Wednesday, 15 January 2020

Job at Associated Supplies Limited – Sales & Marketing Officer

Position: Sales & Marketing Officer Location: Dar es salaam Job Summary We require a highly skilled and experienced personnel to fill-in the title of Sales & Marketing Officer  Qualifications: Good communication in English and Interpersonal skills. Customer focused. Capacity to work under pressure. Ability to adapt in a changing and fast paced environment Positive can-do attitude, proactive, flexible, enthusiastic,… Read More »

The post Job at Associated Supplies Limited – Sales & Marketing Officer appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Tanzania All scholarships & Opportunities For Youths 2020 academic year [#DailyUpdates]

Tanzania scholarship 2020, embassy finder embassy of belgium scholarship in tanzania, tanzania scholarship 2020, scholarships for tanzanians in canada, china embassy in tanzania scholarship 2020, embassy finder embassy of ireland scholarship in tanzania, masters scholarships in Tanzania 2020, commonwealth scholarship tanzania.   Browse All Recently announced Scholarships and Other OPPORTUNITIES across the world for Tanzania and Africans  … Read More »

The post Tanzania All scholarships & Opportunities For Youths 2020 academic year [#DailyUpdates] appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Job at Diamond Trust Bank (DTB)

Overview Diamond Trust Bank (DTB) is a leading regional bank, listed on the Nairobi Securities Exchange (NSE). An affiliate of the Aga Khan Development Network (AKDN), DTB has operated in East Africa for over 70 years. DTB’s focus on the SME sector and commitment to enhancing convenience for customers through branch network expansion has driven the Bank’s growth… Read More »

The post Job at Diamond Trust Bank (DTB) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Mvua Zinazoendelea Kunyesha Zaleta Maafa Dodoma

Zaidi ya nyumba 120 zimebomoka na madaraja kuharibika Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Maeneo yaliyoathiriwa na mvua hizo ni Bahi Sokoni, Bahi Misheni, Mji mpya, Nkogwa, Mbuyuni, Uhelela, Laloi, Mugu na Nagulo.

Juzi Mkuu wa Wilaya, Mwanahamisi Mukunda akiongozana na wataalamu wa Halmashauri ya Bahi na watendaji wa vijiji, walitembelea baadhi ya wakazi walioathirika na mafuriko hayo na madaraja ambayo yameharibika.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kijiji cha Sokoni, Sifael Mbeti alisema mvua imesababisha mito mingi kufurika na hivyo kusababisha maji kuleta madhara kwa kubomoa nyumba na madaraja.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Bahi Sokoni, Fredrick Kachiwile alisema zaidi ya nyumba 86 katika kijiji hicho zimebomoka.

Alisema katika Kijiji cha Uhelela taarifa za awali zinaonyesha nyumba 35 zilibomoka na katika Kijiji cha Nagulo barabara imekatika na mawasiliano ni ya shida.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Nagulo, Ashery Silla alisema jumla ya nyumba 18 zimeanguka.


Share:

Rose Muhando Afunguka yale yaliyojiri Wakati akitolewa mapepo Kanisani Nchini Kenya

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Rose Muhando hatimaye amezungumza kuhusu video iliyosambaa sana mitandaoni mnamo 2018.

Huku watu wakiendelea kuwa na maswali kuhusu kudidimia kwake, video ya msanii huyo akijibingirisha sakafuni akiwa amelala chali iliwaacha wengi na hisia kinzani.

Akizungumza na SDE ya Kenya, Rose alikiri kwamba anafahamu fika kuwa tukio hilo lilitokea katika kanisa la Pasta Ng’ang’a.

Hata hivyo, hana ufahamu wowote wa namna alijipata katika kanisa hilo ama kile kilichojiri wakati alikuwa anaondolewa mapepo.

Mwimbaji huyo anayesifika sana kwa wimbo Yesu Nibebe, pia alikanusha madai ya kumuomba mchungaji huyo mwenye utata kumuombea uponyaji kama ilivyobainika awali.

Muhando anaamini kuwa alifungwa macho kuingia katika kanisa hilo kwani alipoteza fahamu kipindi kizima cha maombi.

Rose pia alitambua kwamba Ng’ang’a alimpigia simu baada ya kufahamu alikuwa mgonjwa na akajitolea kumuombea.

Msanii huyo ambaye alikumbana na maumivu makali tumboni alikubali ombi la pasta huyo na kutembelea kanisa lake.

“Pasta Ng’ang’a alinialika katika kanisa lake na niliwasili mapema siku moja. Wakati wa kukombolewa, nilikuwa na maumivu makali tumboni na aliniambia ataniombea. Nilizirai baada ya kusikia maneno yake matatu na hadi leo, siwezi nikaelezea kile kilitokea," alisema Rose.

Muhando, kisha alikiri kwamba wanawe wana baba tofauti na wanaendelea vyema popote walipo na pia wanaume walikuwa wamezoea kumwacha baada ya kujifungua.

“Watoto wangu wote wako shuleni. Wote wana baba tofauti kwa sababu wote waliniacha wakati nilikuwa na mimba ama wakati mtoto alikuwa mchanga," alifunguka Rose.

Credit: Tuko Kenya


Share:

Non-Executive Director at Vodacom

Description Providing effective leadership in collaboration with the management team; Facilitating setting up of appropriate corporate governance structures for the management of the company’s operations; Establishing board committees, policies and procedures that shall facilitate the most effective discharge of the Board’s roles and responsibilities; Reviewing and approve Vodacom’s annual budget proposed by the management team; Selecting, monitoring, evaluating,… Read More »

The post Non-Executive Director at Vodacom appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Job at Geita Gold Mining, Public Relations and Communications Manager

Public Relations and Communications Manager   Geita Gold Mining Ltd (GGML) is Tanzania’s leading gold producer with a single operation in Geita Region. The company is a subsidiary of AngloGold Ashanti, an international gold producer headquartered in South Africa, with operations in more than ten countries, in four continents. The mine is situated in the Lake Victoria Gold fields… Read More »

The post Job at Geita Gold Mining, Public Relations and Communications Manager appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Rais wa Iran azihimiza nchi za kikanda kuvifukuza vikosi vya Marekani

Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema nchi za kanda ya Mashariki ya Kati zinapaswa kuvifukuza vikosi vya jeshi la Marekani kutoka kwenye kanda hiyo.

Rais huyo ameyasema hayo alipokutana na waziri mkuu wa Syria Bw. Imad Khamis ambaye yupo ziarani nchini Iran. 

Amesema nchi za kanda hiyo zinapaswa kujitahidi kumaliza uwepo wa vikosi vya Marekani, na kuwafukuza wakaliaji kutoka kanda hiyo.

Bw. Khamis amesema uwepo wa vikosi vya Marekani nchini Syria ni mfano mzuri wa ukaliaji, na nchi za kanda hiyo zinapaswa kujitokeza kupinga uwepo haramu wa vikosi vya Marekani katika kanda hiyo.


Share:

Picha : WADAU WA MAJI MKOA WA TABORA WATEMBELEA CHANZO CHA MRADI WA MAJI YA ZIWA VICTORIA


Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Wadau wa Maji mkoa wa Tabora wamefanya ziara kwenye chanzo cha mradi mkubwa wa maji ya Ziwa Victoria cha Ihelele wilayani Misungwi mkoani Mwanza ili kujionea na kujifunza namna Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira katika mji wa Kahama na Shinyanga( Kahama Shinyanga Water Supply and Sanitation Authority( KASHWASA) inavyozalisha na kusambaza maji katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.

Wadau hao wa maji wakiwemo viongozi wa serikali ya mkoa na wilaya,madiwani,viongozi wa vyama vya siasa na dini na wananchi wa Tabora wametembelea chanzo cha mradi wa maji ya ziwa Victoria Jumanne Januari 14,2020.

Wakiwa Ihelele wadau wa maji wameshuhudia jinsi maji yanavyotolewa katika Ziwa Victoria,yanavyotibiwa, yanavyochujwa na kusukumwa kwenda kwenye Tenki kubwa la maji lenye ujazo wa lita Milioni 35 za maji lililopo kwenye mlima Mabale wenye urefu wa mita 400 ambapo pia wametembelea tenki hilo.

Akitoa taarifa ya Mradi huo,Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa alisema lengo la kuanzishwa kwa mradi huo mwaka 2009 ukigharimu shilingi Bilioni 251 za mapato ya ndani ya nchi ilikuwa ni kutatua changamoto ya maji katika mji wa Shinyanga na Kahama na sasa wanaendelea kusambaza maji katika maeneo mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Tabora.

Alisema hivi sasa wanahudumia wateja saba ambao ni Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA), Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (KUWASA),Ngudu,Kishapu,Maganzo,Mgodi wa Mwadui na kusambaza maji katika kamati 64 maji Misungwi na Kwimba na kamati za wateja wadogo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Kahama Mji na Msalala.

Mhandisi Mgeyekwa alisema hivi sasa wanaendelea na ujenzi wa mradi wa Maji katika Mkoa wa Tabora ambao hadi kukamilika kwake utagharimu zaidi ya Bilioni 600 na tayari maji yamefika katika tenki la maji Ushirika Nzega lenye ujazo wa lita  milioni 2.5,Kilichobaki ni kuyaweka katika mfumo wa usambazaji.

Alisema miradi inayoendelea kujengwa itafikisha uzalishaji maji hadi lita milioni 64 ifikapo Juni,2025.

"KASHWASA haipati ruzuku kutoka serikalini lakini serikali inawekeza kwenye miradi mikubwa ya maji",alisema.

“Mapato yetu kwa mwezi ni shilingi Bilioni 1.1 ambapo asilimia 60 inakwenda kwenye gharama za umeme na dawa,asilimia 40 inayobaki inakwenda kwenye mishahara ya watumishi wetu na mambo mengine”,alisema Mhandisi Mgeyekwa.

Alisema kutokana na hali hiyo sasa KASHWASA inajitegemea kwa asilimia 100 kwa upande wa gharama za umeme na madawa ya kutibu maji na mishahara ya watumishi hivyo inapata ruzuku kutoka serikalini asilimia 20 tu.

“Changamoto iliyopo ni wateja kutotumia maji. Uwezo wa mtambo wetu ni kuzalisha lita milioni 80 kwa siku lakini kwa mahitahi ya sasa tunazalisha lita milioni 43 tu kwa siku.Tunahitaji wateja wengi zaidi ili watumie maji tunayozalisha”,aliongeza Mhandisi Mgeyekwa.

Akizungumza katika ziara hiyo, Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Tabora , Rukia Manduta alisema wamepokea kwa furaha mradi wa maji ya Ziwa Victoria akibainisha kuwa watakuwa wateja wazuri wa KASHWASA.

Manduta alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi wa Tabora kuwa walipaji wazuri wa Ankara za maji,kuwa walinzi wa miundo mbinu ya maji ili kuepuka upotevu wa maji.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Igunga,John Mwaipopo aliipongeza serikali kwa kutekeleza mradi wa maji ya Ziwa Victoria na kuwataka wananchi kuyalinda na kuyatunza maji hayo pindi yatakapofika mkoani Tabora ili kuondokana na changamoto ya maji ambayo imekuwa ikiwakabili kwa muda mrefu.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira katika mji wa Kahama na Shinyanga (Kahama Shinyanga Water Supply and Sanitation Authority( KASHWASA) Mhandisi Joshua Mgeyekwa akiwakaribisha wadau wa maji kutoka mkoa wa Tabora walipotembelea chanzo cha mradi mkubwa wa maji ya Ziwa Victoria cha Ihelele wilayani Misungwi mkoani Mwanza Januari 14,2020. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa akiwaelezea wadau wa maji kutoka Tabora kuhusu Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria unaosimamiwa na KASHWASA.
Wadau wa maji kutoka mkoa wa Tabora wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa wakati akitoa taarifa ya Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria.
Wadau wa maji kutoka mkoa wa Tabora wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa wakati akitoa taarifa ya Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria.
Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa akiwaelezea wadau wa maji kutoka Tabora kuhusu Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria unaosimamiwa na KASHWASA.
Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Tabora , Rukia Manduta aliyeongoza msafara wa wadau wa maji kutoka mkoa wa Tabora akizungumza wakati wa ziara yao kutembelea hanzo cha mradi mkubwa wa maji ya Ziwa Victoria cha Ihelele wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
Mkuu wa wilaya ya Igunga, John Mwaipopo akizungumza wakati wa ziara yao kutembelea hanzo cha mradi mkubwa wa maji ya Ziwa Victoria cha Ihelele wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa (mwenye suti nyeusi) akiwaongoza wadau wa maji kutoka mkoa wa Tabora kuelekea katika Ziwa Victoria.
Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa (mwenye suti nyeusi) akiwaongoza wadau wa maji kutoka mkoa wa Tabora  wakiwa katika eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya kuchukua maji ya Ziwa Victoria kupitia mfereji uliojengwa kitaalamu.
Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa (mwenye suti nyeusi) akiwa na wadau wa maji kutoka Tabora katika Ziwa Victoria.
Wadau wa maji kutoka mkoa wa Tabora wakiondoka katika Ziwa Victoria.
Meneja Ufundi wa KASHWASA,Mhandisi Laurence Deus Wasala akielezea namna wanavyochukua maji katika ziwa Victoria kisha kuyaingiza katika jengo lililopo karibu na Ziwa Victoria lenye mitambo ya kusukuma maji kutoka Ziwani na kuyapeleka katika kituo cha Kutibu Maji.
Wadau wa maji wakiwa ndani ya jengo lenye mitambo ya kusuma maji kutoka Ziwa Victoria wakiangalia mitambo hiyo (haionekani,angalia hapa chini).
Sehemu ya mitambo ya kusuma maji kutoka Ziwa Victoria iliyopo katika jengo lililopo karibu na Ziwa Victoria.
Hapa ni katika kituo cha kutibu maji cha Ihelele: Kulia ni Meneja Ufundi wa KASHWASA,Mhandisi Laurence Deus Wasala akielezea namna wanavyotibu maji ya Ziwa Victoria.
Wadau wa maji kutoka Tabora wakiwa juu ya mitambo inayotumika kutibu maji ghafi yanayotoka katika Ziwa Victoria.
Wadau wa maji kutoka Tabora wakiwa juu ya mitambo inayotumika kutibu maji ghafi yanayotoka katika Ziwa Victoria.
Wadau wa maji kutoka Tabora wakiangalia namna maji ghafi kutoka Ziwa Victoria yanavyotibiwa katika kituo cha kutibu maji cha Ihelele.
Wadau wa maji kutoka Tabora wakiangalia mitambo inayochuja maji ya Ziwa Victoria.
Wadau wa maji kutoka Tabora wakiangalia mitambo inayochuja maji ya Ziwa Victoria.
Wadau wa maji kutoka Tabora wakiangalia mitambo inayochuja maji ya Ziwa Victoria.
Wadau wa maji kutoka Tabora wakiangalia jinsi maji ya Ziwa Victoria yanavyochujwa ili yawe tayari kutumiwa.
Wadau wa maji kutoka Tabora wakiangalia jinsi maji ya Ziwa Victoria yanavyochujwa  kwa kutumia mitambo ya kisasa.
Wadau wa maji kutoka Tabora wakiendelea kutembelea mitambo ya KASHWASA.
Meneja Ufundi wa KASHWASA,Mhandisi Laurence Deus Wasala  akionesha chumba chenye gesi ya kuua vimelea vilivyopo katika maji.
Wadau wa maji wakiendelea kupata elimu jinsi mitambo ya KASHWASA inavyofanya kazi.
Wadau wa maji wakiangalia mitambo inayosukuma maji kutoka kituo cha kutibu maji cha Ihelele kwenda Mlima Mabale ambapo kuna kuna tenki kubwa la maji ambayo husambazwa kwenda kwenye maeneo mbalimbali nchini. 
Wadau wa maji wakiangalia mitambo inayosukuma maji kutoka kituo cha kutibu maji cha Ihelele kwenda Mlima Mabale.
Meneja Ufundi wa KASHWASA,Mhandisi Laurence Deus Wasala akielezea namna maji yanavyosukumwa kwenda katika Mlima Mabale ambapo kuna tenki kubwa la maji.
Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Tabora , Rukia Manduta (katikati) na Mkuu wa wilaya ya Igunga, John Mwaipopo (kulia) wakifurahia jambo wakati wakiendelea kutembelea kituo cha Kutibu maji cha Ihelele. Kushoto ni kurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa.
Wadau wa maji kutoka mkoa wa Tabora wakipiga picha ya pamoja katika kituo cha Kutibu Maji cha Ihelele. Nyuma ni maji yakiruka juu.
Wadau wa maji kutoka mkoa wa Tabora wakipiga picha ya pamoja katika kituo cha Kutibu Maji cha Ihelele.

Wadau wa maji kutoka mkoa wa Tabora wakipiga picha ya pamoja katika kituo cha Kutibu Maji cha Ihelele.
Muonekano wa  mlima Mabale wenye urefu wa mita 400 ambapo kuna tenki kubwa la maji lenye ujazo wa lita Milioni 35 za maji yanayosukumwa na mitambo kutoka katika kituo cha Kutibu Maji cha Ihelele.

Maandishi katika tenki kubwa la maji lenye ujazo wa lita Milioni 35 za maji lililopo katika Mlima Mabale.


Wadau wa maji waliofanikiwa kupanda juu ya tenki kubwa lenye ujazo wa lita Milioni 35 za maji lililopo katika Mlima Mabale wakipiga picha ya kumbukumbu.

Wadau wa maji waliofanikiwa kupanda juu ya tenki kubwa lenye ujazo wa lita Milioni 35 za maji lililopo katika Mlima Mabale wakipiga picha ya kumbukumbu.
Wadau wa maji wakiwa katika Mlima Mabale palipojengwa tenki kubwa la maji baada ya kutembelea tenki hilo.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

Job at Geita Gold Mining Ltd (GGM) Community Engagement Superintendent

Community Engagement Superintendent   Geita Gold Mining Ltd (GGML) is Tanzania’s leading gold producer with a single operation in Geita Region. The company is a subsidiary of AngloGold Ashanti, an international gold producer headquartered in South Africa, with operations in more than ten countries, in four continents. The mine is situated in the Lake Victoria Gold fields of North… Read More »

The post Job at Geita Gold Mining Ltd (GGM) Community Engagement Superintendent appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Jeshi la Sudani Lazima Jaribio la Mapinduzi

Jeshi la Sudan linayashikilia makao makuu ya kikosi cha usalama wa taifa cha nchi hiyo ambacho awali kilikuwa kitiifu kwa rais aliyepinduliwa Omar al-Bashir, ripoti zinaeleza.

Mapambano yalianza Jumanne katika jiji la Khartoum ambapo milio ya milipuko ilisikika. Kitengo hicho cha usalama wa taofa kwa sasa kinavunjwa.

Serikali inaadai kuwa uasi huo umechochewa na malipo ya mafao, lakini pia kuna mashaka juu ya tukio hilo kulenga kuchelewesha mabadiliko ya kisiasa nchini humo.

Kiongozi mwandamizi wa baraza huru linaloongoza Sudan kwa sasa, Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo, amemtuhumu mkuu wa zamani wa usalama wa taifa Salah Gosh kuwa yupo nyuma ya uasi huo.


Share:

Job at Geita Gold Mining, Senior Manager Community Affairs & Projects

Senior Manager Community Affairs & Projects   Geita Gold Mining Ltd (GGML) is Tanzania’s leading gold producer with a single operation in Geita Region. The company is a subsidiary of AngloGold Ashanti, an international gold producer headquartered in South Africa, with operations in more than ten countries, in four continents. The mine is situated in the Lake Victoria Gold… Read More »

The post Job at Geita Gold Mining, Senior Manager Community Affairs & Projects appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Waziri Mkuu Amwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Uapisho Wa Rais Wa Msumbiji, Filipe Nyusi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, wakati akiondoka nchini, katika uwanja wa Julius Nyerere, kuelekea Msumbiji kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli, kwenye uapisho wa Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi. Januari 14, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Share:

Job at German Embassy, Field of Politics and Translator

Job Opportunity at German Embassy, Jobs in Field of Politics and Translator Jobs in field of politics and translator TRANSLATED JOB ADVERT: The embassy of the Federal Republic of Germany in Dar es Salaam is looking for the earliest possible time an employee in the field of politics and translator The activity includes the following tasks: All kinds… Read More »

The post Job at German Embassy, Field of Politics and Translator appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Stores Assistant at Diageo

Job Opportunity at Diageo, Stores Assistant Stores Assistant   Job Description : Scope: The role holder will be responsible for serving the engineering and utilities section at the Dar es Salaam plant catering for all engineering spares and fuel needs. Purpose of Role: The role is meant to cater for all needs of the utilities/engineering services at the Dar… Read More »

The post Stores Assistant at Diageo appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Human Resources Intern at UNDP

Job Opportunity at UNDP, Human Resources Intern Human Resources Intern  Background The Human Resources Unit is part of the Operations section of the United Nations Development Programme Tanzania country office. The HR unit provides human resource and development services to UNDP and to the rest of the UN country team through implementation of the business operations strategy or… Read More »

The post Human Resources Intern at UNDP appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Job at UNDP, Monitoring And Eval Analyst

Job Opportunity at UNDP, Monitoring And Eval Analyst Monitoring And Eval Analyst  Background With the 2030 Agenda for Sustainable Development at its core, and in response to the General Assembly resolution 71/243 on the quadrennial comprehensive policy review of operational activities for development of the United Nations system, the UN Secretary General’s report (December 2017) “Repositioning the United… Read More »

The post Job at UNDP, Monitoring And Eval Analyst appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger