Thursday, 19 March 2020

Meneja wa Diamond 'Salam SK' Apata Corona....Jokate, Wasanii Mbalimbali Wampa Pole

Meneja wa mwanamuziki nyota nchini Diamond Platnumz,   aitwaye Sallam SK,    ametangaza kuambukizwa virusi vya Corona,  lakini amewatoa hofu Watanzania na kuwa anaendelea vizuri.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Sallam amepost picha na kuandika caption hii;

HABARI…!! Napenda kuwajulisha na kuwatoa hofu ndugu, jamaa na marafiki kuwa nimepata majibu ya vipimo na nimeonekana nikiwa na Corona Virus, kwa sasa nipo chini ya uangalizi mzuri na afya yangu inaendelea vizuri.

Pia naishukuru serikali kwa maandalizi mazuri na huduma ninayopata wodini, kwenye kituo toka juzi nipo peke yangu kama nimekikodisha vile 😅, wahudumu wana ushirikiano mzuri Mungu awalinde na awape afya njema maana wamejitolea nafasi zao kutupatia huduma sisi waathirika.

Hili janga la kimataifa linakwepeka kama tutafuata ushauri nasaha kutoka kwenye wizara husika, naomba kwa wote tuwe salama na familia zetu, tuchukue tahadhari mapema. Be Strong and Be Safe Everyone out there #AllahBlessUsAll.

Baadhi ya wasanii na watu mashuhuri  waliompa pole ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, msanii Ambwene Yesaya ‘AY’, Rita Paulsen, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, Hamisi Taletale ‘babutale’, Mbwana Yusuph ‘Mbosso’ na wengine wengi.


Share:

Watu 27 waliochukuliwa sampuli ya vipimo vya Corona Tanzania Akiwemo Na Yule Dereva Tax Aliyembeba Isabella Wako Salama, Hawajaambukizwa

Watu 27 waliofanyiwa uchunguzi kama wameambukizwa ugonjwa wa corona, akiwepo dereva wa taxi ambaye alimbeba mgonjwa wa kwanza Isabella Mwampamba wamebainika hawana virusi vya ugonjwa huo.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi msaidizi wa kitengo cha ufuatiliaji wa magonjwa ya mlipuko katika Wizara ya Afya, Dk Janeth Mghamba akiwa na mtaalam wa majanga wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk Faraja Msemwa. 

Wakizungumza na waandishi wa habari mjini Arusha, maafisa hao wa Wizara ya Afya nchini Tanzania, wamesema watu hao 27 walichukuliwa sampuli baada ya kubainika kuwa walikutana na dereva wa teksi ambaye alimbeba mgonjwa wa kwanza wa  Corona nchini Tanzania.

"Watu hawa walikuwa karibu na dereva na baada ya kuchukuliwa vipimo na kupelekwa maabara kuu iliyopo jijini Dar es Salaam wamebainika hawajaambukizwa." Amesema Dk Mghamba. 

Pamoja na hayo amesema kuwa watu hao, wataendelea kufuatiliwa hadi vitakapofanyika vipimo vya mara tatu kama ambavyo Shirika la Afya Duniani WHO imeagiza.


Share:

Msanii Mwana FA Akutwa na Virusi Vya Corona...Atoa Ujumbe Kwa Watanzania

Msanii wa muziki wa Hip Hop hapa nchini Mwana FA, amekutwa na maambukizi ya homa kali inayosababishwa na virusi vya Corona na kwamba amewekwa karantini na kwa sasa anaendelea vizuri.

Kupitia video aliyorekodi Mwana FA ameeleza kuwa siku chache zilizopita alikwenda nchini Afrika Kusini na wakati anarudi alianza kujihisi kuwa na homa kali.

Hali hiyo ilimfanya kwenda hospitali na kutaka apimwe kubaini kama ana corona na majibu yametoka leo yakionyesha kuwa ana ugonjwa huo.
 
"Nilivyorudi nikajitenga ili kuhakikisha siambukizi wengine, ugonjwa huo unaweza ukampata mtu yoyote na homa niliyokuwa nayo juzi haipo tena kwa sasa nipo shwari, tujihadhari tu, COVID-19 si ugonjwa wa kutisha sana, kwa sababu tumekuwa tukipata magonjwa mabishi zaidi ya hii" amesema Mwana FA.



Share:

NIDA YAHAKIKI UPYA MAOMBI YA VITAMBULISHO VYA TAIFA VYENYE CHANGAMOTO ZA URAIA


Wafanyakazi wa NIDA wakiwa katika zoezi la kuwasajili wananchi mbalimbali wanaoomba vitambulivyo vya
Taifa.



Wafanyakazi wa NIDA wakiwa katika zoezi la kuwasajili wananchi mbalimbali wanaoomba vitambulivyo vya
Taifa.
Baadhi ya wananchi wakitoka na kuingia katika ofisi moja wapo ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) katika zoezi linaoendelea la uhakiki wa vitambulisho vya Taifa.

**************************

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), inaendelea kutekeleza agizo la Serikali la kuhakiki kwa kina maombi yote ya waombaji wa Vitambulisho vya Taifa yenye
changamoto na upungufu mbalimbali ukiwemo uraia wa waombaji ili kuondoa mianya ya udanganyifu unaoweza kujipenyeza na hivyo kutoa Vitambulisho vya raia
kwa watu wasio raia wa Tanzania.

Kwa mujibu wa Afisa Habari Mkuu wa NIDA Bw. Geofrey Tengeneza, NIDA kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji, Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya na Mikoa, Serikali za Mitaa, Idara ya Wakimbizi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) wameanza kufanya uhakiki wa kina kwa kupitia maombi yote ya waombaji wa Vitambulisho vya Taifa.

Zoezi la uhakiki linakwenda sambamba na usajili wa raia, wageni wakaazi na Wakimbizi, ugawaji wa NIN na vitambulisho kwa wakazi wa mikoa iliyoko kanda ya
ziwa ambayo ni Kigoma, Kagera, Tabora, Geita, Mwanza Simiyu, Shinyanga na Mara, zoezi linaendeshwa kwa kushirikiana na wadau wengine wa mawasiliano.

Katika Kuhakikisha kuwa wanaopata Vitambulisho hivyo ni watu wanaostahili NIDA imejipanga kufanya uhakiki wa mara kwa mara kulingana na Sheria ya Usajili na
Utambuzi wa Watu ambayo inaeleza kuwa mwombaji yeyote wa Kitambulisho cha Taifa atakayebainika kutoa taarifa za uongo kuhusu uraia wake, Sheria itachukua
mkondo wake sambasamba na kunyanganywa Kitambulisho hata kama atakuwa tayari alikwishapata.

“Niwasihi wale wote wenye nia ya kutaka kujipenyeza na kupata Vitambulisho kinyume cha utaratibu, haitawasaidia kwani uhakiki unaofanywa na Mamlaka kwa kushirikiana na wadau ni endelevu na utafikia mikoa yote nchini, hivyo ni vyema kama kuna mwombaji yeyote anajua amedanganya taarifa za uraia wake akajisalimisha mapema kabla ya mkono wa sheria haujamfikia” amesema Bw. Tengeneza.

Akizungumzia sababu ya kuanza na mikoa ya Kanda ya Ziwa msemaji huyo wa NIDA amedokeza kuwa japokuwa zoezi hili litafanyika nchi nzima lakini limeanza katika
mikoa ya kanda ya ziwa kutokana na mikoa hiyo kuwa mipakani ambapo kunakuwa na mchangamano wa wakaazi kutoka nchi jirani hivyo kuwa rahisi kwa raia wa nchi
hizo kujipenyeza ili wajisajili kama raia wa Tanzania.

Sambamba na zoezi la uhakiki wa taarifa za waombaji hususan zenye mapungufu ya uraia wa waombaji, NIDA inaendelea pia kutoa huduma ya Usajili kwa wananchi wa
Kanda ya Ziwa na katika kila wilaya nchini kupitia Ofisi za Kudumu za Usajili za Mamlaka hiyo pamoja na vituo mbalimbali vya muda vilivyowekwa kwenye kata
mbalimbali kulingana na mahitaji ya wilaya husika.

Aidha, NIDA imefanikiwa kuwafikia idadi kubwa ya wananchi ambapo zaidi ya watu milioni 21,721,416 wamesajiliwa huku miongoni mwao watu milioni 17,674,812 wameshatambuliwa kwa kupatiwa Namba za Utambulisho wa Taifa na wengine Vitambulisho vya Taifa. Taarifa za waombaji wengine waliosajiliwa zinaendelea
kuchakatwa ili Namba zao za Utambulisho na Vitambulisho vyao vya Taifa vitolewe mapema iwezekanavyo.

Share:

Picha : MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA JASINTA MBONEKO AFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA MAJI



Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, amefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji katika eneo la Uzogole, Lubaga pamoja na Masengwa, miradi ambayo itawaondelea changamoto wananchi ya ukosefu wa maji safi na salama.

Mboneko amefanya ziara hiyo leo Machi 19,2020, kwa kukagua utekelezaji wa miradi hiyo ya maji yanayotoka Ziwa Victoria, kwa usimamizi wa Wakala wa Maji Vijjini (RUWASA), kwa kushirikiana  na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA).

Akizungumza baada ya kukagua miradi hiyo ya maji, Mboneko amewataka wananchi ambao wanatekelezewa miradi hiyo waitunze miundombinu yake na kutoiharibu, ili idumu kwa muda mrefu pamoja na kuwaondolea adha ya kutumia maji ambayo siyo salama kwa afya zao.

Amesema Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi  kutekeleza miradi ya maji kwa wananchi, hivyo ni vyema miradi hiyo wakaitunza huku akiwataka wasimamizi wa vituo vya kuchotea maji wawepo muda wote ili wananchi wasikose huduma ya maji hata mara moja.

“Leo nimefanya ziara ya kukagua miradi hii ya maji ambayo inatekelezwa kwa fedha za Serikali katika eneo la Uzogole, Lubaga, pamoja na Masengwa ili kuona inaendeleaje na wananchi waanze kutumia huduma hii ya maji safi na salama, maji kutoka Ziwa Victoria,” amesema Mboneko.

“Na kwenye vituo vya kuchotea maji mfano hapa Lubaga ambapo mradi umeshakamilika na kuanza kutoa maji, wasimamizi wa kituo hicho wauze maji kwa kufuata bei elekezi ya Serikali Shilingi 25 kwa ndoo moja, na siyo kuzidisha na uongozi usome mapato na matumizi kwa wananchi,”ameongeza.

Pia amemtaka mkandarasi anayejenga mradi wa maji Masengwa (Emirates Bulder) aongeze kasi ya utandazaji wa mabomba ya maji pamoja na ujenzi wa tenki la maji, ili mradi huo ukamilike haraka na wananchi waanze kutumia maji safi na salama.

Aidha amempongeza mkandarasi huyo kwa kutekeleza agizo la Serikali, la kununua vifaa vya kutekelezea mradi huo wa maji Masengwa kutoka ndani ya nchi jambo ambalo litakuza uchumi wa nchi.

Naye Kaimu Meneja Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) wilaya ya Shinyanga  Emmael Mkopi, alisema katika mradi wa maji Uzogole, ulianza Februari mwaka huu na unatarajiwa kukamilika Aprili 15, 2020 kwa gharama ya Shilingi Milioni 150, ambap mradi wa Masengwa ulianza Juni 2018 na utakamilika Aprili 27 mwaka huu na umegharimu Shilingi Bilioni 4.19.


TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, akifungua maji kwenye mradi wa maji Lubaga ambao umeshakamilika kwa kutekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) leo Alhamis Machi 19,2020 wakati akifanya ziara ya kutembelea miradi ya maji katika wilaya ya Shinyanga .Kushoto ni Meneja Ufundi wa SHUWASA Mhandisi Yusuph Katopola. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi, akimuelezea Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko namna mradi wa Maji Lubaga utakavyomsaidia pia mwanamke jinsi ya kubeba ndoo ya maji na kutoinama kuepuka kuumia mgongo.

Mzee Martine Shila mkazi wa Uzogole akiipongeza Serikali pamoja na mkuu huyo wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, kwa kutekeleza mradi huo wa maji safi na salama.

Kushoto ni Meneja ufundi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola, akiingiza namba kwa ajili ya kununua maji kwa mfumo wa Luku kwenye mita ya maji Uzogole, kulia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, akikagua zoezi la uchimbaji mitaro kwa ajili ya kulaza mabomba kwenye mradi wa maji ya Ziwa Victoria eneo la Uzogole.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (katikati), akikagua ubora wa mabomba ambayo yatawekwa kwenye mradi wa maji ya  Ziwa Victoria katika eneo la Uzogole. Kulia Kaimu Meneja Wakala wa Maji  Vijijini (RUWASA) Emmael Mkopi, kushoto ni Meneja ufundi wa SHUWASA, Mhandisi Yusuph Katopola.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikagua ubora wa mabomba ambayo yanatandazwa kwenye mradi wa maji Masengwa, kulia ni msimamizi wa mradi huo kutoka kampuni ya Emirates Bulder ya jijini Dar es salaam Said Msangi.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, akikagua ufukiaji wa mabomba kwenye mradi wa maji Masengwa.

Zoezi la ufukiaji mabomba likiendelea.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) akiangalia namna mabomba yanavyounganishwa kwenye mradi wa maji Masengwa.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akiangalia namna mabomba yanavyounganishwa kwenye mradi wa maji Masengwa.

Mabomba ambayo yanatandazwa kwenye mradi wa maji Masengwa.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na wananchi wa Isela na kuwataka wakulima wa mpunga wakipata fedha wajenge nyumba bora na vyoo bora. Wananchi hao waliomba wapate pia maji ambapo Mkuu wa wilaya aliwaambia kuwa watapata kwa mradi mwingine wa Wafaransa wa kusambaza maji kutoka katika mabomba makubwa.

Awali mkuu wa wilaya ya Shinyanga  Mhe. Jasinta Mboneko akiwa Uzogole,akigawa Jezi ya mpira pamoja na mpira katika timu ya vijana ya Uzogole, kushoto ni Nahodha wa timu hiyo Mussa Juma.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akigawa Jezi za mpira kwa timu ya Veterani ya Uzogole, kushoto ni Nahodha wa timu hiyo Paulo Maige.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiangalia Green house ya zao la nyanya iliyopo katika eneo la Nhelegani Kata ya Kizumbi.

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 blog
Share:

Bunge Lasitisha Utaratibu wa Kupokea Wageni Ili Kukabiliana na Virusi vya Corona

Bunge la Tanzania limesitisha utaratibu wa kupokea wageni mbalimbali wakiwamo wanafunzi wanaokwenda bungeni kwa lengo la kuona na kujifunza shughuli za Bunge.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Machi 19, 2020 na kitengo cha mawasiliano na uhusiano wa kimataifa cha ofisi ya Bunge imesema hatua hiyo ni mikakati ya muhimili huo uliotangazwa na Spika Job Ndugai wa kujinga na maambukizi ya ugonjwa wa corona.

Taarifa hiyo imesema wageni watakaoruhusiwa kuingia bungeni ni wale wenye kazi na vibali maalum tu.



Share:

Taarifa Kwa Umma Toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa




Share:

DEREVA TAXI ALIYEMBEBA MGONJWA WA KWANZA WA CORONA TANZANIA HANA VIRUSI VYA CORONA


Msemaji wa Wizara ya Afya wa masuala ya Corona Mkoa wa Arusha, Dkt Janeth Mghamba.

Dereva wa tax aliyembeba mgonjwa wa kwanza wa Virusi vya Corona mkoani Arusha, sampuli ya vipimo vyake kutoka maabara, zimeonesha kuwa hana maambukizi ya virusi hivyo.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Msemaji Mkuu wa Wizara ya Afya wa mambo yote, yanayohusiana na Ugonjwa wa Corona kwa upande wa Mkoa wa Arusha Dkt Janeth Mghamba na kusema kuwa, Serikali ilichukua juhudi za makusudi kabisa za kuhakikisha zinawapata wale wote waliokutana na dereva huyo na kuwafanyia vipimo.

"Waliokuwa wakifuatiliwa ni 27 pamoja na dereva, sampuli zao zote zilichukuliwa na zote zimeonekana hazina Virusi vya Corona na majibu haya yamechukua muda kwa sababu vipimo hivi vinaangaliwa zaidi ya mara moja na tumejiridhisha kwa kina baada ya kuviangalia mara tatu, bado tutaendelea kuwa nao kwa muda wa siku 14" ameeleza Dkt Janeth.
Chanzo - EATV
Share:

BREAKING: Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Latangaza kuahirisha mitihani ya kidato cha sita na ualimu Ili Kukabiliana na Virusi Vya Corona

Baraza la Mitihani nchini (Necta) limetangaza kuahirisha mitihani ya kidato cha sita na ualimu iliyokuwa ifanyike Mei 4 mwaka huu 2020 hadi pale itakapotoa taarifa mpya.

Hatua hiyo imekuja baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutangaza Machi 17, kufungwa shule na vyuo vyote  ili kuondoa misongamano na kupambana na virusi vya ugonjwa wa corona.


Kupitia maagizo hayo Necta imetoa maelekezo kwa maofisa elimu wa wilaya kuwajulisha wakuu wa shule na vyuo vya ualimu nchini wawajulishe watahiniwa kuhusu kuahirishwa kwa mitihani hiyo.


Share:

UDSM Yatoa Saa 48 wanafunzi wote kuondoka chuoni

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) nchini Tanzania kimewataka wanafunzi wote kuhakikisha ifikapo Ijumaa Machi 20, 2020 wawe wameondoka kurejea nyumbani.

UDSM imetoa taarifa hiyo  Jumatano Machi 18,2020 baada ya  Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa kutangaza  kuvifunga vyuo vyote kutokana na kujikinga na virusi vya ugonjwa wa corona (CODIV-19).
 
Katika taarifa ya Makamu mkuu wa UDSM, Profesa William Anangisye imesema katika kutekeleza maelekezo na ushauri wa Serikali kwa lengo la kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo, shughuli zote za masomo chuoni hapo zimesitishwa kuanzia leo Machi 20 2020 hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo.


Share:

Tumia Mwika Kujitibu Busha, Nguvu za Kiume

Mwika ni dawa  ya asili ya nguvu za kiume yenye kutibu matatizo kwa wakati mmoja ;

(1)Nguvu za kiume
(2) Kunenepesha Maumbile
(3)Kuchelewe kufika kileleni

Yajuwe matatizo yanayosababisha upungufu wa nguvu za kiume

(1) Ngiri ya kupanda na kushuka
2.Korondani moja kuvimba
3.Tumbo kuunguruma kujaa gesi
4.Kisukari
5.Presha
6.Kiuno kuuma
7.Kutopata choo vizuri 

Pia tunatibu kisukari siku (14) vidonda vya tumbo siku (30), Miguu kufa ngazi, kuwaka moto .

Pia tunayo dawa ya mvuto wa mpenzi hata yupo mbali amekuacha atarudi na kutimiza ahadi zote mvuto wa biashara.

Wasiliana nasi kwa namba 0747100745 (Whatsap/ Kupiga kawaida)


Share:

Maofisa Afya Mipakani Watakiwa Kuongeza Umakini Katika Kuwapima Virusi vya Corona Wageni Wote Wanaoingia Nchini

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amewataka wataalamu wa afya maeneo ya mipakani kote nchini kuongeza umakini wakati wa  ukaguzi kwa wasafiri wanaopita katika maeneo yao na si kupima joto la mwili pekee.

Waziri Ummy ameyasema hayo jana Jumatano Machi 18, katika Mpaka Namanga unaotenganisha Tanzania na Kenya wakati alipokuwa akifanya ukaguzi ukaguzi katika eneo hilo.

Alisema ni muhimu kufanya ukaguzi wa kina zaidi ikiwamo kuhoji wasafiri kabla ya kuwaruhusu kupita ili kubaini historia ya maeneo waliyotoka.

“Maofisa afya mipakani tunatakiwa tuweke umakini zaidi katika ukaguzi wa wasafiri na watu wanaopita katika maeneo yetu siyo kuangalia joto la mwili tu.

“Juzi  nilikuwa naangalia China kuna mtu amemeza vidonge vya kushusha homa kusudi aweze kupita, maofisa afya ni wajibu wenu kufanya uchunguzi zaidi.

“Kwa mfano kesi ya Isabela, wangepata muda wa kumuuliza zaidi angeweza kusema alikwenda Ubelgiji, Sweden na wangeenda mbali zaidi wangemuuliza una dalili zozote angesema nina kikohozi. Kwa hiyo hakuna muda wa kulaumiana ni kuhakikisha maofisa afya wanaongeza umakini,” amesema.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ameiomba serikali kuongeza wataalamu wa afya na vipimo vya kisasa maeneo ya mipakani hasa wa Namanga kutokana na idadi kubwa ya wanaopita kwa sasa wakiwamo wanafunzi waliokuwa wanasoma nchini Kenya.


Share:

Angalizo Toka Wizara Ya Afya: Kunywa pombe hakuzuii maambukizi ya virusi vya Corona.

Kumekuwa na tetesi kwamba eti ukinywa Pombe basi hutaweza kuambukiwa Virusi hatari vya Corona. 

Uvumi huo sio kweli na Wizara ya Afya imetoa ufafanuzi na kuwataka watanzania wazingatie miongozo mbalimbali ya namna ya kujikinga na virusi hivyo inayotolewa na serikali



Share:

Breaking News: Wagonjwa Wa Virusi Vya Corona Nchini Tanzania Wafika 6

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema idadi ya wagonjwa wenye virusi vya corona hapa nchini sasa imefika sita



Share:

WAGONJWA WA CORONA WAFIKIA 6 TANZANIA... WATU 112 WANAFUATILIWA

Share:

JESHI LA MAGEREZA LASITISHA HUDUMA ZOTE ZA KUWATEMBELEA WAFUNGWA NA MAHABUSU GEREZANI ILI KUKABILIANA NA CORONA




Share:

BENKI KUU YA TANZANIA YATOA UFAFANUZI KUHUSU NOTI ZA TANZANIA NA VIRUSI VYA CORONA


Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuutarifu umma kwamba noti zetu zimetengenezwa kwa namna ambayo zinaweza kuzuia vimelea kusalia kwenye noti. 


Hata hivyo, kwa kuwa noti hizo zinapita katika mikono mingi, tunawashauri wananchi kuzingatia miongozo mbalimbali inayotolewa na mamlaka zenye dhamana ya afya ya jamii, ikiwa ni pamoja na kunawa mikono mara kwa mara kwa kutumia maji yanayotiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono (sanitizers). Kufanya hivyo kutasaidia kuua vimelea kwenye mikono.

Aidha, tunawashauri wananchi kufanya miamala kwa kutumia njia mbadala za malipo kama vile simu za mkononi, intaneti na kadi bila kulazimika kufika kwenye kaunta za benki au ATM kuchukua noti.

Kama ilivyotangazwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), Ugonjwa wa Corona ni tishio duniani kote na tayari umeingia nchini tangu Jumatatu Machi 16, 2020 kwa mgonjwa wa kwanza kupatikana mkoani Arusha na wagonjwa wengine wawili mmoja huko Zanzibar na mwingine jijini Dar es Salaam ambao walitangazwa jana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, na hivyo kufanya jumla ya wagonjwa wa Corona (COVID-19) hapa nchini kufikia watatu.

Tunawasihi wananchi katika kipindi hiki ambacho taifa liko katika mapambano dhidi ya COVID-19 kuzipuuza taarifa zinazozagaa mitandaoni ambazo hazina vyanzo vya uhakika, zinazozihusisha noti zetu na usambazaji wa virusi vya corona



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger