Saturday, 25 January 2020

Senior Supply Chain Officer Job at International Rescue Committee Tanzania Dar es Salaam

Senior Supply Chain Officer Job at International Rescue Committee Tanzania Dar es Salaam Job Summary Job Description The International Rescue Committee (IRC) is an International Non-Governmental Organization working in 40 countries, responding to the world’s worst humanitarian crises and helps people to survive and rebuild their lives. With funding from donor governments, institutions, companies and individual supporters we… Read More »

The post Senior Supply Chain Officer Job at International Rescue Committee Tanzania Dar es Salaam appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi January 25













Share:

Admin Officer Job Vacancy at Seedstars Dar es Salaam, Tanzania

Admin Officer Job Vacancy at Seedstars Dar es Salaam, Tanzania Are you looking to join a fast-growing international and impact-driven startup, work in a flexible environment, and be surrounded by a young and diverse team? Who We Are Seedstars is a global organization with headquarters in Switzerland and a presence in 70+ emerging markets. We are on a… Read More »

The post Admin Officer Job Vacancy at Seedstars Dar es Salaam, Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Tanzania Program Associate at One Acre Fund Morogoro

Tanzania Program Associate We are seeking an exceptional candidate with 5+ years of consulting, project management or entrepreneurial experience and a demonstrated passion for poverty alleviation.   ABOUT ONE ACRE FUND Founded in 2006, One Acre Fund supplies smallholder farmers with the agricultural services they need to make their farms vastly more productive. We provide quality farm supplies… Read More »

The post Tanzania Program Associate at One Acre Fund Morogoro appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Friday, 24 January 2020

Area Sales Manager at Corteva Agriscience

GROWING WHAT MATTERS STARTS WITH YOU Corteva Agriscience™, the world’s first dedicated agriculture start-up, serves to enrich the lives of those who produce and those who consume, ensuring progress for generations to come. Our employees fulfill this purpose everyday by building/ participating in an inclusive culture where we encourage each other to stay curious, think differently, act boldly… Read More »

The post Area Sales Manager at Corteva Agriscience appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

 Acquisition & Assistance Specialist (Career Ladder) Job opportunity at USAID January 2020

Acquisition & Assistance Specialist (Career Ladder) Job opportunity at USAID January 2020 Position Title: Acquisition & Assistance Specialist (Career Ladder) – PDF 473KB Vacancy Number: 72062120R10004 Open to: All Interested Candidates/ All Sources Job Description: FSN-9 (PDF 69KB) Job Description: FSN-10 (PDF 69KB) Job Description: FSN-11 (PDF 73KB) Opening Date: January 21, 2020 Closing Date: February 14, 2020   How to apply: Eligible Offerors are required to complete and submit… Read More »

The post  Acquisition & Assistance Specialist (Career Ladder) Job opportunity at USAID January 2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Kabudi: Niliandika Barua Ya Kujiuzulu Baada ya Mchakato Kuwa Mgumu, Lakini Ilichanwa

Rais Magufuli leo ameshuhudia utiaji saini wa makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya madini ya Barrick.

Kabla ya utiwaji wa saini Waziri wa Mambo ya Nje nchini Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi  amezungumzia namna mchakato ulivyokuwa na changamoto.

Kabudi anasema alichukua uamuzi wa kuandika barua ya kujiuzulu  baada ya mchakato wa majadiliano na wajumbe wa Barrick kuwa magumu, kwamba aliona aibu kushindwa kazi aliyotumwa.

“Wakati wa mchakato wa makubaliano na Kampuni ya Barrick, nilisumbuliwa sana kule Canada ikafika wakati nikakata tamaa, nikasema sijawahi kutumwa kazi na Mkuu wangu na nikashindwa nikaandika barua ya kujiuzulu, wengine wakanipokonya wakaichana“ - Amesema Waziri Kabudi


Amesema wakati huo alikuwa katika wakati mgumu kwani Rais  Magufuli alikuwa akiuliza mambo yanayoendelea, huku bungeni wabunge wakihoji majadiliano ambayo wakati huo hayakuwa yakienda vizuri.

“Kuna wakati walikuja Wachina tofauti wa kuwekeza tukaongea nao ila wakaingia mitini, huku bungeni unapigwa mijeledi, huku Wachina wale wameingia mitini, huku Rais anasubiri umalize, huku unajiuliza utatoka kwa aibu ila Mungu akasimama na sisi,” amesema Profesa Kabudi.


Waziri huyo ameomba radhi kwa lolote litakalopungua, akibainisha kuwa utakuwa upungufu wa kibinadamu


“Tumeanzisha Kampuni ya Twiga, hatuna Barrick pekee Tanzania, tuna Barrick na Serikali ya Tanzania ndani ya Twiga

“Wakati wa majadiliano kati ya Tanzania na Barrick Prof. John Thornton alikubali mikataba haikuwa mizuri na lazima irekebishwe, na Rais Magufuli alisema sitaki mikataba irekebishwe kwa ajili yangu, fedha yote itakayopatikana itakwenda kwenye shule, afya, miundombinu nk"


Share:

Kampuni ya Barrick Gold Yaahidi Kujifunza Kutokana Na Makosa Yaliyofanyika Tanzania

Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya Barrick Gold,  Dk Mark Bristow amesema kampuni hiyo itajifunza kwa makosa iliyoyafanya nchini Tanzania miaka 10 iliyopita.

Dk Bristow ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Januari 24, 2020 Ikulu jijini Dar es Salaam katika hafla ya utiaji saini makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na kamati ya madini ya Barrick.
 
Amesema tangu Rais Magufuli alipoingia madarakani kumekuwa na safari ndefu ya majadiliano kati ya kampuni hiyo na Serikali yaliyowezesha kugawana mapato sawa.

“Sisi wawekezaji tunapokuja kwenye nchi kama hii tuna jukumu kubwa la kuchimba rasilimali ya Taifa si kwa faida yetu tu bali kwa faida pia ya Taifa na wadau wengine. Wadau hao siyo tu wanahisa, bali wananchi ndiyo maana ni wajibu wetu kulipa kodi.”

“Vilevile siyo tu kwa Watanzania wa sasa bali pia vizazi vijavyo vina haki ya kupata mgawo. Kuna jamii zinazozunguka migodi, lazima zishiriki shughuli za uchumi,” amesema.

Baada ya mgogoro uliodumu tangu mwaka 2017, Kampuni ya Barrick na Serikali ziliunda kampuni ya Twiga itakayosimamia migodi mitatu iliyokuwa chini ya kampuni ya Acacia.


Share:

Serikali Yaanza Kuwatambua Wachunaji Wa Ngozi Kisheria, Yatoa Onyo Kwa Wasiyokuwa Na Leseni

Na. Edward Kondela
Serikali imesema itasimamia sheria ya ngozi nchini ya mwaka 2008 ili kuhakikisha zao hilo linaongezewa thamani kwa kuhakikisha inawatambua rasmi wachunaji wa ngozi na kuzifungia machinjio na viwanda vya ngozi visivyokuwa na wachunaji wa ngozi wanaotambulika kisheria.

Hayo yamebainishwa jana (23.01.2020) Mjini Morogoro na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega wakati wa hafla fupi ya kuzindua rasmi mafunzo ya uchunaji ngozi nchini pamoja na kukabidhi leseni kwa wahitimu 161 wa mafunzo ya uchunaji ngozi kutoka katika Manispaa ya Morogoro ambao wametakiwa kufanya kadi kwa weledi mkubwa na kutaka Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA) kuhakikisha inaendeleza elimu hiyo katika ngazi ya wilaya.

“Ninaiagiza LITA kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ieneze katika wilaya zote mafunzo haya ili wachunaji wa ngozi wapate vitambulisho ili tusiweze kukwamisha shughuli za uchunaji wa ngozi katika wilaya zetu, mkakati wa serikali na mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli ni kuona kwamba hatuendelei kutumia fedha zetu kuagiza bidhaa za ngozi kutoka mataifa ya nje kuleta hapa Tanzania, lazima tujitosheleze sisi wenyewe na tayari ngozi zetu ziwe zimetengenezwa katika hatua ya mwisho pamoja na kutengeneza bidhaa za ngozi, tumeamua kusimama imara bidhaa za ngozi zianze kutengenezwa katika utaratibu unaotakiwa.” Amesema Mhe. Ulega

Mhe. Ulega amesema Sheria Na. 18 ya Mwaka 2008 Kifungu Na. 15 katika sheria inayosimamia biashara ya ngozi, inawataja wataalam wa uchunaji wa ngozi na kwamba kama machinjio haina wataalamu wa uchunaji ngozi au kiwanda hakina wataalam sheria inakataza.

Amefafanua kuwa sheria hiyo inaeleza wazi kuwa ikiwa mtu anafanya kazi ya kuchuna ngozi bila kutambuliwa rasmi kisheria zipo adhabu ikiwemo ya kupelekwa mahakamani ambapo kifungu kidogo cha pili kinabainisha kuwa atakayebainika kufanya kazi ya kuchuna ngozi bila kutambuliwa kisheria, atalipishwa faini ya shilingi Milioni Moja au kifungo kisichozidi Miezi Sita au adhabu zote mbili.

Naibu waziri huyo amefafanua kuwa maandalizi ya Tanzania ya viwanda ambayo ni kipaumbele cha serikali ya awamu ya tano ya kukuza viwanda nchini ambavyo vinategemea malighafi zinatokana na kilimo, mifugo na uvuvi, ngozi ni malighafi muhimu katika kutengeneza bidhaa zitokanazo na zao hilo.

“Zao la ngozi limekuwa zao muhimu katika sekta ya mifugo kwa kuliingiza pato taifa kwa mwaka 2019/20 kuanzia mwezi Julai mwaka jana hadi Desemba, Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Ngozi imepata jumla ya makusanyo ya Shilingi Bilioni 5.3, aidha zao la ngozi limeendelea kutoa ajira na kukuza kipato kwa watanzania na wafanyabiashara wa ngozi.” Amefafanua Mhe. Ulega

Awali akizungumza wakati akimkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Mazao ya Mifugo, Usalama wa Chakula na Lishe kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Gabriel Bura amesema mafunzo yaliyotolewa ya uchunaji ngozi kwa washiriki 176 ni utekeleaji wa sheria baada ya kukutana na wadau mbalimbali ambao wamebainisha kuwa ngozi ya Tanzania ina ubora hafifu  kutokana na sababu mbalimbali.

“Ngozi inaharibika kwa mfugaji kwa asilimia 30 kutokana na kupiga mfugo chapa katika maeneo yasiyofaa, mnyama kupita kwenye vichaka, lishe duni na magonjwa ya kupe na ndorobo, aidha asilimia 50 ngozi inaharibika kwenye machinjio namna mnyama anavyochinjwa na namna mchunaji anavyoichuna ngozi hiyo pamoja na vifaa anavyotumia.” Amesema Bw. Bura

Bw. Bura amesema mafunzo ya uchunaji ngozi na utoaji wa leseni tayari yametolewa katika mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro na katika Manispaa ya Morogoro na yanatarajia kuendelea Mwezi Februari mwaka huu katika mikoa ya Kanda ya Ziwa Victoria ili wachunaji wa ngozi waweze kufanya kazi kwa mujibu kwa sheria.

Bw. Mapinduzi Ernest akizungumza kwa niaba ya wachunaji wenzake wa ngozi katika Manispaa ya Morogoro waliopatiwa mafunzo na hatimaye kukabidhiwa leseni ameishukuru serikali kwa kutoa elimu ya uchunaji bora wa ngozi ili kupandisha thamani ya ngozi ambayo inahitajika katika viwanda mbalimbali hapa nchini kutengenezea bidhaa.

Amesema ngozi ya mnyama ikichunwa vizuri itatoa tathmini ya ubora wa ngozi na kuiomba serikali kuhakikisha elimu hiyo inakuwa endelevu ili malighafi ya ngozi iweze kuwa bora zaidi.


Share:

Rais Magufuli Atoa onyo kwa Viongozi wa CCM Kuelekea Uchaguzi Mkuu.....Asema ATCL Sasa Kupaa China Moja kwa Moja

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) , Rais John Magufuli amewataka viongozi wa mikoa wa chama hicho kutokuwa na majina yao mfukoni katika  mchakato wa kura maoni kuwapata wagombea wa udiwani na ubunge.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Ijumaa Januari 24, 2020  jijini Dar es Salaam alipokutana na viongozi wa mikoa, wilaya na jumuiya za chama hicho kutoka mikoa yote nchini.

“Nawashukuru sana wajumbe, kwa kweli leo nina raha sana, na kama ndugu Bashiru unafikiri lolote baya leo hakuna baya shetani ameshindwa. Leo ni siku ya raha ya kukutana na Chama kikubwa kilichoshika hatamu ya uongozi wa Taifa hili.

“Niliona tukutane hapa kwanza tukishamaliza hapa tutakwenda Ikulu kupiga picha na kama kuna maji tutakunywa wote pamoja, Ikulu ni yenu na ninyi ndiyo mlinipeleka Ikulu ahsanteni sana.

“Eneo la fedha na uchumi tumeweza kuchukua hatua mbalimbali kuhakiki, kurejesha na kuthaminisha upya mali na rasilimali za Chama, na jitihada hizo zimeongeza mapato kutoka Tsh Bil 46.1 hadi mwaka 2015/16 hadi tsh Bil 59.8 mwaka 2018/19.

“Baada ya tathimini na shughuli ya uhakiki wa mali za Chama, thamani yake imepanda kutoka Bilioni 41.033 Mwaka 2016/2017 na kufikia Bilioni 974.66 mwaka 2020, ongezeko la asilimia 2275.3%. Tathmini hii ni ya mikoa13 tu na kazi bado inaendelea.


“Niwaombe Viongozi wenzangu ndani ya Wilaya na Mikoa wakati wa mchakato wa uchaguzi tusiende na majina mfukoni tuoneshe ukomavu mwaka huu, tuwaache wengine wakurupuke kuvunja taratibu wagombane, tusikate majina ya Wagombea kwasababu zetu binafsi

“Mtu unajijua ni Mchezaji mzuri unaficha chenga zako kwanini?, tujiandae na uchaguzi, CCM hii sio ile ya nyuma na Wapinzani wetu sio wale wa nyuma, Wapinzani wamebadilisha mikakati yao, mingine wanaiweka hadharani na mingine ni ya kificho, tusibweteke

“Fedha zilizopo sasa hivi tuna uwezo wa kuendesha nchi kwa miezi 6, hatakama tusipokusanya leo hela tunaweza kuendesha nchi kwa miezi 6 ndiyo maana tunapata fedha za kujenga miradi mikubwa.

“Wala pasitokee Kiongozi yoyote ndani ya Serikali atakaye sema Chama kinanifatafata, lazima Chama kikufate kama hutaki kufatwa ondoka upishe tuweke watu wengine.

“Hatutaki Chama hiki kuwa ombaomba ambacho kinategemea matajiri ambao baadae wamekuwa wakikiweka Chama mfukoni. Serikali iliyopo madarakani leo ni ya CCM. Viongozi niliyowateuwa wote, ujue unakwenda kutekeleza masuala ya ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.

“Watendaji wa serikali nataka kutoa wito na Waziri Mkuu uko hapa, wasisitizeni viongozi wa serikali walioko madarakani chama lazima kitawafuata, chama lazima kiangalie matokeo halisi ya miradi inayotekelezwa kule.

“Tuliomba mikopo hawakutupa, tukabana fedha za mafisadi tukajenga wenyewe, huu mradi wa umeme ndugu zangu umepigwa vita sana lakini ulikuwa unapigwa vita kwa sababu watu walikuwa wana interest ya Selou.

“Idadi ya Watalii wameongezeka kutoka Mil. 1.1 mwaka jana hadi zaidi ya Mil. 1.5, tunataka tujenge uchumi wa nchi iliyo tofauti, lakini hata kuzaana hatuko nyuma, kuzaa ni uchumi msidanganywe.

“Mwezi Februari Tanzania itaanza Safari za Ndege kutoka Nchini kwenda China moja kwa moja. Ndege nyingine zinakuja na tumenunua kwa fedha taslimu. Tajiri huwezi kununua kwa kukopa,” amesema Rais Magufuli. 


==>>Msikilize hapo chini


Share:

Refrigeration and Air Conditioning Mechanic Jobs at US Embassy Tanzania

Refrigeration and Air Conditioning Mechanic Jobs at US Embassy Tanzania Announcement Number: DaresSalaam-2020-004 Hiring Agency: Embassy Dar Es Salaam Position Title: Refrigeration and Air Conditioning Mechanic Open Period: 01/23/2020 – 02/06/2020 Vacancy Time Zone: GMT+3 Series/Grade: LE – 1210 5 Salary: TZS TSh19,187,512 Work Schedule: Full-time – 40 hours a week – work schedule Promotion Potential: LE-5 Overview… Read More »

The post Refrigeration and Air Conditioning Mechanic Jobs at US Embassy Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

VIDEO: Utiaji Saini Wa Makubaliano Kati Ya Serikali Ya Tanzania Na Kampuni Ya Madini Ya Barrick

VIDEO: Utiaji Saini Wa Makubaliano Kati Ya Serikali Ya Tanzania Na Kampuni Ya Madini Ya Barrick


Share:

ADMINISTRATIVE CLERK-Jobs at the US Embassy Tanzania

ADMINISTRATIVE CLERK-Jobs at the US Embassy Tanzania Hiring Agency: Embassy Dar Es Salaam Position Title: ADMINISTRATIVE CLERK Open Period: 01/23/2020 – 02/06/2020 Salary: TZS TSh19,187,512 Work Schedule: Full-time – 40 hours a week – work schedule Summary: The U.S. Mission in Dar es Salaam is seeking eligible and qualified applicants for the position of Administrative Clerk (Utility Management… Read More »

The post ADMINISTRATIVE CLERK-Jobs at the US Embassy Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Employment Opportunities at Search for Common Ground (SFCG)

Employment Opportunities at Search for Common Ground (SFCG) Search for Common Ground is an international non-profit organization operating in 36 countries whose mission is “to transform the way the world deals with conflict away from adversarial approaches toward cooperative solutions” Employment Opportunities at Search for Common Ground (SFCG) Program Officer at Search for Common Ground (SFCG) DME Officer… Read More »

The post Employment Opportunities at Search for Common Ground (SFCG) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Supervisory Budget Analyst/Accounting Technician Jobs at the US Embassy (Tanzania)

Supervisory Budget Analyst/Accounting Technician Jobs at the US Embassy Announcement Number: DaresSalaam-2020-003 Hiring Agency: Embassy Dar Es Salaam Position Title: Supervisory Budget Analyst/Accounting Technician Open Period: 01/23/2020 – 01/30/2020 Vacancy Time Zone: GMT+3 Series/Grade: LE – 0405 9 Salary: TZS TSh48,361,493 Work Schedule: Full-time – 40 hours a week – work schedule The incumbent supervises the budget work… Read More »

The post Supervisory Budget Analyst/Accounting Technician Jobs at the US Embassy (Tanzania) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Vacancies at The Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation January 2020

Job Vacancies at The Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation January 2020 Elizabeth Glaser started the Pediatric AIDS Foundation with her close friends Susie Zeegen and Susan DeLaurentis, after her daughter, Ariel, lost her battle with AIDS in 1988. The foundation had one critical mission: to bring hope to children with HIV and AIDS. Today, the Elizabeth Glaser Pediatric… Read More »

The post Vacancies at The Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation January 2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO WAZINDUA GAZETI LAO JIPYA 'SAUTI KUU' JIJINI DAR


Askofu mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato jimbo la Kusini mwa Tanzania (Southern Tanzania Union STU) Mchungaji Mark W Malekana akitambulisha gazeti la Sauti Kuu linalomilikiwa na kanisa hilo kwa waandishi wa habari (Hawapo Pichani) jana Januari 23,2020.Utambulisho wa gazeti hilo ulifanyika katika ofisi za makao makuu ya jimbo yaliyopo Mbweni jijini Dar es saalam.
Askofu mkuu wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato jimbo la Kusini mwa Tanzania Mch. Mark Malekana (wa tatu kulia) akiwa na viongozi wa Shirika la Vyombo vya habari vya Kanisa hilo (TAMC) wakiwa na nakala za Gazeti la Sauti Kuu, lililotambulishwa kwa waandishi wa Habari mapema Jana Januari 23,2020 . Kutoka kushoto ni Reuben Mbonea (Mhazini), Mch. Christopher Ungani (Mkurugenzi mkuu) na Hosiana Mwasomola (Wa kwanza kushoto, Mkurugenzi Mwenza).Utambulisho wa gazeti hilo ulifanyika katika ofisi za makao makuu ya jimbo yaliyopo Mbweni jijini Dar es saalam


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger