Saturday, 2 March 2019

Picha : DIAMOND PLATNUMZ AFIKA KARIMJEE KUMUAGA RUGE MUTAHABA

Msanii Diamond Platnumz na Mama yake mzazi Bi Sandra, wamefika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam kuungana na watanzania waliojitokeza katika taratibu za kuuaga mwili wa Marehemu Ruge Mutahaba.  ...
Share:

MSANII NANDY AMWAGA MACHOZI AKIMWIMBIA MAREHEMU RUGE

MSANII wa Bongo Fleva, Nandy ameshindwa kabisa kuendelea kuimba wimbo wa Angel Benard, Nikumbushe ambao Nandy aliufanya Cover. Wimbo huo ulikuwa kati ya nyimbo bora sana kwa marehemu Ruge na akiwa hospitali ulipigwa mara nyingi sana kumfariji. Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji...
Share:

Picha : RAIS MAGUFULI AONGOZA MAELFU YA WAKAZI WA DAR KUAGA MWILI WA RUGE MUTAHABA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshima zake za mwisho kwa Marehemu Ruge Mutahaba alipoongoza maelfu ya waombolezaji kuuaga mwili wa marehemu ambaye aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja...
Share:

HARMONIZE,BABU TALE WATUA KARIMJEE KUMUAGA RUGE MUTAHABA

Babu Tale ambaye ni mmoja wa mameneja wa mwanamuziki, Diamond Platnumz amefika katika viwanja vya Karimjee inapoendelea shughuli ya kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji, Ruge Mutahaba. Mbali na Babu Tale, Msanii Harmonuze naye ameshafika kujumuika na waombolezaji kuuaga Mwili wa...
Share:

MTOTO WA RUGE AMUOMBEA MSAMAHA BABA YAKE KWA ALIOWAKOSEA ENZI ZA UHAI WAKE

 Mwachi ambaye ni mtoto wa kwanza wa marehemu, Ruge Mutahaba amemuombea msamaha baba yake kwa watu aliowakosea enzi za uhai wake. Mwachi aliyasema hayo leo Jumamosi Machi 2, 2019 wakati akisoma wasifu wa baba yake katika shughuli za kumuaga zinazoendelea katika viwanja ya Karimjee jijini Dar...
Share:

KIKWETE ACHEKELEA LOWASSA KURUDI CCM "HONGERA KWA UAMUZI WA BUSARA"

Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Kikwete amempongeza Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwa uamuzi wake wa kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM). Lowassa alijiunga CHADEMA Julai 2015 baada ya jina lake kuenguliwa kwenye mchakato wa kutafuta mgombea wa urais ndani ya CCM. "Karibu tena nyumbani,...
Share:

Video : RAIS MAGUFULI, WAZIRI MKUU MAJALIWA, KIKWETE WALIVYOFIKA KUMUAGA RUGE, KARIMJEE

 Rais Magufuli, Waziri Mkuu Majaliwa, Kikwete walivyofika Kumuaga RUGE, Karimjee ...
Share:

AFARIKI KWENYE DIMBWI LA MAJI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Thobias Sedeyoka, amethibitisha kutokea kwa vifo vya watu wawili kulikosababishwa na mvua kubwa za masika zilizoanza kunyesha visiwani humo. Waliofariki dunia ni Hassan Mohamed (4) aliyezama kwenye dimbwi la maji ya mvua, na Skachi Abdallah Zahor...
Share:

LIPUMBA : LOWASSA AMERUDI CCM BILA AIBU...MBOWE BADO YUPO GEREZANI

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema anashangazwa na uamuzi wa Edward Lowassa kurejea CCM katika kipindi ambacho mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwa gerezani. Akizungumza na Mwananchi jana Ijumaa Machi 1, 2019, Profesa Lipumba, ambaye mwaka 2015 alijivua uenyekiti kutokana na...
Share:

Friday, 1 March 2019

AGPAHI YAWAPIGA MSASA WASHAURI WAVIU SIMIYU

Afisa wa AGPAHI, Bw. Emmanuel Mashana, akiwezesha mada ya ufuatiliaji wa mahudhurio ya WAVIU CTC katika warsha iliyokutanisha Washauri WAVIU wa mkoa wa Simiyu ili kuwaongezea uweledi katika shughuli zao hivyo kuimarisha mapambano dhidi ya UKIMWI. Afisa wa AGPAHI, Bi. Harieth Novat, akiwaonyesha...
Share:

SUMAYE : UAMUZI WA LOWASSA KUREJEA CCM HAUNIPI SHIDA...KAMA KAAMUA ACHA AENDE

Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye amesema uamuzi uliochukuliwa na Edward Lowassa kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM) hauwezi kumshtua. Sumaye ambaye pia ni Waziri Mkuu mstaafu akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Machi 1, 2019 muda mfupi baada ya Lowassa kuchukua uamuzi huo amesema,...
Share:

CHADEMA YAFUNGUKA LOWASSA KUREJEA CCM..."YEYE NI MTU MZIMA ANAJUA ANACHOKIFANYA"

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) nchini Tanzania kimesema kuondoka kwa mwanachama wake, Edward Lowassa na kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM) hakutakuwa na madhara yoyote. Hayo yamesemwa leo Ijumaa Machi 1, 2019 na Katibu Mkuu wa chama hicho kikuu cha upinzani Tanzania, Dk Vicent Mashinji...
Share:

HII HAPA RATIBA YA KUAGA MWILI WA RUGE MUTAHABA KARIMJEE DAR KESHO

Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba umewasili nchini leo mchana, 2, Machi, 2019. Mwili wake unatarajia kuagwa Jumamosi, 2 Machi, 2019 katika ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam kabla ya kusafirishwa mkoani Kagera kwaajili ya mazishi yatakayofanyika...
Share:

Picha 11 : MAPOKEZI YA LOWASSA BAADA YA KUHAMA CHADEMA NA KUREJEA CCM

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa leo Ijumaa Machi Mosi, 2019 ametangaza uamuzi wa kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM). Lowassa amerejea katika chama chake cha zamani shughuli iliyofanyika ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa Tanzania,...
Share:

RAIS MAGUFULI ATOA ONYO KALI KWA VIONGOZI WANAOWATOZA USHURU WAJASILIAMALI

...
Share:

LOWASSA : NIMETAFAKARI NA KUAMUA KURUDI NYUMBANI... "CCM WACHEKELEA KILA KONA

Mwenyekiti wa CCM,Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu wa zamani Mh.Edward Lowassa mara baada ya kutangaza kurejea CCM leo kwenye ofisi ndogo za chama hicho Lumumba jijin Dar es salaaam. WAZIRI Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Edward Lowassa ametangaza rasmi kurudi Chama...
Share:

Breaking : LOWASSA AIFYEKELEA MBALI CHADEMA...ATANGAZA KURUDI CCM

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa leo Ijumaa Machi Mosi, 2019 ametangaza uamuzi wa kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM). Lowassa amerejea katika chama chake cha zamani shughuli iliyofanyika ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa...
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger