Thursday, 2 May 2019
BREAKING: Mwenyekiti wa makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi amefaiki dunia
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP , Dkt Reginald Abraham Mengi (75) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Dk Mengi amefariki dunia akiwa jijini Dubai, Falme za Kiarabu (UAE).
Dk Mengi alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa barani Afrika, ambapo sehemu ya utajir wake aliuelekeza kwa jamii kwa kutoa misaada mbalimbali.
Kwa mujibu wa jarida la Forbes mwaka 2014, utajiri wa bilione huyo ulitajwa kuwa ni TZS trilioni 1.3 ($560 milioni).
Enzi za uwahi wake na katika shughuli zake aliweza kushinda tuzo mbalimbali za kitaifa na kimataifa, pamoa na kuandika kitabu chake cha I Can, I Must, I will.

Mungu Ailaze Roho yake Mahali Pema Peponi. Amina
Wednesday, 1 May 2019
Rais Magufuli Atoa Maagizo Bodi za Mishahara nchini
Rais Magufuli amesema haelewi sababu za bodi za mishahara nchini Tanzania kutokutana kwa maelezo kwani yeye hana tatizo na kuonya vikao vyao kutokuwa uchochoro wa kutumia fedha za Serikali vibaya.
Ameyasema hayo leo katika sikukuu ya wafanyakazi Mei mosi, maadhimisho hayo kwa Tanzania yamefanyika katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
“Kwangu mimi hata wakitaka kukutana leo sina shida, sina tatizo namuagiza waziri mwenye dhamana kuhakikisha bodi hizo zinakutana lakini vikao vyao visiwe vichochoro vya kutumia fedha za Serikali vibaya,” amesema Rais Magufuli na kuongeza:
“Lazima nitoe angalizo hilo maana unaweza kusikia wameenda kufanya vikao Dubai lakini suala la kukutana na kujadili masuala mbalimbali kati ya wafanyakazi na yale yanayopaswa kutatuliwa mapema nasema kwa dhati sina tatizo mkutane.”

MWANAFUNZI AJINYONGA JIKONI BAADA YA KUIBA BEGI
Mwanafunzi Magreth Kayuni (15) wa kidato cha kwanza katika shule ya Sekondari Vwawa iliyopo wilayani Mbozi mkoani wa Songwe, amekutwa amejinyonga jikoni leo asubuhi kufuatia adhabu ya kupigwa na bibi yake baada ya kuiba begi la mwanafunzi mwenzake.
Shuhuda wa tukio hilo ambaye ni mdogo wa marehemu, Abraham Kalinga, amesema mapema leo asubuhi walipoamka bibi yao alimuagiza apike maharage, huku yeye akifanya kazi ya kufagia uwanja, marehemu Magreth Kayuni baada ya kupika maharage aliaga kuwa anaenda kuchota maji na ndipo alipofikia uamuzi wa kujinyonga.
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa, Seleman Mgala amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema limewastua wakazi wa eneo hilo ambapo amesema tukio kama hilo halijawahi kutokea mtaani hapo na hiyo ni mara ya kwanza.
Picha : DIWANI ZUHURA WAZIRI AENDESHA BONANZA LA MICHEZO IBADAKULI
Diwani wa viti maalumu Manispaa ya Shinyanga Zuhura Waziri anayetoka tarafa ya Ibadakuli ameendesha Bonanza la michezo kwenye Kata ya Ibadakuli mjini Shinyanga ili kuibua vipaji vya vijana kimchezo, pamoja kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Bonanza hilo la michezo limefanyika leo Mei Mosi 2019 kwenye viwanja vya michezo vya Bugweto, kwa kucheza mpira wa miguu, kukimbiza kuku, kuvuta kamba, kucheza drafti pamoja na mbio za baiskeli, ambapo washindi walipewa zawadi zao.
Akizungumza kwenye Bonanza hilo Diwani huyo wa Viti maalumu Zuhura Waziri, amesema lengo na madhumuni ni kuinua vipaji vya vijana, kuimarisha umoja, kudumisha amani, pamoja kumuunga mkono Rais John Magufuli ambaye amekuwa mfano wa kuigwa kusaidia kuinua michezo hapa nchini.
“Bonanza hili limeshirikisha timu nne za mpira wa miguu kutoka Uzogole, Mwagala, Ibadakuli, pamoja na Bugweto , wananchi wameshiriki kwenye michezo mbalimbali ikiwamo kukimbiza kuku, kuvuta kamba, kucheza drafti na mbio za baiskeli, ili kuwauganisha kuwa kitu kimoja na kuinua vipaji vya vijana,”amesema Waziri.
“Mbali na bonanza hili pia natarajia kuunda timu ya kata ya Ibadakuli ambayo itakuwa ikishiriki kucheza ngazi ya wilaya, ili kuendelea kuinua vipaji vya vijana kwenye kata hii, ambapo watakuja kuchezea kwenye Timu kubwa na hatimaye kupunguza tatizo la ajira, ikiwamo timu ya hapa nyumbani Stand United,” ameongeza.
Naye Mgeni rasmi Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Hafeez Mukadamu, amempongeza diwani huyo wa viti maalumu kwa kuanzisha bonanza hilo, ikiwa michezo kwa sasa inatoa ajira nyingi kwa vijana na kutoa wito kwa wanamichezo hao wajitume kwenye michezo hiyo, ili baadae wakacheze kwenye timu kubwa.
Pia amewatahadharisha vijana kuwa makini kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa, wasikubali kurubuniwa na baadhi ya vyama na kuvuruga amani ya nchi, bali wawe makini pamoja na kuchagua viongozi ambao watawaongoza vyema na kuwaletea maendeleo kama inavyofanya Serikali ya CCM Chini ya Rais John Magufuli.
Kwa upande wao vijana walioshiriki michezo hiyo akiwamo Makoja Seni , wamemshukuru diwani huyo kwa kufanya Bonanza hilo la michezo ambalo limewapa moyo wa kufanya mazoezi ili kuendeleza vipaji vyao, ambavyo hapo baadae vitakuja kuwapatia ajira na kuinuka kiuchumi.
Aidha katika Bonanza hilo,Makoja Seni aliibuka mshindi wa mbio za baiskeli, kukimbiza kuku kwa upande wa wanawake Halima Husein, huku wazee akiibuka Loyce Jiledya, Draft Samweli Kashinje, kuvuta kamba ukipata ushindi mtaa wa Mwagala kwa wanaume, wanawake mtaa wa Bugweto “A”.
Upande wa mpira wa miguu timu ya Bugweto ndiyo wameibuka washindi ambapo wamepewa seti moja ya jezi pamoja na Mpira, wakifautiwa na Timu ya pili ambayo ni Ibadakuli ambao walipata seti moja ya jezi, huku mshindi watatu akiwa ni Mwagala akifuatiwa na Uzogole ambapo wote walipewa mpira mmoja mmoja.
TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI
Diwani wa Viti maalumu manispaa ya Shinyanga Zuhura Waziri akizungumza kwenye Bonanza la Michezo Kata ya Ibadakuli lililofanyika kwenye eneo la Bugweto na kuelezea madhumuni kuwa ni kuinua vipaji wa vijana pamoja na kutekelezea ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Abuu Hafeez Mukadamu akiwaasa vijana kujituma kwenye michezo yao ili ipate kuwasaidia kupata ajira na kuwainua kiuchumi.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini (UVCCM) Dotto Joshua, akiwataka vijana kupenda michezo ambayo pia itawasaidia kupata afya njema, kupendana pamoja na kudumisha amani ya nchi.
Diwani wa Kata ya Ibadakuli Msabila Malale akizungumza kwenye Bonanza hilo na kuwataka vijana kudumisha nidhamu kwenye michezo yao na kumpongeza diwani huyo wa viti maalumu Zuhura Waziri kwa kufanya Bonanza hilo ambalo ni muhimu kwa vijana.
Vijana wakisikiliza nasaha kutoka kwa viongozi mbalimbali kwenye Bonanza hilo la Michezo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Hafeez Mukadamu, akifungua Bonanza hilo la Michezo kwenye viwanja vya michezo Bugweto.
Bonanza likianza kwa mashindano ya mbio za Baiskeli.
Mbio za Baiskeli zikiendelea.
Wananchi wakishuhudia mashindano ya mbio za Baiskeli.
Mshindi wa mbio za Baiskeli Makoja Seni akiibuka na ushindi mara baada ya kuwashinda wenzake kwa kuzunguka Round 60.
Mashindano ya kufukuza kuku yakiendelea.
Halima Husein akiibuka mshindi wa kufukuza Kuku na kisha kuondoka na kitoweo hicho.
Mzee Loyce Jiledya akiibuka mshindi wa kufukuza kuku mara baada ya kuwazidi wazee wenzake na kisha kuondoka na kuku huyo.
Mashindano ya uvutaji wa kamba ukiendelea ambapo washindi waliibuka vijana kutoka Mtaa wa Mwagala.
Mashindano ya kucheza Draft yakiendelea ambapo mshidi aliibuka Samweli Kashinje.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Hafeez Mukadamu.
Penat zikipigwa mara baada ya Timu ya vijana ya ufunguzi wa Bonanza hilo, kutoka Bugweto A na B kumaliza dakika 90 bila ya kufungana, ambapo mwenye Jezi ya Njano ni mchezaji kutoka Bugweto B, akipiga Penati na kupata Goli na hatimaye kupata ushindi.
Mchezo kati ya Bugweto FC wenye Jezi Nyekundu ambao ndiyo mabigwa wa Bonanza hilo , wakicheza mchezo wa kirafiki na Bugweto Veterani wenye Jezi ya Njano, ambapo Bugweto FC waliibuka na ushindi wa Goli Moja.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Aboo Hafez Mukadamu, katikati, akiwa na Diwani wa Kata ya Ibadakuli mkono wa kulia na kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Dotto Joshua, wakiangalia mashindano mbalimbali kwenye Bonanza hilo.
Kabumbu likiendelea kusakatwa kwenye Bonanza hilo.
Mmoja wa wananchi akiwa amepanda juu ya mti kushuhudia michezo mbalimbali kwenye Bonanza hilo la michezo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Hafeez Mukadamu akitoa zawadi kwa washindi wa mbio za Baiskeli kwa mwenyekiti wao Kande Maganga.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Hafeez Mukadamu akitoa zawadi kwa mshindi wa Draft Samweli Kashinje.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Hafeez Mukadamu akitoa zawadi kwa washindi wa Tatu na Wanne wa mpira wa miguu.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Hafeez Mukadamu akitoa zawadi kwa washindi wa Pili wa mpira wa miguu Timu ya Ibadakuli kwa kupewa Seti moja ya Jezi.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Hafeez Mukadamu akitoa zawadi kwa washindi wa kwanza wa mpira wa miguu kutoka Timu ya Bugweto ambapo walipewa Seti moja ya jezi pamoja na Mpira.
Mfugaji Bora kwenye michezo ya mpira wa miguu kwenye Bonanza hilo Raymond Peter akipewa zawadi.
Washindi kutoka timu ya Bugweto wakipiga picha ya pamoja.

Mara baada ya kumaliza Bonanza hilo la michezo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Hafez Mukadamu akimkabidhi kadi ya uanachama ya CCM Daudi Msabila ambaye amehamia kwenye chama hicho kutoka upinzani.
Burudani zikiendelea kutawala mara baada ya Bonanza hilo la michezo likimalizika ambapo Diwani huyo wa Viti maalumu Zuhura Waziri ambaye ndiye muandaaji, akicheza wimbo na wananchi uitwao Iokote wa msanii Maua Sama
Wimbo wa msanii Maua Sama Iokote ukiendelea kutawala kwenye kufunga Bonanza hilo la michezo.
Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog
Kesi Ya Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu Yakwama
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu na wenzake watano jana walishindwa kufika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusikiliza shauri linalowakabili ikielezwa kuwa basi la Magereza limeharibika.
Maimu na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 100, likiwamo la kuisababishia Serikali hasara ya Sh1.175 bilioni katika kesi ya uhujumu uchumi namba 7/2019.
Wakili kutoka Takukuru, Leonard Swai jana mbele ya Hakimu Mkazi, Salum Ally alieleza kuwa, wamepewa taarifa na askari magereza kuwa basi linalowabeba washtakiwa hao kutoka gereza la Segerea kuelekea mahakamani hapo ni bovu.
Kutokana na hali hiyo Swai aliiomba Mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kesi hiyo kutajwa.
Hakimu Ally baada ya kusikiliza maelezo ya upande wa mashtaka aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 14 itakapotajwa tena.
Mbali na Maimu Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni meneja biashara wa Nida, Aveln Momburi, mkurugenzi wa kampuni ya Aste Insurance Brokers, Astery Ndege, ofisa usafirishaji, George Ntalima, mkurugenzi wa sheria, Sabina Raymond na Xavery Kayombo.
Kati ya mashtaka yanayowakabili, 24 ni ya kutakatisha fedha, 23 ya kughushi, 43 ya kutumia nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri na matano ya kuisababishia hasara mamlaka hiyo.
Mengine ni mawili ya kula njama ya kulaghai, mawili ya matumizi mabaya ya madaraka na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na matumizi mabaya ya madaraka.
Rais Magufuli awataka wafanyakazi kuwa wavumilivu kuhusu nyongeza ya mishahara
Rais Magufuli amesema kuwa hatoongeza mshahara mwaka huu, kwani ahadi yake ya kupandisha mishahara katika uongozi wake haijaisha kwa sababu bado hajamaliza muda wake madarakani.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo May 1, 2019 mara baada ya hapo awali TUCTA kumuomba atimize ahadi yake ya kuwaongeza wafanyakazi mishahara.
"Niwaambie ndugu zangu, Katibu mkuu TUCTA alinikumbusha kuhusu ahadi yangu, ninaikumbuka na ninasema muda wangu bado nipo madarakani, ninachoomba muwe na subira.
"Niwaambie ndugu zangu, Katibu mkuu TUCTA alinikumbusha kuhusu ahadi yangu, ninaikumbuka na ninasema muda wangu bado nipo madarakani, ninachoomba muwe na subira.
“Ni kweli kwenye sherehe kama hizi mwaka jana niliahidi kuwa nitaongeza mishahara ya wafanyakazi kabla sijaondoka madarakani, ndugu zangu tuvumilie tu sikutaka kuwadanganya hapa kuwa nimewaongezea mishahara halafu fedha mtakazozipata hazipo, nyinyi endeleeni kuvumilia tupo katika muelekeo mzuri wa suala hili”, Amesema Rais Magufuli na kuongeza;
“Ningeweza kuwaongezea elfu 5 au 10, kesho tu bidhaa zingeanza kupanda hivyo lazima kwanza tujenge uchumi imara. Mimi mwenyewe nilikuwa mwalimu na nikaenda kuoa mwalimu anayejua shida zetu Serikali inawapenda wafanyakazi.
Kujichua Kwa Muda Mrefu Husababisha Maumbile ya Kiume Kusinyaa na Kupungukiwa Nguvu za Kiume
Wanaume wengi waliofanya mchezo wa kujichua kwa muda mrefu hupatwa na madhara ya kuwa na kusinyaa na kudumaa kwa maumbile yao ya kiume ambayo huenda pamoja na tatizo a Ukosefu au upungufu wa nguvu za kiume.
Tendo la kujichua kwa mwanaume linapofanyika kwa kipindi kirefu huathiri na kuharibu mishipa na misuli ya uume na hivyo kusababisha kujengeka kwa mafuta na tishu zisizo vutika kwenye mishipa ya ateri. Jambo hili husababisha makuu mawili; 1. Huzuia mishipa ya ateri kupanuka na kuongezeka jambo linalotajwa na wanasayansi kama jambo muhimu sana katika kukua kwa uume. 2. Huzuika kutirika kwa damu kuingia kwenye misuli ya uume.
Mambo hayo mawili huathiri sana ukuaji wa maumbile ya kiume kwa sababu yanapo tokea huathiri uzalishaji wa homoni muhimu zinazo husika na ukuaji wa misuli ya uume na matokeo yake husababisha uume wa mhusika kudumaa, kusinyaa,kunywea na kurudi ndani kiasi cha kuufanya uonekane kama uume wa mtoto.
Hii ndio sababu kwanini watu wengi walio athirika na punyeto hulalamika kwamba maumbile yao ya kiume hayajaongezeka tangu walipo anza kujihusisha na punyeto wakiwa na umri mdogo.
Maumbile yao huonekana kama ya watoto kwa sababu hayakupata nafasi ya kupokea vichochea vya kuyafanya yakue na kuongezeka tangu walipo anza kujihusisha na punyeto.
Suluhisho La Tatizo La Maumbile Ya Kiume Yaliyo Sinyaa Kwa Sababu Ya Punyeto.
Kama bado unaendelea kujihusisha na punyeto basi jitahidi uache tabia hiyo mara moja kwani inakuharibu. Inaweza isiwe rahisi sana kuacha mara moja lakini ukiweka nia thabiti basi unaweza kuacha kabisa kama walivyofanikiwa kuacha wengine ambao walikuwa wametopea kwenye tabia hiyo lakini wakajitahidi kujilazimisha na hatimaye wakafanikiwa kuachana kabisa na tabia hiyo.
==>> Acha kuangalia video chafu za ngono.
Video hizi ndio chanzo kikuu cha punyeto kwa watu wengi hua zinajenga picha nyingi kwenye ubongo na kila picha unayoiona utataka ukaipigie punyeto hivyo kuacha kuziangalia tu ndio nafuu yako..
Weka mipango ya kuzuia kupiga punyeto wakati wa kuoga: bafuni ndio sehemu ambayo inatumika sana na watu wengi kupiga punyeto hivyo ni vizuri kua na mikakati ya kujizuia ukiwa huko kwa kuoga haraka na kuondoka, kuoga maji ya baridi ambayo mara nyingi hayatoi muhemko wa kupiga punyeto.
==>>Epuka kukaa nyumbani peke yako;
Mara nyingi kukaa peke yako kunakufanya ushawishike kufanya tendo hilo, hebu ondoka na ujichanganye na watu wengine au tafuta majirani wa kukaa na kuongelea mambo mengine.
Fikiria kuhusu madhara yake: kila aliyewahi kupiga punyeto kuna madhara mabayo ameshayapata kama vile misuli ya uume kulegea, kushindwa kurudia tendo uwapo na mwenzi wako, kuishiwa nguvu za kiume, maumbile kusinyaa, kurudi ndani na kuwa kama ya mtoto mdogo.
Acha kusema eti hii punyeto ni ya mwisho: siku zote wapiga punyeto wana akili moja ya kufikiria eti sasa leo napiga afu sirudii tena. Hicho kitu hakipo, kwani kesho yake utasema hivyohivo, kama unaacha acha mara moja ili utunze heshima yako mbele ya mwenzi au mke wako.

Kama utaona kuna ugumu wa kuacha tabia hiyo na tayari ushaapata madhara ya maumbile kusinyaa na kupungiwa nguvu za kiume, basi wasiliana nasi kwa ushauri zaidi; Simu 0716-263605
Video Mpya: Gumbo ft Baba Diamond – Charanga
Kikosi cha Taifa Stars cha AFCON chatajwa
Hiki ndicho kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kilichoitwa kwaajili ya mashindano ya AFCON na CHAN.
Maduro alipongeza jeshi la Venezuela kwa kuzima jaribio la mapinduzi
Rais Nicolás Maduro wa Venezuela amelipongeza jeshi la nchi hiyo kwa kuzima jaribio la mapinduzi dhidi ya serikali yake, harakati ambazo anasema zinaungwa mkono na Marekani.
Maduro amesema Marekani ndiyo iliyochochea na kufadhili kwa hali na mali ghasia zilizoshuhudiwa jana katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo ya Amerika ya Latini, lakini amesisitiza kuwa vyombo vya usalama vilifanikiwa kuzima ghasia hizo.
Amesema asilimia 80 ya askari waliotangaza jana kuliasi jeshi na kuyauga mkono maandamano ya wananchi walirubuniwa kufanya hivyo, lakini walipogundua kuwa hizo zilikuwa njama za vinara wa upinzani nchini humo Juan Guaidó na Leopoldo Lopez waliachana na njama hizo.
Vladimir Padrino López, Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo sambamba na kupongeza juhudi za Rais Maduro kwa ajili ya kuimarisha usalama na demokrasia, amesema kuwa jeshi lingali linamuunga mkono kikamilifu rais wa nchi hiyo aliyeingia madarakani kwa kura za wananchi.
Hii leo waungaji mkono wa serikali ya mrengo wa kushoto ya Caracas wanatazamiwa kufanya maandamano makubwa na kuonyesha uungaji mkono wao kwa serikali ya Maduro, mkabala wa ubeberu na njama za Washington.
Mgogoro unaoshuhudiwa hivi sasa nchini Venezuela ulishtadi mwezi Januari mwaka huu baada ya Juan Guaidó, kiongozi wa upinzani ambaye ni kibaraka wa Marekani na madola ya Magharibi, kujitangaza kuwa rais wa muda wa Venezuela, suala ambalo linakiuka katiba ya nchi hiyo.
Jana Jumanne, Guaido alitangaza kuwa ni siku ya kwanza ya duru ya mwisho ya 'harakati za ukombozi' za kumng'oa madarakani Rais Maduro.
DRC yafuta uchunguzi dhidi ya Moise Katumbi, huenda akarudi nyumbani
Waendesha Mashitaka wa Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamefuta uchunguzi wa shitaka la jinai dhidi ya Moise Katumbi, mwanasiasa wa upinzani ambaye kwa sasa yuko uhamishoni.
Moise Katumbi alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya kuajiri askari mamluki wa kigeni wakiwemo askari kadhaa wa Kimarekani waliostaafu kwa lengo la kuangusha utawala uliopita wa Joseph Kabila.
Timothee Mukuntu, Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Kijeshi wa DRC alitoa rasmi tangazo hilo jana Jumanne na kufafanua kuwa, "Kwa kuzingatia kuwa rais wa Jamhuri ametoa kipaumbele kwa suala la kupunguza taharuki za kisiasa, tumeona kuwa ni vyema tufutilie mbali uchunguzi huo."
Ingawaje waraka kuhusu tangazo hilo ulitiwa saini tarehe Mosi mwezi Machi, lakini uliwekwa hadharani kwa umma jana Jumanne. Wakili wa Katumbi amesema huu ni wakati mwafaka kwa mteja wake kurejea nyumbani. Hata hivyo Katumbi mwenyewe hajazungumza chochote kuhusu uamuzi huo.
Septemba mwaka jana, Ofisi ya Mashtaka ya Umma nchini humo ilimzuia Moise Katumbi kuwania urais na kutishia kuwa angelikamatwa iwapo angelitia mguu wake nchini DRC, akikabiliwa na tuhuma za kuhatarisha usalama wa taifa. Felix Tshisekedi alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo wa urais wa Disemba mwaka jana 2018.
Meya huyo wa zamani wa Katanga mwenye umri wa miaka 54, alikimbilia uhamishoni mwezi Mei mwaka 2016 baada ya kuhitilafiana kisiasa na rais mstaafu Joseph Kabila.
Biteko akutana na viongozi waandamizi wa wizara na Tume ya madini
Waziri wa madini Doto Biteko amewataka wafanyakazi wa wizara ya madini pamoja na taasisi zake kufanya kazi na kutekeleza majukumu yao kwa wakati ili kufikia malengo ya wizara hiyo.
Ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa kikao chake na viongozi waandamizi wa wizara ya madini na tume ya madini. Katika kikao hicho pamoja na mambo mengine amezungumzia juu utekelezaji wa maagizo anayoyatoa na usimamizi wa utekeleza wa maagizo yake. Ameongeza kuwa anawategemea sana viongozi hao na wafanyakazi wote katika kufanikisha kazi na malengo ya wizara hiyo.
Ametolea mfano wa maagizo aliyowahi kuyatoa ni pamoja na ufutwaji wa leseni zisizo hai ndani ya siku 7 na zingine siku 30 na lile linalo husu mgodi wa North Mara kuhusu utiririshaji wa maji yenye sumu kwenda kwenye makazi ya wananchi ambapo alitoa pia siku 30 kuhakikisha maji hayo yanadhibitiwa.
Amewaambia viongozi hao kuwa akishatoa maagizo, kazi ya kusimamia utekelezaji wa maagizo hayo ni kazi yao. Amemshukuru na kumpongeza Mwenyekiti wa Tume Prof. Idris Kikula na tume yake kwa kazi nzuri wanayoifanya na ziara zake mikoani zimekuwa na tija.
Biteko amesisitiza kuwa anatambua mchango wa watumishi wote wa wizara yake hivyo amewaomba kuongeza bidii na kuongeza umakini katika utekelezaji wa majukumu yao huku wakizingatia weledi na uadilifu.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila na Makamishna. Kwa upande wa tume ya madini waliohudhuria ni pamoja na Mwenyekiti wa Tume Prof. Kikula, Mtendaji mkuu wa tume ya madini Prof. Shukrani Manya, Mkurugenzi wa Leseni Mhandisi Yahya Samamba, Mkurugenzi wa Biashara Dkt. Venance Bahati.
Rais Magufuli Awaonya Wakurugenzi Awanaowatoza Ushuru Wakulima
Rais John Magufuli amesema ni marufuku kwa wakurugenzi na watendaji wa halmashauri kuwatoza ushuru wasafirishaji wa mazao chini ya tani moja na wafanyabiashara wadogo wenye vitambulisho vya wajasiriamali.
Ametoa onyo hilo jana Jumanne Aprili 30 katika viwanja vya Mwakangale wilayani Kyela katika ziara yake ya siku nane mkoani Mbeya.
Alisema wapo watendaji wa halmashauri wanaoendelea kutoza ushuru kwa wafanyabiashara hao kwa kudhani kuwa wanapoacha wanapunguza mapato.
“Narudia kwa wakurugenzi na watendaji wote wa halmashauri msiwatoze wananchi ushuru wa mzigo wowote usiozidi tani moja. Mkulima wewe safirisha kutoka hapa peleka mahala popote hakuna wa kukutoza ushuru, na hii sheria imepitishwa na Bunge hayupo yeyote wa kuitengua kwa hivyo mkurugenzi ukitengua umevunja sheria una wajibu wa kufukuzwa kazi.”
“Tuzingatie sheria ya kuwalinda wakulima, pakia viazi, maharage, njugu, chochote ilimradi kisizidi tani moja hakuna kulipia, ukizidisha mie simo,” alisema Rais Magufuli.
Waziri Lugola afanya ziara ya kushtukiza Kituo cha Polisi Stakishari Dar
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amefanya ziara ya kushtukiza Kituo cha Polisi Stakishari jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufuatilia utendaji kazi wa Kituo hicho.
Waziri Lugola aliwasili kituoni hapo Saa 6:16 mchana ambapo alikutana na wananchi mapokezi ya kituo hicho ambao walifika kwa ajili ya kuwachukulia dhamana ndugu zao walipo katika mahabusu ya kituo hicho, aliwahoji kama wanapata huduma nzuri kutoka kwa askari wa kituo hicho.
Pia Waziri Lugola akiwa katika mapokezi ya kituo hicho, alikichukua kitabu cha taarifa za watuhumiwa wote waliopo mahabusu na baadaye kuelekea katika mahabusu hiyo akiwahoji watuhumiwa wote kwa kuwaita kwa majina kujua makosa yao yaliyoyafanya wawepo kituoni hapo.
Akizungumza mara baada ya kumaliza kuiwahoji mahabusu hao, alisema ziara yake ni ya kawaida ya kufuatilia utendaji kazi wa vituo vya polisi, pia kufuatilia ahadi zake ambazo alizitoa Bungeni kufuatilia vituo mbalimbali vinavyolalamikiwa, na pia yeye Waziri ni wajibu wake kufuatilia utendaji kazi pamoja na maagizo anayoyatoa mara kwa mara ya dhamana zitolewe saa 24 ikiwemo Jumamosi na Jumapili na pamoja na polisi kutowabambikizia kesi wananchi.
“Lengo la hii ziara yangu ni kuboresha utendaji kazi wa vituo vya polisi nchini, sijaja kumuadhibu mtu mimi, hivyo msiwe na wasiwasi, bali kilichonifanya hapa nije nikufuatilia maagizo mbalimbali ambayo niliyatoa kama kweli mnayafanyia kazi,” alisema Lugola.
Lugola aliwataka Makamanda wa polisi mikoa mbalimbali nchini, kusimamia utendaji kazi bora na kuakikisha maagizo yake anayoyatoa yanafanyiwa kazi ipasavyo, na ataendelea kuyafuatilia maagizo yote anayoyatoa na endapo yakipuuzwa hatamvumilia mtu.