Thursday, 16 July 2020

Live : RAIS MAGUFULI ANAWAAPISHA VIONGOZI WATEULE, IKULU CHAMWINO, DODOMA

LIVE: Rais  Magufuli Anawaapisha Viongozi Wateule, Ikulu Chamwino, Dodoma


Share:

MWANDISHI WA HABARI MARCO MIPAWA 'NG'WANA NGOLELWA' AJITOSA UBUNGE MSALALA


Msimamizi wa Uhuru Media Group (UMG) Mkoa wa Shinyanga Marco Mipawa 'Ng’wanangolelwa' leo Julai 16,2020 amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Msalala mkoa wa Shinyanga.
Kushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya Kahama Emanuel Lameck Mbamange akimkabidhi Mwandishi wa Habari Marco Mipawa Ng’wanangolelwa fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge wa Jimbo la Msalala
Share:

IDD KASSIM ACHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MSALALA


Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Geita  Iddi Kassim Iddi  leo Julai 16, 2020 amechukua fomu za kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Msalala kupitia CCM. Kushoto ni  Katibu wa CCM wilaya ya Kahama Emanuel Lameck Mbamange akimkabidhi fomu Iddi Kassim Idd.
Share:

DR HUSSEIN MWINYI APOKELEWA KWA KISHINDO ZANZIBAR


Mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hussein Mwinyi, jana alipata mapokezi ya kishindo kutoka kwa wanachama wa chama hicho, alipowasili Zanzibar.


Mgombea huyo ambaye aliteuliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa CCM jijini Dodoma Ijumaa kisha kuthibitishwa na Mkutano Mkuu wa chama hicho Jumamosi, aliwasili Zanzibar akitokea jijini Dodoma, vilikofanyika vikao vya CCM.

Dk. Mwinyi alipokelewa na umati uliojitokeza kumpokea katika Uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume hadi ofisi kuu za CCM Kisiwandui.

Mapokezi hayo yalisababisha baadhi ya huduma za kijamii kusimama kwa takribani saa tatu kupisha ujio wa mgombea huyo, huku rangi za kijani na njano zikiwa zimetanda katika maeneo mbalimbali ya mji wa Zanzibar.

Mapokezi hayo yalipambwa na burudani mbalimbali za ngoma za asili, taarabu na wasanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Zanzibar na Tanzania Bara, akiwamo msanii Ali Kiba alietumbuiza.

Dk. Mwinyi aliwasili uwanja wa ndege majira ya saa 5:30 asubuhi ambapo alitembea kwa gari la wazi na kuwasili Kisiwandui saa 7:00 mchana.

Baada ya kufika ofisi kuu za CCM alizuru kaburi la Rais wa kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume na kupata tambiko kutoka kwa wazee wa CCM.

Akimtambulisha mgombea huyo kwa wanachama wa CCM, Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, alisema Dk. Mwinyi ni mzaliwa wa Zanzibar na wale wanaosema kuwa sio kwao Zanzibar waache kasumba hizo.

Aliwataka baadhi ya wananchi na wanasiasa kuacha kufanya siasa za ‘kufilisika’ kwa kumchafua mgombea wa urais wa Zanzibar kwa kumhusisha na mambo ambayo hayamhusu.

Alieleza kuwa Mwinyi ana sifa zote za kuwa Rais wa Zanzibar pia ni mtu mtiifu, mwadilifu mwenye hekima na busara.

Kwa upande wake, Dk. Mwinyi aliahidi kuendeleza na kuimarisha umoja wa kitaifa wa Wazanzibari wote na kuyalinda Mapinduzi na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.


Share:

MTIFUANO CCM UBUNGE, 700 WAJITOKEZA KUCHUKUA FOMU MKOANI SINGIDA

 Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Singida, Edina Kiguru (kushoto) akimkabidhi fomu mgombea Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Sara Mwambu.
 Mgombea Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Jemima Richard Billiah (katikati) akionesha fomu yake baada ya kukabidhiwa juzi. Kushoto ni Mpambe wake Hamisi Soud na Kulia ni kaka yake, Pascal Billiah.
 Mgombea Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Diana Chilolo, akionesha fomu yake baada ya kukabidhiwa juzi. Kulia ni Mpambe wake Jamila Juma. 
 Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Singida, Edina Kiguru (kushoto) akimkabidhi fomu Aysharose Mattembe aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, ambaye anatetea nafasi yake hiyo.

Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Singida, Edina Kiguru (kushoto) akimkabidhi fomu mgombea Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Martha Mlatha.

 Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Singida, Edina Kiguru (kushoto) akimkabidhi fomu mgombea Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Mhadhiri Dkt. Theresia Mnaranara.

  Mgombea Ubunge Singida Mjini, Charles Kisuke, akionesha fomu yake baada ya kukabidhiwa juzi.

  Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi, Noverty Kibaji (kulia) akimkabidhi fomu aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu ambaye anatetea nafasi yake.
   Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Singida Mjini, Hamis Shaban (kushoto) akimkabidhi fomu aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Musa Sima ambaye anatetea nafasi yake.
 Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Singida, Edina Kiguru (kushoto) akimkabidhi fomu mgombea Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Martha Gwau.

 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi, Noverty Kibaji (kulia) akimkabidhi fomu aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu ambaye anatetea nafasi yake.
 Mwanahabari Haris Kapiga (kulia) akikabidhiwa fomu kwa ajili ya kugombea Ubunge Jimbo la Iramba Mashariki.
  Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Singida, Edina Kiguru (kushoto) akimkabidhi fomu mgombea Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Stellah Mwagowa.

 Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Singida, Edina Kiguru, akikabidhi fomu. 
 Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Singida, Edina Kiguru, akikabidhi fomu.
**
Na Dotto Mwaibale, Singida
UCHAGUZI wa nafasi ya Ubunge mwaka huu umetia fora baada ya wagombea zaidi 700 kujitokeza kuomba ridhaa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika nafasi mbalimbali za majimbo na kata mkoani Singida.

Idadi hiyo imekuwa ni gumzo kwa wananchi na wana CCM ambapo cha miaka iliyopita hakukuwa na wingi wa wagombea kama ilivyo uchaguzi wa mwaka huu.

Akizungumza jana wakati akitoa taarifa za awali Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM wa Mkoa huo, Ahmed Kaburu Kaburu alisema kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu kunaonesha mwamko mkubwa na wanaikubali Serikali hii ya awamu ya tano jinsi inavyofanya kazi.


Akizungumzia mchakato wa uchukuaji wa fomu alisema kwa makundi yote manne ya vijana, wazazi, madiwani, viti maalumu  na majimboni wagombea 710 wamejitokeza kuchukua fomu kwa juzi tu hadi kufikia saa 10 jioni.

Alisema akianza na Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi mpaka juzi jioni ni mgombea mmoja aliyekwisha chukua fomu kupitia wanawake ambapo kwa Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM walikuwa wanne.

Kaburu alisema kwa Umoja wa Wanawake wa chama hicho UWT mpaka muda huo waliochukua fomu walikuwa 27 huko wagombea wote katika majimbo 8 ya Mkoa wa Singida wakiwa 119.

Aidha Kaburu alisema kwa nafasi ya udiwani waliichukua fomu katika kata zao walikuwa 420 huku madiwani wa viti maalumu ambao wanagombea kitarafa waliochukua fomu ni 129.

"Ndugu waandishi wa habari napenda kuwaambia kwamba tu kazi bado inaendelea na mwisho wa mchakato huu wa kuchukua fomu nitatoa majina ya wagombea wote na kata zote ili muwafahamu" alisema Kaburu.




Share:

PAKUA APP YA MALUNDE 1 BLOG ILI TUWE TUNAKUTUMIA HABARI NA MATUKIO MSIMU HUU WA UCHAGUZI BURE KWENYE SIMU YAKO

Share:

FULL POWER, ZATI 50 NI KIBOKO YA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA UUME MDOGO

Zati 50
Full Power
Sababu za upungufu wa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume:


⇒Ngiri,

⇒Henia

⇒Kisukari

⇒Tumbo kujaa gesi

⇒Kutopata choo vizuri

⇒Utumiaji madawa kwa muda mrefu

⇒Unywaji wa pombe kupita kiasi

⇒Msongo wa mawazo 



⇮⇒Haya yote hupelekea mwili kutokuzalisha homoni ya gesrtogine au kuwa chache na kushindwa kupata mzunguko mzuri wa damu na vichocheo vingine kama madini ya zinki ambayo hukufanya kuwa na msisimko  na kufanya kuwa na muda  mrefu na nguvu za kutosha.



FULL POWER



⇨Ni dawa ya vidonge ya miti shamba inaongeza nguvu za kiume na kutibu kabisa tatizo hilo.



⇨Inaongeza hamu ya tendo la ndoa

⇨Inakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya Dakika 30 na kurudia tendo zaidi ya mara nne na zaidi.

Zati 50


⇨ Inarutubisha maumbile ya uume  na kunenepesha urefu nchi 6,unene sentimita 4


⇨Dawa hii ni ya kutibu kabisa tatizo hilo.



Pia tunatibu Magonjwa mengine Kama



Matatizo ya pumu,Bawasiri, vidonga vya tumbo,Kisukari,Magonjwa sugu ya zinaa,Kaswende,U.T.I , kiuno,miguu kuwaka moto, Fangasi sehemu za Siri, kupunguza unene wa mwili,tumbo kuunguruma,kujaa gesi, matatizo ya uzazi kwa wanawake, kurutubisha mbegu za uzazi kwa akina baba, matatizo ya meno tunatibu bila kungoa

Kliniki yetu inapatikana Zanzibar, Dar es salaam na Shinyanga.

Wasiliana nasi kwa simu namba 071770 22 27
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS JULAI 16,2020


















 

Share:

TUME YA USHIRIKA YAFANYA KIKAO CHA PAMOJA NA TAKUKURU


Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU ,Brigedia Jenerali John Mbungo (kulia) akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya TCDC na Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa wenye lengo la kuimarisha usimamizi na Maendeleo ya Vyama vya Ushirika nchini.

Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt.Benson Ndiege akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya TCDC na Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa wenye lengo la kuimarisha usimamizi na Maendeleo ya Vyama vya Ushirika nchini.

Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika,Charles Malunde akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya TCDC na Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa wenye lengo la kuimarisha usimamizi na Maendeleo ya Vyama vya Ushirika nchini.



Viongozi wa tcdc wakiwa katika katika kikao cha pamoja kati ya TCDC na Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa wenye lengo la kuimarisha usimamizi na Maendeleo ya Vyama vya Ushirika nchini.

Viongozi wa TCDC na TAKUKURU wakiwa katika Picha ya Pamoja mara baada ya kikao cha pamoja kati ya TCDC na Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa wenye lengo la kuimarisha usimamizi na Maendeleo ya Vyama vya Ushirika nchini.


Tume ya Maendeleo Ushirika Tanzania (TCDC) imekutana katika Kikao cha Pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa lengo la kuimarisha usimamizi na maendeleo ya Vyama vya Ushirika nchini.

Kikao hicho kimefanyika Julai 15, 2020 Jijijini Dodoma katika makao makuu ya Tume ya Maendeleo Ushirika Tanzania, ambapo ujumbe wa TAKUKURU uliongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Brigedia Jenerali John Mbungo, na ujumbe wa TCDC uliongozwa na Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtedaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Dkt. Benson Ndiege.

Kikao hicho kililenga kuainisha majukumu ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) na majukumu ya TAKUKURU ili kuwa na uelewa wa pamoja katika kuimarisha usimamizi na maendeleo ya Vyama vya Ushirika nchini.

TAKUKURU iliwasilisha Taarifa ya Uchunguzi na Fedha zilizokusanywa na Taasisi hiyo kwa niaba ya Vyama vya Ushirika nchi nzima baada ya kukabidhiwa kazi hiyo na Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga.

Wajumbe wa Kikao hicho vilevile walijadili mfumo na utaratibu unaotumiwa na TAKUKURU katika urejeshaji wa fedha zilizokusanywa kwenye Vyama vya Ushirika na kuangalia njia na mbinu za kuzuia mianya ya wizi na ubadhirifu katika Vyama vya Ushirika. Aidha, TAKUKURU na TCDC walikubaliana kuhusu maeneo ya kushirikiana kati ya taasisi hizo mbili.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbungo, amepongeza ushirikiano uliotolewa na Tume ya Maendeleo Ushirika kwa TAKUKURU wakati wakitekeleza maagizo ya viongozi Serikali katika urejeshaji wa fedha kwenye Vyama vya Ushirika zilizokuwa zimechukuliwa bila kufuata utaratibu.

“Tuleteeni matatizo na changamoto zinazohusu ubadhirifu unaofanywa na baadhi ya watu wanaoviibia Vyama vya Ushirika ili tushughulike nao na kuhakisha kuwa mali za wanaushirika zinakuwa salama,” amesema Brigedia Jenerali Mbungo.

Mrajis wa Vyama vya Ushirika, Dkt. Benson Ndiege amesema kuwa kazi iliyofanywa na TAKUKURU katika katika urejeshaji wa fedha kwenye Vyama vya Ushirika zilizokuwa zimechukuliwa bila kufuata utaratibu imewezesha kutoa ujumbe mahsusi kuwa fedha na mali za Wanaushirika hazitakiwi kuchezewa.

“Tutaendelea kushirikiana na TAKUKURU katika kuhakikisha kuwa mali za wanachama wa Vyama vya Ushirika zinalindwa na kuwanufaisha Wananchi na Warajis Wasaidizi wa Vyama vya Ushirika wa Mikoa na Maafisa Ushirika wa Wilaya waendelee kushirikiana na Maafisa wa TAKUKURU katika maeneo yao ili kulinda mali za Wanaushirika,” amesema Dkt. Ndiege.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger