Thursday, 9 January 2020

Picha : WAZIRI WA MAJI PROF. MBARAWA AZINDUA BODI MPYA YA SHUWASA...AAGIZA WAKUSANYE MIL 700 KILA MWEZI

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa amezindua rasmi Bodi Mpya ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA) na kuagiza Mamlaka hiyo kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato akitishia kuvunja bodi hiyo endapo watashindwa kukusanya shilingi milioni 700 kila mwezi.

Prof. Mbarawa amezindua Bodi mpya ya SHUWASA leo Alhamis Januari 9,2020 katika ofisi za SHUWASA zilizopo Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa maji kutoka ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga.

Akizindua bodi hiyo ya nane tangu SHUWASA ianzishwe mwaka 1998, itayoongozwa na Bi. Mwamvua  Jilumbi, Prof. Mbarawa aliitaka SHUWASA kukusanya mapato na kupanua mtandao wa maji kwa kujenga miradi yenye ubora ili kuondoa changamoto ya maji kwa wananchi.

“Kazi ya kwanza ambayo natoa kwa bodi hii mpya ni kwamba nataka mkusanye mapato yasiyopungua shilingi milioni 7 kila mwezi,mkishindwa kukusanya sitakuwa na msalie mtume kuvunja bodi hii”,alisema Prof. Mbarawa.

“Pesa mtakayokusanya muitumie kulipa KASHWASA na kupanua mtandao wa maji siyo kila siku mje kuomba fedha Wizarani. Fedha mnayopata ipelekeni kwenye miradi na mjenge miradi hiyo nyinyi wenyewe kwa kutumia wakandarasi wa ndani”,aliongeza Prof. Mbarawa.

Waziri huyo wa Maji aliitahadharisha bodi mpya ya SHUWASA kutothubutu kutumia fedha za mapato kujilipa posho na kupeana safari zisizo na tija akisema SHUWASA siyo mahala pa kula fedha bali ni kwa ajili ya kusaidia wananchi wapate maji safi, salama na ya kutosha.

“Naagiza bodi hii iwe inafanya maamuzi kwa wakati,msukume maamuzi yenu yafanyike kwa haraka kwani Watanzania wamechoka wanataka maji”,aliongeza.

Katika hatua nyingine alisema changamoto ya Taasisi za serikali ikiwemo Jeshi la Wananchi (JWTZ), polisi na Magereza kudaiwa na SHUWASA wanaifanyia kazi na serikali itawalipa huku akishauri taasisi hizo kufungiwa mita za malipa ya kabla ‘ Prepaid Meter’.

Akitoa taarifa ya Mwenyekiti wa Bodi ya SHUWASA iliyomaliza muda wake ambayo ilizinduliwa Novemba 14,2016,Deogratius Sulla,alisema taasisi za serikali hasa idara ya ulinzi na usalama zinasuasua katika kulipa ankara zake za maji kila mwezi,jambo ambalo linasababisha deni la maji kukua na kufikia sh. 949,11,561/=, akieleza kuwa jitihada za kufuatilia madeni hayo hazijazaa matunda makubwa hivyo kumuomba Waziri awasaidie kutatua changamoto hiyo.

"Mpaka mwezi Desemba 2019, JWTZ ilikuwa inadaiwa shilingi 520,244,975.50/=, Magereza shilingi 256,520,120.50/= na polisi shilingi 172,346,465/=",alieleza .

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Flaviana Kifizi, alisema hivi sasa mamlaka imeongezewa maeneo mengine matatu ya kutoa huduma ambayo awali yalikuwa yanahudumiwa na RUWASA ambayo ni Tinde,Didia na Iselamagazi.

Alisema SHUWASA hukusanya mapato ya wastani wa shilingi 497,891,531 kwa mwezi ambacho asilimia tano tu hutumika katika kuongeza mtandao katika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma ya maji safi.

Kifizi alieleza kuwa SHUWASA inahuhudumia wakazi wa Manispaa ya Shinyanga wapatao 186,671 ambapo hadi sasa jumla ya wakazi 149,710 sawa na asilimia 80.2 wamefikiwa na huduma ya maji safi.

“Hadi kufikia Desemba 2019 Mamlaka ilikuwa na wateja wapatao 21,505 na mtandao wa maji safi wenye jumla ya kilomita 549.12. Mahitaji ya maji safi kwa wakazi wa Manispaa ya Shinyanga yanakadiriwa kuwa mita za ujazo 21,266 kwa siku”,alieleza Kifizi.

“Wastani wa matumizi ya maji kwa siku ni mita za ujazo 12,500 kwa siku sawa na asilimia 58.8 tu ya maji kwa manispaa yote.Kwa mwezi Desemba 2019 mamlaka ilisambaza maji yenye mita za ujazo 324,357 sawa na wastani wa mita za ujazo 11,709 kwa siku”,alisema Kifizi.

Aliongeza kuwa SHUWASA inasimamia na kujenga miradi wa Force account katika wilaya za Shinyanga (Negezi – Mwawaza) na Kahama (Ngogwa – Kitwana) ambapo Miradi hiyo inahusisha ujenzi wa matenki na mtandao wa maji safi.


ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa (mwenye suti ya bluu) akiwasili katika ofisi za Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA) kwa ajili ya uzinduzi wa Bodi Mpya ya SHUWASA leo Alhamis Januari 9,2020. Wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Bi. Flaviana Kifizi. Wa kwanza kulia mbele ni Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Bw. Albert Msovela. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akizungumza wakati akizindua rasmi Bodi Mpya ya SHUWASA. Wa kwanza kulia ni Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akifuatiwa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Stephen Masele na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga,Gulam Hafeez Mukadam.
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akizungumza wakati akizindua rasmi Bodi Mpya ya SHUWASA na kuitaka bodi hiyo kufanya kazi kwa uadilifu ili kuwaisaidia wananchi ambao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya maji.
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akizungumza wakati akizindua rasmi Bodi Mpya ya SHUWASA.
Wakurugenzi wa Mamlaka mbalimbali za Maji nchini wakimsikiliza Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa.
Wakuu wa taasisi mbalimbali na wafanyakazi wa SHUWASA wakimsikiliza Waziri wa Maji Makame Mbarawa.
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack wakati uzinduzi wa bodi mpya ya SHUWASA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Flaviana Kifizi akitoa taarifa kuhusu kazi  zinazofanywa na SHUWASA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Flaviana Kifizi akitoa taarifa kuhusu kazi  zinazofanywa na SHUWASA.
Wafanyakazi wa SHUWASA wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea.
Mwenyekiti wa Bodi ya SHUWASA iliyomaliza muda wake Deogratius Sulla, akitoa taarifa kuhusu bodi iliyomaliza muda wake.
Mwakilishi wa wafanyakazi wa SHUWASA,Paulina Shagile akitoa taarifa ya wafanyakazi wa  SHUWASA.
Wadau wa maji wakiwa eneo la tukio.
Wafanyakazi wa SHUWASA wakiwa kwenye uzinduzi wa bodi mpya ya SHUWASA.
Wadau wa maji wakiwa kwenye uzinduzi wa bodi mpya ya SHUWASA.
Wadau wa maji wakiwa kwenye uzinduzi wa bodi mpya ya SHUWASA.
Wafanyakazi wa SHUWASA wakiwa kwenye uzinduzi wa bodi mpya ya SHUWASA.
Wafanyakazi wa SHUWASA wakiwa kwenye uzinduzi wa bodi mpya ya SHUWASA.
Wadau wa maji wakiwa kwenye uzinduzi wa bodi mpya ya SHUWASA.
Wafanyakazi wa SHUWASA wakiwa kwenye uzinduzi wa bodi mpya ya SHUWASA.
Wadau wa maji kutoka taasisi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi wa bodi mpya ya SHUWASA.
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akikabidhi zawadi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya SHUWASA iliyomaliza muda wake, Deogratius Sulla wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA). 
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akikabidhi zawadi kwa Aliyekuwa Katibu wa Bodi ya SHUWASA iliyomaliza muda wake, Eng'. Silvester Mahole wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA). 
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akikabidhi vitendea kazi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya SHUWASA Bi. Mwamvua Jilumbi wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA). 
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akikabidhi vitendea kazi kwa Mjumbe wa  Bodi ya SHUWASA,Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA). 
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akikabidhi vitendea kazi kwa Mjumbe wa  Bodi ya SHUWASA,Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Geofrey Mwangulumbi wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA). 
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akikabidhi vitendea kazi kwa Mjumbe wa  Bodi ya SHUWASA,Ziporah Pangani wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA). 
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akikabidhi vitendea kazi kwa Katibu wa  Bodi ya SHUWASA,Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Flaviana Kifizi wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA). 
Wajumbe wa Bodi Mpya ya SHUWASA wakiwa na vitendea kazi vyao.
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akipiga picha ya pamoja na Wajumbe wa bodi ya SHUWASA iliyomaliza muda wake.
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akipiga picha ya pamoja na Wajumbe wapya wa  bodi ya SHUWASA.
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akipiga picha ya pamoja na Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama.
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akipiga picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Mamlaka mbalimbali za Maji nchini.
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akipiga picha ya pamoja na Viongozi wa taasisi mbalimbali.
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akipiga picha ya pamoja na viongozi wa dini.
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa SHUWASA.
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa SHUWASA.
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa SHUWASA.
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa SHUWASA.
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa SHUWASA.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

WAZIRI UMMY AMWAGA KOMPYUTA 20 KWENYE SHULE ZA SEKONDARI JIJI LA TANGA


 Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akigawa msaada wa moja ya kumpyuta 20 kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari kulia leo ambapo shule 10 zitanufaika na msaada huo ambao umetolewa na Tume ya Mawasiliano nchini wenye thamani ya milioni 16.

 Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akigawa msaada wa moja ya kumpyuta 20 kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Mnyanjani Saida Mahadhi kushoto jana ambapo shule 10 zitanufaika na msaada huo ambao umetolewa na Tume ya Mawasiliano nchini wenye thamani ya milioni 16 kulia  ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Msaafu wa Jeshi Mkoba
 Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akigawa msaada wa moja ya kumpyuta 20 kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari kulia leo ambapo shule 10 zitanufaika na msaada huo ambao umetolewa na Tume ya Mawasiliano nchini wenye thamani ya milioni 16 katikati mwenye miwani ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji na kushoto Mwenye Kaunda suti ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
 MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa halfa ya makabidhiano hayo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
 Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa halfa hiyo kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji
Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji akizungumza wakati wa makabidhiano hayo
 Afisa Elimu Jiji la Tanga Lusajo Gwakisa akitoa taarifa ya elimu wakati wa makabidhiano hayo
 Sehemu ya wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo walimu wakuu wa shule za sekondari na wadau wakifuatilia makabidhiano hayo
Sehemu ya walimu wa shule ya Sekondari Mkwakwani wakifuatilia makabidhiano hayo

 Sehemu ya Kompyuta zilizotolewa na Waziri Ummy kwa shule 20 za sekondari Jijini Tanga
 Sehemu ya Kompyuta zilizotolewa na Waziri Ummy kwa shule 20 za sekondari Jijini Tanga 


MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa wa Afya Maendeleo ya Jamii Ummy Mwalimu leo ametoa msaada wa kompyuta 20 kwa 10 za Sekondari Jijini Tanga ili kutoa fursa kwa wanafunzi kusoma somo hilo kwa vitendo ikiwemo kusaidia utendaji wa kazi wao.

Makabidhiano hayo yalifanyika leo kwenye shule ya Sekondari Mkwakwani Jijini Tanga kwa niaba ya shule zote ambazo zitanufaika na msaada huo ambao umetolewa na Tume ya Mawasiliano nchini wenye thamani ya milioni 16.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo Mbunge Ummy alisema kwamba ametoa kumpyuta hizo sio wanafunzi watumie kucheza karata bali ni kurahisisha bajeti za shule katika n gazi ya shule, uandaaji wa malipo kwa kutumia mfumo wa FFARS.

“Lakini pia zitasaidia usajili wa wanafunzi na usajili wa watahiniwa vyote vitasaidia hivyo Mkurugenzi wa Jiji Daudi Mayeji wasaidia WIFI kwa lengo la kurahisisha baadhi ya mambo yanayohitajika kutumia mtandao”Alisema

Mbunge huyo alisema kwamba kwa shule ambazo hazijapata msaada huo atakwenda kutafuta lengo lake ni kutafuta vishkwabi kwa ajili ya wanafunzi kuhakikisha wanasoma somo la kompyuta huku akihaidi pia kujengwa vyumba vitano vya madarasa

“Niwashukuru lakini niendelee kuwaomba wanafunzi fanyeni kazi kwa kujitumua na tunatambua vipi changamoto za walimu tutaendelea kuzipatia ufuimbuzi”Alisema

Hata hivyo amehaidi kwamba ataendelea kuwasemea wananchi wa Jiji la Tanga kwa kutumia nafasi yake kuhakikisha maslahi ya walimu yanakuwa mazuri.

Awali akizungumza katika makabidhiano hayo Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa alisifu juhudi zinazofanywa na Mbunge Ummy kuhakikisha anawasaidia wananchi wa Jiji la Tanga kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya elimu.


Alimpongeza Waziri Ummy kwa msaada huo ambao amewapatia shule hizo kwani miongoni mwao ni zile ambazo zinaupungufu wa madarasa zimenufaika na msaada huo wa kompyuta.


Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji alisema kwamba msaada huo wa komputa utakuwa chachu kubwa kwao kwani serikali ya sasa imefanya mageuzi makubwa.


Alisema kutokana na mageuzi hayo hakuna malipo yanayoweza kufanyika bila mfumo kwa hiyo msaada huo wa kumputa 20 shule hizo zitakuwa zimeondolewa kwenye tatizo la kutokuweza kufanya malipo kutumia mfumo.
 

“Kutokana na kwamba shule nyingi au Taasis zimekuwa zikienda shule za jirani kutokana wengi kutokuwa nazo hivyo msaada huo utakuwa chachu kubwa kwa kuongeza ufanisi katika utendaji wao “Alisema.
 

Awali akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Afisa Elimu Jiji la Tanga Lusajo Gwakisa alimshukuru Mbunge Ummy kwa msaada huo wa kompyuta 20 utakwenda kupunguza upungufu uliopo wa Kompyuta bali italeta tija katika maendeleo.
 

“Maendeleo hayo ambayo msaada huu utaleta tija ni utayarishaji wa bajeti katika ngazi za shule lakini pia uandaaji wa malipo kwa kutumia mfumo wa FFARE pamoja na usajili wa wanafunzi wanaoanza kidato cha kwanza “Alisema

Hata hivyo alisema kwamba pia vitasaidia uhamishaji wa taarifa za wanafunzi kwa kutumia mfumo wa PREM ikiwemo usajili wa watahiniwa wa kidato cha pili,nne na sita na kutunza kumbukumbu nyengine za utawala.
Share:

Breaking: Matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Pili Yametoka....Bofya Hapa

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne na kidato cha pili kwa mwaka 2019.

1.Matokeo Kidato cha NNE:  <<BOFYA HAPA>>

2.Matokeo Kidato cha PILI : <<BOFYA HAPA>.


Share:

Ijue Sayansi ya Kusimama na Kusinyaa kwa Maumbile ya Kiume ( Sayansi ya Nguvu za Kiume)


Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani.

Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ?
Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu


Hatua  mbili  Muhimu 
Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  maumbile yake ya kiume yapitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo :

Hatua  ya  kwanza, ni  lazima  yaweze  kusimama  barabara  na  kuwa  magumu  kama  msumari.

Na  hatua  ya  pili  ni  lazima, yaendelee  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.  Hatua  zote  mbili  zinapo  kamilika, ndipo  tunapo  pata  kitu  kinaitwa  STRONGER  AND  LONGER  ERECTION

Endelea na Makala hii kwa <<Kubofya Hapa>.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger