fattah al-Sisi anafuatilia kwa karibu utekelezaji wa mradi huo ambao unajengwa kwa ubia na kampuni za Arab Contractors and El Sewedy Electric kutoka Misri.
“Rais wetu anafuatilia kwa karibu maendeleo ya mradi huu na tunatarajia utaisha ndani ya muda uliopangwa. Kukamilika kwa mardi huu kutahakikisha nishati ya umeme inakuwa ya uhakika katika kuleta maendeleo,” alisema.
Katika hatua nyingine, Waziri wa Umeme na Nishati Jadidifu wa Misri, Dkt. Mohamed Shaker El-Markabi alisema Serikali ya nchi hiyo iko tayari kubadilishana uzoefu na wizara ya nishati ya Tanzania na kwamba itatoa mafunzo kwa Watanzania 25 kwa miaka mitatu ijayo.
“Tunawapongeza Watanzania kwa hatua hii ya kihistoria. Wizara yetu iko tayari kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo na Wizara ya Nishati ya Tanzania, na katika kipindi cha miaka mitatu ijayo, tutatoa mafunzo (full training) kwa Watanzania 25,” alisema.
Alisema upatikanaji wa umeme wa uhakika ni suala la muhimu kwa wananchi kama ilivyo kwa maji na huduma nyingine muhimu. “Uzalishaji wa megawati 2,115 utaiwezesha Tanzania kuwa na umeme wa uhakika, itaongeza kiwango cha upatikanaji wa umeme na kutengeneza fursa za ajira na za kibiashara.”
“Ndani ya miaka mitatu ijayo, Tanzania itakuwa kinara wa uzalishaji nishati katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Mradi wa umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) utakapokamilika, unatarajiwa uweze kutoa ziada ya kuuza kwenye nchi za jirani,” alisema.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka alisema ujenzi wa mradi huo umefikia asilimia 75.76 na kwamba uchepushaji wa maji ya mto uliofanyika sasa ni wa muda tu ili kupisha ujenzi wa tuta kuu. “Tumekwepesha umbali wa mita 700 tu, na tukimaliza ujenzi wa tuta, tutarudisha maji ya mto kwenye njia yake ya awali,” alisema.
Wahamiaji Haramu 36 Wakamatwa Dar, RC Kunenge Atoa Onyo
Vyombo vya ulinzi na usalama mkoa wa Dar es salaam, vimefanikiwa kuwatia mbaroni wahamiaji haramu 36 raia wa Ethiopia na Somalia walioingia nchini kinyume na taratibu, ambapo mkuu wa mkoa huo Aboubakar Kunenge ametoa onyo kali kwa raia wa Tanzania, wanaoshiriki kuwafadhili na kuwasafirisha ili wapate fedha.
Kunenge amesema Wahamiaji hao walikamatwa usiku wa kuamkia November 15, 2020 kwenye fukwe za Mbweni ambapo kati yao, 30 wanatoka nchini Ethiopia na Sita wanatokea nchini Somalia.
Aidha Kunenge amesema hata utaratibu unaotumika kusafirisha watu hao unakiuka sheria, haki na utu wa binadamu sababu wengi wao wanafungiwa kwenye kontena zisizokuwa na hewa na pindi wanapobainika kufariki Dunia maiti zao hutupwa kwenye vichaka.
Pamoja na hayo RC Kunenge amevipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya.
Kwa upande wake Afisa uhamiaji mkoa wa Dar Es Salaam, Kamishna Msaidizi Edmund Mrosso amesema kinachofuata baada ya wahamiaji hao kukamatwa watafikishwa mahakamani kwa kosa la Kuingia nchini kinyume na taratibu.
Aidha Kamishna Mroso amesema kwa wale wanaowasafirisha au kuwahifadhi wahamihaji hao, adhabu inaelekeza kifungo cha miaka 20, faini ya shilingi milioni 20 au vyote kwa pamoja ikiwa ni pamoja na kutaifisha mali zilizotumika.
V30 Cubex Driller at AUMS
This position is responsible in carrying out Underground V 30 Cubex service & slot holes as well as some production drilling of various sized holes, and other tasks directed by the Shift Supervisor. African Underground Mining Services (AUMS) is an international leader in mechanized hard rock underground mining. AUMS is part of Perenti (Formerly the Ausdrill […]
The post V30 Cubex Driller at AUMS appeared first on Udahiliportal.com.
Yanga SC yamsimamisha kazi Katibu Mkuu
KAMATI ya Utendaji ya klabu ya Yanga imemsimamisha kazi Kaimu Katibu Kkuu wa klabu hiyo, Wakili Simon Patrick ambaye pia alikuwa mkurugenzi wa sheria na wanachama ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili ambazo hazikuwekwa wazi.
Maamuzi hayo yamekuja mara baada ya kamati hiyo kufanya kikao cha dharura kilichofanyika tarehe 17 novemba 2020, kwa ajili ya kujadili swala hilo.
Katika taarifa yao ambayo imesainia na Mwenyekiti wake, Dk. Mshindo Msolla imeleza kuwa uongozi wa klabu hiyo, ili kuhakikisha haki inatendeka kamati ya utendaji itateuwa kamati huru kuchunguza jambo hili na kutoa maamuzi yenye tija kwa pande zote.
Wakili Simon amekaimu nafasi hiyo ya katibu mkuu mara baada kuondolewa kwa aliyekuwa katibu mkuu wa klabu hiyo Dk. David Luhago tarehe 16 Juni, 2020.
Security Assistant Grade II at Kariakoo Markets Corporation
Kariakoo Markets Corporation is an autonomous Government Institution established under the Kariakoo Market Corporation Act no 36 of 1974 (Revised by the Act No 16 of 1985, to manage and control the Kariakoo Market, establish and manage other markets within Dar es salaam Region. Administratively the Kariakoo Markets Corporation reports to the President’s Office – […]
The post Security Assistant Grade II at Kariakoo Markets Corporation appeared first on Udahiliportal.com.
Office Attendant Grade II at Kariakoo Markets Corporation
Kariakoo Markets Corporation is an autonomous Government Institution established under the Kariakoo Market Corporation Act no 36 of 1974 (Revised by the Act No 16 of 1985, to manage and control the Kariakoo Market, establish and manage other markets within Dar es salaam Region. Administratively the Kariakoo Markets Corporation reports to the President’s Office – […]
The post Office Attendant Grade II at Kariakoo Markets Corporation appeared first on Udahiliportal.com.
Assistant Trade Officer Grade II – 3 posts at Kariakoo Markets Corporation
Kariakoo Markets Corporation is an autonomous Government Institution established under the Kariakoo Market Corporation Act no 36 of 1974 (Revised by the Act No 16 of 1985, to manage and control the Kariakoo Market, establish and manage other markets within Dar es salaam Region. Administratively the Kariakoo Markets Corporation reports to the President’s Office – […]
The post Assistant Trade Officer Grade II – 3 posts at Kariakoo Markets Corporation appeared first on Udahiliportal.com.
Clerk of Works at African Wildlife Foundation
Classroom Africa (CA) is AWF’s Education Program that seeks to improve educational outcomes for children in schools based in communities within or adjacent to critical wildlife habitats; by improving access to quality education that promotes greater participation in, and support for, AWF’s conservation efforts. Since its inception in 2013 Classroom Africa focused on building world […]
The post Clerk of Works at African Wildlife Foundation appeared first on Udahiliportal.com.
Serikali yafunga kamera 306 ukuta wa madini Mirerani
Asteria Muhozya na Issa Mtuwa, Mirerani
Kwa mara nyingine tena Ukuta unaozunguka Migodi ya Tanzanite Mirerani wenye urefu wa kilomita 24.5 umeingia kwenye historia nyingine baada ya kufungwa jumla ya Kamera 306 za Usalama zenye uwezo wa kufanya kazi katika mazingira yoyote ikiwemo kumbaini mhalifu.
Kamera hizo zimewekwa kufuatia kuwepo umuhimu wa eneo husika kufungwa mfumo wa CCTV kwa lengo la kugundua vitu na watu wanaoingia eneo la Ukuta, kuhifadhi taarifa za Kudumu, kuzuia wanaokusudia kufanya uhalifu na kufuatilia matukio yanayofanyika eneo la ukuta huo.
Hayo yalibainishwa Novemba 17, 2020 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila wakati wa Hafla fupi ya kukabidhi mfumo huo kwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
“Kamera hizi zina uwezo wa kurekodi matukio wakati wa usiku, mchana, wakati wa jua, Kwenye vumbi, wakati wa mvua na zina uwezo wa kumtambua mhalifu aliyekwishafanya uhalifu kwenye Ukuta,’’ alisema Prof. Msanjila.
Kufuatia kufungwa kwa mfumo huo, Prof. Msanjila aliwaasa Wafanyakazi wa Wizara ya Madini na Taasisi zilizo chini yake kuendelea kufanya kazi kwa bidii huku wakisisitiwa kuzingatia Kanuni na Maadili ya Utumishi wa Umma.
Aidha, alitumia fursa hiyo kutoa rai kwa wadau wote katika eneo tengefu la Mirerani kujiepusha na vitendo vya rushwa, utoroshaji wa Madini ama kukiuka Sheria, Kanuni, Taratibu na miongozo mbalimbali inayosimamia Sekta ya Madini na kuiwezesha Serikali kufikia malengo yake na kuwapo kwa tija katika Uwekezaji mkubwa wa miundombinu uliofanyika hapa Mirerani.
Pia, kufuatia matokeo chanya ambayo yanaonekana katika sekta ya madini,Prof. Msanjila alimwakikishia Rais John Magufuli na watanzania kuwa wizara yake kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ndani na nje itahakikisha kuwa sekta hiyo inadhihirisha kuwa muhimu katika kujenga wa nchi.
Akizungumzia mipango mingine iliyobaki kukamilishwa katika eneo hilo, alisema kwamba ujenzi wa Scanner katika geti kuu la kuingia uko mbioni kujengwa.
Akizungumzia mchakato wa zabuni, alisema kabla ya kutangazwa kwa kandarasi hiyo, zipo kampuni zilizojitokeza huku zikianisha gharama kubwa Na kueleza Kampuni ya StarFix iliyoshinda zabuni hiyo ilitumia shilingi bilioni 1.2 kukamilisha kazi husika.
‘’Kampuni ya kwanza iliandika andiko la shilingi bilioni 83, la bilioni 76, la tatu bilioni 33, la Nne bilioni 27 lakini huyu mzalendo Kampuni ya Starfix Enterprise ametumia gharama ya Shilingi Bilioni 1.2. Uwekezaji huu wa Serikali kwa pamoja umegharimu takriban kiasi cha shilingi bilioni 4.284,923,915.98,’’ alisema Prof. Msanjila.
Akielezea kazi nyingine zilizofanyika katika eneo hilo, Prof. Msanjila alisema Wizara imekamilisha ujenzi wa jengo la Kituo cha Pamoja ndani ya Ukuta, uwekaji miundombinu ya umeme na taa kuzungukia Ukuta umekamilika.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Timu ya Wataalam waliosimamamia kufungwa kwa mradi huo akieleza namna kamera hizo zinavyofanya kazi alisema kuwa, zina uwezo wa kuhakikisha maeneo yote ya ukuta pamoja na maeneo mengine ikiwemo Geti Kuu la kuingilia, chumba cha kuthaminisha madini na vyumba vingine vinaonekana muda wote. Kituo Maalum (CCTV Control Room) cha uangalizi wa mienendo mbalimbali inayooneshwa na kamera zilizofungwa kimekamilika na kuanza kufanya kazi.
‘‘Mfumo uliyofungwa una uwezo wa kuonesha maoneo yote vilevile uwezo wa kufanya kazi Kwenye mazingira yote wakati wa mvua, jua Kali, vumbi, hivyo kutoruhusu Tukio lolote kupiga bila kurekodiwa, unauwezo kwa kutoa taaifa mubashara kwa wanaousimamia pindi kuna mtu anaporuka ukuta au matukio yaliyoanishwa kwenye mfumo kama hatarishi,’’ alisisitiza Moshiro.
Pia, alieleza kuwa, mfumo huo unao wezo wa kuwabaini wale wote waliokwishafanya matukio ya uhalifu pindi wanapotaka kuingia kwenye lango kuu au wanapotaka kutoka nje ya eneo.
Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kuejnga Taifa Dkt. Faraji Mnyepe akipokea Mfumo huo alisema kuwa,yapo manufaa yanayotokana na kufungwa kwa kamera hizo ikiwemo kukuza Pato la Taifa kutokana na udhibiti uliokuwa unafanywa wasio waaminifu.
Alissitiza kuwa, wizara hiyo itaimarisha usalama kuzunguka Migodi yote, na kueleza kuwa jukumu la kulinda Usalama usalama ni la wizara hiyo na hivyo kuwahakikishia wachimbaji wote wadogo na Wakubwa usalama.
‘’Shahidi wa hili ni bilionea Saniniu Lazier. Tulimlinda tangu kuzalisha hadi anauza madini yake. Tunawaomba Wananchi na watanzania wote kulinda Madini Yetu, rasilimali ni jukumu letu wote. Ni malengo yangu wananchi wa Mirerani mtatusaidia kulinda Rasilimali hii,’’ alisema Dkt. Mnyepe.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mhandisi Zephania Chaula alichukua fursa hiyo kuwaalika wawekezaji katika Wilaya hiyo na kuelezea kuwa, mbali tanzanite wizara hiyo imebarikiwa kuwa na madini mengine ikiwemo Green garnet.
Mbali na kukabidhiwa kwa mfumo huo, Afisa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya StarFix Jason Kyando iliyofunga kamera hizo, alisema kuwa,
baada ya zoezi la kufunga mfumo kukamilika tulitoa mafunzo kwa wasimamizi wa mfumo huo ambao wote ni vijana wa Kitanzania walipatiwa mafunzo ya namna ya kusimamia mfumo huo na katika hafla ya jana Watapatiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo hayo.
Geological Technician at Bulyanhulu Gold Mine
POSITION DESCRIPTION: Bulyanhulu Gold Mine is seeking to recruit Geological Technicians to join our team. The successful candidate for this position is expected to align to the Barrick DNA and drive a change within his team and the business and on a practical note will ensure activities in the geology department are effectively planned and […]
The post Geological Technician at Bulyanhulu Gold Mine appeared first on Udahiliportal.com.
Rigger at Bulyanhulu Gold Mine
POSITION DESCRIPTION: Bulyanhulu Gold Mine is seeking to recruit Rigger to join our team. The successful candidate for this position is expected to align to the Barrick DNA and drive a change within his team and the business and on a practical note will ensure activities in the Engineering Section are effectively planned and undertaken in […]
The post Rigger at Bulyanhulu Gold Mine appeared first on Udahiliportal.com.
Trump amfuta kazi afisa wa uchaguzi aliyepinga madai yake
Trump amekataa kukubali kushindwa katika uchaguzi wa Marekani, akitoa madai yasiyo na ushahidi ya wizi mkubwa wa kura.
Hata hivyo, Maafisa wa Uchaguzi wanasema kura ya mwaka huu ilikuwa moja ya kura salama zaidi katika historia ya Marekani.
Wiki iliyopita Rais Trump alimfuta kazi Waziri wa Ulinzi, Mark Esper, huku kukiwa na ripoti kwamba alikuwa na wasiwasi juu ya utiifu wa mkuu huyo wa Pentagon.
Kumekuwa na tetesi mjini Washington DC kwamba kabla ya Trump kuondoka madarakani mwezi Januari, Mkuu wa CIA, Gina Haspel na mkurugeni wa FBI Christopher Wray huenda wakawa miongoni mwa wale watakaofutwa kazi na Trump.
Boilermaker at Bulyanhulu Gold Mine
POSITION DESCRIPTION: Bulyanhulu Gold Mine is seeking to recruit Boilermakersto join our team. The successful candidate for this position is expected to align to the Barrick DNA and drive a change within his team and the business and on a practical note will ensure activities in the Engineering Section are effectively planned and undertaken in a […]
The post Boilermaker at Bulyanhulu Gold Mine appeared first on Udahiliportal.com.
Fitter at Bulyanhulu Gold Mine
POSITION DESCRIPTION: Bulyanhulu Gold Mine is seeking to recruit Fitter to join our team. The successful candidate for this position is expected to align to the Barrick DNA and drive a change within his team and the business and on a practical note will ensure activities in the Underground Shaft Maintenance are effectively planned and […]
The post Fitter at Bulyanhulu Gold Mine appeared first on Udahiliportal.com.