Thursday, 8 August 2019

TPDC YAJIPANGA VYEMA KUSAMBAZA GESI KATIKA NCHI WANACHAMA WA SADC


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, (TPDC), Dkt. James Matarajio, akizungumza na wafanyakazi wa shirika hilo, wakati wa maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda ya SADC katika Viwanja vya Ukumbi wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, leo kuelekea Mkutano Mkuu wa Nchi Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika utakaoshirikisha jumla ya Nnchi 16 za Jumuiya hiyo unaoanza Agosti 9 kwa Mawaziri na kwa Marais utafanyika kwa siku mbili.

 Meneja Mawasiliano wa TPDC Bi. Marie Msellemu akiongea na mwananchi aliyetembelea banda lao kujua huduma zao.
 Meneja Mawasiliano wa TPDC Bi. Marie Msellemu akiongea na wanahabari.
Mfanyakazi wa TPDC (kulia) akizungumza na mwananchi aliyetembelea banda lao kujua huduma wanazotoa.

Wafanyakazi wa TPDC wakiwa katika picha ya pamoja.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limejipanga kuendelea kutoa huduma zilizo bora kwa wateja wake ili kuwapunguzia matumizi ya fedha.

Hayo yamesema na Meneja Mawasiliano wa TPDC Bi. Marie Msellemu wakati akizungumza na wanahabari waliofika kujionea huduma wanazotoa katika maonesho ya 4 wiki ya Viwanda kuelekea mkutano mkuu wa 39 wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika (SADC) kwenye Viwanja vya Ukumbi wa Julius Nyerere Dar es Salaam.

Bi. Msellemu amesema kuwa kwa sasa wamejipanga kufungua vituo vingi zaidi kwa ajili ya kusambaza gesi asilia inatumika katika magari ikiwa na kuongeza zaidi upatikanaji wa gesi hiyo majumbani.

"Tupo katika mkakati wa kufungua vituo vingi zaidi vya kujazia gasi kwa wale wateja wetu wanaotumia gesi katika magari na pia tunawashauri Watanzania kununua magari yanayotumia gesi ili kuweza kupunguza matumizi," amesema.

Amesema kuwa mpaka sasa zoezi la kuwaunganishia gesi majumbani linaendelea vyema na wamefikia nyumba zipatazo 1000 toka kwa vile nyumba 70 walizoanza nazo awali katika mkoa ya Mtwara, Lindi na Dar es Salaam.

Ameongeza kuwa mkakati wao mwingine ni Kuchimba gesi yao wenyewe Mnazi Bay Kaskazini na Songosongo Magharibi ... ikiwa na kauli mbiu ya kufanya mazingira wezeshi

Mpaka sasa wamejipanga zaidi kuweza kusambaza gesi katika nchi wanachama wa SADC japo kwa sasa nchi za Kenya, Uganda na Zambia zimeonyesha nia ya kutaka kusambaziwa.
Share:

Wakurugenzi Wakutana Kuboresha Mwongozo Wa Ukopaji Na Upokeaji Misaada

Na. Scola Malinga, WFM, Dar es Salaam
Serikali imejipanga upya kuongeza ufanisi wa kiutendaji kwa kupitia na kuboresha mwongozo wa ukopaji, utoaji wa dhamana na upokeaji misaada nchini.

 Hayo yamebainishwa jijini Dar es Saalam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na mipango, Bw. Doto James,wakati wa ufunguzi wa warsha ya wakurugenzi wa Sera na Mipango wa wizara mbalimbali iliyoangazia kujadili na kuweka mkakati wa mwongozo huo.

Bw. James alisema kuwa, chimbuko la Mwongozo huo ni changamoto ambazo Serikali imekuwa ikikabiliana nazo wakati wa kutekeleza miradi ya maendeleo hususan miradi inayotekelezwa kwa fedha za mikopo na misaada kutoka kwa wadau wa maendeleo.

“Kama Wizara ya Fedha na Mipango, tumeshuhudia uwepo wa maandalizi duni ya miradi,na pia miradi kuchukua muda mrefu kuanza kutekelezwa na hivyo kuigharimu Serikali muda na fedha", alieleza Bw. James.

Aidha, Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Fedha, alieleza kuwa eneo lingine ambalo limekuwa na changamoto katika utekelezaji wa miradi ni misamaha ya kodi. Katika kulifanyia kazi jambo hilo, Wizara ya Fedha na Mipango imeandaa taarifa na mapendekezo kuhusu namna ya kukabiliana na changamoto za masuala ya kodi ili miradi yote yenye changamoto za kodi itekelezwe ipasavyo kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi.

Bw. James, aliwasisitiza wakurugenzi hao kufanya majadiliano ya  rasimu ya Mwongozo na kutoa mapendekezo ambayo yatatumika katika kukamilisha Mwongozo huo ili uje kusaidia katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

Aidha, Mwenyekiti wa Warsha hiyo ambaye ni Katibu Mkuu Msaafu, Bw. Peniel Lyimo, aliwasisitiza wajumbe wa kamati hiyo kuendelea kusaidia usimamizi wa miradi ya serikali kwenye maeneo yao.

Bw. Lyimo aliwapongeza wajumbe wa mkutano kwa michango yao itakayowezesha kufanikisha kukamilika kwa mwongozo huo, ambapo utakapokamilia utasaidia katika kutekeleza na kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo na hivyo kuleta tija kwa wananchi.

Aidha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi Amina Shaaban, alieleza kuwa, nchi ya Tanzania imeshuhudia kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato ya ndani katika miaka ya karibuni, hususan kuanzia mwaka 2016. Pamoja na kuongezeka kwa mapato, bado nakisi ya bajeti imekuwa ikiongezeka kutokana na Serikali kujikita katika kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo, ukiwemo mradi wa Umeme wa Maporomoko ya mto Rufiji, Reli ya Kisasa kwa kiwango cha Kimataifa (SGR), ujenzi na ukarabati wa madaraja na miundombinu mbalimbali.

Alisema ili kuziba pengo la nakisi, Serikali imekuwa ikiingia katika michakato mbalimbali ya madeni, dhamana na misaada kwa kutumia sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada, Suraya 134.

Bi. Amina Shaaban alibainisha kuwa, changamoto iliyojitokeza miaka ya hivi karibuni, ni kupungua kwa mikopo yenye masharti nafuu (concessional loans), hivyo Serikali imelazimika kuingia katika mikopo ya kibiashara (commercial loans).

Aidha, mikopo hiyo huambatana na masharti magumu na hivyo huhitaji umakini mkubwa (responsible borrowing) ili kuepuka kuingiza Taifa katika mikopo isiyolipika.

Alisema kuwa pamoja na michango wajumbe wa warsha hiyo katika kupitia na kuboresha rasimu ya mwongozo huo, Serikali imejipanga kuutekeleza mara utakapokamilika.



Share:

Jeshi la Polisi Latoa ONYO Kwa Madereva Nchini

Jeshi la Polisi nchini limetoa ufafanuzi na kuweka msisitizo kwenye katazo alilotoa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam tarehe 05/08/2019 kuhusu kupiga marufuku magari kufunga taa za vimulimuli au za rangi rangi, taa zenye mwanga mkali (spot light) na kufunga ving’ora kwenye magari ya kiraia au watu binafsi na pikipiki za kiraia.

Akitoa tamkoa hilo Msemaji wa Jeshi hilo SACP, David Misime amesema kuwa, katazo hilo ni kwa nchi nzima, kutokana na kujitokeza kwa baadhi ya watu walioamua kufunga vimulimuli na ving’ora na kuvitumia wawapo barabarani na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara.

Wamefunga vifaa hivyo kutaka kupewa kipaumbele wawapo barabarani kwa kujua au kwa kutofahamu kuwa ni kinyume na sheria, kanuni na taratibu zilizopo.

Na kwa mujibu wa sheria ya usalama barabarani sura ya 168 ya mwaka 1973 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002 kifungu cha 39 B (I) na (2) kinafafanua juu ya matumizi ya ishara ikiwepo ving’ora na vimulimuli.


Share:

Wachimbaji wadogo wa dhahabu Watakiwa Kuzingatia Sheria za Mazingira

Na Lulu Mussa, GEITA
Wachimbaji wadogo wa dhahabu katika Kata ya Mugusu Mkoani Geita wametakiwa kufuata taratibu za hifadhi ya mazingira ili kunusuru afya zao na kuchukua tahadhari ya kukabiliana na uwezekano wa milipuko ya magonjwa.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima mara baada ya kufanya ziara ya kikazi kutembelea eneo la Mgusu, kuona uzingatiaji na utekelezaji wa Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004.

Akiwa katika eneo la Mugusu Naibu Waziri Sima amesema bado kuna tatizo la usafi wa mazingira katika maeneo wanayoyatumia kuchenjua dhahabu kwa kutumia zebaki, na kuna haja wachimbaji hao kukaa na halmashauri ya Geita Vijijini ili kuhakikisha wanakuwa na vyoo bora.

Akitoa kauli ya Serikali kuhusu mpango kazi wa Taifa wa kupunguza matumizi ya zebaki kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu katika shughuli za uchenjuaji, Sima amewataka wakazi wa Mgusu kuendelea na shughuli za uzalishaji wa dhahabu bila kuathiri sekta ya mazingira kwa kupunguza matumizi ya zebaki inayoharibu mazingira na afya za binadamu.

“Nimeona namna vijana wanavyojishughulisha kwa ajili ya kujipatia kipato, hili ni jambo jema kwenye Taifa letu, lakini nimetembea hadi chini kwenye ule mto wa Nyamasenge hakuna vyoo, watu wanatumia pori na mto kwa ajili ya haja ndogo na kubwa.

“Kwa mazingira yetu ni hatari sana, tunaweza kufanya kazi nzuri lakini ugonjwa utasitisha shughuli zetu. Nawasisitiza kuwa Usafi ni jambo la kwanza katika kufanya kazi, huwezi kuwa na nguvu isiyojali usafi,” alisema Sima.

Awali, Naibu Waziri Sima alitembelea chanzo cha maji cha maji cha Mto Mabubi na kujionea hali mbaya inayotishia kutoweka kwa chanzo hicho kutokana na shughuli za kibinadamu zinazoendelea kandokando ya eneo hilo.

“Chanzo cha maji cha mto Mabubi, hakitadumu na maji hayatakuwa salama kwa matumizi ya binadamu endapo kitaendelea kuingia kemikali ya zebaki nanyi wachimbaji kujisaidia katika eneo hilo” Sima alisisitiza.

Diwani wa Kata ya Mgusu Bw. Pastory Ruhusa amesema kuwa ataitisha mkutano wa wananchi mapema iwezekanavyo ili kuweka mikakati ya haraka kutokomeza hali hiyo ikiwa ni pamoja na usafi wa mazingira na kupunguza matumizi ya zebaki.

Naibu Waziri Sima yuko katika ziara ya kikazi Kanda ya Ziwa kukagua uzingatiaji na usimamizi wa Sheria ya Mazingira pamoja na uwaelimisha wananchi mpango wa Serikali wa kupunguza matumizi ya zebaki nchini.



Share:

Waziri Wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga Akagua Utekelezaji Wa Maagizo Ya Waziri Mkuu Kuhusu Ununuzi Wa Pamba Katika Wilaya Ya Bariadi, Itilima Na Maswa

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Simiyu
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) Leo tarehe 6 Agosti 2019 amefanya ziara ya kikazi mkoani Simiyu kukagua utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu aliyoyatoa hivi karibuni kwa wafanyabiashara kununua Pamba ya wakulima.

Mhe Hasunga ametembelea na kukagua Kituo cha ununuzi wa Pamba cha Itemelo kilichopo kata ya Dutwa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Kituo cha ununuzi cha Lugulu katika kata ya Lugulu Wilaya ya Itilima na Kituo cha Kumalija kilichopo katika kata ya Shanwa wilayani Maswa.

Katika ziara hiyo Mhe Waziri amejionea hali ya ununuzi wa Pamba ya wakulima ukiwa unaendelea kutokana na serikali hivi karibuni kupata muarobaini wa mustakabali wa zao hilo.

Waziri huyo wa Kilimo amepiga marufuku Pamba ya wakulima kupimwa katika mizani zisizofahamika badala yake lazima ipimwe katika mizani iliyothibitishwa na wakala wa vipimo.

Katika hatua nyingine pia Mhe Hasunga ametoa kalipio Kali kwa wanunuzi wa Pamba kadhalika vyama vya ushirika vinavyowakata kilo moja wakulima kwa madai ya mifuko ya kupimia badala yake ameagiza mkulima akatwe kutokana na uzito wa mfuko sio kukadiria kilo moja.

Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imekusudia kuwanufaisha wakulima kupitia mazao wanayozalisha kwa kuwaongezea elimu ya Kilimo bora na chenye tija.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga yupo mkoani Simiyu kwa ajili ya sherehe za wakulima (Nanenane) ambazo kilele chake ni tarehe 8 Agosti 2019 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wakati wa kufunga maadhimisho hayo akimuwakilisha Rais wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli.



Share:

Waziri Mpina Ashangazwa Na Uwepo Wa Chama Cha Wavuvi Ngazi Ya Taifa Bila Wizara Yake Kuwa Na Taarifa

Na. Edward Kondela
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina ameitaka Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini kukaa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kupitia kwa pamoja taratibu za usajili wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Wavuvi nchini (CHAKUWATA) ambao hautambuliki katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi ilhali kinafanya kazi na wavuvi.

Waziri Mpina amesema hayo  jana  (07.08.2019) katika Maonesho ya wakulima, wafugaji na wavuvi nchini (Nanenane) kwenye viwanja vya Nyakabindi katika Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Kilimo na kukuta uwepo wa chama hicho CHAKUWATA na kushangazwa kwa kuwa kinajishughulisha na wavuvi bila Wizara ya Mifugo na Uvuvi yenye dhamana na wavuvi kufahamu uwepo wake ambapo hakuridhishwa na sababu zilizotolewa na Naibu Mrajis Uhamasishaji kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini Bw. Charles Malunde juu ya uhalali wa CHAKUWATA.

“Mpaka chama kinasajiliwa wizara haijui, lazima wizara ihusishwe katika hatua zote sasa kama katibu anayehusika na uvuvi hajui, mimi waziri sijui yaani hapa ndiyo tunashangaa kuna Chama Kikuu cha Ushirika wa Wavuvi Tanzania (CHAKUWATA). Sasa kwa sababu mmeshalifikisha hapa nia ya kuanzisha ushirika ni nzuri ibaki palepale lakini nyinyi (Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini) mkae muone namna bora kama kuna vitu havikufuatwa vikamilishwe kwa ukamilifu kwa sababu kuanzishwa huko bado hautuzuii kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza huko nyuma.” Amesema Waziri Mpina

Akitembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho hayo Waziri Mpina amesema ameridhishwa na umati wa watu unaofika katika banda hilo ili kupata elimu na kusema nia ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ni kuwafikia wadau ili kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika sekta za mifugo na uvuvi.

“Tunataka tuwahakikishie zile changamoto ambazo wametuwasilishia hapa tunaenda kuzifanyia kazi ili kuhakikisha tunapokutana mwaka mwingine wa Maonesho ya Nanenane zitakuwa zimesharekebishwa ili mwaka unaofuata wawe mashahidi kwa kushuhudia mageuzi makubwa ambayo yatakuwa  yamefanyika.” Amefafanunua Waziri Mpina

Amefafanua kuwa baadhi ya changamoto kubwa ambazo amekutana nazo ni upungufu mkubwa wa chakula cha samaki na mifugo ambapo amesema anawahakikishia wadau katika sekta za mifugo na uvuvi katika kipindi kinachofuata Wizara ya Mifugo na Uvuvi itapanga mikakati madhubuti kuhakikisha changamoto hizo zinatatuliwa.

Kuhusu masoko ya bidhaa mbalimbali zinazotokana na mifugo ambazo amezishuhudia kwenye Maonesho ya Nanenane Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina amesema wizara itahakikisha wadau wake wanatafutiwa soko la uhakika ili waweze kuuza mazao yao pamoja na bidhaa zinazotokana na mazao ya mifugo.

Akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na watendaji wa taasisi zilizo chini ya wizara ambao wanashiriki katika Maonesho ya Nanenane kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu, Waziri Mpina amesema ameridhishwa na namna wananchi wanavyohudumiwa kwa kupatiwa elimu na ufahamu juu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kesho (08.08.2019) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha maadhimisho ya Maonesho ya Nanenane kitaifa yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi vilivyopo katika Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu.

Mwisho


Share:

Naibu Waziri Wa Maliasili Na Iutalii Mhe, Constantyine Kanyasu Aziagiza Taasisi Za Uhifadhi Nchini Kuunda Vikosi Maalum Vya Kudhibiti Wanyamapori Wakali

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ameagiza kila Taasisi ya Uhifadhi nchini ihakikishe inaunda kikosi maalum cha askari wanyamapori watakaokuwa wakitumika kudhibiti wanyama wakali na waharibifu pindi wanapovamia makazi ya wananchi badala ya kutegemea kikosi kimoja p cha  Askari  kutoka Kikosi Dhidi ya Ujangili (KDU)

Agizo hilo amelitoa jana wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa Shamba la miti la Rondo  ikiwa ni ziara yake ya kikazi katika mkoa wa  Lindi.

Akizungumza na watumishi hao, Mhe.Kanyasu amesema kutokana na Serikali kudhibiti ujangili kwa kiasi kikubwa wanyamapori kama vile tembo, chui na simba  wamekuwa wakitembea kila mahali kwa sababu hawana hofu ya kuuliwa kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma.

Amesema hali hiyo imepelekea mazao pamoja na maisha ya wananchi kuwa hatarini hasa kwa wananchi wanaoishi karibu na Hifadhi.

Amesema licha ya wanyamapori hao kuongezeka ikiwa moja ya sababu ni Serikali  kuzuia kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi wanyama hao wamekuwa wakipita njia zao za asili  ambazo tayari zimevamiwa na hivyo kusababisha matatizo makubwa kwa wananchi.

Kufuatia hali hiyo, Mhe.Kanyasu ameitaka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Hifadhi za Taifa( TANAPA) na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA) ziwe na vikosi maalum vya askari watakaotumika  kukabiliana na wanyamapori hao wakati wanapovamia vijiji.

" Kwa sasa kukutana na kundi la tembo zaidi ya 500 katika miji ya Butiama, Dodoma pamoja Morogoro ni jambo la kawaida, Hatuwezi kutegemea  KDU pekee lazima nguvu iongezwe" alisema Mhe.Kanyasu.

Amesema TFS ihakikishe inakuwa kikosi hicho cha Askari katika Hifadhi za Mazingira Asilia ambako kuna wanyamapori wakali ma waharibifu wakiwemo tembo na viboko, simba na chui.

Amesema kwa sasa Wizara ya Maliasili na Utalii imekuwa ikipokea maombi mengi kwa siku kutoka kwa wananchi walioathiriwa na wanyamapori wakali na waharibifu.

Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu ametoa pole kwa wananchi wa Kijiji cha Rondo kufuatia kifo cha kumpoteza Mwalimu  wa shule ya msingi pekee katika kijiji hicho  aliyekufa baada ya  kuuliwa na tembo baada ya kumpiga picha tembo aliyekuwa akihangaika kumnasua mtoto wake aliyekuwa amenaswa kwenye kichaka.

Aidha, Mhe.Kanyasu amezitaka Halmashauri nchini zinazopakana na Hifadhi zihakikishe zinaajiri askari Wanyamapori watakaokuwa wakisaidia kutoa msaada wa haraka pindi wanyamapori hao wanapovamia vijiji

Pia, Amezitaka Halmashauri ziangalie uwezekano wa kuwatumia askari wanyamapori wa vijiji (VGS) kwa kuandaa utaratibu maalum wa kuwakabidhi silaha pindi wanyamapori wanapovamia mashamba na makazi ya wananchi.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Mgenda amesema kutokana na juhudi za uhifadhi unaofanywa na Mkoa huo umechangia wanyamapori kuongezeka na kuwa huru kutembea kila mahali

Kufuatia na hali hiyo, Mhe. amemuomba Naibu Waziri huyo ahakikishe  Taasisi zake za  Uhifadhi nchini zunatoa elimu kwa wananchi ili waweze kujihami wakati wanyamapori hao wanavamia mali na makazi yao.


Share:

MWAUWASA Yatangaza Bei Mpya za Maji




Share:

Lukuvi awasimamisha kazi watumishi 183 Wizara ya Ardhi

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , William Lukuvi  amewasimamisha kazi watumishi 183 wa wizara hiyo kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.

Watumishi hao ambao waziri huyo amekabidhi majina yao Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa ajili ya uchunguzi, wanadaiwa  kuingilia mfumo wa kukadiria na kukusanya kodi ya pango ya ardhi kinyume na taratibu na kusababisha upotevu wa mapato ya Serikali.




Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi 08 August
























Share:

Wednesday, 7 August 2019

Serikali Yafuta Umiliki wa Kitalu cha Uwindaji wa Kitalii cha Lake Natron




Share:

Petrol, Dizeli na Mafuta ya taa vyashuka Bei

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza kupungua kwa bei ya mafuta ya taa, petroli, dizeli yanayoingizwa nchini kupitia bandari za Dar es Salaam, Mtwara na Tanga kuanzia leo.
 
Taarifa  iliyotolewa na Ewura imesema bei ya jumla na rejareja kwa mafuta yaliyoingiziwa bandari ya Dar es Salaam imepungua huku petroli kwa Sh160 sawa na asilimia 6.9, Dizeli Sh102 sawa asilimia 4.3 na mafuta ya taa yamepungua kwa Sh81 sawa na asilimia 3.7.

Ewura imesema bei ya jumla na rejareja kwa mafuta ya petroli, dizeli na taa yaliyoingizwa nchini kupitia bandari ya Tanga nayo imepungua ikilinganishwa na toleo lililopita la Julai 3, 2019.

Taarifa hiyo imesema bei ya rejareja kwa mikoa ya Kaskazini ambayo ni pamoja na Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara nayo imeshuka.

Petroli imepungua kwa  Sh134 kwa lita sawa na asilimia 5.7, dizeli Sh103 sawa na asilimia 4.6 na mafuta ya taa Sh163 sawa na asilimia 7.3.

Ewura imesema bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya petroli na dizeli yaliyoingizwa kupitia bandari ya Mtwara ambayo inahudumia mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma imepungua kwa Sh105 sawa na asilimia 4.5, Sh124 sawa na asilimia 5.3.


Share:

Mbunge Bobi Wine wa Uganda ashtakiwa kwa kumkasirisha Rais Yoweri Museveni

Mbunge wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi Ssentamu ambaye ni mashuhuri zaidi kwa jina la Bobi Wine ameshtakiwa kwa kosa la kumkasirisha na kumkejeli Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni.

Mbunge huyo na wenzake wanatuhumiwa pia kuurushia mawe msafara wa Rais Yoweri Museveni wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi katika mji wa kaskazini wa Arua mwaka uliopita wa 2018.

 Aidha shitaka hilo jipya limeongezwa katika orodha ya mashtaka mengine yanayomkabili Mbunge huyo wa upinzani likiwemo lile la uhaini. 

Taarifa zaidi zinasema kuwa, iwapo Bobi Wine atapatikana na hatia atakabiliwa na kifungo cha maisha jela.

Bobi Wine bado anakabiliwa na mashtaka katika mahakama nyingine kwa kuongoza maandamano dhidi ya sheria inayoweka kodi katika mitandao ya kijamii pamoja na biashara zinazofanywa kupitia malipo ya simu za mkononi.

Halikadhalika, Mbunge hivi karibuni alitangaza nia yake ya kugombea kiti cha urais katika uchaguzi ujao.
 


Share:

Korea Kaskazini yasema majaribio ya makombora ni onyo kwa Marekani

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amesema majaribio ya makombora yaliyofanywa na nchi yake hapo jana, yalikuwa onyo kwa Korea Kusini na mshirika wake Marekani. 

Shirika la Habari la Korea Kaskazini KCNA limemnukuu Kim akisema kuwa onyo hilo ni jibu kwa mazoezi ya pamoja ya kijeshi yanayofanywa na vikosi vya Marekani na Korea Kusini. 

Awali, wizara ya mambo ya nje ya Korea Kaskazini ilisema kuwasili kwa nyambizi ya Marekani yenye silaha za nyuklia katika bandari ya Korea Kusini, ni sababu tosha ya nchi hiyo kuimarisha mpango wake wa silaha, na kuongeza kuwa sababu zinazotolewa na Marekani pamoja na Korea Kusini kutetea mazoezi yao ya pamoja, haziondoi azma yao ya uchokozi. 

Mapema jana Korea Kaskazini iliyarusha makombora mawili ya masafa ya kati kutoka mkoa wa Kusini wa Hwanghae, na makombora hayo yalisafiri umbali wa km 450 kabla ya kutua Baharini. 

Chini ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa, nchi hiyo hairuhusiwi kuyafanya majaribio hayo.


Share:

WANAKIJIJI ZAIDI YA 200 WAUA MIFUGO NA KUICHOMA MOTO KAGERA



Katika hali isiyo ya kawaida na ya kuogofya, takribani wanakijiji zaidi ya 200 wa kijiji cha Kishanda B Wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera, wamevamia shamba la mwananchi mwenzao kisha kuikatakata migomba yote, kuchinja mifugo huku mbuzi wengine wakiwaua kwa kuwachoma na moto.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Ahmed Msengi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza vitu vilivyoharibiwa ni pamoja na mashamba ya migomba, kahawa na miti pamoja na kuwaua mbuzi wanne na kuwajeruhi mbuzi wawili, huku chanzo cha mgogoro huo ni umiliki ardhi kubwa, mgogoro ambao tayari ulishafika mahakamani.

Tukio hilo lilifanywa wakati mwenye shamba na mifugo iliyoharibiwa, Tryphone Jeremiah akiwa katika ibada kanisani na kudai kwamba wananchi hao takribani 200, walivamia mashamba na mifugo hiyo saa 6:00 mchana, baada ya kuwepo mgogoro wa ardhi baina ya baba yake na wanakijiji hao tangu mwaka 2007.

"Wananchi wanalalamika kuwa ninamiliki ardhi kubwa, baada ya wanakijiji hao kuvamia mashamba kwa makundi makundi, waliyafyeka kwa muda fupi na kuua mbuzi na kuwachoma moto pamoja na kubomoa nyumba," alidai Jeremiah.

Inaelezwa kuwa wananchi hao walitumia takribani masaa matatu kutekeleza unyama huo na kwa mujibu wa mlalamikaji (Jeremiah), anasema alikuwa na mbuzi 100, hivyo kati ya wale waliochinjwa na waliobaki hai wanaonekana 39 na mbuzi 57 hawaonekani kabisa.
Chanzo - EATV
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger