Wednesday, 25 March 2020

Wananchi Watishia Kufunga Mnara Wa simu Za Mkononi Kwa Kudai Kodi Ya Pango

SALVATORY NTANDU
Serikali ya kijiji cha Bunango kata ya Bugarama Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga imeitaka kampuni ya Helious Tower Tanzania inayosimamia minara ya Mawasiliano ya simu za mkononi kuleta majina ya madalali wanaolipwa fedha za kodi ya pango la minara iliopo katika kijiji hicho baada ya kufanya uhakiki na kujiridhisha kuwa si wamiliki halali wa maeneo yaliyojengwa minara hiyo.

Uamuzi huo umetolewa Machi 23 mwaka huu na Mwenyekiti wa kijiji cha Bunango Anna Peter kata ya Bugarama katika Halmashauri ya Msalala wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi wanaomiki maeneo yaliyojengwa minara hiyo kuhusiana na kutolipwa kodi zao za pango.

Alisema kuwa baada ya kupokea Malalamiko hayo walikaa na kufanya uhakiki juu ya umikili wa maeneo hayo ambapo walibaini kuwepo kwa madalali waliofunga mikataba na kampuni za mawasiliano kinyemela na kulipwa kodi za pango kila mwaka huku wamiliki halali wakiachwa bila kupewa kitu chochote.

“Katika eneo la Mzee Robert Busengwa limejengwa minara miwili ya Kampuni za Airtel na Vodacom sisi kama serikali ya kijiji tumebaini katika eneo ulipojengwa manara wa Vodacom kunadalali ambaye amefunga mkataba na kampuni hii na kulipwa kodi ya pango kila mwaka zaidi ya shilingi milioni 5.5 huku mmiliki halali akiendelea kuteseka”alisema Peter.

Amefafanua kuwa kisheria wamiliki wote wa maeneo yenye uwekezaji wa minara wanapaswa kulipa asilimia 20 ya mapato yao kwenye serikali ya kijiji lakini tangu minara hii imejengwa mwaka 2001 haijawai kulipa fedha zozote kwaajili ya maendeleo ya kijiji.

stahiki zangu naiomba Serikali seikivu ya Rais  Dk John Pombe Magufuli inisaidie mimi mnyonge ili nipate haki zangu,nimechoka kuzunguka nimetumia fedha nyingi ila msaada hakuna,”alisema Busengwa.

Akijibu Malalamiko ya Wakazi hao Msimamizi mkuu wa Minara ya Mawasiliano kutoka kampuni ya Helious Tower mkoa wa Shinyanga ambaye hakutaka jina lake litajwe Gazetini kwa madai kuwa si msemaji wa kampuni hiyo aliwataka wananchi hao kuandikika malalamiko yao na kuyapeleka makao makuu jijini Dar es salaam ili waweze kupata haki zao.

“Haiwezekani mnara ujengwe hapa kwa zaidi ya miaka 10 na kodi ya pango inalipwa kila mwezi halafu asijulikane anayelipwa Helious Tanzania inalipa kodi kila mwaka za upangaji andikeni malalamiko yenu kwa maandishi myatume Makao makuu yatafanyiwa kazi,”alisema.

Mwisho.


Share:

Jamii Yatakiwakutowanyanyapaa Wagonjwa Wa Kifua Kikuu Kwa Kuwahusisha Na Ugonjwa Wa Corona

SALVATORY NTANDU
Jamii Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga imeaswa Kutowanyanyapaa na Kuwatenga Wagonjwa wa Kifua Kikuu wanaoendelea  na Matibabu katika Zahanati na Vituo vya Afya  mbalimbali kwa kuwahusisha na  Ugonjwa wa Korona ambao dalili zake zinashabihiana jambo ambalo linaweza kusababisha Wagonjwa wengi kukata Tamaa na kuacha ufuasi wa matibabu .

Hayo yalibainishwa Machi 24 na Anisia Mrigo Afisa Mradi wa Kifua Kikuu kutoka shirika lisilo la Kiserikali la Shidepha+ wakati akizungumza na Waandishi wa habari Mjini Kahama katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya kifua kikuu Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Machi 24 yaliyokwenda sambamba na utoaji elimu kwa Umma kupitia vyombo vya habari kuhusiana na  ugonjwa huo.

Alisema katika Jamii kumeanza kujitokeza vitendo vya unyanyapaa kwa wagonjwa wa kifua kikuu kutoka  kwa  baadhi ya watu wasiokuwa na elimu sahihi juu ya ugonjwa wa Corona wameanza kuwatenga wagonjwa wa kifua kikuu kwa kuwahusisha kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo jambo ambalo linawezea kusababisha kuongezeka wa maambukizi mapya ya kifua kikuu kwenye jamii.

“Endapo tutawatenga wagonjwa wa kifua kikuu katika jami zetu tunaweza kusababisha wakapoteza maisha kwani wapo baadhi ya watu wameanza kuwanyima chakula,kwa madai ya kuwa dalili za ugonjwa wa Corona zinafanana na ugonjwa wa kifua kikuu”,alisema Mrigo.

Awali akizungumzia Suala hilo Naibu Mkurugenzi Miradi wa Shidepha+  Shekha Nassoro ni alisema kuwa  Wagonjwa wa Kifua Kikuu bado wapo kwenye jamii na wanapaswa kusaidiwa kwa kupatiwa msaada wa matibabu na kutoa rai kwa wananchi kuachana na vitendo hivyo ambayo sio vya kiungwana.

“Katika jamii zetu kama kunamgonjwa wa Kifua kikuu toeni taarifa kupitia mawasiliano yafuatayo bure kwa kupiga *152*05*06# katika kipindi hiki ili kuwasaidia pindi wanapopata matatizo ya kiafya”,alisema Nassoro.

Nae  Meneja Mradi wa Kifua Kikuu kutoka Shirika lisilo la kiserikali la  Shidepha+  Elneus Mwinuka alisema kuwa tangu waanze kutekeleza mradi wa kupambana na kutokomeza kifua kikuu katika mikoa ya Geita na Shinyanga umeweza kuleta matokea chanya kwa kufanikiwa kuwafikia wagonjwa wengi ikilinganishwa hapo awali ambapo ilikuwa ni vigumu wagonjwa wa kifua kikuu kujitokeza hadharani.

“Zamani ilikuwa ni ngumu kwa wagonjwa wa kifua kikuu kujitokeza kupima afya zao wengi wao walikuwa wanaamini kuwa kifua kikuu kinasababishwa na imani za kishirikina jambo ambalo halina ukweli wowote,”alisema Mwinuka.

Kwa upande wake Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma kutoka Hospitali ya Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga Mariamu Mabanga amesema maambukizi ya Kifua Kikuu yapo juu katika jamii ambapo kwa mpaka sasa kuanzia Januari hadi sasa wanawagonjwa 200 ambapo wagonjwa wengi wanatoka katika mikoa ya jirani kama vile Tabora na Geita na kuwaasa wananchi kutowanyanyapaa wagonjwa waliothibitika kuwa na ungonjwa huo kwa muda mrefu.

Mwisho.


Share:

Watumishi Wizara Ya Kilimo Watakiwa Kuchapa Kazi Kwa Weledi

Menejimenti ya Wizara ya Kilimo imetakiwa kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia weledi katika kutekeleza maagizo ya Rais kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na uhakika wa chakula.

Kauli hiyo imetolewa jana (24.03.2020) na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya wakati wa hafla ya makabidhiano rasmi ya ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu Mhandisi Mathew Mtigumwe yaliyofanyika makao makuu ya wizara Mtumba mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo vya wizara.

Kusaya alisema wizara ya kilimo ina changamoto ya kuhakikisha watanzania wanakuwa na uhakika wa chakula kwa kuzalisha mazao kwa wingi na kwa ubora.

“Kila mtumishi wa Wizara ya Kilimo ahakikishe anafanya kazi kwa bidii na weledi kutekeleza malengo yote tuliyowekewa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli kuhakikisha nchi inakuwa na uhakika na usalama wa chakula” alisema Katibu Mkuu Kusaya

Kusaya aliongeza kusema anamshukuru Mhandisi Mtigumwe kwa kazi nzuri aliyoifanya kwa wizara ya kilimo wakati wa uongozi wake ikiwemo kupitia mabadiliko yaliyofanyika katika idara na taasisi.

Kwa upande wake Mhandisi Mtigumwe alisema anawashukuru watumishi wote wa wizara ya kilimo kwa ushikiano waliompa alipokuwa Katibu Mkuu na kwamba anajisikia vema kuona wizara na taasisi zake wanachapa kazi

Alitaja changamoto za sekta ya ushirika na umwagiliaji kuwa zinahitaji msukumo mkubwa ili taswira ya wizara ya kilimo iendelee kuwa nzuri.

“Ushirika bado ni changamoto,nawaachia japo tulianza mchakato wa maboresho ya sheria endeleeni ili wakulima wa Tanzania wanufaike na jasho lao “ alisema Mhadishi Mtigumwe ambaye kwa sasa amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu .

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi, Mkurugenzi wa Mipango Bora ya Ardhi ya Kilimo Paulo Tarimo alimshukuru Katibu Mkuu aliyepita Mhandisi Mtigumwe kwa ushirikiano na maelekezo aliyoyatoa wakati wa utumishi wake.

Mkurugenzi huyo ameahidi kwa niaba ya Menejimenti na watumishi wa wizara ya kilimo kutoa ushirikiano zaidi kwa Katibu Mkuu Kusaya ili malengo ya Taifa yafikiwe.


Share:

Nafasi 60 za Kazi TCAA....Mwisho wa Kutuma Maombi ni 06 April

1. Air Traffic Management Officers II 30 Post at TCAA

QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Bachelor Degree with GPA of 3.0 and above either in Air Traffic Management, Physics, Mathematics, Geography, Geographical Information System, Geomatics or Statistics from an accredited Institution. Candidate should have Passes in English and Geography subjects at Grade C or above in Certificate of Secondary Education (CSEE).

___________________________________

2. Aeronautical Information Officers II 30 Post at TCAA 

QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Bachelor Degree with GPA of 3.0 and above either in Information Technology, Geo-informatics, Geographical Information System or Geomatics from an accredited Institution. Candidate should have Passes in English and Geography subjects at Grade C or above in Certificate of Secondary Education (CSEE).




Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano March 35























Share:

Tuesday, 24 March 2020

RAIS MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI LEO CHAMWINO – DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Baraza cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Mawaziri Ikulu Chamwino. Kikao hicho kimehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Mawaziri wote, Manaibu Mawaziri pamoja na Viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama. Chamwino Dodoma. Machi 24, 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya Pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa,Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. John Kijazi, Mawaziri wote, Manaibu Mawaziri pamoja na Viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama mara baada ya kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu Chamwino – Dodoma. Machi 24, 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa Pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu akitoka nje ya ukumbi wa Baraza la Mawaziri mara baada ya kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu Chamwino – Dodoma. Machi 24, 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, ajira Vijana na Walemavu Mhe. Stella Ikupa  na viongozi wengine mara baada ya kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu Chamwino – Dodoma. Machi 24, 2020.
. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipima joto la mwili kabla ya kuingia katika ukumbi wa Baraza la Mawaziri kuongoza kikao cha Baraza hilo. Kikao hicho kimehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Mawaziri wote, Manaibu Mawaziri pamoja na Viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama. Chamwino Dodoma. Machi 24, 2020.

PICHA NA IKULU


Share:

TASAC TANGA YATAKA VYOMBO AMBAVYO HAVIJAKAGULIWA KUTOKWENDA MAJINI KUFANYA KAZI

SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania Mkoani Tanga (TASAC) limetoa wito kwa vyombo vya usafiri vinavyofanya kazi zake majini ambayo havijakaguliwa na kupata cheti cha ubora kutokwenda majini kufanya shughuli zake.


Agizo hilo lilitolewa leo na Afisa Mfawidhi wa Shirika hilo Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua wakati akizungumza na mwandishi wa habari ofisini kwake.


Alisema kwamba wao wanatoa wito kwa vyombo vya majini kwa kipindi hiki cha masika vyombo ambavyo havijakaguliwa na kupata cheti cha ubora haviruhisiwi kwenda majini.


 Afisa Mfawidhi huyo alisema pia  kwa kipindi hicho vyombo vyote vilivyopata vyeti vya ubora ni vizuri kuchukua tahadhari kuhakikisha vifaa vyote vya umuhimu ikiwemo pampu za kutolea maji yaliyoingia kwenye chombo zinafanya kazi na zipo.


Aidha alisema kwa vyombo ambavyo  na vyombo havitakuwa na vifaa vitakavyostahili kuruhusu kwenda majini wanavitaka visienda kufanya shughuli zozote majini kwa kuchukua tahadhari.


“Tunatoa rai kwa vyombo vizingatia maelelezo hayo kwa sababu kipindi cha masika kinaambatana na hali mbaya ya hewa mawimbi makubwa pamoja na mvua ambazo zinasababisha maji kuingia kwenye chombo na kusababisha uzito”Alisema


Alisema kwamba hivyo kama uwezo wa kutoa maji kwenye chombo utakuwa ni mdogo itakuwa rahisi  kuzama na  hivyo tunatoa wito kwa vyombo vyote hasa kwa uvuvi maelekezo hayo yazingatiwe.


Hata hivyo aliwataka watendaji wa serikali za vijiji na mitaa maeneo ya vyombo vya uvuvi,mizigo vinapotoka kwenye maeneo yao vimekaguliwa na kupatiwa cheti cha ubora na idadi ya vifaa vya uokozi maalumu baharini kulingana na idadi ya wafanyakazi waliopo kwenye chombo hicho.
Share:

Auditor II (2 Positions) Jobs at NMB Tanzania

Auditor II (2 Positions) Reporting Line: Audit Manager Job Purpose To maintain an independent Internal Audit that adds value and improves the operations of the Bank through systematic and disciplined approach in evaluating and improving the effectiveness of risk management, control and governance processes. Main Responsibilities Coordinate audit plans (of small audits) for assigned projects by ensuring all… Read More »

The post Auditor II (2 Positions) Jobs at NMB Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

NGULI WA MUZIKI WA AFRO JAZZ MANU DIBANGO AFARIKI DUNIA KWA CORONA

Nyota mkongwe wa muziki wa Afro-jazz Manu Dibango, amefariki dunia leo baada ya kuambukizwa virusi vya vipya corona. 

Wawakilishi wake wamesema mwanamuziki huyo nguli raia wa Cameroon amefariki dunia  leo asubuhi katika hospitali ya eneo la mji wa Paris, Ufaransa. 

Dibango, aliyekuwa na umri wa miaka 86, na anayefahamika kwa kibao cha "Soul Makossa", cha mwaka wa 1972, ni mmoja kati ya nyota wa kwanza wa kimataifa kufariki dunia kutokana na ugonjwa wa COVID-19.

 Ujumbe ulioandikwa kwenye ukurasa wake wa Facebook umesema kuwa mazishi yake yatafanyika kwa usiri mkubwa, na kwamba hafla ya kumbukumbuka itapangwa katika wakati muafaka.

 Dibango alitengeneza muziki wa Afro jazz na pia kuuchanganya na muziki wa kitamaduni wa Cameroon.
Share:

Wash Assistant Danish Refugee Council – Tanzania

Wash Assistant Danish Refugee Council – Tanzania Job Announcement WASH Assistant-Hygiene Promotion – NATIONAL POSITION (01) Danish Refugee Council (DRC) is an international non-governmental organization which provides assistance and promotes durable solutions for refugees and internally displaced people, on the basis of humanitarian principles and human rights. Danish Refugee Council is a humanitarian actor in Tanzania. Since 2015,… Read More »

The post Wash Assistant Danish Refugee Council – Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Director of Operation Nafasi ya Kazi The Elizabeth Glaser Paediatric AIDS Foundation (EGPAF)

Job title: Director of Operation Reporting to: Country Director Dotted Line Manager: Regional Director of Operations Location: Dar es Salaam Job Summary The Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation is seeking a Director of Operations to support the attainment of the Foundation’s overall goals by providing operational and administrative support to the Tanzania EGPAF program. Reporting to the Country… Read More »

The post Director of Operation Nafasi ya Kazi The Elizabeth Glaser Paediatric AIDS Foundation (EGPAF) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Supply Chain Assistant Danish Refugee Council

Name of the Position: – Supply Chain Assistant Reports to: – Supply Chain Manager Duty Station: – Kibondo Start date: Immediately Duration: 09 months Danish Refugee Council is a humanitarian actor in Tanzania. Since 2015, as part of the Burundian Refugee Response in Tanzania, DRC works in the sectors of camp management, community-based protection, livelihoods, protections, WASH, General… Read More »

The post Supply Chain Assistant Danish Refugee Council appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Controls, Compliance & Ethics Business Partner at Serengeti Breweries

Controls, Compliance & Ethics Business Partner   Job Description : Controls, Compliance & Ethics Business Partner – Serengeti Breweries Ltd Reports To: SBL Legal and Controls, Compliance and Ethics Director Serengeti Breweries Limited (SBL) is a fully integrated beverage business in Diageo Africa (supply and demand for beer and spirits) It is a subsidiary of East Africa Breweries Limited… Read More »

The post Controls, Compliance & Ethics Business Partner at Serengeti Breweries appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Logical Access Management (LAM) Analyst at CRDB Bank

Logical Access Management (LAM) Analyst  VACANCIES – DEPARTMENT OF ICT BACKGROUND CRDB Bank Plc is inviting applications from qualified and experienced candidates to fill the vacant positions existing in the Department of ICT. The Bank seeks to recruit highly competent, self-motivated and professional individuals to fill the following positions: Logical Access Management (LAM) Analyst. Job Summary. Performing activities… Read More »

The post Logical Access Management (LAM) Analyst at CRDB Bank appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Specialist; Business Applications at CRDB Bank –

Specialist; Business Applications  VACANCIES – DEPARTMENT OF ICT BACKGROUND CRDB Bank Plc is inviting applications from qualified and experienced candidates to fill the vacant positions existing in the Department of ICT. The Bank seeks to recruit highly competent, self-motivated and professional individuals to fill the following positions: Specialist; Business Applications. Job Summary. Responsible for providing operational support and… Read More »

The post Specialist; Business Applications at CRDB Bank – appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Ngoma Mpya Kabisa : KISIMA 'NYANDA MAJABALA' - KISABHO

Hii hapa ngoma nyingine ya Msanii Kisima ' Nyanda Majabala' inaitwa Kisabho..Itazame hapa chini
Share:

Video Mpya : KISIMA 'NYANDA MAJABALA' - MAGUFULI

Hii hapa ngoma mpya kabisa ya Msanii wa Nyimbo za asili Kisima 'Nyanda Majabala' inaitwa Magufuli..Itazame hapa chini
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger