Sunday, 13 October 2019

ASILIMI 15 YA MAPATO YA KOROGWE MINI MARATHON KUTUMIKA KUSAIDIA WAATHIRI WA MAFUKO WILAYANI KOROGWE

MKUU wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga Kisa Gwakisa katikati kikimbia pamoja na Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi kulia wakikimbia mbio za kilomita 5 za Korogwe Mini Marathon zilizofanyika leo mjini Korogwe 
Wakimbiaji wa Baiskeli wakiwa wameanza mbio zao kwenye Mashindano ya Korogwe Mini Marathon 

Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa kulia akikimbia kilomita 5 wakati wa Mashindano ya Korogwe Mini Marathon leo mjini Korogwe
Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi kulia akivalishwa medali na Mratibu wa Mashindano ya Korogwe Mini Marathon Juma Mwajasho mara baada ya kumaliza mbio za kilomita 5
Mratibu wa Mashindano ya Korogwe Mini Marathon Juma Mwajasho 
 Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi kulia akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa mashindano ya Korogwe Mini Marathon kwa upande wa wanaume aliyekimbia kilomita 10 Jumanne Ndege kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Korogwe Michael John ambaye ni Afisa Tarafa ya Korogwe
 Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akiendelea kutoa zawadi kwa washindi mbalimbali mara baada ya kumalizika mashindano hayo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa 
 Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akiendelea kutoa zawadi kwa washindi mbalimbali mara baada ya kumalizika mashindano hayo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Korogwe Michael John ambaye ni Afisa Tarafa ya Korogwe 
 Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akizungumza wakati wa mashindano ya Korogwe Mini Marathon 
 MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa akizungumza wakati wa mashindano ya Korogwe Mini Marathon

 MKUU wa wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa kushoto akimpongeza Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi 
 Sehemu ya wananchi wakifuatilia mbio hizo
 MKUU wa wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa katikati akiwa pamoja na washiriki wengine waliojitokeza kushiriki mashindano ya Korogwe Mini Marathon kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Timotheo Mzava
NA MWANDISHI WETU, KOROGWE

ASILIMIA 15 ya mapato yanayotokana na mashindano ya Riadhaa ya Korogwe Mini Marathon yanatarajiwa kutumika kwenye kuwasaidia waathirika wa mafuriko wilayani Korogwe ambao wamekumbwa na majanga mbalimbali.

Hayo yalisemwa leo na Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa wakati wa mashindano ya Riadhaa ya Korogwe Mini Marathon yaliyofanyika mjini Korogwe na kuhudhuriwa na washiriki kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.

Alisema maafa hayo ni makubwa kutokana na wamewaacha baadhi ya wananchi wakikosa makazi huku wengine wakipoteza maisha hivyo wameona watumie nafasi hiyo kuwafariji wananchi hao kwa kuwapatia kiasi hicho. 

“Ndugu zangu Korogwe tumekumbwa na maafa wenzetu wamepoteza maisha maji yamekata barabara kwa kutumia Mashindano hayo ya Korogwe Mini Marathon tutatoa asilimia 15 kuwasaidia ndugu zetu waliopata maafa na mvua hizo kuwapa mkono wa Pole kwa kuwa ni watanzania wenzetu”Alisema DC Kissa. 

Aidha alisema kwamba lengo kuu la mashindano hayo ni kumuenzi baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ikiwa leo ni mwaka 2019 anafikisha miaka 20 wao wana Korogwe tunatumia siku hii kwa kuenzi kwa kufanyika mashindano hayo”Alisema

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba Korogwe wameungana na dunia nzima kumuenzi baba wa Taifa ambayo aliwaachia watanzania demokrasia ya vyama vingi kitu ambacho kinaendeleza kwa vitendo na Rais Dkt John Magufuli.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba lengo la pili ni kuchangia miundombinu ya elimu kupitia kampeni ya Nivushe kuhakikisha wanasukuma mbele gurudumu la maendeleo ya sekta hiyo. 

“Lakini pia tunawashukuru Tanapa wametuchangia milioni 30, tunawashuiru marathon hii isingekamilika kama sio wadau hawa wameweza kudhamini huku mdhamini wa kwanza akiwa Tanapa, wa pili ni Gomba, wa cyclyn ...Lakini Tunawashuku pia NMB na CRDB tunategema kipindi kijacho tutakuwa na ongezeko la wadhamini “Alisema.

Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaume waliokimbia kilomita 10 alikuwa ni Jumanne Ndege kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) mkoani Arusha ambaye alikimbia dakika 30 na sekunde 7 ambaye alizawadiwa medali na kitita cha laki mbili.

Nafasi ya mshindi wa pili ilikwenda kwa Jackson Makombe ambaye alikimbia dakika 31 na sekunde 04 ambaye pia akitokea JKT Mkoani Arusha aliyepata kitita cha 140,000 huku mshindi wa tatu ikienda kwa Charles Sule ambaye alikimbia umbali wa dakika 32 na sekunde 07 ambaye pia alitokea JKt mkoani Arusha alizawadiwa kitita cha sh.80,000.

Kwa upande wa wanawake kilomita mshindi wa kwanza ilichukuliwa na Grace Jackson kutoka klabu ya JKT Mkoani Arusha ambaye alikimbia kwa kutumia dakika 35 na sekunde 51 ambaye alipata kitita cha sh.200,000,nafasi ya pili ikichukuliwa na Banuelia Bryson kutoka mkoani Kilimanjaro ambaye alikimbia dakika 41 na sekunde 16 aliyepata kitita cha sh.140,000,huku mshindi wa tatu ikichukuliwa na Pendo Pamba kutoka Klabu ya JKT ya Mkoani Arusha akikimbia kwa dakika 42 na sekunde 18 akizawadiwa kitita cha 80,000.

Hata hivyo kwa upande wa mbio za Baiskeli kilomita 30 wanaume mshindi wa kwanza aliibuka Boniface Saimoni kutoka mkoani Simiyu ambaye alikimbia dakika 49 na sekunde 59 na kupata kitita cha sh.200,000,huku mshindi wa pili ikichukuliwa na Mussa Makala aliyepata kitita cha sh.160,000,na mshindi wa tatu ikichukuliwa na Rashid Ally akizawadiwa kitita cha sh.120,000.

Kwa upande wa mbio baiskeli wanawake kilomita 20 mshindi wa kwanza ilichukuliwa na mshindi wa pili ni Anna Pimax huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa

Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi hizo mgeni rasmi wa mashindano hayo Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi alimpongeza Mkuu huyo wa wilaya kwa kubuni na kuanzisha mashindano hayo ambayo yamekuwa na tija kubwa. 

Alisema licha ya kuwepo kwa changamoto ya mvua lakini mashindano hayo yamefana na kuwa kivutio kikubwa kwa wananchi na wana michezo ambao walijotokeza kushuhudia mashindano hayo. 

“Lakini pia nipongeze kamati ya maandalizi kwa kufanikisha dhumuni hili kubwa ikiwa ni kumuenzi baba wa Taifa ambapo kesho ni kumbukizi yake lakini pia kutumia fursa hiyo kuhamamsisha wananchi kuajiandikisha”Alisema

Mwisho.

Share:

Nafasi Za Kazi 12 Toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Nafasi Za Kazi  12  Toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

==>>Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  imetangaza nafasi 12 za Kazi. Mwisho wa kutuma Maombi ni Tarehe 25 mwezi huu wa 10,2019

👉 ICT Officers (System Developers)- Nafasi 10

👉 Assistant Lecturer-Nafasi 1

👉 Rating II-Nafasi 1
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ 

==>>Pia zipo nafasi mbalimbali za kazi UBER TANZANIA, VODACOM, AIRTEL, JUMIA, NOKIA TANZANIA

Bonyeza hapo chini kujua zaidi

👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇


Share:

Uteuzi wa Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka za Maji




Share:

Wakurugenzi Wa Halmashauri Wana Wajibu Wa Kusimamia Utendaji Sekta Ya Ardhi

Na Munir Shemweta, WANMM MWANZA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka Wakurugenzi wa halmashauri nchini kuelewa kuwa pamoja na watumishi wa sekta ya ardhi kuhamishiwa Wizara ya Ardhi lakini bado wana jukumu la kusimamia utendaji wa sekta hiyo.

Dkt Mabula alitoa kauli hiyo jana alipofanya ziara katika halmashauri ya jiji la Mwanza pamoja na Manispaa ya Ilemela akiwa katika ziara ya kukagua utendaji wa sekta ya ardhi katika Kanda ya Ziwa inayojumuisha mikoa ya Mwanza, Simiyu, Mara na Geita.

Alisema, tangu watumishi wa sekta ya ardhi walivyohamishiwa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakurugenzi wengi wa halmashauri wameona kama wamejivua kusimamia utendaji wa watumishi wa sekta hiyo jambo alilolieleza kuwa siyo sahihi kwa kuwa mamlaka ya upangaji Majiji, Miji na Manispaa unabaki kwa halmashauri.

‘’kazi pekee inayosimamiwa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa watumishi wa sekta ya ardhi ni katika masuala ya nidhamu na ajira ambapo katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi anawajibika’’ alisema Dkt Mabula.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema katika kuboresha sekta ya ardhi nchini huduma za sekta hiyo sasa zimesogezwa katika mikoa badala ya kutegemea ofisi za Kanda alizozieleza kuwa ziko mbali kwa baadhi ya mikoa jambo linalowafanya wananchi kushindwa kupata huduma kwa urahisi.

Katika kufanikisha hilo Dkt Mabula aliwataka Wakuu wa mikoa kuharakisha uanzishwaji ofisi za mikoa kwa kutenga ofisi ili wananchi waweze kupata huduma za ardhi bila usumbufu ambapo alitolea mfano wa mikoa ya Tanga, Ruvuma, Mtwara na Simiyu kuwa tayari ishatenga ofisi kwa ajili ya mikoa yake.

Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwa Makwasa Biswalo alisema mkakati wa ofisi yake kwa mwaka huu ni kuhakikisha uanzishaji ofisi za mikoa usaidie kupunguza changamoto za sekta ya ardhi katika mikoa mbalimbali.

Akiwa katika ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Dkt Mabula lielezwa na Mkuu wa Idara ya Mipango Miji na Ardhi katika halmashauri hiyo Shukurani  Kyando kuwa, halmashauri hiyo imekuwa na mafanikio makubwa katika utoaji hati, urasimishaji na upimaji maeneo  mbalimbali ingawa imekuwa na changamoto kubwa ya utapeli unaofanywa na madali kwa kuuza kiwanja kimoja kwa mtu zaidi ya mmoja.

Hata hivyo, alisema katika kukabiliana na utapeli huo tayari wamewakama matapeli saba na baadhi yao tayari wamefikishwa katika vyombo vya sheria huku mmoja akikabidhiwa kwa Taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa (Takukuru) na kuwataka wananchi wanaotaka kununua viwanja kuhakikisha wanajiridhisha katika ofisi za ardhi ama ofisi za ardhi za kanda ili kuepuka kutapelewa.


Share:

PICHA: Kangi Lugola Ajiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amejiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, katika Kituo cha Senta, Kijiji cha Nyamitwebili, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda, Mkoa wa Mara, leo Oktoba 13, 2019.


Share:

Jinsi Ya Kuandika CV Nzuri Ambayo Itamvutia Mwajiri na Kukufanya Upate KAZI Kirahisi

WATU Wengi nchini wamekosa ajira na makampuni hupokea wastani wa maombi 200 ya kazi kwa tangazo moja la kazi. 

Hivyo, CV yako lazima ikae vizuri ili kumshawishi mwajiri. Utaratibu wa kuomba kazi inaweza ikawa tofauti kati ya makampuni na mashirika, ila yote yatahitaji uwatumie CV.

CV ni nini?
CV ni maelezo ya ujumla kwa kiundani ya historia yako ya kazi na shule. Kawaida, inatumika kwenye maombi ya kazi ya nafasi za kati, za juu na za utafiti.

Mambo yafuatayo yatasaidia kuifanya CV yako iwe bora na hivyo, kukusaidia kupata interview za kazi.

👉Soma na kuelewa maelezo ya kazi
Una ujuzi gani? Mwajiri anatafuta mfanyakazi wa aina gani? Maswali haya ni muhimu kujua kama utaiweza hiyo kazi au la. Pia, ni vizuri kujua nini hasa ni muhimu kwa muajiri na kufanya maombi yako yaendane zaidi na mahitaji ya mwajiri.

Kwa mfano, kama kazi inaweka umuhimu kwenye ujuzi wa kutumia mitandao ya kijamii kwa matangazo, hakikisha CV yako ina kazi zote zilizohitaji matumizi ya mitandao ya kijamii.

👉Andika maneno muhimu yaliyotumika kwenye maelezo ya kazi, uzitumie kwenye CV
Usichukue sentensi nzima kutoka kwenye maelezo ya kazi na ukaitumia vile vile kwenye CV yako. Ila, tumia lugha na baadhi ya maneno yaliyotumika kwenye CV.

👉Fanya utafiti juu ya kampuni iliyotangaza kazi
Pamoja na kuchambua maelezo ya kazi, ni muhimu kufanya utafiti juu ya kampuni yenyewe. Kama wana tovuti au wapo kwenye mitandao ya kijamii, jaribu kujua ni kazi gani na sekta ipi wanayohusika nayo. 

Pia, ikiwezekana jaribu kuwajua wafanyakazi/meneja wa kampuni hiyo. Hii itakusaidia kujua maadili na muelekeo wa kampuni. Hii itakusaidia kuweka maombi yako ya kazi yaendane na kampuni hiyo.

👉Orodhesha ujuzi wako wakufanya kazi
Hapa, usiweke kazi zote ulizozifanya maishani mwako ila, weka zile ambazo zilikuongezea ujuzi utakayo kusaidia kufanya kazi unayoomba.

==>Format/Staili inayotumika zaidi kwenye kuandika CV:
   1. Lengo la CV na ujuzi wako
    2.Ujuzi wako wa kazi
   3. Mafanikio maalum
   4. Elimu
   5. Ujuzi muhimu binafsi

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬
Angalizo:
  1.  Tumia maandishi ya kawaida ya Times New Roman
  2.  Tumia size 9 – 12 ya herufi
  3.   Hakikisha unatumia staili moja ya kuandaa CV kote
  4.   CV isiwe zaidi ya ukursasa 2
  5.   Usitumie sentensi ndefu
  6.  Hakikisha CV yako inasomeka kiurahisi na inawasilisha   mafanikio yako kwa uwazi.
  7.  Anza na kazi yako ya sasa hivi au ya hivi karibuni alafu rudi nyuma.
   ▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ 
   ==>.Hakikisha Yafuatayo:
1.Ukiwa unaandika jina la kampuni uliyo fanya kazi, andika jina la kampuni kikamilifu. 
2.Eleza kwa ufupi kampuni yao inahusika na nini. Tatu, weka muda uliyofanyakazi hapo (mwezi na mwaka).  
3.Baada ya hapo, orodhesha kazi na majukumu lako kwenye hilo kampuni.
4.Usidanganye

👉Maandalizi ya Mwisho

1.Pitia kila kitu kwa mara ya mwisho
 -Print CV yako alafu ipitie. Hii huwa inasaidia kuona makosea yako.

2.Mpe Rafiki  yako apitie CV
-Muombe rafiki yako apitie CV yako. Macho manne ni bora zaidi ya mawili!

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ 

Hatua ya kwanza kwenye kupata kazi unayotaka ni kutuma maombi. Tunatumaini kwamba maelezo yaliyoelezwa humu yatakusaidia kuandaa CV bora kwa ajili ya mwajiri.

👉Sasa, kwa kuwa umeshajua jinsi ya kuandika CV safi, anza kutafuta kazi unayoitaka kwa kubofya hapo chini.

AU 



Share:

Wilaya Ya Bukoba Mkoani Kagera Yafanikiwa Kwa Asilimia 82.4 Katika Zoezi la Uandikisha Wa daftari la mpiga kura Mkoani Humo

Na Avitus Benedicto Kyaruzi, Kagera.
Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Genelari Marco Elisha Gaguti ameendelea kuwasisitiza wananchi mkoani kagera kujitokeza  na kujiandikisha kwa wingi kwenye daftari la mpiga kura ndani ya siku mbili ambazo zimesalia kufikia tarehe 14 mwezi wa 9 mwaka huu ambapo itakuwa ni mwisho wa zoezi hilo.
 
Akizungumza na wananchi wa kata Kemondo katika mkutano wa hadhara, mkuu wa mkoa wa Kagera amebainisha tofauti iliyopo kati ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura na zoezi la kujiandikisha katika daftari la mpiga kura ambapo amesema zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura lililohusisha pia uboreshaji wa taarifa mbalimbali za wananchi kuwa vitambulisho hivyo vilivyotolewa ni kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa madiwa,wabunge na Rais.
 
Brigedia Gaguti amesema kuwa zoezi linaloendelea kwasasa ni kwaajili ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa na vijiji,  hivyo amewataka wananchi ambao bado hawajajiandikisha kutumia vyema siku hizi mbili kujitokeza  nakujiandikisha katika vituo vilivyopo katika maeneo yao.
 
Sanjari na hayo Brigedia Gaguti ametoa pongezi kwa wananchi na viongozi wa halmashauri ya wilaya Bukoba kwa ushirikiano nakusema kuwa kwataarifa za awali zinazohusu uandikishaji wa wapiga kura zilizotolewa tarehe 11 mwezi huu wilaya ya Bukoba imefanikiwa  kwa asilimia 82.4 ambacho ni kiwango kikubwa ukilinganisha na wilaya za Karagwe,Kyerwa,Misenyi,Mleba,Ngara,Biharamulo pamoja na manisipaa ya Bukoba.
 
Hata hivyo mkuu wa mkoa amesema viongozi wa ngazi za mitaa na vijiji  ndio  viongozi muhimu na  watakaotumika kuleta maendeleo kutokana na ukaribu wao kwa wananchi katika kufikia uchumi wakati na wa viwanda kama ilivyo azima ya nchi.


Share:

Waziri Mhagama Ahimiza Vijana Kutumia Michezo Kuimarisha Mshikamano

Na; Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amewamiza vijana nchini kutumia michezo ili kuimarisha amani, upendo na mshikamano.

Waziri Mhagama alitoa kauli hiyo wakati wa Bonanza la michezo kwa vijana lililofanyika katika shule ya Sekondari Lindi ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya vijana nchini kuelekea kilele cha mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2019 na Kumbukizi ya Miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa bonanza hilo ambalo vijana walikusanyika kwa lengo la kushiriki katika michezo mbalimbali, Mheshimiwa Mhagama alieleza kuwa michezo imekuwa ikitumika kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha ushirikiano na kuwajengea vijana ari ya uzalendo.

“Kupitia michezo mnayofursa kama vijana kuendelea kuenzi falsafa za waasisi wa taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Mzee Abeid Amani Karume ambao walikuwa wazalendo kwa taifa lao na waliimarisha muungano kwa maslahi ya watanzania wote,” alisema Mhagama

“Ni matumaini yangu kuwa kupitia michezo hii mtaendela kujikumbusha falsafa za waasisi hao kupitia michezo hii tunayoifungua leo kwa kuwa itatoa hamasa kwa vijana kupenda nchi yao na itajenga ari ya kuendeleza kuimarisha mshikamano kupitia michezo,” alisema Mhagama

Aliongeza kuwa michezo hiyo iliyowakutaisha vijana ikatumike kama sehemu ya kuwa na amani, uvumilivu na mshikamano.

“Vijana mnatakiwa kujenga taifa kwa vitendo vinavyodumisha amani, upendo na mshikamano kama ambavyo Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere alivyotujengea taifa lenye umoja,” alieleza Mhagama

Aidha Waziri Mhagama aliendelea kuwasihi vijana kutambua wajibu wao katika jamii na kuifanya michezo kuwa ni miongoni mwa mambo muhimu wanayopaswa kuyaendeleza katika kutekeleza mipango waliyonayo.

Pamoja na hayo alirejea ujumbe wa Mwenge wa uhuru mwaka huu ambao pia umesisitiza ushiriki wa wananchi katika uchaguzi wa Serikali za Mtaa. Aliwaomba vijana kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika uchaguzi ili waweze kupata viongozi bora kwa maendeleo ya taifa.

Waziri Mhagama alitumia fursa hiyo pia kuwapongeza wadau mbalimbali na vijana walioshiriki bonanza hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi alisema kuwa Bonanza hilo la michezo limejumuisha vijana kutoka sehemu mbalimbali ikiwa ni njia moja wapo ya kuwaendeleza vijana ili waweze kuimarika kiafya na kiakili.

MWISHO


Share:

Naibu Waziri Wa Madini Alitembelea Eneo Lenye Mgogoro Wa Wachimbaji Wadogo

Serikali imeingilia kati mgogoro uliodumu kwa muda mrefu katika eneo la wachimbaji wadogo lililopo katika Mlima wa Sakenke kata ya Misigiri Wilaya ya Iranga Mkoani Singida.
 
Mgogoro huo uliodumu kwa takribani miaka 3 ni kati ya mchimbaji mdogo aliyekuwa afisa usalama  wa taifa mstaafu John Lutebeka, na Nabii Elia wote wanagombea eneo hilo ambalo Lutebeka anamiliki ardhi ya juu na Elia ameliombea Leseni ya Uchimbaji Madini.
 
Akizungumza kwenye eneo linalogombewa, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, amewataka Lutebeka, Nabii Elia na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida, Chone Malembo wafike ofisini kwake Jijini Dodoma siku ya Jumatano Oktoba 16 mwaka huu kwa ajili ya kutatua mgogoro huo na kila mmoja aje na vielelezo vinavyomruhusu kuchimba madini katika eneo hilo.
 
Aidha, Nyongo amewataka Maafisa Madini kote Nchini kutoa elimu kwa wachimbaji juu ya sheria za madini ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima maana kuna haki ya umiliki wa ardhi ya juu na kuna haki ya umiliki wa ardhi ya chini kwa maana ya leseni ya uchimbaji hawa wote wana haki sawa wanaweza wakakaa wakazungumza  wakachimba pamoja.
 
Wakati huo huo Naibu Waziri Nyongo, amemtaka Nabii Elia aachane na uchimbaji wa madini karibu na nguzo za umeme anatakiwa awe mita 100 kutoka kwenye nguzo za umeme, vinginevyo atachukuliwa hatua.
 
Pia nyongo amewapongeza wachimbaji wa madini wa Mkoa wa Singida kwa ulipaji mzuri wa kodi na amesema rasilimali ya madini ni ya Watanzania wote, hatuko tayari kumuoneo mtu wala hatakubari mtu achimbe amdhulumu mwingine.
 
“Kwenye uchimbaji kuna kelele nyingi, kuna wengine wanamiliki leseni nyingi hata kuzihudumia hawawezi, mpaka sasa tumefuta leseni elfu 13 hivyo wale wanaojua wasitumie ujuaji wao kuwadhuru wengine tutampa haki mwenye haki yake,” alisema Nyongo.
 
Awali Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida, Malembo, alisema kwa nyakati tofauti, ofisi yake imesuluhisha  mgogoro huo, lakini Lutebeka huwa haridhiki na maamuzi tunayofikia ikabidi tuligawe eneo hilo leye hekari 7.2 na kumpa Lutebeka hekari 4 lakini bado hakuridhika.
 
Akizungumza kwa  masikitiko, Mkuu wa Wilaya ya Iramba Huhahuka amesema anasikitika kuingizwa kwenye mgogoro huo ambapo Afisa Usalama wa Taifa Mstaafu Lutebeka amekuwa akimtuhumu kuwa anawadhamini hao wanaotaka kuchimba eneo hilo.
 
Kwa mujibu wa Afisa Madini Mkazi wa Singida, Malembo amesema, kati ya Julai na Oktoba 11 mwaka huu, wamekusanya mapato ya zaidi ya shilingi 1.3 bilioni, Mapato hayo ni sawa na asilimia 271.94 ya lengo  kwa awamu ya kwanza la kukusanya shilingi 500,000,000, na asilimia 90.65 ya lengo la mwaka la kukusanya shilingi 1,500, 000,000/=.


Share:

Ujerumani, Ufaransa, Uholanzi Zasitisha Mauzo ya Silaha kwa Uturuki Baada ya Kuivamia Kijeshi Syria

Ujerumani haitaidhinisha tena mauzo ya silaha  ambazo zinaweza kutumika katika mashambulizi ya kijeshi ya Uturuki kaskazini mwa Syria, waziri wa mambo ya kigeni Heiko Maas ameliambia gazeti la Bild am Sonntag.

"Kutokana  na mashambulizi  ya  kijeshi  ya  Uturuki kaskazini mashariki  mwa Syria , serikali  ya shirikisho haitatoa  tena vibali vipya  kwa  ajili  ya  vifaa  vya  kijeshi  ambavyo vinaweza  kutumika na  Uturuki nchini  Syria," Maas  amesema.

Maas  aliongeza kwamba  serikali  ya  Ujerumani  tayari imeweka vizuwizi katika  mauzo ya  nje ya  silaha  zake  kwa  Uturuki katika mwaka  2016 kutokana  na  mashambulizi  ya  nchi  hiyo katika  jimbo la  Afrin.

Washirika  wa  mataifa  ya  magharibi wamekosoa operesheni  ya Uturuki ndani  ya  Syria, ambayo  ilianza siku  ya  Jumatano , ikisema inatishia  mzozo  mkubwa  wa  kibinadamu pamoja  na  kufufua  kundi la itikadi  kali la  Kiislamu  linalojiita  Dola  la  Kiislamu  katika  eneo hilo.

Siku  ya  Jumamosi , wizara ya  mambo  ya  nje  na  ulinzi mjini  Paris zilisema  kuwa  Ufaransa  inasitisha  mauzo  yake  ya  silaha  kwa Uturuki  kutokana  na  mashambulizi  ya  Uturuki kaskazini  mwa Syria.

Serikali  mjini  Paris imeamua  kusitisha  mipango  yote ya  mauzo ya  silaha  kwa  Uturuki  ambayo  inaweza  kutumiwa  katika mashambulizi, wizara  hizo zilisema  katika  taarifa  ya  pamoja.

Siku  ya  Ijumaa , Uholanzi ilisema  imesitisha  kwa  muda mauzo yake  ya  silaha  kwa  Uturuki, na  Sweden  ikasema itatafuta kuungwa  mkono kwa  ajili  ya  kuwekewa  vikwazo  vya  Silaha Uturuki  na  mataifa  yote  ya  Umoja  wa  Ulaya katika  mkutano  wa mawaziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa  Umoja  huo wiki  ijayo.

-DW


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili October 13


















Share:

NAIBU WAZIRI WA MADINI ALITEMBELEA ENEO LENYE MGOGORO WA WACHIMBAJI WADOGO

 Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo katikati, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Immanuel Luhahula,  Kulia ni Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida Chone Malembo wakielekea eneo lenye mgogoro
  Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akisikiliza kero za wachimbaji wadogo wa Madini ya dhahabu katika eneo la Misigiri Wilayani Iramba Mkoa wa Singida
 Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo kushoto akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Immanuel Luhahula wakijadiri jambo baada ya kuwasili kwenye eneo lenye mgogoro katika Kata ya Misigiri Wilayani Ilamba Mkoa wa Singida
 Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Immanuel Luhahula kulia akimuelekeza Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo eneo lenye mgogoro
 Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akizungumza kwenye kutatua mgogoro wa eneo la kuchimba dhahabu linalogombewa na wachimbaji wadogo, Afisa Usalama wa Taifa Mstaafu, John Lutebeka na Nabii Elia
Afisa usalama wa taifa mstaafu, John Lutebeka, akitoa malalamiko yake kwa Naibu Waziri Madini Stanslaus Nyongo (hayupo kwenye picha) yanayohusu eneo lake lakuchimba dhahabu kuvamiwa na Nabii Elia
Nabii Elia, akitoa taarifa inayohusu  eneo lenye mgogoro analochimba dhahabu katika mlima wa Sekenke Wilaya ya Iramba Mkoani Singida

SERIKALI imeingilia kati mgogoro uliodumu kwa muda mrefu katika eneo la wachimbaji wadogo lililopo katika Mlima wa Sakenke kata ya Misigiri Wilaya ya Iranga Mkoani Singida.
Mgogoro huo uliodumu kwa takribani miaka 3 ni kati ya mchimbaji mdogo aliyekuwa afisa usalama  wa taifa mstaafu John Lutebeka, na Nabii Elia wote wanagombea eneo hilo ambalo Lutebeka anamiliki ardhi ya juu na Elia ameliombea Leseni ya Uchimbaji Madini.
Akizungumza kwenye eneo linalogombewa, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, amewataka Lutebeka, Nabii Elia na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida, Chone Malembo wafike ofisini kwake Jijini Dodoma siku ya Jumatano Oktoba 16 mwaka huu kwa ajili ya kutatua mgogoro huo na kila mmoja aje na vielelezo vinavyomruhusu kuchimba madini katika eneo hilo.
Aidha, Nyongo amewataka Maafisa Madini kote Nchini kutoa elimu kwa wachimbaji juu ya sheria za madini ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima maana kuna haki ya umiliki wa ardhi ya juu na kuna haki ya umiliki wa ardhi ya chini kwa maana ya leseni ya uchimbaji hawa wote wana haki sawa wanaweza wakakaa wakazungumza  wakachimba pamoja.
Wakati huo huo Naibu Waziri Nyongo, amemtaka Nabii Elia aachane na uchimbaji wa madini karibu na nguzo za umeme anatakiwa awe mita 100 kutoka kwenye nguzo za umeme, vinginevyo atachukuliwa hatua.
Pia nyongo amewapongeza wachimbaji wa madini wa Mkoa wa Singida kwa ulipaji mzuri wa kodi na amesema rasilimali ya madini ni ya Watanzania wote, hatuko tayari kumuoneo mtu wala hatakubari mtu achimbe amdhulumu mwingine.
“Kwenye uchimbaji kuna kelele nyingi, kuna wengine wanamiliki leseni nyingi hata kuzihudumia hawawezi, mpaka sasa tumefuta leseni elfu 13 hivyo wale wanaojua wasitumie ujuaji wao kuwadhuru wengine tutampa haki mwenye haki yake,” alisema Nyongo.
Awali Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida, Malembo, alisema kwa nyakati tofauti, ofisi yake imesuluhisha  mgogoro huo, lakini Lutebeka huwa haridhiki na maamuzi tunayofikia ikabidi tuligawe eneo hilo leye hekari 7.2 na kumpa Lutebeka hekari 4 lakini bado hakuridhika.
Akizungumza kwa  masikitiko, Mkuu wa Wilaya ya Iramba Huhahuka amesema anasikitika kuingizwa kwenye mgogoro huo ambapo Afisa Usalama wa Taifa Mstaafu Lutebeka amekuwa akimtuhumu kuwa anawadhamini hao wanaotaka kuchimba eneo hilo.
Kwa mujibu wa Afisa Madini Mkazi wa Singida, Malembo amesema, kati ya Julai na Oktoba 11 mwaka huu, wamekusanya mapato ya zaidi ya shilingi 1.3 bilioni, Mapato hayo ni sawa na asilimia 271.94 ya lengo  kwa awamu ya kwanza la kukusanya shilingi 500,000,000, na asilimia 90.65 ya lengo la mwaka la kukusanya shilingi 1,500, 000,000/=.
Share:

Saturday, 12 October 2019

Assistant Lecturer Jobs: Arusha Technical College (ATC)

1.0 ARUSHA TECHNICAL COLLEGE (ATC) Arusha Technical College (ATC) is an autonomous institution established by the  Government Notice No.78 of 30th March 2007 that replaced by then Technical College Arusha that existed since 1978. The vision of ATC is to be a premier provider of  demand-driven Training, Research and Consultancy through Science, Technology and  Innovation (STI) for sustainable development. … Read More »

The post Assistant Lecturer Jobs: Arusha Technical College (ATC) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Research Assistant – Traditional Vegetables Genebank  (Arusha, Tanzania) 

Position Announcement Research Assistant – Traditional Vegetables Genebank  (Arusha, Tanzania)  The World Vegetable Center (WorldVeg) is a non-profit, autonomous international agricultural research center with headquarters in Taiwan and five regional offices around the globe. WorldVeg conducts research and development programs that contribute to realize the potential of vegetables for healthier lives and more resilient livelihoods. For more information… Read More »

The post Research Assistant – Traditional Vegetables Genebank  (Arusha, Tanzania)  appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Communication for Development Officer (two positions), Mbeya & Zanzibar, Tanzania

TA Communication for Development Officer, NO-B, Mbeya & Zanzibar, Tanzania (Two Posts- 6 months) Job no: 526989 Position type: Temporary Appointment Location: Tanzania,Uni.Re Division/Equivalent: Nairobi Regn’l(ESARO) School/Unit: United Republic of Tanzania Department/Office: Mbeya, United Rep. of Tanzania Categories: Communication for Development (C4D), NO-2 Advertised: Oct 10 2019 E. Africa Standard TimeUNICEF works in some of the world’s toughest places, to reach the world’s most disadvantaged children. To… Read More »

The post Communication for Development Officer (two positions), Mbeya & Zanzibar, Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Hubert Kairuki Memorial University (HKMU)- Selection 4th Round 2019

Hubert Kairuki Memorial University (HKMU) was established in 1997, being among the first private universities to be accredited in Tanzania in the year 2000, it has since then received local, regional and international recognition. It was the idea of Prof Hubert C.M Kairuki and his wife Mrs Kokushubira Kairuki to establish the University, moved by the situation in… Read More »

The post Hubert Kairuki Memorial University (HKMU)- Selection 4th Round 2019 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

CUHAS UNDERGRADUATE SELECTION-FOURTH ROUND 2019

CUHAS UNDERGRADUATE SELECTION-FOURTH ROUND 2019 he Catholic University of Health and Allied Sciences – Bugando (CUHAS-BUGANDO) is located at Bugando Hill, within the Bugando Medical Centre (BMC) premises in Mwanza. Our core business is training, research and consultancy services. We train health professionals in the fields of Medicine, Pharmacy, Medical Laboratory Sciences, Nursing and Public Health through our… Read More »

The post CUHAS UNDERGRADUATE SELECTION-FOURTH ROUND 2019 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger