Saturday, 8 June 2019

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi June 8




Share:

Friday, 7 June 2019

Picha : MBUNGE AZZA HILAL ACHANGIA MIL. 4.8 KWA AJILI YA UPAUAJI WA JENGO LA AKINA MAMA ZAHANATI YA ZUNZULI

Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) amechangia shilingi 5,895,000/= kwa ajili ya upauaji wa jengo la wodi ya akina mama katika zahanati ya kijiji cha Zunzuli kata ya Mwenge halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo Ijumaa Juni 7,2019 katika kijiji cha Zunzuli,kilichohudhuriwa pia na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe.Jasinta Mboneko,mbunge huyo alisema fedha hizo zitatumika kununua mbao na mabati kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya akina mama.

“Baada ya kuona zahanati hii ya Zunzuli haina wodi ya akina mama,nilichokifanya ni kutafuta fedha kwa ajili ya upauaji,namshukuru Mungu wadau wangu wamenishika mkono,nimepata kiasi cha shilingi milioni 4.8 kwa ajili ya kununua mbao na mabati ili wodi hii ya wazazi ambayo wananchi wameijenga hadi kwenye renta ili iweze kupauliwa”,alisema Azza.

“Zahanati hii ya Zunzuli iliyojengwa mwaka 1994 ina chumba kidogo tu chenye vitanda viwili, akina mama wanapokuwa wengi huduma inakuwa tatizo,takwimu zinaonesha zahanati hii inapokea akina mama wanaojifungua kati ya 20 hadi 25 kwa mwezi ndiyo maana nikaona umuhimu wa kuwatafutia fedha za upauaji ili akina mama waweze kupata huduma wanayostahili”,aliongeza mbunge Azza.

Alisema jukumu lake kubwa kama mbunge wa viti maalum na mbunge mwanamke ni kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa na hiyoni kuunga mkono kwa vitendo jitihada zinazofanywa na Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli katika kuboresha sekta ya afya.

Kwa upande wake,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko aliwataka wananchi kutumia fedha zilizotolewa na mbunge kwa malengo yaliyokusudiwa na kuwakumbusha kuwa mstari wa mbele kuchangia shughuli za maendeleo badala ya kusubiri serikali pekee iwaletee maendeleo.

Mboneko pia aliwahamasisha wanawake kuhudhuria kliniki na kujifungulia kwenye vituo vya afya huku akiwasisitiza akina baba kutunza na kukaa vizuri na wake zao badala ya kuwanyanyasa na kupeleka watoto shule badala ya kuwaozesha.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI


Wa pili kulia ni diwani wa kata ya Mwenge Edward Maganga akimwongoza Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (wa pili kushoto) na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe.Jasinta Mboneko (katikati) walipowasili katika zahanati ya Zunzuli leo Juni 7,2019 . Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Muonekano wa jengo la wodi ya akina mama katika zahanati ya Zunzuli kata ya Mwenge ambapo limefikia kwenye renta na tayari Mbunge amepata fedha kwa ajili ya upauaji.
Mganga mfawidhi Zahanati ya Zunzuli Dkt. Manumi Julius akionesha jengo la zahanati ya Zunzuli.
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Zunzuli na kuwaambia amepata fedha kwa ajili ya upauaji wa jengo la zahanati ya akina mama zinawekwa kwenye akaunti ya kijiji.
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Zunzuli.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Zunzuli.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe.Jasinta Mboneko akizungumza katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Zunzuli na kuwahamasisha wananchi kuendelea kujitokeza kushiriki katika shughuli za maendeleo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza na wananchi wa kijiji cha Zunzuli.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Mhe. Hoja Mahiba akizungumza kwenye mkutano huo.
Afisa Mtendaji wa kata ya Mwenge,Gabaruda Gidawadini Gidaweda akizungumza katika mkutano huo.
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM),Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko  na Diwani wa kata ya Mwenge, Mhe. Edward Maganga wakifurahia jambo kwenye mkutano wa hadhara kijiji cha Zunzuli.
Viongozi mbalimbali wa CCM wakiwa kwenye mkutano huo.
Diwani wa kata ya Mwenge, Mhe. Edward Maganga akizungumza katika mkutano huo.



Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akifurahia jambo wakati akiagana na wakazi wa kijiji cha Zunzuli kata ya Mwenge halmashauri ya wilaya ya Shinyanga baada ya kufanya mkutano wa hadhara.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Share:

Picha : MBUNGE AZZA HILAL ATOA MSAADA WA KOMPYUTA SHULE YA SEKONDARI SOLWA

Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) ametoa msaada wa Kompyuta nne zenye thamani ya shilingi milioni 8 katika shule ya Sekondari Solwa iliyopo katika jimbo la Solwa mkoani Shinyanga ili waitumie katika masomo yao kuendana na ulimwengu wa teknolojia.

Kompyuta hizo ni sehemu ya Kompyuta 15 zenye thamani ya shilingi milioni 30 zilizopatikana kutokana na juhudi za Mbunge Azza Hilal Hamad kwa kushirikiana na wadau ambao ni Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) shule mbalimbali mkoani Shinyanga.

Akikabidhi Kompyuta hizo kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe, Jasinta Mboneko leo Juni 7,2019 katika shule ya sekondari Solwa,Mhe. Azza amesema kupitia kompyuta hizo wanafunzi watajifunza teknolojia ya kisasa.

“Nimeleta kompyuta hizi 8 kwenye shule ya Solwa yenye jumla ya wanafunzi 708 kwa sababu nataka na nyinyi mtoe tongotongo za kompyuta. Nimeona ni vizuri angalau tukaangalia shule zilizopo pembezoni walau wanafunzi wakapata uelewa wa kompyuta angalau kwa uchache wa hizi nilizopata”,alisema Azza.

“Kilichonisukuma ni kuona shule zetu nyingi za vijijini mwanafunzi hadi anamaliza kidato cha nne hata sura ya Computer haijui, kwa hiyo inakuwa changamoto kubwa pale anatoka na kuendelea na masomo ya kidato cha tano au chuo kinaonekana ni kitu kigeni kabisa kwake”,aliongeza.

Mhe. Azza aliushukuru Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kushirikiana naye kuhakikisha angalau shule za sekondari zinapata kompyuta ili watoto waweze kujifunza teknolojia ya kisasa.

“Nawashukuru sana UCSAF kwa kunipatia kompyuta, nitaendelea kuwasumbua naomba msinichoke kwani shule nyingi Shinyanga hazina kompyuta. Niwaombe pia wadau wengine waweze kutusaidia katika mkoa wa Shinyanga ili kuondoa changamoto ya Kompyuta katika shule zetu”,alisema Azza.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe.Jasinta Mboneko alishukuru mbunge huyo kwa kufanikisha kupatikana kwa kompyuta hizo na kuwataka wanafunzi kutunza na kuzitumia vizuri katika kujifunzia masomo yao.

“Sasa hivi dunia imebadilika imekuwa ya Kidigitali zaidi,tumieni kompyuta kujifunza mambo mazuri,mnaweza kuzitumia pia kupata taarifa mbalimbali za nchi hii. Nanyi walimu hakikisheni mnawasimamia vizuri wanafunzi hawa”,alisema Mboneko.

Naye Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Mhe. Hoja Mahiba alisema shule ya sekondari Solwa imekuwa ya kwanza kwenye halmashauri hiyo kupata kompyuta kupitia mbunge Azza na kubainisha kuwa zitasaidia kuwaandaa wanafunzi katika maisha yao.
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (wa pili kulia) na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe.Jasinta Mboneko (wa tatu kushoto) wakipokelewa na viongozi mbalimbali wa kata ya Solwa wakati wakiwasili katika shule ya sekondari Solwa kwa ajili ya zoezi la makabidhiano ya Kompyuta leo Juni 7,2019.wa pili kushoto ni diwani wa kata ya Solwa Mhe. Awadhi Aboud.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza wakati wa kukabidhi kompyuta nne kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari Solwa leo.Kushoto  Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Mhe. Hoja Mahiba. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akizungumza katika shule ya sekondari Solwa wakati akipokea kompyuta zilizopatikana kwa juhudi za mbunge Azza Hilal.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Solwa wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko.
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akikabidhi moja ya kompyuta hizo aina ya Dell kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko (kulia).
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akishikana mkono na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko (kulia) wakati wa makabidhiano ya kompyuta hizo.
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) na  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko (kulia) wakifurahia wakati wa kukabidhiana Baobonya ya kompyuta.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Solwa wakiwa wamebeba moja ya kompyuta zilizotolewa na Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Solwa wakiwa wamekaa wakati wa makabidhiano ya kompyuta.
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad akiwasisitiza wanafunzi wa shule ya sekondari Solwa kuzingatia masomo yao na kuacha tamaa ya mapenzi ili waweze kutimiza ndoto zao.
Kaimu Afisa Elimu halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Jesse George akimshukuru Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad kwa kuwapatia kompyuta ambazo zitawasaidia wanafunzi katika masomo na maisha yao.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Mhe. Hoja Mahiba akizungumza wakati wa makabidhiano ya kompyuta huku akiwataka wanafunzi wa kike kutoa taarifa kwa walimu na viongozi mbalimbali pale wanaume wenye tamaa za mapenzi wanapowasumbua.
Mkuu wa shule ya sekondari Solwa akimshukuru Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad kwa kuwapatia msaada wa kompyuta.
Diwani wa kata ya Solwa Mhe. Awadhi Aboud akimshukuru Mbunge Azza Hilal kwa msaada wa kompyuta kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Solwa huku akielezea misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikitolewa na Mbunge huyo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi katika sekta ya elimu na afya.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akiwasisitiza wanafunzi wa shule ya sekondari Solwa kuepuka mimba na ndoa za utotoni.
Kushoto  Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Mhe. Hoja Mahiba akifuatiwa na Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko wakifurahia jambo wakati wa makabidhiano ya kompyuta kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari Solwa.
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad  akiagana na wanafunzi wa shule ya Sekondari Solwa baada ya kuwakabidhi kompyuta nne aina ya Dell ili wazitumie kujifunzia masomo yao.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Share:

Rais Magufuli: Natamani kuona mabilionea wengi nchini Tanzania

Rais Magufuli  amesema kuwa anatamani wakati atakapomaliza muda wake wa uongozi, Tanzania iwe na mabilionea zaidi ya 100.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo katika Ikulu ya Dar es Salaam wakati akizungumza kwenye mkutano kati yake na wafanyabiashara kutoka wilaya zote za Tanzania kwa lengo la kujadili changamoto zinazokwamisha sekta hiyo.

Magufuli amesema jambo hilo litamfanya afurahi kuona anamaliza muda wake huku akiacha mabilionea wengi nchini  kutokana na kile alichokuwa akikifanya katika kuboresha mazingira ya biashara. 

“Thubutuni na msiogope kufanya biashara ya aina yoyote, nchi yetu imebarikiwa kuwa na ardhi nzuri, rutuba, maji kwa ajili ya uvuvi, mifugo, madini fursa nyingi za uwekezaji zitumieni ili ziwanufaishe ili siku nikiwa naondoka angalau niache wafanyabiashara mabilionea zaidi ya 100, nitafurahi sana.” Amesema.

Rais Magufuli pia ameashiria changamoto za biashara katika mipaka ya nchi hiyo na amewataka wafanyabiashara hao kutumia fursa ya masoko ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).


Share:

Waziri Mkuu Uingereza May ajiuzulu rasmi wadhifa wake

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May ameachia uongozi wa chama tawala cha Conservative hii leo hatua inayofungua mlango wa kinyang'anyiro cha mrithi wa nafasi hiyo. 

May hatauhutubia umma lakini amewasilisha barua ya kuthibitisha kujiuzulu kwake kwa kamati ya chama chake yenye nguvu ijulikanayo kama "Kamati ya 1922".

 May ataendelea kuwa waziri mkuu hadi wabunge watakapomchagua kiongozi mpya wa chama hicho mchakato utakaouchukua hadi miezi miwili. 

Waziri wa zamani wa mambo ya nje Boris Johnson anapewa nafasi kubwa ya kushinda nafasi hiyo. 

Waziri Mkuu May alitangaza kujiuzulu nafasi hiyo Mei 24 baada ya kushindwa kufanikisha makubaliano ya Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya ama Brexit.


Share:

Serikali yakabidhi Mfumo wa Usimamizi wa Mashauri Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.

Na.Paschal Dotto-MAELEZO.
 Serikali Kupitia Wakala ya Mtandao (e GA) imekabidhi rasmi Mfumo wa Taarifa wa Usimamizi Mashauri, kwa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ili kuiwezesha Ofisi hiyo Kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi Mkubwa. 

Akizungumza ya Waandishi wa Habari katika makabidhiano kati ya Wakala ya Serikali ya Mtandao na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Mkurugenzi Wa Usimamizi wa Huduma za TEHAMA wa Wakala ya Serikali, Injinia, Benedict Ndomba, amesema kuwa Ofisi yake inatumia wataalam wake wa TEHAMA kutengeneza mifumo inayorahisisha kufanya kazi katika Taasisi mbalimbali nchini. 

Injinia Ndomba, alisema kuwa serikali ya Awamu ya Tano inalo kusudi kubwa la kutekeleza ahadi zake kama utoaji huduma nzuri kwa wananchi ikiwemo hiyo ya utengenezaji mifumo ya huduma kwa ajili ya kero za wananchi. 

“Serikali hii ya Awamu ya Tano, ina hazina kubwa ya wataalam wa TEHAMA, ambapo kielelezo kimojawapo ni kuwa mfumo huu umebuniwa, umesanifiwa na kutengenezwa na Watumishi wa Umma na tumekubaliana na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kuwa Mfumo huu utekelezwe kwa awamu mbili ili kuweza kukidhi mahitaji ya wadau wote”, Injinia Ndomba alisema. 

Katika awamu ya Kwanza ya Utengenezaji Mfumo huo, Ndomba alisema wametengeneza Moduli itakayoisaidia Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kutekeleza majukumu yao hasa ya ndani kwenye masuala ya Usimamizi Mashauri, ambapo pia itakuwa ni nyenzo muhimu wa utekelezaji majukumu kwa haraka. 

Naye, Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Clement Mashamba  ameipongeza Wakala ya Mtandao wa Serikali (e GA) kwa kutengeneza mfumo huo kwa mahitaji ya ofisi ya Wakili wa Serikali na kudai kuwa watakuwa wanatekeleza majukumu kwa haraka na kwa ufanisi zaidi katika kutatua kero za wananchi. 

“Ofisi yangu itaendelea kushirikiana na Wakala ya Serikali ya Mtandao ili kuhakikisha awamu zote za utengenezaji wa mfumo huu zinatekelezwa kwa wakati na kwa ubora unaostahili, lakini pia Ofisi yangu inatambua Mchango huu mkubwa kwa kazi zetu ya kisheria,” Dkt. Mashamba. 

Aidha Dkt. Mashamba alisema kuwa mfumo huo utakuwa ni muhimu katika kutatua kero za wananchi, hususani Usimamizi wa majalada ya Mashauri; Usajili wa Mashauri; Upangaji wa Mashauri yanayoshughulikiwa; Ufutiliaji wa Maendeleo ya Mashauri; Huduma zingine ni Usimamizi wa Ratiba ya Mashauri; Utoaji wa Taarifa; Uhakiki wa Mwenendo wa Mashauri na Uhamishaji wa Taarifa na Takwimu. 

Dkt. Mashamba alieleza kuwa mfumo huo una umuhimu mkubwa kwani unaweza kutumiwa na idara mbalimbali za Serikali na unapatikana mahali pamoja kwa hiyo ni mfumo ambao Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali itaweza kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa. 

Mwisho.


Share:

Rais Magufuli, Wafanyabiashara Wajadili Fursa na Changamoto za Biashara Nchini

Adelina JohnBosco, MAELEZO Dodoma
Rais John Pombe Magufuli amekutana na wawakilishi wa wafanyabiashara nchini leo Ikulu Jijini Dar es salaam ili kujadili changamoto zinazowakabili wafanyabiashara na jinsi ya kuzitatua kwa ajili ya kukuza uchumi kupitia sekta binafsi nchini.

Licha ya jitihada zinazoendelea kuleta uboreshaji katika sekta ya biashara, Rais ametaja uwepo wa changamoto mbalimbali kwa pande wa Serikali na wafanyabiashara wenyewe ambazo zimekuwa ni kikwazo katika kufanya biashara nchini.

Rais Magufuli amebainisha vikwazo vinavyosababishwa na wafanyabiashara kuwa ni pamoja na ukwepaji kodi unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara na vitendo vya rushwa kuwa ni miongoni mwa changamoto zinazozuia uboreshaji wa sekta ya biashara nchini.

Amesema kuna kampuni 17,446 zinakwepa kodi kwa njia ya mauzo hewa ya biashara za ndani na nje, manunuzi hewa kutoka makampuni hewa na kuagiza kampuni hizo kuchunguzwa zaidi na zikithibitika kukwepa kodi zitalazimika kulipa kodi hiyo katika kipindi cha siku 30 kuanzia sasa.

''Baadhi yenu sio waaminifu mnakwepa kodi, mnatoa rushwa na wengine mmekuwa mkifanya kazi za udalali hasa kwenye biashara ya sukari, mafuta ya kula na korosho'' ameeleza Rais Magufuli

Changamoto nyingine kutoka kwa wafanyabiashara ni kuhujumu uchumi kwa kutokuwa wawazi katika mahesabu yao kwa kuwasilisha vielelezo tofauti vya taarifa ya fedha zinazopelekwa benki na TRA.

Aidha, amewaonya wafanyabiashara wanaobadilisha matumizi ya viwanda yaliyokusudiwa awali wakati yakisajiliwa na kuanzisha biashara nyingine pasipo kufuata utaratibu.

Upande wa Serikali, Rais Magufuli amebainisha changamoto mbalimbali ambazo ni kikwazo kwa biashara nchini kuwa ni pamoja na wingi wa taasisi za udhibiti kama vile TRA, OSHA, TBS, TFDA, Ofisi ya Mkemia Mkuuu, Tume ya Ushindani, EWURA, na SUMATRA ambazo husababisha mwingiliano kimajukumu na kutoza tozo mbalimbali zinazofanana hivyo kudhoofisha ukuaji wa biashara nchini.

Ametaja vitendo vya rushwa kwa baadhi ya watumishi wachache  wa Serikali wasio waadilifu kuwa ni miongoni mwa changamoto inayorudisha nyuma jitihada za wafanyabiashara hasa maeneo ya vizuizi barabarani, bandarini, na TRA.

Katika kuhakikisha changamoto hizi zinatatuliwa, Rais amebainisha mikakati ya Serikali iliyoweka ikiwa ni pamoja na kuandaa kitabu cha mwomgozo na kwamba mapendekezo mbalimbali yameanza kutekelezwa kwa lengo la kuboresha mazingira ya biasha nchini.

''Sasa Brela inatumia utaratibu mpya wa kusajili biashara kwa njia ya mtandao, kufuta baadhi ya ada na tozo zilizokuwa zikitozwa na taasisi za OSHA na Zima moto kabla ya kuanzisha biashara,'' amesisitiza Rais Magufuli.

Aidha amezitaka mamlaka husika katika Serikali kuweka mikakati thabiti ya kuwaendeleza wafanyabiashara wadogo na wakati kama ilivyofanyika kwa wafanyabiashara wakubwa.

''Wafanyabiashara wadogo na wakati ndiyo kitovu cha kukuza uchumi katika nchi, hivyo nashauri waendelezwe kama ambavyo tumeshaanza kwa kutoa vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo nchini'', alisisitiza Rsi Magufuli.

Kwa upande mwingine, Rais amezionya taasisi za kifedha kutokana na kuwa na mitaji midogo huku zikiweka masharti magumu na kutoza riba kubwa ikiwemo kuendesha shughuli zake zaidi mijini kuliko vijijini.

''Serikali kupitia Benki Kuu imekuwa ikikopa fedha nyingi kwenye taasisi za kimataifa ikiwemo benki ya dunia kwa ajili ya kutoa dhamana na kuwakopesha wajasiriamali wa hapa nchini, lakini sina hakika kama fedha hizo zinawafikia walengwa,'' amehoji Rais Magufuli.

Rais amewaonya mawakala wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) nje ya nchi wanaowasababishia hasara wafanyabiashara kwa kuidhinisha bidhaa ambazo zinagundulika kuwa hazina viwango zinapokaguliwa baada ya kuingizwa nchini.

Aidha ameziagiza mamlaka husika kuangalia uwezekeno wa kuunganisha baadhi ya mifuko inayosimamia sekta ya biashara ili kuiimarisha na kupunguza gharama za uendeshaji huku akizitaka mamlaka zinazosimamia sekta ya biashara ikiwemo wizara, idara, wakala wa Serikali kuhakikisha changamoto hizo zinafanyiwa kazi mara moja ifikapo mwezi Julai mwaka huu, kwa kuzingatia mapendekezo yote yaliyomo katika kitabu cha mwongozo (Blue Print).

Hata hivyo, rais ametoa pongezi kwa wafanyabiashara halali wanaofuata taratibu elekezi ikiwemo kulipa kodi kwa wakati.

Mkutano huu ni mwendelezo wa mikutano inayofanywa na Rais kwa kuyahusisha makundi mbalimbali ikiwemo viongozi wa dini, wachimbaji wa madini, wazee na watendaji Serikalini lengo likiwa ni kujadiliana na kuweka mikakati itakayosaidia kukua kwa uchumi kwa maslahi ya Taifa.

-Mwisho-


Share:

Rais Magufuli Aonesha Kutoridhishwa na Utendaji Kazi TPSF

Rais Magufuli amesema licha ya taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPSF) kuwa ya muda mrefu hana uhakika kama inawasaidia wafanyabiashara.

Kiongozi mkuu huyo wa nchi ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Juni 7, 2019 katika mkutano wake na wafanyabiashara kutoka Wilaya zote nchini uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam.

Magufuli amesema kuna ujio wa wafanyabiashara kutoka nje ya nchi lakini hajaona matokeo ya ujio wao tangu waanze kutembelea nchini.

Amesema baadhi ya wafanyabishara wanasema TPSF ni jukwaa la kuwakandamiza  na kuwatengeneza kundi la watu wanaojitiita wawakilishi wakati sivyo.


Share:

Waziri Mkuu wa Ethiopia aelekea Sudan kupatanisha jeshi na raia

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed leo anatazamiwa kuitembelea Sudan kwa lengo la kujaribu kuwapatanisha watawala wa kijeshi na makundi ya raia kufuatia kuendelea mgoggoro nchini humo baada ya Omar al Bashir kuondolewa madarakani.

Taarifa zinasema Abiy Ahmed atatembelea Khartoum na kukutana na wakuu wa baraza la mpito la kijeshi na muungano wa kiraia wa upinzani unaojulikana kama Alliance for Freedom and Change. 

Taarifa zinasema Waziri Mkuu wa Ethiopia analenga kutatua mgogoro wa kisiasa nchini Sudan katika mkutano wake na pande hasimu.  

Dkt. Abiy anatembelea Sudan baada ya uanachama wa nchi hiyo katika Umoja wa Afrika kusimaishwa hadi pale wanajeshi watakapowakabidhi raia madaraka.

Mgogoro wa nchi hiyo uliibuka Disemba mwaka jana baada ya wananchi kumiminika mabarabarani wakilalamikia hali mbaya ya kiuchumi ambapo kufuatia maandamano hayo, tarehe 11 Aprili mwaka huu jeshi la Sudan lilitangaza kumuondoa madarakani Rais Omar al-Bashir na kutwaa madaraka ya nchi hiyo. 

Baada ya hapo jeshi hilo liliunda Baraza la Kijeshi la Mpito ingawa wananchi wanalipinga na kulitaka liruhusu kuundwa serikali ya kiraia.




Share:

Video Mpya: Nuh Mziwanda Ft. Dully Sykes - Machete

Video Mpya: Nuh Mziwanda Ft. Dully Sykes - Machete


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger