Friday, 3 May 2019

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa May 3




Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA MEI 3,2019.......HABARI KUBWA 'KIFO CHA DR MENGI'


Magazetini leo Ijumaa May 3,2019




Magazeti mengi zaidi yatakuja baadae...Endelea kutembelea Malunde1 blog
Share:

Thursday, 2 May 2019

MFALME AMUOA MLINZI WAKE...AMTAWAZA KUWA MALKIA

Mfalme anaonekana akimwaga maji ya baraka kwenye kichwa cha Malkia Suthida.

Mfalme wa Thailand amemuoa Naibu mkuu wa kikosi cha walinzi wake , na kumpa cheo cha malkia, imesema taarifa ya ufalme huo.


Tangazo hilo la kushitukiza limetolewa huku sherehe za kutawazwa kwake zikitarajiwa kuanza Jumamosi, wakati atakapochukua wadhfa wake.

Mfalme Maha Vajiralongkorn, mwenye umri wa miaka 66, alikuwa mfalme kikatiba baada ya kifo cha baba yake aliyependwa sana kilichotokea mwaka 2016.

Amekwisha wataliki wanawake mara tatu na ana watoto saba.

Ufalme ulisema kuwa: Mfalme Vajiralongkorn "ameamua kumpandisha cheo Generali Suthida Vajiralongkorn Na Ayudhya, na kuwa Malkia Suthida na atakuwa na cheo cha kifalme na hadhi kama sehemu ya familia ya kifalme".

Malkia Suthida ni mpenzi wa muda mrefu wa Mfalme Vajiralongkorn na amekuwa akionekana hadharani pamoja nae kw amiaka mingi, ingawa mahusiano yao haukuwahi kukubalika rasmi.Malkia Suthida alipewa cheo cha Generali mwaka 2016

Picha kutoka kutoka katika sherehe za harusi zilionyeshwa moja kwa moja kwenye vituo vya televisheni vya Thailand Jumatano, ambapo watu wa wengine wa familia ya ufalme na washauri wa ufalme walihudhuria.

Mfalme alionekana akimwagia maji ya baraka Malkia Queen Suthida kichwani. Baadae wawiloi hao walisaini cheti cha ndoa.

Mnamo mwaka 2014 Vajiralongkorn alimteua Suthida Tidjai, ambaye ni mhudumu wa zamani wa Thai Airways,kama naibu kamanda wa kikosi cha walinzi wake. Alimpandisha cheo na kuwa Generali kamili jeshini Disemba 2016.

Mfalme aliyetangulia Bhumibol Adulyadej, alitawala kwa miaka 70 na kuwa ndiye mfalme aliyetawala kwa muda mrefu zaidi duniani na alifariki dunia mwaka 2016.
Chanzo - BBC
Share:

Angalia Picha : TAMASHA LA KUABUDU NYOKA

Share:

SERIKALI YAFUNGA VITUO 13 VYA RADIO NA TV KWA UCHOCHEZI ...WAANDISHI WA HABARI 30 MATATANI


 
Tume ya Mawasiliano nchini Uganda imeagiza kufungwa kwa vituo 13 vya radio na televisheni pamoja na kufutwa kazi baadhi ya waandishi wa habari kwa ''kupotoshaji na kuchochea ghasia kwa kutangaza taarifa zenye ujumbe na hisia kali.

Hatua hiyo imechukuliwa saa chache baada ya mwanasiasa machachari wa upinzani na Mbunge wa Kyadondo Mashariki, Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine kukamatwa na kushtakiwa mahakamani.

Kuna madai kuwa huenda hatua hiyo imetokana na mtangazo ya moja kwa moja ya kukamatwa na kushtakiwa kwa Bobi Wine.

Kyagulanyi kwa sasa anazuiwa rumande na alitarajiwa kufikishwa tena mbele ya hakimu mkuu wa Mahakama ya Buganda Road leo Alhamisi.

Tume hiyo imesema vyombo hivyo vya habari vimekiuka kanuni ya kifungu cha 31 ibara ya 4 ya sheria ya mawasiliano ya Uganda ya mwaka 2013.

Hata hivyo, haikufafanua jinsi sheria hiyo ilivyokiukwa katika agizo lake kwa vyombo hivyo vya habari ambavyo ni vituo vya televisheni vya NBS, Bukedde TV, NTV, CBS FM na Capital FM.

Tume hiyo inataka hatua dhidi ya wazalishaji vipindi, wahariri wakuu na wasimamizi wa matangazo kusimamishwa kazi katika muda wa siku tatu.

"Hii ni kufuatia jinsi wanavyoshughulikia mada zinazorushwa hewani wakati wa matangazo ya moja kwa moja, habari za hivi punde na habari nyingine kwa ujumla bila kuzingatia kanuni," imesema UCC.

Ilivyopokelewa

Chama cha wanahabari nchini Uganda (UJA) kimeelezea kughadhabishwa na hatua hiyo.

''Wanahabari karibu 30 wanakabiliwa na tishio la kufutwa kazi na hili litakuwa na athari hasi si kwa taaluma zao tu, bali mamilioni ya Waganda watakosa huduma ya kupashwa habari,'' imesema taarifa ya chama hicho.

UJA imesema Serikali kupitia mashirika yake ya udhibiti wa mawasiliano inatakiwa kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari.

Baadhi ya watu pia wameileza BBC kuwa hatua hiyo inaleta taswira mbaya kwa Uganda wakati ulimwengu unapoadhimisha siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari duniani.

Tume hiyo imedai kuwa iliwahi kutoa onyo kuhusiana na suala hilo lakini baadhi ya vyombo vya habari havikutilia maanani onyo hilo.

Mamlaka nchini Uganda imekuwa ikijaribu kuzima umaarufu wa mwanamuziki na mbunge huyo kwa kuvilazimisha vyombo vya habari kutomtangaza.

Umaarufu wa Bobi Wine umemfanya kuonekana tishio kwa utawala wa Rais Yoweri Museveni ambaye huenda akagombea tena urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2021 ikiwa ni miaka 35 tangu aingie madarakani.

Share:

KC,UZALENDO KWANZA KUWAMILIKISHA WASANII ARDHI


Mwenyekiti wa kundi la Uzalendo Kwanza na Mugizaji wa Filamu Nchini, Steve Nyerere akiongea na Waandishi wa Habari juu ya Makubaliano ya Wasaniii wa kampeni ya uzalendo kwanza na kampuni ya KC Land Development Plan Ltd Juu ya Mpango wao wa kukopeshwa Viwanja kwa gharama nafuu pasipokuwa na riba. Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya KC Land Development Plan Ltd,Khalid Mwinyi akitoa maelezo juu ya mradi na Viwanja vitakavyojulikana kama mji wa Wasanii. Msaniii wa na Meneja wa Bendi ya Twanga Pepeta, Luiza Mbutu akieleza ni namna gani bendi yake itakavyotumbuzi siku ya chakula cha pamoja baina ya Wasanii na Kampuni ya KC Land Development Plan Ltd. Msanii mkongwe wa Filamu nchini Chick Mchoma akieleza faida za wasanii watakaochukua Viwanja vya Kampuni ya KC Land Development Plan Ltd ambavyo vinalipwa ndani ya miaka miwili kwa gharama nafuu. Msanii mMahaurufu wa mvchezo wa Bongo Dar es Salaam, Kuwa Kikumba maharufu kama Dude akieleza nini kama wasanii watakwenda kufanya kuhakikisha kuwa wanamiliki viwanja hivyo.  Promota wa Mchezo wa Ngumi ambaye ni Mwanachama wa kundi la Uzalendo kwanza akieleza faida za Viwanja hivyo kwa mabondia ambao wamekuwa wakipata pesa na kufanya anasa pasipo kumiliki ardhi. Msanii wa kike wa Siku nyingi Maya akieleza namana wasanii wakike watakavyokwenda kumiliki nyumba zao na kuacha kunyanyasika. Wasanii kwa pamoja wakiwa wamesimama kama ishara ya kumkumbuka Mzee Reginald Mengi aliyetutoka usiku wa kuamkia leo.Sehemu ya Waandishi wa habari walioshiriki mkutano huo wakitimiza majukumu yao kama wanavyoonekana pichani.
Share:

MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI 2019 YAANZA DODOMA


Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2019 yameanza hii leo jijini Dodoma ambapo yanafanyika kitaifa kwa awamu ya pili mwaka huu. Kilele cha maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka Mei 03 ambapo wadau wa habari hukutana pamoja kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uhuru wa vyombo vya habari/ wanahabari katika gurudumu la maendeleo.Picha na KD Mula, Funguka Live Blog
Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akiwasilisha mada kwa niaba ya makundi ya washiriki kwenye maadhimisho hayo.
Lilian Kallaghe kutoka taasisi ya SIKIKA akiwasilisha mrejesho wa majadiliano kwa niaba ya washiriki wengine. 
Mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya elimu (UNESCO) nchini Tanzania, Nancy Kaizirege akitoa salamu za shirika hilo kwenye ufunguzi wa maadhimisho hayo.
Washiriki wa maadhimisho hayo walisimama kwa muda kama ishara ya kumuombea aliyekuwa Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) na pia mmiliki wa makampuni ya IPP, Mzee Reginald Mengi aliyefariki usiku wa kuamkia leo akiwa nchini Dubai akiwa na miaka 75.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa (katikati) akimsikiliza kwa umakini Mweka Hazina wa taasisi hiyo, Michael Gwimile kwenye maadhimisho hayo (kulia).
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Salome Kitomari wakifuatilia mada kwenye maadhimisho hayo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada kwenye maadhimisho hayo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania.
Baadhi ya washiriki wa maadhimisho hayo akiwemo Mkurugenzi wa kampuni ya Uhuru Media Group, Ernest Sungura wakifurahia jambo kwenye maadhimisho hayo.
Wahadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam wakifuatilia kwa umakini uwasilishaji mada kwenye maadhimisho hayo.
Washiriki wa maadhimisho hayo akiwemo Joyce Shebe kutoka Clouds Media Group (kushhoto) wakifuatilia mada kwa umakini.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2019 yameanza hii leo jijini Dodoma, yakilenga kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uhuru wa vyombo vya habari na wanahabari.

Msisitizo mkubwa umetolewa kwa wadau wa habari kujadili viashiria vya kushuka kwa uhuru vya habari nchini Tanzania na namna ya kuviepuka hususani baadhi ya waandishi wa habari kupotea, kukamatwa na kushikiliwa kwa muda na mamlaka nchini.

Aidha wanahabari pamoja na wahariri wamepewa changamoto ya kuhosi sababu za Tanzania kushuka kwa nafasi 25 kutoka nafasi ya 93 mwaka jana hadi nafasi ya 118 mwaka huu kwenye orodha ya uhuru wa vyombo vya habari duniani.

“Tunapaswa kuhoji kwa nini tumeshuka kwenye nafasi ya uhuru wa vyombo vya habari duniani, mwaka jana tulishuka kwa nafasi 10 kutoka nafasi ya 73 hadi nafasi ya 93 na mwaka huu tumeshuka kutoka nafasi ya 93 hadi nafasi ya 118”, wamehoji washiriki kwenye maadhimisho hayo.

Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa amesisitiza waandishi wa Habari Tanzania kuongeza kiwango chao cha elimu ili kuendana na matakwa ya sheria hatua itakayosaidia kufanya shughuli zao kwa mujibu wa taaluma bila vikwazo kutoka kwa mamlaka za kisheria.

Mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya elimu (UNESCO) nchini Tanzania, Nancy Kaizirege amesema waandishi wa habari wanapaswa kushikamana pamoja ili kulinda usalama wao.

“Waandishi 99 waliuawa mwaka jana wakiwa kazini na tangu mwaka 1994 hadi 2018 jumla ya waandishi 1,377 wameuawa kutokana na majukumu hayo”, amebainisha Kaizirege akieleza jinsi usalama wa waandishi wa habari ulivyo mashakani.

Taasisi mbalimbali zimeshiriki kwenye maandalizi ya maadhimisho hayo ikiwemo MISA Tanzania, Internews, IMS, UTPC, TMF, TEF, UK Aid, TAMWA, MCT, UN Tanzania, FES, Unesco na Serikali ya Tanzania, kauli mbiu ikiwa ni “Vyombo vya Habari kwa Demokrasia, Tasnia ya Habari na Uchaguzi nyakati za upotoshwaji wa taarifa” ambapo kilele cha maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka Mei 03.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger