Sunday, 9 February 2020

Idadi ya Waliofariki kwa Virusi vya Corona China Yafika Watu 811

Idadi ya waliokufa kutokana na maambukizi ya virusi vya corona nchini China imeongezeka kwa vifo 89 na kufikia watu 811. 
 
Mmarekani na Mjapani pia ni miongoni mwa waliokufa. Watu hao ni raia wa kwanza wa kigeni kufa tangu kuzuka kwa mripuko huo.
 
 Shirika la afya duniani limesema kumekuwa na jumla ya maambukizi 34,800 duniani kote. 
 
Eneo lililoathirika zaidi ni China Bara, ambako kumethibitishwa watu 34,546 walioambukizwa.
 
 Raia watano wa Uingereza akiwemo mtoto wamegundulika kuwa na virusi hivyo nchini Ufaransa.
 
 Waziri wa Afya wa Ufaransa Agnes Buzyn amesema raia hayo waliambukizwa na raia mwingine wa Uingereza ambae katika siku za hivi karibuni alikuwa nchini Singapore.



Share:

Mangula atangaza kuwafyeka wanachama wanaojipitisha majimboni

Makamu  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula ametangaza kuwafyeka mapema wanachama wanaojipitisha kwenye majimbo na kata kabla ya wakati katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu kwa kuwa ni kosa kimaadili

Mangula ametoa onyo hilo jana katika kongamano la maadhimisho ya miaka 43 ya kuzaliwa CCM jijini Dodoma.

Amesema “Uchaguzi ni mwaka 2020 nafasi bado zina wenye nafasi, Rais bado ni Rais, Mbunge, Diwani bado ni wabunge na madiwani, yeyote anayekwenda kwenye jimbo ambalo bado Mbunge halali hadi kuvunjwa kwa bunge, ukionekana unajipitisha, unanusa nusa huko ni kosa la kimaadili, mwaachie atimize yale aliyotarajiwa kwa kipindi cha miaka mitano.”

Makamu Mwenyekiti huyo, amesema baada ya kuvunjwa bunge ndio jimbo litakuwa wazi na kwamba atayeenda kinyume na hapo atakatwa kabla ya kwenda kwenye mchakato wa kura za maoni.

“Kuna kanuni za uongozi na maadili, zinasema katika kupambana na vitendo vya rushwa wakati wa chaguzi mbalimbali, kiongozi yeyote atakayethibitika ameshinda uchaguzi kutokana na kitendo chochote rushwa atanyang’anywa ushindi atakaopata na pia atazuiwa kugombea nafasi yeyote kugombea tena uchaguzi mwingine wowote kama itakavyoamuriwa na Halmashauri Kuu ya Taifa,”amesema

Mangula amesema katika uchaguzi huo watakuwa makini kupita kiasi.

“Ile ya kwenye jimbo kuchukua fomu watu 10 wanaanza kukimbizana huyu kata ile huyu ile ndio inachochea rushwa na kugawanya watu kwenye makundi, lakini ukute kapata kwa njia haramu kanunua ushindi atanyang’anywa,”

Aliongeza “Mambo yanayozuiwa ni kutoa michango, misaada katika eneo ambalo mwanachama anakusudia kugombea nafasi ya uongozi.Viongozi wa kuchaguliwa wanaruhusiwa kutoa misaada, michango katika kipindi ambacho si cha uchaguzi, mtu mwingine ujitie kimbelembele uende kule tunawachuja kabla hata ya kwenda kuzunguka kwa wananchi.”

Mangula alisema “Tukipata yale majina 10 yanayotaka kuomba jimbo Fulani tunaanza kuangalia, malalamiko ya kujipitisha pitisha toa pembeni huyo, wanakatwa waliobaki sasa tuwajadili hata wakiwa watatu ndivyo tutakavyofanya, walioanza kimbelembele cha kujipitisha.”

Akizungumzia kuhusu amani, Mangula alisema mazingira ya amani yanawekwa serikali na kwamba wachafuzi wa amani ni wanasiasa.

“Badala ya kutizama kanuni na taratibu, kwa mfano kuna watu wamesuasa kutambua serikali za mitaa, wanasema hawakubali, bahati mbaya wanasahau hata historia, nina kumbukumbu mwaka 1994 kulikuwa na vyama vingi CCM ilipata ushindi asilimia 97  ya vitongoji vyote, hakuna aliyegoma, wala mashirika ya kimataifa kusema hakukua na demokrasia,”amesema.

Ameeleza mwaka 1999 CCM ilipata asilimia 88, mwaka 2004 ilipata asilimia 92.4, mwaka 2009 asilimia 91.23, mwaka jana imepata ushindi zaidi ya asilimia 90 lakini zimeibuka kelele kuwa hakuna demokrasia na haki za binadamu.

“Hawa wanafiki hawa, kwanini badala ya kujiuliza kwanini wenzetu wanashinda, nitawapa siri tangu mwanzo tulipopata Uhuru alitoa umuhimu kwa chama baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere baada ya Uhuru alitoka na kwenda kuimarisha chama na kumuita Mzee Kawawa endesha serikali hadi mwaka 1962 ndio akarudi kuwa Rais,”amesema

Amesema CCM ina wanachama zaidi ya milioni 10 ndio nguvu ya chama na pia mfumo na mpangilio ya uongozi inatoa nafasi kwa wanachama kukutana na kutatua matatizo na kushauri na hiyo ndiyo nguzo ya chama.


Share:

Mwanajeshi awapiga risasi na kuwaua watu 26 nchini Thailand

Watu 26 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa nchini Thailand baada ya kupigwa risasi kiholela na mwanajeshi mmoja wa nchi hiyo katika mji wa Nakhon Ratchasima.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Thailand ameziambia duru za habari kwamba, Jakraphanath Thomma, afisa wa madaraka ya chini alimshambulia mkuu wake kabla ya kuiba bunduki na risasi kutoka katika kambi ya kijeshi.

Baadaye aliwafyatulia risasi waumini waliokuwa katika hekalu na duka la jumla katika mji huo.

Picha za vyombo vya habari zilionekana zikionyesha mshukiwa huyo akitoka katika gari moja katika eneo moja la duka hilo la jumla katika wilya ya Muang na kuwafyatulia watu risasi kiholela.

Picha nyengine zilionyesha moto nje ya jengo hilo, huku kukiwa na ripoti kwamba ulisababishwa na gesi iliolipuka baada ya kupigwa risasi .

"Mwanajeshi huyo alitumia bunduki ya rashasha kuwapiga risasi watu wasio na hatia na kuwajeruhi wengi huku wengine wakifariki''.

Msemaji wa idara ya ulinzi Luteni jenerali Kongcheep Tantravanich alisema kwamba watu zaidi ya 20 waliuawa.

Moja ya machapisho yake ya mitandao yanaonyesha picha ya selfie yake huku moto ukiwaka nyuma yake.

Ripoti zaidi zinasema kuwa, vikosi vya usalama vilimzingira mshambuliaji huyo na kumuua kwa kumpiga risasi.


Share:

Mgumba: “Wakulima wa Zao la Muhogo walime kwa tija”

Wakulima wa zao la muhogo nchini wameelekezwa kulima kwa tija ili waweze kutosheleza masoko ya ndani na nje ya nchi, huku wakihimizwa kufuata maelekezo ya wataalamu kwenye matumizi sahihi ya mbegu bora na safi badala ya kutumia mbegu yoyote bila kuzingatia hali ya ekolojia.

Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe Omar Mgumba (Mb) alipokuwa akizindua Umoja wa Wazalishaji na Wasindikaji wa Zao la Muhogo nchini (TACAPPA) katika mkutano wa wadau wa muhogo ulioandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) jijini Dar es Salaam.

Mhe Mgumba amesema kuwa zao la muhogo huzalishwa katika mikoa mbalimbali nchini kutokana na uwezo wake wa kustahimili mazingira tofauti ya ekolojia. Kwa mwaka 2018, muhogo ulikuwa zao la pili kwa uzalishaji yenye asili ya chakula hapa nchini baada ya zao la mahindi na ulichangia zaidi ya asilimia 17 ambapo mahindi ilikuwa asilimia 37 na mchele asilimia 13 katika uzalishaji wa mazao hayo ya chakula.

Aliendelea kueleza kuwa pamoja na uzalishaji huo changamoto kubwa katika zao hilo ni uzalishaji mdogo na wenye tija. Kwa mwaka 2017/2018 uzalishaji wa muhogo ulifikia wastani wa tija ya tani nane kwa hekta moja ambayo iko chini sana ukilinganisha na viwango vya nchi zingine zilipofikia kama Indonesia, Nigeria ambao wao wamefikia zaidi ya tani 21 hadi 30, na hii ndio changamoto kubwa sana inayopelekea kushindwa kushindana katika masoko ya Kimataifa.

“Tija ndogo hutokana na matumizi hafifu ya mbegu bora, kutokuzingatia kanuni za mbegu bora, magonjwa mbalimbali yanayokabili zao hilo hasa batobato na michirizi ya kahawia, ukosefu wa masoko ya uhakika, ubora duni wa bidhaa tunazozalisha ambazo zinashindwa kushindana na bidhaa zingine kwenye soko la Kimataifa, matumizi hafifu ya zana za kilimo katika mnyororo wa thamani na matumizi finyu ya bidhaa za muhogo nchini” amesema Mhe Mgumba.

Ili kutatua changamoto hizo Serikali imeboresha Sheria ya vituo vya utafiti wa mazao mbalimbali, kwa sasa kuna vituo saba maalum ambavyo vinafanya tafiti kwa ajili ya zao la muhogo ili kuja na mbegu bora zenye uwezo wa kupambana na magonjwa,

mabadiliko ya tabia nchi na zenye tija hadi sasa aina ya mbegu 21 zimezinduliwa kwa ajili ya zao la muhogo pekee. Aina tisa za mbegu zilizozinduliwa ni kwa ajili ya ukanda wa kusini, aina nane kwa ajili ya ukanda wa mashariki na aina nne kwa ajili ya ukanda wa Ziwa na magharibi.

Nae Mwakilisha kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, amesema kuwa tarehe 4 Juni, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli alizundua programu ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili iitwayo ASDP II na alielekeza programu hiyo itekelezwe na wadau wote katika mnyororo wa thamani, hivyo muhogo ni kipaumbele kwenye programu hiyo. Hivyo uanzishwaji wa Umoja huu ni utekelezaji wa maelekezo hayo.

Bw Edwin Rutageruka Mkurugenzi, Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade. amewasihi wazalishaji wa bidhaa hiyo kujipanga kupitia umoja wao kwa kupenya katika masoko mbalimbali, kuweza kuwahudumia wawekezaji nchini na kuongeza thamani zao hilo.

Ameongeza kwa kusema kuwa TanTrade imesimamia uanzishwaji na usajili wa umoja wa Wazalishaji na Wachakataji wa Muhogo Tanzania baada ya maazimio ya mkutano uliofanyika tarehe 28 Januari, 2019 lengo ni kuwa na sauti ya pamoja katika kuendeleza zao hilo.

Pia Mhe Godwin Gondwe, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Tanga amesema kuwa kwa mkoa wa Tanga wamelichukua kama zao la kimkakati katika kukuza uchumi kupitia kila kaya katika mkoa huo na wameona mafanikio makubwa kupitia zao hilo.

Nae Bi Mwantumu Mahiza Mwenyekiti wa Umoja wa Wazalishaji na Wasindikaji wa Zao la Muhogo nchini (TACAPPA) amesema kwa sasa muhogo ni zao la kilimo cha biashara na sio cha chakula tu, hivyo wakulima waingie kwenye kilimo cha mikataba ili kuondoa udidimizaji kwa wakulima. Pia amehimiza mawakala maarufu kama madalali wajiunge na umoja huo.


Share:

Ujenzi Kiwanda Cha Bidhaa Za Ngozi Cha Karanga Wapamba Moto

Moshi. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amepongeza kasi ya ujenzi wa Kiwanda kipya cha Bidhaa za Ngozi cha Karanga kinachojegwa kwa Ubia baina ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Jeshi la Magereza.

Waziri Mhagama ameyasema hayo Februari 8, 2020 wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Kiwanda kipya cha Bidhaa za Ngozi cha Karanga kilichopo Moshi, Mkoani Kilimanjaro ambapo asilimia 60 ya ujenzi wa kiwanda hicho imekamilika.

Akiwa katika ziara hiyo amethibitisha kuridhika kwa hatua za awali zilizofikiwa na kueleza azma ya Serikali katika kuhakikisha kiwanda hicho kinakamilika kwa wakati kwani kina manufaa makubwa kwa taifa ikiwemo kutoa fursa za ajira na kuchangia katika ukuaji wa pato la taifa.

“Nimeridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huu, na niwaombe mwendelee kutekeleza majukumu yenu usiku na mchana na mjipange kukamilisha kwa wakati, ninaamini kama mgekuwa mmejipanga mapema mradi huu ungekuwa umekamilika hivyo mjipange vizuri kwa kuwa uwezo mnao,” alisema Mhagama

Alifafanua kuwa kiwanda hicho kikikamilika maapema kitaiwezesha Tanzania kuufikia azma inayoitaka ya uchumi wa viwanda kwa kuwa bidhaa bora na zitakazozalishwa katika kiwanda hicho.

“Tunataka Kiwanda hiki kiwe ni mfano wa kuigwa katika Afrika Mashariki kwa kuwa kitazalisha bidhaa zitakazo uzika ndani na nje ya nchi, hivyo mapato yatakayopatikana yataleta faida kubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi,” alisema Mhagama.

Aidha Waziri Mhagama alitoa maagizo kwa wasimamizi na Mkandarasi wa mradi huo na kuwataka kuandaa mpango kazi utakawawezesha kufuatilia kila hatua inayoendelea kwenye ujenzi wa kiwanda hicho, pia kuandaa mapema mpango mkakati wa biashara na masoko utakao wezesha bidhaa zitakazozalishwa zinapata soko la uhakika.

Sambamba na hayo Mhe. Mhagama amemwagiza Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kukutana na Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Makampuni na Wadau wa sekta ya ngozi ili kuangalia upatikanaji wa ngozi bora kwa ajili ya matumizi ya kiwanda hicho ili kitakapokamilika kianze uzalishaji haraka.

Kwa Upande wake Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe amesema kuwa maagizo yaliyotolewa na Waziri alipofanya ziara Januari 15 mwaka huu ataendelea kuyasimamia ili kasi ya ujenzi wa kiwanda hicho kiweze kukamilika kama ilivyokusudiwa.

Wakati huo huo Mhandisi wa mradi huo, SP. Julius Sukambi akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi alieleza kuwa hatua iliyofikiwa sasa ni kutokana na utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Waziri ikiwemo suala la kuongeza nguvu kazi.

“Hivi sasa ujenzi unafanyika masaa 24 yani Usiku na Mchana kwa kutumia wataalam wa Jeshi la Magereza, Mafundi wabobezi na wafungwa ili kukamilisha ujenzi kwa wakati uliokusudiwa,” alisema Sukambi

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, Ndg. Hosea Kashimba alisema kuwa tayari Ofisi yake imeshafika hatua za mwisho kwa ajili ya kupokea Mashine za kutengeneza viatu vitakavyo kuwa vikizalishwa kwenye kiwanda hicho kilichopo Moshi, Mkoani Kilimanjaro.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili February 9















Share:

Saturday, 8 February 2020

Freelance Business Executives at Mwananchi Communications

Freelance Business Executives   Mwananchi Communications Limited, publishers of the leading Tanzania newspapers, Mwananchi, The Citizen and Mwanaspoti is looking for motivated and highly experienced individuals to fill the position of: FREELANCE BUSINESS EXECUTIVES Job Purpose: To develop, maintain and increase a solidly dependable client base, to sell advertising space and provide an effective service to clients so as… Read More »

The post Freelance Business Executives at Mwananchi Communications appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Sales & Business Development at Tancoa

“Tancoal is a limited liability company incorporated and operating in Tanzania. Tancoal is largely a Coal mining and trading company with its mine situated at Ngaka, Mbalawala Area, Mbinga District, Ruvuma Region. ’Tancoal welcomes candidates to join the company to fill the below mentioned post. Title: Sales & Business Development Manager Department: Sales & Marketing Overall Purpose of the… Read More »

The post Sales & Business Development at Tancoa appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Picha : WAKENYA WAJITOKEZA KUUAGA MWILI WA RAIS MSTAAFU WA KENYA DANIEL ARAP MOI


Mwili wa rais mstaafu wa Kenya Daniel Toroitich Arap Moi ukiwasili katika bunge kutoka chumba cha kuhifadhi maiti cha Lee Funeral jijini Nairobi mapema leo.
Rais mstaafu Daniel Toroitich Moi
Mwili wa rais mstaafu wa Kenya Daniel Toroitich Arap Moi umewasili katika bunge kutoka chumba cha kuhifadhi maiti cha Lee Funeral jijini Nairobi mapema leo.

Wakenya kutoka matabaka mbalimbali tayari wameanza kuutazama mwili huo wa kiongozi huyo wa zamani .


Onyo: Baadhi ya wasomaji wanaweza kufadhaishwa na picha hizi

Hatua hiyo inajiri baada ya rais Uhuru Kenyatta aliewasili kutoka nchini Marekani mapema leo kuwa mtu wa kwanza kuutazama mwili huo.Rais Uhuru Kenyatta na mkuu wa majeshi Meja jenerali Samuel Mwathethe

Uhuru alipokewa na naibu wake wa rais William Ruto na mkuu wa majeshi Samson Mwathethe huku usalama ukiimarishwa.

Ruto aliwasili katika majengo ya bunge mwendo wa saa tatu na dakika 50 akiandamana na maafisa wa serikali.

Msafara wa gari lililokuwa likiusafirisha mwili huo kutoka chumba cha Lee ulipitia barabara ya alley Road na kuingia Kenyatta Avenue kabla ya kuingia katika barabara ya bunge ambapo gwaride la kijeshi lilifanywa kutoa heshima.

Moi ambaye aliaga dunia siku ya Jumanne akiwa na umri wa miaka 95 atazikwa nyumbani kwake huko kabarak katika kaunti ya Nakuru tarehe 12 mwezi Februari.Wakati rais Uhuru Kenyatta alipowasili katika majengo ya bunge kutoa heshima zake za mwisho kwa marehemu rais Mstaafu Daniel Moi

Serikali ilitangaza siku ya Jumanne tarehe 11 mwezi Februari kuwa siku kuu kwa raia kushiriki katika ibada ya mazishi ya mwili wa kiongozi huyo wa zamani.
Wakenya walipanga milolongo mirefu ili kutoa heshima yao ya mwisho kwa rais mstaafu

Kwa sasa wananchi waliopanga milolongo mirefu wamepewa fursa kuutaza mwili huo .Shuguli ya kuutazama mwili huo itafanyika kwa siku tatu hadi lkufikia Jumatatu.Wakenya waliojitokeza katika maeneo ya bunge la Kenya ili kutoa heshima zao za mwisho kwa rais mstaafu Daniel arap MoiWakenya wakizidi kumiminika ndani ya majengo ya bunge ili kutoa heshima kwa zao za mwisho kwa rais mstaafu Daniel Moi

Tangazo kutoka Ikulu lilisema kuwa mzee Moi, hata baada ya kuondoka madarakani aliendelea kulitumikia taifa la Kenya na Afrika kwa kuwafundisha viongozi wa Kenya na nje ya Kenya, akiendelea kushiriki kwenye maendeleo ya miradi mbalimbali na kazi za misaada akiihubiri amani, upendo na umoja barani Afrika na duniani.

Mzee Moi aliiongoza Kenya kuelekea kurudisha mfumo wa vyama vingi na katika vipindi vingine vingi vya changamoto; na kumalizika kwa mchakato wa kukabidhi madaraka kwa amani mwezi Desemba mwaka 2002, wakati huo mchakato ambao ulikuwa nadra kufanyika Afrika, ambao uliweka mfano barani afrika na nje ya bara tangu wakati huo.
Daniel Arap Moi: Maisha yake ya siasa na mitazamo kinzani

''Hiba yake inaishi Kenya hata leo. Filosofia ya Nyayo kuhusu 'amani, upendo na umoja' ilikuwa wimbo wake kipindi chake kama kiongozi wa nchi na serikali''. Ilieleza taarifa ya Ikulu.
CHANZO - BBC
Share:

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aagiza haki za malipo ya wasanii wote, waliofariki na waliohai zifuatiliwe na kila msanii apate haki yake

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo ufuatilie hatma za malipo ya kazi za wasanii na wampatie taarifa Katibu Mkuu wao.

Ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Februari 8, 2020)  wakati akizungumza na viongozi wa wizara mbili za Habari na Utamaduni, na ile ya Maliasili na Utalii na wa Chama cha Muziki wa Rhumba Tanzania (CHAMURUTA) kwenye kikao kilichofanyika ofisini kwake, Mlimwa, jijini Dodoma kuangalia namna muziki huo unavyoweza kutumika kutangaza utalii.

“Wakurugenzi nataka mfuatilie hatma ya malipo ya kazi zao. Hivi ni kwa nini mwimbaji wa Tanzania anatunga wimbo wake, unapigwa nchi nyingine Afrika au Ulaya, unauzwa kwenye CD ndani na nje ya nchi, wanafaidi wao lakini mwanamuziki wetu hapati malipo yoyote?”

“Nimewasikia wakisema Taifa fulani mwanamuziki anafaidika hata baada ya kufariki. Hivi Taifa hili wanafanya nini hadi wanafaidika na sisi tunafanya nini, hawa wanafaidika na sisi hatufaidiki. Ni kitu gani hicho kinawafanya wenzetu wananufaika na sisi wa kwetu wasinufaike?

“Msanii anapotoa kazi yake, labda ya muziki na unapigwa Kenya, kuna mfumo gani wa kuhakikisha nchi inapata mapato ili naye aweze kupata haki yake?” amehoji.

Waziri Mkuu amesema aliwahi kuwasikia akina Harmonise, Diamond na Ali Kiba wakisema kwamba wao wanaingiza kazi kwenye YouTube na wanalipwa, inakuwaje sasa wanamuziki wa rhumba wao nyimbo zao haziwekwi huko.

Amesema aliwahi kumsikia mke wa Mbaraka Mwinshehe akiomba Serikali imsadie apate haki kutokana na nyimbo za mume wake ambazo zinaigwa kila mara ili aweze kusomesha watoto. “Inakuwaje huyu mama anakosa hela wakati nyimbo za marehemu mumewe zinapendwa sana na zinapigwa kila mahali?”

“Wakurugenzi nenda mkafanye kazi yenu, leteni taarifa kwa Katibu Mkuu wenu na yeye ataifikisha kwa Waziri. Na kama itabidi kuileta Bungeni, tutalifanyia kazi ili wasanii wetu waweze kunufaika.”

Mapema, akijibu hoja ya kupatiwa mafunzo, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Bi. Juliana Shonza alisema Wizara itaangalia ni aina gani ya kozi zinatolewa na Chuo Kikuu cha Sanaa Bagamoyo (TASUBA) kwani ziko za muda mrefu na za muda mfupi.

“Tutamwambia Kaimu Mkurugenzi wa Sanaa ili awaandalie hayo mafunzo hasa ya muziki wa dansi. Tutahakikisha yanafanyika ndani ya mwaka huu na tutashirikiana nao kuhakikisha muziki wa rhumba haufi,” alisema.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Bw. Costantine Kanyasu alisema wako tayari kushirikiana na wanamuziki wa rhumba kutangaza lakini akataka wafanye mabadiliko makubwa na wabadili mtazamo wao ili waweze kuendana na hali halisi ya soko la sasa.

“Bendi zetu zinahitaji kufanya mabadiliko makubwa ili kwenda na wakati wa sasa na kuweza kuwavuta watu wengi zaidi. Ni Lazima wanamuziki wafikirie muziki kiuchumi, waanze kwenda kidijitali zaidi kuliko kuwa jukwaani peke yake,” alisema.

Naye, Mlezi wa CHAMURUTA, Mzee Kikumbi Mwanzo Mpango (King Kiki) alisema kipaji alichonacho hajakipata kwa kusoma shule bali amepewa na Mungu, na ndiyo maana kiko kwenye damu.

“Niko tayari kuwafundisha vijana wengine kabla Mungu hajaniita, ili vipaji nilivyonavyo visipotee bure. Niko tayari kushirikiana na Serikali kuitangaza Tanzania, na kutangaza utalii,” alisema.

Naye Mwenyekiti wa CHAMURUTA, Dk. Salim Omar Mwinyi alishauri Serikali iangalie uwezekano wa kuanzisha maktaba ya kutunza ala za muziki ili kutunza kumbukumbu kwa vizazi vijavyo. Pia aliomba Serikali iwapatie mafunzo wanamuziki kwa kila mkoa ili waweze kuata uelewa wa mambo mbalimbali ikiwemo uongozi na utunzaji fedha.

(mwisho)
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU


Share:

Trump awafuta kazi mashahidi wawili waliokuwa katika kesi yake ya Kuvuliwa Urais

Rais Donald Trump amewafuta kazi maafisa wawili waandamizi waliotoa ushahidi dhidi yake katika kesi ya kutokuwa na imani naye iliyokuwa inamkabili.

Balozi wa Marekani kwa Muungano wa Ulaya, Gordon Sondland, amesema "Nimeambiwa kwamba rais anataka nirudi nyumbani mara moja".

Awali, Luteni kanali Alexander Vindman, mtaalamu mkuu katika masuala ya Ukraine, alisindikizwa kutoka nje ya Ikulu ya Marekani.

Inasemekana kwamba Bwana Trump amesema anataka kufanya mabadiliko baada ya bunge la Seneti kumuondolea mashtaka yaliyokuwa yanamkabili Jumatano.

Katika kura ya kihistoria iliyopigwa, Bunge la Seneti limeamua kutomuondoa rais huyo wa 45 wa Marekani madarakani kwa madai yaliyokuwa yameibuliwa dhidi yake kutokana na mahusiano yake na Ukraine.


Share:

Iran Yasema Ina Jeshi Imara la Anga Licha ya Mashinikizo na Vikwazo Vya Marekani

Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amesema leo kuwa jeshi la anga la Iran ni madhubuti licha ya vikwazo vilivyowekwa dhidi ya nchi hiyo na Marekani tangu mapinduzi ya kiislamu ya mwaka 1979. 

Khamenei ametoa matamshi hayo wakati alipozungumza na makamanda pamoja na wafanyakazi wa jeshi la anga la Iran.

Kulingana na shirika la habari la serikali nchini humo IRNA, Khamenei amesema tangu mapinduzi ya kiislamu, lengo la Marekani limekuwa kuwazuia kuwa na jeshi thabiti la la anga hali sivyo ilivyo. 

Iran inaadhimisha miaka 41 ya mapinduzi ya kiislamu yaliooiondoa mamlakani serikali ya Shah Mohammad Reza Pahlavi iliyokuwa ikiungwa mkono na Marekani.

Taifa hilo la kiislamu, limeaapa kuimarisha uwezo wake wa kijeshi licha ya shinikizo kutoka kwa mataifa ya Magharibi ya kutaka kukatiza uwezo wake wa kijeshi ikiwa ni pamoja na mpango wake wa makombora.


Share:

Mufti atoa tamko tukio la kuchanwa kwa Quran

Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amewataka Waislamu nchini kuwa watulivu wakati vyombo vya sheria vikiendelea kuchukuwa hatua kwa tukio la kuchanwa kwa Quran.

Amesema kuwa kitendo cha kuchanwa kwa kwa kitabu kitukufu cha Quran kilichofanywa na Afisa Biashara wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, Daniel Malaki hakihusiani na mitazamo yoyote ya kidini bali ni utashi wake binafsi

Ameongeza kuwa kitendo hicho ni cha uzalilishaji wa maneno ya Mungu yanayopelekea kuwaudhi Waislamu na kusababisha kuleta mfarakano miongoni mwa jamii.

“Niwaombe Waislamu kuendelea kuwa na subira na uvumilivu huku wakisubiri kauli za viongozi wao wa Bakwata ambao wanafuatilia kwa ukaribu kesi iliyopo mahakama kwa sasa, “amesema Mufti Zubeir.


Share:

Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye atangaza kujiuzulu nafasi hiyo

Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye ametangaza kujiuzulu kuanzia Machi 31, 2020 baada ya kuitumikia taasisi hiyo kwa miaka nane.

Jana Ijumaa Februari 7, 2020 kwa niaba ya bodi ya wakurugenzi,  kaimu mwenyekiti wa taasisi hiyo Angelina Ngalula alitoa taarifa ya kujiuzulu kwa Simbeye.

 “Kwa niaba ya bodi ya wakurugenzi napenda kuwataarifu wanachama wa TPSF, wabia, wadau na umma kwa ujumla juu ya kujiuzulu kwa Simbeye..., Simbeye alikuwa na mchango mkubwa sana kwa taasisi yetu tangu alipojiunga nayo,” anaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Ngalula amesema Simbeye aliyehudumu nafasi hiyo  tangu mwaka 2012 amejiuzulu ili apate muda wa kutekeleza majukumu yake mengine.
 
Taasisi hiyo imemshukuru kwa utumishi wake na kumtakia kila la kheri katika mambo anayokusudia kuyafanya.


Share:

Taarifa Toka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais IKULU




Share:

Madiwani Ushetu Wataka Mitambo Ya Kutengeneza Barabara Ifanyiwe Matengenezo.

SALVATORY NTANDU
Baraza la madiwani la halmashauri ya ushetu wilayani kahama mkoani shinyanga limeshauri kufanyika kwa matengenezo ya haraka ya  mitambo ya ujenzi wa barabara ya halmashauri hiyo ambayo imeharibika ili kufanya ukarabati wa miundo mbinu ya barabara ambayo imeharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Baraza hilo limetoa ushauri huo febuari 6 mwaka huu katika, kikao cha robo ya pili ya mwaka wa fedha kilichofanyika katika makao makuu ya halmashauri hiyo Nyamilangano na kuhudhuriwa na wakuu wa idara na vitengo na wananchi mbalimbali.

Hoja hiyo imetolewa na Kurwa Shoto diwani wa kata ya Bukomela ambapo alisema kuwa halmashauri hiyo inapaswa kufanya matengenezo haraka ya mitambo yake ili kutatua changamoto ya uharibifu wa miundombinu ya barabara.

“Tusikimbilie kukodisha mitambo yetu bali tuifanyie matengenezo kwanza ile iliyoharibika kabla hatujapanga kuikodisha haiwezekani tukawa na mitambo isiyokuwa inafanya kazi kisa ni mibovu”alisema Shoto.

Kwa upande wake diwani wa kata ya mapamba, Yohana Mango alishauri halmashauri iongeza nguvu katika maeneo yenye changamoto ya barabara ambazo hazipitiki kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali.

“Tumekaribia kuanza msimu wa mavuno kwa mazao kama mahindi,kataranga na Tumbaku hivyo ni budi tukahakikisha halmashauri yenu inakuwa na barabara zenye kiwango na kupitika na kuongeza mapato ya ndani kutoka na ushuru unaotarajiwa kukusanywa”alisema Mango.

Awali akitoa taarifa ya utengenezaji wa Mitambo hiyo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Ushetu, Michael Matomora alisema mitambo hiyo imeshatengenzwa na kwa sasa imebaki kwenye maeneo ambayo wanatengeneza barabara na sio kwamba imeharibika kama inavyodhaniwa.

“Ushetu tunajivunia kuwa na mitambo ya ujenzi wa barabara kwani mpaka sasa tumeweza kutengeneza barabara kilomita  1030 za changarawe ikilinganishwa na halmashauri zingine katika mkoa wa Shinyanga alisema Matomora.

Nae Katibu Tawala msaidizi wa serikali za mitaa kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Alphose Kasanyi aliwataka madiwani hao kujivunia kuwa na mitambo yao ya kutengenezea barabara na wanapaswa kuitunza ili iweze kuleta tija.

“Mkoa wa Shinyanga nyinyi ndio halmashauri pekee yenye kujitosheleza kwa kuwa na mitambo ya kutengenezea barabara hebu jikiteni kufunga njia ambazo hazipitiki ili kuwawezesha wananchi mnao wahudumuia kupata huduma mbalimbali kwa wakati” alisema Kasanyi.

Katika kikao hicho cha kawaida cha baraza la madiwani robo ya pili ya mwaka wa fedha 2019/20 Madiwani wa kata 20 katika halmashauri hiyo wamewasilisha taarifa za maendeleo za kata zao ili ziwezekufanyiwa kazi na wataalamu wa halmashauri ya Ushetu.

Mwisho.


Share:

Wananchi Mkoani Kagera Waweka Itikadi Zao Za Kisiasa Pembeni Na Kuanza Kuchapa Kazi Kwa Pamoja.

Na Avitus Benedicto Kyaruzi,Kagera.
Itikadi za kisiasa zimetajwa kama changamoto kubwa inayowakumba wananchi katika Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera kushindwa kuhudhuria vikao mbalimbali vya maendeleo ususani katika sekta ya maji.
 
Hayo yalibainishwa na Diwani wa kata ya Katoma Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera Mh Deusdelith Rwekaza  kupitia Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo (CHADEMA) mnamo tarehe 07/02/2020 katika kikao cha majumuisho ya kujadili rasimu ya taarifa ya ufatiriaji na uwajibikaji jamii katika setka ya maji katika halmashauri hiyo kikao kilichoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Faraja For Hope And Development Organization(FAHODE) .
 
Katika kikao hicho  ambacho kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa sekta ya maji akiwemo Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa halmashauri, Afsa maendeleo jamii mkoa pamoja na wilaya, Afisa mipango, Afisa Takukuru wilaya, Madiwa wa kata za Kemondo, Katelero,Ibwela,Katoma,Kemondo pamoja na Maruku, ambapo mradi huo wa maji unahudumu, Watendaji wa Kata pamoja na Vijiji na wadau mbalimbali wa maendeleo ususani katika sekta ya maji, kikao ambacho kilifanyikaa katika ukumbi wa mikutano wa Chemba uliopo katika halmashauri hiyo.
 
Katika kikao hicho diwani wa Kata ya Katoma mkoani Kagera Mh  Deusdelith Rwekaza alisema kuwa wananchi wa kata hiyo walikuwa wanahudhuria wachache katika vikao vya maendeleo ususani sekta ya maji  uku sababu ikitajwa kuwa ni itikadi za kisiasa jambo ambalo lilikuwa linarudisha nyuma ukamilishwaji wa miradi ya maji katika kata hiyo.
 
Katika kuhakikisha kwamba  wanamaliza tofauti zao mh Rwekaza alisema kuwa walikaa kikao cha pamoja huku wakimuusisha Mkuu wa Wilaya hiyo Mh Deodatus Kinawilo na wakaridhia kuweka pembeni itikadi hizo na kuwa kitu kimoja katika suala la maendeleo.
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali la Faraja For Hope And Development Organization(FAHODE) ameitaka jamii kufatilia kwa kina juu ya uwajibikaji pamoja na kutunza  vyanzo vya maji na kuviendeleza kwa ajili ya vizazi vilivyopo pamoja na vijavyo.
 
Aidha amewataka wananchi kuhoji miradi mbalimbali iliyopo kwenye kata zao ili kujua kwa kina kuhusu miradi hiyo uku akitumia nafasi hiyo kuipongeza timu iliyoundwa ili kutekeleza miradi ya maji ambayo iliweza kuzungukia miradi hiyo na kuweza kubaini changamoto mbalimbali zinazo ikabiri sekta hiyo ili kuweza kutafutiwa ufumbuzi.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger