Friday, 4 October 2019

Watumishi 42 wakiwemo watendaji wa Kata na Vijiji Wafikishwa TAKUKURU Rukwa

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amekabidhi watumishi 42 wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Rukwa kwa uchunguzi wa upotevu wa fedha wa zaidi ya shilingi milioni 916 baada ya kuonekana utetezi wao juu ya upotevu wa fedha hizo kutokuwa na vielelezo vya kutosha.

Mh. Wangabo ametoa maelekezo hayo baada ya kuitisha kikao cha Wakurugenzi, Wawekahazina, wahasibu na watendaji wa vijiji na kata wa halmashauri zote nne mkoani hapa ambao mfumo wa ukusanyaji mapato ngazi ya halmashauri (Local Government Revenue Collection Information System – LGRCIS) kuonesha kuwa fedha za makusanyo yao kubaki mifukoni mwao.

Aidha, Ametoa siku saba kwa wale wote ambao hawajawasilisha fedha za makusanyo yao benki kuhakikisha wanawasilisha fedha hizo ikiwemo wale waliokabidhiwa kwa TAKUKURU na kuonya kuwa endapo fedha hizo hazitawasilishwa kesi hiyo itatoka TAKUKURU na Kuhamia Jeshi la Polisi ili kuwafikisha mahakamani.

“Mimi natafuta fedha ukishindikana tutakufunga, na ndio maana nimesema jambo hili kwanza lishughulikiwe kwanza na TAKUKURU mpaka uturudishie hizo fedha kwa muda maalum ambao nimeutoa, nimeshatoa siku sita zimeisha leo hii natoa siku saba nyingine, wacha hawa ambao watakuwa wamerudisha, wale ambao watakuwa hawajakabidhisha fedha zao, nitatoa siku saba baada ya hapo kesi hii itatoka TAKUKURU na kuhamia polisi ili iende mahakamani,” Alisema

Katika kujadili sababu mbalimbali zinazopelekea fedha za makusanyo kutumiwa bila ya utaratibu maalum mkaguzi wa ndani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Joseph Sengerema amesema kuwa matatizo ya upotevu wa fedha hizo yanasababishwa kutokana na kukiuka sheria ya fedha za Serikali za Mitaa ambayo hairuhusu Mtendaji kufanya matumizi yoyote bila ya ridhaa ya mkurugenzi wa Halmashuri na kabla ya kuwasilisha fedha hizo benki.

“ Ukiangalia katika Halmashuri ya Wilya ya Nkasi mimi nishatahadharisha kwamba, kuna hatari kubwa mtendaji wa kijiji anapokusanya fedha halafu anapeleka fedha hiyo kwa mtendaji wa kata bila ya kuwa na nyaraka maalum inayokiri upokezi wa fedha hizo, kwa hali hiyo unawezaje kusimamia ili fedha hizi zisipotee? Na pia mtendaji wa kata anapozifikisha idara ya fedha anahakikishaje zinfishwa benki kwa wakati?” Alihoji.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda limshukuru Mh. Wangabo kwa kuwasaidia kupambana na upotevu wa mapato katika halmashauri jambo ambalo wamekuwa wakilitolea maelekezo akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya bila ya matunda.

“Usikivu wa watendaji wetu ni mdogo sana lakini nikuahidi kwamba maelekezo uliyoyatoa ya siku saba nitayafanyia kazi na kesho Defaulters (wadaiwa) wote tukutane pale ukumbi mdogo wa halmashauri ili niweze kuwakabidhini kwa Halmashauri ili Mkaanze utaratibu wa uchunguzi,” Alisisitiza.

Mmoja wa Watendaji hao Lusilus Bruno wa Kata ya Kirando, Wilayani Nkasi alikiri kuwepo kwa makosa ya kufanya matumizi kabla ya fedha hizo kufikishwa kwenye halmashauri jambo linalokwamisha kupokelewa kwa fedha pungufu wakati wa kuzipeleka benki na kusema kuwa upungufu huo unatokana na matumizi wanayoyafanya katika shughuli za kila siku za vijiji na kata.

“ Mtendaji wangu wa kijiji Tarehe 15 alinikabidhi shilingi 439,500/= ambazo tulitoa matumizi ya shilingi 150,000/= ambayo tuliandika dokezo kama kawaida na kumpa Mkurugenzi akakataa na kusema kuwa matumizi hayo ni makubwa, hilo deni likafika shilingi 540,100 kwa maana kwamba ile bili ilikuwa bado inasubiri ile 150,000 ili iende benki lakini mpaka jana ilikuwa bado makusanyo ni shilingi 100,800/= ambazo alinikabidhi kwahiyo tulishindwa kusafisha bili kwasababu ya upungufu wa shilingi 150,000,” Alisema.

Kati ya hao waliokabidhiwa TAKUKURU watumishi 22 ni watendaji wa kata na vijiji kutoka Halmashauri ya wilaya ya Nkasi, na watumishi 18 ni watendaji wa kata na vijiji kutoka Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga na mmoja ni mweka hazina na mhasibu wote wa Wilaya ya Nkasi na wengine 16 kutoka halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga walitakiwa kuandika maelezo pamoja na kuambatanisha vielelezo vya kuwasilisha fedha zao kwa mweka hazina wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. 

IMETOLEWA NA
OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA


Share:

Lugola Awaondoa katika nyadhifa zao vigogo watatu wa Jeshi la polisi Nkasi

Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amewaondoa katika nyadhifa zao vigogo watatu wa polisi wa Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa kwa madai ya kushindwa kutimiza majukumu yao.

Walioondolewa ni mkuu wa polisi Wilaya ya Nkasi, mkuu wa upelelezi wa Wilaya hiyo na mkuu wa kituo cha polisi Namanyere.

Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Oktoba 4, 2019 katika ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Twitter ya wizara hiyo inaeleza kuwa Lugola amewasimamisha viongozi hao kwa kushindwa kudhibiti wizi wa ng'ombe 278 za wananchi na kuupuza taarifa zinaporipotiwa katika vituo cha polisi.



Share:

Ditram Nchimbi Aongezwa Kwenye Kikosi Cha Taifa Stars, Baada Ya Jana Kupiga Hat-trick

Kaimu Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars”, Ettiene Ndairagije amemuongeza kwenye kikosi cha Taifa Stars, mshambuliaji wa timu ya Polisi Tanzania, Ditram Nchimbi baada ya jana kuifungia timu yake ya Polisi Tanzania magoli matatu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) ulimalizika kwa sare ya kufungana 3-3 na Yanga SC katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaaam.



Share:

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Awatimua wanafunzi wa Kidato cha Tano na Sita.....Ni baada ya jana Kuwacharaza vikobo Wanafunzi 14

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila, jana October 4 alichalaza bakora wanafunzi 14, katika Shule ya Sekondari Kiwanja iliyopo Chunya mkoani Mbeya kwa madai ya kukutwa na simu za mkononi jambo ambalo ni kinyume na na utaratibu wa shule

Asubuhi ya Leo Ijumaa, RC  Chamila  amefika tena  katika shule hiyo   na kuagiza wanafunzi wote wa kidato cha 5 na 6  warudi nyumbani hadi Oct 18,2019   kwa kosa la kuchoma Bweni.

RC Chalamila ameeleza sababu ya kuwarudisha wanafunzi hao makwao ni kutokana na kile kinachodaiwa, waliteketeza kwa moto mabweni yao baada ya walimu wao kuwanyang'anya simu, ambapo amewataka warudi, Oktoba 18, huku kila mmoja akipaswa kulipa kiasi cha Shilingi 200,000 na wale waliokamatwa na simu za mkononi, ameamuru walipe  kiasi cha Shilingi 500,000 na warudi shuleni wakiwa na wazazi wao.

"Mliochoma Mabweni, nawaambia kama mna hamu na mnawashwa kuchoma vitu, mkachome nyumba za wazazi wenu. Kuanzia sasa nafunga form 5 na 6, mnaondoka kwenda kwenu, na ikifika saa 4 bado mnang'ang'a hapa, mtakung'utwa kichapo cha kufa mtu na Walimu mnaowafundisha mtaenda likizo kidogo na ninyi wote mtakuja na laki 2 na waliokamatwa moja kwa moja na simu mtakuja na laki 5 na wazazi juu.

"Kwa hiyo Mkuu wa Shule, Afande RPC, Afande OCD, sitaki kuona form 5 na 6, wataondoka watarudi hapa tarehe 18. Na nyie form 4 kama kuna watu watafanya fujo, nitawatimua hata kama mitihani ni kesho, nafuta darasa zima.  - RC Chalamila

Akizungumzia suala la kuwachapa viboko wanafunzi hao 14, Chalamila amesema kuwa yeye ndio bosi wa Mkuu wa shule katika mkoa na hivyo anaowajibu wa kutoa adhabu kwa wanafunzi wote wanaoonesha utovu wa nidhamu shuleni.

"Jana niliwacharaza viboko watoto, wengine wamenijadili kwenye mitandao wakihoji Mkuu wa Mkoa anatoa wapi mamlaka haya. Bosi wa Mkuu wa Shule ni Mkuu wa Mkoa. Sasa kama Mkuu wa Shule anaruhusiwa kuwachapa, basi mimi (Mkuu wa Mkoa) natakiwa niwacharaze sana."- RC Albert Chalamila

Aidha RC Chalamila ameongeza kuwa hakuna mwanafunzi yeyote atakayeruhusiwa kuhama shule,hadi pale atakapokuwa amekamilisha kulipa kiasi hicho cha pesa na kuuagiza uongozi wa shule, kuhakikisha ujenzi wa mabweni hayo unaanza mara moja pindi pesa hizo zitakapoingizwa kwenye akaunti ya shule.


Share:

Serikali Yafungua akaunti maalum ya watuhumiwa wa uhujumu uchumi waliokiri makosa yao .....DPP Awaonya mawakili

Serikali imefungua akaunti maalum ambayo watuhumiwa wa uhujumu uchumi waliokiri makosa yao wataweka fedha wanazotuhumiwa kuhujumu, ili kuachiwa huru. 

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) nchini Tanzania, Biswalo Mganga  jana Alhamisi October 3.

DPP hakuna fedha itakayolipwa kwenye akaunti ya mahakama, ofisi ya Taifa ya Mashtaka au Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

 “Ambaye atalipa kwingine huko tusilaumiane, lazima fedha ziende zinapotakiwa kwenda, si mawakili wa Serikali, si watumishi wa ofisi hii au mtu yeyote atakayefanya vitendo vya rushwa tutamvumilia,” amesema

Biswalo amefikia hatua hiyo baada ya kuwepo baadhi mawakili wanaochukua fedha kwa washtakiwa na kusema wanapeleka ofisini kwake ila hawafikishi. Amewaonya kuacha tabia hiyo kwa sababu wanatafuta ugomvi.


Share:

Walichokisema CHADEMA Kuhusu Barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekiri kupokea barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini kuhusu Uchaguzi Mkuu wa ndani wa Chama hicho, na kusema Chama hicho hakijakiuka Sheria ya Vyama vya Siasa Nchini wala Katiba ya Chama.

CHADEMA wamesema Katiba ya Chama hicho, ibara ya 6.3.3 (a) inatoa mamlaka kwa Kamati Kusogeza mbele uchaguzi mkuu wa ndani ya Chama, na kwamba Mamlaka ya kufanya marekebisho hayo yameachwa kwa Kamati Kuu .

CHADEMA wamesema Kamati Kuu ya Chama ilikaa katika kikao chake cha tarehe 27 na 28, Julai, 2019, na kurekebisha ratiba ya uchaguzi ambapo utakamilika mwezi Disemba kwa ngazi ya Taifa na Katika hatua ya sasa, Chama kinaifanyia kazi barua hiyo ili iweze kuifikia Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ndani ya muda husika uliotajwa.



Share:

Umoja Wa Mataifa Waipongeza Tanzania Kwa Ulinzi Wa Amani Ukanda Wa Maziwa Makuu

Na Mwandishi Wetu,
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Amina Mohammed ameisihi Tanzania kuendelea kuimarisha amani katika ukanda wa maziwa makuu pamoja na kuendelea kuchangia kutoa askari wa vikosi vya ulinzi wa amani duniani.

Naibu Katibu Mkuu Dkt. Amina Mohammed ametoa wito huo alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiorikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) Jijini New York nchini Marekani na kuongeza kuwa Umoja wa Mataifa unatambua mchango wa Tanzania katika ulinzi wa amani duniani na kwamba Umoja huo uko tayari kushirikiana na Tanzania katika kuendeleza jitihada hizo ili kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi.

“Tanzania imekuwa muhimili muhimu katika kuhimiza amani katika ukanda wa maziwa makuu ikiwa ni pamoja na kuhifadhi wakimbizi kutoka ukanda huo kwa miaka mingi bila kuchoka” alisema Dkt. Amina

Kwa upande wake waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amesema kuwa Tanzania inatambua nafasi ya Umoja wa Mataifa na kwamba itasalia kuwa mwanachama wa umoja huo.

“Napenda kukuhakikishia kuwa Tanzania itaendelea kutoa askari wake katika vikosi vya ulinzi wa amani katika maeneo mbalimbali duniani,” alisema Prof. Kabudi

Waziri Kabudi aliendelea kumueleza Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa hatua mbalimbali ambazo Tanzania imepiga katika masuala ya maendeleo endelevu (SDGs) ikiwa ni pamoja na afya,maji, ushirikishwaji wa wanawake katika maamuzi pamoja na masuala ya kuimarika kwa demokrasia nchini.

Prof. Kabudi amehitimisha ziara yake ya kikazi nchini Marekani alipokuwa akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.


Share:

Watu 13 wafariki dunia katika ajali ya basi Kisumu Kenya

WATU 13 wamefariki dunia na wengine kujeruiwa katika ajali ya basi lililokuwa linatoka soko la Awasi Kisumu kuelekea Nairobi nchini Kenya.

Kwa mujibu wa duru za Kenya ajali hiyo ilitokea majira ya saa tano na nusu, usiku wa kumkia leo.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Kisumu, Benson Maweu amethibitisha kutokea ajali hiyo na kusema kuwa, miili 13 imetolewa katika eneo na ajali na kwamba, kuna watu wengine kadhaa waliojeruhiwa katika ajali hiyo.

Kamanda huyo wa polisi amesema kuwa, basi hilo lilikuwa likisafiri kutoka Kisumu kuelekea Kericho.

Imeelezwa kuwa, ajali hiyo ilihusisha basi hilo na lori moja na kwamba, miongoni mwa waliofariki dunia yumo mtoto mmoja.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, dereva wa lori ni miongoni mwa watu waliofariki dunia katika ajali hiyo na  kwamba majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa October 4























Share:

Thursday, 3 October 2019

JAMAA AJITUPA BAHARINI KUJARIBU KUVUKA BAHARI KWA KUOGELEA

Kizaazaa kilizuka katika kivukio cha feri Likoni kaunti ya Mombasa nchini Kenya baada ya jamaa kujitupa Bahari Hindi na kujaribu kuvuka kwa kuogelea. 


Baada ya kujirusha baharini, Timiza alianza kuogelea akielekea ng'ambo ya pili huku umati ukiachwa na mshtuko. 

Inasemekana kuwa Timiza alichukua hatua hiyo kufuatia kusitishwa kwa muda kwa kuhuduma za feri kufuatia mkasa uliotokea Jumapili, ambapo gari lililokuwa limewabeba mama na mwanawe lilidondoka na kutumbukia baharini.

Iliwalazimu wapiga mbizi kuchukua hatua ya dharura na kumuokoa kabla ya kumkabidhi kwa maafisa wa polisi.

Shughuli ya kuitafuta miili ya Mariam Kigenda na bintiye Amanda Mutheu imefikia siku ya nne bila mafanikio kutokana na utata ambao umeikumba oparesheni nzima.

Mariam Kigenda na bintiye Amanda Mutheu

Oparesheni hiyo imekumbwa na utata wa aina yake hususan baada ya mpiga mbizi wa binafsi aliyetafutwa na familia ya waathiriwa kujiuzulu kwa madai ya kuhangaishwa na Jeshi la Wana Maji. 

Jeshi hilo lilimshutumu Musa Sila kwa kutoa taarifa ya kupotosha kwa familia ya waathiriwa wa mkasa huo kuhusu oparesheni nzima inavyoendeshwa na kule iliko miili ya wapendwa wao. 
Chanzo - Tuko
Share:

Wizara Ya Afya Yatoa Taarifa Ya Mwenendo Wa Magonjwa Ya Milipuko Nchini...Yasisitiza TANZANIA HATUNA UGONJWA WA EBOLA

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekuwa kiktoa taarifa kwa wananchi mara kwa mara kuhusiana na mwenendo wa magonjwa ikiwemo magonjwa ya milipuko (epidemic diseases) nchini na hatua zinazochukuliwa kuzuia na kudhibiti magonjwa haya.

Magonjwa yanayofuatiliwa kwa karibu na kutolewa taarifa mara moja pindi yakitokea ni, kumi na nne (14) ambayo ni pamoja na  Kipindupindu, Polio, Kimeta, Kuhara Damu, Homa ya Uti wa Mgongo, Mafua makali ya ndege, Surua, Pepopunda ya watoto wachanga, Kichaa cha Mbwa, Ndui, Magonjwa yanayosababishwa na Virusi na Homa yanayosababisha damu kuvuja (Ebola, Marburg, RVF, Homa ya Dengue, Chikungunya), Macho mekundu, Tauni, na Homa ya Virusi ya Manjano.

Utoaji wa taarifa za magonjwa haya zimerahisishwa, ambapo vituo vyote vya kutoa huduma za Afya  nchini kuanzia ngazi ya chini hutoa taarifa hizi kwa kupitia mfumo maalum kwa njia ya simu (Integrated Disease Surveillance and Response – IDSR). Hii hupelekea taarifa zote muhimu kuhusu magonjwa kupatikana kwa haraka na hatua kuchukulia mapema na wizara ili kudhibiti magonjwa haya.

Kwa kipindi cha mwezi Septemba 2019, Wizara imeendelea kufuatilia magonjwa haya na matukio  hatarishi kwa afya, kutoka kwenye mikoa yote nchini. Katika mwezi Septemba, ugonjwa wa Dengue na Surua tu ndio magonjwa ya milipuko yaliyotokea hapa nchini.

Kwa Kipindi cha mwezi Septemba 2019, jumla ya wagonjwa 10 walithibishwa kuwa na Homa ya Dengue na hakukuwa na kifo. Wagonjwa hawa walitolewa taarifa kutoka mikoa 2 ambayo ni Dar es salaam – wagonjwa 4 (Hospitali ya Taifa Muhimbili – 4) na Tanga – wagonjwa 6 (Tanga jiji – 6). 

Ugonjwa huu umeendelea kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa nchini na umeendelea kupungua mwezi hadi mwezi.

Takwimu za miezi mitatu (Julai, Agosti na Septemba, 2019) zimeonyesha kupungua kwa ugonjwa huu kwa kiasi kikubwa ambapo mwezi Julai 2019 kulikuwa na wagonjwa waliothibishwa 732, mwezi Agosti wagonjwa 92 na mwezi Septemba wagonjwa – 10.  

Aidha tangu mlipuko huu uanze mwezi Januari  2019 hadi kufikia tarehe 30 Septemba, 2019 kumekuwa na  jumla ya wagonjwa waliohisiwa kuwa na Dengue 14,369 na kati yao  waliothibishwa ni 6,785 na vifo 13 (Dar-6259, Tanga-365, Pwani-115, Morogoro-22, Lindi-8, Arusha-5, Singida-3, Dodoma-3, Ruvuma-2, Kagera-2 na Kilimanjaro-1).

Ili kukabiliana na magonjwa yaenezwayo na wadudu dhurifu wakiwemo mbu,  Wizara ilizindua mpango mkakati wa kukabiliana na wadudu dhurifu na mbu (National Vector control strategy 2019 – 2023) tarehe 27 Julai 2019, Dar es Salaam. 

Uzinduzi huu uliambatana na uzinduzi wa kitaifa wa zoezi la upuliziaji wa dawa kupambana na mbu wapevu na unyunyiziaji wa dawa za kuua viluwiluwi  wa mbu waenezao magonjwa kama vile Malaria, Dengue na nk,. 

Dawa za kuangamiza wadudu zilinunuliwa pamoja na mashine kubwa (4) za kupulizia dawa (Fogging Machine) ambazo zilisambazwa katika mikoa iliyoathirika na ugonjwa wa Dengue yaani Dar es Salaam, Tanga pamoja na Dodoma. Wizara imeshaagiza mashine nyingine 4 ili kuweka mkakati endelevu wa zoezi hili.

Mikoa hii pia (Dar es salaam, Dodoma, Tanga) ilishafanya uzinduzi wa Mkakati wa Kudhibiti Mbu na Wadudu wadhurifu pamoja na kuendesha zoezi la kuangamiza mbu. Hatua hii imesaidia kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Dengue nchini kama inavyoonyeshwa katika takwimu. 

Aidha, zoezi hili la uzinduzi linaendelea kufanyika katika Mikoa yote ili kutokomeza magonjwa yaenezwayo na wadudu hao. Elimu endelevu pia inaendelea kutolewa kwa wananchi juu ya namna kujikinga na kudhibiti ugonjwa huu

Mwenendo wa Ugonjwa wa Kipindupindu nchini.
Ugonjwa wa Kipindupindu umedhibitiwa, na kwa sasa HATUNA KABISA mgonjwa wa Kipindupindu nchini. Mara ya mwisho kupata mgonjwa wa Kipindupindu nchini ilikuwa tarehe 14 mwezi Julai 2019.

Kwa kipindi cha kuanzia tarehe 1 Januari hadi Julai 2019, kulikuwa na jumla ya wagonjwa 424 na vifo 8 vya ugonjwa wa Kipindupindu. 

Wizara inaendelea kuchukua hatua za kudhibiti ugonjwa huu, ikiwa ni pamoja kufuatilia hatua zinazochukuliwa za kuzuia ugonjwa huu na timu ya Mkoa na   Halmashauri ambazo ni pamoja na; Kutoa elimu ya afya kwa wananchi ya namna  kujikinga kupata ugonjwa huu, Ufuatiliaji wa usafi wa mazingira.

Wizara inakamilisha Mpango Mkakati wa Kipindupindu wa mwaka 2019 hadi 2023 ambao utekelezaji wake utajikita katika maeneo yanayotoa wagonjwa mara kwa mara (Hotspot areas) ambayo ni Dar es Salaam (Halmashauri zote), Ngorongoro (Arusha), Simanjiro (Manyara), Handeni na Mkinga (Tanga), Kilwa (Lindi), Ulanga (Morogoro), Mbarali na Chunya (Mbeya), Songwe, Sumbawanga DC (Rukwa), Mpanda (Katavi), Nyasa (Ruvuma) na Iringa DC (Iringa). Mpango huu, unalenga kutokomeza Kipindupindu kabisa. 

Katika mpango huu maeneo yalijikita ni pamoja na: Uratibu na ushirikishwaji wa wadau katika ngazi zote katika kudhibiti ugonjwa, kuimarisha ufuatiliaji na upimaji wa wagonjwa, Kuimarisha utoaji wa matibabu sahihi na mapema kwa wagonjwa, ushirikishwaji wa jamii katika kudhibiti na ugonjwa, kuweka mazingira ya kuwepo kwa maji safi na salama na masuala ya matumizi ya vyoo na vilevile kuimarisha utoaji wa chanjo kwa maeneo sugu na vigezo vitakavyotumika.

Wizara imeendelea pia na utekelezaji wa Kampeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira yenye kaulimbiu isemayo “USICHUKULIE POA NYUMBA NI CHOO”, ikiwa ni moja ya mikakati ya kutokomeza Kipindupindu na magonjwa ya kuhara. Kampeni hii ambayo ipo katika awamu ya pili, ilizinduliwa rasmi Disemba, 2017 na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Uanzishwaji wa Kampeni hii ni sehemu ya jitihada za serikali kujielekeza katika kutekeleza lengo namba 6.2 la Malengo ya Maendeleo Endelevu (Sustainable Development Goals) pamoja na lengo namba 3 linahusu kuboresha Afya. Katika kipindi cha miaka mitatu ya utekelezaji (2016-2019), jumla ya kaya 2,464,225 zimejenga au kuboresha vyoo kufikia kiwango cha ubora kati ya lengo la kaya 3,360,000. Hii ni sawa na asilimia 73.3. Kwa upande wa taasisi, shule 1,670 kati ya lengo la shule 2,520 zimejenga vyoo bora kwa kuzingatia uwiano.

 Kwa ujumla kaya zenye vyoo bora katika ngazi ya kaya zimeongezeka kutoka asilimia 46 Julai, 2016 hadi asilimia 57.2 Juni, 2019, na kaya zisizokuwa na vyoo zimepungua kutoka asilimia 7.5 hadi asilimia 2.5 katika kipindi hicho.

Mwenendo wa Ugonjwa  wa Surua nchni.
Katika kipindi cha mwezi Septemba 2019, mlipuko wa ugonjwa Surua ulitokea katika kitongoji cha Kashasha, Kakoma na kijiji cha Kibare wilayani Kyerwa mkoa wa Kagera. 

Jumla ya wagonjwa 17 walipatikana na ugonjwa wa surua ambapo kati yao; wagonjwa saba walithibitishwa kwa kipimo cha maabara. Mgonjwa wa mwisho kupatwa na dalili za surua katika eneo la Kibare ilikuwa tarehe 14/09/2019. Kwa takribani wiki mbili sasa hakuna mgonjwa mwingine aliyepatikana. Wagonjwa wote wamepona na elimu ya jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa surua imetolewa na pia kuhamasisha kuwaleta watoto katika kampeni ya kitaifa shirikishi  ya chanjo ya surua na rubella, watoto wote chini ya miaka mitano.

Katika ufuatiliaji wa ugonjwa surua nchini wagonjwa wenye dalili za homa na vipele hufuatiliwa na kuchukuliwa sampuli kupima kubaini kama wana ugonjwa wa surua. Kwa kipindi cha mwezi Septemba 2019, jumla ya sampuli 222 za wagonjwa waliokuwa na dalili ya homa na vipele zilipokelewa na kufangashwa na kuwasishwa maabara ya Taifa kutoka  kwenye mikoa 23 ya Tanzania bara.

Mwenendo wa Ugonjwa wa Polio nchini.
Hadi sasa hakuna mgonjwa wa Polio aliyethibika hapa nchini tangu mwaka 1996. Hii inatokana na jitihada kubwa za Serikali katika kutoa chanjo na kufuatilia dalili za wagonjwa wenye ugonjwa huu na pia kwa kununua chanjo za Polio ambazo zimeweza kuwafikia watoto wote chini ya miaka mitano (5) kwa zaidi ya asilimia 90%. 

Katika ufuatiliaji wa ugonjwa huu, wagonjwa wote wa dalili za kupooza ghafla (Acute Flaccid Paralysis – AFP) hufuatiliwa na sampuli kuchukuliwa na kupimwa kujua kama wana ugonjwa wa Polio. Kwa mwezi Septemba 2019, jumla ya sampuli 63 za AFP 63 zilifungashwa na kupelekwa maabara kwa ajili ya vipimo.  

Aidha katika  ufuatiliaji wa virusi vya polio katika mazingira, ambapo kirusi hiki pia hukaa kwa muda nao unaendelea na hadi sasa kirusi hiki kimeonekana kuwa hakipo katika mazingira yetu. Ufuatiliaji wa mara kwa mara unaendelea. .

Katika mpango wa kutokomeza vifo na ulemavu kutokana na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo. Wizara ya Afya kupitia Mpango wa Taifa wa Chanjo na kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, itaendesha kampeni ya chanjo dhidi ya Magonjwa ya Surua, Rubella na Polio mnamo tarehe 17 hadi 21 mwezi Octoba 2019. Kampeni hii itafanyika nchi nzima kwa watoto wote lengwa walio na umri wa chini ya miaka mitano. Nawasihi wananchi wote washiriki ili Serikali ifikie lengo la kampeni hii.

Mwenendo wa Ugonjwa wa Ebola unaoendelea kuripotiwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)
Wizara imekuwa ikifuatilia kwa karibu mwenendo wa ugonjwa wa Ebola unaoendelea kuripotiwa nchini DRC na kuchukua hatua za tahadhari za kuzuia na kukabiliana na ugonjwa huu hususani kwa kuwa kwa sasa ugonjwa huu unaendelea kusambaa na kuingia kusini mwa DRC. 

Takwimu zinaonyesha kuwa hadi kufikia  tarehe 30 Septemba 2019, jumla ya wagonjwa 3,194 walithibitishwa kuwa na ugonjwa huu, na vifo 2133 (CFR 66.8%). 

Kutokana na ukaribu wa nchi hii na Tanzania, Wizara imeendelea kuchukua hatua za utayari kuzuia na kujiandaa kukabiliana na ugonjwa huu

Hatua za utayari na kujiandaa kukabiliana na ugonjwa huu nchini ni pamoja na  kuimarisha uchunguzi wa Wasafiri kwenye mipaka yetu yote. 

Kuimarisha utambuzi katika ngazi ya vituo vya kutolea huduma za Afya; Kuhakikisha uwepo vya Vifaa Kinga hususani kwa watumishi wa Afya; Kuimarisha utambuzi  wa Ugonjwa na kuendelea kutoa Elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kujikinga ugonjwa huu. 

Wizara inayo namba ambayo hutumika bila malipo na wananchi kutoa taarifa za kuwepo kwa tetesi za ugonjwa huu ambazo ni 0800110124 au 0800110125. 

Kuanzia 2018 hadi sasa, tetesi 28 za wagonjwa wanaohisiwa kuwa na Ebola (washukiwa 2 kwa mwezi Septemba), zimekwisha kutolewa taarifa na uchunguzi kufanyika kwa ukamilifu na kuthibitisha wagonjwa hawa hawakuwa na Ebola, na taarifa zake kupelekwa pia katika Shirika la Afya Duniani. 

Aidha Wizara imeendelea kufanya pia mazoezi ya kujinoa na kijipima utayari wa kukabiliana na ugonjwa huu (Simulation Exercises) katika mikoa ya Dar es Salaam, Kagera, Kigoma, Kilimanjaro na Arusha.

NAPENDA KUSISITIZA KUWA HADI SASA HAKUNA MGONJWA ALIYETHIBITISHWA KUWA NA UGONJWA WA EBOLA HAPA NCHINI. WIZARA INAWASIHI WANANCHI KUTOKUWA NA HOFU NA KUPUUZA TAARIFA ZINAZOTOLEWA KILA KUKICHA NA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI NA MITANDAO YA KIJAMII.

Katika kudhibiti ugonjwa wa Ebola na magonjwa mengine ya milipuko yenye madhara makubwa duniani, nchi yetu kila wakati imekuwa mstari wa mbele ikiwa ni pamoja na kusimamia kwa ukamilifu na kutekeleza Kanuni za Kimataifa za Afya (International Health Regulation – IHR 2005). 

Mnamo mwaka 2016, Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza duniani kuweza kukubali bila kipingamizi kuleta wataalam duniani kuja kupima utayari wa nchi yetu katika kukabiliana na magonjwa haya hatarishi (Joint external evaluation). 

Hatua hii kubwa na ya uwazi ilifanywa kwa mara ya kwanza Duniani, kama moja ya njia ya kuhakikisha nchi wanachama wa Shirika la Afya Duniani, wanatekeleza Kanuni hizi za Kimataifa (IHR 2005). 

Aidha nchi nyingine zenye uwezo mkubwa duniani zilisita kufanyiwa tathmini hadi miaka miwili baadae, na nyingine hadi sasa hazijafanya zoezi hili. 

Hivyo basi, taarifa zinazoenea kuelezea kuhusu Tanzania kutokuweka wazi taarifa za magonjwa hususan uwepo wa ugonjwa wa Ebola nchini, si za kweli na hivyo ziendelee kupuuzwa. 

Taratibu za utoaji wa taarifa za magonjwa ya milipuko zinajulikana  na ninatoa rai kwa sote tuzingatie sheria na taratibu za nchi husika na za kimataifa.

Ikumbukwe kuwa, ugonjwa wa Ebola ambao unaweza kusambaa kwa haraka, na ambao madhara yake ni makubwa na yanajulikana duniani kote, kamwe hauwezi kufichwa na nchi yetu. 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua madhara makubwa ya kuficha ugonjwa kama huu kwa wananchi. 

Narudia tena na kuwataka wananchi  kutulia na kupuuza taarifa zisizo rasmi kutoka kwenye baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, maana HAKUNA UGONJWA WA EBOLA NCHINI TANZANIA. 

Inaonekana kuna njama ovu za kueneza taarifa hasi dhidi ya nchi yetu. Ninaendelea kuwasihi Wananchi kuwa watulivu na kushikamana kwa pamoja katika kuzuia ugonjwa huu usiiingie nchini. 

Aidha, Serikali inapenda kuwahakikishia Mataifa yote kuwa nchi yetu ni SALAMA na HATUNA UGONJWA WA EBOLA. 

Nirudie tena kusisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na nchi na mashirika mbalimbali ya kimataifa ikiwemo Shirika la Afya Duniani katika kujenga utayari wa kukabiliana na tishio la ugonjwa wa Ebola. 

Na endapo kutatokea mtu atakaethibishwa kuwa na ugonjwa wa Ebola nchini tutaendelea kuzingatia miongozo na taratibu za kimataifa ikiwemo kutoa Taarifa WHO kwa mujibu wa Kanuni za Kimataifa za udhibiti wa magonjwa hatari ya kuambukiza (IHR 2005).

Kipaumbele cha Wizara kwa sasa ni kuendelea kuimarisha utayari wa kukabiliana na ugonjwa huu usiingie nchini na endapo kutatokea kisa cha ugonjwa huu nchini tuweze kukabiliana nao na kuudhibiti mara moja.


Share:

Mtalaam Na Bingwa Wa Magonjwa Yote Sugu Nayaliyoshindikana Kama Vile Pumu, Vidonda Vya Tumbo, Busha, Nguvu Za Kiume, Kisukari

Tatizo la upungufu ukosefu wa nguvu za kiume, maumbile madogo  limekuwa kubwa kwa rika zote hapa duniani

Matatizo hayo sio mageni kigeni ni ile tiba sahihi yakutibu na kuponya haya.chanzo cha hayo matatizo ni:KISUKARI, NGIRI,CHANGO, TUMBO KUUNGURUMA NA KUJAA GESI, KIUNO KUUMA, MAUMIVU YA MGONGO,MAGONJWA YA ZINAA, KORODANI KUVIMBANAKUUMA,VIDONDA VYA TUMBO, NK.

Tiba sahihi nabora ya tatizo la nguvu zakiume ni 3Power,Nidawa ya vidonge asilia vilivyotengenezwa kwa kiwango bora na salama kwa ajili yakutibu mojakwamoja tatizo la nguvu za kiume maradufu

1,hutibu nguvu za kiume mda mfupi sana kati ya umri wa miaka 18-85 naitakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 20 hadi 40 tendo lakwanza bila kuchoka naitakufanya uwe nahamu yakuendelea na tendo la ndoa zaidi ya mara 5 bila hamu kuisha.

FINA Power Nidawa yakuboresha maumbile ya kiume kwa kunenepesha na kurefusha kwa saizi uipendayo inchi 6,7 hadi 8 kwa mda mfupi sana.dawa hizi huanza kufanya kazi kwa mda wa dk 67

Pia tunatibu,KISUKARI, PRESHA, UZAZI, NGIRI, PUMU,MALARIA SUGU, VIDONDA VYA TUMBO, CHANGO AINA ZOTE, BP, BUSHA BILA UPASUAJI NK.

ISHOSHA,Nidawa ya mvuto wa biashara,humvuta mme,mke,hawara,mchumba,unaemhitaji

SHEPU EXRA,Nidawa ya yakupunguza matiti,unene tumbo,kitambi kwa akina baba,hutoa mafuta mabaya mwilini,makovu sehemu mbalimbali mwilini,chunusi sugu,minyama uzembe,michirizi mwilini

HUDUMA HIZI NANYINGINE NYINGI MTALAAM BINGWA DR SHEIKH OMARY
Anapatikana dar magomeni moroco
SIMU NO 0767 14 53 57/0629 03 45 50.

NAKAMA NAFASI YAKUFIKA OFISINI HAIPO UTALETEWA HAPO ULIPO.


Share:

Naibu Waziri wa Afya Dr.ndugulile Awataka Wananchi Kuacha Matumizi Mabaya Ya Pombe Ili Kuepukamadhara

Na.Faustine Gimu Galafoni.Dodoma.
Leo ikiwa ni  oktoba 3 ,2019 ni siku  ya kuadhimisha upingaji wa unywaji wa pombe duniani wananchi wameshauriwa kupunguza matumizi mabaya ya pombe ili kuepuka madhara kama ajali,ukatili wa kijinsi na magonjwa mbalimbali.
 
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Dk Faustine Ndugulile alipo hudhuria maadhimisho hayo yaliyo andaliwa na shirika lisilo la kiserikali linalo pinga matumizi mabaya ya pombe TAAnet   ambapo amesema kuwa matumizi ya pombe yanasababisha madhara mengi katika jamii hususani vifo vya watu.
 
Aidha amezitaka mamlaka husika kuwachukulia hatua watu wote ambao wanauza pombe kiholela na kufanya msako wa kukamata wote wanao uza pombe bila leseni.
 
Naye Anna Baraka Chaula Afisa Maendeleo ya jamii Kata  Kising’a Mkoa wa Iringa amesema kuwa katika kata yake watu wengi walikuwa wanatumia muda mwingi kunywa pombe bila kufanya kazi za maendeleo huku akisema baada ya kupata elimu kwa sasa wamepunguza unywaji wa pombe.
 
TAAnet kwa sasa ina dhamira ya kutetea kushawishi sera na wafanya maamuzi kutengeneza kutekeleza sera ya Taifa ya kudhibiti matumizi mabaya ya pombe ambayo yatapunguza madhara ya kiafya na kijamii.  


Share:

Dawa Komesha Ya Maumbile Madogo , Nguvu Za Kiume Na Magonjwa Mengineyo

*NGETWA MIX*/
√Hii ndio dawa bora ya mitishamba kiboko ya maumbile Madogo(KIBAMIA) Hurefusha na kunenepesha maumbile  mafupi pia  yaliyoingia ndani kutokana na kitambi ama kuathirika na punyeto

*📌SUPER MORINGA MIX*/
Ni dawabora ya nguvu za kiume yenye mchanganyiko wa miti shamba 10 yenye maajabu yafuatayo:/
🔖(1)Inatibu upungufu wa nguvu za kiume mara dufu na kuimarisha misuri   ilio legea na kusinyaa wakati wa tendo la ndoa/
🔖(2)Kuongeza hamu ya tendo kukufanya uweze kurudia tendo hadi mara tatu bila kuchoka
🔖(3)Itakufanya uchelewe kufika kileleni dk 15-30 kwa tendo la Kwanza na utakuwa na uwezo wa Kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara 3-4 bila hamu kuisha na inatibu kabisa/
.
*MATATIZO HAYA HUSABABISHWA NA*/
🔖(1)Tumbo kujaa gesi, na kuunguruma chini ya kitovu/
🔖(2) Choo kuwa kama Cha mbuzi/
🔖(3)Ngiri/
🔖(4)Kama umejichua sana punyeto/
🔖(5)Kisukari/
🔖(6)Presha ya kupanda na kushuka/
🔖(7)Vidonda vya tumbo,/
.
Na haya yote husababisha/
📍Kuishiwa kwa nguvu za kiume 📌/
. _______________________
Bado hujachelewa dawa hizi ni mpya kabisa  ni tofaut na ulizo wahi kutumia pia zimeonesha mafanikio kwa watu wengi sana/

Pia tuna tibu  KISUKARI,PRESHA,VIDONDA VYA TUMBO N.K/
._______________________
DR .SELEMANI OMARY ANAPATIKANA  DAR ES SALAAM , PIA UNAWEZA KULETEWA POPOTE ULIPO  NDANI NA NJE YA NCHI .SIMU NO:/
*📞+255788468114*


Share:

MTUMISHI WA AFYA AJINYONGA KWA WAYA JUU YA MTI KAHAMA

Mtumishi wa afya kituo cha afya Ushetu wilayani Kahama,Moses Amasha Mbilinyi (26) amefariki dunia kwa kunyonga kwa kutumia waya wa Extension juu ya mti nje ya nyumba aliyopanga.

Kwa Mujibu wa Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Adax Majaliwa tukio hilo limetokea Septemba 29,2019 majira kati ya saa tisa hadi saa 11 alfajiri katika kijiji cha Mbika kata ya Ushetu halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama.

"Moses Amasha Mbilinyi ambaye ni nurse assistant katika kituo cha afya Ushetu amekufa baada kujinyonga kwenye mti na kuacha ujumbe wa maandishi usemao "chanda ,kama kikitokea chochote nimeacha viwanja viwili kahama anavijua malubalo, viwili nyamilangano,kimoja sijalipia laki tano hivyo ni mali ya Nancy",ameeleza Kamanda Majaliwa

Amesema chanzo cha tukio inasemekana ni msongo wa mawazo.

Na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Share:

Waziri Jafo Awataka Wakurugenzi Wapya Wajiamini na kusimamia vyema mapato na miradi mbalimbali ya maendeleo

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri wa nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa[TAMISEMI] Mhe.Seleman Jafo amewataka Wakurugenzi wapya 10 walioteuliwa hivi Karibuni na Rais Magufuli kujiamini katika nafasi zao na kusimamia mahusiano mema ya Utumishi.
 
Waziri Jafo amesema hayo leo Oktba 3,2019 jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha Wakurugenzi hao Wapya pamoja na Ofisi ya TAMISEMI kilichoenda sambamba na kula kiapo cha utumishi kwa Watumishi hao.
 
Waziri Jafo amesema suala la kujiamini ,kusimamia mahusiano mema pamoja na Maadili ni jambo la msingi kwa kila mtumishi,hivyo amewataka wakurugenzi hao kuacha kutengeneza manung’huniko ya madaraja katika halmashauri zao.
 
Aidha ,Waziri Jafo amewataka wakurugenzi hao kusimamia vyema mapato na miradi mbalimbali ya maendeleo kwani wasipozingatia mambo hayo halmashauri zao zitayumba kutokana na kukosa mapato.
 
Katika hatua nyingine Waziri Jafo amewataka wakurugenzi kujiheshimu katika kazi zao .
 
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mkurungezi ni heshima kubwa ,Itakuwa jambo la ajabu mkurugenzi umeweka miito ya Muziki wa Ovyo,sijui Singeli kwenye simu yako,Sijui mkurungezi ukipanga foleni kwenye chakula sahani ya ubwabwa unaijaza mpaka unamwagika,au unanunua miwa unakula ovyo barabarani.kwa hiyo ukurugenzi ni heshima kubwa.Amesema.
 
Kaimu  katibu Mkuu TAMISEMI,Mathias Kabundugulu  amewataka wakurugenzi hao kushirikiana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kusimamia vyema uchaguzi wa serikali za Mitaa utakaofanyika hivi karibuni.
 
Ikumbukwe kuwa ,Oktoba Mosi 2019 Rais Wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli alifanya uteuzi wa wakurugenzi watendaji 10 wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa na kuwahamisha wawili.


Share:

Waziri wa Kilimo Atangaza Bei Elekezi Kwa Mbolea Ya Kukuzia (Urea) Kwa Msimu Wa Kilimo 2019/2020

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Katika kuhakikisha kuwa tija ya uzalishaji wa mazao ya kilimo inaongezeka ili kujitosheleza kwa chakula na malighafi za viwandani; serikali imeendelea kuhamasisha matumizi ya mbolea ili kufikia kilo 50 za virutubisho kwa hekta moja kama ilivyopendekezwa na wakuu wa nchi za Afrika kupitia Azimio la Abuja la mwaka 2006. 

Ili kufikia lengo hilo Wizara ya Kilimo ilianzisha Mfumo wa Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja (BPS - Bulk Procurement System), kufuta tozo mbalimbali za mbolea, kusimamia utaratibu wa usafirishaji wa mbolea na kuweka bei elekezi za mbolea kwa mkulima.

Uingizaji wa mbolea kupitia BPS unahusu mbolea za Urea, DAP, NPK, CAN na SA. Hata hivyo, kwa sasa BPS inatumika kuingiza mbolea za DAP na Urea ambazo zinazotumika kwa zaidi ya asilimia 50.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 3 Octoba 2019 Jijini Dar es salaam wakati akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari katika Ofisi ndogo za Wizara ya Kilimo.

Alisema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 4(1)(u) cha Sheria ya Mbolea ya Na. 9 ya mwaka 2009 na Kanuni ya 56 ya Kanuni za Mbolea, 2011 na marekebisho yake ya mwaka 2017 (The Fertilizer (Amendment) Regulations, 2017), mbolea aina zote zinatakiwa kuuzwa kwa bei iliyopangwa na Serikali. Hata hivyo, bei elekezi zinazotangazwa ni kwa mbolea zinazoagizwa kupitia BPS ambazo ni mbolea ya kupandia (DAP) na ya kukuzia (Urea).
 
1.Zabuni za Mfumo wa Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja (BPS)
Waziri Hasunga amesema kuwa Mfumo wa Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja (BPS) umeanzishwa kwa lengo la kupata punguzo la bei litokanalo na kununua na kusafirisha mbolea nyingi kwa wakati mmoja (Economies of scale). Tangu kuanza kwa BPS mwaka 2017, huu ni msimu wa tatu wa kilimo wa utekelezaji wake ambapo mbolea zimeingizwa nchini kwa punguzo la bei katika chanzo (FOB – Free on Board) kwa asilimia 6 – 17 ikilinganishwa na bei katika soko la Dunia inayosimamiwa na taasisi inayofuatilia bei ya mbolea katika soko la Dunia iitwayo Argus Gmbh. Aidha, BPS imefanya gharama za usafirishaji wa mbolea baharini kushuka kwa kiasi kikubwa kutoka Tshs 23,000/= hadi Tshs 3,500/= kwa mfuko mmoja wa kilo 50. Kutokana na BPS, matumizi ya mbolea yamekuwa yakiongezeka kila mwaka.
 
2.Mjengeko wa bei elekezi
Ikumbukwe kuwa, zaidi ya asilimia 90 ya mbolea zinazotumika nchini kwa sasa huagizwa kutoka nje ya nchi. Hivyo, katika kutengeneza mjengeko wa bei, gharama mbalimbali huzingatiwa hususan bei ya ununuzi katika chanzo, usafirishaji wa mbolea baharini, bima, tozo za Mamlaka ya Bandari (TPA) na taasisi mbalimbali za udhibiti, gharama za vifungashio, kufungasha, usafirishaji hadi kwa muuzaji wa rejareja na faida ya mfanyabiashara.
 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amesema kuwa bei elekezi za mbolea hutegemea umbali wa sehemu inakopelekwa kutokea bandarini. Maeneo yote itakapopelekwa mbolea yana umbali kati ya kilometa 1 na 1,600 kutoka bandari ya Dar es salaam. Kwa Wastani, gharama ya kusafirisha mfuko mmoja wa mbolea wa Kilo 50 kwa barabara kutoka Bandari ya Dar es salaam hadi makao makuu ya Halmashauri kwa barabara ni Sh. 5,500/= kwa kilometa 1,000. Gharama hii hupanda na kushuka kutegemeana na hali ya barabara na hali ya hewa (masika au kiangazi). Aidha, usafiri kwa njia ya Reli ni nafuu zaidi kwa sababu gharama za kusafirisha mbolea kwa kilometa 1,000 kwa mfuko wa kilo 50 ni Tshs 4,160 (TRC) au Tshs 4,600 (TAZARA).
 
3.Mwenendo na mchanganuo wa bei elekezi za mbolea ya kukuzia (Urea)
 
4.1.Mwenendo wa bei elekezi katika soko la ndani ya nchi
Ushindani wa zabuni za BPS zilizofunguliwa Julai 04, 2019 ulifanya bei za mbolea aina ya Urea kununuliwa kwenye chanzo kwa punguzo la dola saba (7) za kimarekani ikililinganishwa na bei za zabuni ya Julai, 2018.

Sambamba na punguzo lililotokana na zabuni hizo, Wizara ya kilimo ilifanya utafiti kati ya Juni na Julai, 2019 wenye lengo la kufanya marejeo ya kikokotoo cha bei elekezi ambacho kimetumika kwa misimu ya kilimo 2017/2018 na 2018/2019. Utafiti huo ulishirikisha wadau wa mbolea wakiwemo wauzaji (waingizaji, wasambazaji, wauzaji wa jumla na rejareja), wanunuzi (wakulima wadogo kupitia vyama vyao vya ushirika, wakulima wakubwa, viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo na wanunuzi wa mazao).

Ushindani wa zabuni za BPS pamoja pamoja na utafiti wa kupitia upya kikokotoo umefanya bei ya mkulima kupungua kwa wastani kimkoa kutoka Tshs 57,482 hadi wastani wa Tshs 53,997/=. Hili ni punguzo la wastani wa Tshs 3,485/= au asilimia 6 kwa mfuko wenye uzito wa kilo 50.




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger