Wednesday, 2 October 2019

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Laua Majambazi Watatu

Jeshi  la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limewaua watuhumiwa wa ujambazi watatu akiwamo aliyeuawa nje ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa, alisema jana kuwa katika tukio la kwanza, Jeshi la Polisi limemuua mtuhumiwa Emmanuel Peter ambaye alikuwa anasakwa kwa muda mrefu.

Alisema mauaji hayo yalitokea juzi eneo la Ilala Boma majira ya mchana, ambapo polisi ilipata taarifa kutoka kwa msiri kuwa mtuhumiwa huyo yupo na wenzake wanne.

Kamanda Mambosasa alisema kikosi kazi kilifika eneo hilo la tukio na kumkuta mtuhumiwa huyo na ghafla alishtukia amezungukwa na askari, ndipo alipotoa silaha kwa nia ya kuwafyatua risasi polisi.

“Polisi waliokuwa eneo la tukio walimuwahi na kumjeruhi mtuhumiwa huyo na kumnyang’anya bastola ikiwa na risasi mbili, risasi moja ikiwa chemba imepakiwa tayari kwa kufyatuliwa,” alisema.

Alisema mtuhumiwa huyo alipelekwa hospitali, lakini alifariki dunia na mwili wake umehifadhiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Katika tukio la pili, Mambosasa alisema Alhamisi iliyopita mchana eneo la Mbezi Msakuzi njia panda ya Mpiji Magoe.

“Tulipata taarifa kuna watuhumiwa wa ujambazi ambao wamejipanga kwenda kuvamia Vyama vya Akiba na Mikopo (Saccos) ya Msakuzi. Tuliweka mtego na ilipofika saa sita mchana zilifika pikipiki mbili aina ya Boxer ambazo hazikusomeka namba zake zikiwa na watu wanne, mmoja akiwa na bastola,” alisema.

Alisema watu hao walipogundua wanafuatiliwa, walikimbia ndipo askari walipofyatua risasi kwa nia ya kuwasimamisha, lakini nao walijibu mapigo.

Alisema katika majibizano ya risasi, polisi iliwajeruhi watuhumiwa wawili ambao walifariki dunia baadaye na wengine walikimbia.

Alisema majeruhi hao walikutwa na bastola moja na risasi tatu ndani ya magazine na maganda mawili ya risasi.


Share:

Profesa Tibaijuka kurejesha shilingi 1.6 bilioni za mgao wa Rugemarila

Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka amesema uongozi wa Shule ya Sekondari Barbro Johansson Model Girls utarejesha fedha za msaada walizopokea  kutoka kwa mfanyabiashara, James Rugemarila ili aweze kutoka gerezani.

Profesa Tibaijuka amesema hayo kupitia Kituo cha televisheni cha Azam TV.

Amesema uongozi wa shule hiyo umekaa kikao na kuamua kurejesha  fedha hizo walizopokea ili kumsaidia  mtuhumiwa huyo anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kutoka gerezani.

Alipoulizwa kama fedha walizopewa msaada zilikuwa hazijatumika hadi sasa,  Profesa Tibaijuka amesema licha ya fedha hizo kutumika kulipa deni la kujenga bweni la shule lakini zitatafutwa na zitarejeshwa.

==>>Msikilize hapo chini


Share:

Wauguzi Waomba Wapunguziwe Ada Za Leseni Za Uuguzi

Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Wauguzi kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara wameomba Baraza la Uuguzi na Ukunga nchini(TNMC) kupunguza  gharama za ada ya leseni za uuguzi ambazo wamedai kuwa ni kubwa na zinaathiri vipato vyao.

Ombi hilo limetolewa na Katibu wa Chama cha wauguzi Tanzania Bara(TANNA) Bw. Sebastian Luziga wakati akisoma risala mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka alipofungua Kongamano la kisayansi na Mkutano wa 47 wa wauguzi kwa niaba ya Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, Oktoba 01, 2019 Mjini Bariadi.

Luziga amesema awali ada hiyo kwa ngazi ya astashahada ilikuwa 20,000/=  stashahada na shahada na shahada ya uzamili  ilikuwa shilingi 40,000/=, hivi sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la ada ambapo astashahada wanapaswa kulipa shilingi 40,000/=, stashada 60,000/=shahada 80,000 na shahada ya uzamili na uzamivu ni 120,000/=.

“Ongezeko hili ni kubwa na linaathiri sana kipato cha wauguzi  kwani hakuna uwiano kati ya kupanda huko kwa ada na ongezeko la mshahara; kupitia Wizara ya Afya tunaomba lishughulikiwe upya kwa kufuata utaratibu wa kushirikisha wadau,” alisema Luziga

Akizungumza mara baada ya kupokea risala hiyo Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameahidi kulifikisha suala hilo pamoja na mengine yaliyowasilishwa kwa Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, huku akiwaomba viongozi kulitafakari kwa upya ongezeko la ada wakizingatia hali halisi ya mishahara ya wauguzi, kodi na makato na waone busara kama ipo haja na hoja ya kuongeza ada hiyo.

“Suala hili ni hoja ya walio wengi, ninyi nyote mmemuona Mhe. Rais akizungumzia kuondolewa kwa tozo nyingi zisizo na sababu kwenye kilimo, mifugo, uvuvi; hata hili la kwenu linaweza kusababisha serikali iwe na nia ya kufahamu mabaraza yake yote na tozo zao, nawaomba viongozi mlitafakari muone kama ipo hoja na haja ya kuongeza gharama za ada,” alisema Mtaka.

Naye Mganga Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Dkt. Festo Dugange amesema mkoa unatambua kazi inayofanywa na wauguzi  ya kutoa elimu kwa wajawazito na kuhamasisha wajifungulie  kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, ambapo mwaka 2017 wanawake waliojifungulia kwenye vituo vya afya ni asilimia 55 na mwaka 2018 ikapanda kufikia  asilimia 70.

Naye Afisa Muuguzi kutoka Halmashauri ya Ubungo Bi. Aliho Ngeregenza amesema  wauguzi walio wengi vipato vyao wanavyopata haviendani na gharama za leseni wanazolipia hivyo ombi lao wapunguziwe gharama hizo

Kongamano la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa 47 wa wauguzi Tanzania Bara ambalo linahusisha wauguzi zaidi ya 800 litafanyika kwa muda wa siku nne Mjini Bariadi mkoani Simiyu.

MWISHO


Share:

Waziri Simbachawene Ahimiza Matumizi Ya Nishati Mbadala Kupikia Ili Kuhifadhi Mazingira

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene amehimiza matumizi ya nishati mbadala kupikia ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira unaotokana na ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa.

Mhe. Simbachawene ametoa rai hiyo wakati akihutubia wanafunzi na wananchi katika mahafali ya kumaliza kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Pwaga wilayani Mpwapwa.
 
Aliwataka wananchi kuacha mara moja kukata miti kwa ajili ya kuni au mkaa na kusema kuwa vitendo hivyo huchangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya tabianchi.
 
Mhe. Simbachawene ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Kibakwe alisema kuwa wakati umefika sasa kwa wananchi kuanza kutumia gesi katika shughuli za kupika hivyo kuepuka matumizi ya mkaa au kuni ambayo huchangiwa kwa kiasi kikubwa na ukaaji wa miti.
 
"Tukiyachezea mazingira tunachezea uhai wetu na ukataji hovyo wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa unaishia kusababisha kumalizika kwa maeneo yenye miti mikubwa na wengine wanakata miti kwa kiwango kikubwa hata tukae miaka mingi hatutakuja kupata tena miti kama hiyo," alisisitiza.
 
Aidha, Waziri Simbachawene ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe wilayani humo aliwapongeza wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao na kuwatia moyo.
 
Pia alikemea tabia ya baadhi ya wanafunzi wa kike kuanza kushiriki katika vitendo vya ngono kabla ya umri na kuwataka kuzingatia masomo na hivyo kufikia malengo yao na kuwaonya wazazi wanaoficha wahusika wa mimba hizo.
 
Alionya tabia ya baadhi ya wanaume wanaowarubuni wanafunzi wa kike na kushiriki nao ngono vitendo vinavyosababisha kuwapa mimba na hivyo kukatisha masomo yao.
 
Kwa upande wake Afisa Elimu wa Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Nelson Milanzi alitoa mwito kwa wanafunzi na wananchi kwa ujumla kutunza mazingira.
 
Afisa Elimu huyo aliwataka kuunga mkono juhudi za Ofisi ya Makamu wa Rais na Serikali kwa ujumla kutunza mazingira na kupanda miti kwa wingi.


Share:

Serikali Kushirikiana Na Taasisi Mbalimbali Kuboresha Afya Ya Wanyama

Serikali imesema itaendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali katika kuhakikisha inaboresha afya za mifugo na upatikanaji wa madawa kwa wakati ili wafugaji waweze kunufaika na mifugo yao.

Akizungumza mara baada ya kukutana na Mkurugenzi wa Taasisi ya ZOETIS A.L.P.H.A katika Bara la Afrika Dkt. Gabriel Varga ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amesema ili kufuga kisasa ni muhimu kwa wafugaji kushirikishwa na wataalamu katika kutambua magonjwa ya mifugo yao na kupatiwa elimu ya namna ya kuwahudumia mifugo.

Ameongeza kuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi imejipanga vyema katika katika kutekeleza majukumu yake kwa vitendo ili kuhakikisha matokeo chanya yanapatikana katika sekta ya mifugo nchini.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah akiwa katika mazungumzo na Dkt. Varga amesema taasisi hiyo ambayo katika bara la Afrika inafanya kazi na taasisi ya Bill and Melinda Gates (BMGF), malengo yao yanafanana na mikakati ya wizara katika kuhudumia ukuzaji viumbe kwenye maji hivyo wizara inatarajia katika kipindi cha miaka miwili au mitatu itafanya kazi na taasisi hiyo ya ZOETIS A.L.P.H.A. katika sekta ya uvuvi.

Dkt. Tamatamah amefafanua kuwa ufugaji samaki kwa sasa hapa nchini unawekewa kipaumbele katika kuendeleza na kuongeza uzalishaji wa samaki kwa kuwa mahitaji ya ulaji wa samaki yameongezeka kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya ongezeko la idadi ya watu.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya ZOETIS A.L.P.H.A katika Bara la Afrika Dkt. Gabriel Varga amewaambia makatibu wakuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Elisante Ole Gabriel anayeshughulikia Mifugo na Dkt. Rashid Tamatamah anayeshughulikia Uvuvi, kuwa taasisi yake inatarajia kuanzisha maabara hivi karibuni katika mikoa ya Iringa, Dar es Salaam, Mwanza na Morogoro ili kuboresha afya ya wanyama.

Aidha. Dkt. Varga amefafanua kuwa taasisi hiyo ambayo kwa sasa inahudumia nchi zaidi ya 100 kote ulimwenguni imekuwa ikiwasaidia wafugaji wa bara la Afrika kwa kuwapatia elimu ya huduma ya wanyama ili waweze kufuga kwa tija.

Mazungumzo hayo yamehudhuiriwa pia na Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Dkt. Hezron Nonga, Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji Dkt. Nazael Madala na Msajili wa Baraza la Veterinari Tanzania Dkt. Bedan Masuruli wote kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Mwisho.
Imetolewa: Kitengo cha Mawasiliano serikalini
   Wizara ya Mifugo na Uvuvi


Share:

TECNO Ikishirikiana Na Tigo Yazindua Rasmi TECNO Spark 4.

Sasa TECNO imewapa tena wateja wake nafasi ya kurahia ladha mpya ya simu janja na hii kutokana na ujio wa simu mpya ya TECNO Spark 4 yenye sifa malukuki na kwa bei nzuri.

Akizungumza na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi wa TECNO Spark 4 uliofanyika katika duka jipya la TECNO ‘TECNO Smart Hub Kariakoo’ manager wa masoko wa kampuni ya TECNO, Bwana William Motta alisema, “teknolojia ya AI iliyopo ndani ya TECNO SPARK 4 imebeba uwezo mkubwa wenye kuzipa support kamera tatu za nyuma za TECNO Spark 4 kwa picha nzuri na videos zenye ubora. 
 
William Motta amevieleza vyombo vya habari kuwa TECNO Spark 4 imekuja na sifa zifuatazo Kasi ya mtandao wa 4G, Kamera tatu za nyuma, GB 32 za memory na kioo cha nchi 6.52 super full-view. 
 
Wakati huo, Mkuu wa idara ya kitengo cha bidhaa wa kampuni ya TIGO Mkumbo Mnyonga alisema, “pindi unaponunua simu ya TECNO Spark 4 basi hapo hapo utazawadiwa na ofay a GB 18 kutoka tigo.uzinduzi wa simu hii mpya unaenda sambamba na ofa ya GB 18 kutoka tigo”. 
 
Mkumbo Mnyonga “lengo letu ni kuhakikisha jamii ya kitanzania inahamia katika mfumo mpya wa kijital. Na hiyo ndio sababu ya kampuni ya TIGO kushirikiana na TECNO ili kulifikia dhumuni lakuongeza wimbi la watumiaji smartphone nchini”.
 
TECNO Spark 4 inapatikana katika maduka yote ya TECNO na TIGO nchini na hizi ni baadhi ya sifa za TECNO Spark 4: Megapixel 13+8+2 nyuma, GB 32 ROM+ GB 2 RAM, 4000battery, kioo cha nchi 6.52 na warranty ya miezi 13. 
 
Kwa maelezo zaidi tembelea https://www.tecno-mobile.com



Share:

Viwanda Vya Ndani Vyapongezwa Kwa Kuwa Na Uwezo Wa Kuongeza Thamani Korosho Ya Tanzania

Viwanda vya ndani nchini vimepongezwa kwa kuwa na uwezo wa kuongeza thamani korosho ya Tanzania tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alipotangaza uamuzi wa Serikali kununua korosho zote za wakulima tarehe 12 Novemba, 2018.

Hayo yamesemwa na Prof. Joseph Buchweishaija, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara alipofanya ziara ya kufuatilia ubanguaji wa korosho kwenye viwanda vilivyopo Mikoa ya Mtwara na Lindi na usafirishaji wa korosho hizo nje ya nchi unaoendelea katika bandari ya Mtwara.
 
“Nimejionea mwenyewe korosho zetu zilivyo na ubora unaostahiki, zinabanguliwa kwa utaalam na zimefungashwa kwa kutumia vifungashio vizuri (vacuumed packed) katika madaraja yote hususan daraja la WS320 linalopendwa na wanunuaji wengi kutoka nje ya nchi. Hakika viwanda vyetu vinafanya kazi nzuri “amesema Prof. Buchweishaija.
 
Prof. Buchweishaija ameendelea kusema kuwa ubanguaji wa korosho uligawanyika kwa viwanda vya aina mbili yaani viwanda vidogo vinavyosimamiwa na SIDO pamoja na viwanda vikubwa. Katika kutekeleza mpango wa ubanguaji, Serikali kupitia Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) iliingia mikataba na viwanda vikubwa pamoja na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) kwa niaba ya viwanda/wabanguaji wadogo ili kubangua korosho. 

Kwa viwanda vidogo kwa Mkoa wa Mtwara vilikuwa vitano ambavyo ni Siwa Food Products, Mama Vitu Super Cashewnut, Mikindani Food Processing, Akross Ltd – SIDO, Mtwara na Kitama Farmers- Tandahimba na kwa Mkoa wa Lindi vilikuwa viwanda vitatu ambavyo ni Waigero Ltd, Wabanguaji Wadogo BUCO, na Uwakoru, Ruangwa. 

Hadi sasa viwanda vitano vilivyochini ya usimamizi wa SIDO Mtwara ambavyo vimekamilisha ubanguaji wa korosho na viwanda viwili ambavyo ni Waigero na Uwakoru chini ya usimamizi wa SIDO Lindi vinaendelea na uzalishaji  na ubanguaji. 

Hadi kufikia tarehe 23 Septemba, 2019 Korosho tani 607.75 zimebanguliwa na viwanda vyetu vidogo na kuwezesha wabanguaji wadogo takribani 1,000 kupata ajira.

Kwa upande wa viwanda vikubwa Serikali iliingia mikataba na viwanda sita (6) ambavyo ni Amama Framers kilichopo Tandahimba, Perfect Cashew kilichopo Masasi, Hawte Investment kilichopo Mtwara, Al-Andalus kilichopo Lindi, Micronix kilichopo Masasi na Korosho Afrika kilichopo Tunduru. 

Hadi kufikia tarehe 23 Septemba, 2019 Korosho tani 3,309.64 zimebanguliwa na viwanda vikubwa na viwezezesha kutoa ajira takribani 2,511 ambao kwa asilimia kubwa ni akina mama. 

Hadi kufikia tarehe 23 Septemba, 2019 viwanda vinne ambavyo ni Amama Farmers, Perfect Cashew,  Hawte Investment Ltd na Al-Andalus Ltd vinaendelea na ubanguaji wakati Kiwanda cha Micronix na Korosho Afrika vimemaliza ubanguaji wa korosho ghafi kama makubaliano ya mkataba yao ambapo kwa sasa viwanda hivyo viwili vinaendelea kubangua korosho zao walizouziwa na Serikali kiasi cha tani 1,000.
 
Kwa upande wa usafirishaji wa korosho kutoka kwenye Ghala mbalimbali kwenda melini, zoezi linaendelea vizuri. Hadi tarehe 23 Septemba, 2019 Korosho takribani tani 40,050 zimeshapakiwa kwenye meli tayari kwenda nje ya nchi kupitia bandari ya Mtwara.
 
“Hivi sasa ninavyozungumza tayari meli mbili zimepakia korosho na kuondoka, meli ya tatu imeanza kupakiwa ambapo itabeba kontena 1015 ambazo sawa na tani 23,328 na zoezi zima litakamilika kwa siku mbili ukizingatia kuwa kuna meli zingine mbili zipo majini na zitatia nanga na kuanza zoezi la kupakia korosho kwenda nje ya nchi” ameeleza Prof. Buchweishaija.
 
Alihitimisha kwa kusema kuwa zoezi la ubanguaji wa korosho zilizonunuliwa na serikali zimeweza kutoa ajira hasa kwa wanawake kwa asilimia 92 hivyo tumefanikiwa vizuri na kuonesha dalili kuwa Tanzania inaweza hasa tunapozungumzia nchi ya viwanda maana tukiuza korosho ghafi tunahamisha ajira na akatoa wito kwa viwanda kuendelea kuongeza uzalishaji ili ikiwezekana korosho zote zinazozalishwa Tanzania zibanguliwe nchini.


Share:

Bashe Awataka Maafisa Ugani Kutumia Fomu Maalum Kukusanya Taarifa Za Wakulima

Na Bashiri Salum,Wizara ya kilimo-Shinyanga
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe. Husseni Bashe jana 01.10.2019 amemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Zeinabu Telaki fomu maalumu (call sheet ) ambayo itatumiwa na Maafisa Ugani wakati wa kuwatembelea wakulima na kujaza taarifa zao muhimu zikiwemo namba za simu, aina ya mazao anayolima,mbolea wanayotumia pamoja na changamoto zinazowakabili .

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mhe,Naibu Waziri amesema kwamba Kituo cha Utafiti cha Ukiriguru kitapita kila Halmashauri katika Ukanda wote inapolimwa pamba na kutoa mafunzo kuanzia ngazi ya Maafisa watendaji wa Vijiji ili kusaidia na kushauri shughuli za kilimo ngazi ya chini.

Amesema zoezi hili litaisida kupunguza tatizo la ukosefu wa Maafisa Ugani ambao wangeweza kushauri wakulima.

Aidha amesisitiza kwamba kila Afisa Kilimo wa Kata au Kijiji atatakiwa kutembelea wakulima wasiopungua watano (5) na kuchukua taarifa muhimu zikiwemo majina ya wakulima ukubwa wa shamba, aina ya kilimo kinachofanyika, mbolea iliyotumika mwaka jana na mawasiliano ya
mkulima.

Hata hivyo amemsahuri mkuu wa Mkoa huo kukutana na wenyeviti wa Halmashauri ili kujadili uanzishwaji wa mashamba ya mfano yatakayomilikiwa na Halmashauri hizo ili wakulima waweze kuyatembelea na kujifunza kilimo cha kitaalamu.

Pamoja na mambo mengine Mhe. Bashe amesema umefika wakati ambao zao la pamaba linatakiwa lijitegemee kama yalivyo mazao mengine na serikali imejipanga kuleta viuatilifu kwa wakati na kwa bei nafuu ili wakulima waweze kununua .

Hata hivyo Mhe. Bashe amewatoa hofu wakullima kuhusu upandaji wa bei za mbegu amesema mwaka huu bei haitafika shilingi 1,000 bali itakuwa katika ya sh. 600 na 650 iwe kama namna ya kupunguza machungu ambayo wakulima wa pamba wameyapata kwa mwaka huu.

Amewataka wataalamu wa kilimo kusaidia kuongeza uzalishaji wa pamba kutoka miche 7,000 hadi 20,000 kwa ekari kwa kuwa kutasaidia kuondoa tatizo la bei ya pamba kwa sababu pamba itakuwa nyingi kwa ekari.

Aidha Mhe. Bashe amezishauri Halmashuri nchini kote kujenga maghala kwa ajili ya kuhifadhia mazao ya wakulima baada ya mavuno ili kuondokana na changamoto za mara kwa mara wakati wa mvua.

Naye Mkuu wa Mkoa huo Bi Zainabu Telaki amesema, sasa wameanza jitihada za kuhamia katika kilimo cha umwagiliaji kutokana na uhaba wa mvua katika mkoa huo na kuiomba wizara ya kilimo kusaidia upatikanaji wa miundombinu ya umwagiliaji.

Katika zoezi la ununuzi wa pamba Bi Telaki anasema pamba nyingi ya mkoani kwake imenunuliwa isipokuwa kawma walikuwepo wakulima walioficha majumbania na ile ambayo ilibainika kupenyezwa kinyemela kutoka Mikoa ya jirani wakitafuta soko.

kama kuna pamba iliyobaki "itakuwa ni kidogo sana katika baadhi ya AMCOS na kwa wale ambao walificha ili ipande bei"alisema Bi Telaki amesema wakulima wengi mkoani humo ikiwemo wilaya ya Kishapu washaanzana kuandaa msimu wa kilimo hivyo amemumba Naibu Waziri kusaidia pembejeo zifike kwa wakati ili wakulima hao wawahi mvua za kwanza.

Awali Mhe. Bashe aliagazi Iadara ya Mazao iliyoko chini ya Wizara ya Kilimo (DCD)kufanya tathmini kwenye sikimu zote katika mkoa huo ili Kujua idadi ya skimu zinazohitaji marekebisho na zinahitaji kujengwa upya.


Share:

Tuesday, 1 October 2019

SYSTEMS DEVELOPER JOBS at Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) 4 POST

SYSTEMS DEVELOPER III – 4 POSTS – 4 POST Employer: Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Date Published: 2019-10-01 Application Deadline: 2019-10-14 JOB SUMMARY: System developer shall be responsible for developing and supporting .NET/C# Java projects, functions and completing specific work, projects and miscellaneous tasks while ensuring commitment and quality through to completion. This Highly responsible position involves using… Read More »

The post SYSTEMS DEVELOPER JOBS at Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) 4 POST appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam Yakamata Magari 50 huku 19 Yakiwa ya Serikali Kwa Kosa la kupita katika barabara ya mabasi ya mwendokasi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa, amesema Jeshi la polisi kwa kipindi cha kuanzia Septemba 19, 2019 hadi sasa linashikilia jumla ya magari 50 huku 19 yakiwa ya Serikali na 31 binafsi kwa kosa la kupita katika barabara ya mabasi ya mwendokasi.

Akizungumza leo Oktoba 1, 2019 Kamanda Mambosasa amesema kuwa japo kuna watu wamezoea kutoa faini pindi wanapokiuka sheria, lakini kwa upande wa barabara ya mwendokasi hakutakuwa na utaratibu wa kutoza faini badala yake watu watapelekwa rumande.

''Unakuta mtu anandaa fedha kwanza afu anaingia mwendokasi kwakuwa faini ni elfu 30, katika mwendokasi sitakubali kutoza faini, hatuko kwa ajili ya kutafuta fedha tunachotaka nikuleta nidhamu ya matumizi sahihi ya barabara hiyo, atakamatwa mhusikia atapelekwa polisi, atawekwa rumande maandalizi yatafanyika kupelekwa kwa Mwanasheria wa Serikali na kufunguliwa mashtaka'' amesema SACP Mambosasa.

Kamanda Mambosasa ameongeza kuwa magari pekee yanayoruhusiwa kutumia njia hizo ni yale yanayowahisha wagonjwa hospitali na kwamba ikitokea gari la wagonjwa limetumia njia hiyo likiwa halina mgonjwa lazima litakamatwa.


Share:

LIVE: Hafla Ya Uapisho Wa Mkurugenzi Wa Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi(NEC) ,Balozi Na Mkuu Wa Itifaki (CP)

LIVE: Hafla Ya Uapisho Wa Mkurugenzi Wa Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi(NEC) ,Balozi Na Mkuu Wa Itifaki (CP)


Share:

Mtalaam Na Bingwa Wa Magonjwa Yote Sugu Nayaliyoshindikana Kama Vile Pumu, Vidonda Vya Tumbo, Busha, Nguvu Za Kiume, Kisukari

Tatizo la upungufu ukosefu wa nguvu za kiume, maumbile madogo  limekuwa kubwa kwa rika zote hapa duniani

Matatizo hayo sio mageni kigeni ni ile tiba sahihi yakutibu na kuponya haya.chanzo cha hayo matatizo ni:KISUKARI, NGIRI,CHANGO, TUMBO KUUNGURUMA NA KUJAA GESI, KIUNO KUUMA, MAUMIVU YA MGONGO,MAGONJWA YA ZINAA, KORODANI KUVIMBANAKUUMA,VIDONDA VYA TUMBO, NK.

Tiba sahihi nabora ya tatizo la nguvu zakiume ni 3Power,Nidawa ya vidonge asilia vilivyotengenezwa kwa kiwango bora na salama kwa ajili yakutibu mojakwamoja tatizo la nguvu za kiume maradufu

1,hutibu nguvu za kiume mda mfupi sana kati ya umri wa miaka 18-85 naitakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 20 hadi 40 tendo lakwanza bila kuchoka naitakufanya uwe nahamu yakuendelea na tendo la ndoa zaidi ya mara 5 bila hamu kuisha.

FINA Power Nidawa yakuboresha maumbile ya kiume kwa kunenepesha na kurefusha kwa saizi uipendayo inchi 6,7 hadi 8 kwa mda mfupi sana.dawa hizi huanza kufanya kazi kwa mda wa dk 67

Pia tunatibu,KISUKARI, PRESHA, UZAZI, NGIRI, PUMU,MALARIA SUGU, VIDONDA VYA TUMBO, CHANGO AINA ZOTE, BP, BUSHA BILA UPASUAJI NK.

ISHOSHA,Nidawa ya mvuto wa biashara,humvuta mme,mke,hawara,mchumba,unaemhitaji

SHEPU EXRA,Nidawa ya yakupunguza matiti,unene tumbo,kitambi kwa akina baba,hutoa mafuta mabaya mwilini,makovu sehemu mbalimbali mwilini,chunusi sugu,minyama uzembe,michirizi mwilini

HUDUMA HIZI NANYINGINE NYINGI MTALAAM BINGWA DR SHEIKH OMARY
Anapatikana dar magomeni moroco
SIMU NO 0767 14 53 57/0629 03 45 50.

NAKAMA NAFASI YAKUFIKA OFISINI HAIPO UTALETEWA HAPO ULIPO.


Share:

HESLB CORRECTIONS OF NECESSARY INFORMATION IN LOAN APPLICATIONS

HESLB HOW TO CORRECT NECESSARY INFORMATION IN LOAN APPLICATION 2019/2020 During the exercise of processing 2019/2020 loan application forms, the Board has come across loan applications which are missing some vital information such as applicant’s and guarantor’s signatures. For that reason, the Board would like to inform loan applicants with such incompleteness to do the following: 1. Visit HESLB website www.heslb.go.tz and… Read More »

The post HESLB CORRECTIONS OF NECESSARY INFORMATION IN LOAN APPLICATIONS appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Waziri Mkuu Ashuhudia Usafirishaji Wa Korosho

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea bandari ya Mtwara na ameshuhudia shehena ya korosho ziliyonunuliwa na kampuni ya Tang Long zikipakiwa katika meli kubwa yenye jina la AS Christiana kwa ajili kusafirishwa kwenda nchini Vietnam.

“Ni faraja kuona mzigo wa korosho ukiondoka na kutoa nafasi ya kuingiza mzigo mwingine mpya wa korosho utakaopatikana baada ya kuanza msimu mpya mwezi huu. Na mnunuzi huyu ameahidi kununua tani 100,000 katika msimu wa mwaka huu.”

Waziri Mkuu ametembelea Bandari ya Mtwara leo (Jumanne, Oktoba 1, 2019) kwa ajili ya kujionea kazi ya usafirishaji wa korosho inavyofanyika  na amesema kwamba ameridhishwa na kasi na utaratibu unaoendelea badarini hapo.

Amesema kampuni ya Tang Long ya nchini Vietnam licha ya kuahidi kununua korosho katika msimu wa mwaka huu, pia imeomba kupatiwa eneo kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha kubangua korosho nchini na kwamba wapo tayari kuanza hata Desemba, 2019.

Waziri Mkuu amesema suala la ujenzi wa viwanda vya kubangulia korosho nchini litaongeza thamani na kuwezesha dunia nzima kutambua kuwa korosho hizo zimetoka Tanzania kwa sababu kwenye vifungashio watakuwa wameandika, hivyo kuongeza soko.

Akizungumzia kuhusu msimu wa uuzaji wa korosho wa mwaka huu, Waziri Mkuu amesema kipaumbele cha kwanza watapewa wenye viwanda vya ndani na kisha tani zinazobaki zitauzwa kwa wanunuzi kutoka nje.

“Wito wa Rais Dkt. John Magufuli wa ujenzi wa viwanda  unalenga katika kuongeza  ajira kwa wananchi kwa kuwa viwanda vinaajiri watu wengi wenye kada tofauti. Wakuu wa mikoa endeleeni kurahisisha mazingira ya uwekezaji.”

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania, Geoffrey Mwambe amesema licha ya kampuni ya Tang Long kununua korosho nchini pia  imeomba ikodishwe kiwanda kimojawapo cha Serikali ili waweze kuanza ubanguaji wa korosho ikiwa ni mpango wa muda mfupi na katika mpango wao wa muda mrefu wameomba eneo kati ya mkoa wa Lindi au Mtwara ili wajenge kiwanda cha kubangua korosho. Taratibu zinaendelea.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Dawa Komesha Ya Maumbile Madogo , Nguvu Za Kiume Na Magonjwa Mengineyo

*NGETWA MIX*/
√Hii ndio dawa bora ya mitishamba kiboko ya maumbile Madogo(KIBAMIA) Hurefusha na kunenepesha maumbile  mafupi pia  yaliyoingia ndani kutokana na kitambi ama kuathirika na punyeto

*📌SUPER MORINGA MIX*/
Ni dawabora ya nguvu za kiume yenye mchanganyiko wa miti shamba 10 yenye maajabu yafuatayo:/
🔖(1)Inatibu upungufu wa nguvu za kiume mara dufu na kuimarisha misuri   ilio legea na kusinyaa wakati wa tendo la ndoa/
🔖(2)Kuongeza hamu ya tendo kukufanya uweze kurudia tendo hadi mara tatu bila kuchoka
🔖(3)Itakufanya uchelewe kufika kileleni dk 15-30 kwa tendo la Kwanza na utakuwa na uwezo wa Kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara 3-4 bila hamu kuisha na inatibu kabisa/
.
*MATATIZO HAYA HUSABABISHWA NA*/
🔖(1)Tumbo kujaa gesi, na kuunguruma chini ya kitovu/
🔖(2) Choo kuwa kama Cha mbuzi/
🔖(3)Ngiri/
🔖(4)Kama umejichua sana punyeto/
🔖(5)Kisukari/
🔖(6)Presha ya kupanda na kushuka/
🔖(7)Vidonda vya tumbo,/
.
Na haya yote husababisha/
📍Kuishiwa kwa nguvu za kiume 📌/
. _______________________
Bado hujachelewa dawa hizi ni mpya kabisa  ni tofaut na ulizo wahi kutumia pia zimeonesha mafanikio kwa watu wengi sana/

Pia tuna tibu  KISUKARI,PRESHA,VIDONDA VYA TUMBO N.K/
._______________________
DR .SELEMANI OMARY ANAPATIKANA  DAR ES SALAAM , PIA UNAWEZA KULETEWA POPOTE ULIPO  NDANI NA NJE YA NCHI .SIMU NO:/
*📞+255788468114*


Share:

Serikali Itaendelea Kuwalinda Wazee Dhidi Ya Ukatili

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuwalinda wazee dhidi ya vitendo vya ukatili, kuwawekea miundombinu na mazingira bora katika kutumia vyombo vya usafiri na kuweka utaratibu na vigezo vitakavyowawezesha kulipwa pensheni.

Waziri Mkuu ameyataka mashirika ya wazee yaelekeze rasilimali wanazozipata katika kutoa huduma za msingi kwa wazee na waepuke kutumia fedha nyingi kwenye mikutano, warsha na makongamano ambayo hayawafaidishi moja kwa moja wazee wenye uhitaji.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Oktoba 1, 2019) wakati akihutubia wananchi katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja Nangwanda Sijaona Manispaa ya Mtwara.

Amesema utoaji wa huduma kwa wazee ni moja ya vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli na kwamba itaendelea  kuchukua hatua za makusudi kwa lengo la kuboresha hali na maisha ya wazee nchini.

Amesema miongoni mwa hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kuimarisha ustawi na maendeleo ya wazee ni pamoja na kuanzishwa kwa mpango wa TASAF wa kunusuru kaya masikini uliolenga kuyasaidia makundi mbalimbali ya jamii yanayoishi katika umasikini uliokithiri likiwemo kundi la wazee.

“Hadi kufikia Septemba 2019 jumla ya wazee 680,056 kutoka kaya 1,118,747 wananufaika na mpango wa TASAF kwa Tanzania Bara na Zanzibar. Mpango huu, umesaidia wazee kujikimu na kumudu majukumu ya kulea wajukuu ambao wazazi wao wamepoteza maisha kwa sababu mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa ukimwi.”

Amesema Serikali pia inaendelea kutekeleza Sera ya Taifa ya Afya ya mwaka 2007 ambayo inatambua kuwa wazee ni kundi maalumu linalohitaji kupewa kipaumbele katika kupata huduma bora za afya, inaweka mkazo kuwa wazee wote wenye umri wa miaka 60 na kuendelea na wasiokuwa na uwezo watibiwe bila malipo.

Hata hivyo, Waziri Mkuu ameendelea kuziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha zoezi la kuwatambua na kuwapatia vitambulisho wazee wasiokuwa na uwezo linakuwa endelevu ili waweze kunufaika na huduma ya matibabu bila malipo  wanapougua.

Kadhalika, Waziri Mkuu amevitaka vituo vyote vya kutoa huduma za afya vya umma kutoa huduma bora na za haraka kwa wazee wenye vitambulisho hivyo na watenge dirisha maalumu kwa ajili ya kuwahudumia wazee ili wasikae kwenye foleni muda mrefu.

Akizungumzia kuhusu matunzo ya wazee, Waziri Mkuu amesema Sera ya Taifa ya Wazee ya Mwaka 2003 inatamka kuwa familia na jamii zina wajibu wa msingi wa kuwatunza na kuwahudumia wazee.

“Hii ni kutokana na ukweli kuwa mazingira ya familia yanamuwezesha mzee kujiona sehemu ya jamii na hivyo, kumfanya aondokane na msongo wa mawazo unaotokana na upweke na kutengwa. Familia kwa mtazamo wa hapa nchini kwetu inajumuisha baba, mama, watoto pamoja na ndugu wengine.”

 Waziri Mkuu ametoa  wito kwa familia, jamii na Mamlaka za Serikali za Mitaa kutimiza wajibu wao wa kutoa matunzo na malezi kwa wazee wasiojiweza, hatua ambayo  itaonesha kuwa jamii inathamini mchango mkubwa walioutoa wazee kwa ustawi na maendeleo ya Taifa. “Vilevile, nisisitize kuwa jukumu la kuwatunza wazee ni la kila mmoja wetu, hivyo kila mmoja anawajibika kuwatunza wazee.”

“Nyote mtakubaliana nami kuwa matunzo ya wazee katika makazi hutolewa kwa wazee wasiojiweza na wasio na ndugu wa kuwatunza. Suala la kumpeleka mzee katika makazi ya wazee litakuwa ni kimbilio la mwisho baada ya njia nyingine zote za matunzo katika familia na jamii kushindikana.”

Waziri Mkuu amewataka vijana  na jamii kwa ujumla wasikwepe jukumu la kuwatunza wazee kwa sababu bila wao wasingekuwa hivyo walivyo leo. Ikumbukwe kuwa wazee hao nguvu zao za uzalishaji mali zimepungua kutokana na kazi waliyoifanya wakiwa vijana kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa familia zetu na Taifa kwa ujumla.

Pia, Waziri Mkuu ameziagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa ziombe vibali vya ajira ili waajiri Maafisa  Ustawi wa Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii Wasaidizi ambao wanahitajika kufanya kazi  kuanzia ngazi za Kata hadi Halmashauri ikiwemo kushughulikia changamoto za wazee katika jamii.

Pia, Waziri Mkuu ameielekeza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto iendelee kuimarisha na kusimamia Mabaraza ya Wazee ili yashiriki kikamilifu kuelimisha familia na jamii kutimiza wajibu wao wa kutunza wazee.

Pia, Waziri Mkuu ametaja changamoto zinazowakabili wazee ni pamoja na vitendo vya mauaji ya wazee kutokana na imani za kishirikina. “Napenda kurudia Wito kwa jamii kuhusu kuongeza mapambano ya kutokomeza vitendo vya mauaji kwa wazee wasiokuwa na hatia. Wakuu wa mikoa na wilaya waweke utaratibu maalumu wa kuwalinda wazee.”

Awali,Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema lengo la maadhimisho hayo ni kuongeza uelewa wa jamii kuhusu masuala mbalimbali ya wazee ikiwa ni pamoja na kutafakari fursa za changamoto zinazowakabili wazee na namna ya kuzitatua.

Waziri Ummy alisema kupitia maadhimisho hayo jamii inakumbushwa kuzingatia kwa kutekeleza kwa umuhimu haki za wazee na wazee nao wanakumbushwa wajibu wao kwa wajibu wao kwa jamii. Sens aya watu na makazi ya 2012 Tanzania inakadiriwa kuwa na wazee 2,507,568 sawa na asilimia 5.6 ya wananchi wote.

Alisema taarifa kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI, hadi Desemba 2018 jumla ya wazee 1,837,162 wametambuliwa na kati yao wazee 684,383 sawa na asilimia 37 ya wasiokuwa na uwezo wamepatiwa vitambulisho vinavyowawezesha kupata huduma za matibabu bila ya malipo. Idadi hiyo ni sawa na ongezeko la asilimia 319 mara tatu zaidi ya idadi ya wazee 214,370 waliopewa vitambulisho vya matibabu kwa 2016/2017.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Serikali Yaleta Mfumo Mpya Kukusanya Taarifa Za Kibiashara

Eric Msuya – MAELEZO
Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Stellah Manyanya amewataka wadau wa Sekta hiyo kutumia mfumo mpya wa kukusanya Taarirfa za Kibiashara Nchini kwa lengo la kupiga hatua kuelekea Tanzania ya Viwanda na Uchumi wa kati. 
 
Kuanzishwa kwa mfumo huo ujulikanao kama Trade Information Module, ni utekelezaji wa makubaliano ya kimataifa yaliyopo kwenye mkataba wa uwezashaji wa Kibiashara unaosimamiwa na Shirika la Biashara Duniani. 
 
Manyanya aliyasema hayo jana, Jijini Dar es Salaam katika mkutano wa Wafanyabaishara na Wadau wa Biashara,  kuhusu mfumo wa utoaji wa Taarifa za Kibiashara Nchini, ambapo alisema, mfumo huo mpya utasaidia utunzanzaji na upatikanaji  wa taarifa za Leseni pamoja na Vibali mbalimbali vya kufanyia Biashara Nchini. 
 
“Kama manavyojua, upatikanaji wa Taarifa ni muhimu sana katika kufanya maaamuzi ya kila jambo hivyo  uwepo wa Taarifa hizi za Biashara mahali pamoja utasaidia Wafanyabiashara kujua mahitaji, utaratibu na mahali pa kupata vibali mbalimbali” alisema  Mhe. Stellah 
 
Alisema mfumo huu utaliwezesha Taifa kupata Fedha za kigeni sambamba na kumsaidia mfanyabiashara kujua taratibu na masharti ya kuingiza Bidhaa zao Nchini kupitia Masoko ya Nje ya Nchi. 
 
Sambamba na hilo, Mhe. Stellah aliwataka Wafanyabiashara na Wadau mbalimbali kutumia mfumo huo vizuri kwani utaleta Mapinduzi makubwa katika Sekta ya Biashara Nchini pamoja na kuondoa kero mbalimbali. 
 
“Lakini pia mfumo huu utaongeza ukaribu baina ya Wafanyabaishara na Ofisi za Umma, utaongeza ufanisi na kupunguza gharama za Kibiashara, utapunguza muda anaotumia Mfanyabiashara kupata Leseni,  hivyo kwa ujumla mfumo huu utaboresha Mazingira ya Kibiashara Nchini kwa kuchangia Uchumi wa Nchi” alisema Mhe Stellah. 
 
Pamoja na hilo, Serikali ya awamu ya Tano, kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara, inaendelea kufanya jitihada mbalimbali za za kuboresha Mazingira ya Kibiashara Nchini (Blueprint  For Regulatory Reform to Improve Business Environment)  ili kuweza kuwavutia  wawekezaji wa ndani na Nje ya Nchi kuja kuwekeza  hapa kiurahisi. 
 
“tunafanya jitihada nyingi sana ili kuboresha mazingira nchini hususan mfumo wa udhibiti wa biashara Tanzania” alisema Manyanya. 
 
MWISHO.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger