Friday, 10 January 2020
Vyombo vya habari vya Marekani vyadai makombora ya Iran Yaliitungua Ndege ya Ukraine
Marekani wanaamini Ndege ya Abiria ya Ukraine 'Boeing 737 iliyoanguka Iran na kuua watu 176 ilitunguliwa kwa bahati mbaya na Iran
Maofisa wa Marekani kwa mujibu wa runinga ya CBS wanasema mitambo ya Satellite imenasa makombora mawili ambayo yalirushwa kabla ya Ndege kuanguka yakifuatiwa na mlipuko mkubwa.
Ukraine awali ilisema kuwa inachunguza endapo ndege yake iliangushwa na kombora, jambo ambalo mamlaka za Iran zilikanusha vikali.
Kuanguka kwa ndege hiyo kulitokea saa chache baada ya Iran kushambulia kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq kwa makombora ya masafa marefu.
Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Alhamisi alisema: "nina mashaka" juu ya (kuanguka) kwa ndege. "Inawezekana kuna mtu amefanya kosa kubwa."
Iran imetangaza kutokabidhi kisanduku cheusi cha kuhifadhi taarifa za ndege kwa kampuni ya ndege ya Boeing ama serikali ya Marekani kwa uchunguzi wa ajali hiyo.
Hatua hiyo inatokana na mzozo uliokomaa baina ya Marekani na Iran
Maofisa wa Marekani kwa mujibu wa runinga ya CBS wanasema mitambo ya Satellite imenasa makombora mawili ambayo yalirushwa kabla ya Ndege kuanguka yakifuatiwa na mlipuko mkubwa.
Ukraine awali ilisema kuwa inachunguza endapo ndege yake iliangushwa na kombora, jambo ambalo mamlaka za Iran zilikanusha vikali.
Kuanguka kwa ndege hiyo kulitokea saa chache baada ya Iran kushambulia kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq kwa makombora ya masafa marefu.
Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Alhamisi alisema: "nina mashaka" juu ya (kuanguka) kwa ndege. "Inawezekana kuna mtu amefanya kosa kubwa."
Iran imetangaza kutokabidhi kisanduku cheusi cha kuhifadhi taarifa za ndege kwa kampuni ya ndege ya Boeing ama serikali ya Marekani kwa uchunguzi wa ajali hiyo.
Hatua hiyo inatokana na mzozo uliokomaa baina ya Marekani na Iran
Bandari Ya Dar Es Salaam Yapokea Meli Kubwa Ya Utalii Iliyobeba Watalii 600
MALENGO ya Tanzania kufikisha Watalii Milioni mbili kwa mwaka yameanza kutimia, baada ya Watalii zaidi ya 600 kutoka mataifa mbalimbali duniani kuwasili nchini kwa ajili ya ya kufanya utalii katika maeneo ya jiji la Dar es Salaam na Bagamoyo Mkoani Pwani.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Alhamisi (Januari 9, 2020) Kaimu Meneja wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Joseph Sendwa alisema ujio wa watalii hao utaongeza chachu ya Mapato na kuufanya uchumi wa nchi kuinuka kupitia sekta ya Utalii.
“Ujio wa Meli ya Watalii hapa nchini pamoja na Watalii kutembea katika Jiji letu la Dar es Salaam, watatumia magari hivyo mzunguko wa mapato utakuwa mkubwa ukiachilia mbali na mapato ya uhamiaji pindi wageni wanakiwasili nchini” alisema Sendwa.
Sendwa alisema TTB itaendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya Awamu ya Tano katika kukuza sekta ya utalii nchini ambapo imedhamiria kuweka mazingira rafiki katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuhakikisha kuwa gati na. 1, 2, 4, 5 na 7 katika Bandari ya Dar es Salaam zinapokea idadi kubwa ya watalii kutoka sehemu mbalimbali duniani.
“Meli hii ya watalii imetia nanga hapa kwenye Gati jipya kabisa, kwetu sisi ni fahari na tunajivunia sana kwa hili, hivyo mataraijio yetu hapo baadaye zije meli kama hizi mbili kwa pamoja ili kuongeza mapato katika nchi yetu” alisema Sendwa.
Kwa upande wake Mtalii, Whori Warabisako nchini Japani amesema kuja kwake Tanzania ni fursa moja wapo ya yeye kujifunza utamaduni wa Matanzania na kujione mazingira tulivu yaliyopo hapa nchini.
“Nafurahi kuwepo hapa Tanzania, hii ni mara yangu ya kwanza kufika Tanzania na nina amini kufika Tanzania nitajifunza mengi katika kuutembelea maneo ya kitalii ya Tanzania” alisema whori Warabisako.
Watalii hao kutoka Japani, Marekani, China, Tawain, Uingereza wamewasili leo Alhamisi Januari 9, 2020 saa 12 asubuhi wakiwa katika Meli kubwa ya Kisasa ya kampuni AZAMARA inayofanya safari zake Dunia nzima katika kutangaza utalii wa majini.
Meli hiyo ya AZAMARA itaondoka leo Alhamisi Januari 9, 2020 saa 4 usiku kuelekea Zanzibar kwa lengo la kufanya utalii wa ndani katika maeneo ya kihistoria ikiwemo Mji Kongwa,
Ujenzi Wa Majengo Ya Utawala Kuongeza Tija Utoaji Huduma Tamisemi
UTAWALA bora ni nyenzo muhimu katika kuharakisha maendeleo endelevu ya nchi kwa kuzingatia misingi ya sheria, uwazi na uwajibikaji ili kutoa huduma bora kwa wananchi.
Ofisi ya Rais-TAMISEMI inasimamia utekelezaji wa shughuli za utawala bora kwa kuzingatia matakwa ya Ibara ya 146(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inayohusu ugatuaji wa madaraka kwa wananchi ili kuboresha utoaji wa huduma za kijamii na maendeleo.
Katika Mwaka wa Fedha 2018/2019, Ofisi ya Rais-TAMISEMI imeendelea kuimarisha utawala bora ikiwa ni pamoja na ujenzi wa majengo ya utawala katika Mikoa, Halmashauri, Tarafa, Kata, Mitaa na Vijiji ili kuboresha mazingira ya kufanyia kazi.
Aidha ili kufikia malengo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi wake, Serikali imeendelea kuwajengea uwezo viongozi na Watendaji kwenye Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na kuimarisha misingi ya uwazi, uwajibikaji na usawa katika matumizi ya fedha kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Tangu mwaka 1984, Serikali iliporejesha Mfumo wa Serikali za Mitaa, jitihada kubwa zimekuwa zikifanyika katika kujenga mfumo imara wa kitaasisi ili kusimamia na kuratibu shughuli za utawala, utendaji na maendeleo katika ngazi ya Mikoa, Wilaya, Halmashauri, Tarafa, Kata, Kijiji, Mtaa na Kitongoji.
Agenda ya kuziimarisha Serikali za Mitaa iliyoidhinishwa mwaka 1996, ina lengo la kukidhi mahitaji ya kuwawezesha wananchi kushiriki kwa ukamilifu katika shughuli za maendeleo na kutanzua changamoto kadhaa zilizozikumba Serikali za Mitaa kwa muda mrefu.
Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2019/2020, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo anasema Ofisi ya Rais-TAMISEMI imeendelea kutimiza jukumu la msingi la kuzijengea uwezo Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Anasema katika katika Mwaka wa Fedha 2018/2019, Tawala za Mikoa zimetumia jumla ya shilingi bilioni 31.64 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa Ofisi na nyumba za viongozi katika Mkoa, Wilaya na Tarafa.
‘Kati ya Fedha hizo, shilingi bilioni 20.6 zimetumika kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Tarafa na shilingi bilioni 11.04 zimetumika kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa nyumba za viongozi kwenye Mikoa, Wilaya na Tarafa’’ anasema Waziri Jafo.
Waziri Jafo anasema ujenzi na ukarabati wa Ofisi za Wakuu wa Mikoa umefanyika katika Mikoa ya Katavi, Simiyu, Njombe, Geita, Pwani, Arusha, Ruvuma, Dodoma na Singida kwa gharama ya shilingi bilioni 7.2 na pia ujenzi na ukarabati wa Ofisi za Wakuu wa Wilaya umefanyika katika Wilaya 29 sambamba na kujenga ofisi 60 za za Maafisa Tarafa kwa gharama ya Tsh. Bilioni bilioni 3.3.
Kwa mujibu wa Waziri Jafo anasema katika mwaka 2018/19, Serikali imejenga nyumba za viongozi 72 katika Mikoa na Wilaya kwa ajili ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Wilaya, Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Wilaya na Maafisa Tarafa, ambapo hadi kufikia mwezi Februari 2019 ujenzi na ukarabati wa nyumba hizo umegharimu jumla ya shilingi bilioni 11.04.
Akifafanua zaidi Waziri Jafo anasema Halmashauri 78 zimeendelea na ujenzi wa majengo ya utawala zikiwemo Halmashauri 55 zilizotengewa bajeti ya shilingi bilioni 61.7 kuanzia mwaka wa Fedha 2015/16 hadi 2017/18, ambapo ujenzi wa majengo hayo upo katika hatua mbalimbali za ukamilishaji.
‘Halmashauri 23 zilizoanzishwa mwaka 2014 ziliidhinishiwa jumla ya shilingi bilioni52.9 katika mwaka wa fedha 2018/2019 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya utawala ya Halmashauri. Hadi Februari, 2019 Halmashauri 23 zimepokea jumla ya shilingi bilioni 23 sawa na asilimia 43.4 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa majengo ya utawala ya Halmashauri’’ anasema Waziri Jafo.
Aidha Waziri Jafo anasema katika kuzijengea uwezo Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, Serikali katika mwaka 2018/19 imetoa mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya 27 walioteuliwa Oktoba, 2018 katika nyanja za mifumo, taratibu za mawasiliano Serikalini na mahusiano baina ya Taasisi za Serikali.
Kwa mujibu wa Waziri Jafo, mafunzo hayo yameimarisha utendaji kazi wa Wakuu wa Wilaya katika usimamizi wa miradi ya maendeleo, utawala bora na utatuzi wa kero za Wananchi, na pia Mwezi Desemba 2018, Wakuu wa Mikoa 26 na Makatibu Tawala wa Mikoa 26, Wakurugenzi wapya wa Halmashauri 39 walioteuliwa walifanyiwa mafunzo juu ya utawala bora.
‘Vilevile, Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mipango na Uratibu 26 wa Mikoa na Maafisa Mipango185 wa Halmashauri walipatiwa mafunzo kuhusu mipango na Bajeti,na mafunzo hayo yamesaidia kuboresha utendaji ndani ya Serikali na kutatua kero za wananchi ili kuboresha utoaji wa huduma’’ alisema Waziri Jafo.
Mamlaka za Serikali za Mitaa ni vyombo vya wananchi vinavyowawezesha wananchi kuwa na sauti katika maamuzi mbalimbali ama kwa kushiriki moja kwa moja au kupitia kwa wawakilishi wao katika shughuli za maendeleo na utawala.
Basi Lapinduka Morogoro....9 Wajeruhiwa
Watu 9 wamejeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria la kampuni Kidinilo kuacha njia jana Alhamisi Januari 9, 2020 na kupinduka eneo la Mangae barabara ya Morogoro Iringa huku chanzo kikitajwa ni uzembe na mwendokasi.
Basi lililokuwa kilitokea Ifakara kwenda Dar es Salaam lilikuwa na abiria 68 kwamba majeruhi watatu hali zao sio nzuri kutokana na majeraha makubwa waliyoyapata na wamepelekwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa, ameeleza chanzo cha ajali hiyo ni Dereva wa Basi la Kidinilo kutaka kulipita gari jingine bila kuchukua tahadhari, Dereva huyo anaitwa Shabani Sultan (54) amekamatwa wakati akijaribu kutoroka kwa kutumia Bodaboda.
“Kati ya majeruhi tisa walionusurika kwenye ajali ya basi la Kidinilo, wawili wamevunjika miguu, mmoja hali yake si nzuri, wengine wamepata majeraha ya kawaida wanapatiwa matibabu" - RPC, Morogoro, Wilbroad Mutafungwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa, ameeleza chanzo cha ajali hiyo ni Dereva wa Basi la Kidinilo kutaka kulipita gari jingine bila kuchukua tahadhari, Dereva huyo anaitwa Shabani Sultan (54) amekamatwa wakati akijaribu kutoroka kwa kutumia Bodaboda.
“Kati ya majeruhi tisa walionusurika kwenye ajali ya basi la Kidinilo, wawili wamevunjika miguu, mmoja hali yake si nzuri, wengine wamepata majeraha ya kawaida wanapatiwa matibabu" - RPC, Morogoro, Wilbroad Mutafungwa.
Rais Magufuli Kuanza Ziara Ya Kikazi Visiwani Zanzibar leo
Rais Magufuli aliyekuwa mapumzikoni nyumbani kwake, Chato mkoani Geita amewasili jana Alhamisi Januari 9, 2020 jijini Dar es Salaam.
Mara baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa na mkewe, Janeth, Rais Magufuli alisalimiana na baadhi ya wafanyakazi katika uwanja huo.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais- Ikulu ya Tanzania, Gerson Msigwa amesema leo Ijumaa Januari 10, 2020 Rais Magufuli ataanza ziara ya kikazi ya siku tano visiwani Zanzibar.
Thursday, 9 January 2020
SHULE 10 JIJINI TANGA ZANUFAIKA NA MSAADA WA KOMPYUTA ZILIZOTOLEWA NA MBUNGE UMMY MWALIMU
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akigawa msaada wa moja ya kumpyuta 20 kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari kulia leo ambapo shule 10 zitanufaika na msaada huo ambao umetolewa Mbunge huyu kwa ufadhili wa Tume ya Mawasiliano nchini wenye thamani ya milioni 16.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akigawa msaada wa moja ya kumpyuta 20 kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Mnyanjani Saida Mahadhi kushoto jana ambapo shule 10 zitanufaika na msaada huo ambao umetolewa Mbunge huyo kwa ufadhiliwa na Tume ya Mawasiliano nchini wenye thamani ya milioni 16 kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Msaafu wa Jeshi Mkoba
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akigawa msaada wa moja ya kumpyuta 20 kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari kulia leo ambapo shule 10 zitanufaika na msaada huo umetolewa na Mbunge Ummy kwa ufadhili wa Tume ya Mawasiliano nchini wenye thamani ya milioni 16 katikati mwenye miwani ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji na kushoto Mwenye Kaunda suti ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa halfa ya makabidhiano hayo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa halfa hiyo kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji
![]() |
| Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji akizungumza wakati wa makabidhiano hayo |
Afisa Elimu Jiji la Tanga Lusajo Gwakisa akitoa taarifa ya elimu wakati wa makabidhiano hayo
Sehemu ya wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo walimu wakuu wa shule za sekondari na wadau wakifuatilia makabidhiano hayo
Sehemu ya walimu wa shule ya Sekondari Mkwakwani wakifuatilia makabidhiano hayo
Sehemu ya Kompyuta zilizotolewa na Waziri Ummy kwa shule 20 za sekondari Jijini Tanga
Sehemu ya Kompyuta zilizotolewa na Waziri Ummy kwa shule 20 za sekondari Jijini Tanga
SHULE 10 za sekondari Jijini Tanga zimenufaika na msaada wa Kompyuta 20 ambao zimetolewa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu.
Msaada huo ambao umetolewa na Mbunge Ummy ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kwa ufadhili wa Tume ya Mawasiliano nchini wenye thamani ya sh.milioni 16.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika kwenye shule ya Sekondari Mkwakwani, Mbunge Ummy alisema kwamba uwepo wa kompyuta hizo utatoa fursa kwa wanafunzi kusoma somo hilo kwa vitendo ikiwemo kusaidia utendaji wa kazi wao.
Alisema piaa ametoa kompyuta hizo kwa shule hizo ili kuwasaidia wanafunzi kujifunza somo na kurahisisha bajeti za shule ngazi ya shule na uandaaji wa malipo kwa kutumia mfumo wa FFARS na sio watumie kucheza karata bali
“Lakini pia zitasaidia usajili wa wanafunzi na usajili wa watahiniwa vyote vitasaidia hivyo Mkurugenzi wa Jiji Daudi Mayeji wasaidia WIFI kwa lengo la kurahisisha baadhi ya mambo yanayohitajika kutumia mtandao”Alisema
Mbunge huyo alisema kwamba kwa shule ambazo hazijapata msaada huo atakwenda kutafuta lengo lake ni kutafuta vishkwabi kwa ajili ya wanafunzi kuhakikisha wanasoma somo la kompyuta huku akihaidi pia kujengwa vyumba vitano vya madarasa
“Niwashukuru lakini niendelee kuwaomba wanafunzi fanyeni kazi kwa kujitumua na tunatambua vipi changamoto za walimu tutaendelea kuzipatia ufuimbuzi”Alisema
Hata hivyo amehaidi kwamba ataendelea kuwasemea wananchi wa Jiji la Tanga kwa kutumia nafasi yake kuhakikisha maslahi ya walimu yanakuwa mazuri.
Awali akizungumza katika makabidhiano hayo Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa alisifu juhudi zinazofanywa na Mbunge Ummy kuhakikisha anawasaidia wananchi wa Jiji la Tanga kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya elimu.
Alimpongeza Waziri Ummy kwa msaada huo ambao amewapatia shule hizo kwani miongoni mwao ni zile ambazo zinaupungufu wa madarasa zimenufaika na msaada huo wa kompyuta.
Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji alisema kwamba msaada huo wa komputa utakuwa chachu kubwa kwao kwani serikali ya sasa imefanya mageuzi makubwa.
Alisem kutokana na mageuzi hayo hakuna malipo yanayoweza kufanyika bila mfumo kwa hiyo msaada huo wa kumputa 20 shule hizo zitakuwa zimeondolewa kwenye tatizo la kutokuweza kufanya malipo kutumia mfumo.
“Kutokana na kwamba shule nyingi au Taasis zimekuwa zikienda shule za jirani kutokana wengi kutokuwa nazo hivyo msaada huo utakuwa chachu kubwa kwa kuongeza ufanisi katika utendaji wao “Alisema.
Awali akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Afisa Elimu Jiji la Tanga Lusajo Gwakisa alimshukuru Mbunge Ummy kwa msaada huo wa kompyuta 20 utakwenda kupunguza upungufu uliopo wa Kompyuta bali italeta tija katika maendeleo.
“Maendeleo hayo ambayo msaada huu utaleta tija ni utayarishaji wa bajeti katika ngazi za shule lakini pia uandaaji wa malipo kwa kutumia mfumo wa FFARE pamoja na usajili wa wanafunzi wanaoanza kidato cha kwanza “Alisema
Hata hivyo alisema kwamba pia vitasaidia uhamishaji wa taarifa za wanafunzi kwa kutumia mfumo wa PREM ikiwemo usajili wa watahiniwa wa kidato cha pili,nne na sita na kutunza kumbukumbu nyengine za utawala.
Picha : WAZIRI WA MAJI ATEMBELEA NA KUKAGUA ENEO LA UJENZI WA MRADI WA MAJI MWAWAZA- SHINYANGA
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa ametembelea na kukagua eneo la ujenzi wa Mradi wa Maji kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga ambao utagharimu shilingi Bilioni 1.4 hadi kukamilika kwake.
Prof. Mbarawa ametembelea eneo la Mwawaza panapojengwa Tenki la Maji litakalogharimu shilingi milioni 100 na kuzungumza na wananchi wa kata ya Mwawaza leo Alhamis Januari 9,2020.
Prof. Mbarawa alisema mradi huo unajengwa kwa usimamizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga SHUWASA na kuwataka wananchi wa Mwawaza kuchangamkia fursa kwa kushiriki katika ujenzi kwani watakuwa wanalipwa.
Prof. Mbarawa aliagiza mradi huo ambao tayari ujenzi wake wa Matenki umeanza ukamilike kufikia Machi mwaka 2020 ili kuondoa changamoto ya maji safi na salama ambayo imekuwa kero ya muda mrefu.
“Nataka mradi huu umalizike haraka matenki yajengwe ndani ya miezi miwili zoezi la kulaza mabomba lianze mara moja. Tunaleta mabomba yenye ubora kwa gharama nafuu hivyo wananchi mnapaswa kulinda miundo mbinu ya maji ili idumu”,aliongeza.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele aliishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli kwa kusikia kilio cha wananchi wa Mwawaza kuwapatia huduma ya maji safi na salama.
Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Flaviana Kifizi, alisema SHUWASA inasimamia na kujenga miradi ya maji kwa kutumia wataalamu wa ndani “Force account” katika wilaya za Shinyanga (Negezi – Mwawaza) na Kahama (Ngogwa – Kitwana) ambapo Miradi hiyo inahusisha ujenzi wa matenki na mtandao wa maji safi.
“Miradi hii inahusisha ujenzi wa matenki na mtandao wa maji safi. Hadi kufikia tarehe ya leo utekelezaji wa miradi hii upo katika hatua mbalimbali,ujenzi wa matenki umeanza na mafundi wapo site wakiandaa maeneo ambayo matenki hayatajengwa”,alisema Kifizi.
Alisema ulazaji wa mabomba unasubiri upatikanaji wa msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani VAT ambao maombi tayari yamewasilishwa wizara ya fedha.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Flaviana Kifizi akimweleza jambo Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa (kulia) leo Alhamis Januari 9,2020 alipotembelea na kukagua eneo la ujenzi wa tenki la maji katika eneo la Mwawaza ikiwa ni sehemu ya Mradi wa Maji kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga ambao utagharimu shilingi Bilioni 1.4 hadi kukamilika kwake. Kushoto ni Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog.
Eng. Christopher Shiganza akielezea kuhusu ujenzi wa tenki la maji katika kata ya Mwawaza.
Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akiishukuru serikali kuwapatia maji wananchi wa Mwawaza.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi akiteta jambo na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa alipotembelea na kukagua eneo la ujenzi wa Mradi wa Maji kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwawaza na kuwaeleza kuhusu mradi wa maji unaojengwa katika kata hiyo.
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akiwahamasisha wananchi wa Mwawaza kushiriki katika mradi wa maji kwenye kata hiyo.
Wakazi wa Mwawaza wakimsikiliza Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa.
Wakazi wa Mwawaza wakimsikiliza Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa.
Wakazi wa Mwawaza wakimsikiliza Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa.
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela akizungumza katika kata ya Mwawaza wakati Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akiwaeleza wananchi kuhusu mradi wa maji unaojengwa katika kata ya Mwawaza.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza katika kata ya Mwawaza wakati Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akiwaeleza wananchi kuhusu mradi wa maji unaojengwa katika kata ya Mwawaza.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Gulam Hafeez Mukadam akizungumza katika kata ya Mwawaza wakati Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akiwaeleza wananchi kuhusu mradi wa maji unaojengwa katika kata ya Mwawaza.
Diwani wa Kata ya Mwawaza Mhe. Juma Nkwabi akiomba wananchi wa Mwawaza washiriki katika mradi wa maji.
Mwananchi wa Mwawaza Catherine Francis akiishukuru serikali kwa kuwapatia huduma ya maji.
Mkuu wa shule ya Sekondari Mwawaza Juliana Limbe akiishukuru serikali kwa kuwapatia huduma ya maji.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
























