"Tume ya uchaguzi imeteua wagombea wa kiti cha Rais/Makamu wa Rais kutoka vyama 15 vya siasa. Katika uteuzi huo wanawake wawili walijitokeza na kuteuliwa kugombea kiti cha Urais na wanawake watano walijitokeza na kuteuliwa kugombea nafasi ya Makamu wa Rais",alifafanua Nuru
Friday 2 October 2020
Picha : TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) YAKUTANA NA WADAU WA UCHAGUZI SHINYANGA… ‘YAONYA UVUNJIVU WA AMANI KWA KISINGIZIO CHA UCHAGUZI’
"Tume ya uchaguzi imeteua wagombea wa kiti cha Rais/Makamu wa Rais kutoka vyama 15 vya siasa. Katika uteuzi huo wanawake wawili walijitokeza na kuteuliwa kugombea kiti cha Urais na wanawake watano walijitokeza na kuteuliwa kugombea nafasi ya Makamu wa Rais",alifafanua Nuru
MGOMBEA URAIS DR. JOHN POMBE MAGUFULI KESHO KUUNGURUMA ZANZIBAR..WASANII KIBAO WATAKUWEPO
AIRO AWASHUKIA WANAODAI HAMUUNGI MKONO CHEGE....ASEMA NI NJAMA ZA WAPINZANI KUWACHONGANISHA WANA CCM
Polisi Dar es Salaam wasitisha wito wa kumuita Tundu Lissu
“Jeshi la Polisi limesitisha wito huo na kumtaka Tundu Lissu kuendelea na kampeni zake za Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020.”
“Jeshi la polisi limeona ni vema kutumia busara kumuacha Lissu kuendelea na ratiba zake kipindi hiki cha kampeni na kwa kuwa tayari IGP Sirro alishatoa maelekezi kwa Lissu kuripoti Kituo cha Polisi Moshi Mkoa wa Kilimanjaro. Hivyo Jeshi la Polisi Kanda Maalum limesitisha wito huo,” amesema Kamanda Mambosasa.
SHIRIKA LA UWO KUTOA FARAJA KWA WAHANGA WA AJALI NCHINI
Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi isiyo kuwa ya Kiserikali ya Utu Wangu Organization (UWO) Fatuma Mgeni, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mjini hapa jana kuhusu kuanzishwa kwa Asasi hiyo yenye makao makuu yake mkoani Singida.
Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi isiyo kuwa ya Kiserikali ya Utu Wangu Organization (UWO) Fatuma Mgeni, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) huku akionesha mguu uliojeruhiwa katika ajali aliyoipata Kibaha kwa Mathias mkoani Pwani Desemba 5, 2018.
Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi isiyo kuwa ya Kiserikali ya Utu Wangu Organization (UWO) Fatuma Mgeni, akionesha cheti cha usajili wa Asasi yake ya Utu Wangu Organization (UWO) kwa waandishi wa habari.
Na Dotto Mwaibale, Singida.
WAHANGA wa ajali hapa nchini ambao wanakosa huduma baada ya kutelekezwa ama kutokuwa na ndugu wataanza kupatiwa msaada wa hali na mali kutoka Asasi isiyo kuwa ya Kiserikali ya Utu Wangu Organization (UWO) yenye makao makuu yake mkoani hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi hiyo Fatuma Mgeni ambaye ni mhanga wa ajali na Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Mkoa wa Pwani, Mkufunzi, Mwamuzi na Kocha wa Mchezo wa Mpira wa Meza (Table Tennis) ngazi ya kwanza ya Dunia, alisema jamii bado ipo nyuma kusaidia wahanga wa ajali ambao wanakosa msaada na kuiachia Serikali ambayo ina majukumu mengi.
"Suala la kuwasaidia wahanga wa ajali lipo ndani ya uwezo wa wanajamii wenyewe kikubwa ni jamii kuhamasika na kuwa na moyo wakusaidia wahanga hao" alisema Mgeni.
Alisema lengo la kuanzisha asasi hiyo ni baada ya kupata ajali Kibaha kwa Mathias na kujeruhiwa vibaya mguu wake wa kulia na kukaa Hospitali ya Rufaa ya Tumbi Kibaha karibu mwaka mmoja tangu Desemba 5, 2018 hadi leo akipatiwa matibabu ingawa yupo nje ya hospitali.
Mgeni alisema akiwa hospitalini ndipo aliona changamoto ya maisha ya wahanga wa ajali ambao walikuwa hawana msaada baada ya kutelekezwa na jamaa zao na wengine kutokuwa na ndugu kabisa licha ya kupatiwa matibabu.
"Niliguswa na jambo hili nikaona nianzishe asasi hii kwa ajili ya kutoa matumaini kwa wahanga hao kwa kushirikiana na jamii ikiwa ni kumuunga mkono Rais Dkt.John Magufuli za kuboresha huduma katika sekta ya afya na kuhakikisha wahanga hao wanapata haki zao kutokana na majanga walioyapata na kuwa na afya bora ili waweza kurudi katika afya zao za zamani na kuweza kufanya shughuli za maendeleo na kuinua uchumi wao binafsi na Taifa kwa ujumla." alisema Mgeni.
Mgeni alisema kumekuwa na dhana potofu kuwa wahanga wa ajali ni lazima wasaidiwe mahitaji yote na Serikali wakati kumbe jamii ikielimishwa inaweza kuwa sehemu ya kutoa faraja kwa wahanga hao kwa kupambana na changamoto zao kuanzia pale wanapopata ajali mpaka kupona kwao wakiwa wazima au na ulemavu uliotokana na ajali.
Aidha Mgeni alisema changamoto kubwa iliyopo ni kwa jamii kuwa nyuma katika jambo hilo ambapo imefikia baadhi ya watu kuwatelekeza wagonjwa hospitali na majumbani na kuwaacha wakiteseka na kukosa matumaini ya maisha.
Alisema kupitia Shirika hilo ambalo limesajiliwa na litakuwa likifanya kazi mikoa yote Tanzania Bara litakuwa likijihusisha zaidi kwa ajili ya kuhamasisha jamii kwa ajili ya kuwasaidia wahanga hao wa ajali.
Mgeni alitumia nafasi hiyo kuwa pongeza madaktari na wauuguzi na wafanyakazi wote wa Hospitali ya Rufaa ya Tumbi Kibaha kwa jitihada zao kubwa za kitabibu wanazo zitoa kwa jamii hasa kwa watu wanaofikishwa katika hospitali hiyo baada ya kupata ajali kwa kuwapa matibabu kwanza bila ya kuwadai fedha na kuwa ana amini hata hospitali zingine hapa nchini zinafanya utaratibu huo.
Mgombea ubunge jimbo la Bariadi Mhandisi Andrea Kundo aahidi kumaliza changamoto ya tembo kuvamia makazi.
Bariadi, Mgombea ubunge jimbo la Bariadi Mhandisi Andrea Kundo, Ameahidi kumaliza kero ya wanyama( tembo ) kuvamia makazi ya wakazi wa kata ya Gilya na Gibeshi katika wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.
Mhandisi Kundo aliyasema hayo jana alipo kuwa katika mkutano wa kuomba kura kwa wananchi wa kata hizo na kusema kuwa changamoto ya Tembo kuvamia makazi imakuwa ni ya muda sasa hivyo ni muda muafaka kuweza kuimaliza.
Aliongeza kuwa licha ya uwepo wa juhudi za kuhakikisha tembo hao hawaingii kwenye makazi lakini inabidi kuongeza nguvu ili kuhakikisha wananchi wanakuwa salama muda wote.
"Kumekuwa na tembo ambao wamekuwa ni tatizo kubwa kwa wananchi sababu wanaharibu mazao wakati wa mavuno na hata kusababisha vifo, hivyo nitahakikisha magari ya doria za polisi yanakuwa mengi maeneo haya ili tembo waweze kudhibitiwa kuingia katika makazi," alisema Mhandisi Kundo.
Jambo ambalo wananchi wa kata hizo wamelitaja kuwa ni licha ya uwepo wa changamoto zingine lakini hilo ni tatizo kubwa zaidi kwani uvamizi wa wanyama hao kwenye makazi unawaachia balaa la njaa.
Hali inayopelekea mazao yao wanayo vuna kutoka mashambani kwenda kuyahifadhi vijiji vya nkololo na Ihusi umbali wa zaidi ya kilometa 15 ili kuwakepa wanyama hao kwani wanapoingia vijijini wanavunja nyumba na kula mazao yote wanayoyakuta.
Hivyo njia hiyo ya kuhifadhi vijiji vya jirani inafanya mazao yabaki salama lakini changamoto inakuja pale wanapohitaji chakula kutokana na umbali uliopo kwenda kuvifata vyakula vyao kwa ajili ya familia zao.
"Tembo anapo vamia kwenye kaya anabomoa nyumba na anakula chakula chote anachokikuta wanakula michembe, mahindi hata unga na ni ngumu kwafukuza na wengine ni wabishi akigoma kuondoka inabidi wewe ndiye umkimbie," Alisema Monwa Kilatu mkazi wa kata Ihula.
Kwandu Maluguabili alieleza hali anayokutana nayo wanyama hao wanapofika katika makazi yake "Nyumbani nilipoweka mahindi huwa wanakuja kubomoa nyumba wanakula chakula na kuharibu kila wanachokutana nacho lakini baada ya kuwa hatuna chakula hatupati msaada wowote hivyo tunabaki bila chakula".
Wahanga hao walisema kuwa wanahitaji msaada wa serikali ili kuweza kuwadhibiti wanyama hao kwa sababu juhudi zao zinagonga amwamba kutokana na namna ambavyo wamekuwa wakiwafukuza kienyeji hali inayosababisha mapambano kati yao na kusababisha vifo kwa baadhi ya vijana wao.
Tangu mwaka 2017 tembo walinza kupita katika vijiji vya kata hizi wakiwa wanatafuta njia, na tangu waka 2018 wanyama hawa walianza kuvamia makazi nyakati za usiku na kufanya uharibifu katika makazi.
Mwisho.
TARURA yatekeleza ahadi za Magufuli
Na. Erick Mwanakulya, Kagera.
Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), unaendelea kutetekeleza miradi ya Ahadi za Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kukamilisha ujenzi wa Barabara zenye urefu wa Km 2.76 kwa kiwango cha lami katika Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, mkoani Kagera.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo, Meneja wa TARURA katika Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Mhandisi Dativa Telesphory alifafanua kuwa utekelezaji wa miradi ya Ahadi za Mhe. Rais umekamilika kwa asilimia 100 baada ya ujenzi wa barabara hizo kwa kiwango cha lami kukamilika na kuanza kutumika.
“Kabla ya TARURA kuanzishwa, Wilaya ya Muleba haikuwa na lami hata Mita 1 lakini hadi sasa kupitia kuanzishwa kwa Wakala na pia utekelezaji wa miradi ya Ahadi za Mhe. Rais tumetekeleza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami zenye urefu wa Km 2.76 ambazo zimekamilika na wananchi wameanza kunufaika na ujenzi wa barabara hizi”, alisema Mhandisi Dativa.
Mkazi wa Muleba Bi. Edvina Jackson ameishukuru Serikali kwa kutengeneza barabara za lami kwenye eneo lao ambalo lilikuwa limesahaulika kwa muda mrefu kwani kwa kiasi kikubwa ujenzi wa barabara hizo umesaidia kupunguza kero ya usafiri na kufanya barabara hizo kupitika muda wote.
‘‘Tunashukuru sana Serikali barabara ni nzuri na pia usimamizi ni mzuri, pale mwanzoni tulikuwa tunapata shida kwenda mashambani na hata masokoni, sasahivi barabara ni nzuri hakuna vumbi wala matope katika kipindi cha mvua na kiangazi”, Bi. Edvina.
Aidha, mbali na utekelezaji wa miradi ya Ahadi za Mhe. Rais, TARURA wilaya ya Muleba imetekeleza ujenzi wa Daraja la Kishara lenye urefu wa Mita 36 katika Mto Ngono linalounganisha Kata za Katoke, Kamachumu na Kata ya Mafumbo ambapo kwa mujibu wa meneja wa TARURA katika Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, amesema wananchi walikua wanazunguka umbali mrefu lakini sasa kero hiyo imeisha.
Naye, Mkazi wa Kitongoji cha Kyamuhaya Bi. Goodselda Liberius alisema kuwa upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii katika eneo hilo umerahisishwa na uwepo wa daraja hilo kwasababu umewasadia kuvusha mazao yao na bidhaa nyingine za biashara kwa urahisi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
“Tunashukuru kwa kujengewa daraja hili kwasababu limekuwa ni mkombozi kwa sisi wafanyabiashara kusafirisha mazao yetu na tunaishukuru Serikali kwa kutujengea daraja hili,” alisema Goodselda.
Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijni (TARURA) katika Halmashauri ya Wilaya ya Muleba unaendelea na kazi mbalimbali zikiwemo za matengenezo ya barabara na vivuko katika Wilaya hiyo ili kuwawezesha wananchi kusafiri na kusafirisha bidhaa zao kwa urahisi.
Trump na Mkewe wakutwa na virusi vya corona
Rais Donald Trump wa Marekani amesema kwamba yeye na mke wake Melania Trump wamepatikana na virusi vya corona na wako kwenye karantini. Ametoa tangazo hilo kwenye mtandao wa Twitter.
Tangazo hilo linawadia baada ya Trump na wasaidizi wake wawili kuthibitishwa kuambukizwa virusi vya corona.
Hope Hicks, 31, mshauri wa rais amekuwa msaidizi wa karibu wa Bwana Trump kupatikana na virusi vya corona hadi hivi sasa.
Bi. Hicks alisafiri na yeye kwa ndege ya kijeshi kwenda kwenye mdahalo wa Televisheni uliofanyika Ohio mapema wiki hii.
Baadae Alhamisi, Bwana Trump alisema yeye na mke wake wanakwenda karantini baada ya Bi. Hicks kuthibitishwa kuwa na corona.
Tonight, @FLOTUS and I tested positive for COVID-19. We will begin our quarantine and recovery process immediately. We will get through this TOGETHER!
— Donald J. Trump (@realDonaldTrump) October 2, 2020
UN YAMUUNGA MKONO RAIS DKT MAGUFULI KUTOKOMEZA UKATILI WA MWANAMKE IKUNGI
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe, Dk. Rehema Nchimbi akizungumza baada ya uzinduzi wa mradi kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania Zlatan Milisic |
Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi na wawakilishi wa mashrika ya umoja wa mataifa ,wadau wa maendeleo na kmati ya ulinmzi na usalama ya wilaya ya Ikungi
Na John Mapepele, Ikungi
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe, Dk. Rehema Nchimbi leo amezindua miongoni mwa miradi mikubwa iliyowahi kutekelezwa nchini, mradi wa pamoja baina ya Mashirika ya Kimataifa ya UN Women na UNFPA kupitia ufadhiri wa Shirika la KOICA wa “Tuufikie usawa wa jinsia kupitia kuwawezesha wanawake na wasichana”.
Mradi huo utagharimu takribani bilioni 11.5 za kitanzania ambao utatekelezwa katika Wilaya ya Ikungi mkoani Singida na Msalala mkoani Shinyanga katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia sasa.
Dk. Nchimbi amesema lengo kuu la mradi huo ni kuchangia katika kuwawezesha wanawake na wasichana kuwakwamua kiuchumi na kijamii katika mikoa ya Singida na Shinyanga ili kufikia usawa wa kijinsia ambapo amewataka watendaji wote wa Serikali ambao watatekeleza mradi huo kuwa makini katika utekelezaji wa mradi ili malengo ya mradi huo yaweze kufikiwa.
Amesisitiza kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua kali watendaji ambao kwa namna moja au nyingine hawataendana na kasi ya utekelezaji wa miradi chini ya Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli ambapo amesema mrai huo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ili kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa KOICA Tanzania, Bi Jieun Mo, walengwa wasio wa moja kwa moja takribani wakazi 40,000 kutoka kwenye wilaya ya Ikungi na Msalala na walengwa wa moja kwa moja 2350 wanawake na wasichana kutoka katika wilaya hizo watanufaika na mradi huu ambapo pia wanaume na wanawake 6000 wa Wilaya ya Ikungi watanufaika kwenye eneo la muingiliano wa hati za ardhi.
Mo ameainisha kuwa shughuli za mradi katika kuwaweza wanawake kwenye eneo la uchumi zitajikiza zaidi kwenye kuimarisha uwezo wa wanawake na vijana wakulima ili waweze kutumia njia nzuri za kilimo na hali ya hewa katika uzalishaji wa alizeti na kilimo cha bustani, kukuza uuzaji wa pamoja, ujuzi wa ujasiriamali na wakala wa uchumi wa wanawake na kuimarisha usalama wa ardhi na umiliki.
Amesisiza kuwa shughuli hizo zitatekelezeka kupitia kuunda vikundi vya uzalishaji wa kilimo cha bustani kwa wanawake, kuunganisha wanunuzi wa vikundi vya wakulima vya wanawake,kusaidia ujenzi wa ghala kubwa moja la alizeti na kituo cha ukusanyaji kilomo cha bustani ili kuboresha uuzaji wa pamoja na utunzaji baada ya kuvuna,.
Alisema pia watatoa mafunzo ya ujasiriamali na ufikiaji wa habari za kifedha na kufuatilia ushauri wa usimamizi wa biashara na fedha na kukuza umiliki wa ardhi pekee na wa pamoja wa wanawake kupitia utoaji wa Hati za Haki za kimila za Makaazi(CCROs).
Mwakilishi wa UN Women Bi, Hodan Addou ameishukuru Serikali ya Tanzania kuwa ushirikiano wake katika kuhakikisha kuwa mradi huu hatimaye umeanza kutekelezwa ambapo amesema Shirika lake linaunga mkono juhudi za Serikali za kumkomboa mwanamke ili kuondokana na unyanyasaji wa kijinsia.
Bi Addou amesisitiza kuwa mradi huo utasaidia uwezeshaji kijamii kwa kuwawezesha wanawake kusimamia haki zao, kujenga ujuzi wa ujasiriamali wa wanawake na wasichana kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia na kuimarisha mifumo ya kuzuia na kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia kupitia kuanzisha na kuandaa vifaa katika madawati matatu ya Polisi ya Jinsia na Watoto.
Aidha alisema pia wataaanzisha vituo vitatu vya huduma ya dharura katika vituo vya wilaya, kuunda nafasi salama ya umma, kujenga uwezo wa nambari ya msaada ya watoto kitaifa, kuunda na kuimarisha Klabu za Wasichana na kuunda Kamati za ulinzi na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania Zlatan Milisic ameipongeza Serikali kwa kuwa na mradi huo na kuongeza kuwa mradi huo unaendana na malengo ya endelevu ya 2030 hususani lengo namba 5 kuhusiana kuwaendeleza wanawake katika nyanja mbalimbali na kuongeza kuwa mwaka 2020 ni mwaka muhimu sana kwa kuwa tunaelekea katika kutimiza miaka 25 ya azimio la wanawake la Beijing.
Ameeleza kuwa malengo endelevu ya 2030 yameeleza kuwa ili kufikia maendeleo ya nchi kumtambua mwanamke ni jitihada muhimu sana katika kuharakisha na kutimiza malengo yote ya maendeleo ambapo ameihakikishia Serikali ya Tanzania kuendelea kufanya kazi kwa karibu sana ili kuhakikisha wanawake wanakuwa chachu ya maendeleo katika nchi ya Tanzania.
Mwakilishi wa UNFPA, Dk. Winfred amesema kuwa uzinduzi wa mradi umelenga kutokomeza aina zote za unyanyasaji wa kijinsia na kuimarisha usawa katika jamii ikiwa ni pamoja na kuimarisha maisha ya wanawake ambapo amesisitiza kitovu cha matatizo ya kijinsia ni wanaume na mila na desturi potofu zinazomtazama mwanamke kwa kumdharirisha hivyo juhudi za makusudi zinatakiwa kufanywa za kuwaweka wanaume mbele ili kutokomeza unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Edward Mpogolo amesisitiza kuwa kazi nzuri zinazofanywa na Rais John Pombe Magufuli katika Nyanja mbalimbali ndiyo zinazoyafanya jumuiya za kimataifa kuunga mkono kwa kutoa misaada kupitia miradi mbalimbali hapa nchini.
Tundu Lissu atakiwa kuripoti kituo cha Polisi Moshi mkoani Kilimanjaro - IGP Sirro
IGP Sirro amesema hayo jana ambapo alimtaka Mwenyekiti wa Chama hicho Mhe. Freeman Mbowe kukaa na watu wake wazungumze suala la utii wa sheria bila shuruti.
Aidha IGP Sirro ameongeza kuwa Jeshi la Polisi limepewa mamlaka ya kulinda usalama wa raia na mali zao huku akiwaeleza kuwa hakuna mtu yeyote anayeweza kupambana na Jeshi hilo na kwamba wote wanaovunja sheria za nchi watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Mgr: Data Warehousing & Bus Analysis at Vodacom
Joining Vodacom is more than a job, what we do matters. We don’t just carry minutes, texts and data – we carry people’s lives. And that’s a huge responsibility. If you think for a minute about the people you rely on…the likelihood is they rely on us. Customers are at the heart of everything we […]
The post Mgr: Data Warehousing & Bus Analysis at Vodacom appeared first on Udahiliportal.com.
TBS YATOA MAFUNZO KWA WADAU WA MAFUTA YA KULA KANDA YA KATI
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetekeleza mpango wa mafunzo kwa wazalishaji, wasambazaji na wauzaji wa mafuta ya kula kanda ya kati, yaliyofanyika Mkalama, Kiomboi, Sikonge, Urambo, Shelui, Manispaa ya Tabora,Nzega, Igunga, Manispaa ya Singida, Kondoa Irangi, Kongwa, Mpwapwa, Kibaigwa, Chamwino, Itigi, Manyoni, Dodoma jiji na Bahi.
Mafunzo haya yamelenga kuwaelimisha wadau hao juu ya uzalishaji bora, uhifadhi sahihi wa bidhaa za mafuta haswa sehemu za kuuzia, ufungashaji sahihi na salama na umuhimu wa kuzingatia na kuweka taarifa sahihi na muhimu katika vifungashio.
TBS imetoa elimu hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya viwanda, SIDO, maafisa biashara, afya na maendeleo wa wilaya ili kuwajulisha wadau wa mafuta ya kula fursa zilizopo ndani ya Serikali ili kuwawezesha kuboresha bidhaa zao ziweze kukidhi matakwa ya viwango na hatimaye kupananua wigo wa soko la ndani na nje ya nchi na kuwafanya kuongeza uzalishaji utakaopelekea kuinua uchumi wao.
Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora (TBS),Bw. Lazaro Msasalaga aliwashauri wadau hao kuzingatia kanuni za uzalishaji na uhifadhi bora na salama ili kuepuka kupoteza masoko na kero ya kukutwa na bidhaa hafifu ambayo itawalazimu kuteketeza kwa gharama zao.
Pia aliwashauri kuwasiliana na ofisi ya TBS mara kwa mara pale wanapohitaji msaada wa kitaalamu katika mnyororo mzima wa uzalishaji, uhifadhi na ufungashaji sahihi.
Kwa upande wake Meneja wa Utafiti na Mafunzo (TBS ), Bw. Hamis Sudi Mwanasala alisema mafunzo haya kwa wadau wa sekta ya mafuta ya kula yataendeshwa katika mikoa yote nchini na kwa kuanzia yameendeshwa katika kanda ya kati ikijumuisha mikoa ya Dodoma, Singida na Tabora.
"Huu ni mwanzo, kwani Shirika litahakikisha mafunzo kama haya yanamfikia kila mdau na katika ngazi ya chini kabisa, leo tupo kanda ya kati, ila tumeshapita kanda ya kusini, nyanda za juu kusini na kwingineko kwa wadau wa bidhaa nyinginezo"Alisema
Alieleza kwamba mafunzo haoa ni bure na Serikali inagharamia kupitia TBS na tunampango wa kufikia wadau wa mafuta ya kula Nchi nzima" alisema.
Pamoja na mada juu ya bidhaa ya mafuta ya kula TBS inatumia mafunzo haya kuelezea majukumu ya Shirika ikiwa pamoja na yale yaliyokua yakifanywa na iliyokuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa ( TFDA).
Kaimu Mkuu wa Kanda ya kati TBS , Bi Salome Emmanuel aliwasisitiza wajasiriamali ambao bado bidhaa zao za mafuta hazijapatiwa nembo ya bora, kuchangamkia fursa ya bure kwa kutuma maombi ya kutumia alama ya ubora kupitia SIDO ili Serikali iwatambue kama wajasiriamali wadogo na kati na waweze kuhudumiwa bure kwa kuwa bidhaa ya mafuta inaangukia katika kiwango cha lazima hivyo kulazimika kukidhi matakwa ya viwango kwa mujibu wa sheria.
Mafunzo haya yalihusisha wadau walioweza kushiriki katika kumbi mbalimbali zilizoandaliwa lakini vilevile utembelewaji wa moja kwa moja wa wadau hao katika maeneo yao ya uuzaji au uzalishaji kama vile maeneo ya Pandambili (Kongwa),soko kuu la Singida, Tarafa ya Pahi ( Kondoa), soko la majengo (jijini Dodoma), Mitundu ( Itigi), soko kuu la Singida, soko kuu la Nzega, soko kuu la Tabora na kwa wauzaji wa barabarani waliopo wilaya ya Shelui
Lengo ni kuwaelimisha madhara yanayotokea pindi mafuta yanapoanikwa juani kwani mwanga,joto na hewa hupelekea mafuta kuharibika kabla ya muda wa mwisho wa matumizi na kusababisha madhara ya kiafya na kuwaelekeza kuboresha mazingira ya utunzaji kwa kuongeza kivuli cha vibanda vyao na kuweka taarifa za vifungashio.
Mzalishaji wa Mafuta ya kula, Bw. Daud Abel Makala na Muuzaji wa Mafuta hayo Bi.Eunice Maneno ambao walibahatika kushiriki mafunzo hayo katika jiji la Dodoma, walipongeza juhudi zinazofanywa na TBS katika kuhakikisha wanawasaidia wadau wa sekta mbalimbali hususani mafuta ya kula kuzingatia viwango ili kuweza kupata masoko ndani na nje ya nchi na kuwa na ushindani huru sokoni.
Hata hivyo waliitaka TBS kuhakikisha huu mpango wa mafunzo sambamba na kaguzi za mara kwa mara masokoni ni endelevu kwa bidhaa zote na haswa maeneo ya vijijini, ili kumlinda mlaji dhidi ya bidhaa hafifu na zile zilizokwisha muda wa matumizi au zisizotakiwa kabisa masokoni.
Nao wauza mafuta ya kula katika soko kuu la Singida na Tabora wameiomba Serikali kurahisisha upatikanaji wa vifungashio na kuhakikisha vinauzwa kwa bei nafuu ili hata wajasiriamali wa chini waweze kupaki mafuta yao kwa vifungashio bora na salama tofauti na sasa ambapo wanatumia zaidi vifungashio vilivyokwishatumiwa awali kwa bidhaaa nyinginezo.
TBS ilianza kutoa mafunzo hayo Septemba 21 hadi Oktoba 01, 2020 na kufikia wadau zaidi ya 1700 katika kanda ya kati.