Saturday, 1 February 2020

RC TELACK : MWAKA HUU TUNAINGIA MIKATABA YA KAZI NA WALIMU


Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bw. Albert Msovela akizungumza na watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa Mhe. Zainab Telack, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama Annamringi Macha na kulia ni Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza na Maafisa Elimu kata, Watendaji wa kata na Wakuu wa shule za msingi na sekondari(hawapo pichani) wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Elimu, ambaye ni Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Bw. Mohamed Kahundi akitoa mwongozo wa Wizara ya Elimu kuhusu upangaji wa vipindi shuleni katika kikao hicho
Baadhi ya washiriki wa kikao hicho wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa katika kikao hicho
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiwa darasani katika shule ya msingi Ukune, Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu akifuatilia ufundishaji na ujifunzaji wa wanafunzi, kulia ni Katibu Tawala Mkoa Bw. Albert Msovela
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiagiza kukarabatiwa kwa viti na meza katika shule ya sekondari Ukune, Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu 
***
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amesema mwaka huu 2020 ataingia mkataba wa kazi na Waratibu wa Elimu kata ili kuweka mikakati ya kuhakikisha ufaulu mzuri katika mitihani ya Taifa ya darasa la saba na kidato cha nne.

Akizungumza katika kikao cha pamoja na Watendaji wa kata, Waratibu Elimu kata na Wakuu wa shule za msingi na sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, Wilaya ya Kahama jana tarehe 31/01/2020, Mhe. Telack amesema lengo la mikataba ni kuhakikisha kuwa kila mmoja anasimamia Elimu kikamilifu kwenye eneo lake ili kuongeza ufaulu.

"Mimi mwenyewe nitasaini Mikataba moja kwa moja na Waratibu Elimu kata nao watasaini na Wakuu wa shule pamoja na walimu, nataka kuona watoto wanatoka darasa la kwanza wanajua kusoma na kuandika, mjipangie mikakati ya kuondoa sifuri" amesema Telack.

Ili kufanikisha mkakati huo, Mhe. Telack amewataka Waratibu wa Elimu kata kuwasilisha kila mwezi taarifa ya maendeleo ya taaluma kwenye kila shule.

Aidha, amesema kuwa kuanzia mwezi Machi mwaka huu kila baada ya miezi miwili ifanyike mitihani ya kuwapima wanafunzi ili kubaini changamoto na kuzifanyia kazi.

Amesisitiza pia ni lazima kuhakikisha mitaala inakamilishwa ili wanafunzi wapate nafasi ya kufanya marudio kabla ya mtihani.

Telack amekemea tabia ya baadhi ya walimu kuwaachia wanafunzi kujisimamia ikiwemo kufuatlia mahudhurio yao wakati walimu wa madarasa wapo. "Walimu tumefikia pabaya, walimu wa madarasa hawafanyi kazi yao, sitaki kusikia"

Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Elimu ambaye ni Afisa Elimu Mkoa, Bw. Mohamed Kahundi amewataka wasimamizi wote Elimu Mkoani hapa kufuata miongozo na maelekezo ya Wizara ya Elimu katika kuandaa ratiba za vipindi ili kukamilisha mitaala.

"Tusibadilishe miongozo na melekezo ya Wizara katika kuandaa vipindi" ,amesema Kahundi.

Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa amewapa siku tatu Wakuu wote wa shule za msingi na sekondari Mkoani hapa kukarabati madawati, viti na meza kwa fedha ya ukarabati inayoletwa na Serikali kila mwezi.


Share:

SERIKALI IMEBORESHA KANUNI ZA USIMAMIZI ELEKEZI WA MAZINGIRA


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima amesema Serikali imeboresha Kanuni za Usimamizi Elekezi wa Mazingira ili kurahisisha na kuharakisha utoaji wa vibali vya tathmini ya mazingira.

Sima ametoa kauli hiyo jana bungeni jijini Dodoma wakati akichangia taarifa ya Kamati ya Viwanda, Biashara na Viwanda ya kipindi cha Julai hadi Desemba 2019 ambayo pamoja na mambo mengine ilizungumzia urasimu wa kutoa vibali.

Alisema kuwa kupitia maboresho hayo sasa wataalamu hao wanaotambuliwa na Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) sasa utendaji kazi wao utaboreka kwakuwa kipengele cha kanuni hizo kitawabana wafanyde kazi kwa ueledi zaidi.

“Hili jambo tumelichukua kama lilivyo ili sasa twende tukakae na wataalamu wetu tukaweke njia sahihi kuondoa urasimu na tunatambua tumebadilisha kanuni lakini pia tunatambua katika suala la vibali leo tunatoa vibali vya muda mfupi ndani ya siku saba mtu anapata kibali wakati anasubiri kibali cha tatmnini ya mazingira ambacho kinachukua muda mrefu na ndio maana inawezekana wawekezaji wanaona kama kuna urasimu,” alisema.

Kwa upande mwingine kuhusu udhibiti wa biashara ya vyuma chakavu Naibu waziri aliwaondoa hofu wafanyabishara wa vyuma chakavu kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Wizara za Fedha na Mipango, Viwanda na Biashara pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha tunalinda miundombinu isiharibiwe.

Hata hivyo Naibu Waziri Sima alikiri kuwa ipo changamoto ya uelewa mdogo wa masuala ya mazingira miongoni mwa baadhi ya wananchi ambapo alisema Ofisi hiyo imeendelea kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari na semina ili kulipa uelewa kundi hilo la watu.


Share:

Taarifa Kwa Umma: Kusitishwa Kwa Matumizi ya Passport za Zamani




Share:

Naibu Katibu mkuu Wizara ya mambo ya ndani Ramadhan Kailima Awasili TAKUKURU Kuhojiwa

Naibu Katibu mkuu Wizara ya mambo ya ndani Ramadhan Kailima amewasili  TAKUKURU Makao Dodoma  majira ya saa 8:50 asubuhi  kwa ajili ya kuhojiwa akiwa na gari ya  Land cruiser T.830 DNL
 
Kailima alikwepa kuingilia lango kubwa la mapokezi akaingilia lango dogo la moja kwa moja hadi chumba cha mahojiano ili kukwepa kamera za wanahabari.

Naibu  waziri wa Mambo ya ndani Hamad Masauni atawasili saa sita mchana


Share:

Uingereza yajitoa rasmi Umoja wa Ulaya

Uingereza imeondoka rasmi katika Umoja wa Ulaya saa sita usiku tarehe 31 Januari 2020 kwa saa za Brussels, Ubelgiji kwa mujibu wa makubaliano, na imekuwa ni nchi ya kwanza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya katika historia ya umoja huo.

Mchakato wa kujitoa kwenye umoja huo uliodumu kwa miaka mitatu na nusu umekamilika jana, ambapo pia utakuwa ni mwanzo wa uhusiano wa aina mpya kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya katika siku za mbele.

Baada ya kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya, Uingereza itakuwa na kipindi cha mpito cha miezi 11 hadi tarehe 31 Desemba 2020. Katika kipindi hicho, pande hizo mbili zitafanya mazungumzo kuhusu uhusiano baina yao, ambapo ajenda kubwa itakuwa ni kufikia makubaliano ya biashara huria.

Hata hivyo muda wa miezi 11 ni mfupi kuweza kukamilisha mazungumzo hayo, na matokeo yake yatajulikana baadaye. Uingereza ilijiunga kama mwanachama mwaka 1973.


Share:

Makonda apigwa marufuku kuingia Marekani

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amepigwa marufuku kuingia Marekani.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani jana  Ijumaa, Januari 31 2020 marufuku hiyo pia inamhusisha mke wa Makonda Bi Mary Felix Massenge.




Share:

Naibu Waziri Shonza: Wazazi Ndiyo Walezi Wa Kwanza Wa Mtoto

Na Anitha Jonas – WHUSM
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amewataka wazazi na familia kuwa walezi wa kwanza kwenye jukumu la kumlea mtoto.

Mheshimiwa Shonza ametoa kauli hiyo jana  Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Mgeni Jadi Kadika (CUF) lilikokuwa likisema serikali haioni sasa ni wakati muafaka kwa vijana wetu kuwekewa umri maalumu wa kutumia mitandao ili kupunguza mmomonyoko wa maadili.

Akijibu swali hilo la msingi Mhe.Shonza alisema kuwa ni kweli utandawazi umechangia sana katika kuleta mmomonyoko wa maadili kwa kiasi kikubwa kwa jamii zetu hususani vijana kupitia intaneti,mitandao ya kijamii na maudhui ya nje kupitia muziki na filamu na ndiyo maana serikali ilileta Sheria ya Makosa ya Mtandao (Cybercrime Act) ya Mwaka 2015 pamoja na Kanuni za Maudhui ya Mtandao na Maudhui ya Redio na Runinga za Mwaka 2018.

‘’Serikali iliiona changamoto hii mmomonyoko wa maadili na ndiyo maana ikaunda Sheria hiyo ambayo ilipigiwa sana kelele ndani na nje ya nchi kuwa ibana uhuru ,‘’alisema Shonza.

Mhe.Shonza akiendeleza kuzungumza wakati ajibu swali la hilo alisisitiza kuwa familia na wazazi ndiyo wenye jukumu la ujumla la kumlea mtoto na taasisi za elimu ya awali,Msingi,Sekondari hadi Elimu ya Juu ambao huwaelimisha kwa maneno na vitendo watoto na vijana kuhusu utambuzi wa mambo mema na mabaya yanayofaa na yasiyofaa, na baada ya hatua hizo ndipo wajibu mkubwa wa serikali unapojitokeza.

Akiendelea kujibu swali la nyongeza la mbunge huyo lilihoji je, serikali haioni haja kufanya kama nchi zilizoendelea kuzuia watoto kuingia katika mitandao na kuangalia picha chafu katika mitandao,Naibu Waziri huyo alijibu kwa kusema kuwa serikali imekwisha fanya kazi kubwa ikiwa ni pamoja na kuunda sheria zinazosimamia masuala hayo, hivyo alitoa wito kwa viongozi kuwa wakwanza kuzisimamia sheria hizo na alisisitiza kuwa suala la malezi ya watoto siyo la serikali peke yake bali ni pamoja na wazazi.


Share:

Mahakama Kenya yazuia wananchi kusajiliwa kwa alama za vidole

Mahakama Kuu Kenya imesitisha kutekelezwa kwa mfumo wa usajili wa wananchi kwa njia ya alama za vidole hadi hapo sheria ya kulinda taarifa itakapopitishwa.

Mbali na kuzuia utekelezaji huo, mahakama imesema kuwa kukusanya taarifa za eneo (GPS) na vinasaba (DNA) ni kinyume na katiba ya nchi.

Serikali ya Kenya imekuwa ikikusanya taarifa mbalimbali katika usajili huo ikiwa ni pamoja na alama za vidole, taarifa za familia, na eneo kamili mtu analoishi.

Wakati wa zoezi hilo ambalo serikali ilisema ni la lazima wale wote ambao hawatojiandikisha hawatopata huduma za msingi za serikali kama vile pasi ya kusafiria (passport), na cheti cha kuzaliwa.

Mahakama imezuia zoezi hilo kwa kile ilichoeleza kwamba wananchi wanaweza kujikuta katika hatari isiyorekebishika endapo taarifa zilizokusanywa zitatumiwa vibaya.

Majaji watatu wa mahakama hiyo waliamuru kusitishwa kwa mpango huo unaofahamika kama Huduma Namba hadi sheria ya kina ya kulinda taarifa zinazotolewa na wananchi upitishwe.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi February 1


















Share:

Friday, 31 January 2020

PICHA: Aliyekuwa Katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani balozi Jacob kingu Naye Awasili TAKUKURU Kuhojiwa

Aliyekuwa Katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani ya nchi, balozi Jacob kingu amefika ofisi za Takukuru jijini hapa kwa ajili was mahojiano kufuatia agizo la Rais John Magufuli kuhusu mkataba tata wa Tsh trilioni 1 wa ununuzi wa vifaa vya zimamoto.  


Kingu ametanguliwa na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Kangi Lugola


Share:

Intern Opportunity at Tegeta Branch NBC

Intern Tegeta Branch NBC NBC is the oldest serving bank in Tanzania with over five decades of experience. We offer a range of retail, business, corporate and investment banking, wealth management products and services. Job Description No role profile available as this role has no assigned corporate grade: This role should not be used to create new positions.… Read More »

The post Intern Opportunity at Tegeta Branch NBC appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Rais Magufuli ateua wenyeviti watatu wa bodi.




Share:

Packaging Engineer at SBL Dar es Salaam

Packaging Engineer SBL Dar es Salaam, Tanzania Job Description : Context/Scope: Serengeti Breweries Ltd (SBL), a subsidiary of East Africa Breweries Ltd (EABL) operates exclusively in Tanzania and is the 2nd largest beer company. The company is an integrated demand/supply business with 3 operational breweries in Dar Es Salaam, Mwanza, and Moshi. SBL’s flagship brand is Serengeti Premium… Read More »

The post Packaging Engineer at SBL Dar es Salaam appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Head of Corporate & Investment Banking at NBC Head Office

Head of Corporate & Investment Banking Head Office NBC NBC is the oldest serving bank in Tanzania with over five decades of experience. We offer a range of retail, business, corporate and investment banking, wealth management products and services. Job Description Commercial/Business Leadership:: Enterprise leadership of a banking product or function; Coordinates activities at a product or functional… Read More »

The post Head of Corporate & Investment Banking at NBC Head Office appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

HR Manager at SICPA Tanzania

HR Manager Req ID: 15868 Posted on: 30-Jan-2020 Location: Dar Es Salaam (TZ10), Tanzania Department: ID-Human Resources & General Administration (50007 Job Family: Human Resources HUMAN RESOURCES MANAGER Fundamental Purpose: Responsible for staffing the needs of SICPA Tanzania, this will involve an active recruitment across Tanzania within short time frame, focus on integration and retention of employees and… Read More »

The post HR Manager at SICPA Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

WHO yatangaza virusi vya corona kuwa hali ya dharura

Shirika la Afya UIimwenguni - WHO limetangaza mlipuko wa virusi vipya vya corona nchini China ambavyo vimesambaa katika nchi nyingine kadhaa kuwa hali ya dharura ya kimataifa. 

Hii ni baada ya visa vya maambukizi ya virusi hivyo kusambaa kwa kasi katika kipindi cha wiki moja, ikiwemo idadi ya vifo vya watu 24 viliyotokea katika saa 24 leo Ijumaa. 

China imeripoti wagonjwa 9,692 waliothibitishwa kuambukizwa huku idadi ya vifo ikifikia 214. Nyingi ya visa hivyo vimeripotiwa katika mkoa wa Hubei na mji mkuu wake Wuhan, ambao ndio kitovu cha mlipuko huo. 

Hakuna vifo vilivyoripotiwa nje ya China. Akizungumza na wanahabari mjini Geneva, Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus ametaja hofu iliyopo ya kusambaa kwa virusi hivyo miongoni mwa watu nje ya China.

 Amesema tangazo hilo la hali ya dharura sio la kura ya kutokuwa na imani na China. Badala yake, WHO inaendelea kuwa na imani na uwezo wa China kuudhibiti mripuko huo.


Share:

Spika Ndugai Asema Wanamsubiri Zitto Kabwe awaeleze kwanini aliandika barua kwa benki ya dunia kuzuia mkopo kwa ajili ya elimu nchini

Spika wa Bunge, Job Ndugai Leo Ijumaa Januari 31, 2020 amesema wanamsubiri Mbunge Zitto Kabwe awaeleze kwanini aliandika barua kwa benki ya dunia kuzuia mkopo kwa ajili ya elimu nchini 

Fedha za mkopo huo ambazo ni zaidi ya Sh1.2 Trilioni zingeelekezwa katika programu za shughuli za elimu.

Kikao hicho kilipangwa kufanyika Jumanne Januari 28, 2020  kwa ajili ya kuidhinisha mkopo huo, lakini kikaahirishwa dakika za mwisho kutokana na kile kilichoripotiwa na vyombo vya habari vya nje kuwa ni ombi la taasisi ya kijamii ambayo ina wanachama wake Tanzania.

“Mtu unaweza kuwa na tofauti na sera au mtazamo kati ya wewe mbunge au upande wa Serikali na kadhalika, lakini kufikia mahali pa ‘kublock’ Tanzania isipate fursa fulani nadhani ni kwenda mbali mno.

“Kwa sababu watoto watakaokosa fursa hiyo ni watoto wa Tanzania ni walimu wa Tanzania ni miundombinu ya elimu ya Tanzania, sijui katika hilo kama mbunge unanufaika nini maana kama ni suala la utofauti la kisera haya ni mambo ya kujadiliana tu,” amesema Spika Ndugai.

Katika kusisitiza hilo, Spika Ndugai amesema, “ningependa kutoa ushauri wa ujumla tu kwamba ni vema kutumia fursa yetu kama wawakilishi wa wananchi tukaelimishana tukaelezana kuliko kuwakosesha Watanzania fursa wakati baadhi yetu watoto wetu wapo Feza Boys, wapo Marian Girls halafu unablock msaada kwa watoto walio wengi wa wapiga kura wetu jambo ambalo halifai kabisa.”


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger