Monday, 6 January 2020
Sunday, 5 January 2020
Mmiliki Mabasi ya Sahara Akutwa Amekufa Gesti
Mfanyabiashara na mmiliki wa mabasi ya Sahara, Abdalah Msangi (47) mkazi wa Usangi Mkoani Kilimanjaro, leo Jumapili Januari 5, 2020 amekutwa amekufa kwenye moja ya nyumba ya wageni iliyopo Mtaa Dar es Salaam Mjini Moshi.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Tanzania, James Manyama amethibitisha kutokea kwa kifo hicho.
Amesema mfanyabiashara huyo alikuwa na rafiki yake wa kike chumbani, lakini baada ya kuona mwenzake anaishiwa nguvu na kuanza kutokwa na povu puani na mdomoni akakimbia.
“Huyu Mfanyabiashara alikuwa na rafiki yake wa kike kwenye chumba cha wageni huko Dar es Salaam street, baada ya kuona ameishiwa nguvu na kuanza kutokwa na povu mdomoni alitoroka, amedai Kamanda Manyama.
Aidha, amesema baada ya kupata taarifa na kufika eneo la tukio na kulipekua gari la Msangi kulikutwa dawa ya kienyeji ambayo imechukuliwa kwa uchunguzi.
Amesema Mwili wa marehemu umepelekwa Hospitali ya Mkoa Mawenzi kwa uchunguzi zaidi.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Tanzania, James Manyama amethibitisha kutokea kwa kifo hicho.
Amesema mfanyabiashara huyo alikuwa na rafiki yake wa kike chumbani, lakini baada ya kuona mwenzake anaishiwa nguvu na kuanza kutokwa na povu puani na mdomoni akakimbia.
“Huyu Mfanyabiashara alikuwa na rafiki yake wa kike kwenye chumba cha wageni huko Dar es Salaam street, baada ya kuona ameishiwa nguvu na kuanza kutokwa na povu mdomoni alitoroka, amedai Kamanda Manyama.
Aidha, amesema baada ya kupata taarifa na kufika eneo la tukio na kulipekua gari la Msangi kulikutwa dawa ya kienyeji ambayo imechukuliwa kwa uchunguzi.
Amesema Mwili wa marehemu umepelekwa Hospitali ya Mkoa Mawenzi kwa uchunguzi zaidi.
WAVUTA BANGI TISHIO KITANGILI , VIBAKA NGOKOLO.... "TUNAKOMBWA MCHANA", MBUNGE ATAKA VITUO VYA POLISI KILA KATA
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele akizungumza katika kata ya Ngokolo wakati akifanya ziara yake kusikiliza kero za wananchi na kuzungumza na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Ngokolo leo Januari 5,2020. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkazi wa Ngokolo Rehema Mkono akimweleza Mbunge wake Stephen Masele kero ya vibaka wanaotishia amani katika mitaa ya Ngokolo.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele akizungumza katika kata ya Ngokolo na kuahidi kuzungumza na mamlaka mbalimbali ili kuhakikisha changamoto ya vitendo vya uhalifu katika Jimbo lake vinakomeshwa.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Songambele katika kata ya Kitangili Madeha Khamis akitoa kero ya wahalifu wanaotishia amani kwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele aliyetembelea kata hiyo Januari 4,2019.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele akizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Kitangiri na kupokea kero mbalimbali za wananchi Januari 4,2020.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele akizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Kitangili Januari 4,2020.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Vijana wanaovuta bangi na kunywa pombe aina ya gongo katika kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga wametajwa kuwa tishio na kuchochea vitendo vya ubakaji wa wanawake na watoto,kuvamia watu na kupora mali za wananchi huku vibaka Kata ya Ngokolo wakiwakosesha amani wananchi kwani sasa wanaiba mchana kweupe.
Hayo yamebainika wakati wananchi wakitoa kero zao kwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele alipofanya ziara katika kata 17 za Jimbo la Shinyanga kusikiliza kero za wananchi na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Kata zilizolalamikiwa kuongoza kwa vitendo vya uhalifu ni Ndala, Ngokolo na Kitangili katika mitaa ya Songambele,Busulwa na Kitangiri.
Wananchi hao walimweleza Mbunge wao Stephen Masele kuwa katika maeneo hayo wananchi wamekuwa wakiuawa,kuvamiwa na kuibiwa mali zao majumbani huku Jeshi la Polisi likidaiwa kutochukua hatua stahiki kwa wahalifu wanaosumbua mitaani.
Wakazi wa Kitangili walisema licha ya vijana wanaojihusisha na uvutaji bangi na kunywa pombe aina ya gongo kuwa tishio lakini kila wanapotoa taarifa jeshi la polisi limekuwa likichelewa kufika eneo la tukio na kushindwa kuchukua hatua kwa wahalifu hao.
"Ukubwa wa tatizo la uhalifu Kitangili ni pale tunapowaita polisi pindi panapotokea tukio huwa wanachelewa kufika kwenye matukio. Lakini pia huwezi amini kama kuna polisi wanawajua hao wavuta bangi na wanajua bangi zinakonunuliwa,wakikutana na wavuta bangi mtaani wanaishi vizuri na wavuta bangi ",walisema wananchi hao.
"Mhe. Mbunge hapa Kitangiri kuna tatizo la hawa vijana wanaovuta bangi,vijana hawa wanaovuta bangi hawalimi bangi wapo wanaolima na kuuza bangi na hatujui wanakonunulia bangi. Tunaomba wanaouza bangi wadhibitiwe kwani bangi na gongo ni kichocheo cha masuala ya ubakaji,kuvamia watu na wizi",alieleza Mwenyekiti wa Mtaa wa Songambele Madeha Khamis.
Naye Rehema Mkono mkazi wa kata ya Ngokolo alisema Ngokolo inakabiliwa na changamoto ya vibaka akisema hivi Sasa Ngokolo inazalisha kundi la 'Panya Road' bila kujua ambapo vijana wenye umri chini ya miaka 20 wamekuwa wakifanya vitendo vya uhalifu mchana kweupe kwa kuvizia nyumba za watu na kuiba mali.
"Ngokolo tunaibiwa mchana na usiku. Mimi mwenyewe nimeibiwa vitu ndani ya nyumba mchana kweupe 'Tunakombewa mchana kweupe' tunaomba tujengewe kituo cha polisi hapa Ngokolo ili kukomesha tatizo hili",alisema Mkono.
Kwa Upande wake,Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele alieleza kusikitishwa na vitendo vya uhalifu vinavyoendelea katika baadhi ya maeneo katika Jimbo la Shinyanga akisema upo umuhimu wa kujenga vituo vya polisi katika kila kata.
"Katika ziara yangu kutembelea kata 17 za Jimbo la Shinyanga nimepewa taarifa ya vitendo vya uhalifu nitazungumza na mamlaka mbalimbali ili kuhakikisha tunamaliza changamoto hii ili wananchi wetu wawe salama na mali zao",alisema Masele.
Masele ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika alianza ziara yake kukagua miradi ya maendeleo,kusikiliza kero za wananchi na kuzungumza na wajumbe wa kamati za siasa CCM ngazi ya matawi na kata zote 17 za Jimbo la Shinyanga Mjini kuanzia Desemba 27,2019 na kuhitimisha ziara yake Januari 5,2020.
Picha : MBUNGE MASELE ACHANGIA SHILINGI MIL. 13 KUSAIDIA UJENZI WA KITUO CHA AFYA NDEMBEZI, ZAHANATI YA NGOKOLO
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele amechangia shilingi milioni 11 kusaidia ujenzi wa kituo cha Afya cha kata ya Ndembezi kinachojengwa katika Mtaa wa Butengwa.
Akizungumza katika kikao chake na Viongozi wa CCM ngazi ya matawi na kata ya Ndembezi leo Jumapili Januari 5,2020,Mhe. Masele amesema katika awamu ya kwanza alitoa shilingi milioni tano na sasa anatoa shilingi milioni 6 kusaidia ujenzi wa zahanati hiyo ili kuwasogezea karibu wananchi huduma za afya.
“Ujenzi wa kituo cha afya Ndembezi ulianza kwa nguvu za wananchi,nilichangia shilingi milioni 5 na sasa naongeza tena shilingi milioni 6 na nimeomba serikalini shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi huu. Naamini pindi ujenzi utakapokamilika kituo kitawasaidia wananchi wa Ndembezi lakini pia wananchi wa kata za jirani”,alieleza Masele.
Akiwa katika kata ya Ngokolo,Masele pia ameahidi kuchangia shilingi Milioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa zanahati ya Ngokolo ili kuwasogezea huduma za afya wananchi.
“Nitaendelea kushirikiana na serikali na wadau mbalimbali kutatua changamoto za wananchi hususani katika sekta ya elimu,afya,barabara,maji na umeme kwani tunachohitaji ni wananchi wapate maendeleo",alisema Masele.
Mhe. Masele leo Jumapili Januari 5,2020 amehitimisha ziara yake iliyoanza Desemba 27,2019 kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo,kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuzungumza na wajumbe wa kamati za siasa CCM ngazi ya matawi na kata 17 za jimbo la Shinyanga Mjini.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Ndembezi leo Jumapili Januari 5,2020 wakati akihitimisha ziara yake Jimboni aliyoanza Desemba 27,2019. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Ndembezi.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Ndembezi.
Katibu wa CCM kata ya Ndembezi Pendo Sawa akizungumza kwenye kikao cha Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Ndembezi.
Mwenyekiti wa CCM kata ya Ndembezi Victor Thobias akitoa akizungumza kwenye kikao cha Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Ndembezi.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Shinyanga Mjini, Amri Migeyo akizungumza kwenye kikao cha Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele (CCM) na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Ndembezi.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Raphael Patrick Nyambi akizungumza kwenye kikao cha Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Ndembezi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Esha Stima akizungumza wakati wa ziara ya Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele katika kata ya Ndembezi.
Viongozi wa CCM ngazi ya matawi na kata ya Ndembezi wakiwa kwenye kikao na Mbunge Stephen Masele.
Viongozi wa CCM ngazi ya matawi na kata ya Ndembezi wakiwa kwenye kikao na Mbunge Stephen Masele.
Viongozi wa CCM ngazi ya matawi na kata ya Ndembezi wakiwa kwenye kikao na Mbunge Stephen Masele.
Viongozi wa CCM ngazi ya matawi na kata ya Ndembezi wakiwa kwenye kikao na Mbunge Stephen Masele.
Mbunge Masele akiongea jambo na Viongozi wa CCM kata ya Ndembezi baada ya kumaliza kikao chake.
Mbunge Masele akiwa na Viongozi wa CCM kata ya Ndembezi baada ya kumaliza kikao chake.
Viongozi wa CCM kata ya Ndembezi wakipiga picha ya kumbukumbu na Mbunge wao Stephen Masele.
Viongozi wa CCM kata ya Ndembezi wakipiga picha ya kumbukumbu na Mbunge wao Stephen Masele.
Wenyeviti wa mitaa ya kata ya Ndembezi wakipiga picha ya kumbukumbu na Mbunge wao Stephen Masele.
Mbunge Masele akiagana na Viongozi wa CCM kata ya Ndembezi baada ya kumaliza kikao chake.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Ngokolo leo Jumapili Januari 5,2020.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Ngokolo leo Jumapili Januari 5,2020.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Ngokolo leo Jumapili Januari 5,2020.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Ngokolo leo Jumapili Januari 5,2020.
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Mjini Shumbuu Katambi akizungumza wakati wa ziara ya Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele katika kata ya Ngokolo.
Katibu wa Mbunge Jimbo la Shinyanga Mjini Mwajuma Rabia akizungumza wakati wa ziara ya Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele katika kata ya Ngokolo.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Bunge Iraq lapiga kura kuwafukuza wanajeshi wa kigeni Baada ya Marekani Kumuua Jenerali wa Iran
Hatua hiyo imechukuliwa katika kikao cha dharura kilichoitishwa leo.
Azimio hilo hasa linalenga kumaliza makubaliano yaliyoafikiwa mika minne iliyopita yaliyoiruhusu Marekani kutuma vikosi vyake vya kijeshi kusaidia katika vita vya kupambana na kundi linalojiita Dola la Kiislam IS.
Kura hiyo imepigwa siku mbili baada ya Marekani kumuua jenerali wa kijeshi wa Iran Qassem Soleiman akiwa nchini Iraq.
Azimio hilo limeungwa mkono na wabunge wa madhehebu ya Kishia wenye mafungamano na Iran, ambao ndiyo wenye viti vingi bungeni.
Gonjwa la Ajabu Laikumba China
Mamlaka ya China imeanzisha utafiti kuchunguza virusi vinavyosababisha ugonjwa wa ajabu ambao umewaambukiza watu kadhaa katika mji wa Wuhan.
Kesi za watu 44 zimeripotiwa na kuthibitishwa hadi sasa, visa 11 kati yake vinatajwa kuwa hatari zaidi, maofisa wamesema
Mlipuko wa ugonjwa huo umefanya mji wa Singapore na Hong Kong kuanza kuchunguza watu wanaosafiri kutoka mji huyo.
Ugonjwa huo umezua hofu mtandaoni na kuhusisha virusi hivyo kuwa unaweza kusababisha kuwa na mtindio wa ubongo na madhara mengine yanayoweza sababisha vifo.
Uwezekano wa ugonjwa huo kufanana na ugonjwa wa ‘sars’ ambao uliua watu zaidi ya 700 ulimwenguni kote mwaka 2002-03, baada ya kutokea nchini China.
Kumekuwa na uvumi kwenye mitandao ya kijamii na kuhusisha ugonjwa huo kuwa unaambukiza kwa kasi sana.
Polisi wa Wuhan amesema kuwa watu wanane wameadhibiwa kwa kuchapisha taarifa za uongo katika mitandao bila ya kuwa na uhakika kuhusu ugonjwa huo.
Tume ya afya ya Wuhan imesema kuwa inafanya uchunguzi wa chanzo cha mlipuko wa ugonjwa huo.
Katika hotuba yake katika mtandao umesema kuwa tayari imeangazia vyanzo vya maambukizi ya ugonjwa huo na dalili zake lakini hotuba hiyo haikutaja kuwa unafanana na ugonjwa wa ‘Sars’ ambao uliwahi kusambaa duniani kote na kuua watu huku ukiwa umeanzia China.
Vilevile hakutaja iwapo kuna maambukizi ya kati ya binadamu na binadamu.
Hatua ya kuhusisha maambukizi hayo na soko la samaki, lilisababisha mamlaka kutaka kufanya usafi katika maeneo hayo.
Msemaji kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) amesema kuwa wana taarifa kuhusu ugonjwa huo na walikuwa wanawasiliana kwa karibu na Serikali ya China.
Jeshi la Kenya lazima shambulizi la al-Shabaab Lamu...Wanne Wauawa
Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) limetangaza habari ya kuwaua wanachama wanne wa kundi la kigaidi la al-Shabaab katika kaunti ya Lamu, kusini mashariki mwa Kenya, mpakani na Somalia.
KDF imesema katika taarifa kuwa, hakuna askari au raia aliyeuawa katika shambulizi hilo lililofeli la alfajiri ya leo mwendo wa saa kumi na moja, dhidi ya kambi ya jeshi iliyoviziwa na wanamgambo wa al-Shabaab, karibu na uwanja mdogo wa ndege wa Manda, eneo la Magogoni.
Kamishna wa Kaunti ya Lamu, Irungu Macharia amethibitisha kutokea uvamizi huo ambao al-Shabaab imekiri kuhusika nao. Hata hivyo Jeshi la Ulinzi la Kenya limefanikiwa kuzima shambulizi hilo kwa kutumia ndege ya kijeshi.
Duru za habari zinaarifu kuwa, kambi hiyo ya kijeshi ina askari wa Kenya na Marekani.
Haya yanajiri siku chache baada ya wapiganaji wa kundi hilo la kigaidi kuteka nyara basi la abiria katika kaunti hiyo ya Lamu, na kuua watatu miongoni mwao.
Siku ya Ijumaa, wanamgambo wasiopungua 33 wa kundi la kigaidi la al-Shabaab waliangamizwa katika operesheni mbili tofauti za jeshi kusini magharibi mwa Somalia.
Trump: Iran Wakithubutu Kulipa Kisasi Tutashambulia Maeneo Yao 52 Ndani ya Dakika Chache
Rais Donald Trump wa Marekani ameonya kuwa nchi yake itayashambulia haraka na vikali maeneo 52 ya Iran iwapo Jamhuri hiyo ya Kiislam itafanya mashambulizi dhidi ya raia wa Marekani na mali zake kulipiza kisasi kwa mauaji ya Jenerali Qassem Soleimani.
Katika ujumbe wa kitisho kupitia ukurasa wa Twitter, Trump amesema maeneo yatakayolengwa ni yale yaliyo muhimu kwa Iran na utamaduni wake na kuonya Marekani haiko tayari kuendelea kutishwa na Iran.
Ujumbe huo wa Trump unafutia onyo la makundi ya wanamgambo yanayoiunga mkono Iran la kuvishambulia vituo vya Marakani nchini Iraq kutokana na mauaji ya kamanda huyo muhimu wa jeshi la Iran.
Katika ishara za mwanzo za uwezekano wa kulipa kisasi, makombora mawili yalilipiga eneo lililo karibu na ubalozi wa Marekani mjini Baghdad siku ya Jumamosi.
Makombora mengine mawili yaliishambulia kambi ya kijeshi ambayo inahifadhi wanajeshi wa Marekani lakini hakuna athari kubwa zilizoripotiwa.
....targeted 52 Iranian sites (representing the 52 American hostages taken by Iran many years ago), some at a very high level & important to Iran & the Iranian culture, and those targets, and Iran itself, WILL BE HIT VERY FAST AND VERY HARD. The USA wants no more threats!— Donald J. Trump (@realDonaldTrump) January 4, 2020
Marekani yajiandaa na shambulizi la kulipiza kisasi kutoka Iran... Wanajeshi Wengine 3500 Kutumwa Mashariki ya Kati
Marekani kwa sasa inajiandaa na shambulizi la kulipiza kisasi kutoka Iran baada ya shambulizi lake la anga kumuua kamanda mkuu wa Iran, hatua ambayo imetia wasiwasi nchi zote duniani na hata kutiliwa shaka na baadhi ya wabunge wa Marekani.
Shambulizi la anga la Marekani Alhamis lilimuua Meja Jenerali Qassem Soleiman, mkuu wa kikosi cha Quds, pamoja na kamanda wa wanamgambo wa Iraq, karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad, na kuchochea vitisho vikali vya kulipiza kisasi kutoka kwa Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei.
Ikijibu tishio hilo linalozidi kuongezeka dhidi ya wafanyakazi na vituo vya Marekani katika Mashariki ya Kati, wizara ya ulinzi ya Marekani imetoa taarifa ikisema itasambaza kikosi huko Kuwait kama hatua ya tahadhari na sahihi, bila kutaja idadi ya wanajeshi.
Hata hivyo vyombo vya habari vya Marekani jana vilitangaza kuwa nchi hiyo itatuma zaidi ya askari 3,500 wikiendi hii. Na askari wengine wa ziada kutoka divisheni ya 82 ya askari wa parashuti watapelekwa Iraq, Kuwait na sehemu nyingine za kanda hiyo.
Shambulizi la anga la Marekani Alhamis lilimuua Meja Jenerali Qassem Soleiman, mkuu wa kikosi cha Quds, pamoja na kamanda wa wanamgambo wa Iraq, karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad, na kuchochea vitisho vikali vya kulipiza kisasi kutoka kwa Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei.
Ikijibu tishio hilo linalozidi kuongezeka dhidi ya wafanyakazi na vituo vya Marekani katika Mashariki ya Kati, wizara ya ulinzi ya Marekani imetoa taarifa ikisema itasambaza kikosi huko Kuwait kama hatua ya tahadhari na sahihi, bila kutaja idadi ya wanajeshi.
Hata hivyo vyombo vya habari vya Marekani jana vilitangaza kuwa nchi hiyo itatuma zaidi ya askari 3,500 wikiendi hii. Na askari wengine wa ziada kutoka divisheni ya 82 ya askari wa parashuti watapelekwa Iraq, Kuwait na sehemu nyingine za kanda hiyo.























