Tuesday, 2 April 2019
Monday, 1 April 2019
Waziri Biteko Awasimamisha Kazi Maafisa Madini Ofisi Ya Madini Chunya
Waziri Biteko ametoa kauli hiyo Wilayani Chunya Mkoani Mbeya , wakati akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini katika ukumbi wa halmashauri ya Chunya.
Amesema, baada ya serikali kupitia Wizara husika kuhakikisha inadhibiti mapato yake, utafiti umebaini kwamba Wilaya ya Chunya inashika namba moja kwa wizi na utoroshaji wa madini aina ya dhahabu ikifuatiwa na Kahama.
“Baada ya kufanya utafiti tumeabaini kunawizi mkubwa na usio na aibu ambapo unakuta mtu amepata kilo 1 na gramu 1620 lakini serikali inapata gramu 208, lakini kuna mahali mtu anapata kilo nne anawasilisha taarifa za gramu 155,sasa wizi namna hii tukiendelea kunyamaza nchi haiwezi kuwa na afya.,”alisema.
Kutokana na hali hiyo Waziri Biteko amewataka watendaji na viongozi husika kubadilika na kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu.
“Ukiangalia sasa, wazalishaji wengi wanakimbilia Chunya na hii ni kwa sababu ya utaratibu wa eneo husika kushindwa kubaini wizi huu unaofanyika kupitia taarifa za kiwango cha uzalishaji ambacho ndicho kinachohalalisha mapato kwa serikali kupitia mrahaba wa Madini “Amesema Waziri Biteko
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila, alimueleza Biteko kuwa Wilaya ya Chunya inahitaji msaada hasa wa kielimu na utaalamu wa madini na kuomba watendaji wasafi wapatikane kwenye sekta hiyo.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amesema kwa sasa wanataka kuzungumza na uongozi wa Mkoa wa Songwe ili kuunda nguvu ya pamoja itakayosaidia kuimalisha Ulinzi katika maeneo hayo ili kuepusha wizi wa Madini.
PICHA: Rais Magufuli Alivyokutana na Godbless Lema Katika Msiba wa Dada yake Mchungaji Msigwa
Maandalizi Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa Yaanza
Rais Magufuli Atoa Pole Kwa Mbunge Wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa Aliyefiwa Na Dada Yake Jijini Dar Es Salaam
Wakiwa nyumbani kwa Marehemu Kimara Stopover, Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli na Mama Janeth Magufuli wameungana na wanafamilia kumuombea Marehemu apumzike mahali pema peponi, Amina.
Rais Magufuli ataka TRA iache kuwa kamua walipa kodi wachache
Hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao imehudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, Makatibu Wakuu, Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango.
Akizungumza baada ya kuwaapisha, Rais Magufuli ameitaka TRA na Wizara ya Fedha na Mipango kupanua uwigo wa kodi kwa kuongeza idadi ya walipa kodi na kuibua vyanzo vipya vya mapato, pamoja na kujenga mazingira rafiki kwa watu wengi zaidi kulipa kodi ili kuongeza makusanyo ya kodi.
Rais Magufuli ameelezea kutoridhishwa kwake na utendaji wa TRA ambayo mpaka sasa inakusanyaji kodi kwa walipa kodi Milioni 2 na Laki 7 tu kati ya Watanzania wote zaidi ya Milioni 55, na amesema kwa mtindo huo TRA itakuwa inazidi kuwakamua walipa kodi wachache wakati ingeweza kupanua uwigo wa kodi na kuweka viwango vya kodi vinavyolipika na vitakavyowavutia watu wengi zaidi kulipa kodi.
“Ukienda mipakani wafanyabiashara wanafungua maduka upande nchi za wenzetu na sio upande wa Tanzania, na sababu ni kwamba wakifungua upande wa Tanzania wanasumbuliwa na TRA, wekeni viwango vya kodi vinavyolipika ili watu wengi waweze kulipa kodi badala ya kukwepa” Rais Magufuli.
Rais Magufuli ameelezea kutofurahishwa na mrundikano wa kesi za kodi mahakamani na ametaka tatizo hilo lifanyiwe kazi kwa kuwa linasababisha kodi nyingi kutolipwa kwa kusubiri mivutano ya kesi.
Amempongeza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji kwa ufuatiliaji mzuri wa fedha za bajeti zinazoelekezwa katika miradi mbalimbali na kuchukua hatua zinazostahili ikiwemo kuzirejesha hazina na kuzielekeza mahali pengine zinapohitajika.
Aidha, Rais Magufuli amemtaka Naibu Katibu wa Fedha na Mipango Mkuu Ndunguru na Naibu Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Mbibo kwenda kurekebisha dosari zote zilizopo katika ofisi zao ikiwa ni pamoja na kuwaondoa watumishi wanaoonekana kuwa kikwazo cha kutekeleza mipango ya Serikali.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema viongozi hao wanatarajiwa kufanya vizuri zaidi katika nafasi walizopewa hivi sasa hasa ikizingatiwa kuwa wanakwenda kufanya kazi katika ofisi zenye mchango mkubwa katika uchumi wa nchi.
Nae Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji na Kamishna Mkuu wa TRA Charles Kichere wamemshukuru Rais Magufuli kwa uteuzi wa viongozi hao na wameahidi kwenda kusimamia kwa ukaribu zaidi utekelezaji wa fedha za bajeti na kufanyia kazi changamoto ya kupanua uwigo wa kodi na kuongeza idadi ya walipa kodi.
Form four graduates in 2018 to change Combination for 2019/2020 form five selection
Form four graduates in 2018 to change Combination for 2019/2020 selection
How to change form five Combination – Students who wish to join Form Five and Colleges for 2019/2020
The Government has provided opportunities for students who passed the Form four exam in 2018 and who are expecting to joining Form Five and varous colleges in 2019 to change their Combination.
“For the first time students will be able to change options or choose from Form Five to College or College to Form Five as per their requirements and how they passed their examinations” said Jafo.
How to change form five Combination – Students who wish to join Form Five and Central Colleges for 2019/2020
Monday 1st, April 2019 @Tanzania entire Date Released for Students who are hoping to join Form Five and Central Colleges, this date has been announced by the Minister of State OR-TAMISEMI.
Download and read the Guide for details….. Selform _ Student Manual.pdf
You can Log in to the System via the following Address After reading the Manual http://selform.tamisemi.go.tz/Account/Login
Click here to change your combination
This modification process will take place from 01/04/2019 to 15/04/2019.
The post Form four graduates in 2018 to change Combination for 2019/2020 form five selection appeared first on Udahiliportal.com.