Sunday, 12 January 2020

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya January 12















Share:

Saturday, 11 January 2020

QUEEN ELIZABETH COMMONWEALTH SCHOLASHIPS (QECS) TENABLE IN THE HOSTING UNIVERSITIES FOR QECS 2020

1.0 Call for Application The General public is hereby informed that, the Government of the United Kingdom has opened the new Queen Elizabeth Commonwealth Scholarships (QECS) to eligible Tanzanians to pursue Masters Studies in the hosting Universities for QECS in the academic year 2020-2021. Interested candidates are highly encouraged to apply under the Association of Commonwealth Universities. 2.0… Read More »

The post QUEEN ELIZABETH COMMONWEALTH SCHOLASHIPS (QECS) TENABLE IN THE HOSTING UNIVERSITIES FOR QECS 2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

RAS SHINYANGA AWATAKA VIONGOZI NA WATENDAJI KUZINGATIA UADILIFU


Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bw. Albert Msovela amewataka viongozi na watendaji kuzingatia suala la uadilifu katika utendaji wa shughuli za Umma ili kuepukana na madhara yanayotokana na mgongano wa maslahi.

Akifungua mafunzo ya sheria ya maadili ya utendaji katika utumishi wa Umma na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi kwa Viongozi na Watendaji wa Mkoa wa Shinyanga, yaliyofanyika jana tarehe 10/01/2020 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Msovela amesema kuwa, ana imani kubwa baada ya mafunzo hayo yenye lengo la kukumbushana kuzingatia Sheria, taratibu na kanuni, washiriki watasimamia vema kwenye maeneo yao ya kazi.

"Hivyo mafunzo haya yanasisitiza katika kutekeleza majukumu yetu kusimamia sheria za Nchi, haki na utu ili kumsaidia mhe. Rais katika kutekeleza majukumu yake na hatimaye kutoa huduma bora kwa jamii" amesema Msovela.

Amesema kuwa tofauti na miaka ya nyuma, suala la mgongano wa maslahi limepungua kwa kiasi kikubwa.

Ameipongeza pia Sekretarieti ya maadili kwa Viongozi wa Umma chini ya Kamishna Jaji mstaafu Nsekela kwa kuendesha mafunzo haya ili kujenga uelewa kwa viongozi hasa katika Mkoa wa Shinyanga tangu mwezi Juni, 2019 kwa njia mbalimbali.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulamhafidh Mukadam aliyeshiriki pia mafunzo hayo amesema mafunzo yanawakumbusha na kuwakosoa pale walipokwenda kinyume na kumshukuru Rais Magufuli kwa utendaji wake ambapo amesema kuwa ni kweli nchi imebadilika sana. 

Mmoja wa washiriki Bw. Nila Mabula ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa ndani katika Sekretarieti ya Mkoa, akitoa neno la shukrani baada ya mafunzo, amesema kuwa wanaishukuru sana Sekretarieti kwa mafunzo hayo na kuwasihi washiriki kuyazingatia na kuyashusha kwa watumishi wa chini ili kufikia lengo. Akiongeza kuwa, faida yake ni kuongeza ufanisi katika kazi kwenye nyanja zote.

"Kanuni tulizotajiwa zimetajwa pia hata kwenye vitabu vya dini, hivyo kuzingatia ni kufuata pia maneno ya Mungu" amesema Bw. Nila.

Viongozi na watendaji mbalimbali ngazi ya Mkoa wameshiriki mafunzo hayo ya siku moja wakiwemo Wakuu wa vyombo vya Usalama, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Makatibu Tawala wa Wilaya, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Idara na Vitengo, watendaji wa Mahakama na Wakuu wa Taasisi za Umma.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bw. Albert Msovela akifungua mafunzo hayo
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mafunzo hayo katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mafunzo hayo katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mafunzo hayo katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Picha ya pamoja na baadhi ya washiriki
Share:

Naibu Waziri Mabula Akabidhi Hati Mia Moja Za Kimila Kwa Wakulima Wadogo Kijiji Cha Litoa Ruvuma

Na Munir Shemweta, WANMM SONGEA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amekabidhi hati mia moja za Kimila kwa wakulima wadogo wa kijiji cha Litoa kilichopo katika jimbo la Peramiho wilaya ya Songea Vijijini mkoani Ruvuma na kuwataka wamiliki wake kuzitunza na kuzitumia hati hizo kujiletea maendeleo.

Akizungumza wakati wa kuwakabidhi hati hizo katika kijiji cha Litoa wilaya ya Songea vijijini akiwa kwenye shughuli za kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi na miradi ya ujenzi ya Shirika la Nyumba la Taifa katika mikoa ya kusini jana, Naibu Waziri Mabula aliwataka wakulima waliokabidhiwa hati kutouza ardhi zao kwa nia ya kupata fedha za haraka.

‘’Mmepiwa msikimbilie kuuza ardhi bila kufuata taratibu kwa tamaa ya kupata fedha za haraka maana mkiuza mnaweza kupunjwa fedha’’ alisema Dkt Mabula.

Aidha, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amezitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha zinaandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi kwenye vijiji ili kuwa na salama za miliki za ardhi zilizoainisha maeneo ya shule, soko, maeneo ya kuabudia, viwanja vya michezo pamoja na maeneo ya uwekezaji.

Dkt Mabula alizitaka pia halmashauri kuandaa maeneo ya uwekezaji sambamba na kuhaulisha maeneo ili kuwa rahisi kwa Mwekezaji atakayekuja kuwekeza katika sekta mbalimbali na kusisitiza kuwa ili kuwaendeleza wananchi kiuchumi ni lazima ardhi ipimwe na kufanyiwa mpango wa matumizi bora ya ardhi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Vijijini Pololeti Mgema aliupongeza Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) kwa juhudi kubwa iliyofanya kufanikisha wakulima wadogo kupata hati miliki za kimila na kubainisha kuwa wilaya yake imejifunza bila kushirikisha wadau zoezi la kuwapatia hati wakulima wadogo lingechukua muda mrefu.

 Naye Mratibu wa MVIWATA katika mkoa wa Ruvuma Laila Haji alisema Asasi yake iliona umuhimu wa wakulima wadogo kuwa na salama za miliki za mashamba yao na ndiyo maana ikafanya juhudi kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya ya Songea ili kuwapatia hati wakulima wa kijiji cha Litoa.

Hata hivyo, alisema changamoto kubwa iliyopo kwa wakulima na wananchi kwa ujumla katika suala la hati miliki za ardhi ni elimu ndogo kuhusiana na masuala hati za ardhi, mfumo dume kwa wanawake kumiliki ardhi pamoja na migogoro ya wakulima na wafugaji.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alitembelea mradi wa ujenzi wa Ofisi na nyumba za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) uliopo Mpepo wilayani Nyasa mkoa wa Ruvuma. Mradi huo pamoja na miradi mingine ya ujenzi wa nyumba na ofisi za TFS katika maeneo mbalimbali nchini unajengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).


Share:

Afisa Biashara Wilaya Ya Ikungi Asimamishwa Kazi Kwa Tuhuma Za Kutafuna Fedha Za Wamachinga

Na Happiness Shayo, Ikungi-Singida.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) amemsimamisha kazi Afisa Biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Paulo Makaka kupisha uchunguzi wa tuhuma za kutumia fedha za wamachinga kwa maslahi
binafsi.

Dkt. Mwanjelwa amechukua hatua hiyo leo wakati wa kikao kazi kati yake na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo.

“Ninaagiza Afisa Biashara huyu asimamishwe kazi wakati taratibu nyingine za kiutumishi zinaendelea na ninatoa mwezi mmoja kwa Kamanda wa TAKUKURU kufanya uchunguzi na kuwasilisha majibu” Dkt. Mwanjelwa
amesisitiza.

Amefafanua kuwa Afisa Biashara huyo amekusanya fedha za vitambulisho zaidi ya 500 vya wamachinga pamoja na ushuru wao bila kuziwasilisha sehemu inayohusika.

Pia, Afisa Biashara huyo amekuwa akitumia muda wa kazi vibaya kwa kuchelewa kuripoti kazini ambapo ni kinyume na taratibu za kiutumishi.

Dkt. Mwanjelwa amesikitishwa na watendaji wa halmashauri hiyo wanaolalamikia ukosefu wa mapato wakati Afisa Biashara huyo amekuwa akitumia makusanyo ya serikali kwa matumizi binafsi.

Aidha, Dkt. Mwanjelwa amewaasa watumishi wengine kuacha kukiuka misingi ya kanuni na taratibu za kiutendaji kwa kuwa serikali haitawaacha salama wote watakaogungulika kukiuka misingi hiyo.

Katika hatua nyingine, Dkt. Mwanjelwa ametoa onyo kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wanaoishi nje ya kituo cha kazi na kuwataka kuhamia haraka iwezekanavyo katika eneo lao la kazi ili waweze
kutoa huduma bora kwa wananchi.

“Ni marufuku kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kuishi nje ya kituo cha kazi kwa kuwa hili linapunguza ufanisi wa kazi na huduma kwa wananchi hazitolewi ipasavyo kutokana na kuishi mbali” Dkt.
Mwanjelwa amesema.

Mhe.Dkt. Mwanjelwa amehitimisha ziara yake ya kikazi Mkoani Singida ambapo alitembelea Manispaa ya Singida na Halmashauri za Wilaya ya Singida, Mkalama, Iramba na Ikungi. Lengo la ziara hiyo ni kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF pamoja na kuzungumza na watumishi,
kusikiliza kero zao na kuzitatua.


Share:

Form one joining instructions for boarding schools in Tanzania (All Regions) 2019/2020

Form one joining instructions for boarding schools in Tanzania (All Regions) Tamisemi: The list of joining instruction for all boarding school in Tanzania , You can now access them through LINKS provided below: Arusha Ilboru sec.pdf Dodoma Mpwapwa sec.pdf Msalato sec.pd Dar es Salaam pugu sec.pdf Iringa Ifunda Tech.pdf Malangali sec.pdf Iringa Girls.pdf Kilimanjaro Moshi sec.pdf Moshi Tech.pdf… Read More »

The post Form one joining instructions for boarding schools in Tanzania (All Regions) 2019/2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Marekani yatangza vikwazo vipya dhidi ya Iran

Utawala wa rais Donald Trump wa Marekani umetangaza awamu mpya ya vikwazo vya kiuchumi kwa Iran kufuatia mashambulizi ya makombora yaliyofanywa na Tehran kwenye kambi za jeshi la Marekani nchini Iraq. 

Siku ya Ijumaa, Wizara ya Fedha ya Marekani ilitangaza kuwawekea vikwazo maafisa 8 wa ngazi za juu wa Iran akiwemo Mohsen Rezai, Katibu wa Baraza la Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu, Ali Shamkhani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran na Mohammad Reza Naqdi Mratibu katika Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC). 

Kwa mujibu wa vikwazo hivyo wakuu hao wa Iran hawataweza kuingia Marekani na iwapo wana mali zozote Marekani basi zitazuiwa. 

Aidha taarifa ya Wizara ya Fedha ya Marekani mbali na kuwawekea vikwazo maafisa hao wa Iran pia imetangaza vikwazo dhidi ya mashirika 18 ya Iran ambayo yanashughulika katika sekta za chuma na madini na hali kadhalika mashirika matatu yaliyoko nchini China ambayo yanahusika katika kununua chuma kutoka Iran.

Taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema: "Sambamba na kutangazwa vikwazo hivyo, Trump ametia saini amri ambayo itaweka vizingiti katika vyanzo vya fedha zinazotumiwa na Iran katika sekta za ujenzi wa miundo msingi, madini na ufumaji.

Mapema wiki hii Iran ilifanya mashambulizi kwenye kambi nchini Iraq ili kulipa kisasi baada ya Marekani kumuua kamanda wa ngazi ya juu wa jeshi lake, Qassem Soleimani.


Share:

Vikao vya kamati za Bunge kuanza tar 13-24 Jijini Dodoma.




Share:

Usajili wa Nyara zinazomilikiwa na wananchi kwa madhumuni mbalimbali




Share:

AKATWA UUME KWA WEMBE GESTI BAADA YA KUSHINDWA KUMLIPA ELFU 5 MWANAMKE ALIYEFANYA NAYE NGONO

Jeshi la Polisi mkoani Mara linamshikilia mwanamke anayefahamika kwa jina la Marusi Samweli kwa tuhuma za kumjeruhi mpenzi wake kwenye uume kwa kumkata na wembe.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, Daniel Shillah  amethibitisha kutokea kwa tukio hilo usiku wa kuamkia tarehe 10 Januari, 2020 katika nyumba moja ya kulala wageni  ya Gibita iliyopo Mugumu wilayani Serengeti.

Akizungumza kwa shida akiwa chini ya uangalizi wa waganga hospitali ya Nyerere akipata matibabu aliyejulikana kwa jina la Joseph amesema alikatwa na mhudumu wa nyumba hiyo baada ya kushindwa kumlipa Sh15,000 badala ya Sh20,000 walizokubaliana kulipana na kwa kila mshindo mmoja ni Sh5,000 na yeye alipiga nne na kutoa fedha pungufu.

"Kwanza tulianza kwa vinywaji kisha tukakubaliana kila (hatua) Sh5,000 lakini akaomba kwanza Sh20,000 nikalipa, tumelala kila baada ya (hatua) nilikuwa nalipa Sh5,000 mitatu nililipa huu wa nne sikulipa akanidai nikamwambia akate kwenye Sh20,000 ya kwanza akagoma.”

“Tukalala alfajiri wakati naaga niwahi kijijini kwenye kazi za uchimbaji dhahabu, kumbe alikuwa na wembe ghafla akashika sehemu yangu ya siri na kukata kuanzia chini kwenye sehemu ili akate kabisa nikapambana lakini akawa ameishaniumiza vibaya," amesema mwanaume huyo.

Amesema akapiga kelele watu wakajitokeza kumsaidia na kutoa taarifa polisi waliofika na kuwachukua wote na mhudumu huyo.

Mganga mkuu wa hospitali hiyo, Tanu Warioba amesema ataongea baada ya kumaliza kumhudumia majeruhi huyo.

Katika tukio lingine, Juma Waryoba maarufu kama (Kisangura) 27, anatafutwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mkewe kwa kumchoma na kisu mara kadhaa mwilini kwake. 

Kamanda Shillah ameongeza kuwa tukio hilo limetokea wilayani Butiama ambapo mwanaume huyo anatuhumiwa kumuua mke wake kwa kuchoma na kisu na kisha kutoroka kusikojulikana huku chanzo kikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi. 

Kamanda ametoa wito kwa wananchi wa mko wa Mara kuacha kujichukulia sheria mkononi kwani kama kuna migogoro ndani ya familia ni vizuri kuitatua kwa njia ya mazungumzo na sio kutumia nguvu, akisema kufanya hivyo ni kinyume cha sheria ya Jamuuri ya Muungano wa Tanzania.
Share:

Iran Yakiri Kuidungua Kwa Kombora Ndege Ya Ukraine

Iran imekubali kuwa iliidungua kwa kombora Ndege ya Ukraine iliyoua Watu 176  siku ya Jumatano, runinga ya taifa ya Iran imeripoti.

Taarifa ya jeshi inaeleza kuwa mkasa huo umetokana na "makosa ya kibinadamu" baada  ya ndege hiyo kupita karibu na eneo nyeti linalomilikiwa na Kikosi cha Mapinduzi (Revolutionary Guards). Maafisa waliofanya kosa hilo wataadhibiwa, taarifa hiyo imeeleza.

Iran awali ilikanusha vikali taarifa kuwa moja ya makombora yake yaliitungua ndege hiyo karibu na mji mkuu Tehran. Watu wote 176 ndani ya ndege hiyo wamepoteza maisha.

Hata hivyo nchi hiyo ilibanwa zaidi  baada ya Marekani na Canada kudai kuwa taarifa za kijasusi walizonazo zinaonesha kuwa Iran iliidondosha ndege hiyo kwa bahati mbaya na moja ya makombora yake.

Kuanguka kwa ndege hiyo kulitokea saa chache baada ya Iran kushambulia kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq kwa makombora ya masafa marefu.

Vyombo vya habari vya Marekani vinadai kuwa Iran ilidhani kuwa ndege hiyo ilikuwa ya kivita ya Marekani, wakati taifa hilo lilipokuwa ikijiandaa kujibu mashambulio dhidi ya Marekani baada ya wao kushambulia vituo vyake vya kijeshi nchini Iraq kwa makombora.


Share:

SULTANI QABOOS BIN SAID WA OMAN AFARIKI DUNIA


Sultani Qaboos bin Said wa Oman aliyeitawala nchi hiyo kwa karibu nusu karne amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79.

Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Oman, ONA, siku tatu za maombolezo ya kitaifa zimetangazwa kufuatia kuaga dunia mfalme huyo . 

Aidha bendera ya Oman itapepea nusu mlingoti kwa muda wa siku 40 kama heshima kwa kiongozi huyo ambaye anapongezwa na wengi kwa kuleta maendeleo na ufanisi mkubwa katika nchi hiyo ya Kiarabu. 

Kiongozi huyo wa Oman aliyeaga dunia alikuwa anaugua saratani ya utumbo mpana ambayo kwa lugha ya Kiingereza inaitwa 'colon cancer' au 'colorectal cancer'. 

Mwezi Disemba Sultan Qaboos alielekea Ubelgiji kwa ajili ya matibabu na kisha akarejea nyumbani kabla ya kumalizika mwaka 2019. 


 Sultan Qaboos hakuwa na mtoto na wala hakutangaza bayana mrithi wa kiti chake lakini taarifa zinasema alikuwa ameandaa wasia kuhusu mrithi wake na akaukabidhi kwa Baraza la Ufalme.

Kwa mujibu wa katiba ya Oman, baada ya kifo cha Sultani, Baraza la Ufahame linapaswa kutangaza mrithi wake baada ya siku tatu. Baraza Kuu la Kijeshi la Oman tayari limeshaitisha kikao na kuitaka familia ya Sultan Qaboos itangaze mrithi wa kiti chake.

Sultan Qaboos alichukua hatamu za uongozi Julai 23 mwaka 1970 na anapongezwa kwa kufuata sera za kigeni zenye mlingano na hivyo kuiepusha Oman na migogoro. 



Share:

Marufuku Taasisi Za Umma Kujenga Mifumo Ya Fedha Bila Ridhaa Ya Wizara Ya Fedha Na Mipango Na eGA

Na. Peter Haule na Farida Ramadhani, WFM, Dodoma
Selikali imezipiga marufuku taasisi zote za Umma nchini kujenga mifumo ya fedha ya kieletroniki bila ridhaa ya   Wizara ya Fedha na Mipango na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA).

Agizo hilo limetolewa Jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, wakati akizundua Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki (GePG) toleo la simu za mkononi (GePG App), hafla iliyowakutanisha Wizara ya Fedha na Mipango na Idara, Wakala, Taasisi, Bodi, Mashirika ya Umma yaliyo katika Kanda ya Kati.

Bw. James alisema kuwa Taasisi zote za Umma nchini zinatakiwa kutekeleza matakwa ya Waraka namba tano (5) wa Hazina unaozitaka taasisi zote kuhakikisha zinapata ridhaa ya Wizara ya Fedha na Mipango na Wakala wa Serikali Mtandao (eGA) kabla ya kufanya ununuzi, uandaaji, usimikaji na utumiaji wa Mfumo wowote wa kielektroniki wa usimamizi wa Fedha za Umma.

“Imebainika kuwa kuna baadhi ya taasisi za umma ambazo zinakiuka maelekezo hayo ya Serikali kwa sababu wanazozijua wao, nitumie fursa hii kutoa onyo kwa taasisi hizo kutoendelea na vitendo hivyo kwa sababu ni ukiukwaji wa maelekezo”, alisema Bw. James.

Akizungumzia kuhusu GePG App, Bw. James alisema kuwa, uboreshaji wa Mifumo ya Kielektroniki inayoandaa Ankara itawezesha kukusanya fedha kwa wakati na kutoa huduma bora kwa Umma.

“Baadhi ya faida za Matumizi ya Mfumo huo ni kuongezeka kwa uwazi na udhibiti katika ukusanyaji wa fedha za umma, kupata taarifa sahihi na kwa wakati zinazohusu makusanyo na kuwa na viwango na utaratibu unaofanana katika ukusanyaji wa fedha za umma kwa taasisi zote za umma”, alisema Bw. James.

Alisema faida nyingine ni pamoja na kuchochea ubunifu katika ukusanyaji wa pesa za Serikali na sekta ya fedha kwa ujumla kwa kuweka mazingira rafiki na ya usawa kwa wakusanyaji, kutoa huduma bora na rahisi ya malipo ya fedha za umma hivyo kuchochea ongezeko la makusanyo na kufika haraka katika akaunti kuu za makusanyo za taasisi.

“Kwa kutofanya usuluhishi wa miamala kwa wakati kunaweza kusababisha upotevu wa fedha nyingi za Umma na pia kuwa na taarifa za fedha zisizo sahihi, hivyo nawaagiza nyote kuhakikisha mnafanya usuluhishi wa miamala inayopitia Mfumo wa GePG kwa usahihi na kwa wakati, na kufanyia kazi kwa wakati changamoto mbalimbali zitokanazo na matokeo ya usuluhishi wa Miamala husika”, alisisitiza Bw. James.

Aidha alimpongeza Mkurugenzi wa Mifumo ya Usimamizi wa Fedha wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Sausi pamoja na timu yake ya wataalam wabobezi kwa kutengeneza Mfumo wa Kieletroniki wa Kukusanya Mapato ya Serikali (GePG) sambamba na toleo la simu za mkononi (GePG App) ambao umerahisisha ukusanyaji wa mapato ya Serikali pamoja na kuwawezesha wadau kupata huduma kwa wakati.

Aliahidi kuwa Wizara yake itaendelea kuiwezesha Idara hiyo ili iweze kutekeleza majukumu yake ya kubuni mifumo kama hiyo kwa faida ya Serikali na wananchi kwa ujumla.

Aidha, Bw. James ambaye pia ndiye Mlipaji Mkuu wa Serikali, alisema kuwa Wizara kupitia Idara ya Mifumo ya Usimamizi wa Fedha inaandaa mfumo mwingine utakaotumika kwa ajili ya matumizi ya Serikali ujulikanao kwa kifupi kama MUCE.

“Mfumo huu umeshaanza kufanyiwa majaribio kwenye taasisi chache za umma na baadae utasambazwa kwenye taasisi zote na kwamba Mfumo huu utakuwa mwarobaini wa matumizi yasiyo sahihi ya fedha za Umma”, aliongeza Bw. James.

Alisema Mfumo huo utakuwa suluhisho la matumizi yasiyofaa ya umma na kuongeza kuwa watendaji wengi Serikalini hawataufurahia mfumo huo lakini hilo haliihusu Serikali. Watajua wenyewe! Alisema huku washiriki wakiangua kicheko ukumbini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mifumo ya Fedha, wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Sausi, alisema kuwa kabla ya kuwa na Mfumo wa Malipo kwa njia ya Kielektroniki (GePG) ilikua inafanyika miamala 10 kwa siku na baada ya mfumo huo inafanyika miamala milioni moja kwa siku.

Alisema kuwa miongoni mwa mafanikio ni kuongezeka kwa Taasisi zinazotumia Mfumo wa GePG,  kutoka taasisi 300  muda mfupi uliopita hadi kufikia taasisi 620 hivi sasa.

Bw. Sausi alisema kuwa Mfumo wa GePG kwa njia ya mtandao wa simu za mkononi uliozinduliwa utasaidia watumiaji kupata huduma mbalimbali kama vile kununua umeme, kulipia Ankara mbalimbali zikiwemo za makosa ya usalama barabarani, maji na nyingine nyingi ndani ya sekunde 30.

Ametoa wito kwa wananchi wanaotumia simu janja (android au IPA App) kupakua application hiyo kupitia play store au App Store na kutafuta neno GePG Tanzania tayari kwa matumizi yao ambayo amesema wananchi watafurahia huduma hiyo.

Naye Mwakilishi wa Benki katika Mkutano huo, Bi Domina Tarimo na Mwakilishi wa kampuni za Simu, Bw. Alafat Ibrahim, walisema kuwa Mfumo wa GePG umezisaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha kazi zao, na kuboresha huduma kwa wateja wao na wameipongeza Wizara ya Fedha na Mipango na Serikali kwa ujumla kwa jitihada zake za kuhakikisha kuna mifumo imara ya fedha inayoongeza uwazi na uwajibikaji.


Share:

Viwanja Vizuri ! Tulivu Kwa Makazi Vinauzwa Bei Nafuu Kabisa

VIWANJA VIZURI ! TULIVU KWA MAKAZI NA BEI NAFUU KABISA !Viwanja vipo km 2 kutoka baharini ,unaingilia Mapinga au Kerege mahakamani, ardhi yake  ni level na upepo wa beach unafika

 20/20 Tsh mil 3.6,   20/30 Tsh mil 5.5 ,   20/40 Tsh mil 7.2.Pia vipo vya mpakani na Bunju km 2 kutoka Bagamoyo road jirani na Hotel nzuri ya Kimere Resort .

Umeme,maji vipo jiran ,20/20 Tsh mil 5,  20/30  Tsh mil 7 , 20/40 Tsh mil 10.Pia kwa mahitaji ya eneo zuri la shamba kwa kufuga au hata kuishi  utapata.

KARIBU SANA ! Piga 0677705808 kwa maelezo zaidi


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi January 11


















Share:

Friday, 10 January 2020

JAMBO YATAMBULISHA BIDHAA TATU MPYA “JAWIZA APPLE CRUSH SODA, JAMUKAYA JUISI YA UKWAJU NA UBUYU”

Jawiza Apple Crush  Soda
Jamukaya Ubuyu Juice
Jamukaya Ukwaju Juice

Na Moshi Ndugulile - Shinyanga 
Kampuni ya Jambo Food Products Limited iliyopo Mkoani Shinyanga imezindua bidhaa mpya ya Jawiza Apple Crush Soda,Juisi ya Ukwaju na Ubuyu zenye ujazo wa mili lita 300 ambazo zinapatikana kwa bei ya reja reja shilingi 500/= bei ambayo ni ya kizalendo kwa kila Mtanzania kwenye kipato cha kawaida. 

Bidhaa hizo tatu zenye ubora wa kimataifa zilizotengenezwa kwa ubora wa hali ya juu kwa kutumia teknolojia ya kisasa yenye mitambo kutoka Ujerumani zimetambulishwa rasmi leo Ijumaa Januari 10,2020. 

Akizungumza wakati wa kutambulisha bidhaa hizo, Meneja masoko wa Kampuni ya Jambo Food Products Innocent Mafuru amesema Bidhaa mpya ya Apple Crush Soda ina ladha ya Apple inayotokana na matunda asili yanayopatikana hapa nchini Tanzania. 

“Jambo Food Products Limited tunayo furaha kuwatangazia wateja wetu nchi Nzima ujio rasmi wa wa bidhaa yetu mpya ya Apple Crush Soda. Apple Crush Soda ni kati ya bidhaa tulizonazo na kila mara tumeona ni vizuri kuwapa wateja wetu kitu kipya kulingana na mahitaji yao. 

Bidhaa ya Apple Crush Soda ina ujazo wa mili lita 300 na inapatikana nch nzima kwenye maduka yote ya jumla na reja reja kwa bei ya kizalendo ya shilingi 500/= pesa ya Kitanzania. Tumeweka bei hii ili kumfanya kila Mtanzania awe na uwezo wa kukata kiu na kuonja ladha tofauti kutoka kwetu”,ameeleza Mafuru. 

Mafuru amesema mbali na kuzindua Apple Crush Soda pia wamezindua bidhaa nyingine mbili za Juisi zenye ladha ya Ukwaju na nyingine yenye ladha ya Ubuyu. 

“Bidhaa za Juisi ya Ukwaju na Ubuyu zote zina ujazo wa mili lita 300 na zinapatikana kwa bei ya reja reja shilingi 500/= bei ambayo ni ya Kizalendo kwa kila Mtanzania mwenye kipato cha kawaida”,ameongeza Mafuru. 

"Ubora wa bidhaa hizi ni wa kimataifa ,mchakato wa utengenezaji wake umechukua miezi nane mpaka kupata ubora huu.Bidhaa hizi ni salama na zina faida mbalimbali kiafya,ikiwemo Vitamini C na virutubisho mbalimbali katika kuupa mwili kinga”,amesema Mafuru. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo food Products Limited Salum Khamis amesema uwekezaji wa biashara zake umezingatia uzalendo kwa Watanzania na kwamba ni fursa kubwa katika utoaji wa ajira hasa kwa wazawa na kwamba kundi la wanawake linapewa kipaumbele zaidi. 

“Jambo Food Products tumeendelea kuwa wazalishaji wa vinywaji baridi vyenye ubora kwa kutumia teknolojia ya kisasa yenye mitambo kutoka Ujerumani na mwaka huu 2020 tumejipanga kuwafikia wateja wetu nchi nzima kwa kuongeza wasambazaji na mawakala nchi nzima ili kusogeza huduma zetu kwa kila Mtanzania”,ameeleza Khamis. 

“Tumekuwepo sokoni kwa muda wa miaka mitatu lakini kwa muda huo tumeweza kuwafikia wateja wengi hususani Kanda ya Ziwa na tunawashukuru wateja wetu kwa kutufanya kuwa chaguo lao namba moja”,amema Khamis. 

Amewaomba wateja wao kuendelea kufurahia bidhaa zao mpya na wajivunie bidhaa zenye ubora wa kimataifa zilizotengenezwa nchini Tanzania kwa bei ya kizalendo.

Share:

Video Mpya : NYUMBU MJANJA - LETA MBEGE


Hii hapa video mpya ya Nyumbu Mjanja  inaitwa Leta mbege. Itazame hapa chini

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger