Thursday, 3 October 2019

MTUMISHI WA AFYA AJINYONGA KWA WAYA JUU YA MTI KAHAMA

Mtumishi wa afya kituo cha afya Ushetu wilayani Kahama,Moses Amasha Mbilinyi (26) amefariki dunia kwa kunyonga kwa kutumia waya wa Extension juu ya mti nje ya nyumba aliyopanga.

Kwa Mujibu wa Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Adax Majaliwa tukio hilo limetokea Septemba 29,2019 majira kati ya saa tisa hadi saa 11 alfajiri katika kijiji cha Mbika kata ya Ushetu halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama.

"Moses Amasha Mbilinyi ambaye ni nurse assistant katika kituo cha afya Ushetu amekufa baada kujinyonga kwenye mti na kuacha ujumbe wa maandishi usemao "chanda ,kama kikitokea chochote nimeacha viwanja viwili kahama anavijua malubalo, viwili nyamilangano,kimoja sijalipia laki tano hivyo ni mali ya Nancy",ameeleza Kamanda Majaliwa

Amesema chanzo cha tukio inasemekana ni msongo wa mawazo.

Na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Share:

Waziri Jafo Awataka Wakurugenzi Wapya Wajiamini na kusimamia vyema mapato na miradi mbalimbali ya maendeleo

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri wa nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa[TAMISEMI] Mhe.Seleman Jafo amewataka Wakurugenzi wapya 10 walioteuliwa hivi Karibuni na Rais Magufuli kujiamini katika nafasi zao na kusimamia mahusiano mema ya Utumishi.
 
Waziri Jafo amesema hayo leo Oktba 3,2019 jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha Wakurugenzi hao Wapya pamoja na Ofisi ya TAMISEMI kilichoenda sambamba na kula kiapo cha utumishi kwa Watumishi hao.
 
Waziri Jafo amesema suala la kujiamini ,kusimamia mahusiano mema pamoja na Maadili ni jambo la msingi kwa kila mtumishi,hivyo amewataka wakurugenzi hao kuacha kutengeneza manung’huniko ya madaraja katika halmashauri zao.
 
Aidha ,Waziri Jafo amewataka wakurugenzi hao kusimamia vyema mapato na miradi mbalimbali ya maendeleo kwani wasipozingatia mambo hayo halmashauri zao zitayumba kutokana na kukosa mapato.
 
Katika hatua nyingine Waziri Jafo amewataka wakurugenzi kujiheshimu katika kazi zao .
 
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mkurungezi ni heshima kubwa ,Itakuwa jambo la ajabu mkurugenzi umeweka miito ya Muziki wa Ovyo,sijui Singeli kwenye simu yako,Sijui mkurungezi ukipanga foleni kwenye chakula sahani ya ubwabwa unaijaza mpaka unamwagika,au unanunua miwa unakula ovyo barabarani.kwa hiyo ukurugenzi ni heshima kubwa.Amesema.
 
Kaimu  katibu Mkuu TAMISEMI,Mathias Kabundugulu  amewataka wakurugenzi hao kushirikiana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kusimamia vyema uchaguzi wa serikali za Mitaa utakaofanyika hivi karibuni.
 
Ikumbukwe kuwa ,Oktoba Mosi 2019 Rais Wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli alifanya uteuzi wa wakurugenzi watendaji 10 wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa na kuwahamisha wawili.


Share:

Waziri wa Kilimo Atangaza Bei Elekezi Kwa Mbolea Ya Kukuzia (Urea) Kwa Msimu Wa Kilimo 2019/2020

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Katika kuhakikisha kuwa tija ya uzalishaji wa mazao ya kilimo inaongezeka ili kujitosheleza kwa chakula na malighafi za viwandani; serikali imeendelea kuhamasisha matumizi ya mbolea ili kufikia kilo 50 za virutubisho kwa hekta moja kama ilivyopendekezwa na wakuu wa nchi za Afrika kupitia Azimio la Abuja la mwaka 2006. 

Ili kufikia lengo hilo Wizara ya Kilimo ilianzisha Mfumo wa Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja (BPS - Bulk Procurement System), kufuta tozo mbalimbali za mbolea, kusimamia utaratibu wa usafirishaji wa mbolea na kuweka bei elekezi za mbolea kwa mkulima.

Uingizaji wa mbolea kupitia BPS unahusu mbolea za Urea, DAP, NPK, CAN na SA. Hata hivyo, kwa sasa BPS inatumika kuingiza mbolea za DAP na Urea ambazo zinazotumika kwa zaidi ya asilimia 50.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 3 Octoba 2019 Jijini Dar es salaam wakati akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari katika Ofisi ndogo za Wizara ya Kilimo.

Alisema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 4(1)(u) cha Sheria ya Mbolea ya Na. 9 ya mwaka 2009 na Kanuni ya 56 ya Kanuni za Mbolea, 2011 na marekebisho yake ya mwaka 2017 (The Fertilizer (Amendment) Regulations, 2017), mbolea aina zote zinatakiwa kuuzwa kwa bei iliyopangwa na Serikali. Hata hivyo, bei elekezi zinazotangazwa ni kwa mbolea zinazoagizwa kupitia BPS ambazo ni mbolea ya kupandia (DAP) na ya kukuzia (Urea).
 
1.Zabuni za Mfumo wa Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja (BPS)
Waziri Hasunga amesema kuwa Mfumo wa Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja (BPS) umeanzishwa kwa lengo la kupata punguzo la bei litokanalo na kununua na kusafirisha mbolea nyingi kwa wakati mmoja (Economies of scale). Tangu kuanza kwa BPS mwaka 2017, huu ni msimu wa tatu wa kilimo wa utekelezaji wake ambapo mbolea zimeingizwa nchini kwa punguzo la bei katika chanzo (FOB – Free on Board) kwa asilimia 6 – 17 ikilinganishwa na bei katika soko la Dunia inayosimamiwa na taasisi inayofuatilia bei ya mbolea katika soko la Dunia iitwayo Argus Gmbh. Aidha, BPS imefanya gharama za usafirishaji wa mbolea baharini kushuka kwa kiasi kikubwa kutoka Tshs 23,000/= hadi Tshs 3,500/= kwa mfuko mmoja wa kilo 50. Kutokana na BPS, matumizi ya mbolea yamekuwa yakiongezeka kila mwaka.
 
2.Mjengeko wa bei elekezi
Ikumbukwe kuwa, zaidi ya asilimia 90 ya mbolea zinazotumika nchini kwa sasa huagizwa kutoka nje ya nchi. Hivyo, katika kutengeneza mjengeko wa bei, gharama mbalimbali huzingatiwa hususan bei ya ununuzi katika chanzo, usafirishaji wa mbolea baharini, bima, tozo za Mamlaka ya Bandari (TPA) na taasisi mbalimbali za udhibiti, gharama za vifungashio, kufungasha, usafirishaji hadi kwa muuzaji wa rejareja na faida ya mfanyabiashara.
 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amesema kuwa bei elekezi za mbolea hutegemea umbali wa sehemu inakopelekwa kutokea bandarini. Maeneo yote itakapopelekwa mbolea yana umbali kati ya kilometa 1 na 1,600 kutoka bandari ya Dar es salaam. Kwa Wastani, gharama ya kusafirisha mfuko mmoja wa mbolea wa Kilo 50 kwa barabara kutoka Bandari ya Dar es salaam hadi makao makuu ya Halmashauri kwa barabara ni Sh. 5,500/= kwa kilometa 1,000. Gharama hii hupanda na kushuka kutegemeana na hali ya barabara na hali ya hewa (masika au kiangazi). Aidha, usafiri kwa njia ya Reli ni nafuu zaidi kwa sababu gharama za kusafirisha mbolea kwa kilometa 1,000 kwa mfuko wa kilo 50 ni Tshs 4,160 (TRC) au Tshs 4,600 (TAZARA).
 
3.Mwenendo na mchanganuo wa bei elekezi za mbolea ya kukuzia (Urea)
 
4.1.Mwenendo wa bei elekezi katika soko la ndani ya nchi
Ushindani wa zabuni za BPS zilizofunguliwa Julai 04, 2019 ulifanya bei za mbolea aina ya Urea kununuliwa kwenye chanzo kwa punguzo la dola saba (7) za kimarekani ikililinganishwa na bei za zabuni ya Julai, 2018.

Sambamba na punguzo lililotokana na zabuni hizo, Wizara ya kilimo ilifanya utafiti kati ya Juni na Julai, 2019 wenye lengo la kufanya marejeo ya kikokotoo cha bei elekezi ambacho kimetumika kwa misimu ya kilimo 2017/2018 na 2018/2019. Utafiti huo ulishirikisha wadau wa mbolea wakiwemo wauzaji (waingizaji, wasambazaji, wauzaji wa jumla na rejareja), wanunuzi (wakulima wadogo kupitia vyama vyao vya ushirika, wakulima wakubwa, viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo na wanunuzi wa mazao).

Ushindani wa zabuni za BPS pamoja pamoja na utafiti wa kupitia upya kikokotoo umefanya bei ya mkulima kupungua kwa wastani kimkoa kutoka Tshs 57,482 hadi wastani wa Tshs 53,997/=. Hili ni punguzo la wastani wa Tshs 3,485/= au asilimia 6 kwa mfuko wenye uzito wa kilo 50.




Share:

MGANGA WA KIENYEJI ADAIWA KUBAKA MTOTO WA MIAKA 8 MAMA AKINUNUA WEMBE


Mganga wa kienyeji mkazi wa Ujiji, Venas Edward (48), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya Mkoa wa Kigoma kwa madai ya kumbaka mtoto msichana mwenye umri wa miaka minane.

Akisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Katoki Mwakitalu, mshtakiwa huyo alikana kutenda kosa hilo na yuko nje kwa dhamana.

Upande wa Mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali Raymond Kimbe, ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba mahakama kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali.

Akisoma maelezo ya awali Wakili wa Serikali Kimbe, alidai kuwa Aprili 23, mwaka huu majira ya asubuhi eneo la Kasoko-Ujiji, mshtakiwa huyo alimbaka mtoto huyo mwenye umri wa miaka minane na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.

Kimbe alidai siku ya tukio mtoto huyo alichukuliwa na mama yake mzazi (jina linahifadhiwa) na kwenda naye kwa mshtakiwa ambaye ni mganga wa kienyeji kwa ajili ya kupata matibabu.

Alidai baada ya kufika kwa mganga huyo mama wa mtoto aliambiwa aende kununua kiwembe dukani na kumuacha mtoto na mganga huyo, ambaye anadaiwa alitumia nafasi hiyo kumbaka mtoto huyo.

Kufuatia tukio hilo ilidaiwa mshtakiwa huyo alikamatwa na askari polisi na baada ya mahojiano alipelekwa mahakamani.

Wakili huyo alidai upande wa mashtaka unatarajia kupeleka mashahidi watano pamoja na kielelezo kimoja cha PF 3 na kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuanza kusikiliza mashahidi.

Hakimu Mwakitalu alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 9 kwa kusikilizwa.
Share:

Bodi Ya Wakurugenzi Ya Mamlaka Ya Maji Morogoro Yavunjwa

Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA)imevunjwa. Hatua hiyo imechukuliwa na Waziri wa Maji Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb) kuanzia tarehe 02 Oktoba, 2019.

Taarifa ya Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo imeainisha kuwa kuvunjwa kwa bodi hiyo ni kwa mamlaka aliyo nayo Waziri wa Maji kwa mujibu wa kifungu Namba 14 cha Jedwali la kwanza la Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira Namba 5 ya Mwaka 2019, kikisomwa pamoja na Kanuni Na. 14 ya Kanuni za Usambazaji wa Maji  (Tangazo la Serikali Na. 90 la tarehe 26/04/2019).

Taarifa hiyo imefafanua kuwa bodi ya MORUWASA imevunjwa kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kuisimamia mamlaka ya maji hivyo kuathiri utoaji wa huduma za majisafi na usafi wa mazingira  katika manispaa ya Morogoro.

Aidha, wakati huo huo Waziri wa Maji Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb) ametaka kuanza kwa  utaratibu utakaowezesha kuundwa kwa bodi mpya.




Share:

Ongeza Nguvu Za Kiume, Maumbire Madogo Pamoja Na Tiba Mbalimbali

MASISA 3 POWER nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa muundo wa vidonge na unga  , Huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-80)   Inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii)  inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa  tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoazaidi ya maratatu (3)bila hamu kuisha wara kuhisi kuchoka na  itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 20-40

SUPER MONGERA  Hurefusha na kunenepesha maumbile madogo yaliosinyaa. Matatizi haya huchagizwa ama husababishwa na tumbo kuunguluma na kujaa gesi,ngili, kisukari, presha korodani moja kuvimba au kuingia ndani nk yote haya yanatibika kabisa na kupona kwa mad mfupi sana,

Pia ninadawa ya vidonda vya tumbo miguu kuwaka moto na kupata nganzi, maumivu ya mgongo na kiuno 

Ni DR CHIPUPA  pekee mwenye uwezo wa kumrudisha mume , mke ,mchumb.

Kwa nini uhangaike na matatizo ya uzazi;   ninadawa ya uzazi kwa pandezote mbili, kupunguza unene kitambi ( nyama uzembe)        kuondoa makovu mwilini, kuzuia mimba kuharibika,kusafisha nyota,  kuzuia majini wachafu, pete ya bahati,

 wasiliana na DR. CHIPUPA 

Call+255 0620510598

watsap +255 0758840958

Huduma hii inakufikia popote ulipo


Share:

Maeneo manne yanayoashiria matumaini ya ugunduzi wa rasilimali ya Mafuta nchini Tanzania

Serikali ya Tanzania ametaja maeneo manne yanayoashiria matumaini ya ugunduzi wa rasilimali ya Mafuta nchini kwa siku za usoni kupitia shughuli za utafiti zinazoendelea.

Maeneo aliyoyataja ni pamoja na ya ukanda wa Ziwa Rukwa, Ziwa Tanganyika na Kitalu cha Eyasi Wembere chenye ukubwa wa kilometa za mraba 19. 2.

Kitalu hicho kinapita katika mikoa ya Arusha, Manyara, Simiyu, Shinyanga na Tabora.

Dk Kalemali ametoa kauli hiyo jana Jumatano Oktoba 2, 2019 Jijini Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Mafuta na Gesi.

“Kuanzia eneo la Ziwa Tanganyika, Ziwa Rukwa, maeneo ya Pwani ya Tanga pamoja na Kitalu cha Eyasi Wembere, tunashukuru timu ya wataalamu ya Uganda inayosaidiana na Shirika letu la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika kusaidia ushauri,” amesema Waziri Kalemani.

Akifungua Mkutano huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Angellah Kairuki akimwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono wawekezaji wanaokuja katika sekya ya Mafuta na Gesi.


Share:

Tambua Visababishi Vikuu Vinavyosababisha Kupungukiwa Nguvu Za Kiume Na Maumbile madogo

1 ugonjwa wa kisukari, 2 presha,usongo wa mawazo,3 magonjwa ya moyo 4 ngiri tumbo, kuunguruma na kuumwa chini ya kitovu 5 kupiga punyeto kwa mda mrefu 6 kukosa choo au kupata choo kama cha mbuzi 7.maumivu ya mgongo na kiuno 8. joto kali kwenye mfuko wa korodani

Ni nini tiba ya nguvu za kiume; MAJINJAS ni dawa yenye virutubisho ambavyo hutibu matizo  yafatayo 1.kushindwa kurudia tendo 2. kuwahi kufika kileleni 3 .maumbile kulegea

MKULUMO; ni dawa ya kuboresha  saizi upendayo inch 5-8 na unene sm 3-5 za upenyo

MTINJETINJE; ni  dawa ya kisukari hurudisha kongosho katika hali yake ya kawida haijalishi unatumia vidonge au sindano za insulin,

Kumbuka dawa hizi ni tofauti na ulizowai kutumia ni salama na adhina suma ya kukuasili

Fika ofisini kwangu MBAGALA ZAKHEMU KARIBU NA KCB BENKI na mwanza yupo wakala nipigie simu whasApp 0783185060. 0620113431 DR AGU pia utaletewa popote ulipo uduma hizi


Share:

Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani amemsimamisha kazi Msimamizi wa Mitambo wa Kituo cha kupooza Umeme cha Ubungo

Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani amemsimamisha kazi Msimamizi wa Mitambo wa Kituo cha kupooza Umeme cha Ubungo Samson Mwangalume, kwa uzembe uliosababisha kukatika umeme jana usiku Oktoba 2, 2019, karibu Jiji zima la Dar es Salaam  huku chanzo kikielezwa kuwa ni uchafu wa vikombe katika njia za kusafirisha nishati hiyo.

Dk Kalemani pia ametoa onyo la mwisho kwa kaimu meneja mwandamizi wa usafirishaji wa umeme, Amos Kahiyula kuhakikisha haukatiki kutokana na uzembe.

Ametoa maagizo mara baada ya kutembelea kituo hicho na kutoridhishwa na maelezo ya Kahiyula aliyetoa sababu hizo baada ya kutakiwa na waziri huyo kueleza chanzo.

"Nataka huyo Samson aliyekuwa mkuu wa zamu asimamishwe kazi kuanzia leo na maelezo yake niyapate leo ofisini kwangu  kwani kama ni vikombe vipo kwa nini hamkuviweka,” amesema Dk Kalemani.


Share:

Afisa mtendaji Kortini Kwa Kujeruhi

Afisa mtendaji wa Kata Syridion Michael (40) mkazi wa kinondoni amepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi kinondoni kwa kosa la kujeruhi.

Akisomewa hati ya mashtaka mbele ya hakimu Happiness Kikoga na Wakili wa Serikali Ester chale alidai Agosti 1, 2019 eneo la kinondoni mkwajuni wilayani kinondoni Dar es salaam alimng’ata upande wa kulia wa mdomo mtu mmoja Tanya Tasaluko na kumsababishia maumivu.

Mshtakiwa alikana kutenda shtaka hili na wakili wa serikali alidai upelelezi wa shauri hili hauja kamilika aliomba tarehe nyingine kwa kutajwa na kwa kukamilisha upepelezi.

Hakimu Kikoga alisema dhamana kwa mshtakiwa ipo wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu, barua za utambulisho, nakala ya vitambulisho vya taifa na kusaini bondi ya sh 500,000.

Hata hivyo mshtakiwa alirudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana na kesi yake itakuja kwa kutajwa tena octoba 15 mwaka huu.


Share:

Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Kijaji Aitaka TRA Kuongeza Wigo Wa Walipa Kodi

Na Ramadhani Kissimba, WFM, Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Kuandaa Mkakati mahsusi utakaosaidia kuongeza wigo wa walipa kodi nchini kutoka idadi ya walipa kodi elfu mbili waliopo sasa.

Dkt. Kijaji aliyasema hayo alipofanya ziara ya kawaida ili kukagua utendaji kazi wa Mamlaka hiyo katika Ofisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania ya Mkoa wa kikodi wa Kinondoni.

Mhe.Naibu Waziri alisema ili kuwaondolea mzigo walipa kodi waliopo sasa, jitihada za makusudi zinahitajika ili kuongeza idadi ya walipa kodi.

Dkt. Kijaji ameitaka TRA kuandaa mpango mkakati utakaoonyesha kuwa baada ya miaka miwili Mamlaka hiyo itakuwa imeongeza idadi ya walipa kodi zaidi ya milioni mbili,kwa kufanya hivyo Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania watakuwa wamejibu hoja iliyotolewa na Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwaondolea mzigo walipa kodi waliopo sasa.

Aidha Mhe. Kijaji ameitaka TRA kumuandalia na kuwasilisha kwake takwimu ya ongezeko la walipa kodi lililotokana na zoezi la kugawa vitambulisho vya wajasiriamali nchini.

“Lengo la kugawa vitambulisho hivyo lilikuwa ni kuongeza wigo wa walipa kodi, hivyo ni vyema kujua tumeongeza walipa kodi wangapi waliotokana na zoezi hilo” alisisitiza Dkt. Kijaji

Kwa upande wa kodi ya majengo, Dkt. Kijaji ameitaka Mamalaka ya Mapato Tanzania kuhakikisha inapata orodha ya nyumba zote nchini kwa kuorodhesha wamiliki wa nyumba hizo na mawasiliano yao na kisha kuandaa kanzi data itakayosaidia kurahisisha ukusanyaji wa kodi hiyo.

Dkt. Kijaji amesema ili kudhibiti upotevu mapato yanayotokana na kodi ya majengo ni lazima TRA wafanye kazi usiku na mchana kuhakikisha kanzidata ‘database’ hiyo inakamilika ambayo itatumika kuwakumbusha walipa kodi kupitia ujumbe mfupi wa simu ambapo itasaidia katika ukusanyaji wa kodi hiyo.

Awali akimkaribisha Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Meneja wa Mkoa wa kodi wa Kinondoni Bw. Massawe Masatu alisema kuwa pamoja na changamoto wanazopitia, Ofisi ya Mkoa wa kodi wa Kinondoni kwa mwaka 2018/19 ilikusanya zaidi ya shilingi bilioni 713ikilinganishwa na makadirio ya kukusanya shilingi bilioni 794, sawa na asilimia 86 ya lengo.

Mhe. Naibu Waziri aliwapongeza watumishi wa Mamlaka hiyo na kuwataka kuwatumia vizuri watumishi hao katika kuongeza mapato ili kuwezesha Serikali kuwahudumia vyema wananchi.

Dkt. Kijaji ameuagiza Uongozi wa Mamlaka hiyo kuwapa ushirikiano watumishi wanaofanya kazi zao kwa weledi, na kutosita kuwachukulia hatua wale wote watakaonekana wana nia ya kuirudisha nyuma Mamlaka hiyo.

Mwisho


Share:

Malipo Ya Wakulima Wa Pamba Simiyu Kufanyika Kielektroniki

Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Malipo ya Wakulima wa zao la Pamba Mkoani Simiyu, katika msimu ujao yanatarajiwa kufanyika kwa mfumo wa kielektroniki kupitia huduma ya T-PESA ya Shirika la Mawasiliano Tanzania(TTCL).

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika Mkutano wa Wadau wa Pamba uliowahusisha viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, wataalam wa kilimo, viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS), kwa lengo la kujadili  juu ya malipo ya wakulima wa zao hilo kupitia huduma ya T-PESA uliofanyika Oktoba 02, 2019  mjini Bariadi.

Mtaka amesema kuwa sambamba na mfumo wa ulipaji wa fedha za wakulima wa pamba kwa njia ya Kielekroniki taarifa zote za kilimo zitapatikana kwa njia hiyo huku akiongeza kuwa mfumo huo utasaidia kuondokana na hasara katika vyama vya msingi vya ushirika(AMCOS) iliyokuwa inasababishwa na baadhi ya viongozi wasio waaminifu.

“Tumewaleta hapa TTCL tunataka tufanye digital farming(kilimo kidigitali) malipo ya pamba, mambo yote ya pamba na kilimo kwa ujumla yawe kwenye kiganja chako kwa sababu leo hakuna nyumba ambayo haina simu; ni vizuri elimu hii viongozi wa AMCOS muifikishe kwa wakulima ili wawe  na uelewa wa pamoja,” alisema Mtaka.

Akizungumza katika Mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano  Tanzania  (TTCL) Waziri Kinamba amesema mfumo  huo mpya utaanza kutumika katika msimu ujao na utawasaidia wakulima kupata fedha zao kwa usalama, urahisi, kwa wakati na kupunguza matumizi yasiyofaa.

“Lengo letu ni kutoa suluhu ya matatizo mbalimbali yanayojitokeza katika vyama vya msingi vya ushirika kama upotevu wa fedha, uporaji na tunaamini wakulima wakipata pesa zao kidigitali itaondoa changamoto hizo na kuwafanya wakulima kuwa na maisha bora kutokana na uchumi utakaoboreka baada ya mauzo watakayofanya kupitia TTCL PESA,” alisema Kindamba.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Ushirika Mkoa (SIMCU), Emmanuel Mwelele amesema  kuwa mfumo huu ni mzuri na unalenga kwasaidia wakulima kupata fedha zao kwa usalama na akaahidi kuwa viongozi wa chama hicho watatoa elimu kwa vyama vya msingi vya ushirika(AMCOS) ili wakulima wote wawe na uelewa wa pamoja.

Hadi sasa mkoa wa Simiyu una wakulima wa pamba wapatao 314,000 na matarajio ya uzalishaji katika msimu wa mwaka huu yalikuwa ni  kilo milioni 180, ambapo hadi sasa jumla ya kilo milioni 148 zimekusanywa kutoka kwa wakulima kupitia vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS).

MWISHO


Share:

Korea Kaskazini Yazindua Kombora Hatari la Majini

Korea kaskazini imethibitisha kufanya jaribio la kurusha aina mpya ya kombora, baada ya kufanikiwa kurusha makombora ya masafa mafupi tangu mwezi Mei.


Jaribio hili nchini humo ni la kumi na moja kwa mwaka huu ambapo makombora yenye uwezo wa kubeba silaha za nyuklia yanarushwa.

Lakini utofauti wa jaribio hili ni kuwa, kombora halijarushwa kutoka ardhini, bali kwenye nyambizi chini ya bahari.

Kombora hili kuwa na uwezo wa kurushwa kutoka majini ni muhimu zaidi kwa nchi hiyo kwa kuwa sasa wanauwezo wa kufanya mashambulizi mbali ya eneo lao.

Kwa mujibu wa maofisa wa Korea Kusini, kombora hili lina uwezo wa kuruka kwa kasi ya km 450 na kufika urefu wa km.910 kabla alijashuka baharini.

Hii ina maanisha kuwa makombora haya yana uwezo wa kuruka umbali mrefu mara mbili wa kiwango cha kimataifa ingawa makombora ya awali ya Korea Kaskazini yalikuwa na uwezo wa kuruka mbali zaidi.

Kombora hilo liliangukia baharini upande wa Japani, unaoitwa upande wa mashariki wa bahari.

Japani imedai kuwa kombora hilo limetua katika umbali wa kilimita 200 kutoka ardhi yake. .

Jaribio hilo linakuja muda mfupi baada ya Korea Kusini kusema kuwa mazungumzo ya nyuklia kati yao na Marekani yataendelea.

Makombora hayo yalizinduliwa baharini siku ya Jumatano majira ya saa saba usiku saa za Afrika mashiriki, kilomita 17 kaskazini mashariki mwa fukwe za mji wa Wonsan .

Ripoti kutoka televisheni ya taifa hilo KCNA imesema kuwa leo Alhamisi, majaribio matatu kutoka juu yatarushwa ," makombora haya yamebuniwa kutoa vitisho kwa mataifa mengine na kujilinda".

KNCA imeongeza kuwa hakuna madhara yatayotokea kwa nchi za jirani. 
 
Kama makombora hayo yalizinduliwa kwa kiwango cha kawaida, basi yale yaliyorushwa kwa kunyooka wima yana uwezo wa kusafiri kwa karibu kilomita 1900.

Hivyo masafa hayo yanaweza kuzifikia Japani na Korea Kusini.

Korea Kaskazini ina nyambizi iitwayo 'Romeo' kilijengwa mwaka 1990, na wanaamini kuwa na kasi ya kilomita 7,000 ,Reuters imeripoti.

Nyambizi hiyo ina uwezo wa kufanya safari ya moja kwa moja mpaka kufikia Hawaii, Marekani.

Chombo hicho cha majini kinachotumia nguvu ya mafuta ya dizeli, hata hivyo kinapiga kelele ambazo zinaweza kurahisisha kugundulika kirahisi.

Kuzinduliwa kwa kombora hilo la majini na Korea Kaskazini ni hatua mbaya zaidi kwa usalama wa majirani zake wa ukanda wa kaskazini mashariki mwa Asia.

Kombora hili limezinduliwa kwa mipango ya baadae ya majini lakini uzinduzi huu hauoneshi hilo.

Wataalamu waliounda kombora hilo Korea Kaskazini wanasema kuwa ni hatari sana kufanya operesheni hiyo ya jaribio la kurusha kombora majini.

Ingawa kurushwa kwake kunaonekana kuwa ni mafanikio makubwa.

Kama kombora hilo lingerushwa kama kawaida, yangeweza kufika katika visiwa vikubwa vinne vya Japan na ukanda wote wa Korea Kusini.

Hii inatajwa kuwa mfumo hatari zaidi wa teknolojia ya kombora kutambulishwa katika taifa hilo.


Credit:BBC


Share:

Waziri Mkuu: Tusiruhusu Mfumo Mpya Ununuzi Wa Korosho

WAZIRI MKUU  Kassim Majaliwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa yote inayolima korosho nchini wahakikishe wanasimamia vizuri zao hilo na wasiruhusu kuingizwa kwa mfumo mpya wa ununuzi ambao haujaeleweka kwa wadau na wanunuzi.

“Mabadiliko  ya mifumo yalitolewa na baadhi ya viongozi ambao sio waaminifu, Serikali iko macho itawachukulia hatua viongozi wa vyama vya ushirika wasiokuwa waaminifu. Tunataka mfumo wenye manufaa ndio utumike.”

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Oktoba 2, 2019) wakati akizungumza na wananchi wa mkoa wa Mtwara baada ya kukagua ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini inayojengwa katika eneo la Mitengo, wilayani Mtwara.

Waziri Mkuu amesema msimu wa korosho kwa mwaka huu unatarajiwa kutangazwa hivi karibuni, hivyo ni lazima kwa wakuu wa mikoa inayolima korosho wakajiandaa vizuri ili kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima.

Waziri Mkuu ameendelea kuwasisitiza wafanyabiashara kutojihusisha na ununuzi wa korosho kwa njia ya kangomba.”Kangomba imepigwa marufuku, watakaojihusisha moto utawawakia huko huko . Tunataka wakulima wenyewe ndio wanufaike”

Pia, Waziri Mkuu ametoa wito kwa wakulima wa zao la korosho kuendelea kujiimarisha na wahakikishe wanajiwekea akiba kwa ajili ya ununuzi wa pembejeo kwa sababu. “Serikali  itaendelea kusimamia zao hili ili wakulima wapate tija.”

Mapema, Waziri Mkuu ametembelea ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini na kukagua kazi ujenzi inayoendelea hospitalini hapo, ambapo amesema itakapomalizika itawapunguzia wananchi safari ya kwenda Muhimbili kufuata huduma.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imejikita katika kuboresha huduma mbalimbali za wananchi zikiwemo za afya, hivyo wananchi wa Kanda ya Kusini watapata matibabu ya kibingwa karibu na maeneo yao.

“Hakuna mashaka wala wasiwasi wa kupata huduma bora za afya kuanzia sasa na kuendelea kwa sababu Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeendelea kuwezesha utaratibu mzuri wa kupata huduma za afya nchini.”

Ujenzi wa hospitali hiyo ya Rufaa ya Kanda ya Kusini unatarajiwa kukamilika Agosti 2020 na kwa sasa inajengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa gharama ya zaidi ya sh. bilioni 15 na tayari Serikali imeshatoa zaidi y ash. bilioni sita.

Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema Serikali imetenga zaidi ya sh. Bilioni 15 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya

Alisema historia ya mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini inayojengwa Mkoani Mtwara ilianzia kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi cha Mkoa cha tarehe 16 Januari 1979. Halmashauri Kuu ilijadili na kuazimia kuishawishi Serikali kujenga hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini itakayohudumia Mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma.

Waziri Ummy aliongeza kuwa hospitali hiyo inajengwa kwa awamu, ambapo awamu ya kwanza  ilianza mwaka wa fedha 2005/2006 kwa kazi ya upimaji wa mipaka na mwinuko wa ardhi kupitia kampuni ya Beacon Consult Ltd kwa gharama ya sh. 26,000,000 na ilikamilika ndani ya siku 30 za mkataba. Kwa sasa ujenzi huo upo katika awamu ya nne.

Awali,Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha kubangua korosho cha Yalin kilichopo katika eneo la Msijute mkoani Mtwara na kukagua kazi ya ubanguaji pamoja na kuzungumza na watumishi wa kiwanda hicho ambao waliishukuru Serikali kwa kuhamasisha ujenzi wa viwanda.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Mafia Yatakiwa Kujipanga Uwekezaji Sekta Ya Utalii

Na Munir Shemweta, WANMM MAFIA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameitaka halmashauri ya wilaya ya Mafia mkoa wa Pwani kuandaa mazingira kupokea uwekezaji wa utalii kwa kupanga na kupima maeneo yake kwa lengo la kuhamasisha wawekezaji wa sekta ya utalii.

Dkt Mabula alisema hayo jana kwa nyakati tofauti aliposikiliza kero za migogoro ya ardhi kwa wananchi wa kata za Baleni na Kilindoni wilayani Mafia mkoa wa Pawani wakati wa ziara yake ya siku mbili kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi, kukagua masijala ya ardhi pamoja na mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi kwa njia ya kielektroniki.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema, eneo la Mafia limekaa kimkakati na yasipofanyika maandalizi mapema kama vile kupima maeneo ya uwekezaji basi migogoro ya ardhi haitaisha na hivyo kuwafanya wawekezaji kushindwa kuwekeza katika wilaya hiyo.

Ameitaka halmashauri ya wilaya ya Mafia kukusaidia kuweka mipango ya matumizi bora ya ardhi katika maeneo ya vijiji na kubainisha kuwa mpango huo unaweza pia kugharimiwa na vijiji husika kwa kuwa gharama yake haizidi shilingi milioni saba kwa kila kijiji na mpango huo utawezesha kuandaliwa maeneo ya kilimo, ufugaji na uwekezaji.

‘’Huu ni mwaka wa uwekezaji Wizara ya Ardhi ni wizara wezeshi tutafanya kila jitihada kupima viwanja katika eneeo la mafia na Kila anayetaka kuwekeza anataka Mafia lakini Mafia yenyewe haijawa tayari alisema Dkt Mabula

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, wizara yake iko tayari kuleta timu maalum ya wapimaji kutoka Wizarani kwa ajili ya zoezi la kupima maeneo mbalimbali katika wilaya hiyo pale ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mafia atakuwa tayari kugharimia fedha ya kujikimu kwa watumishi watakaofanya kazi hiyo.

Hata hivyo, Naibu Waziri wa Ardhi alibainisha kuwa, halmashauri ya Wilaya ya Mafia inaweza pia kuandika Andiko litakalowezesha halmashauri hiyo kupata mkopo kwa ajili ya zoezi la upimaji katika maeneo mbalimbali wilayani humo.

Awali baadhi ya wananchi wa Mafia wamelalamikia halmashauri ya Mafia kwa kushindwa kupima maeneo mengi ya wilaya hiyo jambo walilolieleza limechangia kuwepo migogoro ya ardhi katika wilaya hiyo. Hata hivyo changamoto kubwa inayoikabili wilaya ya Mafia ni kuwa na Mtumishi mmoja wa sekta ya Ardhi.

Maulid Mjenga alimueleza Dkt Mabula kuwa tatizo la upimaji katika wilaya hiyo mbali na mambo mengine lakini limesababisha mipaka ya Shule ya Msingi Kilindoni kutofahamika jambo lililochangia mfadhili aliyejitokeza kujenga ukuta wa shule kushindwa kufanya hivyo kutokana na kutojulikana kwa mipaka ya shule.

Migogoro mikubwa ya ardhi aliyokumbana nayo Dkt Mabula katika ziara yake wilayani Mafia ni pamoja na mgogoro wa wananchi wenye maeneo na kampuni ya Bronkhorst International Contractors Limited unaohusu fidia eneo la Ras Kisimani Mafia, mgogoro wa fidia kati ya kampuni ya Kinasi Lodge na familia ya Mwanahafsa na Bi Lawiya eneo la Utende pamoja pamoja na ule wa fidia katika shamba la Utumaini.


Share:

CHADEMA Walimwa Barua na Msajili wa Vyama Kwa Kutofanya Uchaguzi Wa Viongozi Wa Juu Wa Chama......Wapeswa Siku 7 za Kujieleza

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania ameandika barua kwenda kwa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema akikitaka kutoa maelezo kwa nini kisichukuliwe hatua kwa kutokufanya uchaguzi wa viongozi wake.

Barua ya Msajili iliyoandikwa Oktoba 1, 2019 na kusainiwa na Sisty Nyahonza kwa niaba ya msajili wa vyama vya siasa inasema uongozi wa Chadema chini ya Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe umemaliza muda wake tangu Septemba 14, 2019.

Katika barua hiyo, msajili amekitaka chama hicho kutoa maelezo hayo kabla ya Oktoba 7, 2019 saa 9:30 mchana.


Share:

Naibu Waziri Ikupa: Wenye Ulemavu Wajumuishwe Katika Masuala Ya Ukimwi

NA.MWANDISHI WETU
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masula ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa ameuasa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza kushirikisha kundi la wenye ulemavu katika masuala ya UKIMWI ili kuhakikisha jamii nzima inapata elimu na huduma ya masuala hayo.

Ametoa kauli hiyo oktoba 2, 2019 wakati alipokuwa akizungumza na watendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo mkoani Tanga alipofanya ziara yake ya siku tatu mkoani hapo ili kutembelea na kukagua shughuli zinazotekelezwa wilayani hapo kuhusu masuala ya UKIMWI.

Alieleza kuwa kundi la wenye ulemavu limekuwa nyuma kwa muda mrefu katika kujumuishwa hususan katika masuala ya elimu na huduma za kijamii hivyo ni lazima kuzingatia mahitaji yao katika kuendelea kuwapa elimu na huduma za masuala hayo ili waweze kunufaika na huduma ili kupunguza na kuondoa maambukizi mapya katika mkoa mzima wa Tanga.

“Ni vyema kuhusisha kundi la wenye ulemavu katika upatikanaji wa huduma za masuala ya Ukimwi kwa kuzingatia kundi hili limekuwa likisahaurika na kutofikiwa kama yalivyo makundi mengine,”alieleza Mhe.Ikupa

Aliongezea kuwa miongoni mwa mikakati ya Halmashauri ni vyema kuwa na mipango madhubuti ya kuhakikisha huduma za masuala ya Ukimwi ikiwemo, utoaji elimu juu ya mabadiliko ya tabia na kinga dhidi ya maambukizi ya VVU, kuwashirikisha katika program mbalimbali zinazojikita katika kuimarisha mifumo utoaji wa elimu ya masuala ya watu wanaoishi na VVU na mikakati ya kusaidia makundi hayo.

Alifafanua kuwa, kwa kufanya hivyo itasaidia kupungua kwa masuala ya ubaguzi katika jamii ili kuwa na usawa na haki kwani wenye ulemavu wanastahili kupewa huduma sawa katika jamii.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe. Mwanashaa Rajab alieleza kuwa wameendelea kuwafikia watu wenye ulemavu katika huduma za upimaji, utoaji wa huduma za dawa na kuahidi kuendelea kuwajumusha katika shughuli zote zinazohusu masuala ya ukimwi ili kufikia malengo ya Taifa ya kuwa na tisini tatu (909090).

“Tunakushukuru kwa kuendelea kuunga mkono jitihada zetu na kukuahidi tutatekeleza maagizo yako ikiwa ni pamoja na kutenga bajeti zinazojumuisha mahitaji maalum ya wenye ulemavu, kuwapatia elimu, kuwafikia na kuendelea kuwashirikisha katika program mbalimbali za kimaendeleo,”alisema Mwanashaa.

Naye Mratibu wa Kudhibiti masula ya Ukimwi katika Halmashauri hiyo Herieth Nyangasa alieleza kuwa hali ya maambukizi kipindi cha mwaka 2018 ni asilimia 2.1 kutoka asilimia 2.6 kwa mwaka 2017 ambapo imechangiwa na jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuwafikiwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi ili kuhakikisha maambukizi mapya yanapungua.

“Zipo jitihada nyingi zimefanyika kuhakikisha wanapunguza hali ya maambukizi mapya na kuwapatia huduma watu wanaoishi na VVU ikiwa ni pamoja na wilaya kuwa na vituo 445 vya kutolea huduma ya ushauri nasihi na upimaji wa VVU, vituo 20 vya upimaji kwa hiari, vituo 38 upimaji kwa ushawishi na vituo 45 vya huduma ya kupunguza maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto,”Alesema Nyangasa

Kwa upande wake Mratibu wa kudhibiti Ukimwi Wilayani humo Dkt. Yahaya Mbura alieleza changamoto zinazokwamisha jitihada za serikali katika kuwahudumia watu wanaoishi na virusi vya ukimwi kuwa ni pamoja na tatizo la  utoro wa watumiaji wa dawa za kufubaza Virusi vya ukimwi ambapo alieleza imechangia kwa kikasi kikubwa kudhoofisha jitihada hizo.

“Hadi sasa tuna ripoti za utoro kwa wanaotumia dawa wapatao 388 na hii imechangiwa na changamto za miundombinu kipindi cha mvua, umbali wa vituo kutoka katika makazi yao pamoja na uwepo wa imani potofu kuhusu matumizi ya dawa hizo,”alisisitiza Dkt. Yahaya.

Aliongezea kuwa pamoja na changamoto hiyo, tayari zaidi ya watoro 212 walifanikiwa kuwarejesha katika huduma za upatiwaji wa dawa na kuendelea kutumia dawa.

AWALI

Halmashauri ya Wilaya ya Muheza ni moja kati ya Halmashauri 11 zilizopo Mkoa wa Tanga yeye jumla ya hekta za mraba 1,974 na jumla ya wakazi 204,461 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 ambapo kati yao wanawake ni 103,618 na wanaume ni 100,843.Aidha ina jumla ya Kaya 47,920 yenye Tarafa 4, kata 37, vijiji 126 na Vitongoji 494 ambapo wilaya hiyo inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kwa ajili ya kutekeleza afua za VVU na UKIMWI hasa zisizo za kitabibu.Wadau hao ni pamoja na SWAAT, SHDEPHA, WORLD VISION,KONGA,SHIVYAWATA,ZICOSAD,TIWAMWE, AMREF, AWCYS, MKUTA pamoja na BAKWATA.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger