Wednesday, 9 October 2019

Picha : WAANDISHI WA HABARI RADIO ZA JAMII 25 WAPEWA MAFUNZO NAMNA KURIPOTI MAAFA


 Mratibu wa Mradi wa SDC kutoka UNESCO, Christophe Legay akizungumza na washiriki (hawapo pichani) wakati akifungua mafunzo ya siku 5 kwa waandishi wa redio jamii 25 ya kujifunza namna bora ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine yaliyoandaliwa na UNESCO chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) yanayofanyika katika hoteli ya Millenium Sea Breeze mjini Bagamoyo.
 Mtaalamu wa Sayansi asilia kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Kevin Robert akizungumza na washiriki wakati akifungua mafunzo ya siku 5 kwa waandishi wa redio jamii 25 ya kujifunza namna bora ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine yaliyoandaliwa na UNESCO chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) yanayofanyika katika hoteli ya Millenium Sea Breeze mjini Bagamoyo.
 Mratibu wa Asasi ya Habari za Maendeleo Tanzania (TADIO), Irene Makene akitoa salamu TADIO kwa waandishi 25 wa redio jamii wanaoshiriki mafunzo ya siku 5 ya kujifunza namna bora ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine yaliyoandaliwa na UNESCO chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) yanayofanyika katika hoteli ya Millenium Sea Breeze mjini Bagamoyo.
 Washiriki kutoka redio za jamii wakichangia maoni wakati wa mafunzo ya siku 5 ya kujifunza namna bora ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine yaliyoandaliwa na UNESCO chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) yanayofanyika katika hoteli ya Millenium Sea Breeze mjini Bagamoyo.
Baadhi ya ya waandishi 25 wa redio jamii wanaoshiriki mafunzo ya siku 5 ya kujifunza namna bora ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine yaliyoandaliwa na UNESCO chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) yanayofanyika katika hoteli ya Millenium Sea Breeze mjini Bagamoyo.
Waandishi 25 wa redio jamii wanaoshiriki mafunzo ya siku 5 ya kujifunza namna bora ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine yaliyoandaliwa na UNESCO chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) yanayofanyika katika hoteli ya Millenium Sea Breeze mjini Bagamoyo.

Na Mwandishi Wetu , Bagamoyo
WAANDISHI wa habari kutoka kanda zote nchini ambao wanahudumu katika redio za jamii, wameingia katika mafunzo ya siku 5 mjini hapa kujifunza namna bora ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine.

Katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) washiriki watajifunza namna ya kuripoti maafa na pia mfumo wa kitaifa wa kukabiliana na majanga.
Akizungumza mjini hapa Christophe Legay, Mratibu wa Mradi wa SDC kutoka UNESCO amesema kwamba kutokana na kuongezeka kwa majanga na uelewa duni wa wananchi, UNESCO imeona vyema kufunza wanahabari ili waweze kuelimisha jamii.

Alisema kwamba mafunzo hayo ni ya tatu kwa waandishi wa habari na yamegusa wale ambao hawajawahi kupatiwa mafunzo hayo.
Legay alisema kwamba kutokana na mabadiliko ya tabianchi majanga ya asili yamekuwa yakijitokeza sana na kwa kasi hivyo imeonekana haja ya kuwapatia wananchi mafunzo maalumu ya kukabiliana na majanga hayo ikiwa na pamoja na kujiweka tayari.

"Tunataka wananchi watambue namna ya kukabiliana nayo majanga hayo, ili kusaidia kufikisha taarifa sahihi kwa jamii ambayo wanaitumikia" alisema Legay na kuongeza kuwa wanapowanoa waandishi wamelenga kuwawezesha kuwa na namna bora ya kuandika habari za majanga ili kusaidia kuokoa na kujipanga lisitokee tena.

Alisema kwa sasa wengi wa waandishi namna yao ya kuandika hairidhishi na hivyo kuchochea zaidi hasara badala ya kukabiliana na dhiki hiyo na kuokoa maisha na mali.
Legay alisema watu wakitambua namna ya kusimamia maafa na matumizi ya raslimali na nyenzo za usimamizi hasara kwa mali na watu zitapungua.

Alisema pamoja na majanga ya asili yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi, pia kuna majanga yanayosababishwa na shughuli za binadamu kama vile milipuko ya matanki, ajali mbalimbali ambazo wananchi amekuwa wakijihudumia badala ya kuokoa mali na watu.

Naye Kevin Robert, mtaalamu wa Sayansi asilia kutoka UNESCO alisema ni wajibu wa waandishi wa habari kwanza kutambua namna ya kukabiliana na majanga, elimu ambayo itawapa undani wa nini kinatokea, wafanye nini na nani asaidie wawe na taarifa sahihi za kusaidia wananchi.

Robert alisema wanahabari hao kutoka Redio 25 na Mratibu kutoka mtandao wa Redio za Jamii zilizotawanyika nchini kote ikiwamo mikoa ya Lindi,Katavi, Kilimanjaro Mara wanafundishwa mifumo ya upashanaji habari katika maafa, mifumo ya habari, kitengo cha maafa na utaratibvu wake na namna nzuri ya kusaidia waliokumbwa na mafaa.

Tanzania kwa sasa imeshakabiliwa na majanga ya asili mengi kama  mafuriko, ukame, upepo mkali, tsunami, mmomonyoko wa bahari,  mvua za mawe na upepo mkali  kama wa Kahama na mafuriko ya Mtwara, 2015 na pia kulipuka kwa lori la mafuta mjini Morogoro.
Katika ajali ya Morogoro wananchi badala ya kuokoa walikuwa wanaiba mafuta hadi lori lilipolipuka.

Kevin aliwataka waandishi hao kutambua changamoto zilizopo pamoja na kuelewa Sheria ya Uratibu wa Misaada ya Maafa Namba 9 ya 1990 (iliyofutwa na Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 7 ya 2015) na kujua kazi ya kitengo cha Kuratibu Misaada ya Maafa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Alisema ni matarajio ya UNESCO kuona kwamba mafunzo hayo yanaimarisha upashanaji habari wenye tija kubwa katika kukabili majanga na maafa.
Share:

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA WASHUKA HADI ASILIMIA 3.4

Na Mwandishi Wetu

Mfumuko wa Bei  wa Taifa kwa mwezi septemba, 2019 umepungua  hadi asilimia 3.4 kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2019.

Hayo yamesemwa na Kaimu mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bi. Ruth Minja wakati akitangaza mfumuko wa bei jana Jijini Dodoma.

“Kushuka kwa mfumuko wa bei kunatokana na kupungua kwa bei za bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi cha mwezi Septemba 2019 ikilinganishwa na bei za kipindi cha  Septemba,2018”. Alisisitiza Bi. Minja.

Akifafanua amesema kuwa baadhi ya bidhaa zilizopungua bei kwa mwezi Septemba ni mafuta ya taa asilimia 1.0, Petroli asilimia 3.3 ,majiko ya gesi asilimia 1.5, dawa za kuulia wadudu nyumbani asilimia 2.2 na mafuta ya nywele asilimia 1.3.

Aliongeza kuwa mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2019 umeongezeka hadi asilimia 4.0 kutoka asilimia 3.7 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2019.

Akizungumzia nchi za Afrika Mashariki Bi. Minja amesema kuwa mfumuko wa Bei nchini Kenya  kwa mwezi Septemba umepungua hadi asilimia 3.83 kutoka 5.00 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2019.

Kwa upande wa nchi ya Uganda, mfumuko wa Bei kwa mwaka unaoishia mwezi Septemba 2019 umepungua hadi asilimia 1.9 kutoka asilimia 2.1 kwa mwaka unaoishia mwezi Agosti, 2019.


Share:

Waziri Mkuu Awasili Ruangwa Kushiriki Mbio Za Mwenge

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasili wilayani Ruangwa, mkoani Lindi ili kushiriki mbio za mwenge kitaifa leo . Mwenge huo umewasili mkoani humo jana

Akizungumza na viongozi wa kitaifa na kimkoa mara baada ya kuwasili mkoani humo, Waziri Mkuu alisema leo ataungana na wakazi wa Ruangwa kuupokea mwenge huo. "Kesho( leo) nitaungana na wana Ruangwa ili kesho kutwa uendelee wilaya ya Nachingwea," alisema.

Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa jimbo la Ruangwa, alisema: "Nimeiona hamasa kubwa waliyonayo wanaLindi huu ya mapokezi ya mwenge wa uhuru lakini kikubwa zaidi ni ugeni mkubwa wa wageni akiwemo Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli."

Amesema mbali ya maadhimisho ya kumaliza mbio za mwenge nchi nzima, mwaka huu Tanzania inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa.

"Tuendelee kuwahamasisha wana Lindi na Watanzania wote washiriki kwenye makongamano yanayofanyika nchini kote. Kumbukumbu ya Baba wa Taifa isaidie kuelimisha vijana wetu  ambao hawajui historia ya kazi za waasisi wa Taifa letu."

"Pia walioko madarakani,  watumie fursa hii. Waige na kuenzi kazi za viongozi kama Mwalimu Nyerere na pia wajenge tabia ya kujua tabia ya ulipotoka, na mahali ulipo."

Mapema, akitoa taarifa ya maandalizi ya kilele cha mbio za mwenge kwa Waziri Mkuu,  Waziri wa Nchi OWM - Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alisema mbio hizo zilianza Aprili 2, mwaka huu  na leo zimeingia Lindi ambao ni mkoa wa 31.

Alisema hadi kufikia tarehe 14, ambayo ni siku ya kilele utakuwa umepita katika Halmashauri 195 za nchi mzima. 

"Katika kipindi hicho chote, vijana wetu sita ambao ni wakimbiza mwenge, walizindua miradi ambayo wameridhika nayo na ile yenye dosari, hawakusita kuikemea," alisema.

Alisema makongamano mbalimbali yameandaliwa ili kuenzi kifo cha Baba wa Taifa ambaye Oktoba 14, atatimiza miaka 20. Pia vijana 88 ambao walipanda mlima Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu hizo watashiriki sherehe hizo mjini Lndi.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Rais Magufuli Aweka Jiwe la Msingi Hospitali ya Wilaya Nkasi, Afungua Kituo cha Afya Namanyere

Na Fred Kibano, OR-TAMISEMI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameweka jiwe la msingi katika hospitali ya wilaya Nkasi ambayo ni kati ya hospitali 67 zinazojengwa katika halmashauri mbalimbali hapa nchini na kusema Serikali ipo pamoja na watanzania katika kuboresha huduma za afya.

Pia Rais Magufuli amefungua kituo cha afya Nkomolo kilichopo wilayani Nkasi kwa niaba ya vituo vingine 9 vilivyopo katika mkoa wa Rukwa na kuwashukuru Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto na kusema kuwa Serikali itaendelea kutenga fedha katika sekta ya afya ili kuboresha afya ya watanzania, amewasihi watendaji na wanasiasa kushirikiana ili kuendelea kuboresha huduma za afya kwa manufaa ya jamii.

Rais Magufuli amesema katika mwaka huu pekee wa fedha kiasi cha shilingi Bilioni 270 zimetengwa kwa ajili ya ununuzi wa madawa kwa nchi nzima.

Aidha, amewapongeza madaktari na manesi wilayani Nkasi na nchi nzima kwa kazi nzuri wanayoifanya lakini pia ametoa shukrani za pekee kwa madaktari bingwa kutoka Italia waliokuja na kufanya kazi katika kituo cha afya Namanyere wilayani Nkasi ambapo opereshi mbalimbali ambazo hufanywa katika hospitali za rufaa zinafanyika wilayani hapo.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amefungua barabara ya Sumbawanga hadi Kanazi yenye urefu wa kilomita 75 iliyogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 91 ambazo ni fedha za Serikali na kufanya kuendelea kuboreshwa kwa barabara za ukanda wa nyanda za juu magharibi inayotarajiwa kuchochea uchumi katika eneo hilo. Rais Magufuli amewasihi wananchi kuitumia fursa ya barabara hiyo ili kujiongezea kipato na kukuza uchumi wa Taifa na wananchi mmoja mmoja.

Akitoa maelezo ya awali, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amesema katika histori ya Tanzania Tangu uhuru haijawahi kutokea kujengwa kwa hospitali nyingi kwa wakati mmoja kwani mpaka sasa jumla ya hospitali 69 za wilaya zinajengwa na katika mwaka wa fedha 2019/2020 zinajengwa hospitali 27 na kufanya kuwa na idadi ya hospitali 96 mpya ukilinganisha na hospitali 77 zilizokuwepo tangu uhuru.

Naye Ummy Mwalimu Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto amesema wilaya ya Nkasi hapo awali kabla ya Rais Magufuli kuingia madarakani ilikuwa ikipata kiasi cha shilingi milioni 130.4 kwa mwezi lakini kwa hivi sasa baada ya kuimarika kwa makusanyo ya mapato inapata kiasi cha shilingi 588.5 kwa mwezi ambayo ni sawa na asilimia zaidi ya 90 ya upatikanaji wa dawa na hivyo amewasihi watanzania kuendelea kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.




Share:

Rais Magufuli Afungua Zoezi la Uandikishaji Wapiga Kura Kitaifa

Na Fred Kibano-TAMISEMI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amefungua rasmi zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24 zoezi ambalo linaloanza jana tarehe 08/10/2019 hadi 14/10/2019 na kuwataka wasimamizi kutenda haki ili uchaguzi uwe wa haki na kidemokrasia.

Rais Magufuli ametoa kauli baada ya kufungua zoezi la uandikishaji katika kituo kilichopo kwenye hospitali mpya ya wilaya ya Nkasi na kujionea namna zoezi hilo linavyofanyika mbele ya mawakala wa vyama vya siasa hali Afisa Mwandikishaji wapiga kura akifuata Mwongozo, Sheria, Kanuni na Taratibu za uchaguzi wa Serikali za Mitaa za mwaka 2019

“Mimi nawapongeza  endeleeni  kusimamia zoezi hili wasimamizi hakikisheni mnatenda haki kwa mtende haki kwa watanzania wote wote bila kubagua vyama vyao kwa sababu uchaguzi huu ni wa kidemokrasia ili tuhakikishe watu wapate ule uhuru wao wa  kumchagua mtu wanayemtaka katika Viongozi wa Serikali za Mitaa”

Awali Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo alitoa maelezo ya awali kwa kutoa wito kwa watanzania wote kujitokeza ndani ya wiki moja iliyotengwa na kwenda kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura ili wapate sifa ya kupiga kura mnamo Novemba 24, 2019 kwani ndiyo njia pekee ya kuimarisha utawala wa Serikali za Mitaa usiokithiri mianya ya rushwa na kuibua migogoro miongoni mwa jamii.

Naye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kange Ligola akitoa maelezo ya awali katika viwanja vya Namanyere amewataka wananchi kuchagua Viongozi wacha Mungu na wanaozingatia haki kwani kwa hivi sasa migogoro mingi ya ardhi na makosa mbalimbali yaliyopo katika Serikali za Mitaa yanatokana na viongozi waliochaguliwa ambao hawafuati sheria na kutozingatia maadili ya viongozi.




Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano October 9





















Share:

Tuesday, 8 October 2019

Ole Sabaya Ataja Sababu za Kutumia Polisi Mkutano wa Ndani wa CHADEMA Ulioongozwa na Mbowe

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amesema kitendo alichokifanya cha kuwatuma askari Polisi kuingia kwenye Mkutano wa CHADEMA, kilikuwa sawa na alifanya hivyo lengo lake ni kumlinda Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe.

Lengai Ole Sabaya ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam, wakati akizungumzia uamuzi wa kuagiza Askari wa Jeshi la Polisi kuingia kwenye kikao cha ndani cha CHADEMA, na kusema uamuzi wake ulikuwa sahihi.

"Niliwatuma Askari waingie mkutano wa ndani wa CHADEMA, na niliwaambia wakae ndani ya hicho kikao ila sikuwaambia wavunje mkutano, wao ni chombo cha dola, hata wakija hapa kwenye ofisi zenu sio tatizo."

"Namimi nadhani walipaswa kunipongeza, kwa sababu niliamuru Mwenyekiti wao Freeman Mbowe  alindwe, ila kwa sababu wao ndiyo wamekuwa na mashaka kila wakati ndiyo maana wanalalamika kila mara", ameongeza Ole Sabaya.

Hivi karibuni wilayani Hai, DC Ole Sabaya aliamuru askari polisi mkoani Hai kuingia ndani ya kikao cha ndani cha CHADEMA huku CHADEMA wenyewe wakilalamika kitendo hicho si sawa.


Share:

Korea Kaskazini yaonya iwapo kutazushwa mjadala wa nyuklia kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa

Korea Kaskazini imeionya Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kwamba iwapo wataliibua suala la majaribio yake ya makombora kwenye mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa inawezekana hatua hiyo ikaongeza zaidi nia yake ya kulinda uhuru wa taifa hilo. 

Mataifa 15 wanachama wa baraza hilo wanatarajiwa kukutana katika kikao cha ndani hii leo baada ya Korea Kaskazini wiki iliyopita kufyatua kombora jipya linaloweza kurushwa kutokea kwenye nyambizi.

 Majadiliano hayo yanafuatia ombi la Ujerumani, Uingereza na Ufaransa. 

Alipoulizwa kuhusiana na namna watakavyoulinda uhuru wa taifa hilo balozi wa Korea Kaskazini kwenye Umoja huo Kim Song amewaambia waandishi waendelee kufuatilia kwa makini kuona kile watakachokifanya huko mbeleni na kuongeza kuwa hiyo haimaanishi watafyatua kombora jingine. 

Pyongyang inatoa onyo hilo ikiamini kwamba Marekani iko nyuma ya vuguvugu hilo.


Share:

ALLIANCE FC WAONDOKA KWENDA NCHINI KENYA KUWEKA KAMBI KUJIWINDA KUWAVAA YANGA

Timu ya Wachezaji wa Alliance FC wakiwa pamoja na benchi la ufundi na Wafanyakazi wa Access Bank
Jackson Luka Mwafulango Afisa Habari wa Alliance FC akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano wa Alliance FC Yusuph Budodi na Meneja wa Access Bank Mwanza Emmanuel Venance wakizungumza na Wanahabari kuhusu timu ya Alliance FC kuweka kamba Nairobi Kenya.



Meneja wa Access Bank Emmanuel Venance akizungumza na  waandishi wa habari Ziara ya Alliance FC Kenya

Timu ya Soka ya Alliance FC ya Mwanza imeondoka leo kwenda Nairobi Nchini Kwenye kuweka kambi kujiandaa na mechi ya Yanga itakayochezewa katika Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza tarehe 20 Octoba Mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo wakati wa kuiaga timu hiyo,  Meneja wa Benki ya Access tawi la Mwanza Emmanuel Venance amesema wana faraja kubwa kuwa mmoja wa wadhamini wa timu hiyo kutokana na inavyojituma uwanjani. 

Amesema kama Taasisi ya Kifedha hapa Nchini wataendelea kuunga mkono juhudi za Timu hiyo wakishirikiana na wadhamini wengine kuhakikisha timu ya Alliance FC inakuwa Moja Kati ya timu tishio hapa Nchini.

Awali akimkaribisha Meneja wa Access Bank, Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya Alliance FC Yusuph Budodi ameishukuru Access Bank  pamoja wadhamini wengine wanaoidhamini Timu hiyo, na kuwaahidi kuendelea Kufanya kazi nzuri ili kupata pointi za Kutosha kwenye michuano ya ligi Kuu na mashindano mengine kwa Mujibu wa TFF.

Pamoja na Access Bank, wapo wadhamini wengine Kama Alliance Schools, Emirates Alluminium Profile na Mwanza Pure Drinking Water. Alliance FC wameondoka Leo kwenda Nairobi Kenya, kujiandaa na mechi nguma ya ligi didhi ya  timu ya Wananchi Yanga.
Share:

Job Opportunities at VisionFund Tanzania Microfinance Bank Ltd

VisionFund Tanzania Microfinance Bank Ltd (VFT MFB) is a Micro Finance Bank (MFB), has a loan book of Tshs. 22 billion and 53,000 customer base, more than 3,000 of them being small holder farmers. VFT is seeking to employ dynamic and committed Tanzanian who have passion for people’s economic development to fill in the vacant positions detailed here… Read More »

The post Job Opportunities at VisionFund Tanzania Microfinance Bank Ltd appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

11 Job at Jordan University College (JUCO)

JUCO BACKGROUND AND HISTORY: The religious Superiors of the congregations working in Tanzania agreed early on with the Salvatorian Mission Superior, Fr. Andrew Urbanski, SDS, that there was need for an Institution of Higher Education for their Religious members – especially for those who felt a calling to the presbyteral ministry. To the great satisfaction of all concerned,… Read More »

The post 11 Job at Jordan University College (JUCO) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Quality Engineer Job Opportunity at HRWorld

Position: Quality Engineer Location: NYAKAZI & GEITA HR World on behalf of our reputable client (Construction company) we are looking for a Quality Engineer for site in Nyakanazi and Geita. JOB RESPONSIBILITIES/DUTIES: Provides statistical information for quality improvement by identifying testing methods and samples. Determines quality improvement parameters by identifying statistical methods relevant to manufacturing processes. Establishes statistical confidence… Read More »

The post Quality Engineer Job Opportunity at HRWorld appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Kamishna Jenerali Wa Magereza Nchini, Phaustine Kasike Awataka Wakuu Wa Magereza Wawatumie Vizuri Wafungwa ili Kutatua Uhaba wa Makazi ya Askari

Na Mwandishi wetu, Songwe; 
KAMISHNA Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike amewataka Wakuu wa magereza Tanzania Bara kuhakikisha kuwa wanatekeleza ipasavyo agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu ujenzi wa nyumba za makazi ya askari wa jeshi hilo kote  nchini kwa kutumia nguvu kazi ya wafungwa waliopo magerezani.

Akizungumza Mkoani Songwe mara baada ya kukagua miradi ya ufyatuaji wa matofali ya kuchoma na ujenzi wa nyumba za maafisa na askari katika magereza ya Ileje, Mbozi, Ngwala na Kambi ya Mkwajuni iliyopo Mkoani Songwe,  Kamishna Jenerali Kasike amesema ujenzi wa makazi za askari unaoendelea katika vituo mbalimbali nchini ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli katika kutatua changamoto ya makazi kwa watumishi wa Jeshi hilo.

 “Mkakati wa utatuaji wa changamoto ya uhaba wa nyumba za Maafisa na askari lazima utiliwe mkazo na kupewa kipaumbele katika kuwatumia wafungwa  waliopo magerezani katika suala la ujenzi sambambamba na uzalishaji wa chakula chakutosha ili kuipunguzia Serikali gharama za kuwahudumia wahalifu wote walipo magerezani, ” alisema Kamishna Jenerali Kasike.

Katika hatua nyingine, Kamishna Jenerali Kasike ameupongeza Uongozi wa Wilaya ya Songwe kwa kuanzisha ujenzi wa Gereza jipya katika mji wa Mkwajuni ambao ni Makao Makuu ya Wilaya ya Songwe.

Kamishna Jenerali Kasike amesema uwepo wa gereza hilo katika wilaya ya Songwe utasaidia katika kumaliza tatizo la msongamano wa wafungwa na mahabusu kwenye gereza la wilaya ya Mbozi.

“Kutokuwepo kwa magereza ya wilaya kunasababisha msongamano wa wafungwa na mahabusu katika magereza ya jirani, pamoja na kuchelewesha upatikanaji wa haki hivyo nimpongeze sana Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Mhe. Samwel Opulukwa  pamoja na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama kwa kuwezesha kuanza kwa ujenzi wa Gereza hili kimsingi utatatua tatizo la msongamano wa wafungwa na mahabusu katika Gereza Mbozi,” amesema Jenerali Kasike.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Songwe. Mhe. Samwel Opulukwa ameshukru ujio wa Kamishna Jenerali katika ziara yake ya kikazi katika Gereza la Ngwala pamoja na Kambi ya Mkwajuni ili kujionea hali halisi ya Uendeshaji wa Jeshi hilo, Wilayani Songwe.

“Kamishna Jenerali nikuhakikishie tu kuwa Uongozi wa wilaya utashirikiana na Jeshi la Magereza katika kuhakikisha kuwa tunakamilisha ujenzi wa gereza hili jipya la Mkwajuni ili kusaidia kuondoa usumbufu wa wahalifu kwenda gereza la wilaya ya mbozi,” Alisistiza Mhe. Opulukwa.

Kwa sasa, wakazi wa wilaya hiyo ya Songwe ambao wanakabiliwa na tuhuma mbalimbali au waliohukumiwa vifungo hupelekwa katika Gereza la wilaya ya Mbozi kitendo ambacho kinawanyima wafungwa na mahabusu fursa ya kuonana na ndugu au mawakili wao kutokana na umbali uliopo ambapo kutokana na juhudi za Mkuu wa Wilaya hiyo tayari Bweni moja la Wafungwa lenye uwezo wa kuhifadhi waha;lifu 150 limekamilika pamoja na Ofisi ya Utawala na ujenzi wa Ukuta wa gereza unaendelea katika Kambi hiyo ya Mkwajuni.


Share:

Picha : JESHI LA POLISI SHINYANGA LATOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KWA WATU WALEMAVU


Na Salvatory Ntandu - Malunde 1 blog

Ukosefu wa elimu ya Usalama barabarani kwa watu wenye ulemavu mkoani Shinyanga umetajwa kusababisha vifo kwa watu wenye ulemavu kutokana na kugongwa na magari ambapo kwa kipindi cha miaka minne iliyopita jumla ya walemavu wanne wamepoteza maisha hali ambayo imelilazimu jeshi la polisi mkoani humo kuandaa mafunzo maalumu kwa ajili ya kundi hilo.



Hayo yamebainishwa leo mjini Shinyanga na mwenyekiti wa Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu mkoa wa Shinyanga, Richard Mpongo katika mafunzo maalumu kwao na kusema kuwa kundi la walemavu limesahaulika kwa muda mrefu hali ambayo ilikuwa ikisababisha wengi wao kugongwa na magari wakati wakivuka barabara.

Amesema walemavu wanapata changamoto mbalimbali pindi wanapotumia barabara kutokana baadhi ya madereva kutozingatia matumizi sahihi ya barabara jambo ambalo linasababisha kundi hilo kuendelea kupoteza maisha kutokana na ajali za barabarani.

Awali akimkaribisha kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Mkuu wa Usalama barabarani mkoa wa Shinyanga, Anthony Gwandu amesema mafunzo hayo yamejumuisha walemavu zaidi 30 wa aina mbalimbali na mafunzo hayo yatawafikia walemavu wote katika mkoa wa Shinyanga.

“Jeshi la polisi tunashirikiana na wataalamu mbalimbali wa lugha za alama watahakikisha walemavu wa kuona na kusikia wanapata elimu hiyo muhimu ili kutokomeza ajali za barabarani na kupunguza vifo visivyokuwa vya lazima",alisema Gwandu.


Akifungua mafunzo hayo ya siku moja, Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao amesema Jeshi la polisi limelazimika kutoa mafunzo hayo kwa walemavu baada ya kubaini kusahaulika kwa muda mrefu huku Mkuu wa Usalama barabarani mkoa wa Shinyanga,Anthony Gwandu akiwasisitiza matumizi sahihi ya alama za barabarani.


Ameongeza kuwa hawatasita kuwachukulia hatua kali Madereva wote watakaobainika kutozingatia matumizi sahihi ya alama za barabara ikiwemo katika maeneo ya vivuko vya watembea kwa miguu ambavyo vinatumiwa na watu mbalimbali ikiwemo wenye ulemavu.


TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI


Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Richard Abwao akizungumza jinsi walivyoamua kutoa elimu ya usalama barabarani kwa watu wenye ulemavu mbalimbali ili kuepukana na ajali za barabarani.Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoani Shinyanga (RTO), Athony Gwandu akitoa elimu ya usalama barabarani kwa watu wenye ulemavu mbalimbali mkoani Shinyanga.

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Shinyanga (RTO), Athony Gwandu akimsikiliza Yohana Isabu mwenye ulemavu wa macho namna ya kuwasaidia walemavu kukabiliana na ajali za barabarani.

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Shinyanga (DTO), Emmanuel Palangyo akitoa elimu ya usalama barabarani kwa walemavu ili kuepukana na ajali hasa kwenye maeneo ya vivuko.

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Shinyanga (DTO),Emmanuel Palangyo akiendelea kutoa elimu ya usalama barabarani kwa watu wenye ulemavu ili kuepukana na ajali.

Watu wenye ulemavu mbalimbali wakiwa kwenye mafunzo ya usalama barabarani.

Watu wenye ulemavu mbalimbali wakiwa kwenye mafunzo ya usalama barabarani.

Mafunzo ya usalama barabarani yakiendelea.


Watu wenye ulemavu mbalimbali wakiwa kwenye mafunzo ya usalama barabarani.

Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu Mkoani Shinyanga (SHIVYAWATA), Richard Mpongo
(kulia) akipongeza utolewaji wa elimu hiyo ya usalama barabarani kwa watu wenye ulemavu.

Yohana Isabu ambaye ni mlemavu wa macho, akishukuru elimu hiyo ya usalama barabarani na kuomba wadau wajitokeze kusaidia ugawaji wa fimbo nyeupe hasa kwa walemavu wa macho ili ziwasaidie muongozo wa kutembea na kuepukana na ajali.

Elizabeth Mathayo akishukuru utolewaji wa elimu hiyo ya usalama barabarani kwa watu wenye ulemavu ambayo itakuwa msaada wao mkubwa kuondokana na ajali za barabarani zisizo za lazima.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Richard Abwao akipiga picha ya pamoja na maofisa wa Jeshi hilo kikosi cha usalama barabarani pamoja na watu wenye ulemavu mara baada ya kuwapatia elimu ya usalama barabarani.
Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog
Share:

Uturuki: Maandalizi ya kuivamia Syria yalikwishakamilika

Uturuki imesema maandalizi ya kushambulia eneo la kaskazini mwa Syria yalikwishakamilika ikiwa ni baada ya dalili zenye mkanganyiko kutoka Marekani kuhusu iwapo itaruhusu operesheni hiyo ya kijeshi. 

Wizara ya ulinzi ya Uturuki imeandika kwenye ukurasa wake wa twitter muda mfupi baada ya Marekani kuondoa majeshi yake kwenye eneo la mpaka kwamba maandalizi yote yalikuwa yamekamilika. 

Kuliibuka utata siku ya Jumatatu wakati rais Donald Trump wa Marekani aliposema atauharibu uchumi wa Uturuki iwapo itafanya chochote ambacho hakitampendeza. 

Ankara imesema inataka eneo salama litakalotumiwa dhidi ya vikosi vya Wakurdi na kuruhusu takriban wasyria milioni mbili kurejea nyumbani. 

Katika hatua nyingine rais Trump ametetea uamuzi wake wa kuachana na wanamgambo wa Kikurdi nchini Syria akisema ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya kujiondoa kwenye "vita visivyo na mwisho" huko Mashariki ya Kati.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger