Saturday, 12 October 2019

SUA-FOURTH BATCH OF UNDERGRADUATE DEGREE STUDENTS WITH MULTIPLE ADMISSIONS 2019/2020 ACADEMIC YEAR

SUA-FOURTH BATCH OF UNDERGRADUATE DEGREE STUDENTS WITH MULTIPLE ADMISSIONS 2019/2020 ACADEMIC YEAR Sokoine University of Agriculture wishes to inform the following prospective students with multiple admissions to confirm their readiness to join SUA by using the special code sent to them through their mobile phone number or email address used during application. To confirm please log in into… Read More »

The post SUA-FOURTH BATCH OF UNDERGRADUATE DEGREE STUDENTS WITH MULTIPLE ADMISSIONS 2019/2020 ACADEMIC YEAR appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

SUA-FOURTH BATCH OF STUDENTS SELECTED TO JOIN UNDERGRADUATE DEGREE AND NON DEGREE PROGRAMMES FOR THE ACADEMIC YEAR 2019/2020

SUA-FOURTH BATCH OF STUDENTS SELECTED TO JOIN UNDERGRADUATE DEGREE AND NON DEGREE PROGRAMMES FOR THE ACADEMIC YEAR 2019/2020 The following applicants have been selected in the fourth  round to join various degree and non degree programmes for 2019/2020 academic year which commences on the 4th November, 2019. Prospective Students are advised to observe the following: All candidates selected to join… Read More »

The post SUA-FOURTH BATCH OF STUDENTS SELECTED TO JOIN UNDERGRADUATE DEGREE AND NON DEGREE PROGRAMMES FOR THE ACADEMIC YEAR 2019/2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

MUHAS-List of Selected Applicants for Various Diploma Programs (Second Round)

List of Selected Applicants for Various Diploma Programs (Second Round) The following applicants have been selected to join various Diploma programs for the 2019/2020 academic year at the Institute of Allied Health Sciences (IAHS). Selected students are requested to collect their Joining Instructions and Admission letters in person at MUHAS admissions office from 1st October, 2019 (please come… Read More »

The post MUHAS-List of Selected Applicants for Various Diploma Programs (Second Round) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Udsm-4th Round selection 2019

UDSM UNDERGRADUATE ADMISSIONS RESULTS FOR 2019-2020 ACADEMIC YEAR ROUND FOUR 2019/2020 Background The University of Dar es Salaam (UDSM) started in 1961 as a College of the University of London. In 1963 it became a Constituent College of the University of East Africa. It was formerly established in August 1970, as a National University, through the University of… Read More »

The post Udsm-4th Round selection 2019 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

MWANAMKE ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUKANYAGWA NA TEMBO KILIMANJARO


Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke mmoja aliyefahamika kwa majina ya Majabu Lemahuna mkazi wa tarafa ya Mkongea kijiji cha Ngulu kata ya Kwakoa wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro amenusurika kifo baada ya kujeruhiwa kwa kukanyagwa na tembo kwenye maeneo mbalimbali ya mwili wake wakati akichukua kuni za kupikia nje ya nyumba yake, kisha kuvunjwa miguu, mikono na kupelekea kupoteza fahamu.

Tukio hilo ambalo limetokea Oktoba 6 mwaka huu majira ya saa mbili asubuhi, ambapo mashuhuda wa tukio hilo wanasema kuwa mwanamke huyo hakujua kuwa tembo hao wapo kwenye maeneo ya nyumba yake huku wakiiomba serikali kuwafukuza tembo hao ambao wamesambaa kwenye kijiji hicho. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Ngulu Bw.Modesti Mvungi amethibitisha tembo hao kumjeruhi mtu mmoja huku akiiomba wizara ya maliasili na utalii kuwaondoa tembo hao ili kunusuru maisha ya wananchi wa kijiji cha Ngulu.

Mara baada ya tukio hilo Mamlaka ya usimamizi wa wanyama pori Tanzania (TAWA), wamefika kwenye tukio hilo kisha kumpeleka majeruhi huyo kwenye hospitali iliyopo Moshi mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kupatiwa matibabu, na kisha kuwaswaga tembo hao kuwarudisha hifadhini.
Share:

ELIUD KIPCHOGE AVUNJA HISTORIA MBIO ZA MARATHON

Eliud Kipchoge

Eliud Kipchoge amekuwa mtu wa kwanza katika historia ya mbio za marathon kukimbia kilomita 42 kwa muda wa chini ya dakika mbili.

Raia huyo wa Kenya amekimbia muda wa kilomita 42.2 katika saa moja dakika 59 na sekunde 40 katika shindano la Ineos Challenge mjini Vienna nchini Austria leo Jumamosi.
Share:

MBWANA SAMATTA AFUNGA NDOA


Samatta na mkewe baada ya kufunga ndoa

Ni likizo ya kimataifa na wachezaji wenzake wengi wapo katika zamu ya kimataifa lakini nahodha wa timu ya Taifa Stars na KRK Genk Mbwana Samatta alikuwa na mipango mingine kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania.

Mshambuliaji huyo matata alitumia wakati wake mzuri wa likizo hiyo siku ya Alhamis kufunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi Neima Mgange.

Sherehe ya harusi yake iliofanyika katika kijiji cha kijichi mjini Dar es Salaam ilihudhuriwa na wachezaji wenzake wa Taifa Stars akiwemo Himid Mao na Thomas Ulimwengu kulingaa na gazeti hilo.

Ilikuwa sherehe ya kufana miongoni mwa watu wa familia ya Mgange walipokutana na mshambuliaji huyo ambaye ndiye mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kushiriki katika ligi ya mabingwa Ulaya.

Maelezo kuhusu uhusiano wa Mbwana na Neima yalikuwa ya siri kubwa na ni watu wa familia zote mbili pekee waliokuwa wakielewa kilichokuwa kikiendelea hadi siku ya Alhamisi.

Mshambuliaji huyo hakushirikishwa katika mechi ya kimataifa ambayo Taifa Stars inacheza dhidi ya Uganda wikendi hii.

Alikuwa akiugua jeraha lakini akashirikishwa katika kikosi cha timu ya Genk kilichopoteza 6-2 dhidi ya klabu ya Salzbourg kutoka Austria katika michuano ya kombe la mataifa bingwa Ulaya.

Pia aliisaidia Tanzania katika michuano ya kimakundi ya kufuzu kwa kombe la dunia Qatar 2022.
Share:

MASHIRIKA YAPIMA AFYA MAONESHO YA CHAKULA DUNIANI KITAIFA SINGIDA

 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akisalimiana na Meneja Mipango Mwandamizi wa Shirika la Save The Children Tanzania (SCT) Florian Fanuel na  Afisa Mradi Mkuu wa WFP, Florian Ngali katika Maonesho ya  Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani yanayofanyika Kitaifa mkoani Singida. 
 Mkuu wa Mkoa wa Singida,  Dkt.Rehema Nchimbi akipima uzito katika banda la Mashirika ya  Save the Children Tanzania, Shirika la chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) katika Maonesho ya  Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani yanayofanyika Kitaifa mkoani Singida leo. Kutoka kushoto ni  Msaidizi wa Ofisi ya FAO, Mihambo Gabriel na Afisa Mradi Mkuu wa WFP, Florian Ngali.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi akipima uzito.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi akizungumza na waandishi wa habari.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Kilimo, Revocatus Kassimba, akizungumzia kukamilika kwa maandalizi ya maadhimisho hayo.
 Mwalimu Elias Bubimbi kutoka Chuo cha Kilimo Mati- Mubondo (kulia) akimuelekeza  mwananchi aliyetembelea banda la chuo hicho jinsi ya kutengeneza biskuti za mbaazi.
 Afisa Mifugo Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Deograsias Ruzangi akitoa maelezo kwa  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi alipotembelea banda la wizara hiyo.
 Majasiriamali Rosemary Luhasile kutoka Nantakunganirwa Group akimpa zawadi ya dagaa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi.

 Afisa Mfawidhi Kituo cha Wizara cha Ukuzaji Viumbe Maji (Mwamapuli) akimuelekeza jinsi ya ufugaji wa samaki Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi alipotembelea banda la kituo hicho. Wa tatu kutoka kulia ni Mzee Juma  Ibrahim Mkhofoi mfugaji maarufu wa samaki mkoani Singida.
Afisa Ubora Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB), Idd Mkolamasa, akimuelekeza jambo Mkuu wa Wilaya ya Singida, Paskas Muragili alipotembelea banda la CPB.



Dotto Mwaibale na Boniphace Jilili, Singida 


SHIRIKA la Save the Children Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeendesha zoezi la upimaji wa uzito na urefu kwa wananchi katika maonesho ya maadhimisho ya siku ya chakula duniani ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Singida. 


Akizungumza na waandishi wa habari leo Meneja Mipango Mwandamizi wa shirika hilo, Florian Fanuel alisema wanafanya zoezi hilo katika maonesho hayo kupitia mradi wa boresha lishe ambao unaiwezesha jamii kujenga lishe bora na kuondokana na utapiamlo na lishe duni. 

"Hapa tunaonesha jinsi ambavyo jamii inaweza kujizalishia chakula chenye lishe bora lakini pia tunatumia fursa ya maadhimisho haya kutoa elimu na huduma za lishe"alisema Fanuel. 

Wakati huo huo  mkuu wa mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi  akizungumza baada ya kupima  uzito na urefu aliwahimiza wananchi wa mkoa huo na wa mikoa ya jirani kufika kwenye maonesho  hayo ili kupata elimu hiyo.

Alisema kupitia maonesho hayo ni vyema kila mwananchi kujitathimini juu ya lishe aliyonayo kuwa yuko sawa kilishe ama laa  baada ya kupata elimu kutoka kwa wataalamu hao. 

"Watanzania wengi hawathamini afya zao, mtu yuko tayari kumiliki gari zuri, nguo nzuri lakini anasahau lishe " alisema Dkt Nchimbi. 

Nchimbi alisema pamoja na kupata elimu ya lishe pia maonesho hayo yanatoa fursa ya wananchi kupata elimu ya utunzaji wa ardhi,matumizi ya mbegu sahihi ili kuongeza kiwango cha uzalishaji.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Kilimo,  Revocatus Kassimba alisema maandalizi ya maonesho hayo yamekamili na lengo hasa ni kuwapa elimu ya lishe wananchi ili kuondokana na lishe duni.

Alisema takwimu zinaonyesha uzalishaji wa chakula unatosheleza, hivyo watanzania hawana haja ya kuwa na lishe duni, ni elimu tu ambayo inahitajika ya namna ya kutumia vyakula wanavyovizalisha ili wawe na lishe bora. 

Share:

IGP Sirro Atoa ONYO Kwa Wanaojihusisha na ugaidi, ujangili na ujambazi...Asisitiza Ushirikiano na Nchi Jirani

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amesema ushirikiano wa nchi za Tanzania, Burundi Na DRC hasa kitengo cha ulinzi na usalama utamaliza matukio ya ugaidi na utekaji na kwamba hatua hii ni endelevu kwa nchi zote 3 kumaliza kabisa matukio ya kiuhalifu.

IGP Sirro amesema hayo katika kikao kazi cha usalama kwa Nchi za Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, kilichofanyika Mkoani Kigoma kikiwa na lengo la kuimarisha usalama mipakani na kukabiliana na wahalifu kutoka Nchi hizo.

"Makosa ya ugaidi, ujangili, dawa za kulevya, ujambazi na biashara haramu ya kusafirisha binadamu huwezi kuishinda ukifanya kazi peke yako.

“Ni lazima upate ushirikiano kutoka nchi jirani unazopakana nazo. Ndio maana leo tunakutana na wenzetu wa Burundi kujadili na tutasaini mikataba ya ushirikiano baina ya vikosi vyetu vya polisi," alisema Sirro.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Burundi CPP Melchiade Ruceke ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwa kinara wa kuchochea amani kwa Nchi hiyo na kubainisha kuwa watadumisha amani na kuibua wahalifu 

"Tutaendelea kuwakamata wahalifu wanaofanya ujambazi Tanzania na kukimbilia Burundi na pia nchi ya Tanzania itawakamata wale wanaoingia kutoka Burundi, tunataka amani katika nchi zetu," alisema Ruceke.


Share:

Mwandishi Erick Kabendera ataka kuongea na DPP ili kumaliza kesi yake

Wakili Jebra Kambole  anayemtetea mwandishi wa habari nchini Tanzania, Erick Kabendera katika kesi namba 75/2019, jana ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi mwandamizi, Augustine Rwizile  kuwa wanakusudia kufanya majadiliano na ofisi ya Mwendesha mashtaka kuhusu tuhuma za uhujumu Uchumi zinazomkabili Mwandishi wa habari, Erick Kabendera.

Awali, wakili wa Serikali Wankyo Simon aliieleza  mahakama hiyo kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilika. 

Alisema ni kweli jambo hilo lipo katika mchakato wa kuanza majadiliano na DPP, hivyo taratibu zikikamilika wataipa taarifa mahakama.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Octoba 24 itakapotajwa tena.


Share:

Dont open test post

Test post udahiliportal

The post Dont open test post appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Rais Magufuli Kuwachukulia Hatua Viongozi Watakaoshindwa kuwahamasisha wananchi kujiandikisha ....." Watanzania Mnisilaumu Kwa Hatua Nitakazochukua"

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli, amesema kuwa hatasita kuwachukulia hatua viongozi wa mikoa na wilaya ambao watashindwa kuwahamasisha wananchi kujiandikisha katika daftari la kupigia kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Oktoba 12, 2019, mkoani Katavi, alipokuwa akihutubia wananchi kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda, ambako amezindua safari za ndege za ATCL katika uwanja huo.

"Jana Waziri wa TAMISEMI alitoa takwimu kwa mikoa na wilaya ambazo zimefanya vizuri kwenye kuhamasisha watu kujiandikisha, nasubiri zoezi limalizike na kwa viongozi ambao mikoa na wilaya zao zitafanya vibaya najua watanzania hawatanilaumu kwa hatua nitakazochukua kwa viongozi" Amesema  Rais Magufuli.

Rais Magufuli  ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Katavi kwenda kujiandikisha ili kutumia haki yao ya kidemokrasia kuchagua viongozi watakaowaletea maendeleo.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli ameeleza hatua zilizofikiwa mpaka sasa baada ya kutoa msamaha kwa washtakiwa wa uhujumu uchumi kwa sharti la kukiri na kurejesha fedha walizoiba.

Amesema; "Leo nimezungumza na DPP, amenieleza kuwa mpaka sasa watu 138, waliokuwa wameiba mabilioni ya fedha, wamejitokeza na kuomba msamaha na wameshalipa fedha hizo na tayari wameachiwa huru"

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jafo, jana Ijumaa  October 11, 2019  alimwomba Rais  Magufuli, kupokea dokezo lake la mapendekezo ya kuwachukulia hatua viongozi wa mikoa na wilaya ambao watafanya vibaya kwenye uandikishaji wapigakura uchaguzi wa serikali za mitaa.

Alisema uandikishaji wa wapigakura kwa ajili ya uchaguzi huo si wa kuridhisha kwa mikoa yote nchini na kwamba kinachokosekana ni uhamasishaji.

Kwa mujibu wa Jaffo, mikoa iliyofanya vizuri  ni pamoja na Iringa ambao imefikisha asilimia 53 ukifuatiwa na Mbeya, Songwe na Tanga.

Alisema katika tathmini hiyo, Mkoa wa Dar es Salaam una asilimia nane huku Kilimanjaro ikiwa na asilimia 12 na Arusha asilimia 13.

"Naomba uridhie uandikishaji unaisha Ocktoba 14, mwaka huu. Haiwezekani  siku ya mpira wa Simba na Yanga watu wote wanaenda uwanjani lakini siku ya uandikishaji watu wanasuasu. Endapo siku saba zitakwisha na kuna mikoa haijafika hata asilimia 50 nitaomba nilete dokezo kwako," alisema.

"Kuna wakuu wa mikoa, makatibu tawala wa mikoa na wilaya, kuna wakurugenzi itakapobainika watu walizembea katika kuhamasisha watu kujiandikisha, nitaomba wachukuliwe hatua," alisema. 


Share:

RAIS MAGUFULI AWEKA MAWE YA MSINGI MIRADI YA UMEME, HOSPITALI YA WILAYA NA BARABARA YA MPANDA - IFUKUTWA - VIKONGE

Rais Magufuli jana Oktoba 11, 2019  amezindua mradi wa umeme wa Megawati 132 mkoani Katavi ambapo alisema mradi huo utaokoa zaidi ya Sh5.5 bilioni zilizokuwa zikitumika kununua mafuta kwa ajili ya majenereta ya kufua umeme.


Awali, Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani alisema mradi huo ulianza Mei 2019 na unatarajiwa kukamilika Mei 2020.

Alisema mradi huo utagharimu Sh135 bilioni na ulianza kwa  kujenga kituo cha kusambaza umeme kitakachofungwa mashine mbili za megawati 50 kila moja.


Share:

RAIS MAGUFULI AUWEKA MKOA WA KATAVI CHINI YA UANGALIZI WA JWTZ KUDHIBITI UHALIFU NA UJAMBAZI


Rais John Magufuli ameuweka Mkoa wa Katavi chini ya uangalizi wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), kutokana na kukithiri kwa vitendo vya uhalifu na ujambazi, vinavyohusishwa na wakimbizi.

Amesema kuna baadhi ya wakimbizi ambao wameficha silaha kwenye vichaka hivyo serikali inafuatilia kwa karibu ili kuwanasa wakaonyeshe walikowauzia.

Rais Magufuli aliyasema hayo jana akiwa katika Wilaya ya Tanganyika, mkoani Katavi, wakati akizindua kipande cha barabara ya Mpanda – Uvinza iliyojejwa kwa kiwango cha lami.

Aliagiza JWTZ kupitia Brigedi ya 201 ya Tabora kutekeleza jambo hilo huku akisisitiza kuwa nchi haiwezi kuchezewa na mtu yeyote.

"Kwa hiyo Jeshi la Wananchi Tanzania mpeleke base pale. Brigedi ya 201 ya Tabora ndiyo watakuwa wanahudumia hapa kwa sababu ni karibu. Nchi hii haiwezi kuchezewa na mtu yeyote. Kama kuna mkimbizi anafikiri anaweza kuichezea amepotea, tunahitaji upendo wa kweli mambo ya kui-beep Tanzania hayapo.

"Wapo walioishi miaka mingi, wapo waliopewa uraia na wapo wachache wameanza kuharibu sifa za ukimbizi kwa kujihusisha na ujambazi," alisema

Aidha, aliongeza kuwa kumekuwa na matukio ya uhalifu wa maliasili katika msitu wa Tongwe na kwamba baadhi ya wakimbizi wanaoaminika kuwa na silaha wamekuwa wakihusishwa.

"Waache tabia hiyo mara moja wamekimbia kule kutokana na migogoro waliyoisababisha wao. Ukija hapa kaa utulie, hapa si mahali pa kuleta migogoro na ukikimbilia taifa lingine kaa utulie usijifanye unajua,"alisema.

Pia alisema serikali haina matatizo na wakimbizi ambao ni watulivu kwa kuwa nchi inawapokea kwa maslahi mapana lakini wanapowashambulia wakulima wakiwa shambani, kuvamia mabasi na kupora abiria serikali lazima iingilie kati.


Share:

LIVE: Rais Magufuli anazindua safari za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) za Dar es Salaam - Mpanda.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli anafanya ziara ya siku tatu Mkoani Katavi  ambapo anafungua na kukagua miradi ya Maendeleo pamoja na kuzungumza na Wananchi wa Maeneo mbalimbali ya Katavi na Wilaya zake


Share:

Vijana Wilayani Ruagwa Wapongeza Serikali Kwa Kuwawezesha Stadi Za Kilimo Cha Kisasa

Na; Mwandishi Wetu
Vijana Wilayani Ruagwa wameipongeza Serikali kwa kuwawezesha kupata mafunzo ya kilimo cha Kisasa kwa kutumia teknolojia ya kitalu nyumba (Greenhouse) ambayo yamekuwa ni chachu kwao kujikwamua kiuchumi.

Pongezi hizo zimetolewa Oktoba 11, 2019 wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea vijana hao katika Kijiji cha Chimbila “A” kilichopo Wilaya ya Ruagwa kukagua maendeleo ya mafunzo waliyopata vijana kupitia teknolojia ya Kitalu Nyumba.

Mheshimiwa Mhagama alieleza kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imeonesha kuwajali, kuwatambua na kuwathamini vijana kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo yamekuwa yakiwasaidia sana katika kuwaendeleza vijana kulima kwa mkakati.

“Mafunzo hayo yamewajengea uwezo vijana wa kushiriki kwa wingi kwenye kilimo cha aina hii kwa kuwa kinatija na ufanisi, hivyo vijana watakuwa kupata mavuno zaidi katika eneo dogo kuliko eneo la wazi, uwezo wa kupata soko la mazao utakuwa wa uhakika, matumizi ya maji ni madogo katika kilimo hiko na hudhibiti viwatilifu,” alisema Mhagama

Alieleza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu ilianzisha Programu ya Ukuzaji Ujuzi ikiwemo mafunzo hayo ya kilimo cha Kisasa ikiwa ni mkakati wa serikali baada ya kubaini asilimia 56 ya nguvukazi nchini ambao ni vijana wamekuwa na changamoto ya ajira, katika kutatua changamoto hiyo kundi hilo limewezeshwa kwa kujengewa uwezo wa kupatiwa ujuzi katika fani mbalimbali.

Waziri Mhagama aliongeza kuwa Mafunzo hayo ya kilimo kupitia teknolojia ya kitalu nyumba yatawasaidia kuboresha stadi bora za kilimo kwa vijana hususan waliopo vijijini ili waweze kujiajiri, kuajiri wenzao na kushiriki katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Aidha aliwasihi vijana kuendelea kutunza vitalu nyumba hivyo kwa kuwa watanufaika kiuchumi na sambamba na kuwaleta maendeleo yao na jamii kwa ujumla.

Baadhi ya vijana walionufaika na mradi huo akiwemo Bw. Lucas Mwindima alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli imeonesha dhamira ya dhati katika kuwawezesha vijana wanapata ujuzi utakaowawezesha kukuza ujuzi wao na kuwaondoa katika hali ya umaskini.

“Tunamshukuru Rais Magufuli kwa kutuwezesha vijana kupata mafunzo haya ya kilimo cha kitaalamu yaliyoleta tija tunaona uzalishaji wa mazao ulivyokua tofauti na zamani na mazao tunayozalisha yanafursa ya kupata masoko ndani au nje ya nchi,” alisema Mwindima

Katika kupongeza jitihada hizo wanufaika wa programu ya kilimo hicho walibainisha mafanikio mbalimbali ikiwemo kupata ujuzi wa kilimo cha mazao biashara pamoja na ongezeko la ajira kwa vijana waliowezeshwa elimu hiyo.

Pia Waziri Mhagama alitembelea kikundi cha Ruangwa Materials ambacho kimenufaika na Mkopo wa Maendeleo ya Vijana unaoratibiwa na Ofisi yake kupitia Idara ya Manedleo ya Vijana.

MWISHO


Share:

UVCCM TANGA YATOA KAULI KWA VIJANA KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tanga Omari Mwanga akizungumza wakati wa ziara yake 
Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Mkoa Mbarouk Asilia akziungumza wakati wa ziara hiyo
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tanga Omari Mwanga katika akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wengine

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tanga Omari Mwanga amewataka vijana mkoani humo kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa,vijiji na vitongoji.

Mwanga aliyasema hayo wakati wa ziara kamati ya utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Tanga katika wilaya za Kilindi na Handeni iliyojumuisha mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Mkoa Mbarouk Asilia na Katibu wa UVCCM mkoa wa Tanga Zawadi Nyambo.

Alisema kuwa madhumuni ya ziara hiyo ni kuhamasisha vijana kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa,vijiji na vitongoji ambao unafanyika mwaka huu.

Mwenyekiti huyo alisema pili ni kusisitiza vijana kueleza utekelezaji wa ilani ya CCM 2015-2020 ikiwemo kukagua uhai wa jumuiya ngazi ya Kata ambapo ziara hiyo ilihusisha kata za segera, kabuku, mkata, mabanda, mdoe, chanika, Jaila na mabalanga.

Hata hivyo viongozi hao wa kimkoa waliwahamasisha vijana kugombea nafasi za uongozi katika serikali za mitaa, vijiji na vitongoji vyao kwenye uchaguzi huo
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger