Wizara ya Kilimo inawataarifu wadau wote wa sekta ya kilimo na vijana waliopanga kushiriki kongamano la kujadili fursa za kilimo,mifugo na uvuvi kwa kanda ya Dar es Salaam iliyokuwa ikihusisha mikoa ya Dar es Salaam,Pwani,Morogoro,Lindi na Mtwara kusitisha kuhudhuria kongamano hilo hadi watakapotaarifiwa baadaye.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli ametoa rai kwa Watanzania kuchukua tahadhali na vihatarishi vinavyoweza kusababisha maambukizi ya Corona kwa kuepuka mikusanyiko ya watu wengi isiyo ya lazima alisema Waziri Hasunga.
Mheshimiwa Waziri Hasunga amewataka wakulima na vijana wote nchini kuendelea kuchukua hatua za tahadhali kwa kuzingatia maelekezo ya Wizara ya Afya yaliyotolewa ili kuthibiti maambukizo ya virusi hivi hatari vya Corona hapa nchini.