Monday, 7 October 2019

Tambua Visababishi Vikuu Vinavyosababisha Kupungukiwa Nguvu Za Kiume Na Maumbile madogo

1 ugonjwa wa kisukari, 2 presha,usongo wa mawazo,3 magonjwa ya moyo 4 ngiri tumbo, kuunguruma na kuumwa chini ya kitovu 5 kupiga punyeto kwa mda mrefu 6 kukosa choo au kupata choo kama cha mbuzi 7.maumivu ya mgongo na kiuno 8. joto kali kwenye mfuko wa korodani

Ni nini tiba ya nguvu za kiume; MAJINJAS ni dawa yenye virutubisho ambavyo hutibu matizo  yafatayo 1.kushindwa kurudia tendo 2. kuwahi kufika kileleni 3 .maumbile kulegea

MKULUMO; ni dawa ya kuboresha  saizi upendayo inch 5-8 na unene sm 3-5 za upenyo

MTINJETINJE; ni  dawa ya kisukari hurudisha kongosho katika hali yake ya kawida haijalishi unatumia vidonge au sindano za insulin,

Kumbuka dawa hizi ni tofauti na ulizowai kutumia ni salama na adhina suma ya kukuasili

Fika ofisini kwangu MBAGALA ZAKHEMU KARIBU NA KCB BENKI na mwanza yupo wakala nipigie simu whasApp 0783185060. 0620113431 DR AGU pia utaletewa popote ulipo uduma hizi


Share:

Mvua Yaua Watu Watano Jijini Mbeya

Kufuatia mvua kubwa iliyonyesha Oktoba 06, 2019 katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya imesababisha vifo vya watu watano na uharibifu wa makazi ya watu katika maeneo ya Iyunga Jijini Mbeya.

Mnamo tarehe 06/10/2019 majira ya saa 17:00 jioni huko katika maeneo ya Mwasanga, Kata ya Mwasanga, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya, watu watatu waliofahamika kwa majina ya 1. AJUAYE JAMES @ SANGA [25] fundi ujenzi na Mkazi wa Mwasanga na 2. MARIA JUMA MWASHAMBWA [25] Mkazi wa Uyole na 3. ANGELA SOLO [15] Mkazi wa Mtaa wa Reli – Tembela wamefariki dunia baada ya kusombwa na maji wakati wakivuka darajani baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha kuvunjika kwa daraja la Mwasanga na kuwasomba baadhi ya watu wakiwepo marehemu.

Mwili wa marehemu MARIA JUMA MWASHAMBWA umepatikana leo Oktoba 07, 2019 majira ya saa 07:30 asubuhi pembezoni mwa daraja la Iyunga wakati mwili wa marehemu ANGELA SOLO umepatikana eneo la Utengule ndani ya Mto Nzovwe baada ya jana kupatikana na taarifa za baadhi ya watu waliokuwa wakivuka daraja la Mwasanga kusombwa na maji.

Ufuatiliaji unaendelea kuangalia kama kuna watu wengine wamesombwa na maji. Miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.

Sambamba na hilo, mnamo Oktoba 06, 2019 majira ya saa 18:00 jioni huko eneo la Mbata, Mtaa wa Iyela one, Kata ya Iyela, Tarafa ya Iyung, Jijini Mbeya, watoto wawili waliofahamika kwa majina ya JONATHAS BARAKA MWANGISI [3] na IBRAHIM EFRAHIM [2] wote wakazi wa Mbata Relini wamefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye shimo lenye maji ambalo lilichimbwa udongo kwa ajili ya kufyatulia tofali lakini halikufukiwa hivyo kufuatia mvua iliyonyesha jana shimo hilo lilijaa maji.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya. Upelelezi unaendelea.

Aidha kufuatia maafa hayo yaliyosababisha na mvua kubwa iliyonyesha jana, Kamati ya Ulinzi na Usalama ikiongozwa na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ALBERT CHALAMILA imetembelea na kukagua eneo la daraja la Mwasanga pamoja na maeneo mengine yenye madaraja kama vile Ivumwe na Iyunga na kutoa rai kwa wakazi wa maeneo hayo kuwa makini hasa wakati wa kuvuka maeneo yenye maji mengi pamoja na kuimarisha ulinzi kwa watoto wao.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa rai kwa wananchi wote wa Mkoa wa Mbeya kuchukua tahadhari juu ya mvua na mito inayowazunguka. 

Mvua zinaponyesha msivuke au kufanya shughuli zozote katika maji kwa sasa kikosi maalum cha Polisi kinapita kwenye maeneo yote kuhakikisha usalama wa wakazi wote na madhara yaliyojitokeza yanaratibiwa. Natoa rai pia kwa kamati za maafa za Kata chini ya mtendaji wa Kata kufuatilia usalama wa eneo lake na kupeleka taarifa kwa Mkuu wa Polisi Wilaya [OCD] kupitia kwa Polisi Kata. Kila mmoja awe mlinzi katika muda huu.

Ujenzi mpya wa madaraja unaendelea/unafanywa na Serikali kupitia uratibu unaofanywa na Mhe. Mkuu wa Mkoa.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawapa pole familia zote zilizopotelewa na ndugu zao 05, wapate nguvu katika kipindi hiki cha majonzi.


Share:

MBOWE AMLILIA MTUNZI WA WIMBO WA "CHADEMA PEOPLE’S POWER”

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ametuma salamu za rambirambi kutokana na kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Sanaa ya chama hicho, Fullgency Mapunda (Mwana Cotide).

Mwanacotide ambaye pia ni mtunzi na muimbaji wa nyimbo mbalimbali za chama hicho zikiwamo nyimbo maarufu kama vile Chadema People’s Power na Mafisadi kwa heri, alifariki usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya St. Monica, Manzese jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Katika ukurasa wake wa Facebook, Mbowe amemuelezea msanii huyo kuwa atakumbukwa kwa mazuri yake.

“Nimepokea kwa huzuni kubwa kifo cha Kamanda wetu Fullgence Mapunda Mwanacotide, ni mapema sana Kamanda umeondoka, kimwili haupo nasi lakini utaishi kwenye mioyo ya walio wengi kupitia muziki wako.

“Mara ya mwisho nilikutembelea hospitalini tuliongea mambo mengi, ulisema umefurahi sana kuniona, nikakwambia ni kawaida mtu anapougua binadamu wenzake kumtembelea kumjulia hali na kufarijiana, ukaniambia Chairman (mwenyekiti) wewe una mambo mengi uko busy sana, hadi kuja kunijulia hali ni heshima kubwa Chairman.

“Ulitunga nyimbo nzuri za hamasa katika chama chetu cha Chadema, ambazo zitafanya tukukumbuke kila zitakaposikika masikioni mwetu, kupitia nyimbo zako nzuri kwa chama chetu, daima uliweza kuwagusa wengi kwa njia ya muziki. Vita vizuri umepigana Kamanda na mwendo umemaliza.

“Kwa ujumla ni mengi yapo ya kukuelezea lakini kwa hatua ya sasa tunakuombea kwa Mungu aipokee roho yako na kuipumzisha mahali pema,” ameandika Mbowe.

Share:

MTUNZI WA WIMBO 'CHADEMA PEOPLE'S POWER' AFARIKI DUNIA


Aliyekuwa Mkuu wa Idara ya sanaa CHADEMA makao makuu Fullgency Mapunda (Mwana Cotide) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.


 Enzi za uhai wake aliimba wimbo wa chama hicho wenye maneno "CHADEMA People's Power" ambao ni maarufu hadi sasa. Soma taarifa ya chama hicho hapo chini


Share:

LIVE: Ziara ya Rais Magufuli mkoani Rukwa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli anafanya ziara ya siku tatu Mkoani Rukwa ambapo anafungua na kukagua miradi ya Maendeleo pamoja na kuzungumza na Wananchi wa Maeneo mbalimbali ya Rukwa na Wilaya zake


Share:

Mahakama Kutoa Hukumu Ijumaa Kesi ya Anayedaiwa Kumbaka Binti Yake

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imepanga kutoa hukumu Ijumaa October 11,2019 dhidi ya Kigogo wa TPRI, Aresteric Silayo anayedaiwa kumbaka mwanae wa kike mwenye umri wa miaka 11.

Akizungumza mahakamani hapo juzi, Hakimu Mkazi Aziza Temu, aliyepewa mamlaka na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kusikiliza rufani ya kesi hiyo, alisema amesikiliza hoja za rufani hiyo za pande zote mbili.

"Baada ya kuwasikiliza upande wa utetezi na Jamuhuri, hukumu nitatoa Oktoba 11, mwaka huu," alisema.

Kabla ya hakimu Aziza kupanga tarehe hiyo, alimsikiliza Wakili wa Serikali, Azael Mwiteni, ambaye aliomba mahakama hiyo kutengua uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ya kumwachia huru mtuhumiwa huyo.

"Mheshimiwa naomba utengue uamuzi wa kumwachia huru mtuhumiwa huyu na kuzingatia ushahidi wa mtoto na mashahidi wote waliofika mahakamani hapa kutoa ushahidi unaofanana na usio na mashaka," aliiambia mahakama.

Alieleza ushahidi wa mtoto (jina tunalo) unaonyesha baba (mtuhumiwa) alimbaka mwanawe kwani mtoto aliweza kumweleza Mwalimu shuleni, mahakamani na pia cheti cha daktari aliyemchunguza amethibitisha mtoto huyo kubakwa.

"Kutokana na ushahidi uliotolewa Mheshimiwa utaona utakapopitia jalada hili kuwa mtoto ameeleza bila kubadili maneno, naomba mtie hatiani mshtakiwa na kumpa adhabu stahiki kulingana na kitendo alichokifanya kwa mwanawe.”

Naye Wakili wa Utetezi, John Materu, alidai hoja za Wakili wa Serikali hazina mashiko, kwani mahakama ilimwachia huru baada ya kuona ushahidi uliotolewa mahakamani ulikuwa wa shaka.

Alidai kesi hiyo ya kutengenezwa na ina sababu zake, hivyo hakuna ukweli wowote juu ya tukio hilo.
 


Share:

Mbunge wa Jimbo la Ndanda Cecil Mwambe Ajitosa Kumrithi Mbowe Uenyekiti CHADEMA

Mbunge wa Jimbo la Ndanda (CHADEMA) ambaye ni  Mjumbe wa Kamati kuu na Mwenyekiti wa Kanda ya Kusini Mh Cecil Mwambe ametangaza nia ya kugombea nafasi ya uenyekiti wa chama hicho Taifa, akiahidi kuleta mabadiliko kadhaa katika chama hicho .

Chadema imepanga kufanya uchaguzi wake mkuu Desemba 18, mwaka huu.

Bado haijafahamika kama  Mwenyekiti wa sasa Freeman Mbowe atagombea  tena au  hatagombea.

Uongozi wa Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ulimalizika Septemba 14 na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ilitoa siku saba zinazomalizika leo saa 9.30 alasiri wawe wamewasilisha maelezo kwa nini hawajafanya uchaguzi.


Share:

DC KOROGWE AWAONYA WAANDIKISHAJI NA WAANDAAJI WA ORODHA YA WAPIGA KURA NI WATAKAOBAINIKA KUWAANDIKISHA RAIA WA KIGENI

Share:

Wanafunzi 8 Shule ya sekondari Seeke wilayani Kahama wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa Tuhuma ya kumuua mwanafunzi mwenzao

NA SALVATORY NTANDU
Jeshi la polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga linawashikilia wanafunzi  nane wa shule ya sekondari seeke kwa tuhuma ya kumshambulia na kumjeruhi Costantine Makoye mwanafunzi mwenzao majeraha ambayo yamesababisha kufariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Halmashauri ya Mji Kahama.

Kamanda wa Polisi mkoa  wa Shinyanga ACP Richard Abwao amesethibitisha kushikiliwa kwa wanafunzi hao na kusema kuwa tukio hilo limetokea septemba mwaka katika kanisa la SDA Wasabato Kahama kulikuwa na sherehe ya kuwaaga wanafunzi washirika wa kanisa la SDA wanaotarajia kuhitimu kidato cha NNE.

Kamanda Abwao amewataja Majina wanafunzi hao kuwa ni pamojanaWanafunzi wanane WANASHIKILIWA kuhusiana na tukio hilo AMBAO ni :

1. Isaya  Athuman 18, Muha, mkazi wa nyahanga.

2. Godfrey Fanuel Simon, 18, Mnyiramba, mkazi wa shunu

3.Enock Lazaro Alfred, 17, Mhangaza, Mkazi wa Shunu.

4. Athuman Azizi, 17, Mnyamwezi, mkazi wa shunu,

5. Leonard Emmanuel Lutonja, 17, Msukuma, mkazi wa shunu.

6. Michael Philipo 17, msukuma, Mkazi wa Shunu.

7 . Sadiki Boniface stephen, 18, mfipa, mkazi WA legela

 8.emmanuel musa Sekela, 18, Muha, mkazi wa shunu

Amesema Baada ya sherehe kuisha katika kanisa hilo wakati wanafunzi wanatawanyika alitokea Constantine Makoye akiwa na vijana wenzie wapatao 10 ambao hawajafahamika mara moja na haijulikani kama ni walikuwa ni  miongoni mwa waalikwa katika sherehe hiyo.

Kamanda Abwao amesema wanafunzi hao walimvamia mwanafunzi aitwaye Isaya Athuman (18) mwanafunzi kidato cha nne seeke secondary, na kutaka kumnyang'anya viatu alivyokuwa amevaa na wengine waliwanyang'anya maji ya kunywa wanafunzi waliokuwa katika sherehe hiyo.

Ndipo wanafunzi hao walipopiga kelele na yowe kwamba wamevamiwa, waliungana pamoja na kuanza kuwarushia mawe hao waliovamia sherehe hiyo na Wavamizi hao  walikimbia na kutawanyika lakini Constantine Makoye alizidiwa na kulala chini na wanafunzi hao walimtelekeza hapo.

Amefafanua kuwa Baadae aliamka na kwenda nyumbani kumjulisha Babu yake ambaye alimpeleka kutibiwa katika hospitali ya serikali Kahama bila kutoa Taarifa kituoni hadi alipozidiwa tarehe 01/10/2019 akiwa hawezi kuongea ndipo ndugu walijulisha kituoni na jalada lilifunguliwa kwa kosa la kujeruhi na maelekezo ya mwanafunzi huyo hayakupatikana kutokana na hali yake kuwa mbaya.

 Tarehe 02/10/2019 alifariki dunia wakati anaendelea na matibabu Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na kubaini chanzo cha kifo ni majeraha makubwa kichwani na wamekabidhiwa Ndugu kwa ajili ya mazishi.

Amesema Chanzo cha Tukio hilo ni Madhara ugomvi uliotokana na wanafunzi na watu waliokuwa kwenye eneo la tukio kujichukulia SHERIA mkononi wakimtuhumu marehemu kuwa mwizi.


Share:

Waziri Mkuu Aagiza Afisa Manunuzi, Mzabuni, Kinampanda Wakamatwa Kwa Kughushi Nyaraka

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Singida, Bw. Adili Elinipenda amkamate Afisa Manunuzi wa Chuo cha Ualimu Kinampanda, Bw. Francis Muyombo kwa kukiuka taratibu za manunuzi ya Serikali na kughushi nyaraka.

Pia alimwagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Sweetbert Njewike amkamate na kumhoji Bw. Joseph Kisaka ambaye alikuwa mzabuni wa chuo hicho kwa kuwapatia (kusupply) vifaa ambavyo ni chini ya kiwango.

Alitoa agizo hilo jana jioni (Jumapili, Oktoba 6, 2019), wakati akikagua ukarabati wa majengo ya chuo hicho kilichopo wilayani Iramba, mkoani Singida ambako alibaini delivery note ikionesha kitasa kimoja kimenunuliwa kwa sh. 70,000 badala ya sh. 25,000.

Waziri Mkuu alisema quotation ya manunuzi inaonesha kwamba walipaswa kununua vitasa ambavyo vinafunga mara tatu (vya 3-level) lakini alipokwenda kukagua milango kwenye mabweni, ukumbi, na bwalo alikuta ni vitasa vya kufunga mara moja (vya 1-leavel).

“Serikali imetoa sh. bilioni 1.4 kwa kila chuo ili kufanya ukarabati wa vyuo vya elimu kikiwemo hiki cha kwenu. Ninyi mnanunua vifaa kinyume na utaratibu wa Serikali, hamvikagui, mnaweka tu vitu hafifu ambavyo havidumu. Haiwezekani!”

“Quotation yenu hapa inanionesha mlinunua vitasa 368 vya 3-level kwa gharama ya shilingi 70,000 kila kimoja. Lakini vitasa vilivyoko mlangoni ni vya 1-level ambavyo vinauzwa shilingi 25,000. Haya ni mabweni ya wanafunzi, wanaingi na kutoka kila wakati, ni kwa nini mnaweka vitu cheap wakati mnajua vitaharibika mapema? Maelekezo ya ununuzi wa Serikali yakoje?”

Alipoulizwa wametumia utaratibu gani kununua vifaa hivyo, Mkuu wa Chuo hicho, Bw. Hamisi Njau alisema walikuwa wakitumia kamati ya manunuzi ambayo mwenyekiti wake alikuwa ni Makamu Mkuu wa Chuo na Katibu wake ni Afisa Manunuzi, Bw. Muyombo.

Bw. Muyombo alipoulizwa kama walikuwa wanayo BOQ ambayo ilikua ikiwaongozwa kufanya manunuzi, alijibu kwamba hawakuwa nayo bali alikuwa wakiorodhesha mahitaji yao na kuyapeleka kwa mhandisi.

Alipoambiwa aeleze tofauti ya vitasa vya 3-level na vya 1-level, Bw. Muyombo alijibu kwamba waliambiwa na mhandisi kwamba ndani ya kitasa kuna kibati ambacho kinatofautisha vitasa hivyo.

Waziri Mkuu alisema alisema Serikali inakataa udanganyifu kwenye manunuzi na haitavumilia watumishi wasiokuwa waaminifu. “Tena hili duka la huyo Kisaka ni la nguo wala siyo la hardware (vifaa vya ujenzi).”

Alimwambia Mkuu wa Chuo hicho alipaswa kusimamia ikiwa ni pamoja na ujenzi na ukarabati unaofanyika chuoni hapo.

Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ilitoa sh. 1,439.235,746 ili kukarabati chuo hicho kwenye maeneo ya utawala, maeneo ya kujifunzia, kumbi na mabweni ya wanachuo. Awamu ya kwanza ya fedha hizo iliingia Novemba, 2017 na awamu ya pili ikaingia Juni 2018.

Akizungumza na wanafunzi wa chuo hicho baada ya kufanya ukaguzi huo, Waziri Mkuu alisema Serikali inafanya kazi kubwa ya kuboresha miundombinu ya elimu nchini. “Mheshimiwa Rais alitoa sh. bilioni 1.4 kwa vyuo vyote ili kukarabati na kuboresha hadhi ya vyuo hivyo vikiwemo vya Monduli, Patandi, Kinampanda, Mtwara, Songea, Nachingwea, Korogwe, Kasulu na Butimba.”

“Nimeingia kwenye maktaba yenu nimeona bado vitabu vilivyopo ni vya muda mrefu, lakini kwa upande wa ajira bado tunaendelea kuajiri kwa awamu. Julai mwaka huu tuliajiri walimu 4670 na sasa hivi tumepata kibali cha kuajiri walimu 16,000,” alisema.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Waziri Kigwangalla Afunga Mafunzo Ya Kijeshi Ya Watumishi Mamlaka Ya Hifadhi Ya Ngorongoro – Arusha

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua gwaride la heshima la askari wa jeshi USU alipokwenda kufunga mafuzo ya watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Mbulumbulu wilayani Karatu mkoani ARUSHA.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akikabidhi cheti cha kuhitimu mmoja wa watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro aliyepatiwa mafunzo ya Jeshi USU wakati wa hafla ya kufunga mafuzo ya watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Mbulumbulu wilayani Karatu mkoani ARUSHA.
Askari wa Jeshi USU waliohitimu mafunzo wakionesha uwezo wao wa kufuangua silaha na kuifunga ndani ya muda mfupi wakati wa hafla ya kufunga mafuzo ya watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Mbulumbulu wilayani Karatu mkoani ARUSHA. Askari wa Jeshi USU kikosi maalum wakionesha uwezo wao wa kukabiliana na majangili wakati wa hafla ya kufunga mafuzo ya watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Mbulumbulu wilayani Karatu mkoani ARUSHA.

Askari wa Jeshi USU waliohitimu mafunzo wakipita kwa ukakamavu mbele ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati wa hafla ya kufunga mafuzo ya watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Mbulumbulu wilayani Karatu mkoani ARUSHA.

PICHA – Aron Msigwa –WMU, Arusha.


Share:

Waziri Mhagama: Ni Jambo Jema Vijana Kuenzi Falsafa Za Mwl. Julius Kambarage Nyerere

Na; Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amepongeza vijana kwa kuonesha niya njema ya kuendelea kumuenzi Baba wa Taifa sambamba na kuendeleza mambo mema yote aliyoyafanya enzi za uhai wake.

Ameyasema hayo Oktoba 6, 2019 wakati wa hafla ya kuwaaga vijana 60 waliopanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuadhimisha kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika Marangu, Mkoani Kilimanjaro.

Waziri Mhagama alisema kuwa, Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere alikuwa kiongozi mzalendo kwa nchi yake na aliyejali utu na usawa, hivyo ni jambo zuri kuona vijana wakiendelea kuenzi falsafa za mhasisi wa Taifa hili Mwl. J. K. Nyerere pamoja na Hayati Mzee Abeid Aman Karume ambao kwa kiasi kikubwa wamechangia katika suala zima la kudumisha umoja na msikamano wa Taifa.

“Kitendo hiki wanachofanya vijana kwa kupanda mlima Kilimanjaro ni jambo la kishujaa na uzalendo wa hali ya juu kwa Taifa ni matumaini yangu vijana wengi wataiga mfano huu mzuri,” alisema Mhagama

Alieleza kuwa, Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere alifanya kazi kubwa ya kujenga misingi imara ya nchi kuwa na amani, umoja, mshikamano pamoja na misingi ya kuwa na uchumi wa kujitegemea.

“Vijana mnatakiwa kuendeleza na kuiga utendaji kazi wa Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere alijitolea kwa mambo mengi ili kujenga Taifa, alikuwa mstari wa mbele katika kupambana na mambo mengi ikiwemo  ujinga, maradhi na umaskini ili kila mtanzania awe na maisha bora. Hiyo ilikuwa ni ishara tosha kwa vijana kutambua namna Baba wa Taifa alivyolipigania nchi yetu,” alisema Mhagama

Aliongeza kuwa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Dkt. Alli Mohammed Shein ni mfano tosha wa kuigwa na vijana, wanaonesha namna wanavyojitoa kwa ajili ya Taifa na kuhudumia wananchi pamoja na kukuza uchumi wa nchi. 

Waziri Mhagama alifafanua kuwa, kuelekea kilele cha mbio za mwenge mwaka huu vijana hao waliopanda mlima Kilimanjaro watapata fursa ya kujumuika na vijana kutoka kwenye nchi jirani ikiwemo Angola, Zimbabwe, Msumbiji, Afrika Kusini, Uganda, Rwanda na Kenya katika kongamano la kujadili mchango wa Baba wa Taifa barani Afrika.

Aidha Waziri Mhagama alitoa wito kwa watanzania wote hususan vijana kuendelea kuenzi falsafa za waasisi wa taifa hili Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Mzee Abeid Aman Karume kwa kutambua kuwa waasisi hao ni urithi tosha. Pia aliwasihii vijana kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuyaenzi yaliyofanywa na waasisi hao.

Sambamba na hayo alipongeza vijana ambao walijitolea kupanda mlima huo toka zoezi hilo lilipoanzishwa na Ofisi ya Waziri Mkuu ikiwa ni sehemu ya kuendelea kukumbuka falsafa za Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Pamoja na hayo alitoa shukrani kwa Wizara ya Maliasili na Utali, Uongozi wa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), Taasisi na Wadau kwa kushirikiana na Ofisi yake katika kufanikisha suala hilo muhimu kwa vijana.

Kwa Upande wake, Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Constantine Kanyasu alieleza kuwa suala la vijana hao kujitolea kupanda mlima Kilimanjaro ni kitendo cha kijasiri na kizalendo, itawajengea uwezo wa kuwa mabalozi wazuri wa vijana wenzao na pia wataweza kutangaza Mlima huo na vituo mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini.

“Tumefanikiwa kuweka majina kwenye vituo 5 vilivyopo kwenye mlima huo ili kuwapa hamasa wanaopanda kutambua kuwa wanao uwezo wa kupanda hadi kileleni, kinachotakiwa ni kufuata ushauri utakao kuwa ukitolewa na waongozaji,” alisema Kanyasu

Naye Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba aliwataka vijana kuendelea kutambua kuwa tunu za amani na umoja zilikuwa miongoni mwa falsafa kuu ya Mwalimu Nyerere ambapo matokeo yake ni umoja na mshikamano wa Taifa uliopo hadi sasa.

Pia Mkurugenzi wa Vijana katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bi. Mwanaidi Mohamed Ali alisema kuwa vijana wanapaswa kuendeleza yale yote yaliyofanywa na Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere pamoja na Hayati Mzee Abed Aman Karume ili waendelee kudumisha muungano.

Katika Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2019, Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Maendeleo ya Vijana inaratibu shughuli ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa Vijana. Jumla ya vijana 88 tayari wameshapanda mlima huo ikiwa ni kumbukizi ya miaka 20 ya kifo ca Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

MWISHO


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu Ovtober 7




Share:

Sunday, 6 October 2019

Rais Magufuli Amuagiza IGP Sirro Amtumbue kigogo wa Polisi Rukwa

Rais Magufuli ameagiza kamanda wa polisi wa Wilaya ya Sumbawanga, Polycarp Urio kusimamishwa kazi  kwa madai ya kushindwa kutekeleza maagizo aliyopewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola.

Agizo la Urio aliyekuwa akikaimu nafasi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa kusimamishwa kazi limetolewa leo Jumapili Oktoba 4, 2019 baada ya Rais Magufuli kumpigia simu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro na kumtaka kumsimamisha kazi Urio.

Septemba 30, 2019 alipewa maelekezo ya kuwahamisha kazi askari tisa wa kituo cha polisi Laela kutokana na tuhuma za uonevu na kuomba rushwa lakini hakufanya hivyo.

Leo akiwa kwenye uzinduzi wa barabara ya Tunduma-Sumbawanga,  Rais Magufuli alimuuliza kamanda wa polisi wa mkoa huo,  Mathias Nyange kuhusu askari tisa hao ila alionyesha kutofahamu chochote.

“Sina majina yao, na bahati mbaya sifahamu chochote sikuwepo ofisini aliyekuwepo hakunipa taarifa yoyote kuhusu maelekezo hayo,” amesema Kyando. Baada ya majibu hayo Rais Magufuli alimpigia simu IGP Sirro na kumuagiza kumsimamisha kazi Urio.

Rais Magufuli alimuagiza RPC wa Rukwa, Mathias Nyanda kutekeleza agizo la Waziri Lugola la kuwahamisha vituo vya kazi askari hao 9 wanaotuhumiwa kuwabambikiza kesi wananchi


Share:

Ongeza Nguvu Za Kiume, Maumbire Madogo Pamoja Na Tiba Mbalimbali

MASISA 3 POWER nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa muundo wa vidonge na unga  , Huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-80)   Inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii)  inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa  tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoazaidi ya maratatu (3)bila hamu kuisha wara kuhisi kuchoka na  itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 20-40

SUPER MONGERA  Hurefusha na kunenepesha maumbile madogo yaliosinyaa. Matatizi haya huchagizwa ama husababishwa na tumbo kuunguluma na kujaa gesi,ngili, kisukari, presha korodani moja kuvimba au kuingia ndani nk yote haya yanatibika kabisa na kupona kwa mad mfupi sana,

Pia ninadawa ya vidonda vya tumbo miguu kuwaka moto na kupata nganzi, maumivu ya mgongo na kiuno 

Ni DR CHIPUPA  pekee mwenye uwezo wa kumrudisha mume , mke ,mchumb.

Kwa nini uhangaike na matatizo ya uzazi;   ninadawa ya uzazi kwa pandezote mbili, kupunguza unene kitambi ( nyama uzembe)        kuondoa makovu mwilini, kuzuia mimba kuharibika,kusafisha nyota,  kuzuia majini wachafu, pete ya bahati,

 wasiliana na DR. CHIPUPA 

Call+255 0620510598

watsap +255 0758840958

Huduma hii inakufikia popote ulipo


Share:

Rais Magufuli Atoa Siku 5 TANROADS Wahame Ofisi

Rais Magufuli ametoa siku tano kwa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kuhama katika jengo walilopanga na kuhamia katika jengo la Serikali.

Magufuli ametoa uamuzi huo leo Jumapili, Oktoba 6, 2019 na kumweleza Mtendaji Mkuu wa tanroad Patrick Aron Nipilima Mfugale wakati akizungumza na wananchi wa Sumbawanga wakati wa kuzindua Barabara ya Tunduma – Sumbawanga yenye urefu wa kilomita 223.1 katika eneo la Laela mkoani Rukwa.

Aidha, Magufuli ametoa mwezi mmoja kwa Watendaji akiwamo Mkurugenzi na Meya wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa kuhamisha makazi yao kutoka Sumbawanga Mjini na kuhamia katika mji mdogo wa Laela ili iwe rahisi kuwahudumia wananchi wa maeneo hayo.

Pia, ametoa mwezi mmoja kwa taasisi nyingine za Serikali zilizopanga kwenye majengo ya watu binafsi kuhamia majengo ya serikali.


Share:

Takukuru Ichunguze Watumishi 48 Iramba Kwa Upotevu Wa Fedha ....Asema Ikithibitika Ni Kweli, Lazima Warudishe Fedha Hizo

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Singida, Bw. Adili Elinipenda achunguze watumishi 48 waliojihusisha na upotevu wa fedha kwa njia za udanganyifu.

Ametoa agizo hilo leo jioni (Jumapili, Oktoba 6, 2019), wakati akizungumza na madiwani na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kwenye mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Halmshauri hiyo.

Waziri Mkuu ametoa maeneo saba ambayo ametaka yafanyiwe uchunguzi wa kina ili kubaini upotevu huo. Eneo la kwanza ni upotevu wa makusanyo ya ndani kupitia mawakala wa ukusanyaji mapato (POS) ambapo mawakala wanaokusanya fedha wanashirikiana na watumishi wa Halmashauri na kuzitumia bila kuziingiza benki.

Kuna kundi la watumishi 10 wakiongozwa na mtu wa TEHAMA, wameshirikiana kupata password na fedha zikishakusanywa wanazitoa na kuzitumia bila kuzipelekea benki. Wamesahau kwamba malipo yalipoingizwa mara ya kwanza, data ilirekodiwa kwenye mfumo wa malipo na sisi tunaona ni kiasi gani kimekusanywa.”

Watumishi hao ni Salum Omari (Mtaalamu wa TEHAMA); Adam Mzengi (Mhasibu kahamishiwa Gairo); Rafaeli Nasari; Caroline Makundi (kahamishiwa Singida Manispaa), Edson S. Ally (Afisa Biashara); Martin Kimisho (Mhasibu Msaidizi); Prosper Banzi (Afisa Biashara); Hassan Ponda (Mhasibu kituo cha afya Ndago); Hafidh Ngayunda (Kaimu Mweka Hazina wa Wilaya) na Muhidin Mohammed (Mweka Hazina wa Wilaya) ambaye tayari amesimamishwa kazi kutokana na tuhuma hizo.

Kutokana na upotevu huo, Waziri Mkuu ameagiza Kaimu Mweka Hazina wa Wilaya akae pembeni hadi uchunguzi wa TAKUKURU utakapokamilika.

Akibainisha mchezo mwingine uliochezwa na watumishi wa Halmashauri hiyo, Waziri Mkuu amesema kuna watumishi 38 ambao walilipwa kiasi cha sh milioni 46 ambazo zilikuwa sehemu ya sh. milioni 400 za kujenga vituo vya afya vya Ndago na Kinampanda wilayani humo.

“Hapa nina vocha zote za malipo walipeana fedha watu hawa akiwemo Mkurugenzi wao. Lakini ni kazi gani ambayo kundi lote hili lilikuwa likiisimamia na kustahili kupata malipo hayo? Kutoka makao makuu ya wilaya hadi Ndago au Kinampanda kuna umbali gani?” alihoji Waziri Mkuu.

“Kamanda wa TAKUKURU fanya uchunguzi, fuatilia wote waliohusika sababu majina tunayo, kama hawastahili kulipwa ni lazima warudishe fedha yetu. Hii ni sehemu ya sh. milioni 90 ambazo hazijulikani ziliko na zilikuja kujenga kituo cha afya. Fedha hizi zimekuja na maelekezo rasmi, ni kwa nini zilibadilishwa matumizi,” alihoji.

Waziri Mkuu alisema kuna fedha ya walimu sh. milioni 29 ambayo ilitumwa na TAMISEMI ili kulipa likizo zao lakini Mkurugenzi alitumia kulipia usafirishaji wa makontena ya vifaa vya tiba kutoka Sweden hadi Singida wakati mkataba wa malipo unasema Halmashauri ilipaswa kulipia kutoka bandari ya Tanga hadi Singida.

“Hii fedha ya walimu ya likizo nataka irudishwe mara moja. Pia kuna shilingi milioni 6.86 ambazo mmedai ni malipo ya kukomboa mizigo bandarini wakati vifaa hivyo vilipata msamaha wa kodi. Tena kuna sh. milioni 34 ambazo zililetwa kurekebisha Ikama za walimu lakini hadi leo hazijalipwa. “Kamanda wa TAKUKURU nataka uniambie nafasi ya Afisa Elimu ikoje kwenye suala hili,” alisema.

Pia alisema kuna fedha kujenga machinjio ya kisasa ambayo ililetwa lakini machinjio hayajakamilika hadi sasa. “Tumeleta sh. milioni 100 za machinjio lakini Afisa Mifugo anasema wametumi sh. milioni 20 tu, nataka sh. milioni 80 zimeenda wapi.”

Waziri Mkuu alisema kuna sh. 18,090,000 za Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kutoka vituo vya afya 13 ambazo zimetumika kusafirisha hayo makontena nayo pia irudishwe. “Hivi mnachangisha watu sh. 30,000 kwa ajili ya kupata dawa wakienda kutibiwa lakini leo hawana dawa kwa sababu mmezitumia ndivyo sivyo na wao hawana dawa kwenye vituo hivyo kwa sababu hamjazirejesha.”

“Kamanda wa TAKUKURU fanya uchunguzi kwenye fedha ya mikopo ya akinamama, vijana na wenye ulemavu ambayo ni asilimia 10 ya mapato ya Halmashauri. Fedha hii haijatoka tangu mwaka 2017/2018 na 2018/2019.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger