Tuesday, 8 October 2019

Dawa Komesha Ya Maumbile Madogo , Nguvu Za Kiume Na Magonjwa Mengineyo

*NGETWA MIX*/
√Hii ndio dawa bora ya mitishamba kiboko ya maumbile Madogo(KIBAMIA) Hurefusha na kunenepesha maumbile  mafupi pia  yaliyoingia ndani kutokana na kitambi ama kuathirika na punyeto

*πŸ“ŒSUPER MORINGA MIX*/
Ni dawabora ya nguvu za kiume yenye mchanganyiko wa miti shamba 10 yenye maajabu yafuatayo:/
πŸ”–(1)Inatibu upungufu wa nguvu za kiume mara dufu na kuimarisha misuri   ilio legea na kusinyaa wakati wa tendo la ndoa/
πŸ”–(2)Kuongeza hamu ya tendo kukufanya uweze kurudia tendo hadi mara tatu bila kuchoka
πŸ”–(3)Itakufanya uchelewe kufika kileleni dk 15-30 kwa tendo la Kwanza na utakuwa na uwezo wa Kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara 3-4 bila hamu kuisha na inatibu kabisa/
.
*MATATIZO HAYA HUSABABISHWA NA*/
πŸ”–(1)Tumbo kujaa gesi, na kuunguruma chini ya kitovu/
πŸ”–(2) Choo kuwa kama Cha mbuzi/
πŸ”–(3)Ngiri/
πŸ”–(4)Kama umejichua sana punyeto/
πŸ”–(5)Kisukari/
πŸ”–(6)Presha ya kupanda na kushuka/
πŸ”–(7)Vidonda vya tumbo,/
.
Na haya yote husababisha/
πŸ“Kuishiwa kwa nguvu za kiume πŸ“Œ/
. _______________________
Bado hujachelewa dawa hizi ni mpya kabisa  ni tofaut na ulizo wahi kutumia pia zimeonesha mafanikio kwa watu wengi sana/

Pia tuna tibu  KISUKARI,PRESHA,VIDONDA VYA TUMBO N.K/
._______________________
DR .SELEMANI OMARY ANAPATIKANA  DAR ES SALAAM , PIA UNAWEZA KULETEWA POPOTE ULIPO  NDANI NA NJE YA NCHI .SIMU NO:/
*πŸ“ž+255788468114*


Share:

LIVE: Ziara Ya Rais Dkt.john Pombe Magufuli Mkoani Rukwa Leo October 8

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli anafanya ziara ya siku tatu Mkoani Rukwa ambapo anafungua na kukagua miradi ya Maendeleo pamoja na kuzungumza na Wananchi wa Maeneo mbalimbali ya Rukwa na Wilaya zake


Share:

Taarifa Kwa Umma Kutoka Jeshi La Polisi Mkoani Mwanza

Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Limefanikiwa Kuzima Tukio La Ujambazi Baada Ya Kukabiliana Na Kundi La Watu Wanaotuhumiwa Kujihusisha Na Vitendo Vya Kihalifu Huku Wakiwa Wamejihami Na Bunduki Moja Aina Ya Shot Gun.

Tukio Hilo Limetokea Tarehe 08.10.2019 Majira Ya Saa 8:00 Usiku  Huko Katika Godown La Charles Faida La Vifaa Vya Ujenzi Lililopo Mtaa Wa Igogo Tanesco, Wilaya Ya Nyamagana Katika Jiji La Mwanza,

 Hii Ni Baada Ya Kundi La Watu Watano (5) Wanaotuhumiwa Kujihusisha Na Vitendo Vya Ujambazi Wakiwa Na Silaha Moja Aina Ya Shotgun Yenye Risasi Nne (4) Na Mapanga Waliwavamia Walinzi Wa Kampuni Ya Ulinzi Iitwayo “jurgon Security Gurd” 

 Baada Ya Kuwatishia Kuwaua Kwa Silaha Kisha Kuwafunga Kamba Mikononi, Miguuni Na Baadae  Kuvunja Ghala Hilo Na Kuiba Vitu Mbalimbali Vikiwemo Praise 60pcs, 2cock, 100pc, Hanging Scale 10pc , Spock Shave 72pc, Bolt Nut Pacts 16, Expanded Bolt 12pc.

Askari Waliokuwepo Doria Walibaini Uwepo Wa Majambazi  Hayo Kupitia Kwa Walinzi Wa Ghala La Jirani Na Walipofika Eneo Hilo Jambazi Mwenye Silaha Alijaribu Kuwashambulia Askari Kwa Kuwafyatua Risasi  Na Askari Wakamkabili Kwa Kumpiga Risasi Jambazi Huyo Aliyekadiriwa Kuwa Na Umri Kati Ya Miaka 30-35 Ambapo Alifariki Dunia Wakati Akipelekwa Hospital Huku .Majambazi Wengine Wakifanikiwa Kutoroka.

Aidha, Katika Tukio Hilo Jeshi La Polisi Limefanikiwa Kukamata Silaha Moja Aina Ya Shotgun Iliyofutwa Namba , Ikiwa Na Risasi Tatu, Ganda Moja La Risasi Aina Ya Shotgun, Mkasi, Nondo, Kamba Za Katani Na Mapanga Mawili.

Jeshi La Polisi Linaendelea Na Msako Mkali Wa Kuhakikisha Mtandao Wa Majambazi Hao Unatiwa Nguvuni. Katika Tukio Hilo Hakuna Askari Yeyote Aliyepoteza Maisha Wala Kujeruhiwa, Mali Yote Iliyokuwa Imeibiwa Na Majambazi Hao Imepatikana, Mwili Wa Jambazi Huyo Umehifadhiwa Katika Hospitali Ya Bugando Kwa Uchunguzi Zaidi.

Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza, Linatoa Onyo Kwa Baadhi Ya Watu Wanaojihusisha Na Vitendo Vya Uhalifu Kuwa Waache Kwani Watajikuta Mara Kadhaa Katika Wakati Mgumu. Sambamba Na Hilo Tunaendelea Kuwaomba Wananchi Watupe Ushirikiano Kwa Kutupa Taarifa Za Wahalifu Na Uhalifu Mapema Ili Tuweze Kuwakamata Na  Kuwafikisha Mahakamani.

Imetolewa Na,
Muliro J Muliro-acp
Kamanda Wa Polisi (M) Mwanza
08october, 2019


Share:

TPDC Yaanza Utafiti wa Mafuta ya Petrol Bonde la Eyasi Wembere

Serikali kupitia Shirika la Maendeleo  ya Petroli Tanzania (TPDC) imeanza kufanya utafiti wa mafuta ya petrol katika bonde la Eyasi Wembere ikiwa ni miaka 2 tu imepita tangu Mhe. Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Dkt John Joseph Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Museveni walipotia saini makubaliano ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa Bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga. 
 
Utafiti huu unahusisha uchorongaji wa visima vitatu vya utafiti vyenye urefu wa mita 300 kila kimoja na hivyo kufanya jumla ya mita 900 zitakazochorongwa katika Bonde la Eyasi Wembere ambapo Kisima namba moja kinachorongwa katika Kijiji cha Kining’nila Wilaya ya Igunga,kisima namba 2 na 3 vitachoroongwa katika wilaya za Meatu Mkoani Simiyu na Iramba Mkoani Singida. 
 
Akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa uchorongaji wa kisima namba 1, Meneja utafutaji wa Mafuta na Gesi kutoka TPDC, Bi Venosa Ngowi alisema kuwa utafiti huu unakuja kufuatia ukusanyaji taarifa za bonde hilo uliofanyika mwaka 2015 kwa kutumia ndege maalumu.

 Bi Ngowi alisema baada ya utafiti huo wa kutumia ndege, ulionesha eneo la Bonde la Eyasi Wembere kuwa na miamba tabaka mizuri ambayo inaweza kutumika kwaajili ya utafiti wa Mafuta na gesi hivyo uchorogaji huu wa visima vifupi vya utafiti ni awamu ya pili kufuatia utafiti wa 2015/16. 

Bi Ngowi aliendelea kwa kusema kwamba eneo lote la Bonde la Eyasi Wembere ni muhimu kwaajili ya utafiti huo kutokana na aina ya miamba inayopatikana. 

Akizunguzmia mita zilizochorongwa Katika kisima namba 1 kilichoanza kuchorongwa katika Wilaya ya Igunga amesema tayari zimechoronga mita 116 kati ya 300 zinazopaswa kuchorongwa. 
 
Nae Meneja Mradi wa Utafutaji Mafuta katika bonde la Eyasi Wembere, ndugu Sindi Mduhu alisema eneo la Bonde la Eyasi Wembere ni kubwa na linaanzia katika Mikoa ya Manyara, Singida,Simiyu, Tabora pamoja na Arusha. 

Baada ya ukusanyaji takwimu za eneoo hilo, kilichofanyika ilikuwa ni kuzichakata na kuzitafsiri ili kuweza kuona ni wapi palio  na miamba tabaka yenye kina kirefu ambacho kianweza kutunza mafuta.

 “Kijiji cha Kining’inila ni mojawapo ya eneo ambalo lilanishwa kama moja ya eneo ambalo uchoroongaji wa visima unaweza kufanyika”. 
 
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt James Mataragio aliyefika ene la utafiti kwaajili ya kujionea kinachoendelea katika utafiti huo alisema utafiti huo unafanyika kwa matumaini kuwa Tanzania inaweza kugundua mafuta. 

“Tunafanya Utafiti kwa kutegemea kwamba kwa kipindi kisichozidi miaka mitano (5) huenda tukagundua mafuta na hivo leo nawadhibitishia watanzania kwamba kazi hiyo inaendelea”. Dkt. Mataragio aliendelea kwa kusema “ kama kule Uganda huenda tukawa na mafuta”. 
 
Uchorongaji huo utafuatiwa na ukusanyaji wa taarifa za mitetemo ili kuonesha maeneo ambayo yanaweza kuwa na mafuta.
 
Dkt.mataragio aliongeza kwa kusema kuwa ni nia ya dhati ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuhakikisha kwamba TPDC si kwamba tu inachimba gesi yake yenyewe bila pia kuhakikisha inagundua mafuta. “ Mhe. Rais angependa kwamba katika kipindi ambacho atakuwa madarakani tuwe tumekwishagundua mafuta kwani tayari tunayo gesi asilia ambayo kwa mwaka 2020 tutaongeza visima vingine ambavyo tutavifanya wenyewe TPDC na sio kwa kutumia wawekezaji kutoka nje ya nchi”.  
 
Kwa upande wa ushirikishaji makampuni ya ndani katika utafiti huo, Dkt Mataragio alisema kazi yote inafanywa na TPDC kwa kushhirikiana na STAMICO ambalo ni shirika la Serikali na ndiye Mkandarasi Mkuu katika mradi huo. 
 
Akitaja sifa za maeneo ambayo mafuta yanaweza kugundulika, Dkt.Mataragio alisema ni maeneo ya Bonde la Ufa ambapo kama ilivyo kule nchini Kenya katika eneo la Lokcha au Turkana lipo katika Bonde la Ufa na kule wamegundua mafuta. Vile vile ukienda Uganda Ziwa Albert ambalo lipo katika Bonde la Ufa nao vile vile wamegundua mafuta. 

Kwa upande wa Tanzania, katika eneo la Ziwa Tanganyika ambalo lipo katika Bonde la ufa kuna matonetone ya mafuta hivyo ni dalili nzuri ya uwezekano wa upatikanaji wa mafuta na tayari ukusanyaji wa taarifa za eneo hilo ulikwishafanyika hivyo kitakachofuatia ni ufuatiliaji.

Dkt. Mataragio aliongeza kwa kutaja gharama za mradi wa uchoorgaji visima hivyo mbapo kwa visima vyote vitatu hadi vikamilike vitagharimu fedha za Kitanzania shilingi milioni mia tatu ambapo katika utafiti wa ndege jumla ya shlingi za Kitanzania  shilingi bilioni mbili nukta nne (2.4) zote zikiwa ni fedha za ndani na Serikali.  
 
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kining’inila Christopher Njilezengo ambapo ndipo utafiti huo unafanyika, aliipongeza Serikali kwa kukubali kuwekeza katika mradi huo kwani utakuwa na tija kwa taifa endapo utafanikisha upatikanaji wa mafuta. 

“Tunaishukuru sana Serikali kupitia TPDC kwani tunaamini ya kwamba wanatekeela sera ya chama cha mapinduzi chini ya uongozi shupavu wa Mhe. Rais Magufuli ambapo asingekuwa yeye basi mambo hayo wasingeyaona”. 
 
Bi. Neema Masanja mkazi wa Kijiji cha Kining’inila ambapo ndipo utaifit uanfanyika aliiipongeza Serikali kwa utafiti huo na kunonesha matumaini makubwa katika utafiti unaofanyika na endapo mafuta yatapatikna. “ Mafuta yakipatikana itawezesha upatikanaji wa fursa mbalimbali kwa wanachi ili kuleta maendeleo katika Kijiji chetu na taifa”. 
 
Tayri baadhi ya wanachi wa Kijiji hicho wameanza kuonja neema ya utafiti huo ambao kuna baadhi yao wamepatiwa kazi mbali mbali zisizohitaji elimu kubwa kama vile upishi, ulinzi pamoja na vibarua. 



Share:

Serikali Kuwachukulia Hatua Kali Za Kinidhamu Watumishi Watakaobainika Kujihusisha Na Rushwa Ya Ngono

Na James K. Mwanamyoto, Tunduru
Serikali haitosita kuwachukulia hatua kali za kinidhamu watumishi wa umma watakaobainika kujihusisha na rushwa ya ngono katika maeneo yao ya kazi, kwani kitendo hicho kinadhalilisha na kushusha hadhi ya utumishi wa umma nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) wakati wa kikao kazi chake na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kilichofanyika wilayani humo jana kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Mhe. Mkuchika ametoa kauli hiyo kufuatia baadhi ya Walimu wa shule za msingi wilayani Tunduru kushikiliwa na vyombo vya dola kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa ya ngono jambo ambalo halileti taswira nzuri kwa umma, ikizingatiwa kuwa Walimu wana jukumu la kuwalea wanafunzi katika maadili mema.

“Inakuwaje Mwalimu unaepaswa kuwa mfano bora wa kuigwa kimaadili unataka rushwa ya ngono kwa mwanafunzi, kitendo hicho kinamuathiri mwanafunzi husika kitaaluma na kisaikolojia”, Mhe. Mkuchika amefafanua.

Mhe. Mkuchika ameongeza kuwa, hivi karibuni ofisi yake imesitisha ajira ya Mhadhiri mmoja wa chuo kikuu nchini, ambaye alituhumiwa na kubainika kuwaomba rushwa ya ngono wanafunzi wa kike ili waweze kufaulu mitihani yao kwa upendeleo.

“Wanafunzi wa kike wa chuo hicho waliandika barua ya malalamiko kwenye ofisi yangu na baada ya kuwahoji na kufanya uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na vyombo vya dola ikabainika kuwa ni kweli hivyo akafukuzwa kazi,” Mhe. Mkuchika ameeleza.

Mhe. Mkuchika amewatahadharisha watumishi wa umma nchini kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) iko kazini na ina utayari wa kumshughulikia mtumishi yeyote atakayetumia cheo chake vibaya ili kujinufaisha na rushwa ya ngono.

Aidha, Mhe. Mkuchika amesema nchi yetu imebahatika kuwa na viongozi wenye utashi wa kupambana na rushwa kuanzia Awamu ya Kwanza ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere hadi Awamu hii ya Tano, inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye amejipambanua kwa vitendo kwa kuanzisha Mahakama ya Mafisadi na Wahujumu Uchumi.


Share:

Mahakama Kupunguza Kutumia Wazee Washauri Kwenye Kesi

 Na Lydia Churi-Mahakama, Bunda
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi amesema Mahakama inakusudia kupunguza kuwatumia wazee washauri wa Mahakama katika kuamua mashauri Mahakamani na itabaki ikiwatumia katika mashauri ambayo yataonekana yana ulazima wa kuwatumia wazee hao.

Akizungumza wilayani Bunda ambapo ameanza ziara ya kikazi kukagua shughuli za Mahakama katika Mkoa wa Mara, Jaji Kiongozi amesema wazee hao watatumiwa na Mahakama kwenye mashauri ambayo yatakuwa na ulazima wa kuwatumia lakini yale ambayo siyo lazima, wazee hao wataacha kutumiwa.

Jaji Kiongozi amesema baadhi ya wazee washauri wa Mahakama hujishirikisha na vitendo vya rushwa na wakati mwingine huwatisha Mahakimu wanapokuwa wakitekeleza wajibu wao.

Alisema matumizi ya wazee washauri wa Mahakama wakati mwingine husababisha mashauri kuchelewa kumalizika kutokana na kuchelewa kwao kufika Mahakamani na kusababisha mashauri kutokusikilizwa kwa wakati.

Akizungumza kuhusu rushwa, Mhe. Dkt, Feleshi alisema Mahakama kama Taasisi haijishirikishi na vitendo vya rushwa bali vitendo hivyo hufanywa na baadhi ya watumishi wasio waaminifu ndani ya Mahakama.

“Tuachane na maneno mepesi mepesi kuhusu rushwa kwa kuwa taarifa zipo, pelekeni Takukuru, hakuna anayemlinda mtu”, alisema Jaji Kiongozi.

Alisema Mahakama itashirikiana na Serikali katika kupambanana na rushwa na hivvo aliwataka wananchi wenye taarifa juu ya vitendo hivyo kuwasilisha kwenye Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa –Takukuru.

Aidha, Mhe. Dkt. Feleshi amesema Mahakama na Serikali katika wilaya ya Bunda wanapaswa kushirikiana katika kutatua changamoto nyingine mbalimbali za wananchi kwa kuwa wote wanamtumikia mwananchi.

Akizungumza na watumishi wa Mahakama ya wilaya ya Bunda, Jaji Kiongozi amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na kubeba matarajio ya Taasisi kwa kutoa huduma bora kwa wananchi.

Aliwataka Mahakimu kumalizika mashauri kwa wakati, pamoja na kutoa nakala za hukumu na mienendo ya mashauri ndani ya muda uliopangwa ambao kwa nakala za hukumu ni siku 21 tangu kumalizika kwa shauri na mienendo ya shauri hutolewa ndani ya siku 30.

Aidha, aliwataka watumishi hao kujenga tabia ya kutafuta na kufahamu taarifa mbalimbali za Mahakama kupitia Tovuti pamoja na Blog ya Mahakama ya Tanzania.

Naye Mkuu wa wilaya ya Bunda Bibi Lydia Bupilipili amewashauri Watumishi wa Mahakama kujenga mazingira yatakayowafanya wananchi kuendelea kuiamini Mahakama ya Tanzania kwa kutoa huduma zilizo bora kwa wananchi.

Alisema Serikali pamoja na Mahakama wilayani Bunda wanashirikiana katika kutatua baadhi ya changamoto za Mahakama huku akitoa wito kwa Mahakimu kutumia njia ya usuluhishi katika kutatua baadhi ya migogoro miongoni mwa
wananchi.

Mkuu huyo wa wilaya pia aliishauri Mahakama ya Tanzania kujikita katika kutoa elimu kwa wananchi hasa kwenye maeneo yenye changamoto zaidi wakati wa maadhimisho ya wiki ya sheria ambayo hufanyika kila mwaka nchini.

Alisema wananchi hawana budi kufahamu taratibu mbalimbali za Mahakma hususan zile za ufunguaji wa mashauri Mahakamani.

Jaji Kiongozi ameanza ziara ya kikazi ya siku tano Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Musoma ambapo atakagua shughuli mbalimbali za Mahakama katika wilaya za Bunda, Serengeti, Tarime pamoja na Musoma.


Share:

Zoezi la Kuandikisha Wapiga Kura Serikali za Mitaa Limeanza Leo..... Rais Magufuli Kawataka Wananchi WaitumieVizuri Haki Hii ya Kidemokrasia

Na Fred Kibano
Serikali imewataka wananchi wote nchini kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba, 24 mwaka huu.

Akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa barabara ya Tunduma hadi Sumbawanga eneo la Naila Halmashauri ya Sumbawanga hapo jana, Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amewaasa watanzania wote kuitumia haki yao ya msingi katika kuendeleza demokrasia nchini kwa kuchagua Viongozi bora wanaojali shida za wananchi waishio katika majijij, miji, vijiji, mitaa na vitongoji ambapo viongozi hao huwajibika kwa wananchi waliowachagua na kuleta maendeleo katika maeneo yao.

“Tumieni nafasi hiyo ya kidemokrasia kuchagua watu ambao ni watetezi wenu na  wanajali maslai ya wananchi”

Aidha, Mheshimiwa Magufuli alitoa rai kwa viongozi wa dini na viongozi wengine kuendelea kuliombea Taifa na viongozi ili wapate nguvu na imani ya kuwahudumia watanzania kwa moya na uzalendo ili kukuza uchumi.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akitoa maelezo ya awali kabla ya hotuba ya Mhe. Rais Magufuli amesema zoezi la Uandikishaji wa wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa litadumu kwa wiki moja kuanzia tarehe 08 Oktoba hadi tarehe 14 Oktoba mwaka huu na kuwataka wakazi wa mkoa wa Rukwa na watanzania wote kutumia fursa hiyo kwani bila kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura watakosa moja ya sifa za mpiga kura.

Kuhusu vituo vya afya mkoani Rukwa Waziri Jafo amesema takribani Halmashauri zote za mkoa wa Rukwa zimepata vituo vya afya na kuahidi kuendelea kujenga vituo vya afya katika nchi nzima.

Rais Magufuli anaendelea na ziara yake mkoani Rukwa ambapo anatarajiwa kuhitimisha ziara yake mkoani humo kwa kufungua hospitali mpya ya Wilaya ya Nkasi pamoja na kituo cha afya Namanyere pia kipo wilayani Nkasi kabla ya kuanza ziara yake mkoani Katavi.


Share:

Rais Magufuli Akerwa na Wanaowapa Mimba Wanafunzi

Rais Magufuli amewataka wakazi wa Mkoa wa Rukwa kuacha tabia ya kuwapa ujauzito wanafunzi na badala yake kutafuta watu ambao wameshamaliza shule.

Ametoa kauli hiyo jana Jumatatu Oktoba 7, alipokuwa akizungumza na wananchi katika uwanja wa Mandela baada ya kuzindua mradi wa maji safi na mazingira na Msikiti wa Istiqaama uliopo eneo la Majengo mkoani humo.

“Kwa takwimu nilizo nazo Mkoa wa Rukwa ni miongo mwa mikoa inayowapa wanafunzi ujauzito, nimeambiwa kwa mwaka jana tu wanafunzi 229 walipata ujauzito, tumeeleza tumekua ukitoa fedha kwaajili ya elimu bure kwa watoto wetu ninyi mnatoa mimba bure sasa tutakuwa tunatoa hela kumbe tunapata hasara

“Ninajua mnakula vyakula vyenye nguvu mkatafute ambao wamemaliza muda wao, msiwaonee hawa wanafunzi na nyie watoto muache viherehere mtayakuta tu baadae kwahiyo hili ni lazima tulisimamie na nyie wazazi tuwafundishe watoto wetu yani unamuona kila siku anaenda kusoma hata daftari hana na unamuacha tu

“Hawa ni watoto masikini tusiwarubuni kwakuwa ni malaika na vyombo vya dola muanze kuwashughulikia hawa watu wanaowapa mimba kwani sheria inajulikana ni miaka 30 akishaenda gerezani ataelewa nini maana ya mimba, hii ni aibu kubwa katika mkoa wenu,” alisema.

Aidha amesema kuwa inasikitisha kuona Mkoa wa Rukwa ambao ni wa pili kwa kuzalisha mazao ndio unaoongoza kwa kuwapa mimba watoto, na hivyo akawataka waachane na tabia hiyo na ile ya kuwozesha watoto wakiwa wadogo na badala yake wawaache wamalize masomo yao kwanza.


Share:

NAIBU WAZIRI WA MADINI AKABIDHIWA KITUO CHA UMAHIRI MKOANI MUSOMA


Jengo la kituo cha umahiri lililopo Musoma
 Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo kushoto, anaefata ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Madini Issa Nchasi wakikabidhiwa funguo ya jengo la Umahiri na Meneja wa SUMA JKT Kanda ya Ziwa Kapteni Fabian Buberwa

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo mbele katikati akifanya ukaguzi wa jengo la umahiri kabla ya makabidhiano, mbele kulia ni Meneja wa SUMA JKT Kanda ya ziwa Kapteni Fabian Buberwa, kushoto ni kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mara Samwel Mayuki, nyuma kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt. Vicent Naano, nyuma kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Madini Issa Nchasi
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Caroline Mthapula akitoa maelezo juu ya sekta ya madini Mara, kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Madini. Issa Nchasi, anaefata ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, na kushoto ni Meneja wa SUMA JKT Kanda ya ziwa Kapteni Fabian Buberwa
Kaimu Meneja wa Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) Veronica Francis akiwakirisha taarifa   za Kituo cha umahiri cha Musoma
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Madini Issa Nchasi akitoa taarifa za kukamilika kwa jengo la kituo cha umahiri Mara

 Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo mbele katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na Viomgozi wa Serikali, Wizara ya Madini pamoja na Wachimbaji wadogo wa Mkoa wa Mara

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mara

Na Tito Mselem, Musoma

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo Oktaba 07, 2019 amekabidhiwa jengo lenye thamani ya shilingi bilioni 1.2 ambalo litatumika kama kituo cha umahiri kwa wachimbaji wadogo wa Madini Mkoani Mara.

Jengo hilo lililojengwa na Mkandalasi SUMA JKT na kukabidhiwa kwa Wizara ya Madini kupitia Naibu Waziri Nyongo,nae pia kalikabidhi jengo hilo kwa Tume ya Madini ambapo limekamilika na liko tayari kwa ajili ya matumizi.

Aidha Jengo hilo la umahiri ni kati ya majengo saba ya umahiri na jengo moja la taaluma lililopo Chuo cha Madini Dodoma (MRI)  yaliyojengwa kwa jumla ya thamani ya Bilioni 11.9 na SUMA JKT kupitia mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) ambayo yamejengwa katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Kagera, Musoma, Bariadi, Chunya, Mpanda, Handeni Tanga na Songea.

Akizungumza kwenye makabidhiano hayo Naibu Waziri Nyongo ameipongeza SUMA JKT kwa kazi nzuri waliyoifanya ya ujenzi wa jengo hilo ambalo limekamika kwa wakati.

Naibu Waziri Nyongo amesema lengo kuu la kuanzisha vituo hivyo ni kuwasadia wachimbaji wadogo kufanya shughuli za madini kwa tija kwa kuwapatia elimu ya uchimbaji katika vituo hivyo.

“faida ya ujenzi huu ni kutoa mafunzo ya kitaalamu yahusuyo Madini, tutatoa mafunzo ya Utafiti wa Madini, ikiwa ni pamoja na kuonesha mikanda ya Madini ilipo na muelekeo wake, uchimbaji wa madini wenye tija na salama, Uchenjuaji wenye kuleta uvunaji mkubwa wa madini na hivyo kuwapatia faida kubwa wachimbaji”, alisema Nyongo.

Inakadiliwa kuwa baada ya mafunzo kupatiwa kwenye vituo hivi, wachimbaji watavuna madini kwa zaidi ya asilimia 80 ukilinganisha na hapo awali ambapo wachimbaji wengi walivuna dhahabu kwa asilimia 30 tu,

Imeelezwa kuwa katika vituo hivi vya umahiri kutakuwa na mafunzo ya kuomba leseni kwa njia ya mtandao na kutakuwa na usagaji wa mawe na kupima sampuli mbalimbali za madini.

Aidha Nyongo ametoa rai kwa wachimbaji wadogo wa Mkoa wa Mara wakitumie kituo hicho cha umahiri ili viwaletee tija na faidsa katika shughuri za uzalishaji madini.

Kwa upande wake kaimu meneja wa mradi wa usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) Veronica Francis alisema kuwa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) ulifanya utafiti wa kijiolojia na kubaini maeneo saba nchini kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya umahiri.

“Utafiti umebaini kuwepo kwa kiwango kikubwa cha dhahabu katika eneo la Buhemba yenye takribani wakia 10,737 zenye viwango vya 0.7g/t ndiyo maana kituo hiki kikaja kujengwa hapa Musoma ili kiwasaidie wachimbaji wadogo kupata mafunzo ya namna bora ya uchimbaji madini,” alisema Veronika.

Pia Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt. Vicent Naano ameipongeza Wizara ya Madini kwa Kujenga kituo cha umahiri katika Mkoa wa Mara maana kitawasaidia sana wachimbaji kufanya kazi kwa uhakika na sio kubahatisha.
Share:

Halmashauri 31 zenye ofisi nje ya maeneo ya utawala Zapewa Siku 30 Kuhamia Maeneo Hayo, Vinginevyo Zitafutwa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),  Selemani Jafo amezitaka Halmashauri 31 zenye ofisi nje ya maeneo ya utawala kuhamia katika maeneo hayo katika kipindi cha siku 30 kuanzia leo Jana Jumatatu Oktoba 7, 2019.

Taarifa iliyotolewa na mkuu wa kitengo cha mawasiliano Serikali Tamisemi,  Rebecca Kwandu inaeleza kuwa Jafo ametoa agizo hilo jana mkoani Rukwa baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa Rais wa Tanzania, John Magufuli kuhusu halmashauri hizo.

Amesema halmashauri itakayozembea kutekeleza agizo hilo itafutwa.

Jafo amesema kuwa agizo hilo kutekelezwa mara moja kuanzia Oktoba 7,  2019.


Share:

BIBI HARUSI AFARIKI 'AKIPIGA SELFIE' KWENYE BWAWA

Bibi harusi na watu wengine watatu wa familia yake wamekufa maji katika bwawa moja la maji baada ya kujaribu kupiga picha ya selfie, kulingana na maafisa wa polisi kutoka jimbo la kusini mwa India la Tamil Nadu.

Waliokufa ni miongoni mwa watu sita walioshikana mikono na kusimama katika kina cha maji marefu karibu na bwawa la Pambar kabla ya mmoja wao kuteleza, na kujaribu kumuokoa mwingine.

Mume wa mwanamke huyo aliweza kumuokoa dadaake lakini wengine wakafa maji. India ina idadi kubwa ya watu wanaofariki kutoka na vifo vya selfie.

India iliripoti vifo vya watu 259 kati ya 2011 na 2017 kulingana na utafiti uliofanywa na shirika la maabara ya tiba nchini Marekani. Inafuatiwa na Urusi, Marekani na Pakistan

Katika jimbo la Tamil Nadu siku ya Jumapili . Wanandoa hao wachanga , kutoka eneo la Bargur katika eneo la Krishnagiri, walikuwa wakiwatembelea watu wa familia yao katika eneo la Uthangarai pamoja na dadake bwana harusi , kulingana na gazeti la Hindu.

Watatu hao waliingia katika maji hayo pamoja na vijana watatu wa familia moja , kabla ya mmoja wao mvulana mwenye umri wa miaka 14 kuteleza na kuwashika dada zake wawili mmoja wao akiwa na miaka 18 na mwengine wa miaka 19, pamoja na wanandoa hao wawili na dadake bwana harusi

Dada huyo alivutwa na nduguye lakini wengine wanne wakapotea ndani ya maji. Maafisa wa polisi wanasema kwamba miili yao baadaye ilipatikana na uchunguzi kufanywa.

Ni kisa cha hivi karibuni miongoni mwa msururu wa vile vya kupiga selfie nchini India. Wataalam walionya kwamba watu wanafanya hatari ili kuwafurahisha watu wa familia zao katika mitandao ya kijamii.

Katika jimbo la Haryana mnamo mwezi Mei , vijana watatu waliokuwa wakipiga picha za selfie katika reli waliruka kutoka katika njia ya barabara hiyo ya treni walipoona gari hilo likikaribia walikokuwa, kabla ya kuuawa na treni nyengie iliokuwa inajiri kutoka upande mwengine wa reli.

Mwaka 2017, Jimbo la India la Karnataka lilizindua kampeni ya kuwaonya watu kwamba selfie zinaweza kuua baada ya kifo cha wanafunzi wanne.

Mwaka huohuo, mtu mmoja alifariki katika eneo la Odisha wakati ndovu ambaye aliuwa akipiga selfie naye alimkamata na kumpiga na chini.
Chanzo - BBC
Share:

BASHE AMLILIA MKURUGENZI MSTAAFI IDARA YA USALAMA WA TAIFA

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema, aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), Apson Mwang’onda (75) alikuwa msaada mkubwa kwake kwenye safari ya kisiasa na uongozi.


Kupitia ukurasa wake wa Twitter, ameandika  kuwa, mzee Mwang'onda alikuwa baba, rafiki, mshauri, na kiongozi.

"Nimepokea kwa masikitiko na uchungu, taarifa za kifo cha baba yetu, rafiki, mshauri, kiongozi na mzee wetu mpendwa Colonel Apson Mwang’onda, mtu ambaye wakati wote wa safari yangu ya kisiasa na uongozi alikuwa msaada mkubwa usiomithilika. Pumzika kwa amani baba"ameandika Bashe 

Mzee Mwang’onda (75) aliaga dunia jana nchini Afrika Kusini.


Share:

Haloteli Yaonywa....Serikali Yaitaka Kutumia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kupeleka mawasiliano nje ya nchi

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imeitaka kampuni ya Simu ya Halotel nchini kutumia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kupeleka mawasiliano nje ya nchi

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye wakati wa ziara yake ya kukagua miundombinu na mwingiliano wa mawasiliano Kabanga mpakani mwa Tanzania na Burundi ambapo alifika kwenye maunganisho ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ambapo panatumika kupeleka mawasiliano kutoka nchini kwenda nchi jirani.

Akiwa kwenye maunganisho hayo, Nditiye alibaini kuwa kampuni ya simu ya Halotel imepeleka mawasiliano yake moja kwa moja kutoka nchini Tanzania kwenda nchi jirani ya Burundi kwa kuunganisha jozi za mawasiliano za kampuni hiyo kwenye Mfumo wa Mkongo wa Burundi (Burundi Backbone System) badala ya kufanya maunganisho hayo kupitia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB)

“Nawaelekeza Halotel watumie Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kupeleka mawasiliano nchi jirani ili kufuata utaratibu uliowekwa baina ya nchi moja na nyingine wa kuvusha mawasiliano yake kwenda nchi jirani kwa kutumia maunganisho ya Mkongo wa nchi moja kwenda maunganisho ya nchi nyingine badala ya kuunganisha mawasiliano kutoka kwa kampuni husika kwenda nchi nyingine moja kwa moja,” amesema Nditiye

Amefafanua kuwa Halotel hawaruhusiwi kufanya hivyo kwa kuwa wanakiuka utaratibu, wanaikosesha nchi mapato na inahatarisha usalama wa nchi kwa kuwa hakuna atakayeweza kufuatilia mawasiliano hayo upande wa pili kwenye nchi jirani

Naye Mhandisi wa Shirika la Mawasiliano (TTCL), Marwa Mwita amepokea maelekezo ya Nditiye na kukiri kuwa hakuna kampuni ya mawasiliano ya simu mkononi inayoruhusiwa kuvusha mawasiliano ya kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine bila kupitia Mkongo wa Taifa wa nchi husika kama vile Burundi, RBS; Rwanda, RDB na Tanzania, NICTBB.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Kanali Michael Mntenjele amemuarifu Nditiye kuwa wilaya hiyo na viunga vyake vinahitaji mawasiliano ya uhakika na yasiyokuwa na msongamano ili kufanikisha suala la ulinzi na usalama wa taifa letu kwa kuwa  wakazi waishio wilayani humo wako mpakani mwa Tanzania na nchi jirani za Burundi na Rwanda

Nditiye amemweleza Mntenjele kuwa Serikali imeielekeza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia umoja wa kampuni za simu za Jumuiya ya Afrika (EACO) kudhibiti mwingiliano wa mawasiliano mpakani na kukubaliana kuwa hamna mtandao wa nchi moja kuingia kwenye nchi nyingine ili kila nchi ipate mawasiliano ya nchini kwake


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne Ya October 8




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger