Sunday, 19 July 2020

HALI YA USAJI,UTUNZAJI WA KUMKUMBUKU YA VIZAZI NCHINI BADO HAIRIDHISHI


KATIBU Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Judica Omari akizungumza wakati akifungua semina ya viongozi wa mkoa na wilaya zake kuhusu  usajili wa watoto walio na umri chini ya miaka mitano kilichofanyika katika ukumbi mkuu wa mkoa wa Tanga.


Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) Emmy Hudson akizungumza wakati wa semina hiyo

MKURUGENZI Msaidizi Huduma za Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais Tamisemi Rasheed Maftah akizungumza wakati wa semina hiyo



Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali kutoka kushoto ni MKURUGENZI Msaidizi Huduma za Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais Tamisemi Rasheed Maftah akifuatiwa na Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) Emmy Hudson,Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Jonathan Budemu

Katibu tawala wa wilaya ya Korogwe Rahel Mhando kulia akifuatilia kwa umakini semina hiyo akiwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Handeni Mashaka Mgeta katikati na Katibu tawala wa wilaya ya Muheza Desderia Haule

MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa kushoto akiwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa wakifuatilia kwa umakini semina hiyo

MKUU wa wilaya ya Lushoto January Lugangika kushoto akiwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia wakiwa kwenye semina hiyo

KATIBU Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange kushoto akiwa na Katibu tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilindi wakiwa kwenye semina hiyO

MKUU wa wilaya ya Handeni Toba Nguvila kulia akiwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo wakifuatilia matukio mbalimbali


Katibu Tawala wa wilaya ya Mkinga Joseph Sura akifuatilia kwa umakini semina hiyo Sehemu ya viongozi wa dini wakifuatilia semina hiyo

KUTOKANA na ongezeko la mahitaji na matumizi ya cheti cha kuzaliwa nchini, hali ya usajili na utunzaji wa kumbukumbu ya vizazi bado hairidhishi jambo linalosababisha serikali kukosa takwimu sahihi kwa ajili ya mipango mbalimbali ya maendeleo kwa Taifa ikiwemo elimu,afya na huduma nyengine za msingi .

Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) Emmy Hudson ameyasema hayo katika semina ya viongozi wa mkoa na wilaya zake kuhusu usajili wa watoto walio na umri chini ya miaka mitano kilichofanyika katika ukumbi mkuu wa mkoa wa Tanga.

Hudson alisema alisema kwa mujibu wa takwimu ya sensa ya 2012 ni asilimia 13 tu ya wananchi wa Tanzania Bara waliosajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa hivyo kuifanya kuwa moja kati ya nchi zenye kiwango cha chini cha usajili barani Afrika.

"Hii ni changamoto ambayo serikali kupitia RITA kama Taasisi yenye dhamana ya Usajili wa matukio muhimu ya binadamu kwa kwa kushirikiana na wadau wengine tumechukua hatua stahiki kwa kuandaa mkakati wenye lengo la kukabiliana na changamoto hii" amesema Hudaon.

Hata hivyo amebainisha kwamba tayari hatua madhubuti zimechukuliwa ili kukabiliana na changamoto hiyo kwa kufanya maboresho ya ujumla ya mfumo mzima wa usajili chini ya mkakati wa kitaifa na kuboresha Usajili wa matukio muhimu ya binadamu na takwimu.


Alisema mkakati huo umeandaliwa baada ya kufanyika kwa tathimini ya kina na kubaini mapungufu katika mfumo wa usajili uliopo huku akieleza mpango huo wa Taifa wa kuboresha usajili na matukio muhimu ya binadamu na takwimu umebeba mipango mbalimbali ya utekelezaji ikiwa ni ya muda mfupi na mrefu ukilinganisha na makundi makuu matatu yanayotokana na umri ili kufikia makusudio ya usajili.

Aidha alisema kundi la kwanza ni watoto wa umri chini ya miaka mitano ambapo serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imebuni mpango wa usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa kundi hilo.

“Tayari mpango huu unaendelea kutekelezwa katika mikoa kumi na sita ya Mwanza, Mbeya,Songwe,Iringa,Njombe,Geita,Shinyanga,Mtwara,Lindi,Mara,Simiyu,Dodoma,Singida,Morogoro,Pwani na Ruvuma na kuonyesha mafanikio chanya hivyo kikao hiki ni maandalizi ya kuanza utekelezaji katika mkoa wa Tanga “Alisema

Awali akizungumza wakati akifungua semina hiyo Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Judica Omari ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella alisema maisha ya mwanadamu yanaanzia pale anapozaliwa hivyo basi tukio la kizazi maana yake ni kuongezeka kwa idadi ya watu katika jamii na Taifa kwa upande wao kama serikali inawakumbusha wajibu wa kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi.

Alisema kwa mantiki hiyo usajili na upatikanaji, utunzaji wa kumbukumbu sahihi kila tukio jipya la kizazi linapotokea ni la msingi kuweza kutambulika kwani kufanya hivyo kutaweza kuwa na uhakika wa kuweka takwimu sahihi kwa wakati na kupunguza matumizi ya takwimu za makisio ambazo zote wanazifahamu changamoto zake.
Share:

WAGOMBEA UBUNGE,UDIWANI CCM IRINGA WAONYWA ....MNEC ASAS ASEMA CHAMA HAKINA MGOMBEA MAALUM


Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa NEC Salim Abri Asas akitoa nasaha kwa wagombea ambapo alisema kuwa chama hakina mgombea maalum bali wagombea wote wapo sawa na watapita katika mchakato wa kikanuni ili kumpata mgombea mmoja atakayepigiwa kura na wajumbe.

Na Zuhura Zukheir - Malunde 1 blog Iringa 
Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Iringa kimetoa onyo kali kwa wagombea ubunge na udiwani kuwa hakitawafumbia macho wagombea wote watakaobainika kusaliti chama kwa kukiuka kanuni na taratibu za chama baada ya uchaguzi wa kura za maoni kumalizika na kupatikana mmoja atakayepeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Akizungumza katika mkutano na wagombea wa nafasi za ubunge katika kikao cha maelekezo kuelekea kura za maoni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Iringa Dkt. Abel Nyamahanga alisema kuwa katika kuelekea uchaguzi wagombea wanatakiwa kuwa na moyo wa ujasiri kwani lolote linaweza kutokea na wasipojiandaa wanaweza kuangukia katika usaliti jambo ambalo sio jema kwa watu walioaminiwa na chama.

Alisema katika uchaguzi wanatarajia kuona wagombea wote waliojitokeza katika majimbo saba ya uchaguzi na kata kata 106 za udiwani wataunganisha nguvu zao kuhakikisha ushindi wa kishindo unakuwaCCM hata kama wao watakuwa wamekatwa majina yao. 

"Kila mgombea anatakiwa kutambua kuwa katika uchaguzi kuna kupata na kukosa hivyo hatutegemei baada ya kura za maoni kujitokeze masuala ya usaliti na makundi ya wagombea",alisema.

Aliwataka wagombea kutambua kuwa masuala ya usaliti yamekuwa yakikigawa chama na kusababisha wapinzani kupata nguvu ya kuchukua majimbo jambo ambalo halikubaliki katika uchaguzi wa mwaka huu katika chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa.

Alisema kuwa nafasi ya ubunge waliyoomba ni ya utumishi hivyo ni vyema wakajitoa kwa moyo kuwatumikia wananchi na wanaccm kwa ujumla badala ya kufikiria kupata utajiri kupitia ubunge.” Wagombea ni waeleze hakuna mgombea ambaye yupo juu zaidi ya mwingine wagombea wote wapo sawa hata wale wabunge wanaotetea nafasi zao wote kwa sasa ni wanachama tu wa kawawida.

Alisema kuwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi kuna miongozo ya kikanuni kwa watia nia pamoja na viongozi wa chama hicho ambayo ni mwiko kwa kiongozi yeyote kupendelea mgombea au mtia nia yeyote wa

Aliongeza kusema kuwa Chama Cha Mapinduzi kina nia njema na wagombea wote hivyo wanatakiwa kujenga imani na chama chao na hata ikitokea mmoja amepitishwa wengine wa muunge mkono ili kuhakikisha wanapata ushindi wa kishindo. 

Aidha alisema chama hakitamvumilia mgombea yoyote atakaye mchafua mgombea mwingine kwa kuwa haijulikani jina lipi litarudishwa hivyo ikitokea mgombea aliyechafuliwa akapitishwa chama kinapata wakati mgumu kumsafisha kipindi cha kampeni. 

Nyamahanga pia amewataka wagombea kumtegemea Mungu zaidi badala ya kupishana kwa waganga wakienyeji ambao ndio wamekuwa chanzo cha migogolo katika chama baada ya kuwahakikishia ushindi baadae mambo yanakuwa tofauti.

Akizungumza Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa NEC Salim Abri Asas alisema kuwa chama hakina mgombea maalum bali wagombea wote wapo sawa na watapita katika mchakato wa kikanuni ili kumpata mgombea mmoja atakaepigiwa kura na wajumbe.

Alisema kuwa anaamini katika mchakato huo wa kura za maoni hakutakuwa na manung’uniko kwani kura zitapigwa za wazi na kila mgombea atahusika katika kuhesabu kura ili kuondoa malalamiko.

MNEC Asas aliwaomba watia nia kuunganisha nguvu zao kumsaidia atakaepitishwa nchama baada ya uchaguzi wa kura za maoni ili kuhakikisha wanapata ushin za di wa kishindo pamoja na kupata ushindi wa kishindo katika kura za Rais mh. John Magufuli.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Iringa Brown Mwangomale aliwataka wagombea kujiandaa kisaikolojia katika mchakato wa uchaguzi na wa kubali matokeo kwakuwa katika uchaguzi kuna matokeo mawili ambayo ni kushinda na kushindwa.

Alisema kuwa kitendo cha kujiamini katika uchaguzi wa kura za maoni kuwa utashinda na badala yake matokeo ya kawa tofauti ndipo wanachama wanapogeukia katika usaliti jambo ambalo halikubaliki katika chama.

Alisema kuwa dhambi ya usaliti ni mbaya na adhabu yake kufukuzwa katika chama jambo ambalo halitarajiwi kujitokeza katik uchaguzi huu wa mwaka 2020”ndugu zangu dhambi ya usaliti ni mbaya na kubwa usaliti unaua na ndio maana vitabu vya dini vimekemea vikali usaliti.

Alisema kuwa CCM mkoa wa Iringa wamedhamiria kushinda katika majimbo yote ya uchaguzi hivyo ushindi huo unatemewa zaidi na mshikamano utakaoneshwa na mshikamano wa wagombea wote 319 walioingia katika kuwania nafasi hiyo ya ubunge.

UBUNGE WA JIMBO
Mwangomale alisema aliojitokeza kugombea Jimbo la Iringa Mjini 54,Isimani 9,Kalenga 68, Kilolo 38, Mufindi kusini 31 na Mufindi Kaskazini 33,Mafinga Mjini 20,Ubunge Viti maalumu 28,Jumuiya ya vijana 13, Jumuiya ya wazazi 8,Kundi la Wafanyakazi 4,kundi lawatu wenye ulemavu 5 na Kundi la wasomi 3.

UDIWANI
Walitokeza kugombea ngazi ya udiwani kwa kata 106 za mkoa wa Iringa kutia nia ngazi ya udiwani 787 ammbapo katika kata za Iringa mjini wamejitokeza 148,Wilaya ya Iringa 156,Wilaya ya Mufindi 171 pamoja na kilolo 117.

Mwangomale aliongeza kuanzia jumatatu julai 20 hadi jumatano kutakuwa na mchakato wa kura za maoni kila wilaya za kuwapata wagombea watakaopeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi.
Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa NEC Salim Abri Asas akitoa nasaha kwa wagombea
Share:

ALIYEKUWA MBUNGE RORYA AJIUZULU KUGOMBEA UBUNGE BAADA YA KUREJESHA FOMU... 'MIMI DARASA LA 7 NAWAACHIA WASOMI"


Kulia ni Lameck Airo akirudisha fomu kugombea Ubunge jimbo la Rorya kupitia CCM kabla ya kujiuzulu kugombea


Na Dinna Maningo - Malunde 1 blog Rorya.
Mbunge wa Jimbo la Rorya aliyemaliza muda wake Lameck Airo  ambaye alichukua fomu kutetea nafasi yake ya Ubunge amejiuzulu kuomba  kugombea ubunge kwa kile alichoeleza kuwa ameamua kuwaachia wasomi  na kuunganisha nguvu ya pamoja kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi kinapata ushindi mnono zaidi.

Mnamo Julai 17,2020 Airo alichukua fomu ya kutia nia ya Ubunge na kuirejesha na kufikisha idadi ya Watia nia 49 lakini jana Julai 18,2020 alikabidhi barua mbele ya Katibu wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) wilaya ya Rorya Avelin Ngwada ,Kamati ya Siasa ya Wilaya na Watia nia nafasi ya Ubunge.

"Nimeahirisha kwa roho moja sijashinikizwa  na mtu nimewaachia na wengine waendelee atakayeshinda nitamuunga mkono kwa maslahi ya Rorya kwa hiyo watu wasiwe na shaka",alisema Airo.

Alivyohojiwa na Malunde 1 blog kutaka kufahamu kwanini ameahirisha kugombea licha ya kwamba alichukua fomu ya kugombea kwa hiari alisema : 

"Nilikuwa tu natesti mitambo maana nilishawahaidi wananchi kwenye mikutano yangu kuwa sitogombea napumzika lakini cha hajabu baadhi ya wana Rorya wakiwemo wasomi wakawa wananitukana kwenye mitandao ya kijamii mara mimi ni darasa la saba naongozaje na wasomi  nimevumilia mengi sana na hao waliokuwa wananitukana baadhi yao ni wasaliti wa chama na leo wametia nia kugombea" .

"Nilipoona wananiandama nikasema acha nichukue fomu tujipime na hao wasomi, waliposikia nimechukua fomu wakaanza tena kupata presha kulalamika lakini nimetafakari zaidi nikaona kwanini tusumbuane  na Rorya ni yetu sote ndipo nikaamua kuahirisha ili na wasomi nao waongoze wananchi wapime,nimezaliwa Rorya hivyo naahidi kutoa ushirikiano",alisema Airo.

Airo alisisitiza kuwa atakayefanikiwa kuwa Mbunge asiishie kukaa mjini afike Jimboni ashiriki maendeleo kulinganana na uwezo wake hata kama kipato chake ni kidogo lakini msaada wake utasaidia kulingana na uwezo wake.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Rorya Charles Ochele aliwashukuru Wananchi wa Rorya kwa kuwathamini watu wa elimu ya darasa la saba nakuwapa ridhaa katika nafasi mbalimbali ndani ya chama na Ubunge na nafasi zinginezo

"Airo kaongoza sasa tunarudisha wasomi,sababu ya kuchukua darasa la saba  tulikuwa tunawapa wasomi lakini wanaishia kukaa Dar es Salaam Jimboni anarudi kwa nadra tukasema hatuchagui mtu wa Dar lakini sasa tumeamua kuwapa wasomi ili tuone kama wamebadilika na tuwapime kwa vitendo wasipoleta mabadiliko tutaendelea na msimamo wakuwakataa wagombea wanaotoka Dar ",alisema Ochele.

Ochelle aliwaonya wanachama wanao mchafua Airo na Mwenyekiti huyo kwenye mitandao ya kijamii na badala yake waungane pamoja kuhakikisha CCM inaendelea kuongoza katika Jimbo hilo huku akikemea vitendo vya rushwa kwa watia nia.

Kitendo cha Airo kujiuzulu kugombea kimewafurahisha Watia nia ambao wamedai kuwa walipata hofu baada ya kuona amechukua fomu na baadhi yao hawakupata usingizi lakini sasa hofu imetoweka.

Mtia nia nafasi ya Ubunge Maina Owino alisema : "Kwa kweli mbunge umetusumbua moyoni mwetu umetupa presha sana niliposikia umechukua fomu sikupata usingizi lakini tunashukuru umeachia sasa tutakuwa huru".

Peter Sarungi alimuahidi Airo kuendelea kufauta nyayo zake,busara zake na ushirikiano kwa kuwa wote ni wana Rorya lakini pia alimpongeza yeye  na Ochele kwa kuwasamehe wale waliokuwa wakiwachafua kwenye mitandao ya kijamii na kuahidi kufungua ukurasa mpya ili kuhakikisha Rorya inasonga mbele.

Ngwada alisema kuwa baada ya Airo kujiondoa  wamebaki 48 ambapo waliochukua fomu walikuwa 52 kati ya hao watatu hawakurejesha fomu na mmoja kujiudhuru.
Wa tano mstari wa mbele kutoka kulia ni Lameck Airo akiwa kwenye picha ya pamoja na Watia nia Ubunge Jimbo  la Rorya
Watia nia wakiwa kwenye kikao cha maelekezo kutoka kamati ya Siasa wilayani humo ukumbi wa CCM uliopo Utegi
Share:

Haya Hapa Magazeti ya Leo Jumapili Julai 19,2020















Share:

Saturday, 18 July 2020

Binti wa miaka 19 ashikiliwa mauaji ya mwanafunzi wa chuo Jijini Mbeya

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia SUZY KENNETH KASITEJETA [19] Mkazi wa Dar es Salaam kwa tuhuma za mauaji ya LINUS JAMES MAGESA [21] Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya [MUST] Kitengo cha Biomedical mwaka wa kwanza na Mkazi wa Ikuti kwa kumchoma kitu chenye ncha kali kifuani.

Ni kwamba mnamo tarehe 17.07.2020 majira ya saa 22:00 Usiku huko eneo la Ikuti lililopo Kata na Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya SUZY KENNETH KASITEJETA [19] na LINUS JAMES MAGESA [21] ambao walikuwa na uhusiano wa kimapenzi waligombana na kupelekea LINUS JAMES MAGESA kujeruhiwa sehemu za kifuani kwa kuchomwa kitu chenye ncha kali na SUZY KENNETH KASITEJETA hali iliyopelekea kukimbizwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa matibabu.

Leo tarehe 18.07.2020 majira ya saa 00:05 Usiku LINUS JAMES MAGESA [21] alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya. Chanzo cha tukio hili ni wivu wa kimapenzi. Hata hivyo taarifa zinadai kuwa wapenzi hao walikuwa wakigombana mara kwa mara. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

WITO:
Ninatoa wito kwa jamii kutofumbia macho ugomvi unatokea mbele yao kwa kudhani ni kitu cha kawaida na kukaa kimya, ni wito wa Jeshi la Polisi kwa jamii kutoa taarifa mapema kwa Watendaji wa Kata au Wenyeviti wa Mitaa ambao ni walinzi wa amani katika maeneo yao ili waweze kuchukua hatua za awali kupitia baraza la usuluhishi la Kata au Mtaa.

KUPATIKANA NA MALI IDHANIWAYO KUWA NI YA WIZI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia DICKSON KABUJE [32] Mkazi wa Ikumbi akiwa na mali mbalimbali za wizi.

Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 17.07.2020 majira ya saa 14:00 Mchana huko Kijiji cha Ikumbi, Kata ya Utengule – Usongwe, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya na katika upekuzi alikutwa akiwa na mali za wizi ambazo:-
  1.     Spika kubwa 02,
  2.     Redio Sub-Woofer 01 na Spika zake,
  3.     Stablizer 01, m
  4.     Mtungi mkubwa wa gesi Mihani 01,
  5.     Deki 02 za Singsung,
  6.     Godoro 01 Super Banco.
Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.


Share:

SHIRIKA LA BRAC TANZANIA LAIUNGA MKONO SERIKALI VITA DHIDI YA COVID 19

 Mkurugenzi wa Brac Tanzania Fordson Kapwefu akizungumza kabla ya kukabidhi msaada huo wa vifaa kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Korogwe Dkt Fortunata Silayo
 Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Kasimu Kaoneka akizungumza mara baada ya kukabidhiwa msaada huo
 Mkurugenzi wa Brac Tanzania Fordson Kapwefu kushoto akimkabidhi msaada
vifaa vya kunawia mikono kwaajili ya Shule zilizopo katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe,Vifaa vilivyotolewa na shirika hilo vyenye thamani ya milioni 2.2
 Mkurugenzi wa Brac Tanzania Fordson Kapwefu akinawa mikono kabla ya kukabidhi  msaada vifaa vya kunawia mikono kwaajili ya Shule zilizopo katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe,Vifaa vilivyotolewa na shirika hilo vyenye thamani ya milioni 2.2 kushoto ni Meneja wa Miradi wa Brac Mkoa wa Tanga Wiliam Manoah
 Sehemu ya msaada huo ambao umetolewa na Shirika la Brac wilayani Korogwe
 Sehemu ya msaada huo ambao umetolewa na Shirika la Brac wilayani Korogwe


SHIRIKA la  Brac Tanzania limeunga mkono juhudi za serikali za kupambana na ugonjwa wa Corona (Covid -19) kwa kutoa msaada wa vifaa vya kunawia mikono kwaajili ya Shule zilizopo katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe.

Vifaa vilivyotolewa na shirika hilo vyenye thamani ya milioni 2.2 ni matanki kumi na mbili (12) yaliyofungwa kwenye meza maalumu pamoja na vitakasa mikono (sanitaiza) ambapo makabidhiano hayo yalifanyika kwenye ofisi za mjini Korogwe.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi wa Brac Tanzania Fordson Kapwefu alisema kwamba wameamua kutoa msaada huo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za serikali kupambana na ugonjwa huo.

“Kwa kweli sisi kama Brac tumeguswa na jitihada za Serikali katika mapambano ya ugonjwa wa Corona (Covid - 19) tumeona ni muda muafaka kuziunga mkono kwa kutoa vifaa vya kunawia mikono katika shule”Alisema 

Mkurugenzi huyo alisema kwamba msaada huo ambao wameutoa ni muendelezo wa ugawaji wa vifaa vya kunawia mikono kwaajili ya shule zilizopo katika mikoa mbalimbali hapa nchini kuhakikisha wanafunzi wanaendelea kuchukua tahadhari wanapokuwa shuleni.

Awali akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Korogwe Dkt Fortunata Silayo alilishukuru shirika la Brac Tanzania kwa kuwapatia vifaa vya kunawia mikono katika shule zao ikiwa ni jitihada za kupambana na ugonjwa wa Corona (Covid - 19).

“Tunawashukuru sana Shirika la Brac kwa kuona umuhimu wa kutoa msaada huu ambao umefika wakati muafaka hivyo tunahaidi kuhakikisha vifaa hivyo vinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na sio vyenginevyo”Alisema 

Naye kwa upande wake Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Kasimu Kaoneka alitoa shukrani zake kwa shirika hilo huku akieleza namna watakavyotumia vifaa hivyo shuleni 

Aidha alisema vifaa ambavyo wamepatiwa vitakuwa msaada mkubwa katika mapambano ya ugonjwa wa Corona (Covid – 19) ikiwemo ikiwa kama sehemu ya somo la usafisishaji wa mikono kwa wanafunzi.
Share:

Aboubakar Juma Aboubakar Ajitosa kugombea Urais kupitia chama cha NCCR-MAGEUZI.

Ndugu Aboubakar Juma Aboubakar leo Julai 18,2020 ametia nia kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha NCCR-MAGEUZI.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa NCCR-Mageuzi, Evarist Komu amemtaka mgombea huyo kupeperusha bendera ya chama kwa kusimamia misingi ya chama hicho ambayo ni pamoja na kutetea utu, haki, udugu, usawa na upendo kwa mustakabali wa chama na Watanzania kwa ujumla.

Abubakar ameahidi kusimamia misingi ya chama chake na kuweka mazingira yatakayokuwa chachu ya kuleta maendeleo endelevu nchini.

Komu amesema hadi sasa wanachama 232 wamechukua fomu za kuomba kugombea ubunge na zaidi ya 3,000 wamechukua fomu za kuomba kugombea udiwani.


Share:

Tatizo la kuishiwa nguvu za kiume na maumbile kusinyaa limekuwa tatizo kwa wanaume wengi.

Tatizo la kuishiwa nguvu za kiume na maumbile kusinyaa limekuwa tatizo kwa wanaume wengi.
 ___________________

==>Yajuwe matatizo yanayosababisha upungufu wa nguvu za kiume
___________________

👉(1) Ngiri ya kupanda na kushuka
👉2.Korondani moja kuvimba
👉3.Tumbo kuunguruma kujaa gesi
👉4.Kisukari
👉5.Presha
👉6.Kiuno kuuma
👉7.Kutopata choo vizuri

Ipo Dawa  ya asili ya nguvu za kiume yenye kutibu matatizo kwa wakati mmoja
 ___________________
Pia tunatibu kisukari siku (14) vidonda vya tumbo siku (30), Miguu kufa ngazi, kuwaka moto . 

👉Je umeachwa? Na mke /mume,mchumba na bado unampenda ? Kunamtu unamtaka unashindwa kumwambia? 

Wasiliana na mtalam, humvuta mume, mke,mchumba na mtu yeyote  unayemtaka katika mahusiano na kumfanya atimize unachohitaji kutoka kwake na kumfunga asiwe na mtu mwingine zaidi yako hata kama yupo mbali atakutafuta mwenyewe na kutmiza ahadi zenu .
 ___________________
Wasiliana nae kwa Simu: CALL / WHATSAPP : 0747100745
 



Share:

MSANII MAARUFU PAPA SHIRANDULA AFARIKI DUNIA


Charles Bukeko maarufu kama 'Papa Shirandula' 

Charles Bukeko, msanii maarufu nchini Kenya aliyejulikana sana kwa jina la 'Papa Shirandula' ameaga dunia katika hospitali ya Karen mjini Nairobi 

Kulingana na msemaji wa familia Richard Ekhalie, Papa Shirandula ameaga dunia hospitali ya Karen hii leo.

Mchana huu familia ilikuwa inasubiri ripoti maalum kutoka hospitali ili kuthibitisha kilichosababisha kifo cha mpendwa wao.

Papa Shirandula alifikishwa hospitali leo asubuhi saa mbili na nusu na mke wake, akiwa hajisikii vizuri lakini wakati wanajaribu kuendelea na mchakato wa kulazwa hospitalini, Papa Sharandula akaaga dunia.

Kulingana na msemaji wa familia, Jumatano Papa Shirandula alikuwa ametoka kuandaa vipindi kama ilivyo kawaida yake lakini akawa hajisikii vizuri na kupata dawa, lakini leo usiku, hali ikawa bado inaendelea ndio mkewe akamkimbiza hospitali baada ya kuanza kusikia vibaya karibu saa kumi na moja asubuhi.

Papa Shirandula ni nani?

Charles Bukeko maarufu kama Papa Shirandula anatoka magharibi mwa Kenya eneo la Busia.

Ameacha nyuma watoto wawili na mke wake waliokuwa wanaishi mjini Nairobi.

Bukeko ambaye jina la Papa Shirandula limetokana na kipindi kimoja cha anachoshiriki kinachopeperushwa na runinga ya Citizen, amekaa katika tasnia hii ya uigizaji kwa muda sasa na ingawa msemaji wao wa familia Bwana Ekhalie hakuwa na uthibitisho wa ni lini hasa aliingia kwenye uingizaji amesema kwamba sio chini ya miaka kumi.

Mbali na kushiriki kipindi kilichompa umaarufu mkubwa, 'Papa Shirandula' ameshiriki kwenye utengenezaji wa maudhui ya kipindi hicho na kushinda Tuzo la Kalasha Award, 2010 kama muigizaji mzuri kwenye vipindi vya televisheni, pia alikuwa kwenye filamu ya 'The Captain of Nakara' mwaka 2012.

Aidha amehusika na matangazo ya biashara mbalimbali pamoja na kuendeleza kurudumu lake la uigizaji kwenye maonyesho tele aliyoshiriki katika ukumbi wa taifa wa uingizaji Kenya.
Share:

PAKUA APP YA MALUNDE 1 BLOG ILI TUWE TUNAKUTUMIA HABARI NA MATUKIO MSIMU HUU WA UCHAGUZI BURE KWENYE SIMU YAKO

Share:

SAED KUBENEA AIPIGA CHINI CHADEMA NA KUJIUNGA ACT WAZALENDO


Saed Kubenea.

Aliyekuwa Mbunge wa Ubungo kupitia CHADEMA Saed Kubenea, amesema kuwa maamuzi ya yeye kujiunga rasmi na chama cha ACT Wazalendo yalikuwa ni magumu, kwa kuwa hicho ndiyo chama chake cha pili kujiunga tangu aanze siasa na kudai kuwa ndani ya Jiji la Dar es Salaam upinzani una nguvu kubwa.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Julai 18, 2020, mara baada ya kujiunga rasmi na chama cha ACT Wazalendo, na kupokelewa na kukabidhiwa kadi ya uanachama na Mwenyekiti wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad.

"Kwa kweli maamuzi haya yalikuwa ni magumu sana kwa sababu katika maisha yangu, hiki ndiyo chama cha pili kujiunga lakini nilifika mahali nikasema, kama Maalim Seif alinzisha CUF kwa jasho na damu akaondoka, baada ya kutoridhika na hali iliyokuwa ikiendelea sembuse mimi, nikajifunza kwamba ni lazima safari hii ya mabadiliko iendelee", amesema Kubenea.

Share:

RAIS MAGUFULI AAHIRISHA SHEREHE ZA MASHUJAA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.

Rais Magufuli ameahirisha sherehe za mashujaa zilizopaswa kufanyika Julai 25, 2020, Jijini Dodoma na kuwataka Watanzania kuitumia siku hiyo kuwakumbuka na kuwaombea mashujaa wote waliojitoa kwa ajili ya Tanzania.

Taarifa hiyo imetolewa leo Julai 18, 2020, na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, na kuongeza kuwa Rais Magufuli amewataka Watanzania kuendelea kudumisha amani, upendo, utulivu na mshikamano.

Aidha Rais Magufuli pia amewataka Watanzania kuwaombea Mashujaa wote hata wale ambao wametoa mchango mkubwa katika ngazi mbalimbali, ikiwemo kwa mtu mmoja mmoja ama familia.
Share:

CCM TARIME YAWATAHADHARISHA WANACHAMA 53 WALIOREJESHA FOMU KUGOMBEA UBUNGE



Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tarime Daud Ngicho akizungumza na Watia nia wa Ubunge
****

Na Dinna Maningo - Malunde 1 blog Tar­ime
Wanachama 56 wa CCM wamejitokeza kuchukua  fomu za kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Tarime mjini na Tarime vijijini ambapo kati yao 53 wamerudisha fomu.

Akizungumza na Malunde 1 blog Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya  Tarime mkoani Mara,Hamis Mkaruka alisema kuwa katika Jimbo la Tarime Vijijini wanachama 30 wamechukua fomu na wote  wamezirudisha na katika Jimbo la Tarime mjini waliochukua fomu walikuwa 26 lakini waliorudisha ni 23 na watatu hawakurudisha.

Mkaruka aliyasema hayo mbele ya wanachama wa CCM waliojitokeza kuomba kugombea ubunge katika ukumbi wa Chama Cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Tarime ambapo yeye na viongozi wa chama hicho waliwaonya kutotukanana,kuchafuana na kutotoa rushwa kama njia ya kushawishi wajumbe kuwapigia kura kwani kinachohitajika ni mtu kujieleza nini atakachokifanyia chama,Wanachama na wananchi.

"Mmerudisha fomu kugombea ni haki yako lakini kuteuliwa ni haki ya vikao uchaguzi utafanyika tarehe 21 mwezi wa saba,2020 na usidhani ukiongoza kwa kura nyingi wewe ndiyo mshindi bado kuna michujo mingine maana kuna watu humu ndani ya CCM wanafahamika lakini huko nje hawafahamiki tunataka mgombea mwenye sifa za kuku wa kienyeji kwakuwa yeye uacha mayai kwenye banda nakujitafutia mwenyewe mayai kuliko kuku wa kisasa anaengoja kutafutiwa chakula",alisema Mkaruka.

Katibu Mwenezi  CCM wilaya ya Tarime Marema Solo alisema kuwa wana CCM ni familia moja hivyo ni lazima kuwa wamoja kwa maslahi ya chama nakwamba hakuna aliye mkubwa ndani ya CCM wote ni wanachama sawa huku akiwakumbusha kusoma maandiko ya Biblia Mathayo7:7 kinachosema ombeni,nanyi mtapewa.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tarime Daudi Ngicho alisema kuwa watia nia ni wengi na nafazi za ubunge kwenye wilaya ni mbili zinazohitaji watu wawili nakwamba atakayeshinda watia nia wengine wamuunge mkono kuhakikisha CCM Tarime inashinda majimbo yote mawili.

Ngicho alisema kuwa kuna baadhi ya wanachama wamekuwa wakiwachafua wenzao kupitia mitandao ya kijamii huku akiahidi kuwashughulikia wasaliti  ndani ya  chama lengo kuhakikisha CCM inapita kwa kishindo.

Aliwaonya kutotoa rushwa kwa wajumbe,watiania kutosafirisha wajumbe siku ya uchaguzi nakwamba chama ndicho kitasafirisha wajumbe kwenda katika kumbi zitakazotumika kufanya uchaguzi siku ya tarehe 21 mwezi huu nakusema kuwa Uchaguzi jimbo la Tarime mjini utafanyika ukumbi wa CCM wilaya na Jimbo la Tarime vijijini utafanyika ukumbi wa chuo cha ualimu.

Watia nia katika Jimbo la Tarime mjini  ni Suzy Chambili,Monica Anic­et,Dr.Veronica Robert, Hezbon Mwera, Jackson Ryo­ba, Dr.Edward Machag­e,Julius Mtatiro, Eng­.William Machage,Che­che Andrew,Julius La­baran,Samwel Marwa,E­vangel Otieno,Michael Kembaki,Jeremia Seba,Gerald Martine,M­wita Joseph,Zakayo Wangwe, Manchare He­che Siguta,Mwita James,Ditu Manko,Philip Nyirabu,Robert Mwitango,Justin Mugendi,Deogratius Meck,Segere Shadrack na Col.Kichonge Masero na miongoni mwao watatu hawakurudisha fomu.

Kwa jimbo la Tarime vijijini ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) Mwita Waitara, Joyce Ryoba,Dr.Stella Faustine, Joseph Nyahende,Yusuph Wambu­ra,Chacha Masero,John Gimunta,Mwita Jacob Marwa,Wambura Sagi­re,Thomas Chacha Mwi­ta, Musa Raphael, Ny­erere Mwera,Nyamhanga David,Dr.Abdalah Chogo,Dr.Paul Mwikwab­e,Mordikae Moset,Eli­akimu Maswi,Nicodemas Keraryo,James Bwir­e,Peter Amos Bhusene, Frank Mniko,Lucas Magoti,Samwel Mantarya, Ngocho Darius,Pius Mawa,Harun Kihengu,Maseke Muhono na Dr.Edward Machage na wote wamerudisha fomu.
 Watia nia wa Ubunge  Jimbo la Tarime mjini na Tarime vijijini
Share:

WANACHAMA 49 WA CCM WAREJESHA FOMU JIMBO LA RORYA...YUMO LAMECK AIRO



Lameck Airo akirudisha fomu kugombea Ubunge jimbo la Rorya kupitia CCM
 Irene Makongo akirudisha fomu kugombea Ubunge Jimbo la Rorya kupitia CCM
Maina Owino akirudisha fomu kugombea Ubunge jimbo la Rorya kupitia CCM
**
Na Dinna Maningo - Malunde 1 blog Rorya
Wanachama 48 wa CCM  kati ya 52 waliochukua fomu za kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Rorya mkoani Mara akiwemo Mbunge aliyemaliza muda wake Lameck Airo na  wamerudisha fomu.

Akizungumza na Malunde 1 Blog, Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Rorya mkoa wa Mara Avelin Ngwada aliwataja waliochukua fomu kuwa ni George Kasinga,Hamza Waritu,Irene Makongoro,Peter Sarungi,Evans Rubara,Mahamba Ihonde,Kichere Mwita,Joseph Bura,Charles Ochai,Sospeter Omollo,Robert Alila,Dk.Janes Otieno,Msafiri Marwa.

Wengine ni Chacha Wambura,Timon Saronge ,Francis Olwero,Nicodemus Agweyo,Mwl.Ezekiah Olwoch,Edwano Ngoita,Leonard Otuoma,Mussa Okero,Julius Nyahongo, Frey Edward,Hamis Christopher,Col.Cleophace Mathoro,Fredrick Magadi,Christopher Sanya.

Ngwada aliwataja wengine kuwa ni Jafari Chege,Kenedy Ojuang, Zephania Migire,Nicholaus Omollo,Wambura Mirumbe,Eng.Nchama Cliford,David Wembe,Titus Jumanne ,Adv.Hamis Matiko,Miriam Odemba,Juvenalis Motete,Maganya Abdul,Obuya Matiku,Paul Bosco,Hamis Marandi,Olima Aloyce,Maina Owino,Prof.Johannes Monyo,Fabian Jamhuri,Philip Apiyo ,Naftal Phillip,Dr.Deogratius Magongwe na Dady Igogo.

Ngwada alisema kuwa zoezi hilo limefanyika vyema na kwamba imebaki kazi ya vikao vya maamuzi vitakavyopiga kura nakisha mshindi atapatikana ambaye atagombea Ubunge katika Jimbo hilo.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger