Saturday, 18 January 2020

Mataifa yaliyopoteza raia kwenye ndege ya Ukraine yaidai fidia Iran

Mataifa yaliyopoteza raia katika ajali ya ndege ya Ukraine iliyodunguliwa na Iran yameitaka Tehran iwajibike kikamilifu, uchunguzi wa kimataifa uanzishwe na familia za wahanga zilipwe fidia.

Mawaziri wa mambo ya nje wa Canada, Uingereza, Ukraine, Sweden, Uholanzi na Afghanistan wamekutana jijini London katika ubolozi wa Canada.

Mawaziri hao baada ya mkutano wao walitoa taarifa ya pamoja wakiitaka Iran ifanye uchunguzi wa kimataifa utakao kuwa huru na wazi hasa kwa mataifa yanayoomboleza.

Waziri wa mambo ya nje wa Canada Francois-Philippe Champagne amesema wamekutana  kutafuta uwajibikaji na haki kwa wahanga wa mkasa huo na kuongeza kuwa familia za wahanga hao zinataka majibu, jamii ya kimataifa inataka majibu na dunia nzima pia inasubiri majibu na kwamba hawatapumzika hadi watakapoyapata.

Watu wote 176 waliokuwa ndani ya  ndege ya abiria ya Ukraine walipoteza maisha yao wakati ndege yao ilipodunguliwa na kombora muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Imam Khomeini mjini Tehran tarehe 8 mwezi huu.


Share:

CONSERVATION RANGER III- WILDLIFE MANAGEMENT-DRIVING – 15 POST

POST CONSERVATION RANGER III- WILDLIFE MANAGEMENT-DRIVING – 15 POST POST CATEGORY(S) HR & ADMINISTRATION EMPLOYER TANZANIA NATIONAL PARKS (TANAPA) APPLICATION TIMELINE: 2020-01-17 2020-01-31 JOB SUMMARY N/A DUTIES AND RESPONSIBILITIES (i)Driving assigned motor vehicles, ensuring security and safety of the vehicle, passengers and goods on and off the road; (ii)Accounting for fuels, oil and spares parts as per stipulated… Read More »

The post CONSERVATION RANGER III- WILDLIFE MANAGEMENT-DRIVING – 15 POST appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

CONSERVATION RANGER III- ARTISAN – 6 POST

POST CONSERVATION RANGER III- ARTISAN – 6 POST POST CATEGORY(S) HR & ADMINISTRATION EMPLOYER TANZANIA NATIONAL PARKS (TANAPA) APPLICATION TIMELINE: 2020-01-17 2020-01-31 JOB SUMMARY N/A DUTIES AND RESPONSIBILITIES (i)Identifying materials/spares parts required for the work to be done according to one’s field of specialization; (ii)Performing preventive and routine maintenance to motor vehicles, machine and boats, water pipes systems,… Read More »

The post CONSERVATION RANGER III- ARTISAN – 6 POST appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

CONSERVATION ASSISTANT II- WILDLIFE MANAGEMENT-TOURISM – 1 POST

POST CONSERVATION ASSISTANT II- WILDLIFE MANAGEMENT-TOURISM – 1 POST POST CATEGORY(S) TOURISM AND TRAVEL EMPLOYER TANZANIA NATIONAL PARKS (TANAPA) APPLICATION TIMELINE: 2020-01-17 2020-01-31 JOB SUMMARY N/A DUTIES AND RESPONSIBILITIES (i)Receiving and attending park visitors; (ii)Guiding and providing interpretation to visitors/tourists on walking safari, mountain trekking, game viewing and on other tourism activities; (iii)Collecting and preparing daily visitors reports;… Read More »

The post CONSERVATION ASSISTANT II- WILDLIFE MANAGEMENT-TOURISM – 1 POST appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

CONSERVATION RANGER III- BOAT OPERATOR – 1 POST

POST CONSERVATION RANGER III- BOAT OPERATOR – 1 POST POST CATEGORY(S) TOURISM AND TRAVEL TRANSPORT AND LOGISTICS EMPLOYER TANZANIA NATIONAL PARKS (TANAPA) APPLICATION TIMELINE: 2020-01-17 2020-01-31 JOB SUMMARY N/A DUTIES AND RESPONSIBILITIES (i)Anchoring and de–anchoring; (ii)Securing boats to docks; (iii)Operating and directing boats; (iv)Ensuring safety of passengers and goods in the boat; (v)Keeping and maintaining log book and… Read More »

The post CONSERVATION RANGER III- BOAT OPERATOR – 1 POST appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Waziri Mkuu Ataka Mapitio ya Gharama Za Utalii....Asema si sahihi kuwatoza wazawa kwa fedha za kigeni

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza wadau wa masuala ya utalii nchini wafanye mapitio ya gharama za huduma wanazowatoza watalii na amesisitiza kuwa si sahihi kuwatoza wazawa kwa kutumia fedha za kigeni au gharama sawa na wageni.

Aliyasema hayo jana (Ijumaa, Januari 17, 2020) wakati akizungumza na wanachama wa Umoja wa Wenye Mashamba Jozani (UWEMAJO) mara baada ya kukagua miradi ya umoja huo.

Waziri Mkuu alisema kuwa kuna baadhi ya maeneo ya kutolea huduma za kitalii wazawa wanatozwa gharama sawa na wageni. Hivyo, aliwasisitiza waandae viwango maalumu kwa ajili ya wazawa ili kuhamasisha utalii wa ndani.

Alisema ni lazima wadau hao wakatengeneza mazingira mazuri yatakayowavutia wazawa kutembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii nchini. “Kitendo cha kuwatoza wazawa gharama sawa na wageni kitasababisha baadhi kushindwa kutembelea maeneo hayo.”

Akiwa katika eneo hilo, Waziri Mkuu alisema amefurahishwa na namna ambavyo umoja huo unavyotunza mazingira pamoja na viumbe maliasili nyingine kama kobe, kasa, samaki na hivyo kulifanya eneo hilo kuwa kivutio cha utalii.

Kadhalika, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwasisitiza wananchi hao kuendeleza ushirika wao huo kwa sababu utawawezesha kupata mikopo pamoja na misaada mingine kama elimu kuhusu kilimo bora.

Waziri Mkuu alisema Serikali imedhamiria kuhakikisha wakulima wananufaika kutokana na kilimo chao. Aliongeza kuwa ushirika unapaswa kuwa chachu ya mafanikio, hivyo, amewapongeza wananchi hao kwa kuwa na ushirika imara.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwasisitiza wananchi watumie ipasavyo vyandarua vinavyotolewa na Serikali kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa malaria. Aliyasema hayo wakati alipotembelea Kituo cha Afya cha Kizimkazi Dimbani, Wilaya ya Kusini.

Waziri Mkuu akiwa wilayani humo alishiriki maadhimisho ya Siku ya Afya ya Kijiji kwa kugawa vyandarua kwa wanawake wajawazito. Wakati akigawa vyandarua hivyo, alisisitiza umuhimu wa kutumia vyandarua kwa malengo yaliyokusudiwa badala ya kuvitumia kama uzio katika bustani za mbogamboga.

(mwisho)
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU


Share:

Waziri Mkuu: Tusiruhusu Watu Watugawe

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania washirikiane katika kuulinda na kuutetea Muungano wa Tanzania pamoja na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na kamwe wasiruhusu watu kuingiza sumu ya kutaka kuwagawa.

Ameyasema hayo jana (Ijumaa, Januari 17, 2020) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi katika mikutano iliyofanyika wilaya ya Kati na wilaya ya Kusini alipokuwa katika ziara yake ya kikazi mkoa wa Kusini Unguja.

“Watanzania tusikubali mtu yeyote kutugawa kwa sababu sisi undugu wetu ni wa damu, hivyo ni vema tukaendelea kuudumisha muungano wetu tusiruhusu watu kuingiza sumu ya kutaka kutugawa kwani watu hao hawana tija.”

Waziri Mkuu ambaye awali alikagua miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa maabara ya sayansi katika shule ya sekondari ya Bwejuu, mradi wa kilimo cha kisasa Jozani na kuzindua jengo la mama na mtoto Bambi. Amesema hayo yote ni matunda ya muungano hivyo, hawana budi kuendelea kuudumisha.

Akikagua maendeleo ya ujenzi wa maabara ya sayansi katika shule ya sekondari ya Bwejuu, Waziri Mkuu ametoa muda wa miezi mitatu kwa mkandarasi anayejenga maabara hiyo awe amekamilisha kazi hiyo.

Pia, Waziri Mkuu alimwagiza Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Bw. Ayoub Mohammed Mahmoud ahakikishe watumishi wanatenga muda wa siku nne kwa wiki kwa ajili ya kwenda kuwahudumia wananchi katika maeneo yao hususan ya vijiji.

Vilevile, Waziri Mkuu aliagiza Maafisa kilimo wahamishiwe vijijini ili waweze kuwasimamia vizuri wakulima ikiwa ni pamoja na kuwashauri namna bora ya kulima kwa kufuata kanuni na matumizi mazuri ya pembejeo.

Kadhalika, Waziri Mkuu alisisitiza umuhimu wa kutoa huduma kwa wananchi wote bila ya kujali dini, kabila, rangi wala itikadi za chama kwa kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wote wananufaika na kuhudumiwa bila ya kubaguliwa kwa namna yoyote.

Awali, viongozi mbalimbali wa vyama vya upinzani wakiwemo wa vyama vya CUF, NRA, UPDP, NSSR-MAGEUZI waliipongeza Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kwa kuimarisha huduma za kijamii.
 
Viongozi hao walisema kuwa wapo tayari kushirikiana na Rais Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais Dkt. Ali Mohammed Shein kwa sababu viongozi hao wanafanya kazi kubwa na nzuri ya kuwahudumia wananchi.

“Maendeleo hayana chama naunga mkono jitihada zinazofanywa na SMT na SMZ na nimefurahia ziara ya Waziri Mkuu hapa kisiwani Unguja na ninamuunga mkono Rais Dkt. Magufuli tumepata maendeleo ambayo hatukuyatarajia,” alisema Makamu Mwenyekiti wa Taifa wa NRA Bw. Khamis Faki katika mkutano wa hadhara uliofanyika Shehia ya Bambi.

 (mwisho)

IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU


Share:

Naibu Waziri wa Afya Dr Ndugulile Ashangazwa Na Uchapa Kazi Wa Wanawake Ludewa.

*Ahimiza wanawake wa mikoa mingine kuiga mfano wa udhubutu wa wanawake hao.

 *Aaagiza Halmashauri kuwapatia tenda ndogo katika ujenzi wa barabara na madaraja madogo

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amewtaka wanawake na vijana nchini kutumia changamoto zilizopo katika maneo yao kama fursa ya kujiajiri na kuajiri watu wengine.

Dkt. Ndugulile ameyasema hayo wilayani  Ludewa mkoani Nombe wakati alipotembeela vikundi kazi vya wanawake na vijana vinavyojishughulisha na kutengeneza barabara na madaraja madogo wilayani humo.

Dkt.Ndugulile ameongeza kuwa vijana na wanawake wengi wamekuwa wakilalamika kukosa ajira hasa kwa walimaliza elimu ya juu ila wanawake na vijana wa wilaya ya Ludewa wamedhubutu kuchangamkia fursa ya kutengeneza barabara na madaraja madogo.

“Sijawahi kuona kitu kama hiki tangu nianze ziara zangu katika mikoa na wilaya hongereni mmedhubutu na mkaamua ktuia fursa hii kupatakujiajir ni mwanzo mzuri mtafika mbali" alisisitiza Dkt. Ndugulile.

Ameogeza kuwa jambo linalofanywa na vikundi hivyo linaendana moja kwa moja na dhana ya Maendeleo ya Jamii  ya wananchi kushiriki katika shughuli za kimaendeleo katika maneo  yao kwa kuamsha ari yao katika kushiriki shughuli hizo pamoja na kujiongezea kipato.

Aidha Dkt. Ndugulile amezitaka Hlmashauri nchini kuhimiza wanawake na vijana kujiunga katika vikundi vya kijasiriamali ili kuwawesha  kupata mikopo ya kufanya biashara na miradi mbalimbali kama wanavyofanya wanawake na vijana wa wilaya ya Ludewa.

Dkt. Nduguile amewapa moyo wanawake na vijana hao wa wilaya ya Ludewa katika harakati za kutafuta kazi na kuwasihi vijana na wanawake wengine kutojibweteka wakisubiri ajira za kujiajiri bali wajiongeze na kujiajiri na hata kuajiri watu wengine.

"Jambo hili mnalofanya ni jambo jema la msingi litawasaidia kupata kipato na kujinua kiuchumi kwani kwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya  Mhe.Rais Magufuli inasisitiza watu kufanya kazi hasa vijana na wanawake" alisema Dkt. Ndugulile

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kikundi cha DARE Bi. Theopista Mhagama amesema kuwa jumla ya vikundi 54 vimefanikiwa kujisajili katika Mamlaka mbalimbali ambazo zitawawezesha kuomba na kupata kazi za kutengeneza barabara na madaraja wilayani humo na Tanzania kwa ujumla

“Kwakweli tunafarijika sana kwani tumeamua kwa dhati kujikwamua kiuchumi na sio kukaa na kulalamika na kusbiri kufanyiwa kila kitu na Serikali wakati kama vijana na wanawake tunaweza kufanya kazi tukajiajiri na kuajiri wengine” alisema Bi. Theopista.

Ameongeza kuwa mpaka sasa wamepata kandarasi ya kujenga madaraja madogo katika barabara ya lwilo mbongo na yamefika katika asilimia 75 na wamedhutu kuomba tenda za ujenzi wa barabara na madaraja  za kitaifa kwani wanakidhi vigezo kama wakandarasi wengine.

MWISHO


Share:

Kamati Ya PIC Yaitaka Benki Ya Nmb Kuangalia Uwezekano Wa Kuongeza Gawio Kwa Serikali.

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Kamati ya  kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa mitaji ya umma [PIC] imeitaka benki ya NMB kuangalia uwezekano wa kuongeza gawio kwa serikali hali itakayosaidia  kuongeza mapato katika kuchangia mfuko mkuu wa Serikali.

Akizungumza bungeni jijini Dodoma Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa mitaji ya umma [PIC] Dkt Raphael Chengeni amesema hatua hiyo itafanikisha katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo hapa nchini.

Katika hatua nyingine Dkt Chengeni amemuagiza mwenyekiti wa bodi ya benki  ya NMB  Profesa Joseph Semboja kuhakikisha anapeleka mbele ya kamati hiyo mchakato mzima  wa kumpata mtendaji mkuu wa benki hiyo ili kutoa fursa kwa watanzania wenye uwezo na weledi wa kuongoza taasisi kubwa za kifedha wanajitokeza kwa ajili  ya maslahi mapana ya taifa .

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Bi Ruth Zaipuna amesema benki yake inaunga mkono miradi mikubwa ya kimkakati ya serikali ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) ili kurahisisha shughuli mbalimbali za kimaendeleo kwa mwananchi mmoja mmoja  .

Kamati  mbalimbali za bunge zinaendelea na vikao vyake jijini dodoma tangu Januari 13,2020 huku kikao cha 18 cha Bunge  kikitarajia kuanza Januari ,28,2020.

MWISHO.


Share:

CONSERVATION RANGER III-WILDLIFE MANAGEMENT- LAW ENFORCEMENT – 589 POST

POST CONSERVATION RANGER III-WILDLIFE MANAGEMENT- LAW ENFORCEMENT – 589 POST POST CATEGORY(S) SECURITY TOURISM AND TRAVEL EMPLOYER TANZANIA NATIONAL PARKS (TANAPA) APPLICATION TIMELINE: 2020-01-17 2020-01-31 JOB SUMMARY N/A DUTIES AND RESPONSIBILITIES (i)Conducting patrol activities in and around the Park; (ii)Guarding visitors, staff and their properties and ensuring their security; (iii)Enforcing National Parks laws, rules and regulations; (iv)Responding to… Read More »

The post CONSERVATION RANGER III-WILDLIFE MANAGEMENT- LAW ENFORCEMENT – 589 POST appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Naibu Waziri Wa Maliasili Na Utalii, Mhe.kanyasu Aagiza Ngombe 179 Zilizokuwa Zimekamatwa Ziachiwe

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA) kuiachia na kuirudisha mifugo zikiwemo jumla ya ng'ombe 179 zilizokuwa zimekamatwa ndani ya Pori la Akiba la Mkungunero ambayo ni Mali ya Mathayo Marao,  Mwananchi wa Kijiji cha Kimotorok kilichopo ndani ya Pori hilo katika wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara kwa makubaliano ya kutoingiza tena mifugo hiyo.

Uamuzi huo umekuja kufuatia utata uliopo eneo ilipokamatiwa mifugo hiyo kwa vile  Kijiji hicho cha Kimotorok ni miongoni mwa Vijiji na Vitongoji 366 vilivyo ndani Hifadhi na vinavyosubilia maamuzi ya Rais wa Tanzania, Mhe.John PombeMagufuli na moja kati ya maagizo aliyoyatoa  kwamba  wananchi wa Vijiji hivyo   wasibugudhiwe hadi pale maamuzi ya mwisho yatakapotolewa.


Kwa mujibu wa Wahifadhi, Mifugo hiyo iliyokamatwa mwishoni mwa mwaka jana inadaiwa kukutwa mita 450 ndani ya Pori hilo huku Wananchi wakidai kuwa Mifugo hiyo ilikutwa nje ya mita 450 kutoka kwenye mpaka mahali ambako wamekuwa wakiishi huku wakisubiri kauli ya mwisho ya Mhe.Rais.

 Mvutano huo baina  ya Wahifadhi na Wananchi umempekelea Mhe.Kanyasu kutumia busara na  kufikia uamuzi huo kwa kuzingatia kuwa Kijiji hicho kipo ndani ya Hifadhi.

Kutokana na majadiliano ya pande hizo mbili, Naibu Waziri huyo amelazimika   kutoa uamuzi huo wa kuachia  mifugo hiyo kwa makubaliano ya Wananchi wa Kijiji hicho  kuheshimu sheria za Uhifadhi kwa  kutoingiza mifugo ndani ya Hifadhi  hadi pale maamuzi ya mwisho yatakapotolewa na Rais Magufuli.

Akizungumza jana katika mkutano huo uliofanyika kwenye Kijiji cha Kimotorok, Naibu Waziri Mhe.Kanyasu amesema uamuzi huo umefanyika kwa busara kwa vile mifugo hiyo ilibidi ipelekwe mahakamani.



Amesema kitendo cha kuacha kupeleka kesi hiyo mahakamani kinasaidia kupunguza idadi kubwa ya mifugo kufa ambapo hadi sasa zaidi ya ndama kumi wameshakufa.


Kufuatia hali hiyo, Mhe.Kanyasu amewataka wananchi hao kuacha kutumia vibaya kauli ya Rais Magufuli kwa kuanza kuvamia maeneo mapya ya Hifadhi kwa kisingizio cha kauli hiyo ilhali wanatakiwa kubaki na mifugo yao mahali walipo.


Amefafanua kuwa kulikuwa na uwezekano wa kupeleka mifugo hiyo mahakamani ila kutokana na Wananchi hao kuomba maridhiano kwa kutambua kuwa wametenda kosa imepelekea mifugo hiyo kuachia.

Katika hatua nyingine, Mhe Kanyasu amesema Serikali haipendi kutaifisha mifugo inayokamatwa Hifadhini kama sheria inavyoelekeza kwa vile wananchi wengi wamejikuta kwenye umaskini wa hali ya juu, Hivyo amewataka wananchi hao kuacha tabia ya kuingiza mifugo hifadhini kwa vile watafrisiwa.

" Serikali inafurahi kuona Wafugaji wananeemeka kupitia mifugo yao huku uhifadhi ukiendelea kwa maslahi mapana ya Taifa" alisisitiza Kanyasu

Aidha, Mhe.Kanyasu ametoa onyo kwa Wananchi wanaovamia Wahifadhi wakiwa wanatekeleza majukumu yao na kuahidi kuwa Serikali haitamvumilia Mwananchi yeyote atakayethubutu kutumia mabavu dhidi ya Wahifadhi.

" Tukikubaini ni miongoni mwa Mwanakijiji uliyejitokeza ukiwa umeshika mkuki au unapiga mwano kwa nia ya kuwahamasisha wenzako kwa ajili ya kuwadhuru Wahifadhi, Tutakushughulikia ipasavyo" Alisisitiza

Kwa upande wake Mbunge wa Simanjiro, Mhe. James Millya amewataka wananchi waache tabia ya kuingiza mifugo ndani ya Hifadhi.

Pia amelaani vikali vitendo vya baadhi ya  wananchi wanaohamasisha ghasia kwa Wahifadhi na kuahidi kuwa yeye hatakuwa tayari kumsaidia mwananchi yeyote atakayekamatwa kwa kutenda kosa hilo kwa vile Wahifadhi hao wanafanya kazi za kulinda Hifadhi hizo kwa niaba ya Watanzania wote.


Kufuatia hali hiyo, Mhe.Millya amewataka Wazee wa mila 'Olaibon' kutumia nafasi hiyo kwa kuitaka jamii yao kufuata sheria za Uhifadhi kwa kuheshimu Sheria zilizopo zinazokataza kulisha mifugo ndani ya Hifadhi

Akizungumza kwenye mkutano huo, Mhe.Millya amewataka Wananchi hao kila mmoja awe Mlinzi wa mwenzake kwa kuimarisha ujirani mwema kati ya Wananchi na Wahifadhi badala ya kuendekeza uhasama kwa kuingiza mifugo ndani ya Hifadhi.

Awali, Joseph Olematwaa ambaye ni mkazi wa Kijiji hicho alisema uamuzi wa kuachia mifugo utarudisha mahusiano mema kati ya Wahifadhi wa Pori hilo na Wananchi na kuahidi kuwa hawataingiza tena mifugo ndani ya Hifadhi.


Share:

Territory Manager Job at Upfield Mbeya

Territory Manager- Mbeya Based in Mbeya, Tanzania At Upfield our purpose is clear: we make people healthier and happier with nutritious and delicious, natural, plant-based products that are good for you, our planet; and with packaging that’s free from plastic. We’ve got iconic brands like Rama, Country Crock, Blue Band and Flora that people all over the world… Read More »

The post Territory Manager Job at Upfield Mbeya appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Katibu Mkuu CCM Awataka Wapinzani Wajiandae Kukubali Kushindwa

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally amevitaka vyama vya upinzani nchini kujiandaa mapema kukubali kushindwa kama ambavyo CCM ilikubali kushindwa katika baadhi ya majimbo mwaka 2015.

Ameeleza kuwa CCM ikishindwa huwa inakubali kushindwa kama ambavyo walikubali mwaka 2015 katika majimbo mbalimbali nchini ikiwemo jimbo la Kigoma Mjini, hivyo amevitaka vyama vya upinzania navyo viige mfano huo wa CCM na waanze mapema kujiandaa kukubali kushindwa.

Katibu Mkuu ameyasema hayo, jana tarehe 17 Januari, 2020 alipokuwa akizungumza katika mkutano wa ndani na wajumbe wa mikutano mikuu ya kata, kamati ya siasa ya wilaya ya Uvinza, Waasisi, wazee maarufu, wenyeviti wa mashina, mabaraza ya Jumuiya ngazi ya matawi na kata, wenyeviti wa vijiji na serikali zao, Kata ya Kazuramimba wilayani Uvinza Mkoa wa Kigoma.

“wanaCCM tukishindwa hukubali kuwa tumeshindwa, tuliposhindwa Kigoma Mjini Ubunge na Halmashauri tulikubali na wao wajifunze pia kwamba unaposhinda, unayemshinda akubali na kuwa muungwana kuwa umemshinda, na akirudi awamu nyingine akakung’oa na wewe ukubali”.

Amesisitiza kuwa, “Nimekuja kutoa ujumbe Kigoma nzima, ikiwemo Kigoma Mjini kuwa, tumejipanga kushinda, wajiandae kukubali kushindwa, hivyo nimekuja kufunga mitambo ya ushindi wa maendeleo na kwa hali ya Kigoma ni lazima nifunge mitambo ya kimkakati, ndio maana nilianza Unguja, Pemba, nikaenda Tanga na kisayansi ilinitaka ndani ya masaa 48, niwe nimefunga Kigoma na nimefanya, kwa kuwa jana nilikamilisha Tanga, leo nimeifunga rasmi hapa”.

Aidha, katibu Mkuu pamoja na mambo mengine, amesisitiza uimarishaji wa Serikali za Mitaa ambapo amegusia baadhi ya sifa za wanachama wa CCM watakaowania nafasi za Udiwani ni lazima wawe ni watu ambao tutaamini wanaweza kuongeza tija katika maendeleo ya watu, wenye uelewa juu ya maisha ya watu, kwa kuwa serikali za mitaa ni kiungo muhimu kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

“Diwani wa CCM ni lazima awe na uelewa wa maisha ya watu na hii haihitaji shahada, inahitaji uelewa na ushirikiano na wananchi wenzake, wanamjua vizuri, anawajua vizuri anayajua mazingira vizuri, yupo tayari, je atatumika au anakwenda kutumikiwa? Ni lazima tuwe na uhakika atatufikisha mbali , hata Mbunge naye ni Diwani hivyo ni lazima awe na sifa za kiungo, na atatumika vizuri kwenye Baraza kuunganisha halmashauri na masuala ya kitaifa”.

Mkutano huo wa ndani umehudhuriwa na wanachama wa CCM na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma Ndg. Amandus Nzamba, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa Ndg. Kirumbe Ngenda, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga, Mbunge wa Jimbo la Uvinza Bi. Hasna Mwilima, Mbunge wa Viti Maalum Bi. Zainabu Katimba na Mkuu wa wilaya ya Uvinza Ndg. Mwanamvua Mlindoko.


Share:

Mount Allison University International Award In Canada

Scholarship Description: Mount Allison University International Award in Canada is open for International Students The scholarship allows Bachelor, Undergraduate level programm(s) in the field of All Subjects Offered by University. taught at Mount Allison University The deadline of the scholarhip is 01 Mar 2020. Degree Level: Mount Allison University International Award in Canada is available to undertake Bachelor,… Read More »

The post Mount Allison University International Award In Canada appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

681 Jobs at Tanzania National Parks (TANAPA) January 2020

681 Jobs at Tanzania National Parks (TANAPA) January 2020   THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA PRESIDENT’S OFFICE PUBLIC SERVICE RECRUITMENT SECRETARIAT Ref.No.EA.7/96/01/K/142 17th January, 2020 VACANCIES ANNOUNCEMENT On behalf of Tanzania National Parks (TANAPA) President’s Office, Public Service Recruitment Secretariat invites qualified Tanzanians to fill 681 vacant posts as mentioned hereunder. 1.0 TANZANIA NATIONAL PARKS (TANAPA) Tanzania National… Read More »

The post 681 Jobs at Tanzania National Parks (TANAPA) January 2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

International Financial Aid Program, USA

Scholarship Description: International Financial Aid Program, USA is open for International Students The scholarship allows Undergraduate level programm(s) in the field of All Subjects taught at University of Chicago The deadline of the scholarhip is 15 Feb 2020. Degree Level: International Financial Aid Program, USA is available to undertake Undergraduate level programs at University of Chicago. Available Subjects:… Read More »

The post International Financial Aid Program, USA appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

CONSERVATION OFFICER II-WILDLIFE MANAGEMENT – 32 POST at TANAPA

POST: CONSERVATION OFFICER II-WILDLIFE MANAGEMENT – 32 POST EMPLOYER TANZANIA NATIONAL PARKS (TANAPA) APPLICATION TIMELINE: 2020-01-17 2020-01-31 JOB SUMMARY N/A DUTIES AND RESPONSIBILITIES (i)Organizing and participating in anti–poaching patrols and security of park resources; (ii)Investigating, prosecuting and presenting evidence before the courts of law for issues pertaining to poaching or banditry; (iii)Participating in managing park boundary; (iv)Managing trophies… Read More »

The post CONSERVATION OFFICER II-WILDLIFE MANAGEMENT – 32 POST at TANAPA appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger