Viongozi hasimu nchini Sudan Kusini wameunda serikali mpya ya umoja wa kitaifa leo hii inayotarajiwa kudumu kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Siku moja baada ya Rais Salva Kiir kulivunja baraza la mawaziri la serikali iliyopita, kiongozi wa upinzani Riek Machar ameapishwa kama makamu wa kwanza wa rais wa Sudan Kusini.
Hatua sawa na hiyo iliwahi kushindikana mara mbili zilizopita na kuzua mapigano yaliyopelekea vifo vya watu 400,000.
Maelfu ya vikosi hasimu vya makabila tofauti vitalazimika kujumuishwa katika jeshi la serikali mpya.
Umoja wa Mataifa umesema hatua hiyo bado haikutimizwa kulingana na ratiba ilivyopangwa.
Kiir na Machar wamesema masuala mengine muhimu yatajadiliwa chini ya serikali mpya.