Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya simu ya Safaricom, Bob Collymore amefariki dunia. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Safaricom, matuti yamekuta Collymore asubuhi ya leo Jumatatu Juni 1, 2019 akiwa nyumbani kwake jijini Nairobi.
Vyombo vvya habari vya Kenya vimesema mwenyekiti wa kampuni hiyo Nicholas Ng'ang'a amesema afya ya Collymore ilikuwa mbaya kwa majuma ya hivi karibuni.
Collymore, alichukua likizo ya matibabu ya miezi tisa mwishoni mwa mwaka 2017 na kwenda Uingereza kwa ajili ya matibabu ya saratani na alirejea Kenya Juni mwaka jana.
Collymore alianza kuongoza Safaricom mwaka 2010 kutoka kwa Michael Joseph ambaye kwa sasa ni mmoja wa wajumbe wa bodi ya kampuni hiyo.
Mwaka 2017 wanahisa walipiga kura kuongeza mkataba wa Bob Collymore kwa miaka miwili baada ya mkataba wake kuisha. Mkataba aliokuwa akiufanyia kazi ulikuwa unatarajiwa kufikia tamati mwaka 2020 na kumfanya kuwa Mkurugenzi aliyekalia kiti hicho kwa muda mrefu zaidi.
Viongozi kadhaa wakiwemo Rais Uhuru Kenyatta wametuma salamu za rambirambi kwa familia kutokana na kifo hicho.