Wednesday, 26 February 2020

Naibu Waziri wa Ardhi Angeline Mabula Atoa MAAGIZO Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)

Na Munir Shemweta, WANMM MUSOMA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuongeza kasi ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kwangwa  iliyopo  Musoma mkoa wa Mara ili kukamilika kwa muda uliopangwa.

Hospitali hiyo ya Kwangwa ni ya ghorofa tano yenye shemu tatu (Wing A, B na C) na inarajiwa kuanza kutoa Huduma kwa baadhi ya sehemu kati kati ya mwezi ujao

Dkt Mabula alitoa kauli hiyo jana tarehe 25 Februari mjini Musoma mkoa wa Mara wakati wa ukaguzi wa  maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo unaofanywa na NHC  akiwa katika ziara yake ya siku moja.

Alisema, pamoja na NHC kufanya vizuri katika ujenzi wa jengo la hospitali hiyo ukilinganisha na wakandarasi waliotangulia lakini inapaswa kuongeza kasi ili likamilike katika muda uliopangwa na kuanza kutoa huduma.

Kwa mujibu wa Mabula, Hospitali ya Kwangwa itakayojulikana kwa jina la Mwl Nyerere Memorial Hospital ina historia ndefu kwa kuwa pamoja na kuasisiwa na Rais wa Kwanza Mwalimu Julius Nyerere lakini utekelezaji wake unakamilishwa na serikali ya awamu ya tano.

‘’Ni vyema NHC mkaongeza bidii katika ujenzi wa hospitali hii ili ikamilike kwa haraka kwa kuwa hospitali hii ina historia ndefu na Rais John Pombe Magufuli ameamua ujenzi huu ukamilike kwa kutoa bilioni 15’’ alisema Mabula.

Katika kuhakikisha ujenzi wa hospitali hiyo unakamilika kwa wakati, Naibu Waziri Mabula alimtaka Mkurugenzi Mkuu wa NHC Dkt Maulid Banyani kusimamia kwa karibu maendeleo ya ujenzi huo sambamba na kupatiwa ratiba ya mpango wa ujenzi na maendeleo yake kila baada ya siku mbili kwa nia ya kufuatilia kwa karibu.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Dkt Maulid Banyani alimuahakikishia Naibu Waziri Mabula kuwa, ujenzi wa hospitali hiyo sasa utakamilika kwa wakati baada ya changamoto kadhaa ikiwemo ya Mshauri Mwelekezi  kupatiwa  ufumbuzi.

Kwa Upande wake Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima mbali na kuisifu NHC kwa kufanya mabadiliko makubwa ya utekelezaji  wa ujenzi wa mradi wa hospitali ya Kwangwa alioueleza kuwa ilikwamwa kwa mara kadhaa.

‘’Toka Shirika la Nyumba la Taifa lianze ujenzi wa hospitali hii mwezi Agosti mwaka jana kuna mabadiliko makubwa ya kasi ya ujenzi  na  tunataka mjenge kwa wakati na viwango na Machi mwaka huu Huduma ya Mama na Mtoto ianze kutolewa ‘’ alisema Malima.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, hospitali hiyo itatoa huduma kwa wananchi wa mikoa ya Kanda ya ziwa pamoja na nchi jirani sambamba na kutumika kama sehemu ya utalii kutokana na mazingira ya hospitali.

Historia ya Ujenzi wa Hospitali ya Kwangwa iliyopo Musoma mkoa wa Mara inaanzia mwaka 1977 pale Rais wa kwanza wa  Mwl Nyerere alipotoa wazo la kujengwa kwake lakini ujenzi huo  umekuwa ukikwama kwa nyakati tofauti hadi Rais John Pombe Magufuli alipotoa Shilingi Bilioni 15 kwa lengo la kukamilishwa mradi huo ambapo sasa unatarajiwa kukamilika mwaka huu.


Share:

Waasi wa Syria wanaoungwa mkono na Uturuki wadhibiti mji ulio karibu na Idlib

Waasi wa Syria wanaoungwa mkono na jeshi la Uturuki wamedhibiti mji wa Narab, katika mkoa wa Idlib, kwa mujibu wa vyanzo kutoka Uturuki na wawakilishi wa waasi.

Vikosi vya rais Bashar al-Assad, ambavyo vinaungwa mkono na jeshi la anga la Urusi, wanajaribu kuiteka ngome hii ya mwisho ya waasi nchini Syria baada ya miaka tisa ya vita.

Karibu raia milioni moja wameyahama makazi yao tangu kuanza tena kwa mashambulizi ya vikosi vya serikali vya Syria na mshirika wake Urusi Desemba mwaka jana, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.

Vikosi vya serikali vimeuteka mji wa Kafr Nabel na maeneo jirani, yanayopatikana karibu kilomita 30 Kusini Magharibi mwa Nairab, shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSDH), chanzo cha eneo hilo na vyombo vya habari vimeripoti.

Uturuki imetuma maelfu ya askari na vifaa katika mkoa huo kusaidia waasi wa Syria, na kuongeza mvutano na Urusi, mshirika mkuu wa Syria.


Share:

Watu 17 wafariki dunia na 150 wajeruhiwa katika Vurugu mjini New Delhi, India

Watu 17 wamefariki dunia na wengine wapatao 150 wamejeruhiwa hapo jana katika makabiliano kati ya waandamanaji wa makundi yanayokinzana mjini New Delhi huko India. 

Makabiliano hayo ni mabaya zaidi kushuhudiwa tangu vurugu zilipozuka juu ya sheria mpya ya uraia mwanzoni mwa mwezi Desemba. 

Vurugu hizo zilianza tangu mwishoni mwa juma lakini ziligeuka kuwa mbaya zaidi Jumatatu iliyopita. 

Machafuko mapya yalianza tena jana Jumanne katika maeneo tofauti ya mji mkuu huo wa New Delhi. 

Afisa wa idara ya kukabiliana na majanga ya moto ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba timu yake imekuwa ikipokea simu za dharura za kwenda kuzima moto katika maeneo tofauti. 

Sheria hiyo mpya iliyozua ghasia inawapa fursa wahamiaji wasio Waislamu kutoka nchi tatu jirani kupata urai wa India.

 Waislamu nchini India wanadai kuwa ni sheria ya kibaguzi.


Share:

Algeria Yathibitisha Kuwa na Mgonjwa Wa Corona....Waliofariki Hadi Sasa Kwa Virusi Hivyo ni Watu 2,763

Algeria imethibitisha kisa cha kwanza cha virusi vya Corona, ambapo mgonjwa ni raia wa Italia aliyewasili nchini humo Februari 17. 

Tayari mgonjwa huyo amewekwa eneo maalumu la matibabu. 

Algeria inakuwa nchi ya pili ya Afrika kupata muathirika wa virusi hivyo baaada ya Misri.

Watu waliofariki  hadi sasa kwa virusi hivyo  Ulimwenguni wamefikia 2,763 huku Watu 80,970 wakiathirika
 

Wagonjwa 29,745 wamepona maambukizi hayo nchini China na kuruhusiwa kutoka hospitalini


Share:

Diamond Kadondosha Ngoma Mpya iitwayo JEJE......Itazame Hapa

Diamond Kadondosha Ngoma Mpya iitwayo JEJE......Itazame Hapa


Share:

IGP Sirro Ataka Wazazi Waimarishe Malezi Kwa Watoto Ili Kuwa na Jamii Inayochukia Uhalifu

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Simon Sirro ametoa wito kwa jamii hasa wazazi nchini kuhakikisha wanaimarisha malezi ya watoto wao, jambo litalalosaidia kuwa na jamii itakayochukia uhalifu.

IGP Sirro ametoa wito huo mkoani Dodoma wakati akizungumza na baadhi ya Wakazi wa eneo la Mbande, baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha polisi katika eneo hilo.

Amewashauri wazazi wote nchini kuendelea kuwasomesha watoto wao na kutowaacha wajiingize kwenye vitendo vya uhalifu.


Share:

PICHA: Rais Magufuli Na Mkewe Mama Janeth Magufuli Washiriki Ibada Ya Jumatano Ya Majivu Katika Kanisa La Mtakatifu Petro Jijini Dar Es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipakwa majivu na Paroko wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Padre Dkt. Alister Makubi  wakati wa Ibada ya Jumatano ya Majivu jijini Dar es salaam leo Februari 26, 2020
Mama Janeth Magufuli, Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipakwa majivu na Paroko wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Padre Dkt. Alister Makubi  wakati wa Ibada ya Jumatano ya Majivu jijini Dar es salaam leo Februari 26, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiondoka baada ya kuhudhuria Misa ya Jumatano ya Majivu katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay  jijini Dar es salaam leo Februari 26, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, akiongozana na mkewe Mama Janeth Magufuli, akipakwa majivu na Paroko wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Padre Dkt. Alister Makubi  waliposhiriki  Ibada ya Jumatano ya Majivu jijini Dar
es salaam leo Februari 26, 2020

PICHA NA IKULU


Share:

Darassa Kaachia DUDE La Nguvu Akimshirikisha Sho Madjozi – I Like It. ....Itazamahe Hapa

Video Mpya ya Darassa Ft. Sho Madjozi – I Like It


Share:

Download App Yetu Kwenye Simu Yako Ili Uweze Kupata Habari Zetu Kwa Haraka Zaidi

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa urahisi kabisa kupitia simu yako ya mkononi muda wowote hata usiku wa manane au ukiwa kazini...

Pata kurasa za mbele Magazetini, habari za kitaifa, matukio yote ya kisiasa, burudani na udaku   kupitia simu yako ya mkononi.

Huhitaji tena kuwa na Computer. Ingia Play Store, pakua App yetu  tukuhabarishe masaa 24.



Share:

Chelsea Yachezea Kichapo cha 3-0 Toka Kwa Bayern Munich

Mechi kati ya Chelsea na Bayern Munich iliwashuhudia wababe wa Bundesliga wakipiga hatua kubwa ya kukaribia kufuzu kwa duru ya nane bora ya Ligi ya Mabinwa baada ya kushinda  3-0 uwanjani Stamford Bridge.

Matokeo ya kuridhisha katika awamu ya pili siku ya Jumanne, Februari 25 usiku, yalichochewa na Robert Lewandowski ambaye alisadia Bayern kutwaa ushindi.
 
Upande zote zilionyesha umahiri katika awamu ya kwanza na kutoka sare tasa kuelekea muda wa mapumziko, huku Thomas Muller akikaribia kuvunja kimya baada ya kupiga shuti iliyotua juu ya lango.

Lewandowski pia alinyimwa nafasi mara mbili na Willy Caballero kufunga bao, huku juhudi za Marcos Alonso dakika ya 41 ikizua hatari kwa Chelsea.

Katika kipindi cha pili, wenyeji walionyesha ari ya kuwa kifua mbele huku Manuel Neur akilazimika kupangua mikiki ya Mason Mount na Ross Barkley.

Hata hivyo, Bavarians walifunga bao la kwanza kupitia kwa Serge Gnabry ambaye alivurumisha kombora lililotua kimyani baada ya kuwasiliana na Lewandowski.

Gnabry alisawazisha bao hilo dakika tatu baadaye kufuatia usaidizi wa Lewandowski, kabla ya fowadi huyo kuingia katIka orodha ya watingaji bao dakika ya 76 na kuzima ndoto ya Chelsea.

Matumaini ya wenyeji kupata bao la kufutia machozi ilididimia kunako dakika ya 84 baada ya Alonso kutimuliwa uwanjani kwa kumuangusha Lewandowski.

Masogora wa Frank Lampard kwa sasa wana kibarua kigumu cha kubatilisha matoke hayo wakati wa ziara yao ya Ujerumani kwa mechi ya marudiano ili kufuzu kwa raundi nyingine ya kivumbi hicho cha Uropa.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano February 26





















Share:

DKT NCHIMBI AWATWISHA MZIGO TBS NA SIDO



 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi

Na John Mapepele

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amelielekeza shirika  la  viwango nchini (TBS) na Shirika la Viwanda Vidogo nchini (SIDO) kuanzisha mara moja  operesheni maalum ya  kuwatafuta wamiliki wa viwanda  na wazalishaji wakubwa wa mafuta ya alizeti katika Mkoa wa Singida.

Lengo kubwa ni kukagua viwango vya  mafuta  hayo na kuwaelimisha  ili  kuhakikisha ubora wa mafuta hayo yaweze  kuingia kwenye  masoko ya kimataifa hatimaye kuinua  uchumi wa  mwananchi mmoja mmoja  na taifa kwa ujumla.

Dkt. Nchimbi ametoa maelekezo hayo kwenye mafunzo maalum ya kudhibiti ubora wa bidhaa yaliyotolewa na TBS kwa wajasiliamali  wa zao la alizeti  na asali yaliyofanyika katika ukumbi wa VETA  hivi karibuni.

Ambapo pia amelipongeza TBS na SIDO kwa kubuni utaratibu wa kutoa mafunzo  hayo  nchi nzima  huku akiwataka kwenda mbali zaidi  kwa kuwa karibu na  kufanya tathmini ya mara kwa mara  kwa mafunzo wanayoyatoa kwa wajasiliamali na kuchukua hatua stahiki.


Amesema  katika dunia ya sasa suala la kuzingatia viwango katika  bidhaa zote hususan   bidhaa za vyakula kwa binadamu la lazima na la kisheria  hivyo  mafunzo  yanayotolewa na TBS na SIDO lazima  yawaguse wahusika ili mafunzo hayo yawe na tija  badala ya kuendelea kutoa mafunzo hayo kwa mazoea.

“Inapofika  suala la  viwango  na ubora wa mafuta yetu  ya alizeti kwenye Mkoa wetu wa Singida linakuwa siyo suala la kubembelezana tena ili kinachozalishwa  kufika salama kwa mlaji” alisisitiza Mkuu wa Mkoa

Amewataka  wazalishaji na wamiliki wa viwanda vya alizeti na asali kuondokana  na fikra potofu za  kuona kuwa TBS ni adui badala yake kujenga ushirikiano wa karibu  ili kuhakikisha kuwa wananufaika  na huduma zinazotolewa na  hatimaye kuboresha  bidhaa wanazozizalisha  na kupata ushindani kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi.

Aidha  amesema TBS ni daraja   baina ya mzalishaji, soko na mlaji  na kuwataka  wajasilia mali  kuwa  karibu ili kutengeneza fursa za biashara zao.

Amesema  tafiti nyingi zimeonesha kuwa  magonjwa mengi ya binadamu yanatokana  na  vyakula   tunavyokula hivyo udhibiti wa ubora  ni jambo lisilokwepeka  kwa sasa ili kunusuru vifo ambavyo vingeweza kuepukika.

Akitolea mfano katika kitabu kitakatifu  cha Mungu  cha Biblia amesema  maandiko  yanasema  hata kabla  ya kumuumba binabamu  Mwenyezi Mungu  alimtengenezea   chakula na pia  kinasisitiza kuwa mtu asiyefanya kazi na asile hivyo ni muhimu kuangalia chakula tunachokula  kwa afya ya mlaji.

Aliongeza kuwa  vitabu vyote vitakatifu  hakuna sehemu yoyote vinaposema mfanyabiashara awe  muongo akawataka  wasifanye  mchezo  na maisha ya  binadamu  kwa kukiuka  viwango  ili kupata  faida  ambapo alisisitiza  kwamba baada ya masomo hayo wajasiliamali wote watoke na viapo  vya moyoni vya kutenda haki na kuwa na hofu ya Mungu katika  utekelezaji wa biashara zao.

Amesema  Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli imedhamilia kwenda kwenye safari ya uchumi wa kati wa viwanda  kwa kuwashirikisha  wajasiliamali wote hapa nchini  hivyo kila mjasiliamali ana haki sawa  kwenye  safari  hii ambayo imeshatoa mafanikio makubwa.

 Naye  Mwalimu Hamis Sudi ambaye  ni Kaimu Mkurugenzi wa udhibiti ubora amemshukuru Mkuu wa Mkoa  na kumhakikishia  usimamizi shirikishi kwenye  udhibiti wa ubora kwenye  bidhaa zinazotokana na zao la alizeti katika mkoa wa Singida na kwamba operesheni maalum itafanyika ili kuwafikia  watengenezaji na wamiliki wa viwanda vya alizeti badala ya kutoa  mafunzo kwa wajasiliamali waliofika kuhudhulia mafunzo hayo.

“Mkuu wa Mkoa naomba  nikuhakikishie  hatujafika hapa Singida kupoteza  fedha na muda wa Serikali bali  kuwafikia wadau wetu wote ambao tutawafikia na tutaleta taarifa ya  utekelezaji katika ofisi yako” aliongeza Sudi.

Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa TBS, Rhoida Andusamile amesema Shirika lilianzishwa kwa Sheria ya Bunge – Sheria ya Viwango Na.3 ya mwaka 1975,iliyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 1 ya mwaka 1977.Sheria  hiyo ilifutwa na nafasi yake kuchukuliwa na Sheria ya Viwango Na.2 ya mwaka 2009 ambayo ililipa Shirika uwezo mkubwa zaidi wa kutekeleza majukumu yake.

Ameongeza kuwa Shirika lina majukumu mengi kama yalivyoainisha katika Sheria ya Viwango Na.2 ya mwaka 2009, lakini majukumu makuu manne.

Aliyataja mambo hayo ni kuweka viwango vya kitaifa vya bidhaa,huduma na mifumo ya usimamizi wa ubora katika sekta zote kutekeleza viwango vya kitaifa katika sekta za viwanda,biashara na huduma kwa kutumia skimu mbalimbali za udhibiti ubora.

Hata hivyo aliongeza kwamba pamoja na hayo lakini pia upimaji wa bidhaa kwa lengo la kuhakikisha ubora wake,pamoja na uthibitisho wa usahihi wa vipimo vinavyotumika viwandani na kutoa mafunzo kwa wazalishaji pamoja na wafanyakazi katika taasisi na viwanda kuhusiana na uzalishaji wa bidhaa bora,uzalishaji salama na usimamizi wa ubora.


Share:

Tuesday, 25 February 2020

January Makamba Afunguka...."Watanzania Wanaujua Mchango Wangu na Inatosha"

Mbunge wa Bumbuli na aliyewahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba, amesema kuwa idadi kubwa ya Watanzania wanatambua mchango wake katika suala zima la kutokomeza matumizi ya mifuko ya plastiki, hata kama viongozi wengine wasipotambua.

Hayo ameandika hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter, wakati akimjibu mwananchi aliyehoji kauli ya Waziri wa sasa Azzan Zungu, aliyedai kuwa suala la mifuko hiyo lilisimamiwa na viongozi wa juu bila kumtaja Makamba.

“Waziri hayuko wrong ni kweli viongozi wetu hao walitusimamia kwenye suala hili, kuhusu kutambua mchango wangu, karibu Watanzania wote wameutambua na hao kwangu wanatosha, hofu yangu ni kama tutashindwa kusimamia mafanikio yaliyopatikana na mifuko ya plastiki ikarejea mitaani” Makamba.

Hivi karibuni mara baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo, Waziri Zungu alisema kuwa licha ya Serikali kupiga marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki, lakini mifuko hiyo imeanza kurejea tena sokoni.


Share:

Bondia Deontay Wilder Amtupia Lawama Kocha Wake Baada Ya Kutandikwa na Tyson

Bondia Deontay Wilder amemfukuza kazi kocha wake Mark Breland kufuatia kupigwa TKO round ya 7 vs Tyson Fury na kupoteza Ubingwa wa Dunia uzito wa juu WBC.

Wilder anaamini Mark alikosea kurusha taulo ulingoni kuashiria kuwa Wilder hawezi kuendelea tena na pambano


Share:

TAMASHA LA SHY WOMEN'S DAY OUT KUTIKISA SHINYANGA MACHI 7,2020


Kikundi cha Wanawake na Mabadiliko mkoa wa Shinyanga (Women For Change - WFC) kinachojihusisha na Ununuzi wa Hisa ili kuinuana kiuchumi na chenye  mfuko wa kusaidia jamii na watoto walioko kwenye mazingira magumu kimeandaa 'Tamasha la Shy Women's Day Out' kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani mwaka 2020.

Mwenyekiti wa Tamasha la Shy Women's Day Out, Faustina Kivambe amesema Tamasha hilo litafanyika siku ya Jumamosi Machi 7,2020 kuanzia saa 8 mchana katika ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga /NSSF  ya zamani ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.

"Kabla ya Tamasha, Machi 5,2020 tutakabidhi bweni la watoto wa kiume katika kituo cha kulelea watoto wenye Ualbino cha Buhangija katika Manispaa ya Shinyanga tulilolifanyia ukarabati na mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga pamoja na wadau mbalimbali waliodhamini tamasha hili",amesema Kivambe.

"Siku ya Jumamosi Machi 7,2020 kuanzia saa 8 mchana tutakutana katika Ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga/NSSF ya zamani kwa ajili ya Tamasha ambapo Kiingilio katika Tamasha hilo ni Shilingi 30,000/=. Tiketi zinapatikana katika duka la Fk House of Kids na CPK Gas Point nyuma ya Benki ya CRDB au piga simu namba 0758 016 162 au 0759 725 898",ameongeza Kivambe.

Amesema Tamasha hilo pamoja na uwepo wa burudani,chakula na vinywaji pia litaongozwa na mada mbalimbali ikiwemo Ujasiriamali, Mahusiano,Ndoa na Malezi, Ushauri wa kisheria na afya.

Amewataja watoa mada kutoka ndani na nje ya Shinyanga watakuwepo ni pamoja na  Aunty Sadaka,Hilda Kisoka, Dr. Rose Malissa,Advocate Salome na  Edna Shoo.

Share:

Executive Assistant at World Vision

Executive Assistant  Purpose of the position: To perform a supporting role to the National Director (ND) by effectively and efficiently executing, organizing and coordinating all activities of the National Director. This includes providing administrative support to the functions within the Office of the National Director. The incumbent will all be responsible for ensuring that the Governance function is… Read More »

The post Executive Assistant at World Vision appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Project WASH Engineer at Lifewater

POSITION:  Project WASH Engineer DUTY STATION: Shinyanga REPORTING TO:  Regional Program Manager (RPM) Area Program Manager with doted reporting relationship to Director of Engineering Operations (DEO) REPORTING POSITIONS:  WASH Technicians RESULTS STATEMENT: I am responsible for the best-in-class engineering—for the planning, designing, and quality—of all types/forms of hardware in order to attain basic water access in all program communities,… Read More »

The post Project WASH Engineer at Lifewater appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger