Saturday, 2 May 2020
Friday, 1 May 2020
Mwenyekiti wa Soka la Wanawake Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Maneno Tamba Afariki Dunia.....TFF Waomboleza
KAMPUNI YA AGORA WOOD PRODUCT YAKABIDHI VIFAA VYA KUKABILIANA NA CORONA KWA JESHI LA POLISI IRINGA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Juma Bwire (kulia) akipokea vifaa vya kujikinga dhidi ya Virusi ya Covid 19 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Agora Wood Product, Elisha Edson, vyenye thamani Tsh Milioni 6. 5 kuwasaidia askari Polisi kujilinda afya zao. (Picha na Datus Mahendeka wa Jeshi la Polisi)
Wenye Virusi Vya Corona Nchini Kenya Wafika 411....Ni Baada ya Wengin 15 Kuongezeka
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema leo Ijumaa, Mei 1, wakati wa kikao na wanahabari
Idadi hiyo sasa inafikisha watu walioambukizwa virusi hivyo nchini Kenya kuwa 411.
Aidha watu wanne pia wamefarikina kufikisha idadi ya waliofariki kuwa 21.
Aidha watu wanne pia wamefarikina kufikisha idadi ya waliofariki kuwa 21.
Trump: Virusi vya Corona vilitengenezwa katika maabara ya China
Rais wa Marekani Donald Trump amedai kuwa ameona ushahidi kwamba virusi vya corona vilitoka katika maabara ya China.
Trump amesema hayo huku akitishia kuongeza ushuru kwa China kutokana na ilivyolishughulikia janga la corona ambalo limeukumba ulimwengu mzima.
Hata hivyo, madai hayo ya Rais Trump yamekosa kutiwa uzito baada ya maafisa wa intelijensia pamoja na waziri wake wa mambo ya nje, Mike Pompeo, kusema kuwa hawajui kwa ni wapi virusi hivyo vilianzia.
Ukosoaji wa hivi karibuni wa Trump dhidi ya China umejiri, huku takwimu zinaonesha kwamba Wamarekani milioni 30 wamepoteza ajira kufuatia masharti ya kutotoka nje.

Kampuni Zaununuzi Wa Tumbaku Ushetu Zaingia Mitini Wakulima Wakidai Zaidi Ya Shilingi Milioni 80
Baada ya kuwepo kwa Malalamiko ya Wakulima wa tumbaku kutolipwa fedha na kampuni za ununuzi wa zao hilo katika msimu wa 2019/20 katika Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo limeagiza kufanyika kwa uhakiki wa madai hayo kabla kufanyika kwa Masoko mapya ya mwaka 2020/21.
Uamuzi huo ulitolewa Aprili 30 na Mwenyekiti wa Halmashauri ya hiyo, Juma Kimisha katika kikao cha kawaida cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2019/20 kuanzia Januari hadi Marchi baada ya kupokea taarifa mbalimbali za maendeleo zilizotekelezwa na serikali.
Alisema kuwa katika vyama vya Msingi Kangeme,Tumaini na Ilomelo wakulima wake wanazidai kampuni za ununuzi wa zao hilo zaidi ya Milioni 80 baada ya kuchukua mazao yao katika Msimu uliopita na hadi sasa hawajui ni lini watapata stahiki zao.
“Diwani wa Kata ya Ulowa Paschal Mayengo aliwasilisha malalamiko ya wakulima wake hapa ya kutolipwa fedha na kampuni za Jaspay na Magepa ambazo zinafikia Dola elfu 35000 ambazo mpaka hivi sasa hawajalipwa huku msimu mpya ukitarajiwa kufunguliwa Mwezi Mei mwaka huu,”alisema Kimisha.
Nae Diwani wa kata ya Igunda Tabu Katoto alishauri ofisi ya Mkurugenzi kufuatilia kwa kina Madai yao ili kudhibiti vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na baadhi ya kampuni hizo ambazo hazina nia ya kuwakomboa wakulima wa Ushetu.
“Tuweke msisitizo kwa kampuni zote za ununuzi wa zao hili zihakikishe zinajenga ofisi ili wakulima wetu wasiwe wanahangaika na itasaidia kwabana viongozi wake ikilinganishwa na hivi sasa ambako hatujui wamiliki wake na ni wapi wapatikana,”alisema Katoto.
Akipokea Maelekezo ya kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Michael Matomora alikiri kuwepo kwa madai ya wakulima hao na kuomba kupewa muda kwaajili ya kufanya uhakiki ili kujua uhalali wake.
“Nipeni muda ili niwezekufanya kazi hii kwa ukamilifu niwaahidi nitatoa taarifa kwa kina katika kikao cha Kamati ya fedha ambacho kitaketi hivi karibuni,”alisema Matomora.
Mwisho.
“sijaridhishwa Na Utendaji Kazi Wa Chama Kikuu Cha Ushirika Geita” - Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo ametembelea Chama Kikuu cha Mkoa wa Geita (Geita Cooperative Union-GCU) kilichopo Kasamwa wilaya ya Geita na kutoridhishwa na hali ya kiwanda cha kuchambua pamba kushindwa kufanya kazi muda mrefu.
Ametoa kauli hiyo leo (01.05.2020) wakati alipotembelea na kukagua shughuli za taasisi zilizo chini ya wizara yake na kusema kiwanda cha kuchambua pamba (ginnery) Kasamwa kimeshindwa kujiendesha kutokana na mitambo na majengo yaliyopo kuwa ya kizamani yaliyotumika toka mwaka 1956
“Nimekagua na sijaridhishwa na jinsi kiwanda (ginnery) hii ya Kasamwa kuona haina hata mtambo mmoja unaofanya kazi hali inayopekea pamba ya ya wakulima kuchakatwa kwenye viwanda binafsi “ alisema Kusaya
Amewaagiza viongozi wa Chama kikuu cha ushirika Geita kushirikiana na serikali ya mkoa na wadau kufufua kiwanda hicho ili kitumike kuongeza thamani ya zao la pamba inayozalishwa wa wakulima wa Geita kwa kutafuta mitambo ya kisasa.
Awali Katibu Mkuu Kusaya alikagua kiwanda cha Matongo Farming Limited cha Geita na kukuta kimesimama kuzalisha marobota ya pamba kutokana na upungufu wa malighafi.
Kiwanda hicho kinachomilikiwa na Samson Ng’walida kilianzishwa mwaka 2018 na kina uwezo wa kuzalisha marobota 450 kwa siku na kuchambua pamba mbegu tani 270 kwa siku.
“Uwezo wa kiwanda ni kuchambua tani 48,600 kwa mwaka na msimu huu wa 2019/2020 tumefanikiwa kuzalisha jumla ya robota 9,412 za pamba nyuzi sawa na asilimia 19 ya uwezo wa kiwanda” alisema Mwalida Samson ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa kiwanda cha Matongo Ginery.
Kufuatia hali hiyo Katibu Mkuu Kusaya alitoa wito kwa mikoa yote 17 inayozalisha pamba nchini kutengeneza mazingira rafiki kwa wananchi na wawekezaji ili waongeze uzalishaji wa pamba kukidhi malengo ya Serikali ya awamu ya Tano kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda.
“Napenda kuona uchakataji wa pamba unafanyike mwaka mzima badala ya miezi mitatu au minne ya sasa kutokana na ukosefu wa malighafi hali inayosababisha ajira kupungua na serikali kukosa mapato kutokana na viwanda kutozalisha bidhaa za pamba” alisema Kusaya.
Amewataka wataalam wa kilimo nchini kuwasaidia wakulima kupata ya mbegu bora za pamba zinazozalishwa kituo cha utafiti TARI Ukiriguru pamoja na matumizi ya pembejeo na mbolea ili kuongeza tija na uzalishaji wa zao hilo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba Tanzania Marco Mtunga alisema takwimu zinaonesha mkoa wa Geita umezalisha kilo milioni 33 za pamba katika msimu wa 2019 kiasi ambacho ni kidogo kulingana na mahitaji makubwa ya viwanda vilivyopo mkoani humo.
Aliongeza kusema uwezo wa viwanda vya ndani nchini kwa sasa ni kuchakata pamba ni tani milioni 1.2 wakati uzalishaji umefikia tani 348,910 na kusema bodi yake itaendelea kubuni mikakati mizuri ili uzalishaji pamba uongezeke.
Mwisho
Imetolewa na :
Kitengo cha mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Kilimo
FULL POWER, ZATI 50 NI KIBOKO YA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA UUME MDOGO
Zati 50
Full Power
⇒Ngiri,
⇒Henia
⇒Kisukari
⇒Tumbo kujaa gesi
⇒Kutopata choo vizuri
⇒Utumiaji madawa kwa muda mrefu
⇒Unywaji wa pombe kupita kiasi
⇒Msongo wa mawazo
⇮⇒Haya yote hupelekea mwili kutokuzalisha homoni ya gesrtogine au kuwa chache na kushindwa kupata mzunguko mzuri wa damu na vichocheo vingine kama madini ya zinki ambayo hukufanya kuwa na msisimko na kufanya kuwa na muda mrefu na nguvu za kutosha.
FULL POWER
⇨Ni dawa ya vidonge ya miti shamba inaongeza nguvu za kiume na kutibu kabisa tatizo hilo.
⇨Inaongeza hamu ya tendo la ndoa
⇨Inakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya Dakika 30 na kurudia tendo zaidi ya mara nne na zaidi.
Zati 50
⇨ Inarutubisha maumbile ya uume na kunenepesha urefu nchi 6,unene sentimita 4
⇨Dawa hii ni ya kutibu kabisa tatizo hilo.
Pia tunatibu Magonjwa mengine Kama
Matatizo ya pumu,Bawasiri, vidonga vya tumbo,Kisukari,Magonjwa sugu ya zinaaa,Kaswende,U.T.I , kiuno,miguu kuwaka moto, Fangasi sehemu za Siri, kupunguza unene wa mwili,tumbo kuunguruma,kujaa gesi, matatizo ya uzazi kwa wanawake, kurutubisha mbegu za uzazi kwa akina baba, matatizo ya meno tunatibu bila kungoa
Kliniki yetu inapatikana Zanzibar, Dar es salaam na Shinyanga.
Wasiliana nasi kwa simu namba 071770 22 27
HUYU NDIYO AUGUSTINE MAHIGA...WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA TANZANIA ALIYEFARIKI DUNIA GHAFLA DODOMA
Balozi Dkt Augustine Mahiga alizaliwa Agosti 28, 1945, Kijiji cha Tosamaganga mkoani Iringa, alisoma elimu yake ya Msingi na Sekondari hapa nchini na baadaye mwaka 1968, alijiunga na Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki, DSM na kuhitimu Shahada ya Sanaa akibobea kwenye Elimu mwaka 1971.
Marehemu Balozi Dkt Augustine Mahiga, aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Baadaye alipata ufadhili wa masomo yake nchini Canada, katika Chuo Kikuu cha Toronto na kuhitimu Shahada ya Sanaa na baadaye aliendelea na masomo katika chuo hicho hicho akijikita katika uhusiano wa Kimataifa na kuhitimu mwaka 1975 .
Mwaka 1980 hadi 1983, Balozi Dkt Mahiga alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, baadaye pia aliteuliwa kuwa mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Kimataifa akifanya kazi Geneva - Uswisi, ambapo baadaye mwaka 1992 na 1994 aliteuliwa kuwa kiongozi mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHRC).
Balozi Dkt Mahiga ni Mwanadiplomasia wa Tanzania na Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Tanzania kutoka 2015-2019 na hapo awali aliwahi kuwa Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwa Umoja wa Mataifa, kutoka 2003 hadi 2010 na kama Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa (UN) na Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Umoja wa Mataifa kutoka Somalia 2010 hadi 2013.
Mnamo Machi 03, 2019, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, alimteua Balozi Dkt Augustine Mahiga kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, akichukua nafasi ya Profesa Palamagamba Kabudi, na aliapishwa Machi 4, 2019
Balozi Dkt Augustine Mahiga ameaga Dunia mapema leo Mei 1, 2020, Jijini Dodoma, baada ya kuugua ghafla.
Mungu ailaze roho ya Marehemu Balozi Dkt Augustine Mahiga, mahala pema peponi. Amina.
FISI AUA MTOTO WA MIAKA MITATU AKICHEZA NA WENZAKE KISHAPU
Kamanda wa polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mtoto aitwaye Sungwa Kulwa mwenye umri wa miaka mitatu (03) mkazi wa kijiji cha Dodoma Kata ya Masanga, wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga amefariki dunia baada ya kushambuliwa na fisi sehemu za kichwani wakati akicheza na wenzake nje ya nyumba yao.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema tukio hilo limetokea jana Aprili 30,2020 majira ya saa moja usiku katika kijiji cha Dodoma Kata ya Masanga, Wilaya ya Kishapu
“Mtoto huyo alikuwa akicheza na watoto wenzake nje ya nyumba yao umbali wa mita kumi, ndipo fisi huyo alitokea kwa ghafla kutoka vichakani na kumshambulia kisha kumburuza umbali wa mita 100 ambapo alimuachia baada ya kusikia kelele za wananchi waliokuwa wakimfukuza”,ameeleza Kamanda Magiligimba.
Kamanda Magiligimba ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha watoto wako mazingira salama muda wote, wasiachwe peke yao na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari hasa kwa kipindi hiki ambacho fisi wamekuwa wakionekana maeneo mbalimbali ya mkoa wa Shinyanga.
RAIS UTPC : WAAJIRI KATIKA VYOMBO VYA HABARI WABORESHE MASLAHI YA WAANDISHI WA HABARI KIPINDI HIKI CHA COVID - 19
Leo ni Mei Mosi 2020, tukiadhimisha katika kipindi ambacho tupo katika vita kubwa ya kukabiliana na ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona.
Sekta ya Habari nchini Tanzania ni moja kati ya sekta ambazo zimeathiriwa sana na hali hii.
Wito wangu ni kwa waajiri yaani vyombo vya habari kuboresha maslahi ya waandishi wa habari kutoa ajira rasmi na kuwapa mikataba, kuthamini mchango wa waandishi wa haabri katika vyombo vyao, kulipa kwa wakati madai mbalimbali,kuanza kuwalipa waandishi walau kila wiki ili waweze kukabiliana na changamoto za maisha kwa sasa kutokana na kutokuwepo kwa shughuli na baadhi yao kulazimika kukaa nyumbani.
Ni matumaini yangu wakati tukiadhimisha Sikukuu ya Wafanyakazi, waandishi wa habari nchini wanatumia siku hii kutafakari namna ya kuboresha kazi zao, kuongeza juhudi na maarifa, kuzingatia sheria na taratibu za nchi huku waajiri na wamiliki wakitafakari pia kuzingatia sheria za kazi na sheria nyingine ili kumfanya mwandishi na chombo cha habari kutenda haki na kuwajibika kwa umma.
Nawatakia Sikukuu Njema, TUFANYE KAZI KWA UANGALIFU, TUFUATE MAELEKEZO YA WATAALAMU, CORONA NI HATARI, IPO NA INAUA, TUJILINDE NA TUWALINDE WAPENDWA WETU.
Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).
CHADEMA Yazuia Wabunge Wake Kwenda Bungeni.....Yawataka Wajiweke Karantini Kwa Siku 14
Chama cha Demokrasia na Maendeleo- CHADEMA kimetoa maelekezo kwa Wabunge wake wote, kutohudhuria tena vikao vya Bunge vinavyoendelea,na wajiweke Karantini kwa muda wa siku 14 na wasiende majimboni kwao kipindi hiki mpaka pale watakapothibitika hawana maambukizi ya Virusi vya Corona
Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe leo Ijumaa May 1, 2020 imetoa maelekezo manne kwa wabunge wa chama hicho ambayo ni; Kutohudhuria vikao vya bunge au kamati za bunge,Kutofika eneo la Bunge Dodoma na Dar es Salaam, Wabunge wajiweke karantini kwa muda wa siku 14, wabunge wa chama hicho wasiende mikoani au majimboni bali wabaki Dodoma hadi itakapothibitika hawana maambukizi
Aidha, CHADEMA pia wameshauri Bunge lisitishwe kwa siku 21 ili kuruhusu wabunge wote kwenda Karantini, Wabunge wote wapimwe pamoja na familia zao na Kamati za Bunge zifanye vikao kwa njia ya mtandao

TANZIA: Waziri wa Katiba na Sheria , Mh. Balozi Dkt. Augustine Mahiga, amefariki dunia ......Rais Magufuli Atuma Salamu za Rambirambi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anasikitika kutangaza kifo cha Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Philip Mahiga (Mbunge) kilichotokea leo alfajiri tarehe 01 Mei, 2020 Jijini Dodoma.
Mhe. Balozi Mahiga ameugua ghafla akiwa nyumbani kwake Jijini Dodoma na amefikishwa hospitali akiwa tayari ameshafariki dunia.
Mhe. Rais Magufuli ametoa salamu za pole kwa familia ya Marehemu, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai, Wabunge, Wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria na wananchi wa Mkoa wa Iringa kwa kuondokewa na mpendwa wao, na amesema anaungana nao katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Mhe. Rais Magufuli amemuelezea Marehemu Balozi Mahiga kuwa alikuwa mchapakazi, mwadilifu, mzalendo na Mwanadiplomasia mahiri aliyeiwakilisha na kuipigania Tanzania katika njanya za Kimataifa kwa miaka mingi.
“Pamoja na umri wake mkubwa na uzoefu wa kushika madaraka katika nyadhifa mbalimbali za Kitaifa na Kimataifa, Marehemu Balozi Mahiga alikuwa mnyenyekevu na mtiifu kwa kila jukumu nililomtuma” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Amemuombea kwa Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi, Amina.
Thursday, 30 April 2020
Bilioni 33 Kutumika Kuimarisha Huduma Za Kijamii Nchini Tanzania
NA WAMJW Dodoma
Wizara ya Afya, kupitia Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii inatarajia kutumia Jumla ya shilingi bilioni 33.195 ili kutekeleza shughuli mbalimbali za kijamii hususani zilizopewa kipaumbele kwa mwaka wa fedha 2020/21.
Akiwasilisha Hotuba ya Wizara ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema katika mwaka wa fedha 2020/21 Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii inatarajia kutumia kiasi hicho cha fedha kwa lengo la kuimarisha huduma na mafunzo kwenye Taasisi za Ustawi na Maendeleo ya Jamii, kukarabati makazi ya wazee, kujenga mahubusu za watoto na kutokomeza ukatili wa kijinsia.
Alisema kuwa bajeti hiyo itasaidia kuimarisha Kujenga kumbi pacha na hosteli katika Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru ambapo jumla ya shilingi bilioni 2.7 zimetengwa, pia kuboresha utoaji wa mafunzo ya taaluma ya maendeleo ya jamii ili kukidhi mahitaji ya soko sambamba na kukuza ujuzi wa wahitimu ikiwemo kuwajengea uwezo wa kujiajiri na kuajiriwa kwa kutenga jumla ya shilingi bilioni 6.6.
Maeneo mengine yaliyotengewa fedha ni pamoja na ukarabati wa majengo na miundombinu katika makazi ya wazee kwa shilingi milioni 400, ujenzi wa Shule ya Maadilisho katika Mkoa wa Geita shilingi milioni 200, kuimarisha ujenzi wa mahabusu ya watoto katika mikoa ya Kigoma na Mtwara shilingi milioni 700 na kuwezesha Taasisi ya Ustawi wa Jamii kuboresha utoaji wa mafunzo yanayokidhi mahitaji ya soko shilingi milioni 250.
Aidha, jumla ya shilingi milioni 827.95 zimetengwa kwa ajili ya shughuli za kutokomeza ukatili wa kijinsia katika jamii.
“Ili kutekeleza vipaumbele vilivyoanishwa kwa mwaka 2020/21, Wizara kupitia Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii imekadiria kutumia kiasi cha shilingi bilioni 33 kwa ajili ya kutekeleza majukumu mbalimbali ya Wizara ikiwa ni pamoja na uendeshaji wa ofisi na miradi ya maendeleo” alisema.
Mhe. Ummy amesema Wizara imeendelea kukuza ari ya jamii kushiriki katika kujiletea maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa kutumia nguvu kazi na rasilimali zinazowazunguka na kusimamia masuala yote ya ushirikishwaji wa jamii kwenye sekta mbalimbali.