Tuesday, 1 October 2019

Serikali Itaendelea Kuwalinda Wazee Dhidi Ya Ukatili

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuwalinda wazee dhidi ya vitendo vya ukatili, kuwawekea miundombinu na mazingira bora katika kutumia vyombo vya usafiri na kuweka utaratibu na vigezo vitakavyowawezesha kulipwa pensheni.

Waziri Mkuu ameyataka mashirika ya wazee yaelekeze rasilimali wanazozipata katika kutoa huduma za msingi kwa wazee na waepuke kutumia fedha nyingi kwenye mikutano, warsha na makongamano ambayo hayawafaidishi moja kwa moja wazee wenye uhitaji.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Oktoba 1, 2019) wakati akihutubia wananchi katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja Nangwanda Sijaona Manispaa ya Mtwara.

Amesema utoaji wa huduma kwa wazee ni moja ya vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli na kwamba itaendelea  kuchukua hatua za makusudi kwa lengo la kuboresha hali na maisha ya wazee nchini.

Amesema miongoni mwa hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kuimarisha ustawi na maendeleo ya wazee ni pamoja na kuanzishwa kwa mpango wa TASAF wa kunusuru kaya masikini uliolenga kuyasaidia makundi mbalimbali ya jamii yanayoishi katika umasikini uliokithiri likiwemo kundi la wazee.

“Hadi kufikia Septemba 2019 jumla ya wazee 680,056 kutoka kaya 1,118,747 wananufaika na mpango wa TASAF kwa Tanzania Bara na Zanzibar. Mpango huu, umesaidia wazee kujikimu na kumudu majukumu ya kulea wajukuu ambao wazazi wao wamepoteza maisha kwa sababu mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa ukimwi.”

Amesema Serikali pia inaendelea kutekeleza Sera ya Taifa ya Afya ya mwaka 2007 ambayo inatambua kuwa wazee ni kundi maalumu linalohitaji kupewa kipaumbele katika kupata huduma bora za afya, inaweka mkazo kuwa wazee wote wenye umri wa miaka 60 na kuendelea na wasiokuwa na uwezo watibiwe bila malipo.

Hata hivyo, Waziri Mkuu ameendelea kuziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha zoezi la kuwatambua na kuwapatia vitambulisho wazee wasiokuwa na uwezo linakuwa endelevu ili waweze kunufaika na huduma ya matibabu bila malipo  wanapougua.

Kadhalika, Waziri Mkuu amevitaka vituo vyote vya kutoa huduma za afya vya umma kutoa huduma bora na za haraka kwa wazee wenye vitambulisho hivyo na watenge dirisha maalumu kwa ajili ya kuwahudumia wazee ili wasikae kwenye foleni muda mrefu.

Akizungumzia kuhusu matunzo ya wazee, Waziri Mkuu amesema Sera ya Taifa ya Wazee ya Mwaka 2003 inatamka kuwa familia na jamii zina wajibu wa msingi wa kuwatunza na kuwahudumia wazee.

“Hii ni kutokana na ukweli kuwa mazingira ya familia yanamuwezesha mzee kujiona sehemu ya jamii na hivyo, kumfanya aondokane na msongo wa mawazo unaotokana na upweke na kutengwa. Familia kwa mtazamo wa hapa nchini kwetu inajumuisha baba, mama, watoto pamoja na ndugu wengine.”

 Waziri Mkuu ametoa  wito kwa familia, jamii na Mamlaka za Serikali za Mitaa kutimiza wajibu wao wa kutoa matunzo na malezi kwa wazee wasiojiweza, hatua ambayo  itaonesha kuwa jamii inathamini mchango mkubwa walioutoa wazee kwa ustawi na maendeleo ya Taifa. “Vilevile, nisisitize kuwa jukumu la kuwatunza wazee ni la kila mmoja wetu, hivyo kila mmoja anawajibika kuwatunza wazee.”

“Nyote mtakubaliana nami kuwa matunzo ya wazee katika makazi hutolewa kwa wazee wasiojiweza na wasio na ndugu wa kuwatunza. Suala la kumpeleka mzee katika makazi ya wazee litakuwa ni kimbilio la mwisho baada ya njia nyingine zote za matunzo katika familia na jamii kushindikana.”

Waziri Mkuu amewataka vijana  na jamii kwa ujumla wasikwepe jukumu la kuwatunza wazee kwa sababu bila wao wasingekuwa hivyo walivyo leo. Ikumbukwe kuwa wazee hao nguvu zao za uzalishaji mali zimepungua kutokana na kazi waliyoifanya wakiwa vijana kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa familia zetu na Taifa kwa ujumla.

Pia, Waziri Mkuu ameziagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa ziombe vibali vya ajira ili waajiri Maafisa  Ustawi wa Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii Wasaidizi ambao wanahitajika kufanya kazi  kuanzia ngazi za Kata hadi Halmashauri ikiwemo kushughulikia changamoto za wazee katika jamii.

Pia, Waziri Mkuu ameielekeza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto iendelee kuimarisha na kusimamia Mabaraza ya Wazee ili yashiriki kikamilifu kuelimisha familia na jamii kutimiza wajibu wao wa kutunza wazee.

Pia, Waziri Mkuu ametaja changamoto zinazowakabili wazee ni pamoja na vitendo vya mauaji ya wazee kutokana na imani za kishirikina. “Napenda kurudia Wito kwa jamii kuhusu kuongeza mapambano ya kutokomeza vitendo vya mauaji kwa wazee wasiokuwa na hatia. Wakuu wa mikoa na wilaya waweke utaratibu maalumu wa kuwalinda wazee.”

Awali,Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema lengo la maadhimisho hayo ni kuongeza uelewa wa jamii kuhusu masuala mbalimbali ya wazee ikiwa ni pamoja na kutafakari fursa za changamoto zinazowakabili wazee na namna ya kuzitatua.

Waziri Ummy alisema kupitia maadhimisho hayo jamii inakumbushwa kuzingatia kwa kutekeleza kwa umuhimu haki za wazee na wazee nao wanakumbushwa wajibu wao kwa wajibu wao kwa jamii. Sens aya watu na makazi ya 2012 Tanzania inakadiriwa kuwa na wazee 2,507,568 sawa na asilimia 5.6 ya wananchi wote.

Alisema taarifa kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI, hadi Desemba 2018 jumla ya wazee 1,837,162 wametambuliwa na kati yao wazee 684,383 sawa na asilimia 37 ya wasiokuwa na uwezo wamepatiwa vitambulisho vinavyowawezesha kupata huduma za matibabu bila ya malipo. Idadi hiyo ni sawa na ongezeko la asilimia 319 mara tatu zaidi ya idadi ya wazee 214,370 waliopewa vitambulisho vya matibabu kwa 2016/2017.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Serikali Yaleta Mfumo Mpya Kukusanya Taarifa Za Kibiashara

Eric Msuya – MAELEZO
Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Stellah Manyanya amewataka wadau wa Sekta hiyo kutumia mfumo mpya wa kukusanya Taarirfa za Kibiashara Nchini kwa lengo la kupiga hatua kuelekea Tanzania ya Viwanda na Uchumi wa kati. 
 
Kuanzishwa kwa mfumo huo ujulikanao kama Trade Information Module, ni utekelezaji wa makubaliano ya kimataifa yaliyopo kwenye mkataba wa uwezashaji wa Kibiashara unaosimamiwa na Shirika la Biashara Duniani. 
 
Manyanya aliyasema hayo jana, Jijini Dar es Salaam katika mkutano wa Wafanyabaishara na Wadau wa Biashara,  kuhusu mfumo wa utoaji wa Taarifa za Kibiashara Nchini, ambapo alisema, mfumo huo mpya utasaidia utunzanzaji na upatikanaji  wa taarifa za Leseni pamoja na Vibali mbalimbali vya kufanyia Biashara Nchini. 
 
“Kama manavyojua, upatikanaji wa Taarifa ni muhimu sana katika kufanya maaamuzi ya kila jambo hivyo  uwepo wa Taarifa hizi za Biashara mahali pamoja utasaidia Wafanyabiashara kujua mahitaji, utaratibu na mahali pa kupata vibali mbalimbali” alisema  Mhe. Stellah 
 
Alisema mfumo huu utaliwezesha Taifa kupata Fedha za kigeni sambamba na kumsaidia mfanyabiashara kujua taratibu na masharti ya kuingiza Bidhaa zao Nchini kupitia Masoko ya Nje ya Nchi. 
 
Sambamba na hilo, Mhe. Stellah aliwataka Wafanyabiashara na Wadau mbalimbali kutumia mfumo huo vizuri kwani utaleta Mapinduzi makubwa katika Sekta ya Biashara Nchini pamoja na kuondoa kero mbalimbali. 
 
“Lakini pia mfumo huu utaongeza ukaribu baina ya Wafanyabaishara na Ofisi za Umma, utaongeza ufanisi na kupunguza gharama za Kibiashara, utapunguza muda anaotumia Mfanyabiashara kupata Leseni,  hivyo kwa ujumla mfumo huu utaboresha Mazingira ya Kibiashara Nchini kwa kuchangia Uchumi wa Nchi” alisema Mhe Stellah. 
 
Pamoja na hilo, Serikali ya awamu ya Tano, kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara, inaendelea kufanya jitihada mbalimbali za za kuboresha Mazingira ya Kibiashara Nchini (Blueprint  For Regulatory Reform to Improve Business Environment)  ili kuweza kuwavutia  wawekezaji wa ndani na Nje ya Nchi kuja kuwekeza  hapa kiurahisi. 
 
“tunafanya jitihada nyingi sana ili kuboresha mazingira nchini hususan mfumo wa udhibiti wa biashara Tanzania” alisema Manyanya. 
 
MWISHO.


Share:

Ufafanuzi juu ya taarifa ya uteuzi iliyotolewa na IKULU Leo




Share:

Rais Magufuli Asaini Miswada minne na kuwa sheria rasmi

Rais Magufuli amesaini miswada minne na kuwa sheria rasmi, miswada hiyo ilipitishwa na Bunge  kupitia mkutano wake wa 16 uliofanyika mwezi Septemba mwaka huu.
 
Sheria zilizopitishwa ni pamoja na Sheria ya Serikali Mtandao Na. 10 ya mwaka 2019


Share:

Taasisi Za Kidini Na Jumuiya Za Kijamii Kanda Ya Ziwa Kuhakikiwa Kuanzia Tarehe 7 Oktoba Hadi Tarehe 18 Oktoba, 2019




Share:

Atiwa Mbaroni na TAKUKURU Kwa kwa kuisababishia Serikali hasara ya milioni 15

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) mjini Dodoma imemkamata mratibu  wa mradi wa Belgian Fund for Food Security (BFFS) Wilaya ya Bahi, Emmanuel Mziwanda (62) kwa tuhuma za kuisababisha Serikali hasara ya Sh15 milioni.

Mkuu wa taasisi hiyo mjini humo, Sosthenes Kibwengo akizungumza leo Jumanne Oktoba Mosi, 2019 amesema mtuhumiwa huyo aliyekamatwa akiwa msibani alikuwa akitafutwa na taasisi hiyo tangu Julai,  2017 akikabiliwa na mashtaka ya kughushi nyaraka na kumdanganya mwajiri wake.

Amesema kitendo hicho kimeisababishia Serikali hasara ya Sh15 milioni na kwamba baada ya uchunguzi kukamilika  na mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kutoa kibali cha kumfikisha mahakamani, mtuhumiwa alitoweka kusikojulikana.


Share:

Mbinu Za Matumizi Ya Zana Bora Kuinua Sekta Ya Kilimo

Na Ismail Ngayonga,MAELEZO
KILIMO ni uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania, hii ni kutokana na ukweli kuwa sekta hii huzalisha nusu ya uchumi wa nchi, robo tatu ya mazao yote yanayouzwa nje ya nchi na ni tegemezi la chakula na kutoa ajira ya karibu asilimia 80 ya Watanzania.

Hata hivyo kwa kipindi cha miongo miwili iliyopita, jumla ya uzalishaji wa bidhaa na huduma kitaifa kwa sekta ya kilimo ya kilimo imekuwa ikiongeza kwa wastani wa asilimia 3.5 tu kwa mwaka.

Inaelezwa kuwa ukuaji huu umekuwa ukiathiriwa zaidi na teknolojia duni ya kilimo, hali ya hewa isiyotarabiriwa na kushuka kwa kiwango uzalishaji upande wa ardhi, kutokana na asilimia 70 ya maeneo ya kilimo nchini kutegemea kilimo cha jembe la mkono.

Kuna baadhi ya vikwazo vinavyozuia kuenea kwa kwa matumizi ya teknolojia ya kisasa za kilimo na hivyo kukwamisha uwezo uliopo wa kuongeza uzalishaji katika kilimo, ikiwemo gharama kubwa za kupata huduma za zana za kisasa za kilimo kwa kukodi na ukosefu wa utaalamu na huduma za kufanyia matengenezo zana husika.

Aidha wakulima wadogo wadogo kwa ujumla hawana uelewa, umoja na ari ya kujipanga ili kushughulikia mahitaji yao na changamoto mbalimbali ili waongeze uzalishaji katika Kilimo.

Katika jitihada zake za kukuza matumizi ya zana bora za Kilimo, Serikali imekuwa mstari wa mbele katika kuwahamasisha wakulima katika kubuni mbinu mpya za matumizi ya utafiti, elimu na teknolojia mpya ili kuwa na shughuli za biashara zinazohusiana na kilimo zenye faida ya kuridhisha.

Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2019/2020, Waziri wa kilimo, Japhet Hasunga anasema  takwimu zinaonesha kwamba matumizi ya zana bora za kilimo yanaongezeka miongoni mwa wakulima nchini ambapo kwa mwaka 2018 wastani wa kitaifa umeongezeka hadi kufikia asilimia 20 kwa matrekta na asilimia 27 kwa wanyama kazi.

Naongeza kuwa kutokana na ongezeko hilo, matumizi ya jembe la mkono yamepungua na kufikia asilimia 53 kwa mwaka 2018 ikilinganishwa na asilimia 62 kwa mwaka 2013, juhudi zilizotokana na Serikali kuhamasisha sekta binafsi kuingiza matrekta na zana zake nchini.

“Kati ya mwaka 2016/2017 na 2017/2018, jumla ya matrekta makubwa 2,476 na matrekta madogo 586 yaliingizwa nchini, na Wizara kwa kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), TIB Corporate Bank na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imetoa mafunzo kwa waendesha mitambo 76 kuhusu uendeshaji na matengenezo ya matrekta aina ya URSUS” anasema Waziri Hasunga.

Waziri Hasunga anasema viongozi 108 wa Vyama vya Msingi na 53 wa Vyama vya Mazao (AMCOS) wamepatiwa mafunzo ya usimamizi na uendeshaji wa matrekta na kati ya AMCOS hizo, 50 ni za Mkoa wa Mwanza na 3 za Wilaya ya Bunda Mkoa wa Mara.

Anaongeza kuwa Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) imetoa mafunzo ya uendeshaji wa mitambo ya kuvunia na mashine za kukoboa mpunga kwa maopareta 28 na mafunzo ya usimamizi na uendeshaji mradi wa zana kwa wakulima viongozi katika skimu 14 za umwagiliaji.

Anazitaja Skimu hizo kuwa ni pamoja na Skimu za Mbuyuni, Uturo, na Ipatagwa (Mbarali), Nakahuga (Songea), Magozi (Iringa), Mkindo (Mvomero), Kilangali (Kilosa), Bagamoyo BIDP (Bagamoyo), Mombo (Korogwe), Kivulini (Mwanga), Musa Mwinjanga (Hai), Lekitatu (Arumeru), na Muungano (Babati).

Aidha Waziri Hasunga anasema Serikali kupitia Mfuko wa Taifa wa Pembejeo za Kilimo (AGITF) Wizara yake inaendelea kutoa mikopo ya pembejeo na zana za kilimo ambapo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1994 jumla ya mikopo yenye thamani ya Tsh Bilioni 82 imetolewa.

Akifafanua zaidi Waziri Hasunga anasema katika kipindi cha Julai 2018 hadi Machi 2019, mikopo 33 yenye thamani ya Shilingi 1,495,362,060 ikiwemo 22 ya mitambo ya mashambani, sita (6) ya pembejeo za kilimo na mitano (5) ya umwagiliaji imetolewa na vilevile Serikali imeendelea na ufuatiliaji wa marejesho ya mikopo ya nyuma ambapo katika mwaka 2018/19 jumla ya Tsh Bilioni 1.8 zimerejeshwa.

Matumizi ya zana bora za kilimo unasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza ufanisi na faida pamoja na kupunguza gharama za muda na rasilimali fedha ambazo kwa kiasi kikubwa zimewasaidia wakulima wengi kuongeza ukubwa wa mashamba yao angalau kwa robo hekta hadi kufikia hekta 1 hadi 4.

MWISHO


Share:

MBWA,PAKA 890 WAPEWA CHANJO BURE KAHAMA

Na Salvatory Ntandu - Malunde 1 blog
Zaidi ya mbwa na paka 890 wamepewa chanjo dhidi ya kuzuia kichaa cha mbwa wilayani kahama mkoani Shinyanga katika zoezi maalumu la chanjo hiyo inayotolewa bure na shirika la kuhudumia wanyama Tanazania (TAPO).

Akizungumza katika Maadhidhimisho ya siku ya kichaa cha mbwa duniani ambayo hufanyika kila mwaka Septemba 28,2019 yaliyofanyika wilayani humo, Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, Emmanuel Nangayi alisema chanjo hiyo ni muhimu sana kwa ajili ya kuzuia ugonjwa huo.

Amesema ugonjwa wa kichaa cha mbwa ni miongoni mwa magonjwa hatari ambayo hayana tiba na unaua kwa haraka hivyo ni vyema wakajitokeza kuwaleta mbwa wao na paka ili wapatiwe chanjo hiyo bure.

“Kinga hii ni ya mwaka mmoja na mbwa au paka asipochanjwa ni rahisi kupata ugonjwa huu nichukue fursa hii kuwaomba wananchi wa kahama kuhakikisha wanyama wao wanapewa chanjo hiyo”,alisema Nangayi.

Kwa upande wake Mtaalamu wa wanyama kutoka shirika la TAPO, George Master alisema ni vyema wananchi wakaacha ufugaji wa mbwa nap aka kiholela kwa kutowapatia matunzo maalumu ikiwa ni pamoja na kuwapatia chanjo na chakula hali ambayo inasababisha wanyama hao kuzurura ovyo.

Alisema ni vyema wafugaji wote wa mifugo hiyo wanapokuwa na tatizo wasisite kuwasiliana na shirika la TAPO ili wapatiwe elimu juu ya ufugaji wa kisasa wa wanyama mbalimbali wafugwao majumbani.
Mtaalamu wa wanyama kutoka shirika la TAPO, George Master akizungumza kuhusu chanjo ya mbwa na paka
Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, Emmanuel Nangayi akizungumza kuhusu chanjo kwa mbwa na paka
Share:

Painter Job Opportunity at U.S. Embassy

Painter   The U.S. Mission in Dar es Salaam is seeking eligible and qualified applicants for the positions below. Position Title: Painter Vacancy Number: DaresSalaam-2019-038 A copy of the complete position description listing all duties, responsibilities and qualifications required is available at: https://ift.tt/2p6reJy We Also Recommend you to Read: Top Scholarships 2019-2020 Career Advice and Job Interviews tips HOW TO… Read More »

The post Painter Job Opportunity at U.S. Embassy appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Mason Job Opportunity at U.S. Embassy

Mason The U.S. Mission in Dar es Salaam is seeking eligible and qualified applicants for the positions below. Position Title: Mason Vacancy Number: DaresSalaam-2019-037 A copy of the complete position description listing all duties, responsibilities and qualifications required is available at: https://ift.tt/2p6reJy HOW TO APPLY: Applicants MUST follow instructions in the notice on the website: Failure to do so… Read More »

The post Mason Job Opportunity at U.S. Embassy appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Faith-Based Community Outreach Coordinator Job at MDH

Faith-Based Community Outreach Coordinator   Management and Development for Health (MDH) is a non-profit, non-governmental organization whose primary aim is to contribute to address public health priorities of the people of Tanzania and the world at large. These priorities include: communicable diseases such as HIV/AIDS, Tuberculosis and Malaria; Reproductive, Maternal, New-born and Child health (RMNCH); Nutrition; Non-Communicable Diseases of… Read More »

The post Faith-Based Community Outreach Coordinator Job at MDH appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Finance and Administrative Officer at Winrock International

Finance and Administrative Officer Tabora, Tanzani PROGRAM SUMMARY: The ARISE program is a high-quality, results-oriented program to prevent and help eliminate child labor through improved awareness of the hazards of child labor, greater livelihoods opportunities for vulnerable households, and improved access to education for children and youth. The position has an anticipated start date of September 1, 2019. This… Read More »

The post Finance and Administrative Officer at Winrock International appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Naibu Waziri Mabula Ataka Majina Ya Watumishi Wa Ardhi Waliokacha Kwenda Mafia

Na Munir Shemweta, MAFIA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameagiza kupatiwa majina ya watumishi saba wa sekta ya ardhi awaliopangiwa kuhamia halmashauri ya wilaya ya Mafia mkoani Pwani lakini wameshindwa kuripoti katika kituo chao kipya cha kazi.

Dkt Mabula alitoa agizo hilo jana mwamzoni mwa ziara yake ya siku mbili katika wilaya ya Mafia mkoani Pwani kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi, kukagua mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi kwa njia ya kielektroniki, kukagua Masijala ya ardhi pamoja na kutatua migogoro ya ardhi.

Kauli ya Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi inafuatia kuelezwa na Mkuu wa wilaya ya Mafia Shaib Nnunduma kuwa wilaya yake ina mtumishi mmoja wa sekta ya ardhi jambo linaloifanya wilaya hiyo kushindwa kutekeleza majukumu ya sekta hiyo ipasavyo.

Dkt Mabula alisema, Wizara yake italifanyia kazi suala hilo mapema kwa kuwa ni vigumu wilaya kufanya kazi vizuri katika sekta ya ardhi kwa kutegemea mtumishi mmoja hasa ikizingatiwa sekta hiyo inahitaji kuwa na wapimaji, wathamini pamoja na wataalamu wa mipango miji.

‘’Mafia mna mtumishi mmoja wa sekta ya ardhi? Suala hili inabidi lifanyiwe kazi mapema na wizara yangu italifanyia kazi kuhakikisha wilaya inakuwa na watumishi wa njanja zote katika sekta ya ardhi’’ alisema Dkt Mabula

Awali Mkuu wa Wilaya ya Mafia Shaib Nnunduma alimueleza Naibu Waziri Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa, changamoto kubwa inayoikabili wilaya yake kwa upande wa sekta ya ardhi ni kukosekana watumishi wa kutosha ambapo wilaya hiyo imekuwa na mtumishi mmoja wa sekta hiyo kwa muda mrefu baada ya mtumishi mmoja wa Uthamini kupangiwa majukumu mengine.

Kwa mujibu wa Nnunduma, jitihada za wilaya yake kufuatilia upatikanaji Watumishi wa sekta ya ardhi zimeonekana kukwama kwa kuwa hadi sasa hawajapata mtumishi mwingine jambo linaloifanya wilaya hiyo kushindwa kutekeleza vyema majukumu ya sekta hiyo.

‘’Watumishi saba walipangiwa kuja Mafia lakini wameshindwa kuripoti na hapa unavyotuona tuna mtumishi mmoja, hatuna wataalamu kama wangekuwepo wangesaidia upangaji. Wilaya ni kama imesimama katika sekta ya ardhi’’ alisema Nnunduma

Nnunduma alisema, ujio wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi inaweza kuwa faraja kwao kupata watumishi kwa kuwa tangu kuteuliwa kwake na Rais John Pombe Magufuli kuongoza wilaya ya Mafia ndiyo anashuhudia Waziri wa kwanza wa sekta ya ardhi kwenda wilaya hiyo aliyoieleza kuwa kama itatumiwa vizuri basi itaiwezesha serikali kuingiza mapato mengi kupitia sekta ya utalii.

Mbunge wa jimbo la Mafia Mbaraka Dau alimueleza Dkt Mabula kuwa, pamoja na changamoto nyingine lakini Wilaya hiyo inakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa la Baraza la Ardhi la nyumba  la wilaya jambo linalowalazimu wananchi kufunga safari hadi katika Baraza la Mkuranga kitu alichokieleza kinawafanya baadhi ya wananchi kushindwa kwenda na hivyo kupoteza haki zao.


Share:

Waziri Jafo Awataka Wakuu Wa Shule Kutojihusisha Na Udanganyifu Wa Mitihani.

Na  Faustine Gimu
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) SELEMANI JAFO  amewataka wakuu wa shule za msingi kutojihusisha na suala la udanganyifu wa mitihani kwa kuwa linaporomosha elimu ya Tanzania.
 
Waziri Jafo ametoa agizo hilo  jana jijini Dodoma wakati akifungua mkutano mkuu wa kwanza wa wenyeviti wa walimu wakuu wa shule za msingi Tanzania Bara.
 
Amesema wao wanadhamana kubwa katika kusimamia sekta ya elimu nchini hivyo ikitokea uvujaji wa mitihani hauleti picha nzuri katika Taifa.

Akizungumzia suala la elimu bila ya malipo amesema matumizi ya fedha hizo yameimarika tofauti na ilivyokuwa mwanzo walipoanza ambapo kulijitokeza changamoto mbalimbali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa walimu wakuu wa shule za msingi Tanzania bara(Tapsha), REHEMA RAMOLE ameipongeza serikali kwa uboreshaji wa miundombinu jambo ambalo limepunguza msongamano wa wanafunzi darasani.
 
Kauli mbiu ya mkutano huo inasema Uwajibikaji na Usimamizi makini wa Rasilimali katika elimu ndio Msingi wa Elimu Bora.



Share:

Rais Magufuli Kafanya Uteuzi wa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Wakurugenzi wa Halmashauri za Manispaa na Wilaya




Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne October 1




Share:

Monday, 30 September 2019

Waziri Lugola Aagiza Askari Wote Kituo Cha Polisi Wahamishwe

Na Felix Mwagara, MOHA-Katavi
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ameliagiza Jeshi la Polisi Mkoani Katavi, kuwahamisha askari wote wa Kituo cha Polisi Majimoto kutokana na tuhuma mbalimbali zinazowakabili askari hao.

Waziri Lugola alitoa agizo hilo jana kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na mamia ya wananchi wa Mji wa Majimoto, Wilaya ya Mlele wakati akijibu kero mbalimbali za wananchi.

Akizungumza katika mkutano huo, Waziri Lugola alisema kero zilizowasilishwa na wananchi hao, zinaonyesha askari wa kituo hicho wanajihusisha na vitendo mbalimbali vya rushwa, kupiga wananchi ovyo, kushindwa kudhibiti ulinzi na usalama pamoja na kushughulikia malalamiko ya wananchi.

“Natoa agizo hili liwe fundisho kwa askari wote wasiowaaminifu kote nchini, Kamanda wa Polisi wa Mkoa huu natoa siku saba askari wote wa kituo hiki wahamishwe na waletwe wengine ili wajifunze,” alisema Lugola.

Baada ya agizo hilo, waendesha bodaboda na wananchi wengineo, walishangilia na kusema kuwa mji huo sasa utatulia kutokana na uwepo wa amani bila kuwa na manyanyaso.

Mmoja wa wananchi aliyetoa malalamiko dhidi ya polisi katika kituo hicho ni Malewe Maswe, alilalamikia kuwa baadhi ya askari hao walimpiga na kumsababishia maumivu makali ya miguu kutokana na kuhoji kosa lake la kuletwa kituoni hapo baada ya kugombana na mwalimu mmoja katika mji huo.

“Tulikuwepo na Mwalimu niliyegombana naye kituoni hapo, askari wakaniambia nendeni mkaelewane na mwalimu huyo, nikawaambia hatuwezi elewana maana zoezi hilo lilishindikana, askari wakasema unatufundisha kazi, yule pale dogo (askari ambaye alikuwa katika mkutano huo) simjui jina lake alinipiga kipigo sana, na askari mwingine bonge anachochea hii ndiyo Serikali ya Magufuli,” alisema Maswe.

Aidha, Waziri Lugola alijibu kero mbalimbali, ikiwemo ya Mkazi wa Mji huo, Malugu Mayombi ambaye ni mkulima maarufu wa mpunga wa eneo hilo, aliangua kilio kwa waziri akidai polisi wameshindwa kushughulikia kesi yake ya madai ya shilingi milioni sitini (6000,000/-) anazomdai mfanyabiashara Sali Kulwa maarufu TBS aliyemuuzia gunia 623 za mpunga.

“Waziri wangu, naomba unisaidie mimi maskini, ujiowako utaniokoa, nakuomba Waziri unisaidie nadai shilingi milioni 33 na laki 5 kati ya shilingi milioni 60 nimelipwa shilingi milioni 26 na laki 5 pekee, nimeshindwa kuendeleza kilimo naishi kwa shida, nilikuwa nalima ekari 100 kwasasa nalima ekari 30 tu nisaidie jamani, nateseka mimi,” alisema Mayombi.

Waziri Lugola alimuagiza Kamanda wa Polisi kushirikiana na Mkuu wa Polisi Wilaya kulitatua suala hilo kwa muda wa wiki moja wamkamate mtuhumiwa na aweze kumlipa fedha za Mayombi.

Waziri Lugola amemaliza ziara ya siku tano Mkoani Katavi, na ameelekea Mkoani Rukwa kuendelera na ziara ya kikazi akisikiliza kero za wananchi na kuzitatua katika mikutano mbalimbali ya hadhara mkoani humo.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger