Thursday, 12 March 2020

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi March 12





















Share:

Wednesday, 11 March 2020

Zitto Kabwe Awachangia CHADEMA Milioni 2 Ili Kuwalipia Faini Viongozi Wake Walioko Gerezani

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe akiwa ameambatana na Kaimu Katibu Mkuu Dorothy Semu na Katibu Mwenezi Ado Shaibu wamekabidhi kiasi cha Tsh. Milioni 2 ikiwa ni kusaidia kulipa faini zinazowakabili viongozi wa CHADEMA baada ya kuhukumiwa jana katika kesi iliyowakabili Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Fedha hizo zimepokelewa leo March 11, 2020 na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Said Issa Mohammed katika Ofisi za Makao Makuu ya CHADEMA, Dar es Salaam.
 
Mkurugenzi wa Itikadi, uhusiano na mambo ya nje wa Chadema, John Mrema amesema mbali ya kutoa fedha hizo,  Zitto ameahidi kuhamasisha wanachama wa ACT-Wazalendo  kuchangia Chadema.

Tangu jana Zitto aliandika kwenye ukursa wake wa Twitter akisisitiza kushirikiana na Chadema kuhamasisha wananchi kuchangia faini hiyo.



Share:

ÇHADEMA Kupoteza Jiji la Mbeya Baada ya Madiwan wake Wawili Kumtimkia CCM

Madiwani wa CHADEMA Halmashauri ya Jiji la Mbeya Ndg Lucas Mwampiki, Kata ya Mwakibete na Hussein Japhet Wasuha, Kata ya Itagano wametangaza kukihama chama hiko na kujiunga na CCM wakiungana na wenzao 11 waliojiunga awali. 

Kuhama kwa madiwani hao kunafanya idadi ya waliohama kutoka Chadema kwenda CCM kufikia 14 ambapo Januari 26 mwaka huu madiwani 11 wakiongozwa na aliyekuwa mstahiki meya Mchungaji David Mwashilindi walihamia CCM.

Kutokana na kuhama kwa madiwani hao hivi sasa CCM inakuwa na madiwani 17 huku Chadema ikiwa na madiwani 16 hivyo kuifanya Chadema kuipoteza Halmashauri ya Jiji la Mbeya.


Share:

Picha : WAZEE WAIPONGEZA SERIKALI SHINYANGA KUPUNGUZA MAUAJI YA WAZEE, WALIA KUTUNGIWA SHERIA YA WAZEE



Baraza la Wazee mkoa wa Shinyanga limeipongeza Serikali ya mkoa huo, kupunguza tatizo la mauaji ya wazee pamoja na watu wenye ualbino, ambao walikuwa akiuawa kwa sababu ya imani potofu za kishirikina.

Wazee wametoa pongezi hizo leo Machi 11,2020 kwenye kikao cha Baraza la Wazee Mkoa wa Shinyanga, kilichofanyika kwenye hospitali ya rufani ya mkoa wa Shinyanga, kilichokuwa na lengo la kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi likiwamo suala la matibabu.

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa Baraza la Wazee mkoa wa Shinyanga ,Katibu wa baraza hilo Anderson Lyimo, alisema wanaipongeza Serikali ya mkoa huo kwa kupunguza tatizo la mauaji ya wazee na watu wenye ualbino, ambalo lilikuwa likiwanyima haki zao za kuishi kwa sababu ya watu kuendekeza imani potofu za kishirikina.

“Baraza la wazee mkoa wa Shinyanga tunampongeza sana mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, pamoja na watendaji wake, kwa kudumisha amani, utulivu na usalama, pamoja na kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la mauaji ya wazee na watu wenye ualbino, tofauti na miaka ya nyuma,”alisema Lyimo.

“Tunaendelea kuomba juhudi hizi za kutokomeza unyanyasaji, ukatili, na mauaji ya wazee na watu wenye ualbino, ziendelee ili sisi wazee tupate kuishi kwa amani kwenye nchi yetu, pamoja na Serikali kuwachukulia hatua kali watu ambao wanasababisha mauaji ya watu ambao hawana hatia,”aliongeza.

Katika hatua nyingine aliiomba Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto itunge sheria ya wazee ili watekelezewe masuala yao kwa mujibu wa Sheria , likiwamo suala la upatikanaji wa dawa za wazee, madirisha, madaktari, pamoja na vitambulisho vya matibabu bure, ili waondokane na changamoto za ukosefu wa matibabu.

Naye Afisa Ustawi wa Jamii mkoa wa Shinyanga Lidya Kwesigabo, alisema mkoa Shinyanga una jumla ya wazee 66,717, wanaume 29,917, wanawake 36,800, ambapo wazee walio na vitambulisho vya matibabu bure wapo 20,068 na waliokatiwa Bima ya CHF 4,231.

Kwa upande wake Kaimu Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Nuru Mpuya, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye kikao hicho, alisema Serikali itaendelea kutatua changamoto ambazo zinawakabili wa wazee likiwamo suala la matibabu ambalo ndilo changamoto kubwa kwao.


TAZAMA PICHA HAPA CHINI


Katibu wa baraza la wazee mkoa wa Shinyanga Anderson Lyimo, akisoma taarifa ya utekelezaji wa baraza la wazee mkoa na kuipongeza Serikali kwa kupunguza tatizo la mauaji ya wazee na watu wenye ualbino. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee mkoa wa Shinyanga Faustine Sengerema akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Wazee mkoa wa Shinyanga.

Afisa Ustawi wa Jamii mkoa wa Shinyanga Lidya Kwesigabo, akizungumza kwenye kikao cha baraza la wazee mkoa wa Shinyanga.

Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Nuru Mpuya, akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Wazee mkoa wa Shinyanga, na kuahidi Serikali itaendelea kukatua changamoto za wazee zinazowakabili.

Afisa afya kutoka Ofisi ya Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mussa Makungu, akitoa elimu ya afya kwenye kikao cha baraza la wazee mkoa wa Shinyanga ikiwamo namna ya kujikinga na ugonjwa wa Corona.

Mwenyekiti wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza Kanda ya Ziwa Ruthi Kanoni, ambaye pia ni muuguzi katika hospitali ya rufani ya mkoa wa Shinayanga, akitoa elimu kwa wazee hao namma ya kujikinga na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kikiwamo Kisukari.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha baraza la wazee mkoa wa Shinyanga.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha baraza la wazee mkoa wa Shinyanga.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha baraza la wazee mkoa wa Shinyanga.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha baraza la wazee mkoa wa Shinyanga.

Katibu wa baraza la wazee manispaa ya Shinyanga Iddi Mpyalimi akichangia mada kwenye kikao cha baraza la wazee mkoa wa Shinyanga.

Mratibu wa Shirika la Tawlae linalotetea haki za wazee mkoa wa Shinyanga Eliasenya Nnko, akichangia mada kwenye kikao cha baraza hilo la wazee mkoa wa Shinyanga.

Frola Bundala akisoma taarifa ya baraza la Wazee Kahama Mji, kwenye kikao cha baraza la wazee mkoa wa Shinyanga.

Mwenyekiti wa baraza la wazee wilaya ya Kishapu Suzana Masebu akisoma taarifa ya wazee ya wilaya hiyo kwenye kikao cha baraza la wazee mkoa wa Shinyanga.

Mwenyekiti wa baraza la wazee halmashauri ya Ushetu Samson Kifutumo, akisoma taarifa ya wazee ya halmashauri hiyo, kwenye kikao cha baraza la wazee mkoa wa Shinyanga.

Wataalamu wa afya kutoka hospitali ya mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha baraza la wazee mkoa wa Shinyanga, wakwanza kushoto ni Mwenyekiti wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza Kanda ya Ziwa Ruthi Kanoni, ambaye pia ni muuguzi katika hospitali ya rufani ya mkoa wa Shinayanga, akiwa na Afisa afya kutoka Ofisi ya Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mussa Makungu.

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog


Share:

Picha : MWENYEKITI WA TCDC DK. TITUS KAMANI AZINDUA MNADA WA CHOROKO KWA MFUMO WA MTANDAO SHINYANGA,MWANZA

Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Dk. Titus Kamani akizungumza na Wakulima wa zao la Choroko na wanachama  wa Vyama vya Msingi vya Ushirika wakati akizindua Mnada wa zao la Choroko kwa Mfumo wa Mtandao “Online Trading System”.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (Tanzania Cooperative Development Commission -TCDC ) Dk. Titus Kamani amezindua Rasmi Mnada wa zao la Choroko kwa Mfumo wa Mtandao “Online Trading System” katika Mkoa wa Shinyanga na Mwanza.

Uzinduzi huo umefanyika leo Jumatano Machi 11,2020 katika kijiji cha Manigana kata ya Solwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Dk. Kamani alisema lengo la serikali ni kuhakikisha wakulima wanalipwa fedha zao na kuuza mazao yao kwa bei nzuri hivyo anaamini Mnada wa Choroko kwa kutumia mfumo wa mtandaoni utasaidia wakulima kuuza mazao kwa bei ya juu.

“Wakulima mlikuwa mnauza choroko kwa bei ya chini inayoumiza,vitini vya choroko vilikuwa vinachezewa. Na sasa ili kupata bei nzuri ni kwenda mnadani ambapo kutakuwa na bei ya ushindani na ukiridhika na bei ndiyo unauza na kupewa fedha zako”,alisema Dk. Kamani.

“Hamasisheni wakulima wajiunge kwenye Vyama vya Msingi ‘AMCOS’ ,kwani mnada utafanyika kupitia AMCOS ambapo kila mkulima atapeleka choroko yake na kuangalia bei ya ushindani itakayokuwepo siku ya mnada na atalipwa fedha zake ndani ya saa 72”,aliongeza Dk. Kamani.

Aidha alisema mbali na Mnada kwa mfumo wa Mtandao kumnufaisha mkulima pia utasaidia Chama Kikuu Cha Ushirika na Halmashauri za wilaya kupata fedha huku akisisitiza kuwa bei ya ushindani inakwenda kwa mkulima bila makato.

Kwa upande wake, Kaimu Mrajis Msaidizi Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Benjamini Mwangala alisema uzinduzi huo wa Mnada wa zao la Choroko kwa Mfumo wa Mtandao “Online Trading System” ni sehemu ya utekelezaji wa Tangazo la Waziri wa Kilimo alilolitoa Februari 14,2020 kuzindua Mnada wa Soko la Bidhaa kwa mazao ya jamii ya mikunde na mbegu.

“Tangazo hilo linataka mazao ya Jamii ya Mikunde na mbegu kama vile mbaazi,choroko,dengu,ufuta na soya kuuzwa kupitia Vyama vya Ushirika ili mkulima apate bei nzuri na ya ushindani mahali alipo”,alisema Mangwala.

Naye Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Soko la Bidhaa, Augustino Mbulumi alisema katika mnada wa leo Machi 11,2020 jumla ya kilo 2000 za choroko zimeuzwa kwa bei ya shilingi 1340 kwa kilo moja.

Aliwasihi wakulima wajikusanye wapeleke mazao yao katika AMCOS na kukusanya mazao mengi ili kuvutia wanunuzi wakubwa wenye bei nzuri ili mkulima anufaike kupitia zao hilo la choroko.

Naibu Mrajis wa Vyama Vya Ushirika Tanzania, Charles Malunde alisema serikali itahakikisha mazao yote yanaingia katika mfumo wa Stakabadhi ghalani ambapo mnada utakuwa unafanyika kupitia mtandao ili wakulima wanufaike kupitia kilimo.

Mkulima wa choroko Kwiyolecha Nkilijiwa aliiupongeza serikali kwa kuanzisha mnada wa mazao akieleza kuwa wakulima walikuwa wanapata hasara kutokana na kuuza choroko yao kwa bei ya chini ambapo hapakuwa na vipimo walanguzi walikuwa wananunua kwa Rumbesa/visado kuanzia shilingi 600 hadi 1000.
 
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Dk. Titus Kamani akizungumza na Wakulima wa zao la Choroko na wanachama  wa Vyama vya Msingi vya Ushirika wakati akizindua Mnada wa zao la Choroko kwa Mfumo wa Mtandao “Online Trading System” katika moja ya Ghala kwenye kijiji cha Manigana kata ya Solwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga leo Jumatano Machi 11,2020. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Dk. Titus Kamani akiwahamasisha wakulima kuuza zao la choroko kwa kutumia mnada kupitia mfumo wa Mtandao ili waweze kuuza choroko kwa bei ya ushindani.
Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Dk. Titus Kamani akiwahamasisha wakulima wajiunge kwenye Vyama vya Msingi ‘AMCOS’.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Soko la Bidhaa, Augustino Mbulumi akielezea jinsi Mnada kwa mfumo wa Mtandao 'Online Trading System' unavyofanya kazi na kusaidia kupata wanunuzi kutoka nje ya nchi kwa ushindani.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Soko la Bidhaa, Augustino Mbulumi akionesha matokeo ya mnada wa leo Machi 11,2020 jumla ya kilo 2000 za choroko zimeuzwa kwa bei ya shilingi 1340 kwa kilo moja.
Katika mnada wa leo Machi 11,2020 wanunuzi wawili walijitokeza kununua choroko kiasi cha kilo 2000 ambapo mnunuzi wa kwanza alitoa bei ya shilingi 1340 na mnunuzi wa pili alitoa shilingi 1,248 kwa kilo moja kununua kilo 2000 za choroko.
Naibu Mrajis wa Vyama Vya Ushirika Tanzania, Charles Malunde akizungumza wakati wa uzinduzi Mnada wa zao la Choroko kwa Mfumo wa Mtandao “Online Trading System” ambapo alisema serikali itahakikisha mazao yote yanaingia katika mfumo wa Stakabadhi ghalani ili wakulima wanufaike kupitia kilimo.
Naibu Mrajis wa Vyama Vya Ushirika Tanzania, Charles Malunde akizungumza wakati wa uzinduzi Mnada wa zao la Choroko kwa Mfumo wa Mtandao “Online Trading System” ambapo alisema serikali itahakikisha mazao yote yanaingia katika mfumo wa Stakabadhi ghalani ili wakulima wanufaike kupitia kilimo.
Kaimu Mrajis Msaidizi Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Benjamini Mwangala akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mnada kwa Mfumo wa Mtandao kwa ajili ya zao la Choroko. Alisema uzinduzi huo waMnada wa zao la Choroko kwa Mfumo wa Mtandao “Online Trading System” ni sehemu ya utekelezaji wa Tangazo la Waziri wa Kilimo alilolitoa Februari 14,2020 kuzindua Mnada wa Soko la Bidhaa kwa mazao ya jamii ya mikunde na mbegu.
Wakulima  na  wanachama wa AMCOS wakiwa kwenye uzinduzi wa Mnada wa zao la Choroko kwa Mfumo wa Mtandao “Online Trading System”.
Kushoto ni Naibu Mrajis wa Vyama Vya Ushirika Tanzania, Charles Malunde akifuatiwa na Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga (SHIRECU), Ramadhani Kato na Kaimu Mrajis Msaidizi Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Benjamini Mwangala wakiwa kwenye uzinduzi wa Mnada wa zao la Choroko kwa Mfumo wa Mtandao “Online Trading System”.  
Sehemu ya choroko ikiwa kwenye magunia katika ghala la kijiji cha Manigana kata ya Solwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Kushoto ni Mkulima wa choroko Kwiyolecha Nkilijiwa akiteta jambo na Naibu Mrajis wa Vyama Vya Ushirika Tanzania, Charles Malunde wakati wa uzinduzi wa Mnada wa zao la Choroko kwa Mfumo wa Mtandao “Online Trading System”.  
Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Dk. Titus Kamani akipiga picha ya kumbukumbu na viongozi mbalimbali.
Katikati ni Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga (SHIRECU), Ramadhani Kato akizungumza na Mkulima wa choroko Kwiyolecha Nkilijiwa. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Dk. Titus Kamani.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Share:

CHADEMA Walipa Milioni 110 Kuwatoa Halima Mdee, Ester Matiko na Ester Bulaya Gerezani

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kimeanza mchakato wa kuwatoa gerezani mbunge wa Kawe, Halima Mdee; Esther Matiko (Tarime Mjini) na Ester Bulaya (Bunda).

Mkurugenzi wa itikadi, uenezi, mawasiliano na mambo ya nje wa Chadema, John Mrema amesema mpaka sasa wameshalipa faini ya Sh110 milioni iliyotakiwa kulipwa na wabunge hao watatu ili watoke gerezani.

Viongozi wanane wa Chadema pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji jana Jumanne Machi 10, 2020 walihukumiwa kulipa faini ya Sh350 milioni au kwenda jela miezi mitano baada ya kutiwa hatiani kwa makosa 12 kati ya 13 yaliyokuwa yanawakabili.


Share:

Alichokisema Dkt Vicent Mashinji Baada ya CCM Kumchomoa Gerezani

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleoa (CHADEMA), Dkt Vicent Mashinji, amefunguka mengi baada ya kulipiwa faini yake na Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam na kwamba ameshangazwa kuona jambo hilo lilivyomalizika kwa uharaka.

Dkt Mashinji ameyabainisha hayo leo mara baada ya kuachiwa huru, baada ya jana kushindwa kulipa faini yake na kupelekwa Gereza la Segerea na kuliomba Taifa kuendelea kuboresha zaidi Magereza.

"Niwashukuru sana ndugu zangu wa CCM, miaka miwili iliyopita nilipata kuwa hapo gerezani, sasa hivi kuna improvement kidogo, naomba kama Taifa tuendelee kuboresha maeneo yote tunayowahifadhi wananchi, nilitegemea kama kule nilikotoka hili suala lingekuwa la Kitaifa, lakini nimeshangazwa kuona limefanywa tu na Mkoa, najiona niko sehemu salama zaidi" amesema Dkt Mashinji.

Dkt Mashinji pamoja na viongozi nane wa CHADEMA, kutokana na kesi yao ya uchochezi iliyokuwa ikiwakabili, jana Machi 10, 2020, walihukumiwa faini ama kifungo cha miezi mitano jela na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.


Share:

Bilioni 66.5 zapatikana tangu kuanzishwa kwa masoko ya madini nCHINI

Na Greyson Mwase, Dodoma
KATIBU Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya amesema kuwa, tangu kuanzishwa kwa masoko ya madini nchini mapema Machi mwaka jana jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 66.5 zimepatikana na kuongeza mchango wa Sekta ya Madini kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.

Profesa Manya ameyasema hayo leo tarehe 11 Machi, 2020 kupitia mahojiano maalum jijini Dodoma na kueleza kuwa tangu kuanzishwa kwa masoko ya madini mwezi Machi, 2019 hadi kufikia mwezi Januari, 2020 usimamizi wa masoko ya madini nchini umeendelea kuimarika ambapo, katika kipindi husika kilogramu 9,237.34 za dhahabu; karati 12,973.14 za madini ya almasi; kilogramu 20,099.17 za madini ya bati; na kilogramu 514,683.28 za madini ya vito mbalimbali ziliuzwa kupitia masoko hayo na kuipatia Serikali jumla ya shilingi bilioni 66.57.

Akielezea mfano wa masoko yaliyochangia kwa kiasi kikubwa kwenye ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali na kuipaisha Sekta ya Madini, Profesa Manya alielezea Soko Kuu la Dhahabu Geita ambapo alisema kuwa, kabla ya kuanzishwa kwa soko hilo, ukusanyaji wa mapato ulikuwa wastani wa Shilingi 599,046,378.47 yaliyotokana na wastani wa mauzo ya Kilogramu 101.97 kwa mwezi kwa takwimu za kipindi cha miezi mitano kabla ya kuanzishwa kwa soko.

Alisema kuwa, baada ya kuanzisha soko, makusanyo yaliongezeka hadi kufikia wastani wa shilingi bilioni 2.39 kwa mwezi yaliyotokana na wastani wa mauzo ya Kilogramu 360.94 zilizouzwa katika kipindi cha miezi 11 tangu soko hilo kuanzishwa Machi, 2019 hadi Januari, 2020 na kuongeza kuwa ongezeko hilo lilitokana na uwazi katika biashara ya madini ya dhahabu kwa kuwepo kwa soko hilo.

Aliongeza kuwa, kwa kipindi cha mwezi Oktoba, 2019 pekee katika Soko Kuu la Dhahabu Geita, Serikali ilifanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 3.6 kutokana na mauzo ya kilogramu 537.6 zilizouzwa.

Akitolea mfano wa soko jingine la madini la Chunya lililopo Mkoani Mbeya, Profesa Manya alifafanua kuwa kabla ya kuanzishwa kwa soko hilo, kiasi cha wastani wa Shilingi 177,965,811.06 kilichotokana na mauzo ya dhahabu yenye uzito wa wastani wa Kilogramu 29.67 kilikuwa kikipatikana kwa mwezi kwa takwimu za kipindi cha miezi minne (4) kabla ya kuanzishwa kwa soko.

Aliendelea kusema kuwa, mara baada ya kuanzishwa kwa Soko la Madini la Chunya mapema Mei, 2019 ndani ya kipindi cha miezi tisa Serikali ilikusanya kiasi cha wastani wa Shilingi 961,009,348.85 kilichotokana na mauzo ya dhahabu kwa wastani wa Kilogramu 176.24 kwa mwezi.

Awali akielezea uanzishwaji wa masoko ya madini 28 na vituo vya ununuzi wa madini 28 nchini Profesa Manya alisema kuwa kuanzishwa kwa masoko ya madini nchini kulitokana na changamoto kubwa iliyokuwa inaikabili Sekta ya Madini kwa kipindi kirefu, hasa ya utoroshaji na biashara haramu ya madini.

Akielezea manufaa yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwa masoko na vituo vya ununuzi wa madini nchini Profesa Manya alieleza kuwa ni pamoja na kuwasaidia wachimbaji wadogo kupata huduma ya masoko na upatikanaji wa bei stahiki za madini yanayouzwa na wachimbaji na wafanyabiashara wadogo wa madini.

Alieleza mafanikio mengine kuwa ni pamoja na uwazi katika biashara ya madini, kuimarika kwa ufanisi katika ukusanyaji wa maduhuli na kuondoa tatizo la utoroshaji na biashara haramu ya madini na hivyo kusaidia upatikanaji wa mapato stahiki ya Serikali kupitia tozo za mrabaha (6%) na ada ya ukaguzi (1%) za mauzo ya madini kwenye masoko.

Mafanikio mengine ni pamoja na upatikanaji wa takwimu sahihi za uzalishaji na mauzo ya madini yanayozalishwa na kuuzwa na wachimbaji pamoja na wafanyabiashara wadogo wa madini nchini kupitia masoko.


Share:

TLP Kumteua Rais Magufuli Kuwa Mgombea Wao Wa Urais 2020

Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) kimesema kuwa Mkutano mkuu wa chama hicho  utakaofanyika Mei 9 mwaka huu hautapitisha mgombea yeyote wa Urais kupitia chama hicho na badala yake kitampitisha Mgombea wa Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt.John Pombe Magufuli.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Chama hicho Agustino Latonga Mrema amesema kuwa jina Mgombea Urais lilishapitishwa na Halmashauri Kuu Chama na kilichobaki ni kudhibitisha jina la Mgombea huyo.

Amesema kuwa katika uchaguzi mkuu hakuna haja ya kuweka Mgombea wa Urais kutokana na Rais aliyopo kukidhi mahitaji ya watanzania.

Amesema vyama vingine vijifunze toka kwa  Rais Magufuli namna Tanzania ilivyopata Maendeleo kwa kipindi kifupi ikiwamo kukomesha Rushwa.


Share:

Serikali Kumnyang’anya Shamba Muwekezaji Wa Katani Tanga.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema Serikali imekusudia kumnyanga’anya shamba la mkonge la Kwashemshi Sisal Estate lililopo kata ya Kwashemshi wilaya ya Korogwe Mkoa wa Tanga kwa kusababisha migogoro kwa wakazi wa eneo hilo na kukiuka masharti ya uendelezaji.

Waziri Lukuvi ameyasema hayo wakati akizungumza na wakazi wa eneo hilo pamoja na wamiliki wa shamba hilo la Kwashemshi Sisal Estate mara baada ya kukagua miundombinu ya shamba hilo ambayo imeonekana kuchakaa.

“Kwanza umekiuka masharti ya uendelezaji, kwa sababu umepewa shamba tangu mwaka 2003 na hadi leo ni miaka 17 hujalima lote wakati ulitakiwa uwe umemaliza kulilima mwaka 2011. Pili tunakudai kodi ya pango la ardhi hujalipa, tatu hujatoa ajira kwa wananchi na hujatoa gawio kwa Halmashauri, sasa kwanini nisimshawishi Mhe. Rais afute hili shamba?” amesema Mhe. Lukuvi.

Awali mkazi wa eneo hilo Bwana Musa Majaliwa amemlalamikia mwekezaji huyo kwa madai ya kumiliki shamba hilo lenye ukubwa wa zaidi ya ekari elfu tatu ambapo katika eneo lote ekari mia tatu pekee ndiyo zenye mkonge na sehemu nyingine ni vichaka.

“Tunachoomba Waziri Lukuvi utusaidia kupata sehemu ya ardhi hii kwa matumizi ya kilimo na makazi kwa kuwa ongezeko la watu limekuwa ni kubwa tofauti na hapo awali” alisema Bwana Musa.

Kwa mujibu wa Mhe. Waziri shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 3,703 linamilikiwa na Ndugu Methew Upanga Mnkande maendelezo yake hayaridhishi kwani hadi sasa eneo lenye mkonge wakuvuna (Mature) ni ekari 1,210, eneo lenye mkonge mdogo (Immature) ni ekari 380 na kufanya eneo lililoendelezwa kuwa na ukubwa wa ekari 1,590 sawa na asilimia 42 tu.

Kuhusu kudaiwa kodi, mmiliki huyo tangu amilikishwe mwaka 2003 alikuwa hajalipa kodi ya pango la ardhi na alikuwa anadaiwa shilingi 2//6yyyy 2,218,000 ambapo hadi sasa amelipa shilingi 8, 000,00 na deni hadi sasa anadaiwa shilingi 14,218,000.

Kwa upande wake Mwakilishi wa mwekezaji wa shamba hilo ambae anatambulika kwa jina la mzee Mkande amedai kuwa shamba hilo limeendelezwa kwa kupanda mikonge mikubwa hekta mia nne thamani na mkonge mdogo ambao unatajiwa kuvnwa hivi karibuni ni hekta 150.

Kuhusu madai ya kodi ya pango la ardhi wanazodaiwa na Serikali mwakilishi huyo amekili kuwa awali walikuwa hawalipi kodi, ila sasa wameingia makubaliano na wilaya kulipa ambapo mpaka sasa wameshalipa kiasi cha shilingi milioni 8 na bado wanadaiwa kiasi cha shilingi milioni 14 mpaka sasa.

Hata hivyo, Mhe. Lukuvi aliendelea kumbana mwakilishi huyo kwa kumfahamisha kuwa shamba hili lipo kwenye hatua za ubatilishaji kutokana na uvunjifu wa masharti ya kutoendeleza ipasavyo na kulipa kodi ya ardhi kwa kusuasua.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger