Friday, 3 January 2020

Mauaji ya Kamanda wa Jeshi la Iran: Marekani Yawataka Raia Wake Kuondoka Iraq Haraka....Jeshi la Israel Lawekwa Katika Hali ya Tahadhari Kubwa

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahuu ameikatiza ziara yake ya Ugiriki kufuatia kuuawa kwa Meja Jenerali Qassem Soleimani, mkuu wa jeshi maalum la Iran. 

Hayo ni kwa mujibu wa afisa mmoja kutoka ofisi ya Waziri Mkuu huyo. 

Netanyahu amekuwa mjini Athens kufuatia muafaka uliotiwa saini na Ugiriki, Cyprus na Israel hapo jana, wa kujenga bomba la kusafirisha gesi asili kutoka eneo linakopatikana mafuta la mashariki ya Mediterania hadi Ulaya.

 Redio ya Jeshi la Israel imeripoti kuwa jeshi la nchi hiyo liko katika hali ya tahadhari kubwa, likihofia ulipizaji kisasi wa Iran au washirika wake baada ya kuuliwa kwa Soleimani katika shambulizi la angani mjini Baghdad. 

Wakati huo huo, Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Marekani imewataka raia wa Marekani kuondoka nchini Iraq haraka iwezekanavyo. 

Shughuli za ubalozi wa Marekani mjini Baghdad zilisitishwa mapema wiki hii kufuatia mashambulizi kwenye jengo la ubalozi na wafuasi wa wanamgambo wanaoungwa mkono na Iraq.

Waziri mkuu wa Iraq anaeondoka Adel Abdul-Mahdi amelaani mashambulizi ya Marekani na kuitishia kikako cha dharura cha Bunge kuchukuwa kile alichokiita hatua stahiki zinazohitajika ili kulinda hadhi, mamlaka na uhuru wa Iraq.

Mataifa mengine pia yamezungumzia mauaji hayo ambapo Urusi imesema yanaweza kuchochea zaidi mzozo katika kanda ya Mashariki ya Kati, huku Ufaransa ikisema mauaji ya Soleimani hayatatuliza mzozo bali yatauchochea zaidi.

China kwa upande wake imeomba pande zote kujizuia huku utawala wa Syria ukilaani pia mauaji hayo uliyoyataja kama ya kiuoga kwa upande wa Marekani.


Share:

Mume Atolewa Utumbo na Mkewe Kisa Kuhoji Matumizi ya Tsh. 10,000 Aliyoacha

Benedictor Gogogo (48) mkazi wa Itabagumba, Sengerema mkoani MWANZA amechanwa tumbo na kitu chenye ncha kali hadi utumbo kutoka nje baada ya kutokea ugomvi kati yake na mke wake

Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Jumanne Murilo amesema tukio hilo lilitokea jana na wanamashikilia Mtuhumiwa kwa mahojiano na uchunguzi zaidi

Akiwa hospitalini, Gogogo amesema mzozo kati yake na mke wake aliyemtaja kwa jina la Mama Asteria ulitokana na kuhoji matumizi ya Tsh. 10,000 aliyoacha nyumbani asubuhi ya siku hiyo

Amesema, “Wakati naondoka kwenda kwenye shughuli zangu za uvuvi, asubuhi ya siku ya tukio, niliacha Tsh. 10,000 ya matumizi. Niliporejea nilimwomba anipe Tsh. 1,000 ninunulie vocha ya simu lakini akaniambia fedha yote imeshatumika.”

Ameongeza, “Nilipohoji zaidi akaanza kunitolea majibu yaliyonikasirisha na kunifanya nimpige kofi na kutokea mzozo kati yetu ambao hata hivyo uliisha na mimi kuingia ndani kujipumzisha.”

Aidha, Gogogo ameeleza kuwa akiwa ameanza kupitiwa usingizi, mke wake ambaye wameishi mwaka mmoja na nusu sasa alimvizia na kumchana na kitu chenye ncha kali tumboni hadi utumbo kutoka nje


Share:

Wazazi Wa Watoto Walikuwapotea Mkoani Mbeya Wakabidhiwa Watoto Wao

Na Daud Tiganya
SERIKALI Mkoani Tabora imewakabidhi watoto wawili waliokuwa wamepotea mkoani Mbeya kwa wazazi wao wakiwa na afya njema.

Hatua hiyo inatokana na kupatikana mmoja wao akiwa na mama mmoja Hawa Ally katika Hospitali ya Wilaya ya Nzega baada ya wasamaria wema kuwa na wasiwasi na mtuhumiwa na kutoa taarifa Polisi.

Akikabidhi watoto hao leo Mkuu wa Mkoa wa Tabora ametoa onyo kwa wale wote wanaohusika na vitendo vya aina hiyo ikiwemo kuiba watoto wachanga na kwamba Serikali itahakikisha inawachulia hatua kali za kisheria.

Aliwataka wito kwa wazazi kuwa karibu na watoto wao badala ya kuwategemea wasaidizi wa kazi ndio watumike kuwalea muda mwingi ili kujiepusha na majanga kama haya.

Aidha Mwanri  aliwashukuru wananchi, Jeshi la Polisi kwa ushirikiano wao waliouonyesha na kupelekea kupatikana kwa watoto hao wakiwa na afya njema.

Kwa upande wa baba mzazi wa watoto hao ambaye ni mtumishi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mashaka Juma baba alisema watoto wake walipotea nmamo Desemba 28 mwaka uliopita.

Alisema mtoto wake mmoja akiwa na miaka mitano na mwingine mwaka mmoja na nusu walipotea wakati yeye na mkewe wakiwa wamekwenda sokoni kununua mahitaji na waliporudi ndipo walipobaini hawapo nyumbani kwao.

Juma alivishukuru vyombo vya habari na viongozo wa mikoa ya Mbeya na Tabora pamoja na wananchi huku akisema bado hajaamini kama kweli watoto wake wamepatikana tena wakiwa hai.

Mama wa watoto hao,Zuhura Kaswa,alisema bado haamini na kwamba alipotaa taarifa za watoto wake kupotea alikuwa akilia na kumuomba Mungu muda wote.

Wakati huo huo mtuhumiwa anayedaiwa kuwatorosha watoto wawili wa mkoani  Mbeya na kumtelekeza mtoto mmoja nyumbani kwa mtu eneo la Chechemi katika Manispaa ya Tabora Hawa Ally anashikiliwa na Jeshi la Polisi.

Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Tabora Baraka Makona alisema kuwa mtuhumiwa huyo alimuachia mtoto mkubwa mwenye umri wa miaka mitano kwa nyumba ya mkazi wa Chemichemi kwa madai anaenda na mdogo ili kumtafutia matibabu na kuahidi kurudi baadaye.

Alisema mtuhumiwa hakurudi siku hiyo mwishoni mwa mwaka jana,jambo lililomfanya mwananchi aliyetelekezewa mtoto,kutoa taarifa Polisi kesho yake siku ya mwaka mpya.

Baraka aliongeza mtuhumiwa alienda na mdogo hadi Nzega na kumpeleka Hospitali kutokana na kuugua na ndipo ilipogundulika sio mtoto wake na wasamaria wema kutoa taarifa polisi na mtuhumiwa kukamatwa.

Alisema baada ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kupata taarifa za kupotea kwa watoto hao,walifuatilia na kugundua mtoto mkubwa katelekezwa Manispaa ya Tabora na mdogo akipatikana Mjini Nzega.

Mwisho.


Share:

Jenerali Qassem Soleimani Wa Jeshi la Mapinduzi la Irani Aliyauawa na Marekani Leo ni Nani Hasa?

Tangu miaka ya 80, Meja Jenerali Qasem Soleimani ameongoza vikosi vya kikurdi nchini Iran- kitengo maalum cha jeshi la Iran (Revolutionary Guards) ambacho huendesha opareshani zake nje ya nchi.

Kwa sehemu kubwa aliwakilisha taswira ya ustahamilivu wa kitaifa katikati ya miongo minne ya mbinyo wa Marekani.

Jenerali Soleimani amekuwa shujaa nchini Iran kutokana na juhudi zake za kuipinga Marekani.

Kwa Marekani na Israel  Soleimani alikuwa kiongozi hatari, aliye nyuma ya vikosi vinavyoungwa mkono na Iran na anayehusika na wapiganaji wanaoitetea serikali ya rais Bashar Al Assad nchini Syria.

Kadhalika alibebeshwa wajibu wa vifo vya wanajeshi wengi wa Marekani nchini Iraq.

Soleimani alivishinda vishindo vya vita ya muda mrefu ya Iran dhidi Iraq miaka ya 1980 ili kuchukua nafasi ya kuongoza kikosi cha Quds kilicho sehemu ya kikosi kipana cha walinzi wa mapinduzi ya Iran.

Kikosi cha Quds ndiyo kinahusika na kampeni zote za kijeshi za Iran kwenye mataifa ya kigeni.

Jenerali huyo hakuwa akifahamika na wengi nchini Iran hadi mwaka 2003 wakati Marekani ilipoivamia kijeshi Iraq.

Wasifu na umashuhuri wake uliimarika hatua iliopelekea maafisa kadhaa wa Marekani kutoa wito wa kuuliwa kwake.

Muongo mmoja na nusu baadae Soleimani alifikia kuwa kamanda maarufu wa vita nchini Iran kiasi akipuuza miito ya umma kumtaka aingie kwenye siasa.

Kwa jenerali Soleimani nafasi ya kisiasa haikuwa na umuhimu mkubwa kwa sababu kutokana na ushawishi wake jeshini alifikia nafasi ya kuwa mtu mwenye nguvu nchini Iran pengine kuliko utawala wa kiraia.

Kifo chake kimekuja baada ya kuzushiwa mara kadhaa kufikwa na umauti. Soleimani alizaliwa mwezi Machi mwaka 1957 na kukulia kwenye mji wa kihistoria wa Rabor nchini Iran.

Jina lake liianza kuzingatiwa alipopewa nafasi ya kuongoza kikosi cha Quds na kujenga ukaribu  na kiongozi mkuu wa kidini Ayatollah Khamenei kiasi wakati mmoja Kiongozi  huyo alishiriki na kufungua dhifa ya harusi ya binti ya Jenerali Soleimani.
 
Akiwa mkuu wa kikosi cha Quds Soleimani alisimamia operesheni za kijeshi nje ya Iran na kuingia kwenye uhasama na Marekani wakati wa vita vya Iraq akionekana kuwa mfadhili wa makundi ya wanamgambo wa kishia.

Mwaka 2007 Marekani na Umoja wa Mataifa walimjumisha Soleimani katika orodha ya watu waliowekewa vikwazo lakini aliendelea kusafiri maeneo mbali mbali duniani.

Umashuhuri uliimarika zaidi wakati wa vita vya Syria na kutanuka kwa kundi linalojiita dola la kiislam. Iran ilimtuma Soleimani mara kadhaa nchini Syria kuongoza mashambulzii dhidi ya kundi la IS na makundi yanayopinga utawala wa Bashr Al Assad.

Jenerali huyo alipata mafanikio makubwa kwenye mapambano ya ardhini na alikuwa alama ya ushindi katika vita dhidi ya IS na kuendelea kulipa nuru jina lake, zaidi katika viwambaza vya dola na mioyoni mwa raia wengi wa Iran.


Share:

Taarifa Toka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais IKULU

Rais Magufuli ametoa wito kwa Watanzania wengi zaidi kujitokeza kufuga wanyamapori kupitia bustani za wanyama(Zoo) ili kuongeza idadi ya Wanyamapori hao na kupanua fursa za Utalii na ajira,kwa sasa Tanzania ina Zoo 23, Mashamba ya wanyama 20 na ranchi 06.





Share:

Polisi Tabora Kuanza Msako Wa Wanaotaka Kujinyonga 2020...."Tutawakamata Kabla Hawajajinyonga"

Baada ya kupokea taarifa ya Watu wawili kujinyonga mpaka kupoteza maisha Tabora, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Barnabas Mwakalukwa amesema Polisi wataanza msako wa kuwabaini na kuwakamata wote wanaotarajia kujinyonga mwaka huu na kuwapelekea Mahakamani.

Kwa mujibu wa RPC Mwakalukwa, walijionyonga ni  Mwalimu Basil Sungu (39) wa shule ya msingi Ikongolo Wilaya ya Uyui mkoani Tabora ambaye  amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kipande cha kitenge cha mke wake.

Amesema mwili wa Sungu ulikutwa chumbani kwake ukiwa unaning’inia darini Jumanne iliyopita ya Desemba 31, 2019.

Mwingine ni James Albert (22), mjasiriamali na mkazi wa kata ya Chemchem Manispaa ya Tabora ambaye amekutwa amejinyonga hadi kufa kwa kutumia mkanda wa begi.

“Niwambie mwaka huu tabia hizo zikome kwa wanaotegemea kujinyonga tutaanzisha doria kuhakikisha wote wanaotarajia kujinyonga mwaka huu tunawakamata kabla hawajinyonga na tunawapelekea mahakamani” Amesema RPC  Mwakalukwa huku akisema uchunguzi dhidi ya matukio haya mawili unaendelea ili kujua chanzo


Share:

Mtoto atuhumiwa kumuuwa baba yake Ludewa

Na Amiri kilagalila-Njombe
Mzee Jonaidi Haule (72) mkazi wa Mawengi wilayani Ludewa Mkoani Njombe amesababishiwa kifo kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali na mwanae kutokana na ugomvi wa kifamilia.

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema baada ya ugomvi kuibuka na kusababisha  hali ya kuto kuelewana kati ya mtoto na baba yake, ,mtoto aliyefahamika kwa jina la Jailos Thomas Haule alichukua kitu chenye ncha kali na kumjeruhi baba yake.

Kamanda amesema mara baada ya kujeruhiwa mzee huyo alifikishwa  katika matibabu hospitali ya wilaya ya Ludewa na kupoteza maisha mara baada ya hali yake kuwa mbaya zaidi.

Aidha kamanda wa polisi amesema jeshi hilo linamtafuta mtuhumiwa Jailos Haule aliyetokomea kusikojulikana kwa tuhuma za kesi ya mauaji.


Share:

Iran Yaapa kulipiza kisasi kwa Marekani kufuatia mauaji ya kamanda Mkuu wa Jeshi lake la Quds

Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amesema, nchi hiyo itajibu vikali mauaji ya kamanda wa Kikosi cha Mapinduzi ya Kiislam (IRGC) Meja Jenerali Qassem Soleimani.

Khamenei amesema lengo la Soleimani na harakazi zake za ukombozi hatitasimama kutokana na kifo chake, bali zitaendelea kwa nguvu zaidi, na ushindi dhahiri unawasubiri wale wanaopigana katika njia hiyo.

IRGC leo imethibitisha kuwa, Meja Jenerali Soleimani ameuawa katika shambulizi la anga lililotokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad.

Kiongozi huyo ametangaza siku tatu za maombolezo kufuatia kifo cha Soleimani.

Wakati huohuo, Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema, jeshi lake lilifanya shambulizi lililomuua kamanda huyo wa IRGC.


Share:

Breaking News: Marekani Yamuua Kwa Kombora Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Irani....Bei Ya Mafuta Duniani Yapanda

Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah) Meja Jenerali Qassem Solaimani na naibu mkuu wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq, al Hasdul Shaabi, Abu Mahdi al Muhandes wameuawa shahidi mapema leo Ijumaa katika shambulizi la roketi lililofyatuliwa na helikopta ya Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad nchini Iraq.

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad mapema leo umeshambuliwa kwa maroketi ya helikopta za Marekani. Maafisa wa Marekani wamekiri katika mahojiano yao na shirika la habari la Reuters kwamba, shambulizi hilo limefanyika dhidi ya watu wawili wenye mfungamano na Iran.

Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Javad Zarif, ametaja hatua hiyo kuwa "hatari na uchokozi wa kishenzi".

Gen. Soleimani alikuwa mtu mashuhuri kwa utawala wa Iran. Kikosi chake cha Kikurdi kilikuwa kinaripoti moja kwa moja kwa kiongozi mkuu wa kidini wa Iran Ayatollah Ali Khamenei na alisifiwa kama shujaa wa kitaifa.

Rais wa Marekani Donald Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter picha ya bendera ya Marekani baada ya kutangazwa kuuawa kwa jenerali hiyo.

Bei ya mafuta duniani imepanda kwa asilimia nne baada ya shambulio hilo.

Ripoti za vyombo vya habari vya Marekani zinasema kuwa Jenerali Soleimani na maafisa wa waasi wanaoungwa mkono na Iran nwalikuwa wakiondoka katika uwanja wa ndege wa Baghdad kwa kutumia magari mawili wakati waliposhambuliwa na ndege za Marekani zisizokuwa na rubani karibu na eneo kuweka mizigo.

Kamanda huyo aliripotiwa kusafiri kutoka Lebanon au Syria. makombora kadhaa yaliripotiwa kushambulia msafara wao, ambapo karibu watu watano wanaaminiwa kuawa.

Taarifa iliyotolewa na Pentagon ilisema: "Kufuatia agizo la rais, vikosi vya jeshi la Marekani vilichukua hatua ya kuwalinda wafanyikazi wake nje ya nchi kwa kumuua Qasem Soleimani,"

"Hatua hii ililenga kudhibiti mipango ya Iran ya mashabulio ya siku zijazo. Marekani itaendelea kuchukua hatua madhubuti kuwalinda watu wetu na maslahi yetu kote duniani," ripoti hiyo iliendelea kusema..

Pentagon inasema jenerali Soleimani aliidhinisha mashambulio dhidi ya ubalozi wa Marekani.


Share:

CCM Yaahidi Kuheshimu Maamuzi Ya Umma Uchaguzi Mkuu 2020

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally amesema kuwa, CCM mwaka 2020 itaongoza siasa safi za uchaguzi, ni mwaka wa kudhihirisha CCM inaongoza siasa safi na kuheshimu maamuzi ya Umma kama ilivyofanya mwaka 2019.

Dkt. Bashiru ameeleza kuwa, CCM itakuwa mfano katika kuheshimu uamuzi wa umma katika uchaguzi, na CCM itashinda kwa kura nyingi kwa kuwa, zipo sababu nyingi za kuaminiwa na umma.

Dkt. Bashiru ameyasema hayo jana Januari 02, 2020 wakati akitoa salam za mwaka mpya 2020 katika mkutanao wa ndani wa wenyeviti wa mitaa na vijiji wilaya ya Bukoba mkoani Kagera.

“CCM inatoa salam za mwaka mpya 2020, niwahakikishie wananchi wote wa Tanzania, mwaka huu tutaongoza siasa safi, na ni mwaka wa kudhihirisha CCM inaongoza siasa safi na kuheshimu maoni na uamuzi wa Umma, na itashinda kwa kishindo kwa kuwa wananchi walihitaji huduma ya maji sasa wanapata, walihitaji elimu bure sasa wanapata, walihitaji huduma za afya sasa wanapata na zingine nyingi, na siku zote wananchi sio wanafiki.”

Aidha ameongeza kuwa, Wapo watu wanalilia tume huru iwasaidie kupata ushindi, bila kufahamu kuwa, Tume huru haipigi kura bali inasimamia uchaguzi, kama chama hakina wapiga kura kisitegeme Tume iwape ushindi, CCM imewatafuta wapiga kura kwa kuwasomesha watoto bure, kutoa mikopo kwa wanafunzi, kujenga vituo vya afya, kusambaza maji, kujenga barabara, sasa wao waseme hao wapiga kura wamewapata kwa njia zipi kama ambavyo CCM inajipambanua.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu ameeleza msimamo wa CCM kuendelea kutetea haki za watu wote bila kujali jinsia, rika, dini wala kabila, ambapo akifafanua hilo amesema,

“CCM inapingana na udharirishaji ambao mara nyingi unajitokeza katika Uchaguzi Mkuu, wanawake kabla ya kugombea wanaitwa majembe lakini wakichukua fomu za kugombea wanaanza kuchimbwa na kuwekewa kashfa nyingi, wanajazwa hofu na wanaogopa, awamu hii CCM haitakubali wanawake wadharirshwe na haki ni lazima itendeke kwa wote.’’

Awali akimakaribisha Katibu Mkuu, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Bi. Costancia Buhiye amesisitiza zaidi umoja na mshikamo ndani Chama ambapo Katibu wa CCM wa Mkoa huo Ndg. Michael Chonya akisistiza umuhimu wa viongozi kusikiliza na kutatua kero za watu.

Katibu Mkuu yupo Bukoba mkoani Kagera kwa mapumziko ya siku kumi ambapo anatarajiwa kumaliza mapumziko hayo mwanzoni mwa mwezi Januari, 2020.


Share:

Taarifa Ya Ajali Ya Gari Kuungua Moto Na Kusababisha Majeruhi Na Uharibifu Wa Mali Mkoani Mbeya.

Mnamo tarehe 02.01.2020 majira ya saa 16:05 jioni huko eneo la Meta-Igurusi katika barabara kuu ya Mbeya/Njombe,  
Gari lenye namba za usajili T. 956 DRT/T. 886 DRV aina ya Scania Tanker la Mafuta mali ya kampuni ya “world oil” lililokuwa limepakia mafuta aina ya Petroli kutokea Dar es salaam kuelekea nchini Zambia likiendeshwa na dereva ISSA YUSUPH [35] mkazi wa Jijini Dar es Salaam lilipata hitilafu za kiufundi siku ya tarehe 01/01/2020 majira ya saa 16:30 jioni na baadae liliungua moto na kuteketea wakati wa harakati za kufaulisha mafuta kwenye gari hiyo kwenda kwenye gari namba T 844 AWJ Trailer na kusababisha majeraha kwa watu wawili.

Watu waliojeruhiwa katika ajali hiyo ya moto ni:-

1.    JULIUS DAUDI [30]

2.    STANFORD MWAKYUSA [45]

wote wakazi wa Igurusi Wilayani mbarali.

Aidha katika ajali hiyo kulitokea uharibifu kwa gari namba SM 4633 aina ya Isuzu mali ya Jeshi la Zimamota na Uokoaji na gari namba T 844 AWJ Trailer. 

Chanzo cha ajali ni mlipuko uliotokea kwenye mashine ya kufaulishia mafuta aina ya “water pump”. Majeruhi wamekimbizwa kituo cha afya igurusi kwa matibabu.

Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Share:

BRELA Yaongeza Muda Wa Kuhuisha Taarifa Za Makampuni Na Majina Ya Biashara




Share:

Watoto Waliopetea Mbeya Wapatikana Mkoani Tabora




Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa January 3





















Share:

Thursday, 2 January 2020

JAMAA WAWILI WAFIKISHWA MAHAKAMANI BAADA YA KUIBA POMBE


Jamaa wawili wamefikishwa mahakamani Jumanne ,Disemba 31, 2019 baada ya kukashifiwa kwa kuiba chupa sita za pombe aina ya Jameson.



 Daniel Mbugua na Cliff Obonyo ambao ni wafanyakazi wa kampuni ya Mitchel Cot wanasemekana kutekeleza kitendo hicho Disemba 17, wakiwa mtaani Embakasi. 

Pombe hiyo ni ya thamani ya KSh 15,000. 

Washukiwa hao wanasemekana kuficha pombe hiyo kwenye gari la kampuni ambalo husafirisha mizigo na bidhaa.

 Wawili hao walikana mashtaka dhidi yao na kuachiliwa kwa dhamana ya KSh 20,000 kila mmoja. Kesi dhidi yao itasikizwa tena Aprili 28, 2020. 
Share:

JAMAA ANYWA MIKOJO YA WANAWAKE LITA MOJA NA NUSU


Jamaa mmoja nchini Uganda aliyetambulika kwa jina la Ismail Dholaga mwenye miaka 35, amelazimika kunywa lita moja na nusu ya mikojo ya wanawake ili kurejesha fahamu baada ya kulewa tilalila.

Ismail Dholaga ambaye anafanya kazi ya udereva wa pikipiki (bodaboda) alilazimishwa kufanyiwa kitendo hicho na wakazi wa eneo la mji wa Iganga, baada ya kukutwa akiwa amelewa na wapita njia.

Wakazi wa eneo hilo na wapita njia walikusanya mikojo ya wanawake waliokuwepo kwenye tukio, ikapatikana lita moja na nusu, mmoja wa wanawake waliotoa huduma hiyo amesema “Tulifaulu kupata lita moja unusu ya mkojo na kumlazimisha kunywa kama huduma ya kwanza”.

Hata hivyo huduma hiyo haikufanikiwa ndipo maafisa wa polisi walifika na kumkimbiza katika hosptali iliyokuwa karibu.
Share:

Taarifa Kwa Umma: Usimamizi Kwa Watoa Huduma Ndogo Za Fedha




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger