Friday, 17 July 2020

Breaking : RAIS MAGUFULI AMEFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI ASUBUHI HII... DC KATAMBI OUT




Share:

OMEGA ACHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE MAKAMBAKO


Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa anayeuwakilisha Mkoa wa Njombe Ndg Omega Thobias (kulia) amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Makambako Mkoani Njombe kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi. 
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JULAI 17,2020






















Share:

Thursday, 16 July 2020

JOHN MLYAMBATE ARUDISHA FOMU KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SHINYANGA MJINI


Afisa Habari na Mawasiliano Serikalini, John Mlyambate akikabidhi fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini kwa Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu leo Julai 16,2020.

Akikabidhi fomu hizo, Mlyambate amewakumbusha wajumbe wa Mkutano Mkuu wa wilaya na wagombea wenzake kuzingatia maadili na miiko ya chama katika kuhakikisha zoezi linakuwa huru na haki na hatimaye akapatikane mwakilishi mzuri atakayepeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Shinyanga Mjini. 
Afisa Habari na Mawasiliano Serikalini, John Mlyambate akikabidhi fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjinikwa Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu (kushoto) leo Julai 16,2020.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

MWENYEKITI WA UVCCM SHINYANGA MJINI DOTTO JOSHUA ARUDISHA FOMU KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SHINYANGA MJINI


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Shinyanga, Dotto Simon Joshua akimkabidhi Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu (kushoto) fomu ya kuomba ridhaa ya CCM kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Shinyanga, Dotto Simon Joshua leo Julai 16,2020 amerudisha fomu ya kuomba ridhaa ya CCM kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.

Akizungumza baada ya kurejesha fomu katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini kwa Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu, Dotto Simon Joshua  amesema amefanya mambo mengi kupitia Jumuiya ya Vijana hivyo anakiomba chama chake kimpe nafasi ya Ubunge ili niweze kuwasaidia wananchi wa Jimbo la Shinyanga Mjini katika kuleta maendeleo katika Jimbo letu. 

"Mimi kama Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini na Vijana wote wa Shinyanga Mjini ni Mashahidi wa mambo makubwa ambayo Mhe.  Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli anayafanya katika nchi hii,nimeamua kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya Wanachama wa Chama cha Mapinduzi kuwa mgombea wa Ubunge wa Jimbo la SHINYANGA MJINI ili kuendeleza mazuri yote yanayofanya na yanayoendelea kufanywa na serikali ya CCM",amesema Joshua. 

"Vijana wa Shinyanga mjini wameniamini na kuniomba kuomba ridhaa ya Kuwa mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini ili kukimbiza maendeleo ya Jimbo letu kwa ujumla",amesema.

Share:

Bulombora JKT Selection Form six – National Services Form six JKT Selection 2020

Bulombora JKT Selection Form six – National Services Form six JKT Selection 2020   The Bulombora National Services JKT, has released names of form six students who have been selected attend the National Services training for the 2020 academic year. Bulombora JKT Form six JKT Selection list contains all the Students names selected to attend […]

The post Bulombora JKT Selection Form six – National Services Form six JKT Selection 2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Mkatatue Matatizo ya Wananchi – Rais Magufuli

Na.Immaculate Makilika – MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka viongozi wateule kwenda kutatua matatizo ya wananchi katika maeneo yao.
 
Akizungumza katika hafla ya kuapisha viongozi aliwateuwa hivi karibuni leo Alhamisi (Julai 16, 2020) Ikulu, Chamwino Dodoma, Rais Magufuli aliwataka viongozi wateule kwenda kufanyakazi, kusimamia shughuli za maendelo pamoja na kutatua matatizo ya wananchi ikiwemo migogoro mbalimbali huku akitolea mfano mgogoro wa ardhi wa ulipo katika Wilaya ya Chunya, jinini Mbeya.
 
“Mkatimize wajibu wenu na kufanyakazi vizuri, mkamtangulize Mungu katika shughuli zenu na mkawatumikie watanzania na hasa wananchi masikini waliopo katika maeneo yenu,” alisema Rais Magufuli
 
Aidha, Rais Magufuli alimtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dkt. Maduhu Isaac Kazi  ambaye ni kati ya viongozi aliowateua kuhakikisha  kuwa hakuna urasimu katika kuwawezesha  wawekezaji  kutekeleza miradi yao hapa nchini.
 
“Tusiwazungushe wawekezaji, tuwavutie waje kuwekeza nchini, nchi yetu ina maeneo mbalimbali ya uwekezaji  ikiwemo Kigamboni na Kibaha, tuongeze kasi katika utendaji wetu ili tuendelee kujenga uchumi wetu, na sasa tumeingia uchumi wa kati basi tujitahidi zaidi” alisisitiza Rais Magufuli
 
Kwa upande, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan aliwapongeza wateule wapya na kuwataka kuwa watumishi wa watu badala ya kuhaha na madaraka waliyoyapata.
 
Viongozi walioapishwa ni pamoja na Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya,  Makatibu Tawala wa maeneo mbalimbali na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),ambao waliteuliwa katika nafasi hizo hapo jana  Julai 15, 2020.
 
Mwisho


Share:

Tangaza Biashara Yako Au Bidhaa Yako Kwenye Mtandao huu Kwa BEI NZURI Kabisa


Tunakaribisha  matangazo  ya  aina  zote( Bishara, Viwanja, Bidhaa, matangazo ya Vyuo na mengine mengi)  .Bei  zetu  ni  nzuri  sana  na  kamwe  hutajuta  kutangaza  biashara  yako  kupitia  mtandao  huu....

Kwa mwezi tunafunga na Pageviews zaidi  ya  milioni 4
Kama  una  tangazo, basi  wasiliana  nasi   sasa.

Email  yetu:  mpekuziblog@gmail.com




Share:

MWANAHARAKATI WA HAKI ZA WANAWAKE NA WATOTO MUSA NGANGALA ARUDISHA FOMU KUGOMBEA UBUNGE SHINYANGA MJINI



Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Musa Jonas Ngangala leo Julai 16,2020 amerudisha fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.

Musa Jonas Ngangala alichukua fomu Julai 14,2020 na amerudisha leo kwa katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu.

Musa Jonas Ngangala ni Mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake na watoto ambaye amekuwa akisaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu ikiwemo vifaa vya shule,amesomesha watoto walioshindwa kuendelea na masomo ya sekondari kwa kuwapeleka vyuo vya ufundi na amewezesha vijana kujitegemea kiuchumi na vikundi 120 vya wanawake wajasiriamali katika Manispaa ya Shinyanga.

Musa Jonas Ngangala pia amewezesha ujenzi wa chumba cha kujisitiri watoto wa kike katika shule ya Sekondari Chamaguha na uanzishwaji wwa viwanda vidogo vidogo kwa kushirikiana na Shirika la Viwanda Vidogo vidogo (SIDO) na utekelezaji wa sera za nchi katika Manispaa ya Shinyanga.
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu akipokea fomu ya Musa Jonas Ngangala leo Julai 16,2020 kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde blog
 Musa Jonas Ngangala akiwasili katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini kurudisha fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Musa Jonas Ngangala akiwasili katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini kurudisha fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Musa Jonas Ngangala akinawa mikono baada ya kuwasili katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini kurudisha fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Share:

LEAH KOMANYA AJITOSA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MEATU


Aliyekuwa Mbunge wa  Viti Maalum Meatu, Leah Komanya amechukua fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Meatu mkoani Simuyu. Kushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya Meatu, Dotto Mazuri akimkabidhi fomu Leah Komanya lJulai 15,2020.
Aliyekuwa Mbunge wa  Viti Maalum Meatu, Leah Komanya akichukua fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Meatu mkoani Simuyu.
Share:

Maazimio Ya Mkutano Wa SADC Wa Baraza La Mawaziri Wa Fedha Na Uwekezaji


1.        Jopo la mapitio ya viashiria vya uchumi mpana linalohusisha Mawaziri wa SADC wenye dhamana ya Fedha na Uwekezaji na Magavana wa Benki Kuu, walikutana kwa njia ya mtandao tarehe 15 Julai 2020.

2.        Dhumuni la mkutano huo ambao umefanyika kwa njia ya mtandao lilikuwa ni kupitia hatua iliyofikiwa na nchi wanachama kuhusu mafanikio yaliyofikiwa kuelekea malengo ya uchumi mpana yaliyokubaliwa pamoja na kubainisha changamoto za mwelekeo wa kiuchumi katika kanda na kushauri hatua za kisera za kukabiliana na changamoto hizo. Wakati huo huo, jopo limepokea taarifa kuhusu athari za janga la COVID-19 kwa nchi wanachama wa SADC pamoja na taarifa ya utekelezaji wa hatua za kufikia malengo ya uchumi mpana.

3.        Jopo pia lilipitia na kujadili taarifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo hii ni mara ya pili kwa nchi hizi mbili kufanyiwa mapitio tangu mfumo wa SADC wa nchi moja kuifanyia tathimini nchi nyingine kuzinduliwa mwezi Mei 2013, Maputo, Jamhuri ya Msumbiji.

4.         Jopo lilibaini yafuatayo:-

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
4.1         Katika miaka michache iliyopita, uchumi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umekuwa ukiimarika, na hivyo kuiwezesha nchi kufikia malengo ya msingi na upili (primary and secondary targets) yaliyokubaliwa na nchi wanachama. 
4.2         Ukuaji wa Pato la Taifa uliimarika kutoka asilimia 2.4 mwaka 2016 hadi asilimia 3.7 mwaka 2017 na asilimia 5.8 mwaka 2018, lakini ulipungua na kufikia asilimia 4.6 mwaka 2019 hususan kutokana na kushuka kwa uzalishaji wa madini uliopelekea kuzorota kwa bei ya bidhaa.
4.3         Mfumuko wa bei ulishuka kwa kasi na kufikia asilimia 7.2 mwaka 2018 na asilimia 4.6 mwaka 2019 na inategemewa kufikia asilimia 5.0 mwaka 2020.
4.4         Wakati huo huo, mfumo wa usimamizi wa malipo taslim umewezesha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwa na ziada kwenye bajeti ya asilimia 0.2 ya pato la taifa katika kipindi cha mwaka 2016 na 2018, na kupungua kufikia nakisi ya asilimia 0.2 ya pato la taifa kwa mwaka 2019.
4.5         Mwaka 2019, deni la taifa la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo lilifikia asilimia 13.3 ya pato la taifa, uwiano ambao upo ndani ya lengo lililowekwa na nchi wanachama wa SADC usiozidi asilimia 60 ya pato la taifa.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

4.6         Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kutekeleza mapendekezo ya Jopo la Mapitio la Viashiria vya Uchumi Mpana kutokana na mapitio ya awali yaliyofanyika mwaka 2017.
4.7         Hivyo, uchumi wa nchi ulishuhudia ukuaji wa uchumi wa wastani wa asilimia 6.9 katika kipindi cha mwaka 2016 – 2018 ambao unaendana na shabaha ya Jopo la viashiria vya uchumi mpana la SADC wa angalau asilimia 7.
4.8         Kiwango cha Mfumuko wa bei kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilikua wastani wa asilimia 4.4 kwa miaka minne iliyopita, ambapo kimebakia ndani ya shabaha za SADC ya asilimia 3 – 7 na chini ya shabaha ya muda wa kati ya asilimia 5.
4.9         Nakisi ya bajeti kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliongezeka  katika kipindi cha mapitio kutoka asilimia 1.4 ya pato la taifa mwaka 2016 hadi asilimia 2.5 mwaka 2018 na kuimarika hadi kufikia asilimia 2.3 mwaka 2019. Aidha, deni la Serikali lilifikia wastani wa asilimia 40 ya pato la taifa kati ya mwezi Juni 2016 na Juni 2019, uwiano ambao uko ndani ya ukomo uliowekwa na nchi wanachama wa SADC wa asilimia 60.

5.            Jopo lilijadili na kuidhinisha taarifa na mapendekezo ya kisera ya timu ya wataalam kwa ajili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vilevile, Jopo liliridhika na utayari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutekeleza mapendekezo hayo.
6.            Katika kuhitimisha, Jopo liliipongeza Falme ya Eswatini na Jamhuri ya Msumbiji kwa kuifanyia mapitio Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Jamhuri ya Madagascar kwa kuifanyia mapitio Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
7.            Jopo lilikubaliana kuwa nchi za Angola, Namibia, Shelisheli na Zimbabwe zitakuwa nchi wanachama zitakazofuata kufanyiwa mapitio katika kipindi cha mwaka 2020/2021.
8.            Jopo lilitoa shukran zao za dhati kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa SADC, kwa maandalizi mazuri yaliyofanywa wakati wa mkutano.

Sekretarieti ya SADC
15 Julai 2020


Share:

YUSUPH MBUNDI 'MATAMA' ACHUKUA FOMU KUGOMBE UBUNGE SHINYANGA MJINI



Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Yusuph John Mbundi 'Matama' akichukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Julai 15,2020. Kushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu.

Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Yusuph John Mbundi 'Matama' akionesha fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini
Share:

Rais Magufuli: Sijamtuma mtu kugombea ubunge na Hakuna Kiongozi yeyote Aliyemtuma Mtu Yeyote

Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi amesema kuwa hadi Julai 16, 2020 asubuhi zaidi ya wanachama 8,000 wa chama hicho walikuwa wametia nia ya kugombea ubunge.

Rais Magufuli amesema hayo wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni ambapo ameeleza Mkoa wa Dar es Salaam ndio unaongoza .

Aidha, Rais Magufuli ametumia wasaa huo kusisitiza kuwa taarifa kwamba baadhi ya watia nia wametumwa na viongozi wa serikali na chama akiwemo yeye na viongozi wengine wakiwemo Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Makamu Mwenyekiti wa CCM au Katibu Mkuu wa CCM na viongozi wa vyombo vya ulinzi si za kweli.

Ametaka chama hicho kuwapima watia nia wote kwa usawa na kwamba wao hawajamtuma mtu, bali wanataka wananchi wachague wenyewe wa kumtuma.

Hata hivyo amesema uwepo wa idadi hiyo kubwa ya watia nia ni ishara ya kukomaa kwa demokrasia ndani ya chama hicho.


Share:

BANDORA SALUM MILAMBO ARUDISHA FOMU YA KUWANIA UBUNGE SHINYANGA MJINI

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bandora Salum Milambo amerudisha fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo Julai 16,2020 majira ya saa 6 na robo mchana katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini.

Bandora Salum Milambo ambaye ni Mfanyabiashara mkazi wa Ngokolo Manispaa ya Shinyanga alichukua fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Julai 14,2020.
Bandora Salum Milambo akirudisha fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu (kushoto). Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

RAIS WA UTPC DEOGRATIAS NSOKOLO ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA NSIMBO


Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Deogratias Nsokolo leo Julai 16,2020 amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea Ubunge katika Jimbo la Ndimbo mkoani Katavi.

Nsokolo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabua ya Waandishi wa Habari mkoa wa Kigoma amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Ubunge katika jimbo la Nsimbo katika ofisi za CCM wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi

Nsokolo amesema amechukua fomu ya kugombea nafasi ya ubunge ili kutimiza haki yake ya kikatiba na  ili kama atapata nafasi ya kuchakuliwa aweze kuutumikia umma.

Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania Deogratias Nsokolo leo Julai 16,2020 akionesha fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea Ubunge katika Jimbo la Ndimbo mkoani Katavi.



Share:

Form Six JKT selections 2020- Form Six waliochaguliwa kujiunga na JKT 2020

Form Six JKT selections 2020- Form Six waliochaguliwa kujiunga na JKT 2020 How do I view JKT selection after they have been released ?? JKT National Service selection list will be uploaded online after its official release by JKT, to check your Selection status follow the below lead from:- Go to JKT Official website  Find […]

The post Form Six JKT selections 2020- Form Six waliochaguliwa kujiunga na JKT 2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

MDAU WA MAENDELEO JOSEPH GORYO 'MUDDY' ACHUKUA NA KUREJESHA FOMU YA UDIWANI CCM-LAMADI



Mdau wa Maendeleo Mkoa wa Simiyu, Joseph Goryo 'Muddy' akionesha fomu yake aliyoichukua kutia nia kiti cha Udiwani ndani ya CCM Lamadi.
Mdau wa Maendeleo Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu, Joseph Goryo 'Muddy' ametia nia kuwania kiti cha Udiwani ndani ya Chama Cha Mapinduzi CCM, Kata ya Lamadi.

Goryo amechukua na kurejesha fomu hiyo na kwa sasa anasubiria hatua nyingine zaidi ndani ya Chama chake.


Goryo amekuwa mdau mkubwa wa Maendeleo kwa kusaidia masuala ya kijamii ikiwemo kutoa misaada ndani na nje ya mkoa wake huo wa Simiyu pia ni Mfanyabiashara, Mkulima na mfugaji.

Hata hivyo Goryo hakuwa tayari kuzungumzia hatua yake hiyo akiomba Wanahabari na wadau wasubirie muda muafaka ukifika  ataeleza kwa kina katika nia yake hiyo ya kuwatumikia wana Lamadi kupitia nafasi ya Udiwani endapo atapitishwa na chama na kisha kugombea.

Goryo amekuwa na shauku ya kuona safari ya Lamadi mpya yenye maendeleo ya kisasa inatimia.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger