Friday, 2 October 2020

Mgombea ubunge jimbo la Bariadi Mhandisi Andrea Kundo aahidi kumaliza changamoto ya tembo kuvamia makazi.

Samirah Yusuph,Mwananchi
Bariadi, Mgombea ubunge jimbo la Bariadi Mhandisi Andrea Kundo, Ameahidi kumaliza kero ya wanyama( tembo ) kuvamia makazi ya wakazi wa kata ya Gilya na Gibeshi katika wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.

Mhandisi Kundo aliyasema hayo jana alipo kuwa katika mkutano wa kuomba kura kwa wananchi wa kata hizo na kusema kuwa changamoto ya Tembo kuvamia makazi imakuwa ni ya muda sasa hivyo ni muda muafaka kuweza kuimaliza.

Aliongeza kuwa licha ya uwepo wa juhudi za kuhakikisha tembo hao hawaingii kwenye makazi lakini inabidi kuongeza nguvu ili kuhakikisha wananchi wanakuwa salama muda wote.

"Kumekuwa na tembo ambao wamekuwa ni tatizo kubwa kwa wananchi sababu wanaharibu mazao wakati wa mavuno na hata kusababisha vifo, hivyo nitahakikisha magari ya doria za polisi yanakuwa mengi maeneo haya ili tembo waweze kudhibitiwa kuingia katika makazi," alisema Mhandisi Kundo.

Jambo ambalo wananchi wa kata hizo wamelitaja kuwa ni licha ya uwepo wa changamoto zingine lakini hilo ni tatizo kubwa zaidi kwani uvamizi wa wanyama hao kwenye makazi unawaachia balaa la njaa.

Hali inayopelekea mazao yao wanayo vuna kutoka mashambani kwenda kuyahifadhi vijiji vya nkololo na Ihusi umbali wa zaidi ya kilometa 15 ili kuwakepa wanyama hao kwani wanapoingia vijijini wanavunja nyumba na kula mazao yote wanayoyakuta.

Hivyo njia hiyo ya kuhifadhi vijiji vya jirani inafanya mazao yabaki salama lakini changamoto inakuja pale wanapohitaji chakula kutokana na umbali uliopo kwenda kuvifata vyakula vyao kwa ajili ya familia zao.

"Tembo anapo vamia kwenye kaya anabomoa nyumba na anakula chakula chote anachokikuta wanakula michembe, mahindi hata unga na ni ngumu kwafukuza na wengine ni wabishi akigoma kuondoka inabidi wewe ndiye umkimbie," Alisema Monwa Kilatu mkazi wa kata Ihula.

Kwandu Maluguabili alieleza hali anayokutana nayo wanyama hao wanapofika katika makazi yake "Nyumbani nilipoweka mahindi huwa wanakuja kubomoa nyumba wanakula chakula na kuharibu kila wanachokutana nacho lakini baada ya kuwa hatuna chakula hatupati msaada wowote hivyo tunabaki bila chakula".

Wahanga hao walisema kuwa wanahitaji msaada wa serikali ili kuweza kuwadhibiti wanyama hao kwa sababu juhudi zao zinagonga amwamba kutokana na namna ambavyo wamekuwa wakiwafukuza kienyeji hali inayosababisha mapambano kati yao na kusababisha vifo kwa baadhi ya vijana wao.

Tangu mwaka 2017 tembo walinza kupita katika vijiji vya kata hizi wakiwa wanatafuta njia, na tangu waka 2018 wanyama hawa walianza kuvamia makazi nyakati za usiku na kufanya uharibifu katika makazi.

Mwisho.


Share:

TARURA yatekeleza ahadi za Magufuli


Na. Erick Mwanakulya, Kagera.

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), unaendelea kutetekeleza miradi ya Ahadi za Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kukamilisha ujenzi wa Barabara zenye urefu wa Km 2.76 kwa kiwango cha lami katika Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, mkoani Kagera.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo, Meneja wa TARURA katika Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Mhandisi Dativa Telesphory alifafanua kuwa utekelezaji wa miradi ya Ahadi za Mhe. Rais umekamilika kwa asilimia 100 baada ya ujenzi wa barabara hizo kwa kiwango cha lami kukamilika na kuanza kutumika.

“Kabla ya TARURA kuanzishwa, Wilaya ya Muleba haikuwa na lami hata Mita 1 lakini hadi sasa kupitia kuanzishwa kwa Wakala na pia utekelezaji wa miradi ya Ahadi za Mhe. Rais tumetekeleza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami zenye urefu wa Km 2.76 ambazo zimekamilika na wananchi wameanza kunufaika na ujenzi wa barabara hizi”, alisema Mhandisi Dativa.

Mkazi wa Muleba Bi. Edvina Jackson ameishukuru Serikali kwa kutengeneza barabara za lami kwenye eneo lao ambalo lilikuwa limesahaulika kwa muda mrefu kwani kwa kiasi kikubwa ujenzi wa barabara hizo umesaidia kupunguza kero ya usafiri na kufanya barabara hizo kupitika muda wote.

‘‘Tunashukuru sana Serikali barabara ni nzuri na pia usimamizi ni mzuri, pale mwanzoni tulikuwa tunapata shida kwenda mashambani na hata masokoni, sasahivi barabara ni nzuri hakuna vumbi wala matope katika kipindi cha mvua na kiangazi”, Bi. Edvina.

Aidha, mbali na utekelezaji wa miradi ya Ahadi za Mhe. Rais, TARURA wilaya ya Muleba imetekeleza ujenzi wa Daraja la Kishara lenye urefu wa Mita 36 katika Mto Ngono linalounganisha Kata za Katoke, Kamachumu na Kata ya Mafumbo ambapo kwa mujibu wa meneja wa TARURA katika Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, amesema wananchi walikua wanazunguka umbali mrefu lakini sasa kero hiyo imeisha.

Naye, Mkazi wa Kitongoji cha Kyamuhaya Bi. Goodselda Liberius alisema kuwa upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii katika eneo hilo umerahisishwa na uwepo wa daraja hilo kwasababu umewasadia kuvusha mazao yao na bidhaa nyingine za biashara kwa urahisi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

“Tunashukuru kwa kujengewa daraja hili kwasababu limekuwa ni mkombozi kwa sisi wafanyabiashara kusafirisha mazao yetu na tunaishukuru Serikali kwa kutujengea daraja hili,” alisema Goodselda.

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijni (TARURA) katika Halmashauri ya Wilaya ya Muleba unaendelea na kazi mbalimbali zikiwemo za matengenezo ya barabara na vivuko katika Wilaya hiyo ili kuwawezesha wananchi kusafiri na kusafirisha bidhaa zao kwa urahisi.



Share:

Trump na Mkewe wakutwa na virusi vya corona


Rais Donald Trump wa Marekani amesema kwamba yeye na mke wake Melania Trump wamepatikana na virusi vya corona na wako kwenye karantini. Ametoa tangazo hilo kwenye mtandao wa Twitter.

Tangazo hilo linawadia baada ya Trump na wasaidizi wake wawili kuthibitishwa kuambukizwa virusi vya corona.

Hope Hicks, 31, mshauri wa rais amekuwa msaidizi wa karibu wa Bwana Trump kupatikana na virusi vya corona hadi hivi sasa.

Bi. Hicks alisafiri na yeye kwa ndege ya kijeshi kwenda kwenye mdahalo wa Televisheni uliofanyika Ohio mapema wiki hii.

Baadae Alhamisi, Bwana Trump alisema yeye na mke wake wanakwenda karantini baada ya Bi. Hicks kuthibitishwa kuwa na corona. 
 
-BBC


Share:

UN YAMUUNGA MKONO RAIS DKT MAGUFULI KUTOKOMEZA UKATILI WA MWANAMKE IKUNGI

 

Mkuu wa  Mkoa wa Singida Mhe, Dk. Rehema Nchimbi akizungumza baada ya uzinduzi wa mradi kushoto ni  Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania  Zlatan Milisic

Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi na wawakilishi wa mashrika ya umoja wa mataifa ,wadau wa maendeleo na kmati ya ulinmzi na usalama ya wilaya ya Ikungi

Na John Mapepele, Ikungi

Mkuu wa  Mkoa wa Singida Mhe, Dk. Rehema Nchimbi  leo amezindua  miongoni mwa miradi mikubwa iliyowahi kutekelezwa nchini, mradi wa  pamoja  baina ya Mashirika ya Kimataifa ya UN Women na UNFPA kupitia ufadhiri  wa  Shirika la KOICA wa “Tuufikie usawa  wa jinsia kupitia kuwawezesha wanawake na wasichana”.

 

Mradi huo utagharimu takribani bilioni 11.5 za kitanzania  ambao utatekelezwa  katika Wilaya ya Ikungi mkoani Singida na Msalala mkoani  Shinyanga katika kipindi cha  miaka mitatu kuanzia sasa.

 Dk. Nchimbi amesema lengo kuu la mradi huo ni kuchangia  katika kuwawezesha  wanawake na wasichana  kuwakwamua kiuchumi na kijamii katika mikoa ya Singida na Shinyanga  ili kufikia usawa wa kijinsia ambapo amewataka watendaji wote wa Serikali ambao watatekeleza mradi huo kuwa makini katika utekelezaji wa mradi ili  malengo ya mradi huo yaweze kufikiwa.

Amesisitiza kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua kali watendaji ambao  kwa namna moja au nyingine hawataendana na kasi ya utekelezaji wa miradi chini ya Serikali ya awamu ya Tano  inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli ambapo amesema  mrai huo  ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi  ili kuwaletea wananchi  maendeleo ya  kweli.

Kwa mujibu wa  Mkurugenzi wa  KOICA  Tanzania, Bi Jieun Mo,  walengwa wasio wa moja kwa moja takribani  wakazi 40,000 kutoka kwenye wilaya  ya Ikungi na Msalala na walengwa  wa moja  kwa moja 2350 wanawake na wasichana  kutoka katika wilaya hizo watanufaika na mradi huu ambapo pia  wanaume na wanawake 6000 wa Wilaya  ya Ikungi watanufaika kwenye eneo la muingiliano wa  hati za ardhi.

Mo ameainisha kuwa  shughuli za mradi katika kuwaweza wanawake  kwenye eneo la uchumi zitajikiza zaidi kwenye kuimarisha uwezo wa wanawake  na vijana   wakulima ili waweze kutumia  njia nzuri za kilimo na hali ya hewa katika uzalishaji wa alizeti na kilimo cha bustani, kukuza uuzaji wa pamoja, ujuzi wa ujasiriamali na wakala wa uchumi  wa wanawake  na kuimarisha  usalama wa ardhi na umiliki.

Amesisiza kuwa  shughuli hizo zitatekelezeka  kupitia kuunda  vikundi vya uzalishaji wa kilimo cha bustani kwa wanawake, kuunganisha  wanunuzi wa vikundi  vya wakulima vya wanawake,kusaidia ujenzi wa  ghala kubwa  moja la alizeti na kituo cha ukusanyaji kilomo cha bustani ili  kuboresha uuzaji wa pamoja na utunzaji baada ya kuvuna,.

 

Alisema pia watatoa  mafunzo ya ujasiriamali na ufikiaji wa habari za kifedha na kufuatilia ushauri wa usimamizi wa biashara na  fedha na kukuza  umiliki wa ardhi pekee na wa pamoja  wa wanawake kupitia utoaji wa  Hati za Haki za kimila za Makaazi(CCROs).

Mwakilishi wa UN Women  Bi, Hodan Addou ameishukuru Serikali  ya  Tanzania  kuwa ushirikiano wake katika kuhakikisha  kuwa mradi huu  hatimaye umeanza kutekelezwa ambapo amesema Shirika lake  linaunga mkono juhudi za Serikali za kumkomboa mwanamke ili kuondokana na  unyanyasaji wa kijinsia.

Bi Addou amesisitiza kuwa mradi huo utasaidia uwezeshaji kijamii kwa kuwawezesha  wanawake kusimamia haki zao, kujenga ujuzi wa ujasiriamali wa wanawake na wasichana kukabiliana  na unyanyasaji wa kijinsia na kuimarisha mifumo ya kuzuia na kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia kupitia kuanzisha na kuandaa vifaa katika madawati matatu ya  Polisi ya Jinsia na Watoto.

Aidha alisema pia wataaanzisha  vituo vitatu vya  huduma  ya dharura katika  vituo vya wilaya, kuunda nafasi salama ya umma, kujenga uwezo  wa nambari ya msaada ya watoto kitaifa, kuunda na kuimarisha Klabu za Wasichana na kuunda Kamati za ulinzi na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania  Zlatan Milisic   ameipongeza Serikali kwa kuwa  na mradi huo na kuongeza kuwa mradi huo unaendana na malengo ya endelevu ya 2030 hususani lengo namba 5 kuhusiana kuwaendeleza wanawake  katika nyanja mbalimbali na kuongeza kuwa mwaka 2020 ni mwaka muhimu sana kwa kuwa tunaelekea  katika kutimiza miaka 25 ya azimio la wanawake la Beijing.

Ameeleza kuwa  malengo endelevu ya 2030 yameeleza kuwa ili kufikia maendeleo ya nchi kumtambua mwanamke ni jitihada muhimu sana  katika kuharakisha na kutimiza malengo yote ya maendeleo ambapo ameihakikishia Serikali ya Tanzania kuendelea kufanya kazi kwa karibu sana  ili kuhakikisha wanawake wanakuwa chachu ya maendeleo katika  nchi ya Tanzania.

Mwakilishi wa UNFPA, Dk. Winfred amesema kuwa uzinduzi wa mradi umelenga kutokomeza aina zote za unyanyasaji wa kijinsia  na kuimarisha usawa katika jamii ikiwa ni pamoja na  kuimarisha maisha ya wanawake ambapo amesisitiza kitovu cha matatizo ya kijinsia  ni wanaume na mila na desturi potofu zinazomtazama mwanamke kwa kumdharirisha hivyo juhudi za makusudi  zinatakiwa  kufanywa za kuwaweka wanaume mbele ili kutokomeza unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake.

Naye  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Edward Mpogolo  amesisitiza kuwa kazi nzuri zinazofanywa na  Rais John Pombe Magufuli katika Nyanja mbalimbali ndiyo zinazoyafanya  jumuiya za kimataifa  kuunga mkono kwa kutoa  misaada  kupitia miradi mbalimbali hapa nchini.

Share:

Tundu Lissu atakiwa kuripoti kituo cha Polisi Moshi mkoani Kilimanjaro - IGP Sirro

 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amemtaka mgombea Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mhe. Tundu lissu kuripoti kituo cha Polisi Moshi Kilimanjaro kutokana na kitendo chake alichokifanya  akiwa mkoani humo.

IGP Sirro amesema hayo jana ambapo alimtaka Mwenyekiti wa Chama hicho Mhe. Freeman Mbowe kukaa na watu wake wazungumze suala la utii wa sheria bila shuruti.

Aidha IGP Sirro ameongeza kuwa Jeshi la Polisi limepewa mamlaka ya kulinda usalama wa raia na mali zao huku akiwaeleza kuwa hakuna mtu yeyote anayeweza kupambana na Jeshi hilo na kwamba wote wanaovunja sheria za nchi watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.


Share:

Mgr: Data Warehousing & Bus Analysis at Vodacom

Joining Vodacom is more than a job, what we do matters. We don’t just carry minutes, texts and data – we carry people’s lives. And that’s a huge responsibility. If you think for a minute about the people you rely on…the likelihood is they rely on us. Customers are at the heart of everything we […]

The post Mgr: Data Warehousing & Bus Analysis at Vodacom appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa October 2



















Share:

TBS YATOA MAFUNZO KWA WADAU WA MAFUTA YA KULA KANDA YA KATI


Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetekeleza mpango wa mafunzo kwa wazalishaji, wasambazaji na wauzaji wa mafuta ya kula kanda ya kati, yaliyofanyika Mkalama, Kiomboi, Sikonge, Urambo, Shelui, Manispaa ya Tabora,Nzega, Igunga, Manispaa ya Singida, Kondoa Irangi, Kongwa, Mpwapwa, Kibaigwa, Chamwino, Itigi, Manyoni, Dodoma jiji na Bahi. 

Mafunzo haya yamelenga kuwaelimisha wadau hao juu ya uzalishaji bora, uhifadhi sahihi wa bidhaa za mafuta haswa sehemu za kuuzia, ufungashaji sahihi na salama na umuhimu wa kuzingatia na kuweka taarifa sahihi na muhimu katika vifungashio.

TBS imetoa elimu hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya viwanda, SIDO, maafisa biashara, afya na maendeleo wa wilaya ili kuwajulisha wadau wa mafuta ya kula fursa zilizopo ndani ya Serikali ili kuwawezesha kuboresha bidhaa zao ziweze kukidhi matakwa ya viwango na hatimaye kupananua wigo wa soko la ndani na nje ya nchi na kuwafanya kuongeza uzalishaji utakaopelekea kuinua uchumi wao.

Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora (TBS),Bw. Lazaro Msasalaga aliwashauri wadau hao kuzingatia kanuni za uzalishaji na uhifadhi bora na salama ili kuepuka kupoteza masoko na kero ya kukutwa na bidhaa hafifu ambayo itawalazimu kuteketeza kwa gharama zao. 

 

Pia aliwashauri kuwasiliana na ofisi ya TBS mara kwa mara pale wanapohitaji msaada wa kitaalamu katika mnyororo mzima wa uzalishaji, uhifadhi na ufungashaji sahihi.

Kwa upande wake Meneja wa Utafiti na Mafunzo (TBS ), Bw. Hamis Sudi Mwanasala alisema mafunzo haya kwa wadau wa sekta ya mafuta ya kula yataendeshwa katika mikoa yote nchini na kwa kuanzia yameendeshwa katika kanda ya kati ikijumuisha mikoa ya Dodoma, Singida na Tabora. 

"Huu ni mwanzo, kwani Shirika litahakikisha mafunzo kama haya yanamfikia kila mdau na katika ngazi ya chini kabisa, leo tupo kanda ya kati, ila tumeshapita kanda ya kusini, nyanda za juu kusini na kwingineko kwa wadau wa bidhaa nyinginezo"Alisema 

 

Alieleza kwamba mafunzo haoa ni bure na Serikali inagharamia kupitia TBS na tunampango wa kufikia wadau wa mafuta ya kula Nchi nzima" alisema. 

 Pamoja na mada juu ya bidhaa ya mafuta ya kula TBS inatumia mafunzo haya kuelezea majukumu ya Shirika ikiwa pamoja na yale yaliyokua yakifanywa na iliyokuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa ( TFDA).

Kaimu Mkuu wa Kanda ya kati TBS , Bi Salome Emmanuel aliwasisitiza wajasiriamali ambao bado bidhaa zao za mafuta hazijapatiwa nembo ya bora, kuchangamkia fursa ya bure kwa kutuma maombi ya kutumia alama ya ubora kupitia SIDO ili Serikali iwatambue kama wajasiriamali wadogo na kati na waweze kuhudumiwa bure kwa kuwa bidhaa ya mafuta inaangukia katika kiwango cha lazima hivyo kulazimika kukidhi matakwa ya viwango kwa mujibu wa sheria.

Mafunzo haya yalihusisha wadau walioweza kushiriki katika kumbi mbalimbali zilizoandaliwa lakini vilevile utembelewaji wa moja kwa moja wa wadau hao katika maeneo yao ya uuzaji au uzalishaji kama vile maeneo ya Pandambili (Kongwa),soko kuu la Singida, Tarafa ya Pahi ( Kondoa), soko la majengo (jijini Dodoma), Mitundu ( Itigi), soko kuu la Singida, soko kuu la Nzega, soko kuu la Tabora na kwa wauzaji wa barabarani waliopo wilaya ya Shelui

Lengo ni kuwaelimisha madhara yanayotokea pindi mafuta yanapoanikwa juani kwani mwanga,joto na hewa hupelekea mafuta kuharibika kabla ya muda wa mwisho wa matumizi na kusababisha madhara ya kiafya na kuwaelekeza kuboresha mazingira ya utunzaji kwa kuongeza kivuli cha vibanda vyao na kuweka taarifa za vifungashio.

Mzalishaji wa Mafuta ya kula, Bw. Daud Abel Makala na Muuzaji wa Mafuta hayo Bi.Eunice Maneno ambao walibahatika kushiriki mafunzo hayo katika jiji la Dodoma, walipongeza juhudi zinazofanywa na TBS katika kuhakikisha wanawasaidia wadau wa sekta mbalimbali hususani mafuta ya kula kuzingatia viwango ili kuweza kupata masoko ndani na nje ya nchi na kuwa na ushindani huru sokoni.

 

 Hata hivyo waliitaka TBS kuhakikisha huu mpango wa mafunzo sambamba na kaguzi za mara kwa mara masokoni ni endelevu kwa bidhaa zote na haswa maeneo ya vijijini, ili kumlinda mlaji dhidi ya bidhaa hafifu na zile zilizokwisha muda wa matumizi au zisizotakiwa kabisa masokoni.

Nao wauza mafuta ya kula katika soko kuu la Singida na Tabora wameiomba Serikali kurahisisha upatikanaji wa vifungashio na kuhakikisha vinauzwa kwa bei nafuu ili hata wajasiriamali wa chini waweze kupaki mafuta yao kwa vifungashio bora na salama tofauti na sasa ambapo wanatumia zaidi vifungashio vilivyokwishatumiwa awali kwa bidhaaa nyinginezo.

TBS ilianza kutoa mafunzo hayo Septemba 21 hadi Oktoba 01, 2020 na kufikia wadau zaidi ya 1700 katika kanda ya kati.

Share:

Thursday, 1 October 2020

Waziri Bashungwa Ameruhusu Uuzaji Wa Ethanol Nje Ya Nchi

 



Share:

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Maadhimisho Ya Siku Ya Chakula Duniani


Dodoma, 01 Oktoba, 2020
Wizara ya Kilimo inapenda kuwataarifu wananchi na wadau wote wa sekta ya kilimo nchini kuwa Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani yatafanyika kitaifa mkoani Njombe kuanzia tarehe 10 Oktoba 2020 na kilele chake itakuwa tarehe 16 Oktoba 2020.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo (01.10.2020) na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba jijini Dodoma imesema maandalizi ya maadhimisho hayo yamekamilika na kuwa wizara, taasisi, wakala, mashirika ya kimataifa na kitaifa zinakaribishwa kujitokeza kushiriki kwenye maadhimisho ya mwaka huu.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani  mwaka huu inasema “Kesho Njema Inajengwa na Lishe Bora Endelevu” .

Imetolewa na;
Revocatus Kassimba
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.



Share:

Majaliwa: Tupeni Kiongozi Atakayekuza Mahusiano Na Jirani


MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amesema Tanzania inahitaji kuwa na kiongozi ambaye atakuza mahusiano na nchi jirani.

“Tanzania inazungukwa na nchi tisa ambazo baadhi yake ziko kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki na nyingine hazimo. Tunahitaji kiongozi ambaye ataweza kuhakikisha nchi hii inakuwa na mahusiano mema na nchi jirani na nchi nyingine duniani kote lakini pia anaweza kuilinda heshima ya nchi yetu,” amesema.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Oktoba mosi, 2020) wakati akizungumza na wakazi wa kata za Nyakahura na Nyakanazi, wilayani Biharamulo, mkoani Kagera akiwa njiani kuelekea wilaya za Bukombe na Mbogwe mkoani Geita.

Mheshimiwa Majaliwa ambaye ambaye amemaliza ziara yake mkoani Kagera ya kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli alitumia fursa hiyo kumnadi mgombea ubunge wa jimbo la Biharamulo Magharibi, Eng. Ezra Chiwelesa na wagombea udiwani wa CCM wa kata hizo, Apolinary Mgalula na Amos Madegwa.

Akielezea suala la vitambulisho vya uraia, Mheshimiwa Majaliwa amesema kote alikopita mkoani humo wananchi wanaulizia kuhusu uchelewaji wa kutolewa kwa vitambulisho hivyo. “Ucheleweshaji huu hauko hapa mkoani Kagera tu bali hata kwenye mikoa ya pembezoni ya Kigoma, Songwe, Katavi, Ruvuma, Mtwara, Lindi, Pwani, Arusha na Mara”

“Hii ni kwa sababu tunataka tujiridhishe na uraia wa waombaji kwani hili suala ni kwa usalama wa nchi yetu. Wale walioko jirani umbali wa km. 10 wanaruhusiwa kuja kutembea au kufanya biashara na kurudi kwao. Hawaruhusiwi kupata vitambulisho, hivi ni kwa Watanzania tu.”

Mheshimiwa Majaliwa amewahakikishia wakazi hao kwamba kila Mtanzania mwenye sifa atapata kitambulisho cha Taifa kwa kuwa ndiyo mkakati wa Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Magufuli.

Mheshimiwa Majaliwa amesema Uhamiaji inatakiwa kuwa makini kusimamia mchakato huo kwa sababu wapo baadhi raia wa nchi jirani wanatamani kupata kitambulisho cha Taifa kutokana na amani iliyopo nchini. “Uhamiaji iwe makini haitapendeza kuona Mtanzania anakosa kitambulisho cha Taifa halafu mgeni kutoka nchi jirani anapata,” amesema.

Hata hivyo, amewataka wakazi hao wasikubali kutoa rushwa kwa sababu hiyo ni haki yao na kwamba endapo itatokea kuwa wameombwa rushwa watoe taarifa. “Mtu wa uhamiaji akidai rushwa ili akupatie kitambulisho toa taarifa mara moja ili tumshughulikie,” amesisitiza.


Share:

Usichelewe .....Pakua sasa hivi App Ya Mpekuzi Ikiwa na Maboresho Mapya. Ipo PlayStore

Tumefanya Maboresho Kwenye App Yetu ya Mpekuzi Ili Kukuwezesha Kupata Habari zetu Haraka

Usikubali kupitwa na taarifa muhimu zinazoendelea hapa nchini na Duniani  kwa Ujumla . Tumejipanga vizuri sana kukupatia taarifa sahihi na kwa wakati.

👉1. Tumebadili muonekano na kuufanya kuwa mzuri zaidi
👉2. Kila habari tunayoweka kuanzia sasa utapata notification kwenye simu yako 
👉3. Habari zote kwa sasa zinafika kwa haraka kwenye simu yako kuliko ilivyokuwa hapo awali

KUMBUKA: App yetu ni BURE. Unachotakiwa kukifanya ni kuingia Playstore na kupakua MPEKUZI APP

Kama tayari unayo, basi Ingia Playstore kwa ajili ya kupata UPDATE hii ya Toleo Jipya

Tumekurahisishia, Unaweza pia ...<<KU BOFYA HAPA>> Kupata toleo hili Bure Kabisa


Share:

Msajili Avionya Vyama vya siasa vinavyotaka kuungana siku ya Oktoba 3 mwaka huu


Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini Sisty Nyahoza, ameviasa vyama vya siasa vinavyotaka kuungana siku ya Oktoba 3 mwaka huu, kuacha mara moja mpango huo kwani wanakiuka utaratibu wa sheria na kwamba walianza vizuri hivyo ni vyema kila mmoja akaendelea kunadi sera zake.

Nyahoza ametoa kauli hiyo hii leo Oktoba Mosi, 2020, kwenye kipindi cha Supa Breakfast ya East Africa Radio na kuongeza kuwa hata hivyo tayari Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imekwishaviandikia barua vyama hivyo kwa kuwa ni masuala ya kiofisi huwa hawaziweki barua hizo hadharani.

"Kwanza tunaawaasa hao wanaotaka kufanya hivyo tarehe 3 sisi kama walezi wa vyama vya siasa kwa sababu wanakiuka sheria, walianza vizuri hivyo kila mmoja aendelee kunadi sera yake na wagombea wao wa urais", alisema Nyahoza.

Amesema sheria ya vyama vya siasa inawekwa kwa maslahi ya wanachama na wananchi na unapotaka kushirikiana hutakiwi kufanya kitendo chochote kinachohadaa wananchi kwa hiyo ni kosa kufanya hivyo ghafla wakati wa uchaguzi.

“Ukiunganisha nguvu na chama kingine wakati mmeshakubaliana na wananchi kwamba mtatekeleza sera gani ni kuwahadaa, sisi tulishawasiliana nao na tukawaambia waache," alisema Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini Nyahoza.

Vyama vya siasa vya upinzani vya ACT-Wazalendo na Chama Cha Demokrasia na Mandeleo (Chadema) vimekuwa vikitajwa kuwa na mpango wa kumuunga mkono mgombea mmoja wa urais Oktoba 3, licha ya kuwa vyama vyote hivyo vimeshasimamisha wagombea wao wa urais.



Share:

Bil 5.26/- zatumika kujenga barabara Ngara


 SHILINGI bilioni 5.26 zimetolewa kupitia Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) kwa ajili ya ujenzi na  matengenezo ya barabara katika wilaya ya Ngara, mkoani Kagera.

“Kati ya hizo, shilingi bilioni 1.1 zimetengeneza barabara kwa kiwango cha lami kilomita 4.5 katika makao makuu ya wilaya hii.”

Hayo yamesemwa jana (Jumatano, Septemba 30, 2020) na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Rulenge, katika mikutano uliofanyika kwenye stendi ya Rulenge.

Amesema kiasi kingine cha shilingi bilioni 4.16 zimetolewa kupitia TARURA kwa ajili ya ujenzi na matengenezo ya barabara ikiwemo barabara za Muhweza – Mukarehe, Keza – Nyanzovu, Mukalinzi – Mulonzi, Kibuba – Gwenzaza, Murugwanza – Runzenze (Airstrip), Chivu – Ntobeye – Nyakiziba, Buhororo – Mukididili, Ngara – Kumutana na Buhororo – Ruganzo (Airstrip)

Mheshimiwa Majaliwa ambaye leo anamalizia ziara yake mkoani Kagera ya kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli alitumia fursa hiyo kumnadi mgombea ubunge wa jimbo la Ngara, Bw. Ndayisaba George Ruhoro na mgombea udiwani wa CCM wa kata ya Rulenge, Bw. John Niyonzima.

Mapema, akiwa njiani kuelekea Ngara akitokea Bukoba mjini, Mheshimiwa Majaliwa alisimamishwa na wakazi wa kata za Nyaishozi (Karagwe) na Kasulo Benaco (Ngara) ambako pia aliwanadi madiwani wa kata hizo. Pia aliwaeleza kwamba barabara ya kutoka Omurushaka hadi Benaco itajengwa kwa kiwango cha lami.

“Kwenye Ilani ya uchaguzi iliyopita ambayo inaisha sasa, barabara hii ilielezwa kwamba itakamilishwa kufanyiwa upembuzi yakinifu, na sasa inaenda kujengwa kwa lami kwa sababu kazi imeshafanyika.”

Pia aliitaja barabara nyingine ya kutoka Bugene – Kasulo (BENACO) yenye urefu wa km. 124 ambayo inatajwa kwenye uk. 75 wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwamba ni miongoni mwa barabara zitakazoanza kujengwa upya kwa kiwango cha lami.


Share:

Mama adaiwa kumchinja mwanae wa miaka saba

 Mtoto wa miaka saba  mwanafunzi wa dasara la tatu Shule ya Msingi Ihumwa ameuawa kwa kuchinjwa shingo na mtu anayedaiwa kuwa ni mama yake mzazi, Grace William (45) kisha kutokomea kusikojulikana.

Tukio hilo limetokea usiku wa manane kuamkia jana katika Mtaa wa Ihumwa, nje kidogo ya Jiji la Dodoma ambako mtoto alikuwa akiishi na mama huyo.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Ihumwa ambaye pia ni baba mzazi wa Grace, William Ngilimunji, amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kwamba aliyekufa ni mjukuu wake. Alidai wakati mauaji hayo yanafanyika mtoto alikuwa amelala.

Amedai kwamba aliyehusika na mauaji hayo ni mama wa mtoto huyo ambaye ana matatizo ya akili na kwamba alikuwa akihudhuria kliniki Hospitali ya Wagonjwa wa Akili Mirembe, mkoani hapa.

Ngilimunji amesema mtoto wake huyo (mama wa marehemu) hana mume na amekuwa akiishi Ihumwa.


Chanzo: Majira



Share:

Serikali yaridhia kutoa hekari 1,625 kwa wananchi


SERIKALI imeridhia kutoa hekari 1,625 kwa wananchi kutoka katika ardhi inayomilikiwa na Jeshi la Magereza Kijiji cha Ilagala Wilaya Uvinza mkoani Kigoma kwa lengo la kuendeleza kilimo cha zao la michikichi, pamoja na shughuli nyingine ikiwemo makazi.

Akisoma tamko la serikali kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna wa Polisi Thobias Andengeye, amesema hatua hiyo inalenga kumaliza mgogoro wa ardhi uliokuwepo baina ya wananchi wa kijiji hicho pamoja na Jeshi la Magereza tangu mwaka 1995.

Gereza la Ilagala lina ukubwa wa hekari 15,000 ambapo ni miaka mingi, baadhi ya wananchi wamekuwa wakivamia eneo hilo na kuanzisha makazi pamoja na shughuli za kilimo, hivyo kuhatarisha usalama wa eneo la gereza jambo ambalo serikali imeona ni bora kugawa sehemu ya eneo hilo.

Kamishna Andengenye amesema, wananchi watakaopata ardhi ambayo itakuwa ikipakana na Jeshi la Magereza, watakuwa walinzi wa mipaka ili wengine wasiweze kuvamia eneo lingine la magereza ambapo upatikanaji wa eneo hilo, itakuwa chachu ya wananchi kuendelea kufanya shughuli zao za uzalishaji wa uchumi.


Share:

KISHINDO CHA MGOMBEA URAIS CCM DKT. JOHN POMBE MAGUFULI MJI WA VWAWA SONGWE LEO


Mambo mbalimbali yaliyojiri na aliyoyazungumza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dkt John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wake mkubwa wa Kampeni za Kuomba Kura kwenye Mji wa Vwawa Uliopo Mkoani Songwe leo Oktoba 1,2020. Kila anakopita Watu wanafurika. Nchi inamtaka Magufuli, Watu Wanaitaka CCM.#T2020JPM #MITANOTENA
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger