Saturday, 2 March 2019

Picha 50 : MAELFU WAJITOKEZA KUMUAGA RUGE DAR WAKIONGOZWA NA JPM...WENGI WAZIMIA

Maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kutoa salamu kwa Ruge Mutahaba aliyegusa nyoyo za wengi ziliongozwa na Rais Dkt.John Magufuli, Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Kikwete aliyeambatana na mkewe pamoja na Waziri mkuu Kassimu Majaliwa na mkewe Mary Majaliwa. Wakati huo huo msanii Naseeb Abul maarufu kama Diamond Platnumz , Fleva Ali Kiba, Mwana FA na Ommy Dimpoz pia waliwasili katika viwanja hivyo kwa ajili ya kutoa salamu za mwisho.
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Ruge Mutahaba ambaye aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumamosi March 2, 2019 ( Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii)
Msanii wa muziki wa bongo Flava Nasibu Abdul "Diamond Platinumz" akiwasili katika msiba wa marehemu Ruge Mutahaba ambaye aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumamosi March 2, 2019 
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Ali Kiba pamoja na Mwana FA na Ommy Dimpoz wakitoka kuaga mwili wa marehemu Ruge Mutahaba ambaye aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumamosi March 2, 2019.
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Harmonize akiondoka mara baada ya kuaga mwili wa marehemu Ruge Mutahaba ambaye aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumamosi March 2, 2019.


Msanii wa kizazi kipya Barnaba akiondolewa ukumbini akiwa amebebwa baada ya kuishiwa nguvu kutokana na uchungu mkali alio nao.
Mwili wa marehemu Ruge Mutahaba ambaye aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment ukitolewa kwenye ukumbi wa Karimjee mara baada ya kuagwa leo Jumamosi March 2, 2019


Share:

MSANII BARNABA AANGUKA AKIMUAGA RUGE MUTAHABA


Msanii wa kizazi kipya Barnaba amesababisha vilio kutawala baada ya kushindwa kumalizia hotuba yake huku akiomba afunguliwe jeneza kumuona baba yake mlezi, Ruge Mutahaba.

Msanii huyo kutoka THT aliondolewa ukumbini akiwa amebebwa baada ya kuishiwa nguvu kutokana na uchungu mkali alio nao.

Alisema Ruge alikuwa kama baba kwake na hajawahi kumtoza mtu kati ya wasanii waliopita THT.

“Kama shida ni figo ungeniambia nikupe yangu, wazazi wangu walifariki Ruge ndiyo alikuwa Baba na ndio mama, Watoto wengi unawaoona THT wametoka kwenye maisha ya shida, Ruge alikuwa ndio Baba yetu” Alisema.



Share:

Vurugu : MASHABIKI WA STAND UNITED WALINDA UWANJA SIMBA 'ISIROGE'

Wakati wachezaji wakiendelea na mazoezi, nje ya uwanja hali ni tofauti baada ya viongozi walioambatana na Simba kushindwa kuvumilia hali ya mashabiki wa Stand United jinsi wanavyoshangilia.

Mvutano baina ya wapinzani hao umechukua takribani dakika sita huku viongozi wa Simba wakiwafuata jukwaani mashabiki wa Stand United wakiwataka watoke uwanjani, jambo lililozua vurugu na baadaye Simba kutulia.

Mashabiki wa Stand United wameonekana kukomaa, huku wakidai kuwa hapa ni nyumbani kwao hivyo si rahisi kutokana uwanjani hapo na kuanza kupiga ngoma wakiimba kuwa wanaroga mechi.

Hadi sasa tayari Simba imeshafanya mazoezi mawili tofauti, ikiwa kukimbia kwa kuzunguka uwanja, kupigiana vichwa na kufunga na sasa wanasikiliza maelekezo ya Kocha wao, Patrick Aussems kujua programu inayofuata.

Na Saddam Sadick - Mwanaspoti
Share:

YANGA WAITWANGA ALLIANCE FC 1 - 0 CCM KIRUMBA

Mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Alliance FC dhidi ya Yanga katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza umemalizika kwa Yanga kuichapa Alliance 1 - 0.

Kipindi cha kwanza kilikamilika kukiwa hakuna aliyeona lango la mpinzani wake huku Alliance wakitumia nguvu nyingi kwenye mchezo wa leo.

Heritier Makambo wa Yanga dakika ya sita alikosa penati baada ya kudondoshwa na mchezaji wa Alliance eneo la hatari iliokolewa na mlinda mlango wa Alliance.

Dakika ya 63 Blaise Bigirimana alifunga bao likakataliwa kwa kuwa alikuwa ameotea kwa kitendo cha kuonyesha kitendo kisicho cha kinidhamu alionyeshwa kadi ya njano.

Dakika ya 75 Amis Tambwe akaandika bao la kuongoza kwa Yanga akipokea pasi ya Heritier Makambo na kumalizia kwa mguu wake wa kulia.
Share:

Imevuja : KILICHOMU 'LEFTISHA' LOWASSA CHADEMA HIKI HAPA

Waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Ngoyai Lowassa, ametangaza kurejea katika Chama Cha Mapinduzi (CCM). Lowassa aliondoka CCM katikati ya mwaka 2015, kufuatia chama hicho “kumtosa katika kinyang’anyiro cha urais.” 

Taarifa zinasema, kurejea kwa mwanasiasa huyo kwenye chama tawala, akitoka Chadema 'Akileft' kunatokana na shinikizo kutoka ndani ya familia yake na kile kinachoitwa, “kufungwa kwa njia yake ya kutaka kuwa mgombea tena wa urais kupitia Chadema.”

Ingawa upinzani haujataja mgombea wake, lakini anayepewa nafasi kubwa ya kugombea nafasi hiyo, ni Tundu Lissu, mbunge wa Singida Mashariki na Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni.

Kinachotajwa kuwa shinikizo la familia, taarifa zinasema, linatokana na kesi ya jinai inayomkabili mmoja wa watoto wake, Sioi Solomon.

Sioi mbaye aliyekuwa mwanasheria wa benki ya Stanbic, tawi la Tanzania na wenzake wengine watatu, wanashitakiwa kwa makosa kadhaa, ikiwamo kula njama na kujipatia kwa udanganyifu, kughushi, utakatishaji wa fedha haramu.

Washitakiwa wengine, ni aliyepata kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na mwenyekiti wa kampuni ya Enterprise Growth Market Advisors Ltd (EGMA), Harry Kitilya; aliyekuwa mkuu wa idara ya ushirikiano na uwekezaji wa benki hiyo, Shose Mori Sinare na mwanasheria wa benki, Sioi Graham Solomon.

Washitakiwa wote wako gerezani tokea 1 Aprili 2016. Lowassa ameripotiwa akisema, alikutana na rais Magufuli na kumuomba kumsaidia kumtoa Sioi, ombi ambalo halikuwa limetekelezwa hadi anapotangaza kuondoka upinzani.

Lowassa ambaye alikuwa mpinzani mkuu wa Rais John Magufuli katika uchaguzi mkuu uliyopita, aliondoka CCM na kujiunga na Chadema, kupitia mkutano wake na waandishi wa habari wa tarehe 28 Julai 2015, katika hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.

Via Mwanahalisi Online
Share:

MAKONDA : RUGE NI ZAIDI YA RAFIKI YANGU...NILIOMBA WANIONDOE KWENYE RATIBA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amesema kwamba kutokana na uchungu alioupata wa kuondokewa na 'kaka' yake Ruge Mutahaba, alikosa hata cha kuzungumza kwa jamii, na kuitaka familia kumtoa kwenye ratiba ya kuongea.

Akizungumza kwenye tukio la kuaga mwili wa marehemu Ruge Mutahaba katika ukumbi wa Karimjee, Paul Makonda amesema kwamba alipata wakati mgumu sana kutokana na taarifa za kifo cha Ruge, hivyo walipomwambia yupo kwenye ratiba ya kutoa salam za rambi rambi, aliomba familia isimuweke kwani hana cha kuongea, na kufikia hatua ya kukesha akimuomba Mungu ampe neno la kuongea ambalo mpaka sasa hajajua aseme nini.

“Jana wakati tunajadiliana habari ya kutoa salamu za rambirambi, kwangu nilikuwa na wakati mgumu sana kwa sababu Ruge ni zaidi ya rafiki kwangu, na familia ilikuwa inajua, nikawa natafakari nasema nini mwishowe ikafika hatua nikawaambia niondoeni kwenye ratiba, kwa sababu tangu nilipopata taarifa za kumpoteza kaka yangu Ruge, sikupata nafasi ya kusema chochote kile, si kwa sababu nilikuwa sitaki, lakini niseme nini kwa ndugu yetu mpendwa, usiku kucha nilikuwa namuuliza Mungu naenda kusema nini”, amesema Paul Makonda.

Paul Makonda ameendelea kwa kusema kwamba........ “mpaka leo nimefika hapa asubuhi, sina cha kusema, nimemsihi sana Mungu nipatie hata neno moja la kusema, lakini Mungu bado hajanipa cha kusema, Mungu akinipa kibali cha kusema atanipa na cha kusema”.

Sambamba na hilo Paul Makonda amewaomba radhi wakazi wa Dar es salaam kwa usumbufu walioupata jana wakati wakitoka kupokea mwili uwanja wa ndege, na kusema kwamba alifanya hivyo ili kumpa heshima Ruge Mutahaba.
Share:

KUSAGA ASEMA RUGE ALISEMA " SIKU NIKIFA MSILIE,MSHEREHEKEE YALE MAZURI NILIYOFANYA"

Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga, ameeleza kuwa alikutana na Ruge miaka 25 iliyopita wakati akifanya kazi za disko na wakati huo Ruge akiwa mwanafunzi nchini Marekani ambapo walianzisha urafiki kisha kukaa pamoja na kutengeneza wazo la kuanzisha redio.

Kusaga amesema hayo leo Jumamosi, Machi 2, 2019 katika Viwanja vya Karimjee wakati akitoa wasifu wa marehemu Ruge kabla ya kuagwa mwili wake.

“Ruge alipokuja miaka 25 iliyopita, biashara ya kupiga muziki ilikuwa uhuni..tuliiitwa wahuni…..wimbo wa kwanza kutengeneza pale Mawingu uliitwa ‘Oya Msela oooyaaa’… Tulipopeleka kwenye redio tukaambiwa mnaona sasa wahuni hawa, wimbo gani unaitwa Msela?

“Ruge alitengeneza kina Ruge wengine wengi ambao wapo Clouds, na mimi binafsi kupitia Foundation itakayokuja hivi karibuni nitahakikisha tunaendeleza yale aliyokuwa akifanya Ruge Mutahaba,” alisema Kusaga.

Akielezea kwa utulivu wa majonzi miongoni mwa mambo aliyoambiwa na marehemu, Kusaga alisema kwamba Ruge alimwambia: “Siku nikifa, msilie, msherehekee, msifie yale mazuri mtakayoona niliyafanya…”

Kusaga alisema kwamba maneno hayo alimwambia wakati alipokwenda kumwona nchini India wakati wa matibabu yake ambapo alikwenda kwa kushtukiza na ambapo wawili hao walikumbatiana bila kujua kwamba ilikuwa ni mara yao ya mwisho kufanya hivyo.
Share:

KUTANA NA SAMAKI HUYU WA PEKEE ALIYESOMBWA NA MAJI

Samaki ambaye ni nadra kupatikana anayeaminiwa kuwa anaishi katika eneo la ncha ya kusini mwa dunia amesombwa hadi kwenye ufukwe wa Santa Barbara, California.

Kupatikana kwa samaki huyo mwenye futi saba sawa na (2.1m) kumewashangaza wanasayansi ambao wanajiuliza ni kwa vipi aliweza kusafiri kutoka kwenye makazi yake ya majini.

Mwanafunzi aliyeko mazoezini katika Chuo Kikuu cha California alimuona samaki huyo katika kituo cha hifadhi ya mali asili cha Coal Oil Point.

Iliwachukua watafiti siku kadhaa kumtambua kiumbe huyo ambacho kiligundulika kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2014.

Picha za samaki huyo mwenye umbo kubwa zilionekana kwenye ukurasa wa kituo cha Coal Oil point na wataalam kutoka maeneo mbali mbali ya dunia wakakusanyika kusaidia kumtambua kiumbe huyo wa aina yake.

Myama huyo ilipewa jijna la "hoodwinker" baada ya uvumbuzi wake kuwatatiza watafiti kwa miaka mingi.

Marianne Nyegaard, ambaye ni mwanasayansi wa viumbe wa majini ambaye alimgundua na kumuita jina samaki huyo, aliiambia televisheni ya Marekani CNN kwamba "karibu nianguke kutoka kwenye kiti changu " nilipoiona picha ya samaki huyo''

"Wakati nilipopata picha halisi sikuwa na wasi wasi ," alisema. "Ni shauku iliyomfanya samaki huyo avuke uzio wa Ikweta."

Hoodwinker ni samaki mkubwa sana na ambaye anateleza kuliko samaki wengine wa kizazi cha samaki wa jua (sunfish) , akiwa na uzito wa tani mbilili sawa na kilogramu 2000.

Samani wa aina yake wanasemekana kupenda zaidi maji yenye viwango vya joto vya juu, kama vile kwneye maeneo ya mwambao wa Chile au New Zealand.

Chanzo - BBC
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger