Wednesday, 15 July 2020

Serikali Kuendelea Kununua Mazao Ya Wakulima

Wakulima nchini wamehakikishiwa kuwa serikali itaendelea kununua mazao yao kwa ajili ya kuongeza hifadhi ya kutosha ili kuwa na uhakika na usalama wa chakula nchini.

Kauli hii ya serikali imetolewa jana wilayani Mbalali na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya wakati alipotembelea kituo cha ununuzi zao la mpunga kijiji cha Uturo unaofanywa na Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula ( NFRA) kanda ya Makambako

“Serikali kupitia wizara ya Kilimo itaendelea kununua mazao ya wakulima hususan mahindi na mpunga kwa wingi hivyo wakulima msidanganywe kuwa muda umebaki mfupi wa kupeleka mazao yenu NFRA. Leteni hapa mpunga wenu tutaununua wote” alisema Kusaya.

Akiwa katika ghala la Ushirika Uturo Mbarali Katibu Mkuu huyo aliongea na wakulima wa mpunga na kuwahakikishia kuwa wizara imejipanga kuona nchi inaendelea kuwa na usalama wa chakula ndio maana anapita mikoani kujionea hali ya uzalishaji mazao

Kwa mujibu wa Kaimu Meneja wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Makambako Frank Felix alisema tayari wakala umeshanunua tani 1,700 za mpunga kati ya malengo ya tani 5,000 na mahindi tani 2,933.174 kati 25,000 msimu huu.

Akizungumza kwa niaba ya wakulima wa mpunga Mbarali Said Nkenja alishukuru Serikali kwa uamuzi wake wa kununua mpunga kwani umesaidia kuongeza ushindani wa bei sokoni.

“Tunamshukuru sana Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa uongozi wake unaowajali wakulima nchin.Leo Mbarali tunafurahia kuuza mpunga kwa NFRA tena bei ni nzuri .Tunaomba iendelee kununua zaidi mpunga upo mwingi tunavuna bado” alisema mkulima Said Nkenja.

Katika hatua nyingine  Katibu Mkuu Kusaya alitembelea  Chuo cha mafunzo ya Kilimo na Mifugo  ( MAMRE) cha Wanging’ombe mkoani Njombe  na kutoa agizo kuwa wanafunzi wanaoshindwa kulipa ada ya mafunzo wasifukuze badala yake utafutwe utaratibu rafiki.

Kusaya alitoa agizo hilo kufuatia malalamiko ya wanafunzi kusema baadhi yao wameshindwa kuendelea na masomo baada ya kushindwa kulipa ada na michango mingine.

“Vyuo vyote 29 ( 14 vya serikali na 15 vya binafsi) ni vyangu kwani vinalenga kuzalisha maafisa ugani watakaokwenda kuhudumia wakulima nchini.Nitaendelela kuvisaidia bila kuangalia nani  anakimiliki muhimu vitoe mafunzo bora kwa wanafunzi wa kitanzania” alisema Kusaya.

Kusaya aliusihi uongozi wa chuo cha MAMRE  kutafuta njia rafiki kuwasaidia wanafunzi wenye mazingira magumu yanayosababisha kutolipa ada kwa muda.

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu huyo ameahidi kutoa kompyuta  ili kuwezesha kuanzisha maktaba mtandao ( e- learning) na kugharimia mwanafunzi mmoja kwenda kujifunza kanuni bora za ufugaji kuku kisasa katika vhuo cha Ihemi Iringa kwa gharama za serikali.

Katibu Mkuu amesema katika kuboresha mafunzo kwa vitendo atakipatia Chuo hicho Kitalu nyumba moja (Green House) ili wafundishe klimo cha mbogamboga na matunda ( horticulture).

Chuo cha MAMRE kina wanafunzi 103 wa ngazi ya astashahada na stashahada.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Geofrey  Mapesa alisema changamoto kubwa Kwa sasa ni kukosekana kwa mfumo wa udahili wa pamoja ( Central Admission System) hali inayopelekea upungufu wa wanafunzi.

Tayari wanafunzi 169 wamehitimu mafunzo ya kilimo na mifugo tangu chuo hicho kilipoanzishwa mwaka 2014 chini ya Kanisa Katoliki Jimbo la Njombe.


Share:

Tangazo la kuitwa Kazini TANESCO July 2020

Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO) – TANESCO Job placements as provided by The Public Service Recruitment Secretariat (PSRS)  The Public Service Recruitment Secretariat (PSRS) is a government organ with a status of independent Department established specifically to facilitate the recruitment process of employees to the Public Service.

The post Tangazo la kuitwa Kazini TANESCO July 2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Laboratory Technician at The Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation

Job title:  Laboratory Technician Immediate Supervisor:  Facility In charge Secondary Supervisor:  Council Project Coordinator Job grade:  Grade 1 Duration:  Six Months with possibilities of Extension Location:  Iramba, Singida (1)   ​The Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation is a global leader in the fight against pediatric HIV and AIDS, working in 19 countries and supporting close to […]

The post Laboratory Technician at The Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Data Risk Analyst at NMB Bank

Data Risk Analyst  Job Purpose The Analyst is responsible for executing investigations to identify relationships that pose money laundering, terrorist financing, fraud, and sanctions risks. The Analyst/Investigator compiles evidence and documentation in compliance with AML procedures and regulatory requirements prior to escalations of potential Suspicious Transaction Reports (STRs) to Money Laundering Reporting Officer (MLRO). Ensure […]

The post Data Risk Analyst at NMB Bank appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Education Technical Assistant – Vocation Skills at Tanzania, Norwegian Refugee Council

NRC Tanzania is looking for Education  Technical Assistant – Vocation Skills base at Mtendeli The purpose of the technical assistant position is to assist in the day-to-day implementation of the Education project. All NRC employees are expected to work in accordance with the organization’s core values: dedication, innovation, inclusivity and accountability. These attitudes and believes shall […]

The post Education Technical Assistant – Vocation Skills at Tanzania, Norwegian Refugee Council appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Senior Manager, Compliance at NMB Bank

Senior Manager, Compliance   Job Purpose Serving as the Data Protection Officer of the bank (DPO), is expected to support the design, development and implementation of strategies, standards and procedures to support the Data Governance program while facilitating adherence to NMB Enterprise Data Governance framework for data policies, standards and practices. In close coordination with Head […]

The post Senior Manager, Compliance at NMB Bank appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JULAI 15,2020


Magazetini leo Jumatano July 15,2020...habari kubwa Mafuriko ubunge majimboni




















Share:

Tuesday, 14 July 2020

Atiwa Mbaroni Kwa tuhuma ya kusafirisha shehena ya madawa ya binadamu, sambuli 149 zenye Nembo ya Serikali, MSD

Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linamshikilia Fredrick Anaclet Maxmilian (38) mkazi wa Mbagala Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma ya kusafirisha shehena ya madawa ya binadamu, sambuli 149 baadhi yakiwa na nembo ya MSD.

Hayo yamebainishwa leo na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP. Gilles Muroto wakati akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dodoma.

Aidha Muroto amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa mnamo tarehe 09/07/2020 majira ya saa moja jioni.

Amesema katika mahojiano na mtuhumiwa huyo imeonekana kuwa yeye siyo daktari wala mfamasia na dawa ila anashirikiana na mfamasia ambaye ni mtumishi wa Serikali (jina limehifadhiwa) huko mkoani Tabora.

Kamanda Murotto amesema uchunguzi unaendelea na watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Hoapitali ya mkoa wa Dodoma Dkt.Samuel Seseja amesema shehena hiyo ina dawa aina nane ambapo zipo zenye nembo ya Serikali,pia zipo zenye nembo ya MSD na nyingine hazina nembo.

Hata hivyo amesema dawa hizo hazitakiwi kuuzwa na mtu yeyote kwani kuna wazabuni wa kufanya kazi hiyo katika kila mkoa.

Lengo lilikuwa ni kuziuza kwenye maduka mbalimbali ya dawa jambo ambalo siyo sahihi.

“Uuzaji wa dawa unalindwa na sheria inayotoa namna gani dawa hizo ziweze kununuliwa na kuuzwa, hivyo hicho ni kinyume na sheria inayosimamia suala la dawa na vifaa tiba.”amesema Dkt.Seseja.

Alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa wafanyabiashara na watoa huduma kutojihusisha na ununuzi wa dawa kutoka kwa vyanzo ambavyo havifahamiki na kwamba  wanapaswa kununua kwenye maduka ya dawa yaliyosajiliwa na mfamasia Mkuu wa Serikali.

Pia amewataka kutojihusisha na watoa huduma wasio waaminifu wanaoitia doa Serikali inayofanya kazi nzuri ya kuwahudumia wananchi.


Share:

Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo Achukua Fomu Ya Kugombea Ubunge Jimbo la Kisarawe

Waziri wa TAMISEMI S Jimbo elemani Jafo, leo Julai 14, 2020, amechukua fomu ya kuomba ridhaa  ya chama chake ili kimteue kwa ajili ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Kisarawe.



Share:

Aliyekuwa Mlinzi wa zamani wa Baba wa Taifa ambaye pia alikuwa mlinzi mkuu wa Lowassa Achukua Fomu Ya Ubunge Jimbo la Kilombero

Aliyekuwa Mlinzi wa zamani wa Baba wa Taifa ambaye pia alikuwa mlinzi mkuu wa Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa,  Aloyce Tendewa amechukua fomu ya kuwania ubunge jimbo la Kilombero kwa tiketi ya CCM


Share:

Waziri wa Elimu Prof Joyce Ndalichako Achukua Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Kasulu Mjini

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako, leo Julai 14, 2020, amechukua fomu ya kuomba ridhaa chama chake ili kiweze kumteua, aweze kugombea Ubunge katika jimbo la Kasulu Mjini kupitia


Share:

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga Achukua Fomu Ya Kugombea Ubunge Jimbo La Vwawa Kupitia Tiketi Ya CCM

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga amechukua Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi leo Julai 14, 2020. 

Anayemkabidhi fomu hiyo ni Katibu wa CCM Wilaya ya Nbozi Ndg Julius Mbwiga.


Share:

EUNICE JACKSON WISWA ACHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE SHINYANGA MJINI

Share:

Godbless Lema 'Atamba' Kushinda Ubunge Arusha Mjini....."Natamani Wawe 30 ili Nishindane Nao"

Mbunge wa Arusha Mjini anayemaliza muda wake,  Godbless Lema amesema sheria ingeruhusu, angetaka wagombea wote wa CCM Arusha ashindane nao.

 
“Nime sikia sikia majina ya wagombea Ubunge Arusha Mjini kupitia ccm.Kama sheria ingeruhusu wote 30 kushindana nami na picha zao wote kutokea kwenye karatasi ya kura dhidi yangu,bado wangeimba wimbo walio imba 2010/2015.Twendeni mpaka mwanzo wa bahari,wepesi sana hawa.” ameandika Lema kwenye ukurasa wake wa twitter.

Leo, CCM imefungua pazia kwa wanachama wake kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea nafasi hiyo, zoezi hilo linatarajiwa kusitishwa tarehe 17 Julai 2020.


Share:

Mtoto wa Lowassa Achukua Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Monduli

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Monduli, Langael Akyoo, leo Jumanne July 14,2020 amemkabidhi Fredrick Lowassa fomu ya kuomba ridhaa ya Chama hicho ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Monduli. Fredrick ni Mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa.


Share:

Angela Kairuki Achukua Fomu Ya Ubunge Same Magharibi

Waziri wa Uwekezaji, Angellah Jasmine KAIRUKI akichukua Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Same Magharibi kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi leo Julai 14 , 2020. 

Anayemkabidhi fomu hiyo ni Katibu wa CCM Wilaya ya Same Victoria Mahembe.


Share:

MTOTO WA MUUZA KAHAWA 'HASSAN FATIU' ACHUKUA FOMU KUNYAKUA UBUNGE SHINYANGA MJINI

Wakili  Hassan Athuman Fatiu maarufu 'Mtoto wa Muuza Kahawa' akionesha fomu ya Kuomba Kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo Jumanne Julai 14,2020 katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini. 

Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Hassan Athuman Fatiu ambaye ni Wakili na Mkulima wa mpunga, mkazi wa kata ya Kitangili amesema endapo chama chake kitampa ridhaa ya kugombea ubunge jimbo la Shinyanga kipaumbele chake kikubwa ni Ilani ya Uchaguzi ya CCM na vipaumbele binafsi vitakavyofikishwa katika ofisi ya mbunge. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger