Monday, 21 October 2019

Tanzania Yateuliwa Kuwa Mwenyeji Wa Mkutano Wa Mawaziri Sekta Za Mazingira, Maliasili Na Utalii SADC

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo amefungua mkutano wa Mawaziri wa Sekta za Mazingira, Maliasili na Utalii wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Arusha kaskazini mwa nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki, amesema kuwa, mkutano huo utajadili mwenendo wa hali ya mazingira, mabadiliko ya hali ya hewa na hali ya utalii na misitu katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Aidha amesema kuwa, mkutano huo utajadili utekelezaji wa mikakati ya hifadhi na usimamizi wa mazingira na kupitia mikakati na miongozo juu ya masuala hayo katika kutekeleza majukumu ya kila nchi ndani ya jumuiya hiyo ya SADC.

Wakati huo huo, Tanzania imekabidhiwa Uenyekiti wa Shirikisho la Mashauriano ya Kisheria la Asia na Afrika (Asian-African Legal Consultative Organization (AALCO) 58th Annual Session).

Mkutano huo umefunguliwa na mikutano ya Wataalamu wa Sekta ya Wanyamapori na mkutano wa Makatibu Wakuu wa Sekta za Mazingira, Maliasili na Utalii ulioanza leo Oktoba 21 hadi 24, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Mapema mwezi Agosti mwaka huu, nchi ya Tanzania ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa 39 wa nchi wanachama wa Jumuiya ya maendelea ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Rais John Pombe Magufuli alikabidhiwa na kupokea rasmi jukumu la uenyekiti wa jumuiya hiyo.


Share:

Upelelezi kesi ya anayedaiwa kumuua mkewe kwa Kumchoma Moto Wakamilika

Hatimaye upelelezi wa kesi inayomkabili mfanyabiashara Khamis Said anayedaiwa kumuua na kisha kumchoma na moto wa magunia mawili ya mkaa mke wake, Naomi Marijani, na kisha mabaki ya mwili huo kwenda kuyafukia shambani kwake Mkuranga, umekamilika.

Wakili  wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai hayo leo Jumatatu Oktoba 21, 2019 mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam kuwa shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi umekamilika.

Simon amedai jalada la shauri hilo lipo kwenye hatua ya uchapaji kwa ajili ya maandalizi ili lipelekwe Mahakama Kuu ya Tanzania hivyo ameiomba mahakama hiyo ihairishe kesi hiyo.
 
Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mkuu wa Mahakama hiyo, Salumu Ally, aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 4, 2019.

Mshtakiwa huyo anadiwa kutenda kosa hilo Mei 15, 2019, nyumbani kwake maeneo ya Gezaulole Kigamboni.


Share:

Kilichoendelea Leo Mahakamani Katika Kesi ya Mbowe na Vigogo wengine CHADEMA

Viongozi 9 wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wanatarajia kuanza kujitetea kwa siku tatu mfululizo kuanzia November 4, 5 na 8, 2019 katika kesi ya uchochezi inayowakabili Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Hatua ya viongozi hao wanaokabiliwa na Kesi ya jinai namba 112 ya 2018 inatokana na uamuzi mdogo uliotolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo katika uamuzi huo Viongozi wa CHADEMA wamewakilishwa na Wakili, Jeremiah Mtobesya na Hekima Mwasipu, huku upande wa Serikali ukiwakilishwa na Wakili Faraja Nchimbi, Wankyo Simon na Salim Msemo.

Akitoa uamuzi huo, Hakimu Simba amesema wiki tatu zilizoombwa na upande wa utetezi ni nyingi  hivyo amewapatia wiki mbili ili waweze kuwaanda washtakiwa waanze kujitetea kabla ya mashahidi wao na kusema mashahidi katika kesi hiyo mbali na washtakiwa ni wengi na wanafikia 200, hivyo upande wa utetezi wanahitaji kupewa muda wa maandalizi.

Pia Hakimu Simba amesema kuhusu kielelezo namba 5 ambacho ni video ya maandamano kilichoombwa na upande wa utetezi ili Wataalamu wao wakichunguze kwa sababu wana wasiwasi kimehaririwa, watakitumia kupitia vifaa vya mahakama kama vilivyotumiwa na upande wa mashtaka.


Share:

Announcement For Australia Awards Scholarships Short Courses) For 2020/2021

Applications are invited qualified officials from Public & Private Institutions to apply for the above-mentioned training opportunities in Australia.

Applications are now open for the following Tenable Training Programs:-

Mode of Application:
• Application forms and other relevant documents can also be found on the relevant COUNTRY PAGE


• All applications should be submitted electronically as per instructions on the Website


Closing dates for applications:
i. Short Course Awards: 17th January, 2020.
N.B: - Applications from people with disability are strongly encouraged.
- Applications from women are strongly encouraged.


Kwa taarifa zaidi, <<Bonyeza hapa>>


Share:

Serikali ya Tanzania na Barrick waunda Kampuni Mpya ya Kusimamia Madini inayochukua nafasi ya Kampuni ya Acacia.

Jitihada za Rais John Magufuli za kuhakikisha rasilimali za Tanzania zinalindwa, zimeanza kuzaa matunda baada ya serikali na Kampuni ya Barrick Gold Corporation kuingia ubia na kuanzisha kampuni mpya ya Twiga Mining Co. Ltd inayochukua nafasi ya Kampuni ya Acacia.

Kampuni ya Twiga iliyosajiliwa nchini na makao yake makuu yatakuwa Mwanza, Serikali ya Tanzania itamiliki asilimia 16 na Barrick Gold Corporation itakuwa na asilimia 84.

Sasa ndio itakayosimamia migodi mitatu iliyokuwa inasimamiwa na Acacia ambayo ni Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara na itaendesha shughuli zake zote nchini.

Hatua hiyo, imekuja baada ya Kampuni ya Barrick kuizika rasmi Acacia na kufunga ofisi zake zilizokuwepo jijini London, na kufuta kesi na madeni yote ambayo kampuni hiyo ya Acacia iliyafungua dhidi ya serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi alisema hatua hiyo imeingiza Tanzania katika historia mpya ya ukombozi wa kiuchumi.

Alisema kuanzishwa kwa kampuni hiyo mpya sasa kumefuta migogoro yeyote iliyokuwepo baina ya serikali na Acacia ambayo hisa zake za asilimia 63.9 zote zilinunuliwa na hivyo kumilikiwa na Barrick Gold Corporation.

Alieleza kuwa pamoja na kufuta migogoro hiyo, pia wamekubaliana kuwa Barrick itailipa Tanzania kiasi cha dola za Marekani milioni 300 kwa ajili malipo ya kodi zote zilizokuwa haijalipwa na migogoro mingine.


Share:

TPDC -Kuunganisha Gesi Asilia Katika Nyumba 400 Mwaka Huu

NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
SHIRIKA la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) linatarajia kuunganisha nyumba 400 kupitia mradi wa kuunganisha gesi asilia majumbani ,ambapo kati ya nyumba hizo nyumba125 zitakuwa mkoa wa Mtwara na nyingine  mkoa wa Dar es Salaam.
 
Aidha mpaka sasa viwanda 45 vinafanya uzalishaji kwa kutumia gesi inayosambazwa na TPDC na miongoni mwa viwanda hivyo ni DANGOTE kilichopo mkoani Mtwara na Goodwill kilichopo Mkiu wilayani Mkuranga ,mkoani Pwani.
 
Mtaalamu mwandamizi wa masuala ya Petroli(Geologist)kutoka TPDC Simon Zablon,alisema hayo katika  maonyesho ya bidhaa za viwandani yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Pwani Mjini Kibaha.
 
Alisema, nyumba hizo zinatarajiwa kukamilishwa mwishoni mwa mwaka huu.
 
Zabron alisema,katika upande wa  viwanda ambavyo vitanufaika na mradi huo ni kiwanda cha Lodhia, NAF na Cokacola .
 
“TPDC tupo tayari kutoa huduma ya gesi  kwa urahisi kwenye viwanda vyote vilivyopo katika Mikoa ya Mtwara na Dar es Salaam na ambavyo miundombinu ya bomba la gesi imepita”
 
Katika hatua nyingine, alifafanua magari yanayotumia gesi hadi sasa yamefikia 200, na  kwamba magari yanayounganishwa na huduma hiyo ni yale yaliyokuwa kwenye mfumo wa kutumia petroli.
 
Alisema, awali mradi wa kuunganisha gesi kwenye magari ulianza miaka saba iliyopita lakini ulikuwa unasuasua kutokana  muamko kwenye vituo vya mafuta kuwa mdogo .
 
Zabron alielezea pia kumetokana na kituo kimoja kilichokuwa Ubungo jijini Dar es salam pekee kutoa huduma hiyo tofauti na hali ilivyo sasa.


Share:

Punguzo la bei ya Viwanja: Bunju na Mapinga (Baobab sec)


Kwa Mapinga vipo viwanja vya 15/20 bei tsh 3 milion, 20/20 kwa tsh 4 milion, 25/25 kwa tsh 7 milion, sqm 2000 kwa tsh 25 milion, sqm 2400 kwa tsh 30 milion.


Viwanja hivi viko umbali wa km 3 kutoka main road (Dar to Bagamoyo Road)

Kwa Bunju vipo viwanja vya sqm 1000 kwa tsh 30 milion na sqm 1750 kwa tsh 51 milion.

Biashara hii haina dalali/udalali na Ukipata ujumbe huu, mjulishe ndugu/jamaa/rafiki.


Mpigie mhusika kwa 0758603077 au whatsap 0757489709


Share:

Tanzania Kunufaikana Mikopo Ya Kuendeleza Miradi Ya Miundombinu Kutoka Benki Ya ‘Asianinfrastructure Investment’.

Na Eva Valerian na Ramadhani Kissimba, Washington DC
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango(Mb) amefanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa ‘Asian Infrustructure Investment Bank’ Bw. Danny Alexander jijini Washington DC. 

Katika mazungumzo na Benki hiyo wamekubaliana kusaidia katika miardi endelevu ya Miundombinu kama Barabara na Reli.

Mazungumzo hayo ambayo pia yalihudhuriwa na Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Mhe.Mohammed Abdiwawa, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga na Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt.Yamungu Kayandabila yalikuwa na lengo la kuangalia fursa ambazo Tanzania inaweza kunufaika kutoka katika Benki hiyo.


Share:

Waziri Mhagama Azitaka Halmashuri Kuhakiki Taasisi Ndogo Za Fedha Kubaini Taasisi Zinazowaibia Wananchi

Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu , Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Jenista  Mhagama , ameziagiza  halmashauri zote nchini kufanya uhikiki wa kina wa taasisi ndogo za kifedha zinazotoa mikopo  kwa wananchi na vikundi, ili kuzibaini  taasisi zinazowaibia Watanzania badala ya kuwanufaisha kiuchumi..

Waziri Mhagama ametoa agizo hilo, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, yaliyofanyika Kitaifa katika  Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Oktoba 20, 2019.

“Ninajua baadhi ya taasisi ndogo za fedha badala ya kuwasaidia  wanachama zimekuwa ziifanya kazi ya kuiba fedha za wanachama  na kuwafanya wanachama warudi nyuma badala kusonga mbele, agizo hili Baraza la Taifa la Uwezesheshaji wananchi Kiuchumi mlifuatilie kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI,” alisema Mhagama.

Katika hatua nyingine ameitaka mifuko/programu za uwezeshaji wanachi kiuchumi kutoa mikopo kwa riba nafuu tofauti na taasisi nyingine za kifedha, ambapo amebainisha kuwa takribani wajasiriamali 1,237,984 wamenufaika na mikopo ya mifuko hiyo na hadi kufikia Juni 2019 jumla shilingi bilioni 388.4 zimetolewa.

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga ametoa wito kwa Taasisi za kifedha kuhakikisha zinajibu changamoto za wananchi huku akiwataka wananchi (wajasiriamali) walioshiriki maonesho haya kutumia vema fursa walizoziona katika mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ili wakuze uchumi wao

Baadhi ya wanufaika wa mikopo wilaya ya Bariadi na Busega mkoani Simiyu na Chato Mkoani Geita  wamezishukuru Taasisi za kifedha zilizowakopesha mitaji jambo ambalo limewasaidia kuimarsisha shughui zao za kiuchumi wanazofanya ikiwa ni pamoja na kilimo na ufugaji.

“Naishukuru Benki ya AZANIA na wadhamini wangu Taasisi ya PASS kwa kuniwezesha kupata mkopo wa shilingi milioni 20, kuanzia sasa nitalima kisasa na nitaenda kuongeza miundombinu ya maji kwenye shamba langu maana nilikuwa nalima ekari 10 kwa kumwagilia badala ya ekari 30 nilizo nazo,” alisema Elisha Malugu kutoka wilayani Busega.

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi(NEEC) Dkt. Festus Limbu amesema NEEC inaendelea kufuatilia agizo la Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa alilolitoa Juni 2019 la kila mkoa kuwa na kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi, lengo likiwa kuvifanya vituo hivyo kuwa kitovu cha uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Katibu Mtendaji wa NEEC, Bi. Beng’ Issa amesema Maonesho haya yameshirikisha Taasisi 45, wajasiriamali zaidi ya 200 kutoka mikoa ya Simiyu, Mbeya, Pwani, Mwanza, Tabora, Kagera , Mara, Singida na Dar es Salaam na kutoka nchi jirani za Burundi na Kenya.

Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii chini ya Kauli Mbiu, “Mitaji ni Chachu ya Kujenga Uchumi wa Viwanda” yametanguliwa na maonesho ya kwanza yaliyofanyika Mbeya mwaka 2017, ambapo ya pili yalifanyika mwaka 2018  jijini Dodoma.


Share:

Rais Magufuli Afichua Siri ya Ukamataji Vigogo Waliopiga Bilioni 1.2 za Korosho

Rais John Magufuli amesema Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), inawashikilia viongozi wa vyama vya ushirika 92 mkoani Mtwara kwa tuhuma za kuwadhulumu wakulima wa korosho Sh. bilioni 1.2.

Amesema fedha hizo ni malipo ya korosho katika msimu wa mwaka 2016 hadi 2017, amewaahidi wakulima hao watalipwa fedha zao.

Aliyasema hayo jana, Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati akiwaapisha viongozi aliowateua mwishoni mwa wiki.

“Juzi nilikuwa Mtwara, Brigedia Jenerali Mbungo (Kaimu Mkuu Takukuru) anafahamu tulikuta malalamiko sana ya baadhi ya watu waliodhulumiwa malipo yao ya korosho kuanzia mwaka 2016 hadi 2017,” alisema na kuongeza:

“Na vilikuwa ni vyama vya ushirika 10, baada ya kumwagiza Brigedia Jenerali, akakuta ni vyama vya ushirika 32 ambavyo vilikuwa vinawadhulumu watu. Tulidhani walikuwa wamedhulumu Sh. milioni 80 tukakuta wamezdhulumiwa zaidi ya Sh. bilioni 1.2.”

Rais Magufuli alisema Takukuru imeweza kuwashika viongozi wa Amcos 92 na mpaka juzi walipokuwa wanampatia taarifa (Rais Magufuli) zilikuwa zimerudishwa Sh. milioni 255, na kwamba zilizobakia zinaendelea kurudishwa.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu October 21




Share:

Sunday, 20 October 2019

TAMASHA LA TIGO FIESTA 2019 SAIZI YAKO ILIVYOKONGA MASHABIKI JIJINI DODOMA




Mwanadada Marianne Mdee ‘Mimi Mars’ akifanya vitu vyake kwenye tamasha la Tigo Fiesta 2019 Saizi Yako, lililofanyika juzi Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
Msanii wa Bongofleva Abdul Chande ‘Dogo Janja’ akifanya vitu vyake kwenye tamasha la Tigo Fiesta 2019 Saizi Yako lililofanyika juzi Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma. 
MKALI wa bongo fleva Nurdin Billal 'Shetta' akilishambulia jukwaa kwenye tamasha hilo jana.
MKALI wa nyimbo za injili Godluck Gozbert akilishambulia jukwaa la Tigo Fiesta 2019 Saizi Yako katika tamasha lililofanyika juzi Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma 
NYOTA wa muziki wa bongo fleva Heri Samir 'Mr Blue' akiimba katika tamasha la Tigo Fiesta 2019



Na MWANDISHI WETU, Dodoma
ZAIDI ya wasanii 16 juzi walitingisha baada ya kutoa burudani ya aina yake katika tamasha la Tigo Fiesta Saizi Yako, lililofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.
Juzi ilikuwa zamu ya Jiji la Dodoma na maeneo jirani kupata burudani hiyo ya aina yake baada ya kufanyika mikoa mingine mitatu tangu tamasha hilo lililopozinduliwa msimu huu.
Katika tamasha la Tigo Fiesta 2019 Saizi Yako mjini Dodoma, walihudhuria viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na mawaziri na wabunge pamoja na mashabiki kutoka katika kila kona ya mkoa huo.
Kabla ya kuanza tamasha la Tigo Fiesta 2019, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Paul Kunambi, aliwatambulisha baadhi ya wabunge na mawaziri ambao walihudhuria kwenye tamasha hilo.
Kunambi alisema kuwa tamasha hilo kwa mwaka huu limetoa fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukuza biashara za wajasiriamali kutokana na kuongeza mitaji.
Alisema kuwa kumekuwa na ajira za muda mfupi ambazo zinachangiwa na tamasha hilo ikiwa ni sehemu ya kukuza kipato kwa vijana.
Alisema anaishukuru Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo kutokana na kuonyesha ubunifu wa hali ya juu na kuendeleza vipaji vya vijana kupitia tamasha la Tigo Fiesta 2019 Saizi Yako.
“Tunaishukuru Tigo kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwa na ubunifu wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na kuendeleza vijana kupitia muziki wa bongo fleva,” alisema.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Tigo Kanda ya Kaskazini, Idan Komba, alisema wanaendelea kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Magufuli kwa kuhakikisha wanakamilisha usajili kwa alama za vidole kwa wateja wote wa Tigo nchini.
“Tutaendelea kumuunga mkono Rais Magufuli ikiwa ni pamoja na kuhakikisha usajili wa alama za vidole unafanyika na kuwafikia wateja wote wa simu za Tigo nchini,” alisema.
Tamasha hilo lilianza kwa wasanii chipukizi kupanda jukwaani na baadaye alipanda mkali wa bongo fleva anayefanya vizuri kwa sasa, Badest na kuimba kibao chake cha Nikagongee kilichowainua mashabiki na kuanza kumshangilia kwa kupiga kelele.
Baadaye alipanda jukwaani Heri Samir ‘Mr Blue’, na kuonyesha makali yake ikiwa ni pamoja na kuporomosha vibao vya zamani na vile vinavyotamba kwa sasa katika vituo mbalimbali vya redio nchini.
Mr Blue alianza na wimbo wa Tabasamu ambao aliimba live pamoja na bendi, baadaye akapiga wimbo wa Mbwa Koko, na kumalizia na Mboga Saba iliyowafanya mashabiki kuimba naye mwanzo hadi mwisho wa wimbo huo.
Hata hivyo Mr Blue alionyesha ukomavu wa hali ya juu kwenye onyesho la Tigo Fiesta Saizi Yako baada ya kumpandisha Nurdin Bilal ‘Shetta’, na kushirikiana naye kuimba wimbo wa Hatufanani.
Baadaye Shetta alibaki mwenyewe jukwaani na kutoa burudani kabambe ikiwa ni pamoja na kuimba nyimbo kama Shikorobo ilioonekana kuwavutia sana mashabiki waliohudhuria kwenye tamasha la Tigo Fiesta 2019 Saizi Yako.
Msanii wa bongo fleva, Abdul Chande ‘Dogo Janja’alipanda jukwaani na kutoa burudani murua ambapo aliimba nyimbo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ngarenaro, Kilele na Yente.
Nyota wa muziki wa injili, Godluck Gozbert alipewa nafasi kubwa na mashabiki kwenye tamasha la Tigo Fiesta 2019 Saizi Yako baada ya kupanda jukwaani na kuimba nyimbo mbalimbali zinazofanya vyema kwa sasa.
Staili aliyoingia nayo msanii huyo ilikuwa ya kipekee na kuwafanya mashabiki kumshangilia kwa kiasi kikubwa baada ya kuimba nyimbo za Shukrani, Nibadilishe na Hauwezi Kushindana.
Mwanadada Marianne Mdee ‘Mimi Mars’ alipanda jukwaani na kuonyesha manjonjo akiwa na wanenguaji wake.
Msanii huyo anayefanya vizuri kwenye muziki wa bongo fleva, alitawala vilivyo jukwaa kutokana na kuimba nyimbo zilizoteka hisia za mashabiki wake.
Msanii huyo aliimba wimbo wa Kodo, Polepole pamoja na Muwa na kuwafanya mashabiki kumshangilia vilivyo.
Wasanii wengine waliopanda jukwani kwenye tamasha la Tigo Fiesta 2019 Saizi Yako, ni pamoja na Barnaba Elias, Marioo, Juma Jux na Weusi.

Share:

PICHA: Rais Magufuli Awaapisha Viongozi Mbalimbali Ikulu Jijini Dar Es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mathias Bazi Kabunduguru kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Gerald Godfrey Mweli kuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayeshugulikia Elimu katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ali Sakila Bujiku kuwa Balozi katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Viongozi mbalimbali walioapishwa kutoka kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mathias Bazi Kabunduguru, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Gerald Godfrey Mweli pamoja na Balozi Ali Sakila Bujiku wakila kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Umma mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Viongozi mbalimbali walioapishwa kutoka kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mathias Bazi Kabunduguru, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Gerald Godfrey Mweli pamoja na Balozi Ali Sakila Bujiku wakisaini Hati ya kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Umma mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Augustine Mahiga, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mathias Bazi Kabunduguru wapili kutoka (kushoto), Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Gerald Godfrey Mweli wa kwanza (kushoto), pamoja na Balozi Ali Sakila Bujiku wakwanza (kulia) mara baada ya uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpa sambusa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

PICHA NA IKULU


Share:

Waziri Mkuu Amwakilisha Rais Magufuli Urusi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa anaondoka nchini leo (Jumapili, Oktoba 20, 2019) kwenda Urusi kuhudhuria mkutano baina ya Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa ya Afrika na Urusi (Russia-Africa Summit), utakaofanyika jijini Sochi, Urusi, Oktoba 23 – 24, 2019.

Waziri Mkuu anahudhuria mkutano huo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli.

Mkutano huo utakaoendeshwa chini ya uenyekiti wa pamoja (Co-chaired) wa Rais wa Shirikisho la Urusi, Vladimir Putin, na Rais wa Misri, Abdel Fattah el-Sisi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), unalenga kurejesha na kuimarisha uhusiano baina ya mataifa ya Afrika na Urusi ambao uliyumba baada ya kusambaratika kwa “Union of Soviet Socialist Republic” (USSR) mwaka 1991.

Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi na Serikali utafanyika katika sehemu mbili, ambazo ni Kongamano la Biashara (Russia Business Forum) linalotarajiwa kufanyika Oktoba 23, na Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa Nchi za Urusi na Afrika uliopangwa kufanyika Oktoba 24, 2019.

Waziri Mkuu atashiriki kwenye mikutano yote miwili.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger