Saturday, 8 February 2020

PICHA: Amiri Jeshi Mkuu Rais Magufuli Atunuku Kamisheni Kwa Maafisa Wanafunzi 128 Wa Jeshi La Wananchi Wa Tanzania (JWTZ)




Share:

PICHA: Rais Magufuli Amuapisha Balozi Kanali Ibuge Kuwa Katibu Mkuu Wizara Ya Mambo Ya Nje Na Ushirikiano Wa Afrika Mashariki

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John  Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Kanali Wilbert Augustine Ibuge kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumamosi Februari 8, 2020.


Picha na Ikulu


Share:

Kenyatta na Mkewe wauaga mwili wa Daniel Arap Moi

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amewaongoza wananchi wa Kenya, kuuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Daniel arap Moi, katika majengo ya Bunge jijini Nairobi.

Mwili huo utaendelea kuagwa kesho Jumapili na Jumatatu na Jumanne utapelekwa kwenye Uwanja wa Nyayo kwa ajili ya Ibada.

Mwili wa Moi utazikwa Jumatano Feb. 12, 2020 nyumbani kwake Kabarak, Nakuru.



Share:

Mkuchika Aitaka TIRA Kuhakikisha Kampuni Binafsi Za Bima Zinafanya Kazi Kwa Kuzingatia Sheria, Kanuni Na Taratibu Za Nchi

Na Happiness Shayo -Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst.) George H. Mkuchika ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) kuhakikisha kampuni binafsi za bima nchini zinajiendesha kwa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu ili kutoa huduma zenye ufanisi na ubora kwa wananchi.

Rai hiyo ameitoa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya maadili kwa Kamati ya Uongozi ya Mamlaka hiyo yenye lengo la kuongeza ufanisi wa utendaji kazi, katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma leo.

“Kazi yenu ni kuhakikisha kampuni binafsi za bima zinalipa kodi na zinawalipa kwa wakati wananchi wanaopata ajali za moto, ajali ya gari na majanga mengineyo” Mhe. Mkuchika amesema.

Ameielekeza mamlaka hiyo kufanya ufuatiliaji katika baadhi ya kampuni binafsi zinazotumia muda mrefu kuwalipa wateja wanapopatwa na majanga.

“Serikali iliona umuhimu wa kuwa na chombo kinachodhibiti shughuli za bima nchini ili kuwasaidia wananchi wasiotendewa haki wanapofuatilia stahiki zao baada ya kukumbwa na majanga mbalimbali kwa hiyo nawaomba muwe wakali kuhakikisha wateja wa kampuni hizi wanapata haki zao kwa sababu ninyi ndio kimbilio lao wanapokuwa hawatendewi haki” Mhe. Mkuchika amesema.

Pia, Mhe. Mkuchika ameitaka mamlaka hiyo kusimamia vyema kampuni binafsi ambazo zina matatizo ya mtaji zijiondoe zenyewe ili kupunguza malalamiko ya wananchi wanaodhulumiwa haki zao wakati wa majanga.

Aidha, Mhe. Mkuchika amezikumbusha taasisi na mashirika ya umma nchini kuhakikisha yanatoa gawio kwa Serikali bila kusukumwa kwa kuwa kwa kufanya hivyo ni kutekeleza Utawala Bora.

Naye, Kamishna wa Bima kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania Dkt. Mussa Juma amesema kuwa mamlaka hiyo itaendelea

kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kuwezesha mchango wa sekta ya bima nchini ili kuongeza pato la taifa ikiwa ni sehemu ya kufuata misingi ya Utawala Bora.

“Mamlaka itatoa kinga ya bima kwa sekta zote za uchumi na wananchi dhidi ya majanga mbalimbali ya kiuchumi na kijamii” Dkt.Juma ameongeza.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania imeandaa mafunzo ya maadili lengo ikiwa ni kuboresha utendaji kazi kwa watumishi wa Mamlaka hiyo, kuongeza ufanisi na tija kwa taasisi hiyo katika kutekeleza sera ya Utawala Bora. Mafunzo hayo yamehudhuriwa na wajumbe wa kamati ya uongozi na kamati ya uadilifu kutoka katika Mamlaka hiyo na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.


Share:

RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA BALOZI KANALI IBUGE KUWA KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John  Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Kanali Wilbert Augustine Ibuge kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumamosi Februari 8, 2020,Picha na IKULU


Share:

TAWLA TANGA YATUMIA MIAKA 30 KUTOA MSAADA WA KISHERIA KWA WANANCHI


 Mratibu wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania Mkoa waTanga(Tawla) Wakili Latifa Ayouba akitoa elimu kwa wananchi katika Jiji la Tanga kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria
  Mratibu wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania Mkoa waTanga(Tawla)  Wakili Latifa Ayouba akitoa elimu kwa wananchi katika Jiji la Tanga kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria


 Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba Tanga Doris Wilson Mangwe kushoto akimskiliza mkazi wa Jiji la Tanga wakati wa banda la Tawla.
CHAMA cha Wanasheria Wanawake Mkoani Tanga (Tawla) kimeeleza kwamba wanatumia sherehe zao za kufikisha miaka 30 ya chama hicho kwa kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi mbalimbali mkoani hapa kwa kuwafuata kwenye maeneo yao.

Ambapo mpaka sasa wamekwisha kutoa elimu ya masuala ya kisheria kwa watu zaidi ya 200 ikiwemo utoaji wa msaada wa kisheria kwa watu 60.

Hayo yalibainishwa na Mratibu wa Chama hicho mkoani Tanga Wakili Latifa Ayoub wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kwamba wamejipanga kutoa msaada huo wa kisheria kwa jamii nzima.

“Kwa kweli sisi kama Tawla tunaendelea kushirikiana na jamii ya wakazi wa mkoa wa Tanga kuweza kutoa elimu kwa wananchi kwa lengo la kuwasaidia kuondosha changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili hasa za kisheria”Alisema  

Alisema kwamba tokea waanza kutoa elimu hiyo kuanzia February 1 mwaka huu mpaka February 7 katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye viwanja vya Tangamano, vyombo vya habari na shule za Changa na Usagara.

“Lakini pia elimu kwenye maeneo ya Kwanjeka kwa wakina mama pamoja na msaada wa kisheria kwenye maeneo ya Kata ya Pongwe, Mzizima na Nguvumali na tunaamini itawabadilisha”Alisema

Share:

DC Babati apiga Marufuku Michezo ya kubahatisha maeneo ya Vijijini.

Na John Walter-Babati.
Mkuu wa wilaya ya Babati Elizabeth Kitundu, amepiga marufuku michezo ya kubahatisha (BONANZA)  katika maeneo ya Vijijini na kuagiza waziondoe zote zilizopo.

Amesema kwa vijijini hakuna sifa ya kuwepo kwa michezo hiyo hivyo waipeleke kwenye kumbi za starehe maeneo ya Mijini.

Mkuu wa wilaya Bi. Kitundu amechukua maamuzi hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Babati, kwamba michezo hiyo haisaidii chochote katika maeneo yao zaidi ya kuwapotezea muda vijana.

"Ni kweli hawajakiuka masharti, lakini bado ofisi yangu  inasema hawa watu wa Bonanza wananchi wanawakataa na sijui kama kwenye vijiji vyetu kuna sifa ya kuwekwa mashine hizo, sasa kauli ya mkuu wa wilaya ni kwamba katika halmashauri ya wilaya ya Babati na mkurugenzi ambaye anatoa leseni  anasikia, hakuna mahali ambapo pana kidhi kuweka mashine ya kuchezesha michezo ya kubahatisha, wote watoke waende Mijini ambapo kunastahili" alisema Kitundu.

Amesema mchezo huo unasababisha wanafunzi kuwa watoro na wengine kutoroka muda wa masomo.

Amesema licha ya serikali kutoa leseni katika michezo hiyo lakini wananchi hawaitaki kabisa michezo hiyo.

Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Babati Hamisi Malinga amemueleza mkuu wa wilaya kuwa atasimamia agizo hilo lifanyiwe kazi katika maeneo yote ya vijijini ikiwa ni pamoja na kusitisha leseni zilizotolewa kwa ajili ya mchezo huo.


Share:

Ndege za kivita za Israel zatumia ndege ya abiria kama ngao Syria

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema ndege za kijeshi za Israel zimetumia ndege ya abiria kama ngao ya kujikinga katika uvamizi wake mpya dhidi ya Syria.

Msemaji wa wizara hiyo, Meja Jenerali Igor Konashenkov alisema jana Ijumaa kuwa, ndege ya abiria ya Airbus-320 iliyokuwa na abiria 172 nusra ipigwe na makombora ya mfumo wa Kujikinga ya Syria kielekea Damascus kutoka Tehran wakati ndege za Kijeshi za Israel zilipofanya mashambulizi.

Hata hivyo mfumo wa ngao ya makombora ya Syria mjini Damascus ulifanikiwa kutungua makombora hayo ya  Israel.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Urusi ameeleza bayana kuwa, baada ya kukoswakoswa na makombora , ndege hiyo ya abiria ililazimika kutua kwa dharura katika uwanja wa kijeshi wa Hmeymim katika mkoa wa pwani wa Latakia, magharibi mwa Syria.

Meja Jenerali Konashenkov amekosoa mienendo hiyo ya Israel ya kufanya mashambulizi yake ya makombora bila kujali ndege za abiria zinazoruka katika anga ya Syria


Share:

Idadi ya waliokufa kwa Corona yafikia 722 China

Idadi ya vifo vinavyotokana na maambukizi ya mripuko wa virusi vya corona imeongezeka na kufikia watu 722, ikipindukia rekodi ya vifo vilivyotokana na mripuko mwingine wa virusi vinavyofanana na hivyo vya SARS ambavyo viliikumba China Bara na Hong Kong miongo miwili iliyopita.

Kwa mujibu wa kamisheni ya afya ya taifa idadi nyingine ya watu 86 imepoteza maisha ambapo watano miongoni mwa hao wanatokea katika jimbo la Hubei, ambalo mripuko huko ulizuka Desemba. Kwa rekodi za kila siku kamisheni hiyo pia imesema visa 3,399 vimeripotiwa. 

Kwa hivi sasa zaidi ya watu 34,546 wameambukizwa virusi vyacoronakwa nchi nzima. Katika kipindi cha mwaka 2002 na 2003, ugonjwa wenye kufanana na huu unaosababaishwa na corona uliopewa jina la SARS ulisababisha vifo vya watu 650.

Meli ya starehe ya Japan Princess Diamond imekuwa ikiangaziwa zaidi katika kipindi hiki ambapo pia imeripotiwa visa vitatu vipya na kufanya jumla ya abiria wake 64 kuwekwa katika uangalizi maalumu kwa siku 14. Meli hiyo ilikuwa na jumla ya abiria 3,700. Ijumaa Rais Xi Jinping wa China alizungumza na Rais Donald Trump na kuitaka Marekani kushiriki haraka katika kukabiliana na mripuko wa virusi vya corona, na hasa kutokana na malalamiko ya baadhi ya nchi kuwazuia wasafiri kutoka China.

-DW


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi February 8


















Share:

Katibu Mkuu Dkt.Abbasi:Wizara haitaingia Mkataba na Mtoa Huduma asiye na Kiapo cha Uadilifu

Na Anitha Jonas – WHUSM
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbasi amesema kuwa wizara haitaingia mkataba na mtoa huduma yoyote wa sekta binafsi ambaye hajasaini kiapo cha uadilifu na BRELA.

Dkt.Abbasi ametoa tamko hilo jana Jijini Dodoma, alipokuwa akifanya kikao na wafanyakazi wa Wizara mara baada ya kuapishwa kwa lengo la kuzungumza na wafanyakazi na kutoa maelekezo ya utekelezaji wa majukumu ambapo amesisitiza kuwa sekta zote za wizara ni nguvu laini ya nchi (soft power).

“Katika semina hii ya kiapo cha uadilifu tumejifunza kuwa watoa huduma wote kutoka sekta binafsi wanapokuwa wanaingia mikataba na serikali wanapaswa wawe wamesaini kiapo cha uadilifu na BRELA pia waweke uthibitisho wa kiapo hicho kwenye mkataba na katika kusimamia kiapo hichi nasisitiza uadilifu kwa watumishi,uzalendo na uwajibikaji," alisema Dkt.Abbasi.

Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo wa wafanyakazi Katibu Mkuu huyo alisisitiza mambo mbalimbali kwa wafanyakazi ikiwemo umuhimu wa kuchapa kazi kwa kuzingatia muda pamoja na kuacha majungu kazini na ugoigoi.

Naye Kaimu Katibu Msaidizi Sekretariaeti ya Maadili kwa Umma Kanda ya Kati Bibi. Bibi.Jasmine Bakari alifafanua kuwa utaratibu wa kiapo cha ahadi ya uadilifu hufanyika katika vipindi mbalimbali  ikiwemo pale kiongozi anapobadilishwa, hivyo watumishi hutakiwa kutoa ahadi ya kiapo cha uadilifu kwa kiongozi huyo.

“Semina tuliyotoa leo katika wizara hii ni sehemu ya majukumu ya taasisi  yetu na tumekuwa tukifanya hivi kwa lengo la  kuwakumbusha watumishi wa umma kuhusu kiapo cha uadilifu katika utendaji”. Alisema Bibi.Jasmine.

Halikadhalika nae mmoja wa wafanyakazi wa Wizara hiyo kutoka Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani Bi.Happiness Kalokola alimshukuru Katibu Mkuu huyo kwa kikao alichokifanya pamoja na mafunzo yaliyotolewa kwani  yamesaidia kuwakumbusha watumishi suala la uadilifu.


Share:

Zaidi Ya Ekari Laki Mbili Zatengwa Kwa Ajili Ya Kuwezesha Shughuli Za Vijana – Naibu Waziri Mavunde

NA: MWANDISHI WETU
Serikali imetenga takribani ekari laki mbili katika maeneo mbalimbali hapa nchini ikiwa ni mikakati wa kukuza na kuendeleza shughuli za maendeleo ya vijana.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde (Mb) Februari 7, 2020 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Grace Tendega aliyetaka kufahamu juu ya utekelezaji wa Serikali katika kuendeleza shughuli za vijana.

Naibu Waziri Mavunde alieleza kuwa Serikali imetenga maeneo ya shughuli za uzalishaji mali kwa lengo la kuhamasisha vijana waweze kushiriki katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo na itakayo wanufaisha kiuchumi.

“Serikali itaendelea kuzihamasisha Halmashauri zote nchini kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya shughuli za Vijana ikiwemo kilimo, viwanda na ufugaji ili kuwapa vijana fursa ya kuyatumia maeneo hayo katika shughuli zitakazowaletea maendeleo,” alisema Mavunde.

Wakati huo huo, Mhe. Mavunde alitoa ufafanuzi kwa Mbunge wa Iringa Mjini Mhe. Simon Msigwa (Mb) ambaye aliuliza kuhusu Mpango wa Serikali katika kutoa mafunzo kwa vijana ambao wamehitimu ili waweze kukidhi soko la ajira?

Alieleza kuwa Serikali Kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inatekeleza Programu ya Kukuza Ujuzi nchini ambayo inalenga kuimarisha nguvukazi inapata ujuzi unaotakiwa katika soko la ajira.

Akifafanua baadhi ya Programu ambazo zinatekelezwa ikiwa ni pamoja na Mafunzo ya Kurasimisha Ujuzi uliopatikana nje ya Mfumo usio rasmi, Mafunzo ya Uanagenzi ambayo yanatolewa kwa njia ya ufundi wa fani mbalimbali na Mafunzo ya Kilimo cha Kisasa kwa Teknolojia ya Kitalu Nyumba “Greenhouse”, Mafunzo ya Vitendo Mahali pa Kazi kwa wahitimu n.k.

Aidha alielezea suala la ukosefu wa ajira kwa vijana waliohitimu katika elimu ya juu kwa kigezo cha kutokuwa na uzoefu, “Jitihada za Serikali imekuwa ikiwapeleka vijana hao katika makampuni na viwanda mbalimbali ambapo wanapata mafunzo kwa vitendo kwa muda wa miezi 6 hadi 12 na baada ya hapo  wanapatiwa cheti cha Utambuzi “Certificate of Recognition”, cheti hiko kinawasaidia vijana hao kuwa wanauzoefu wa kazi Fulani,” alisema Mavunde.

Aliongeza kuwa Serikali imekuwa ikiwafadhili vijana kwa kuwapatia mafunzo ya Ufundi stadi katika Vyuo vya Veta, Don Bosco na Vyuo shirikishi ili kuwawezesha vijana wanapata ujuzi unaostahili katika soko la ajira.


Share:

Friday, 7 February 2020

Waziri Mkuu: Serikali Imeboresha Huduma Za Afya, Maji ....Sh. Bilioni 334 Zatumika Kununua Dawa, Chanjo, Vifaa Tiba Na Vitendanishi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeboresha utoaji wa huduma za afya kwa kugharamia ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya vituo 487 vya kutolea huduma za afya.

“Maboresho hayo yanajumuisha vituo vya afya 320, hospitali za halmashauri za wilaya 70, hospitali za zamani tisa na zahanati 88,” amesema.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Februari 7, 2020) wakati akitoa hotuba ya kuahirisha Mkutano wa 18 wa Bunge jijini Dodoma. Bunge limeahirishwa hadi Machi 31, mwaka huu.

Mbali na hayo, Waziri Mkuu amesema Serikali imejenga na kuboresha miundombinu ya hospitali za rufaa za Njombe, Simiyu, Mara, Geita, Songwe, Katavi, Sekou Toure, Burigi - Chato, Mwananyamala, na hospitali za rufaa za kanda ya Kusini Mtwara, kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mbeya, hospitali ya Kibong’oto na ujenzi wa Isolation centre katika hospitali ya Taifa Muhimbili.

“Serikali imekamilisha ujenzi wa nyumba 320 za watumishi wa sekta ya afya pamoja na kugharamia ununuzi wa dawa, chanjo, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi kwa gharama ya sh. bilioni 334,” ameongeza.

Amesema katika kipindi hicho, jumla ya madaktari bingwa 311 wameendelea kulipiwa gharama za masomo ya uzamili katika vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi na kwamba,  katika kipindi cha nusu ya pili, Serikali inakusudia kuajiri zaidi ya watumishi 4,000 wa sekta ya afya.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameelezea mafanikio yaliyofikiwa kwenye sekta ya maji katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2019 ambapo sh. bilioni 325.9 zimetolewa kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maji ikiwemo uchimbaji wa visima  vifupi, vya kati na virefu.

Amesema fedha hizo zimetumika kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama vijijini na mijini. Chini ya  utekelezaji wa miradi hiyo, miradi 631 inaendelea kujengwa ikiwemo 558 ya maji vijijini na 73 ya maji mijini.

“Miongoni mwa miradi mikubwa inayoendelea kutekelezwa ni pamoja na mradi wa maji Arusha, mradi wa maji  wa Same – Mwanga - Korogwe na mradi wa kutoa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika miji ya Isaka, Tinde, Kagongwa, Tabora, Igunga, Uyui na Nzega.

Waziri Mkuu ameema lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ni kuwahudumia wananchi sambamba na kuratibu vyema utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati. Amesema miradi hiyo inayohusisha sekta ya miundombinu wezeshi, nishati, maji, afya na elimu imekuwa chachu ya kuboresha maisha ya Watanzania kupitia ukuaji wa sekta rasmi na isiyo rasmi.

(mwisho)
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU


Share:

Shirika La Shirika la Forodha Duniani (WCO) Kuisaidia Tanzania Kuboresha Huduma Za Forodha

Na. Peter Haule, WFM, Dodoma
Serikali imekubaliana na Shirika la Forodha Duniani (WCO) kuisaidia nchi zana zenye teknolojia za kisasa zinazoweza kung’amua watu wanaofanya biashara za magendo na kuifanya Forodha kuongeza ufanisi wa ufanyaji biashara na ukusanyaji wa mapato.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, alipokutana nan a kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Shirika la Forodha Duniani (WCO), Dkt. Kunio Mikuriya, jijini Dodoma.

Dkt. Mpango alisema kuwa Shirika la WCO limekubali kutoa Boti, mashine za kupiga picha ndani ya Kontena na vifaa vingine vyenye teknolojia za kisasa vinavyoweza kung’amua watu wanaofanya biashara za magendo, hivyo kuifanya Serikali kuwa na uwezo zaidi wa kudhibiti shughuli hizo haramu.

 “Ujio wa Katibu Mkuu wa WCO, katika nchi za Afrika hususani Tanzania na Kenya umelenga kuziwezesha nchi hizo kuzitumia fursa zilizopo katika Shirika hilo na kushirikiana na Idara ya Forodha hapa nchini kurahisisha biashara na ukusanyaji wa mapato jambo ambalo pia ni agenda ya Serikali ya Tanzania”, alieleza Dkt. Mpango.

Dkt. Mpango alisema kuwa, Forodha kwa maana ya Bandari na Vituo vya Forodha vilivyopo katika mipaka ni eneo muhimu katika kukuza biashara katika nchi na Ukanda wa Kusini mwa Afrika, ikizingatiwa kuwa Tanzania ni mlango wa kupitisha mizigo kwenda nchi za Zambia, Zimbabwe, Rwanda, Burundi, Malawi, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na nyingine, hivyo kuwepo kwa Teknolojia hiyo kutakuwa nguzo muhimu ya kuifanya Forodha kuwa ya Kisasa na inayorahisisha biashara.

Alisema kuwa wamekubaliana kutoa fursa kwa vijana wa Forodha kupata uzoefu wa Forodha nyingine zinavyoendeshwa kwa ufanisi na pia kutoa mafunzo kwa wakufunzi ambao si tu watatoa mafunzo nchini lakini pia nje ya nchi.

Wakati huo huo, Dkt. Mpango amewaonya wafanyabiashara za magendo nchini kuachana na biashara hiyo kwa kuwa watapoteza mitaji baada ya Serikali kujipanga kwa teknolojia mpya ya kuwadhibiti kwa kuwa biashara hizo ni hatari kwa uchumi wa Taifa na pia Afya za wananchi.

 “Wito wangu ni kwamba watanzania wote na wengine walio nje ya nchi wanaoshiriki katika biashara za magendo waache vitendo hivyo na wafuate taratibu za Forodha kinyume na hapo watapoteza mitaji yao kwa kuwa tutawakamata’’, alieleza Dkt. Mpango

Waziri Mpango amemuagiza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dkt. Edwin Mhede, kuhakikisha Ushirikiano na WCO unaimarika kwa kuwa Shirika hilo lina manufaa kwa Maendeleo ya Taifa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Shirika la Forodha Duniani (WCO), Dkt. Kunio Mikuriya, alisema kuwa katika kuifanya Forodha iwe na ufanisi lazima kuwe na dhamira njema ya kisiasa, Ushirikiano na wafanyabiashara,wakala na Forodha nyingine nje ya nchi na pia kuwekeza kwenye rasilimali watu, jambo ambalo amehakikishiwa  na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mpango kwamba lipo.

Dkt. Mikuriya ameahidi kuwa Shirika lake litafanya kazi kwa karibu na Tanzania katika mambo yote ambayo wamekubaliana ili kuleta tija katika Sekta hiyo ya Forodha ndani na nje ya Tanzania.

Naye Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa, ameliomba Shirika la WCO kuondoa changamoto zinazoweza kuwakwamisha wafanyabiashara wa Tanzania kuuza bidhaa katika masoko ya Kimataifa na pia waweze kuzitumia fursa za kibiashara katika masoko hayo.

Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dkt. Edwin Mhede, alisema kuwa wamekubaliana na Shirika la WCO, kujenga Maabara ambayo itasaidia kutambua na kupima bidhaa zinazoingizwa kutoka nje ya nchi ili kujiridhisha kama zimezingatia utaratibu, lengo likiwa ni kurahisisha uthaminishaji wa mizigo na uondoshaji wa mizigo bandarini kwa wakati.

“Maabara hiyo itakayojengwa katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato  Jijini Dar es Salaam, itakua miongoni mwa maabara chache Afrika ambayo itakuwa ya mfano katika kusimamia eneo hilo la Forodha”, alieleza Dkt. Mhede.

Alisema kuwa wamekubaliana pia kuweka miundombinu itakayochunguza mizigo inayopita katika Ukanda wa Kusini (Mtwara Corridor), ikizingatiwa kuwa barabara ya Ukanda huo imesajiliwa kwa lengo la kuhakikisha Wajasiliamali na wenye viwanda wanaitumia kwa tija.

Mwisho.


Share:

Waziri Mkuu: Tumeimarisha Ukusanyaji Mapato ...TRA Ilivunja Rekodi Na Kukusanya Tril.1.92 Desemba 2019

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali katika kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa mapato na kurahisisha ulipaji wa kodi zimewezesha mapato ya kodi kwa Desemba, 2019 kuvunja rekodi na kufikia sh. trilioni 1.92.

Amesema hatua hiyo inatokana na jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na RaisDkt. John Pombe Magufuli, baada yakuongezeka kwa uzalishaji katika sekta rasmi na isiyo rasmi, ambazo zimewezesha Serikali kukusanya mapato zaidi.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Februari 7,2020) wakati akiahirisha mkutano wa 18 wa Bunge la 11 bungeni jijini Dodoma. Amesema juhudi hizo zimedhihirika wazi katika nyanja za kiuchumi na kijamii baada ya viashiria vingi vya kiuchumi vinaonesha matokeo mazuri.

Waziri Mkuu amesema mfano, katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2019, mapato ya kodi yaliongezeka hadi kufikia wastani wa sh. trilioni 1.52 kwa mwezi ikilinganishwa na wastani wa sh. trilioni 1.30 katika kipindi kama hicho mwaka 2018

“Katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Septemba 2019, uchumi wa Tanzania ulikua kwa asilimia 6.8. Aidha, ukuaji wa uchumi kwa nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika robo ya tatu ya mwaka 2019 ulikua kwa viwango vifuatavyo: Kenya (asilimia 5.1); Uganda (asilimia 2.7); na Rwanda (asilimia 11.9).”

Amesema ukuaji huo wa uchumi, umechangia kuongezeka kwa uzalishaji katika sekta rasmi na isiyo rasmi pamoja na mambo mengine, juhudi za Serikali zimesaidia kuimarisha uwekezaji katika miundombinu mbalimbali ikiwemo ya barabara, reli, na viwanja vya ndege na kutengemaa kwa upatikanaji wa huduma za maji.

Pamoja na kuimarika kwa huduma za usafirishaji; habari na mawasiliano; kuongezeka kwa uzalishaji wa madini hususan dhahabu na makaa ya mawe; na kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo kumekuwa chachu ya mafanikio hayo.

Kadhalika, Waziri Mkuu amezungumzia kuhusu matumizi katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2019, ambapo amesema Serikali imetumia sh. trilioni 15.32, sawa na asilimia 91.2 ya lengo.

Amesema fedha hizo zimetumika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, ulipaji wa mishahara ya watumishi, ugharamiaji wa deni la Serikali.

Kugharamia ulipaji wa madai ya ndani yaliyohakikiwa (watumishi, wazabuni na wakandarasi) na uendeshaji wa shughuli za Serikali      katika Wizara, Idara Zinazojitegemea, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU


Share:

Kutana Na Mtabibu Mwenye Kubri Kutoka Kwa Allah Chiffu_matunge. Mtabibu Wa Nyota Za Binadamu

Meet with a doctor who no human stars and the natural medicine of Africa who is able to identify you are left and you love him? 

And you have tired many places without success? find Chiffu matunge and see an instant miracle,.He is able to return your relationships and enhance your marriage within just 12 hours,Do you agree with your husband.wife  or lover and he living  with someone else? 

See his help is able to do the top of their relationships if they dont know what they want to direct.

He will make him fulfill all the  promises for a short time.chiffu matunge is using the names of a character or picture to finish your problem,,

He is treating using the books of the Qur-an,the traditional medicine of Africa,the  opening a polytheism..He gives you a genie of wealth ot the one who needs wealth without conditions.Male strength ,and much more +255 712921834

NB:cure for all religions and all  beliefs,,,,
@chiffu_matunge
@chiffu_matunge
@chiffu_matunge



Share:

Tanzania Yaishauri Ethiopia Kutafuta Kiini Cha Raia Wake Kukimbia Nchini Humo

Tanzania imeishauri Nchi ya Ethiopia kuchukua hatua ya kuchunguza kiini cha raia wake kuondoka nchini humo kinyume na utaratibu na kwa njia zisizo halali jambo linalosababisha   mrundikano wa wafungwa ambao wanakamatwa katika nchi wanazopita kama wahamiaji haramu ikiwemo Tanzania.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi ametoa ushauri huo Addis Ababa Ethiopia anakohudhuria mkutano wa 33 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika na kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia kando ya mkutano huo Dkt. Workneh Gebeyehu na ili kuchukua hatua za kudhibiti idadi ya raia wake wanaoondoka nchini humo na kukamatwa katika mataifa mengine Tanzania ikiwemo.

Prof. Kabudi amesema Mpaka sasa takribani raia zaidi ya 1,300 wanashikiliwa katika magereza mbalimbali nchini Tanzania huku idadi ya wanaoendelea kukamatwa ikiongezeka jambo linalosababisha mrundikano wa wafungwa katika magereza ya nchi hiyo.

Ameongeza kuwa katika mazungumzo hayo Tanzania na Ethiopia zimekubaliana kuchukua hatua za pamoja zitakazowezesha kurejeshwa wafungwa na wahamiaji haramu wanchi hiyo wanaoshikliwa Tanzania kwa utaratibu utakaokubalika baada ya majadiliano ya kina na kitaalamu.

Akizungumza kupitia kwa msemaji Waziri wa mambo ya Nje wa Ethiopia Dkt. Workneh Gebeyehu amekiri kuwepo kwa tatizo la vijana wanchi yake kuondoka nchini humo kinyume cha utaratibu na kuitumia Tanzania kama mapito wakielekea katika nchi za kusini mwa Afrika na Ulaya na kuongeza kuwa serikali ya nchi hiyo itachukua hatua madhubuti kukabiliana na hali hiyo.

Pia ameishukuru Tanzania kwa ushirikiano wake katika suala la wahamiaji haramu kwa kutoa taarifa za mara kwa mara kuhusu raia wa Ethiopia wanaoshikiliwa Tanzania na kwamba wana imani kuwa mazungumzo yatakayofanyika yatasaidia kuwarejesha raia hao nchini Ethiopia kwa njia ya pamoja watakayokubaliana.

Kando na masuala hayo ya wahamiaji haramu pia Prof. Kabudi na Dkt. Workneh wamezungumzia masuala mbalimbali ya mashirikiano baina ya Tanzania na Ethiopia ikiwa ni pmaoja na mashirikiano katika masuala ya anga,miundombinu na ubadilishanaji wa utaalamu kuhusu ujenzi wa mabwawa ya umeme ili kuziwezesha nchi hizo kupiga hatua za kimaendeleo katika nyanja ya Uchumi.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger