Saturday, 22 December 2018

HATIMAYE SASA MUSIBA KUBURUZWA MAHAKAMANI,MDOMO WAKE WAMPONZA,MEMBE AKOMAA NAYE KISA–

NA KAROLI VINSENT HATIMAYE anayeejiita na kuitwa Mwanaharakati mzalendo ,Cyprian Musiba, amefunguliwa kesi kwenye mahakama ya Kuu ya Tanzania akitakiwa alipe mabilioni ya fedha kutokana na hatua yake ya kumchafua aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa kimataifa,Benard Membe. Katika shauri hilo ambalo limesajiliwa kwenye Mahakama kuu ya Tanzania tangu wiki iliyopita ni shauri namba 220 ya mwaka 2018 ,washtakiwa wakiwa ni Musiba ,Mhariri wa Gazeti la Tanzania,na wachapishaji gazeti hilo wakidaiwa sh bilioni 10 kwa kumchafuwa Membe ambaye aliwai kuwania Urais ndani ya Chama cha Mapinduzi Mwaka…

Source

Share:

RAY C : AMKA RUGE WE NDO MSIRI WANGU, NAKUPIGIA SIKUPATI

Na Bakari Chijumba, (Beca Love), Mtwara. Mtangazaji wa zamani wa Clouds Fm ambaye pia ni msanii, Rehema Chalamila maarufu kama ‘Ray C’ amefunguka na kuandika ujumbe mzito kwenye ukurasa wake wa instagram akielezea masikitiko yake na vile anavyoguswa na kuugua kwa Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba, ambaye kwa wakati huu yupo nje ya nchi kwa matibabu. Kupitia akaunti ya Ray C ya instagram ameandika: “Amka bwana, nashachoka kusubiri, msg zangu hujibu, simu hupokei, na stori kibao nataka kukwambia ingawa najua utanchamba lakini nishazoea kukwambia…

Source

Share:

MDOGO WAKE ROSTAM AZIZ AHUKUMIWA MIAKA 20 JELA

Na Bakari Chijumba, Mtwara. Mdogo wake mfanyabiashara maarufu nchini Rostam Aziz, Akram Azizi amehukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kulipa faini ya Sh.milioni 259.5 au kwenda jela miaka 20 jela baada ya kukiri mashtaka 73 ya kukutwa na nyara za Serikali zikiwemo silaha. Hukumu hiyo imetolewa jana 21 December 2018, mahakamani hapo ambapo Akram amefanikiwa kulipa faini kwa kulipa fedha hizo, hivyo amekwepa kifungo cha kwenda jela miaka 20 jela. Hata hivyo Mahakama imeamua kuitaifisha nyara hizo na kuwa mali ya Serikali na kuamuru silaha zote ziwe chini ya…

Source

Share:

MAREHEMU AHUKUMIWA JELA MIAKA MITANO

Mahakama ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imemhukumu aliyekuwa Meneja wa Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (Tarura) Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, Godfrey Majuto ambaye ni marehemu sasa, kulipa faini ya Sh milioni 3.6 au kutumikia kifungo cha miaka mitano jela.



Hiyo ni baada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ya kupanga ya uhujumu uchumi, baada ya Majuto na wengine wanne kushtakiwa kwa kosa la kuisababishia Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda hasara ya Sh 61,157,342. 


Aidha, mahakama hiyo imeamuru yeyote atakayeteuliwa kuwa msimamizi wa mirath ya marehemu Majuto atalipa faini ya Sh milioni 3.6 ili fedha hiyo iingine serikalini.


Mbali na Majuto, washitakiwa wengine katika kesi hiyo walikuwa ni Naomi Nko ambaye wakati huo alikuwa ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda, Peter Mwanoni, Beatus Bisesa, mkandarasi na Chiyando Matoke.

Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwanasheria wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Katavi, Bahati Haule, kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo la kuhujumu uchumi kwa nyakati tofauti.

Alidai walitenda kosa hilo Januari 2, 2012 wakiwa watumishi wa Halmashauri ya Mpanda wakidai kuandaa hati ya malipo ya uongo ya kutaka kuonyesha sehemu ya Barabara ya Kasokola kwenda Mtapenda kuwa imetengenezwa kwa gharama ya Sh 64,376,152 wakati si kweli.

Katika kosa la pili lililowahusu washitakiwa wa kwanza hadi wa tatu, walishtakiwa kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi kwa kupitisha malipo hayo kwa Kampuni ya Matoke huku wakijua barabara hiyo haikujengwa kwa gharama hiyo.

Haule alidai kuwa shitaka la tatu liliwahusu washitakiwa wote watano walioshitakiwa kwa kosa la kuisababishia halmashauri hiyo hasara ya Sh 61,157,342.

Baada ya kusikiliza pande zote mbili za mashitaka na utetezi, Hakimu Luoga, aliiambia mahakama hiyo kuwa washitakiwa wa kwanza, wa tatu na wa nne wamepatikana na hatia katika kosa la kwanza huku Majuto naye ametiwa hatiani katika kosa la pili na la tatu.

Pia washtakiwa akiwamo wa pili na wa tano hawakutiwa hatiani kwa kosa lolote lile na waliachiwa huru.

Baada ya maelezo hayo, Haule aliiomba mahakama hiyo itoe adhabu kali kwa washitakiwa kwa kuwa wameisababishia hasara Serikali.

Akisoma hukumu hiyo, Luoga alisema pamoja na mahakama kupokea hati ya kifo cha Majuto kilichotokea Desemba 4, mwaka huu huko Songea ambako alikuwa akifanya kazi kama Meneja wa Tarura wa Manispaa ya Songea, alikohamia kabla ya mauti hayajamfika alikuwa ameshatoa utetezi wake mahakamani hivyo hakuwa na sababu ya kuifanya mahakama ishindwe kutoa adhabu kwake.

Luoga alisema katika shitaka la kwanza Majuto akiwa na washitakiwa wa tatu na wa nne wamepatikana na hatia ya kifungu cha Sheria namba 22 ya kupambana na rushwa ya mwaka 2007, hivyo wameadhibiwa kulipa faini ya Sh 600,000 kwa kila mmoja au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela.

Katika kosa la pili na la tatu limemtia hatiani Majuto peke yake na kosa la pili kwa mujibu wa Sheria namba 31 sura namba 11 ya mwaka 2007, amehukumiwa kulipa faini ya Sh 1,000,000 au kifungo cha miaka mitatu jela.

Katika kosa la tatu, Majuto chini ya kifungu cha Sheria namba 57 (1)na kifungu namba 60 (1) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi, makosa ya kupanga, sura 200, marejeo ya 2002 amehukumiwa kulipa faini ya Sh 2,000,000 au kifungo cha miaka mitano jela.

Hakimu Luoga alisema hukumu hiyo amekukumiwa Majuto na mahakama inaagiza yeyote atakayeteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu alipe faini hiyo ili fedha hizo ziende serikalini.
Share:

WANAWAKE WANNE WAVAMIWA NYUMBANI KISHA KUBAKWA KWA ZAMU


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwalubambo.

Wanawake wanne (majina yamehifadhiwa) wakazi wa kijiji cha Buganzu kata ya Lunzewe Mashariki, Wilayani Bukombe Mkoani Geita wamebakwa na wanaume zaidi ya mmoja baada ya kuvamiwa na watu hao wakiwa majumbani mwao.


Tukio la kubakwa wanawake hao limetokea Desemba 11 majira ya saa nane usiku katika kijiji hicho, walipovamiwa na wanaume wanne wakiwa wamelala kisha kubakwa na kila mmoja na kupelekea kuwasababishia maumivu makali.

Akizungumza Mkoani Geita Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwalubambo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba watuhumiwa waliofanya unyama huo wamekwishakamatwa ambapo amewataja kuwa ni pamoja na George Deogratius(42) maarufu (Tolu) mkazi wa Ibamba, Josephat Emmanuel(25) mkazi wa Kabuhima, Rashid Maganga(18)) na Albert Makisio maarufu Kamkono wote wakazi wa Ibamba.

Kwa mjibu wa Kamanda Mponjoli, matukio mengine ni pamoja na watu wawili kuuawa Desemba 19 majira ya usiku, na wananchi wenye hasira kali wakiwa katika jaribio la kutenda uhalifu katika kijiji cha Nyakahengere kata ya Lukalanga Mjini Geita.
Share:

DISCO TOTO YAPIGWA MARUFUKU DAR

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema hatarajii kuona 'disco-toto' ikifanyika popote pale jijini Dar katika kuadhimisha sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.

Ameeleza kuwa hadi sasa hakuna aliyepeleka maombi kwa jeshi hilo ili kutoa huduma hiyo kwenye siku za sikukuu, ili ukaguzi wa kina ufanyike kwenye kumbi hizo kwa ajili ya usalama wa watoto.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi Desemba 22, 2018 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa.

Mambosasa ametoa kauli hiyo wakati akieleza jinsi polisi walivyojipanga kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.


Amewataka wazazi kuwa makini na watoto wao katika kusherehekea sikukuu hizi ili kuepusha matukio ya watoto kupata ajali, kupotea na kuzama kwenye fukwe, kama ilivyokuwa ikitokea miaka ya nyuma.

“Wazazi katika kipindi hiki cha sikukuu kila mmoja atimize wajibu wake wa kuhakikisha anajilinda yeye mwenye na watoto wake kwa kufanya hivyo sikukuu hii haitakuwa na madhara kwao.

“Ngoma za vigodoro haziendani na ustaarabu wa Dar es Salaam na niseme tu kwamba tutakushugulikia kabla hata haujaanza kucheza ngoma hiyo”.


Kamanda Mambosasa pia ametoa wito pia kwa wakazi wa Dar es Salaam kuhakikisha wanazingatia sheria na taratibu zote katika maadhimisho ya sikukuu hizo ili kuwepo na amani na usalama.
Share:

BASATA YAKANUSHA KUWAFUNGULIA DIAMOND NA RAYVANNY

Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) nchini Tanzania limekanusha kuwafungulia wasanii Diamond Platnumz na Rayvanny wanaotumikia adhabu ya kutojihusisha na sanaa kwa muda usiojulikana baada ya kufanya makosa mbalimbali ndani ya kipindi cha miezi miwili.

Taarifa ya Naibu Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Onesmo Kayanda iliyotolewa leo Jumamosi Desemba 22, 2018 imesema haijawaondolea adhabu hiyo na kuwakata wafuate maagizo waliyopewa ikiwamo kutofanya maonyesho nje ya nchi.

Jana, wasanii hao kupitia mtandao wa Instagram waliomba radhi kwa mamlaka mbalimbali nchini na jioni walionekana wakifanya mkutano na wanahabari nchini Kenya kutangaza maonyesho yao yanayoendelea.

"Ikumbukwe kuwa Desemba 18 tuliwafungia kutojihusisha na sanaa kwa kipindi kisichojulikana kwa kuimba kwa makusudi wimbo Mwanza tulioufungia kwa sababu za kimaadili,

"Baraza linasisitiza kuwa halijawafungulia wasanii hao, pia linawaonya kuacha kutoa taarifa za uongo kabla halijawachukulia hatua kali zaidi," imesema taarifa hiyo ya Kayanda.

Diamond na Rayvanny wameingia matatani wakituhumiwa kufanya makosa mbalimbali ikiwamo la kutumbuiza wimbo uliofungiwa, kufanya tamasha mkoani Mwanza bila kibali, kutoa lugha ya matusi jukwaani mkoani Mtwara na kutofuata taratibu za usajili wa matamasha.
Share:

DRC: UPINZANI WAONYA DHIDI YA KUAHIRISHA TENA UCHAGUZI

Muungano wa kisiasa unaomuunga mkono mgombea wa upinzani Felix Tshisekedi umemshutumu Rais Joseph Kabila kukosa dhamira ya kuandaa uchaguzi na kuondoka madarakani, lakini ukawataka wafuasi wao kuendelea kuwa watulivu.



Muungano huo ujulikanao kama CACH, umeonya kwamba hauwezi kuvumilia kuahirishwa kwingine kwa uchaguzi, hata kwa siku moja baada tarehe mpya iliyotangazwa na tume ya uchaguzi, tarehe 30 Desemba.

Mgombea mwingine wa upinzani, Martin Fayulu pia ametoa tamko kama hilo la muungano wa CACH, akisema hatua za kuendelea kuchelewesha uchaguzi haziwezi kuvumiliwa, na kuwabebesha lawama kikamilifu Rais Kabila na Mkuu wa tume ya uchaguzi, Corneille Nangaa. 


Tangazo la Fayulu limetiwa saini na vigogo wawili wa kisiasa waliozuiliwa kugombea, gavana wa zamani wa jimbo la Katanga Moise Katumbi, na aliyekuwa kiongozi wa waasi, Jean Pierre Bemba.


Na katika makala iliyoandikwa na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Dakta Denis Mukwege na kuchapishwa katika gazeti maarufu la New York Times la nchini Marekani, Mukwege amemtaka Kabila na wale aliowaita vibaraka wake mafisadi, kukabidhi madaraka, akionya juu ya uwezekano wa kuzuka ghasia kubwa ikiwa wataendelea kung'ang'ania uongozini.


Mkwege amesema kuna haja ya dharura nchini Kongo ya kupata serikali ya wataalamu, ambayo itaipa nchi mwelekeo na kuandaa uchaguzi wa kuaminika.


Huku haya yakijiri, juhudi za tume ya uchaguzi, CENI zimepata pigo, baada ya ndege aina ya Antonov iliyokodiwa na tume hiyo kusafirisha karatasi za kura, kuanguka karibu na mji wa Kinshasa jana jioni, ilipokuwa ikirejea katika mji mkuu kutoka katika mji wa katikati ya nchi wa Tshikapa, ambako ilikuwa imepeleka vifaa vya uchaguzi.


Kuna taarifa zinazotofautiana kuhusu idadi ya waliokufa katika ajali ya ndege hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Gomair. Afisa wa ukaguzi wa safari za ndege katika uwanja wa ndege wa Tshikapa, amesema ndani ya ndege hiyo walikuwemo wahudumu 5 na msafiri mmoja, na kwamba wote wameuawa.


Lakini balozi wa Urusi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Alexei Senteboff, amenukuliwa na mashirika ya habari akisema ndege hiyo ilikuwa na wafanyakazi watatu, wote raia wa Urusi, na wote wamekufa. 


Alisema kwamba awali kulikuwepo taarifa ambazo hazikuthibitishwa, zilizodai kwamba walikuwemo watu 23 ndani ya ndege iliyoanguka, wakiwemo wafanyakazi watatu raia wa Urusi.


Hadi sasa hakuna ripoti zozote za machafuko, kufuatia tangazo la CENI la juzi jioni, la kuahirisha kwa wiki moja uchaguzi uliotarajiwa kufanyika kesho Jumapili.


Credit:DW
Share:

RAIS MAGUFULI ATAKA POLISI WANAOUA MAJAMBAZI WASISHTAKIWE

Rais John Magufuli ametaka askari wa Jeshi la Polisi kutoshtakiwa kutokana na makosa yanayojitokeza wakati wakitekeleza majukumu yao ikiwamo kutuhumiwa kuua wahalifu.

Akizungumza jana wakati wa sherehe za kufunga mafunzo kwa askari wa jeshi hilo katika Chuo cha Taaluma za Polisi, Kurasini jijini hapa, Rais Magufuli huku akiahidi kuwa nao bega kwa bega alisema askari wanafanya kazi kubwa ya kuimarisha usalama wa nchi.

Alisema wakati mwingine askari wamekuwa wakishtakiwa kutokana na makosa ambayo hawajayafanya wakati wakitekeleza majukumu yao ikiwamo kutuhumiwa kuua wahalifu na kwamba kufanya hivyo ni kuwavunja nguvu wale wanaojitoa kwa ajili ya Taifa.

“Nataka Jeshi la Polisi linalochukua hatua sio askari anaenda anachukua hatua anashtukia amewekwa ndani, askari amekwenda kupambana na jambazi bahati mbaya jambazi likijipiga lenyewe risasi likafa kule unakuja unamshika askari, hapana,” alisema.

Rais Magufuli ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu alisema askari wa namna hiyo wamejitoa muhanga kulinda amani ya nchi hivyo ni lazima waongezewe vyeo ili kutoa motisha kwa wengine kujitoa kwa ajili ya Taifa lao.


Katika mahafali hayo, jumla ya askari 513 walihitimu kozi za mofisa na wakaguzi wasaidizi wa Polisi baada ya kumaliza mafunzo ya miezi sita huku Mkuu wa chuo hicho, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Anthony Rutta akisema watatu walifariki dunia wakiwa mafunzoni.
Share:

Form One Selection 2019 – Waliochaguliwa kidato cha kwanza 2019 Ruvuma Region for 2019/2020 Ruvuma

Form One Selection 2019 – Waliochaguliwa kidato cha kwanza 2019 Ruvuma Region for 2019/2020 Ruvuma

The List of Selected Candidates is available for each Ward Education Coordinator, Each Board’s Advertising Boards and the Office of the Regional Head Office, Check it here http://Ruvuma.go.tz/

Form one selection for the academic year 2019/2020 

The following students have been selected to join form one for Ruvuma Secondary schools for the academic year 2019/2020.

Click here to access Form One School Selection System for Ruvuma Schools

 

The post Form One Selection 2019 – Waliochaguliwa kidato cha kwanza 2019 Ruvuma Region for 2019/2020 Ruvuma appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Form One Selection 2019 – Waliochaguliwa kidato cha kwanza 2019 Kagera Region for 2019/2020

Form One Selection 2019 – Waliochaguliwa kidato cha kwanza 2019 Kagera Region for 2019/2020 Kagera

The List of Selected Candidates is available for each Ward Education Coordinator, Each Board’s Advertising Boards and the Office of the Regional Head Office, Check it here http://Kagera.go.tz/

Form one selection for the academic year 2019/2020 

The following students have been selected to join form one for Kagera Secondary schools for the academic year 2019/2020.

Click here to access Form One School Selection System for Kagera Schools

The post Form One Selection 2019 – Waliochaguliwa kidato cha kwanza 2019 Kagera Region for 2019/2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Form One Selection 2019 – Waliochaguliwa kidato cha kwanza 2019 Mwanza Region for 2019/2020

Form One Selection 2019 – Waliochaguliwa kidato cha kwanza 2019 Mwanza Region for 2019/2020 Mwanza

The List of Selected Candidates is available for each Ward Education Coordinator, Each Board’s Advertising Boards and the Office of the Regional Head Office, Check it here http://Mwanza.go.tz/

Form one selection for the academic year 2019/2020 

The following students have been selected to join form one for Mwanza Secondary schools for the academic year 2019/2020.

Click here to access Form One School Selection System for Mwanza Schools

 

The post Form One Selection 2019 – Waliochaguliwa kidato cha kwanza 2019 Mwanza Region for 2019/2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Form One Selection 2019 – Waliochaguliwa kidato cha kwanza 2019 Iringa Region for 2019/2020 Iringa

Form One Selection 2019 – Waliochaguliwa kidato cha kwanza 2019 Iringa Region for 2019/2020 Iringa

The List of Selected Candidates is available for each Ward Education Coordinator, Each Board’s Advertising Boards and the Office of the Regional Head Office, Check it here http://Iringa.go.tz/

Form one selection for the academic year 2019/2020 

The following students have been selected to join form one for Iringa Secondary schools for the academic year 2019/2020.

Click here to access Form One School Selection System for Iringa Schools

The post Form One Selection 2019 – Waliochaguliwa kidato cha kwanza 2019 Iringa Region for 2019/2020 Iringa appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

WAGONJWA WA SARATANI WAONGEZEKA KUTOKA 2500 HADI 6500

Na WAMJW-LINDI Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,imesema kuwa kutoka kipindi cha mwaka 2002 mpaka hivi sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wa saratani kutoka wagonjwa 2500 hadi wagonjwa 6500,kutokana na mitindo tofauti ya maisha na mabadiliko ya sayansi na teknolojia. Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akiwa katika ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya na uhamasishaji kwa wakulima kujiunga na mfuko wa Bima ya afya (UshirikaAfya) katika mkoa wa Lindi.…

Source

Share:

KWA SIMBA HII,HIVI NKANA WATATOKEA MLANGO GANI?KOCHA MBELGIJI APIGILIA MSUMALI HUU WA MWISHO

NA KAROLI VINSENT. BILA kupepesa macho kwa Simba hii iliyosheheni wachezaji bora na viwango vya Juu ni wazi timu Nkana Fc ni kama wamekwisha na waataanzaje sasa kutoka wakati wa mchezo ligi ya Mabingwa Barani Afrika  utakaofanyika kesho kwenye uwanja wa Taifa jijini hapa. Simba ambao ni Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kupitia Kocha wake Mkuu ambaye anasifika kwa Fomesheni nzuri, Patrick Aussems, ameonesha kutamba kuwa anajua umuhimu wa mechi hiyo, hivyo wamejipanga ni hao kutoka nchini Zambia . Kocha huyo raia wa Ubelg­iji amejinadi kwa kubainisha kuwa wanataka…

Source

Share:

SABABU ZA BOBAN KUZUIWA KUCHEZA YANGA NI HIZI HAPA

Wakati wapenzi na mashabiki wa Yanga wakiwa na shauku kubwa ya kutaka kumuona uwanjani mchezaji wao mpya, Haruna Moshi ‘Boban’, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), linadaiwa kumzuia mchezaji huyo kuitumikia timu hiyo. Boban alijiunga na Yanga hivi karibuni katika dirisha dogo la usajili akitokea African Lyon ambayo pia aliungana nayo mwanzoni mwa msimu huu akitokea Friends Rangers inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza. Kwa mujibu na Chanzo Changu , Meneja wa Boban, Herry Mzozo, alisema TFF imemzuia Boban kuitumikia Yanga kutokana na maagizo yake iliyoyatoa hivi karibuni kwa timu zote za…

Source

Share:

SAKATA LA KIPA WA YANGA KAKOLANYA NI PASUA KICHWA SASA,HATMA YAKE IMEBAKI HAPA

Na Mwandishi wetu SAKATA la Kipa wa Kipa, Beno Kakolanya wa Yanga sasa ni pasua kichwa baada ya hatma ya kuendelea kuwatumikia Mbingwa hao wa Historia kubaki mikononi mwa kocha Mwinyi Zahera ambaye alionesha kumkataa, ambapo kwa sasa wanasubiria uongozi wa klabu hiyo kuweza kuzungumza na kocha huyo ili kujua lini atarejea. Kakolanya kwa sasa yupo njia panda kuweza kurejea katika kikosi hicho mara baada ya kumalizana na uongozi wake kutokana na mgomo aliokuwa nao hivi karibuni ambapo kwa sasa suala limebakia kwa kocha Zahera kuweza kuamua juu ya kumrejesha…

Source

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger