Wednesday, 8 January 2020

Syrup Room And Water Treatment Team Leader at Coca-Cola Kwanza

Closing Date  2020/01/22
Reference Number CCB190528-4
Job Title Syrup Room and Water Treatment Team Leader
Function Manufacturing
Company Coca-Cola Kwanza (Tanzania)
Job Type Permanent
Location – Country Tanzania
Location – Province Not Applicable
Location – Town / City Mbeya

Job Description
Coca-Cola Kwanza Ltd has an exciting opportunity in Manufacturing Department. We are looking for a talented individual with the relevant skills and experience for a Syrup Room and Water Treatment Team Leader position, to be based in Mbeya. The successful candidate will report directly to the Manufacturing Manager.

Key Duties & Responsibilities
The Syrup Room and Water Treatment Team Leader will be responsible in monitoring the syrup and water treatment plant; Ensure good operational control and equipment maintenance in his/her process area (syrup and water treatment plant) in order to supply syrup and treated water to customers as per daily operational plan. Provide leadership to the Syrup Room and Water Treatment team, communicating the business direction and implementing organisational improvement initiatives. Ensure compliance with all internal and related legal/regulatory requirements with respect to safety, water quality and environmental management. Where necessary assist with the development of operational quality system procedures/guidelines for Syrup Room and Water Treatment. Ensure optimization of resources in daily operations as per budget.

Skills, Experience & Education
The incumbent should have at least a Bachelor’s degree in Food Science and Technology; Chemistry; Micro-Biology or Environment Science. Three (3) years of manufacturing experience which include experience in a leadership or managerial role and 2 years water treatment experience preferably with FMCG; Should also be a good communicator, physically flexible and demonstrate high level of integrity and leadership.



Share:

Customer Sales Agent 3 post at Sokowatch Arusha

Sokowatch is transforming communities across Africa by revolutionizing access to essential goods and services. By connecting small shops to the digital economy, we fix inefficient supply chains and provide services previously unavailable to informal businesses. Sokowatch aims to provide everything a retailer needs, no wholesalers or banks necessary. Thousands of retailers across Kenya, Tanzania, and Rwanda use Sokowatch’s… Read More »

The post Customer Sales Agent 3 post at Sokowatch Arusha appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Officer Reconciliation Job at National Bank of Commerce (NBC)

National Bank of Commerce (NBC) Job Title: Officer Reconciliation Head Office NBC NBC is the oldest serving bank in Tanzania with over five decades of experience. We offer a range of retail, business, corporate and investment banking, wealth management products and services. Job Description​ EXECUTION OF MAIN ROLE Prepare reconciliations of reconcilable accounts of Head office Finance Identify,… Read More »

The post Officer Reconciliation Job at National Bank of Commerce (NBC) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

RC TELACK AMTAKA MWENYEKITI WA KIJIJI KUMTOA MTOTO MACHUNGANI


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack (kushoto) na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Jasinta Mboneko wakimhoji mtoto Majebele Masanja baada ya kumkuta akichunga ng'ombe muda wa masomo hapo jana tarehe 07/01/2020 eneo la shule ya Sekondari Ilindi, kata ya Zongomela Wilaya ya Kahama.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack (kushoto) na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Jasinta Mboneko wakimhoji mtoto Majebele Masanja baada ya kumkuta akichunga ng'ombe muda wa masomo hapo jana tarehe 07/01/2020 eneo la shule ya Sekondari Ilindi, kata ya Zongomela Wilaya ya Kahama.

***
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amemtaka Mwenyekiti wa kijiji cha Ilindi, kata ya Zongomela kuhakikisha mtoto Majebele Masanja anaacha mara moja kazi ya kuchunga ng’ombe na anapelekwa shule.

Mhe. Telack ametoa agizo hilo jana tarehe 07/01/2020 baada ya kumkuta mtoto huyo maeneo ya shule ya Sekondari Ilindi akiwa anachunga ng’ombe badala ya kuwa shuleni ambapo alihojiwa na kusema kuwa anafanya kazi kwa ujira wa sh. 20,000 kwa mwezi na kuwa hasomi kwa sababu mzazi wake hana uwezo.
Akizungumza na Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji wa Halmashauri ya Mji Kahama katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo ambapo ametoa agizo hilo kwa Mwenyekiti huyo, Telack amesema wenyeviti wote wakahakikishe wazazi wanaelekezwa kusimamia mahudhurio ya wanafunzi shuleni.
“Mkazungumze na wananchi, wazazi na walezi kuhusu wanafunzi wasiofika shuleni, mkafanye mikutano ya hadhara na muazimie kusimamia mahudhurio shuleni” amewaambia.
“Haiwezekani wazazi kuacha watoto wanachunga badala ya kusoma, mtoto yule apelekwe shuleni na nitafuatilia” amesema Mhe. Telack.
Aidha, Telack amewasisitiza Wenyeviti wote wa Mitaa na Vijiji kushirikisha wananchi katika shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kujenga maboma ya madarasa, kusaidia kukomesha matumizi ya madawa ya kulevya na kuwaongoza wananchi bila kuendekeza migogoro isiyokuwa na sababu.
Share:

WANANCHI WA KAHAMA WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA KUWACHANGIA UJENZI WA SHULE


 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack (Mwenye ushungi wa njano), Katibu Tawala Mkoa Bw. Albert Msovela (mwenye suti nyeusi), Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Jasinta Mboneko na Viongozi wengine wakiwa kwenye moja ya vyumba vya madarasa ya shule ya msingi Mayila ambapo wanafunzi wa darasa la kwanza wameanza masomo yao hapo tarehe 06 Januari, 2020. 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza na wananchi wakiwemo wazazi na walezi (hawamo pichani) waliokuwa shuleni Mayila kuwachukua watoto wao baada ya muda wa masomo
Shule ya msingi Mayila iliyopo Mtaa wa Mayila, kata ya Nyihogo Wilaya ya Kahama imefunguliwa rasmi huku wananchi wa kata hiyo wakimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kwa kuwachangia shilingi mil. 5 ili kuhakikisha shule hiyo inakamilika.
Wazazi hao wametoa shukrani hizo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack alipokwenda kukagua utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kuhakikisha shule hiyo inafunguliwa mapema jana tarehe 07 Januari, 2020.
Wamesema kuwa, kukamilika kwa shule hiyo kutawapunguzia adha ya umbali wa zaidi ya kilomita 3 watoto wa kata hiyo waliokuwa wanalazimika kuvuka barabara kubwa kufuata shule kata za jirani hali iliyopelekea kuwa katika hatari ya kugongwa na magari.
“Nashukuru sana kwa shule hii, watoto wetu mwanzo walikuwa wanakwenda mbali na sisi kama wazazi tupo tayari kuendelea kushirikiana na Serikali kujenga maboma” amesema Bw. Richard Joseph.
Diwani wa kata ya Nyihogo Mhe. Shadrack Mguami amesema, “kuna wakati naamka usiku kumuombea Mhe. Rais, sikutegemea kupata fedha kutoka kwake kwani angeweza kufanya shughuli nyingine lakini akaona atoe hapa, tunaahidi tutaendelea kumuunga mkono kwa kujenga maboma”
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kahama Mji Bw. Anderson Msumba amesema watoto zaidi ya 200 wameandikishwa kuanza darasa la kwanza hivyo uhitaji ni mkubwa, hata hivyo Halmashauri inaendelea kukamilisha maboma 108 na kufunga shule mpya 8.
“Tunamshukuru Mhe. Rais ametupa mori kuhakikisha shule hii inafunguliwa” amesema Msumba.
Mhe. Rais alichangia shilingi milioni 5 ili kuongeza nguvu ya kukamilisha shule hiyo alipopita Wilayani Kahama akielekea Wilayani Chato mwezi Novemba, mwaka jana 2019 na kuagiza ifunguliwe mwezi Januari mwaka huu 2020.
Shule hiyo iliyokuwa na vyumba viwili vya madarasa, hivi sasa ina vyumba 8 na matundu ya vyoo 12.

Share:

Syrup Room and Water Treatment Team Leader Job Opportunity at Coca-Cola Kwanza

Reference Number CCB190528-4 Job Title Syrup Room and Water Treatment Team Leader Function Manufacturing Company Coca-Cola Kwanza (Tanzania) Job Type Permanent Location – Country Tanzania Location – Province Not Applicable Location – Town / City Mbeya Job Description Coca-Cola Kwanza Ltd has an exciting opportunity in Manufacturing Department. We are looking for a talented individual with the relevant… Read More »

The post Syrup Room and Water Treatment Team Leader Job Opportunity at Coca-Cola Kwanza appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Business Development Workstream Coordinator Job at SVN Mwanza

Business Development Workstream Coordinator • Mwanza, Tanzania • Contract • Contract type: National employment contract Company Description SNV is a not-for-profit international development organisation. Founded in the Netherlands 50 years ago, we have built a long-term, local presence in 39 of the poorest countries in Asia, Africa and Latin America. Our global team of local and international advisors… Read More »

The post Business Development Workstream Coordinator Job at SVN Mwanza appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Job at Coca Cola Kwanza Limited – Distribution Driver

Job Opportunity at Coca Cola Kwanza Limited – Distribution Driver Reference Number CCB200107-23 Job Title Distribution Driver Function Logistics, Warehouse & Distribution Company Coca-Cola Kwanza (Tanzania) Job Type Permanent Location – Country Tanzania Location – Town / City Dar es Salaam Job Description Coca-Cola Kwanza Ltd has an exciting opportunity in Logistics department. We are looking for a talented… Read More »

The post Job at Coca Cola Kwanza Limited – Distribution Driver appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Sekta ya mawasiliano ya simu nchini ina mafanikio makubwa lakini tusibweteke tuboreshe zaidi

Msimu wa shamrashamra za sikuku za mwisho wa mwaka umefika ukingoni na sote tunaishukuru sana teknolojia ya mawasiliano ambayo hakika imechangia kusaidia mawasiliano yetu na wale tuwapendao, katika msimu huu. 

Hata wale ambao walishindwa kusafiri kujiunga na wapendwa wao msimu huu walau waliweza kuzungumza nao au hata kuwapigia video call.  

Sekta ya mawasiliano ya simu kwa hakika imebadili maisha yetu. Katika Afrika, eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara, sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini Tanzania imekuwa ni ya kupigiwa mfano hasa kwa namna ambavyo watumiaji simu wanavyoongezeka siku hadi siku na jinsi mtandao wa intaneti unavyosambaa maeneo mbalimbali nchini.  

Licha ya mafanikio hayo, daima tunaweza kuboresha zaidi. 
Tanzania ni moja ya nchi zenye makampuni mengi zaidi ya simu barani Afrika. 

Hili laweza kuonekana kama jambo zuri lakini hata hivyo wataalamu wa masoko ya mawasiliano na uwekezaji katika sekta hiyo wanaeleza kuwa masoko mengi bora ya mawasiliano ya simu duniani ni yale ambayo yana kampuni chache zenye uwekezaji imara. Katika masoko ya aina hiyo wateja na nchi wanapata tija zaidi. 

Wanaendelea kueleza kuwa kama kampuni hizo zingeunganisha nguvu katika shughuli zao ingeongeza faida na uwekezaji wenye tija zaidi kwa wateja katika eneo la bei ya huduma na ubora.  

Bahati nzuri hili limeanza kufanyika kwa kiasi fulani. Oktoba 2019 kampuni ya Smart ilijiondoa soko la Tanzania na kuacha makampuni 6 sokoni. 

Mwezi Novemba mwaka 2019 kampuni mbili kubwa za Tigo na Zantel nazo zikaunganisha shughuli zao na kufanya jumla ya makampuni sokoni sasa kuwa 5. 

Kama wataalamu wanavyoeleza, hii inamaanisha ni jambo jema japo kuna nafasi ya kuendelea kupunguza namba ya wachezaji na kuongeza ubora na tija zaidi kwa nchi na wateja kuanzia bei za vifurushi hadi ubora na upatikanaji wa mtandao. 

Mwaka ndio umeanza sasa, tutumaini kuwa kutakuwa na maboresho zaidi katika sekta hii ambayo yataleta tija si tu kwa serikali kwenye kodi lakini pia kwetu watumiaji wa simu ili tuendelee kufurahia mapinduzi haya ya kiteknolojia na mawasiliano.


Share:

Jobs at KCB Bank Tanzania Limited

New FRESH GRADUATE Job TRAINING Opportunities at KCB Bank Tanzania Limited Job Title: Fresh Graduate Trainee Location: TANZANIA Organization Name: Oyesterbay Branch JOB PURPOSE The incumbent will be contact person to customers on banking solutions. Responsible for advising bank customers on financial related issues. He/she will handle customers in a professional manner. Brief Description   KEY RESPONSIBILITIES: TYPICALLY NOT BE… Read More »

The post Jobs at KCB Bank Tanzania Limited appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Nafasi Mpya Za Kazi Serikalini: Mthamini Daraja La II, Fundi Sanifu , Afisa Mipango Miji ,mpima Ardhi, Katibu Mahsusi

Share:

Jafo Ataka Wanafunzi Kutozuiwa Kuandikishwa Sababu Ya Kukosa Vyeti Vya Kuzaliwa

Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Mb) amesema ni marufuku mwanafunzi kuzuiliwa kuandikishwa darasa la kwanza kwa sababu ya kukosa cheti cha kuzaliwa.

Jafo ameyasema hayo wakati wa ziara yake Wilayani Bahi kukagua uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza kwa shule za msingi pamoja na mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule za sekondari.

Jafo amesema amepokea malalamiko kutoka baadhi ya maeneo kuwa wanafunzi wa darasa la kwanza hawaandikishi kama hawana vyeti vya kuzaliwa.

“Nimeona nitoe ufafanuzi kuhusu suala hili kuwa cheti cha kuzaliwa ni haki  ya kila mtoto lakini isimzuie mtoto huyo kuanza shule eti kwa sababu tu hajapata cheti hicho; Watoto wote wapokelewa, waandikishwe na waanze masomo huku wazazi wao wakiendelea na mchakato wa kuwatafutia vyeti hivyo” alisisitiza Jafo.

Sitaki kusikia eneo lolote mtoto ameachwa kupokelewa na kuanza shule kwa sababu ya kukosa cheti cha kuzaliwa, mzazi ahakikishe ndani ya miezi minne amepata cheti hicho lakini mtoto huyo aanza masomo wakati masuala ya cheti yanaendea kushughulikiwa kwenye mamlaka husika aliongeza Jafo.

Akizungumza wakati akikagua mapokezi ya kidato cha kwanza amesema wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika muda uliopangwa na wapokelewe bila masharti ya kuleta unga, mahindi au maharage: 

Serikali inatoa Elimmsingi bila malipo hivyo kila mwanafunzi anatakiwa kupata elimu bila bugudha ya aina yeyote.

Waziri Jafo amepongeza uongozi wa Wilaya ya Bahi kwa umakini waliouonyesha katika zoezi zima za uandikishaji wa darasa la kwanza linaloendelea na maandalizi mazuri katika mapokezi ya kidato cha kwanza, halkadhalika katika usimamizi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya hiyo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Mwanahamisi Munkunda amesema katika Halmashauri ya Bahi walishafanya kampeni ya upatikanaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano hivyo watoto wengi wanaonza shule hivi sasa wanavyo vyeti hivyo na endapo mtoto yeyote atakua hajapa basi ataandikishwa shule ndipo mchakato kwa cheti utafuata.

Kwa upande wa mapokezi ya kidato cha kwanza amesema wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika Wilaya ya Bahi ni 2712 na changamoto iliyopo ni uhaba wa madawati ambayo wameshaanza kuitatua kwa kuchonga madawati yatakayokidhi idadi ya wanafunzi hao

Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Mkakatika John Laurent Josephat amesema shule yake ina malengo ya kaundikisha wanafunzi 180 na kwa siku ya kwanza tu shule ilivyofunguliwa wameandikisha wanafunzi 134.

“Wanafuzi wote walioletwa shuleni kwetu tumewaandikisha na endapo mtoto hana cheti cha kuzaliwa tulitumia kadi la Kliniki kupata taarifa sahihi za mtoto na hatujarudisha mwanafunzi hata mmoja wote wamewpokelewa na wameanza masomo” Alisema Mwl. Josephat.

Aliongeza kuwa uandikishaji huu kwa siku ya kwanza tu ni zaidi ya aslimia 70 hivyo anategemea tutaandikisha zaidi ya malengo waliyojiwekea.

Shule ya msingi Mkakatika ni miongoni mwa shule bora katika Wilaya ya bahi na ndiyo iliyoongoza kwa kuwa shule ya kwanza kiwilaya katika matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2019


Share:

Ndege ya Ukraine yaanguka Iran ikiwa na abiria 180

Ndege ya Ukraine aina ya Boeing-737 iliyokuwa na abiria 180 imeanguka Iran, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo.

Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la kimataifa la ndege la Ukraine ilianguka muda mfupi baada ya kuanza safari katika uwanja wa ndege wa Imam Khomeini mjini Tehran.

Ripoti za awali zinadai kuwa ndege hiyo ilikuwa safarini kuelekea mji mkuu wa Ukraine, Kyiv.

Haijabainika ikiwa ajali hiyo ina uhusiano wowote na mzozo wa Iran-na Marekani.

Kikosi cha uokoaji tayari kimetumwa katika eneo la tukio karibu na uwanja wa ndege, eneo ambalo ndege lilianguka.


Share:

Taarifa Ya Ongezeko La Hali Ya Joto Kwa Baadhi Ya Maeneo Nchini.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema kutakua na ongezeko la joto katika baadhi ya maeneo nchini, kufuatia kuwepo kwa hali ya unyevunyevu angani.

TMA imeyataja maeneo yatakayoathirika zaidi ni ukanda wa pwani yanayotarajiwa kuwa na kiwango cha juu cha joto cha nyuzi joto 32 hadi 34 hususan kwa maeneo ya Dar es Salaam, Tanga, Unguja na Pemba.

Taarifa kwa umma iliyotolewa jana Jumanne, Januari 7, 2020 na Mkurugenzi Mkuu TMA, Dk Agnes Kijazi imeeleza kwa kawaida kipindi cha Oktoba hadi Machi kila mwaka 2020 jua la utosi linakuwa katika maeneo ya kizio cha kusini mwa dunia.

Amesema Tanzania ikiwa ni moja ya nchi zilizopo katika kizio cha kusini, huwa na hali ya joto kali katika maeneo mengi ikilinganishwa na miezi mingine.




Share:

Breaking News: Iran Yarusha Makombora Na Kupiga Kambi za Jeshi la Marekani Huko Iraq

Jeshi la Iran (IRGC) limerusha makombora ya balestiki na kupiga kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq, kama jibu la kuuawa  Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha SEPAH.

Taarifa ya IRGC imesema kuwa, Iran imetoa jibu hilo kwa  Marekani alfajiri ya leo, ambapo imelenga uwanja wa ndege wa kijeshi wa Marekani wa Ain al-Assad katika mkoa wa al-Anbar, magharibi mwa Iraq.

Jeshi la Iran limeitaka Marekani iwaondoea wanajeshi wake wote katika nchi hiyo ya Kiarabu, likisisitiza kuwa halitatenganisha kati ya Marekani na Israel katika kujibu mapigo ya kuuawa  Jenerali  wao.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad javad Zarif amezungumzia  kuhusu jibu hilo la Iran katika ujumbe alioutuma kwenye ukurasa wake wa Twitter na kuandika: "Iran imechukua hatua madhubuti ya kujihami kwa mujibu wa Sura ya 51 ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kwa kulenga kambi ya jeshi ambayo ilitumiwa katika shambulizi la kioga dhidi ya raia na maafisa wetu wa ngazi za juu. Hatutaki kukuza mambo wala vita, lakini tutajihami dhidi ya uvamizi wowote."

Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) imethibitisha habari hizo za kuvurumishwa makumi ya makombora ya balestiki kuelekea katika kambi  ya jeshi la Marekani nchini Iraq.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano January 8



























Share:

Tuesday, 7 January 2020

Kesi ya Tito Magoti na mwenzie Yapigwa Kalenda tena

Upande wa Jamhuri umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika kesi inayimkabili Ofisa Elimu kwa Umma wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Tito Magoti (26) na mwenzake, Theodory Gyan (36), kuwa upelelezi katika shauri hilo upo katika hatua nzuri kukamilika.

Hayo ameyaeleza wakili wa serikali, Renatus Mkude, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka matatu likiwamo la utakatishaji fedha wa zaidi ya Sh. Milioni 10 ambapo ameomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Upande wa utetezi akiwemo Wakili Anna Henga ambaye ni Mkurugenzi wa LHRC, umeomba upande wa jamhuri kuharakisha upelelezi huo ili shauri hilo liweze kusikilizwa kwa wakati.

Akijibu hoja hiyo,  wakili wa serikali amesema watajitahidi kuharakisha upelelezi huo kwani mbali na kuhusisha jeshi la polisi pia unahusisha vyombo vingine.

Miongoni mwa mashitaka yao wanadaiwa Februari mosi, 2019 na Desemba 17, 2019 ndani ya jiji na mkoa wa Dar es Salaam kwa pamoja washtakiwa mengine ambao hawapo mahakamani walimiliki programu ya kompyuta iliyotengenezwa mahususi kwa ajili ya kutenda makosa ya jinai.

Washtakiwa hao wanasota korokoroni kwa sababu kesi yao ya uhujumu uchumi na haina dhamana.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger